Search This Blog

SIRI ZA GIZANI - 4

 





    Simulizi : Siri Za Gizani

    Sehemu Ya Nne (4)



     Wazazi wa Nasra walishangaa kumuona Ibra anashindwa kuongea masikini, Ibra alikuwa mjanja sana akafata daftari lake chumbani kisha akaandika ujumbe usemao kwamba "wazazi wangu kila siku nimekuwa nikiwaletea taarifa kuwa Nasra hajafa yupo kwa bibi mnabisha ona sasa bibi mwenyewe amenifanya nisiweze tena kuongea eti kwa sababu nimemkuta anamsuka Nasra chumbani kwake, mama yangu naumia sana kuandika kwamba sitoweza kuongea tena mimi ni bubu baba, lakini kila mnacho kiongea nakisikia na nitakuwa nawajibu kwa kuwaandikia". Baba Nasra alinuna sana alipo sikia wanamtaja mama yake kuwa ni mchawi akatoka pale na kwenda nje kupumzisha mawazo bila kuongea chochote. Mama Nasra alikuwa analia sana akamwambia mwanae, "najua unanisikia mwanangu lakini nakuhaidi utapona mtoto wangu".

    Siku moja usiku Nasra pamoja na bibi yake waliamka kukiwa na giza sana wakajipakaa madawa usoni, mikononi, pamoja na miguuni, kisha wakashikana mikono na kuinamisha vichwa chini ili watoke nje, alafu siku hiyo ibra alikuwa hajalala kabisa yupo dirishani anawaza sana kuhusu hali aliyo kuwa nayo ya ububu. Sasa wakati nasra na bibi yake wanatoka nje ibra akawaona, ndipo akafungua mlango polepole ili akamvute Nasra maana alikuwa anampenda sana, Ibra alikuwa ananyata taratibu anawafatilia polepole kujua wanaelekea wapi, alishangaa kuwaona wanaenda kwenye makaburi ya wa kristo kisha wanapanda juu ya makaburi na kuanza kuimba na kucheza, sasa kilicho kuwa kinamtia ibra aibu ni kwamba walikuwa wanavua nguo zao zote na kulala chini ya makaburi wakiwa uchi wa mnyama. Ibra aliona aibu kutazama sehemu nyeti za bibi yake pamoja na Nasra, ila alifumba macho na kuwakimbilia kisha akamshika Nasra akitamani kuondoka nae, Bibi Nasra alimpulizia dawa Ibra, kisha akamlaza juu ya kaburi, akafumbua jicho moja moja akiwa anapachika dawa jichoni za kumfanya Ibra asiweze kuona tena, bibi Nasra alipo maliza kufanya vile akasema, "umekuwa unanifatilia sana mambo yangu ila naona umezidi yaani unanifata mpaka huku, sasa utalala hapo hapo juu ya kaburi na hatukupeleki nyumbani tutaona utafikaje na upofu wako" wakaondoka.

    Ibra alilia sana maana hakuweza kuona tena, aliona giza tu mbele yake na kusikia sauti tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bibi Nasra pamoja Nasra walimuacha Ibra makaburini akiwa hawezi kuona chochote, Ibra aliogopa sana maana alisikia sauti za ndege kama bundi zikilia pale makaburini, alilia zaidi huku akiwaza akilini mwake wenda kuna mtu angeweza kumsaidia, duhh Ibra aliendelea kutembea bila kuona, akianguka huku na kule kwenye visiki, bahati mbaya Ibra akawa amedondoka kwenye shimo maana aliteleza vibaya mno, kipindi yupo mule shimoni hajui atatoka vipi, Ibra alikata tamaa ya maisha maana aliangukia vibaya mapafu yake akawa ameumia sana mule chini, Ibra alikaa shimoni mpaka asubui.

    Mama Ibra akashangaa kuona Ibra ahamki asubui, ndipo akaenda kumuangalia, bahati mbaya hakubahatika kumuona mwanae, Ndipo mama Nasra akaanza kuangaika kumtafuta mtoto kila kona hapatikani, kumbe Ibra yumo shimoni njaa imemshika hana msaada wowote ule analia tu. Baba nasra akauliza, "Ibra yuko wapi" walimtafuta siku tatu mtoto hapatikani, Mama Nasra akamwambia mme wake, "unaona sasa mme wangu uzembe wako unasababisha tunawapoteza watoto wote hivi hii ni mikosi gani jamani khaa" Baba nasra akasema "hivi we mwanamke unazani mimi naweza kukubali mumuite mama yangu mchawi, siwezi katakata," kulipo kucha Mama nasra akanyata taratibu kwenda kwenye chumba cha bibi Nasra ili aangalie kama atamuona Ibra wake, alipo fika hakuona mtu ila aliona TUNGURI juu ya diaba likiwa na shanga, mama Nasra aliogopa mnoo, akamfata mme wake akasema "mme wangu mama mkwe kweli ni mchawi nimeamini," baba Nasra alimzaba kofi mkewe kisha akamwambia "mpuuzi mkubwa wewe ebu toa mizigo yako yote uondoke kwangu sikutaki, umezidi kumtusi mama, yaani umeanza kumtegea tunguli za uongo ili ucheze na akili yangu nikubali kilaini huwezi na hiyo mitunguli umeiweka wewe makusudi"

    Mama nasra akasema, "mme wangu bado nakupenda usinifukuze, tazama mguu wangu unavidonda, ebu fikilia Ibra na nasra walivyo potea, mimi naenda kuishi wapi sasa, wakati mali tumetafuta wote"

    Baba nasra akasema "toka kwangu tu nimekuchoka, maana sipati ata faida ya ndoa toka tu rudi kwenu"

    Mama Nasra akapiga magoti chini akilia machozi ili asemeewe, lakini wapi..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama Nasra alipo fukuzwa na mme wake, kiukweli alichoka sana akili, maana hakuwa na sehemu yoyote ya kwenda sababu alikuwa ameisha wapoteza wazazi wake wote na kibaya zaidi ndugu zake walikuwa ni watu wenye roho mbaya sana maana kuna ata baadhi ata ya ndugu zake walio kuwa wanauana wenyewe kwa wenyewe, hivyo ikampelekea mama nasra kuogopa ndugu zake, Baba nasra alipo ona mke wake hatoki kwake, akaenda ndani kisha akachukua nguo na dawa za mama Nasra akaleta sebreni, akazirusha chini kisha akasema "mizigo yako hii hapa tokaaa sasa" mama Nasra akamwambia, mme wangu hivi umesahau kuwa hizi mali tumeangaika wote kuzipata, hii nyumba situmejenga wote jamani, kwanini sasa unanifukuza kama mbwa humu ndani au kwasababu mimi ni mwanamke, hivi baba Nasra huoni naumwa mguu naenda wapi sasa mimi jamani" baba Nasra akamjibu, "mimi nimekuchoka sana maana unamtukana sana mama yangu alie nizaa mimi, sio hivyo tu kumbuka mimi ni mwanaume naitaji pia kufanya tendo la ndoa sasa wewe unaumwa sana mimi nateseka sipati raha yoyote ndani ni bora tu uende kwa ndugu zako" mama Nasra akasema "sasa siondoki niue tu nijue moja maana ata haya maisha nimeisha yachoka" baba nasra alichukia sana akasema "we we we, unasema nini, eti nini" ndipo akaanza kumsukuma ili atoke nje mama nasra alikuwa anapata maumivu sana mwilini mwake maana kila alipo kuwa akisukumwa na vidonda vinatonesheka! Hivyo maumivu yakawa makali sana mguuni, baba Nasra alivyo endelea kumsukuma, mama nasra akajivua kitenge chake kisha akajifunga kiunoni akasema "sitoki kwangu kama nyumba umeijenga mwenyewe nitoe sasa" baba Nasra alikuwa mkorofi kama nini, akachukua sahani ya udongo kabatini kisha akampiga nayo mke wake kichwani, mama nasra hakuelewa ata kidogo maana alisema "nipo tayari kufa ila ndani sitoki" huku akivuja damu kichwani na akiwa analia, baba nasra alipo ona mke wake aelewi akaanza kumvuluta ili atoke, akasema "najuta kwanini nilikuoa we mwanamke, aki ya mungu sikupendi ata kidogo, sikutegemea kama ungeweza kunikorofisha na mama yangu mzazi ata siku moja ondoka tafadhali, nasema kwangu leo ulali lazima uondoke tu" kipindi wanapiga kelele mule ndani, bibi nasra pamoja na majirani wakawa wamesikia zile kelele wakaja haraka sebreni kuangalia kuna nini" walipo ingia wakauliza, "jamani mbona ugomvi, mama Nasra damu hizo zote za nini tena" mama nasra akiwa analia akasema, "mme wangu ananifukuza na mimi sina sehemu yoyote ya kwenda, watoto wangu wote wamepotea kwa njia za kutatanisha alafu isitoshe mimi naumwa nitaenda wapi jamani" majirani pamoja na bibi wakamuuliza baba nasra, "kaka tatizo nini, maana umempiga mke wako vibaya sana, angalia alivyo pasuka kichwa, sio hivyo tu umemtonesha sana mguu wake na unajua kabisa anaumwa kwanini lakini" baba Nasra akasema

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nimemchoka sana huyu mwanamke aki ya mungu simtaki tena, maana anamtukana sana mama yangu kipenzi, anasema kwamba mama yangu ni mchawi, na sio mala moja ndugu zangu, kila siku anamuita mama mchawi sasa leo nimeamua kumfukuza aondoke atuache sisi familia ya kichawi nimevumilia sasa leo nimeshindwa" kisha akampiga teke mgongoni, majirani wakaguna, kisha wakasema, "subiri kwanza usimpige, hivi wewe mama Nasra mbona ukua hivi mwanzoni, ujasili umeutoa wapi huu mpaka unamtusi mama mkwe wako, hivi ujui anaweza kukuachia laana" mama nasra akasema, "ndugu zangu kama mnavyo nijua mimi ni mama mstaarabu tu na wala sijawai kumuuzi mtu wala kumtukana mtu yoyote tangu tujuane, ila mimi kilicho sababisha nishawishike kusema hivyo ni kwasababu ya mwanangu Ibra maana kila siku Ibra amekuwa akishtuka usingizini kwa ndoto za kutisha, ata akilala mchana hivyo hivyo, na kila akishtuka tu anatufata sisi wazazi wake kisha anasema binti yetu nasra hajafa tukimuuliza yuko wapi anasema yupo na bibi yake chumbani na hii sio mala moja tu kila siku imekuwa inatokea hivyo mpaka mtoto anakosa amani ndani ya nyumba, lakini kila tunapo mwambia baba Nasra anagomba, na ndiyo maana kanipiga hivi" majirani wakauliza "mama Nasra una uwakika huyu mama ni mshirikina na unauwakika kweli kwamba marehemu mwanao Nasra hajafa amechukuliwa msukule na bibi yake" kabla ya mama nasra kujibu, bibi nasra akaanza kulia kama mtoto akisema, "mkwe wangu hanipendi mimi naondoka" baba nasra akamjibu "mama usiondoke huyu mke wangu ni mshenzi tu alafu ni bora aondoke yeye sio wewe mama" majirani wakasema "hivi mama nasra kwanini hukufanya uchunguzi kwanza lakini, unajua huyu ni mama hivyo ukimuita mchawi ni kama unatengeneza laana ya vizazi kwa vizazi" mama Nasra akasema, "mimi sijawai kumsema mama kwa asilimia zote kuwa ni mchawi, lakini leo nilipo ingia kumtafuta kijana wangu ibra maana amepotea tu katika mazingira ya kutatanisha nikakuta tunguri juu ya diaba ikiwa imeviringishiwa shanga juu ndipo nikamwambia mme wangu kwa kijiamini kuwa mama mkwe ni mchawi, yaani nilipo mwambia tu, ndipo akaanza kunipiga hivi mpaka damu zimebitoka" majirani wakashtuka kwanza kisha wakasema "ebu nenda ukatuletee icho kitunguri ulicho kuiona tukione" mama Nasra akasema sawa nakifata , bibi Nasra alipo sikia vile aliogopa sana maana alijua hapo ndipo anaenda kuaibika na kukamatwa masikini, sasa wakati mama Nasra anaenda chumbani kwa bibi Nasra, kipindi anafungua mlango ili achukue tunguri hakuamini macho yake kwa alicho kiona.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mama nasra alishangaa sana kumuona mwanae Nasra akiwa juu ya diaba amekunja magoti akiwa analia huku ameshikilia kile kitunguri, "nasra mwanangu"alisema mama nasra, lakini alishangaa sana kuona Nasra hajibu chochote zaidi ya kulia tu, majirani sebreni wakasema kwamba, "mama Nasra mbona hurudi tatizo nini" kipindi mama nasra anasema "njooni mumuone Nasra wangu hajafa yupo humu ndani" walikuja spidi sana tena kwa uoga maana watu wote walijua Nasra ni marehemu na wameisha mzika zamani sana. Sasa walipo ingia chumbani ili wamuone Nasra na lile tunguri kwa bahati mbaya akuna alie weza kumuona Nasra, zaidi ya mama nasra mwenyewe, majirani wakauliza kwamba, "mama Nasra mbona mtoto na tunguri lako lenye shanga hatuvioni" mama nasra akasema, "jamani hivi hamna macho au, si Nasra huyo hapo juu ya diaba" baba nasra akachukia sana maana wenyewe hawakuweza kumuona Nasra ata kidogo akasema, "jamani majirani mimi mke wangu leo halali hapa ndani, nazani ushahidi ninao wa kutosha kila siku anasema hivi tu, mimi nahisi yeye mwenyewe ndiyo mchawi hivyo kabla hajaniua mimi lazima nimuepuke kwa njia yoyote ile, naombeni mnisaidie kumfukuza" kweli masikini mama Nasra alishikwa juu juu na vijana watano tu alitolewa kama mwizi mule ndani akiwa hoi. Kipindi hicho pia Ibra bado yupo mule shimoni akiwa amefikisha siku ya nne bila kuweka chochote tumboni, siku moja jioni kuna gari kubwa la usambazi wa soda za jumla lilipinduka maeneo ya pale makaburini, hivyo kutokana na ile ajari, soda zikawa zimeanguka sana chini na kupasuka, baadhi ya watu wa mtaa ule walijaa haraka na kuchukua baadhi ya chupa ambazo zilikuwa hazijapasuka wakanywa, sasa balozi wa ule mtaa akawambia wale wahusika wa zile chupa wakusanye vile vipande vya chupa zilizo pasuka, kisha wakavimwage kwenye shimo la makaburini ili chupa zisizagae maeneno ya watu pale kusudi wasije kukatwa au kuzikanyaga. Sasa wahusika wa lile gari wakakubali, na mda huo Ibra yupo chini ya shimo ina maana wakimwaga chupa zina mpasua na kumuua ibra hapo hapo. Dahh sasa dereva wa lile gari akawaacha vijana wakusanye vile vipande vya chupa, kisha yeye akaenda makaburini kuangalia kama gari inaweza kupita na kuangalia na shimo pia kama ni kubwa au dogo, dereva aliangalia akaona gari linapita vizuri tu, ndipo akaenda kuchungulia kwenye shimo wakati anainama

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuchungulia shimoni ufunguo wa gari ukatoka kwenye mfuko wa shati lake ukadondoka mule shimoni ukaangukia kwenye miguu ya ibra, dereva aliumia sana kuudondosha ule ufunguo akashindwa atautoa vipi maana shimo lilikuwa refu, kuna kaka mmoja akasema, "boss mimi ukinipa pesa ya kula tu naingia humo shimoni sijala tangu jana bosi" dereva akampa 10000 kisha akamwambia "sasa ufate", kweli kijana akaingia mule shimoni mpaka yule dereva akashangaa maana aliweka mtu mnene juu akafunga kamba ndefu kisha akaingia, alipo karibia kufika kulikuwa na giza mule chini. Jamaa akaanza kupapasa chini kuangalia kama atapata ufunguo, kumbe Ibra mule shimoni masikini, alikuwa anahisi anafatwa yeye, na kibaya zaidi bibi yake alimfanya awe bubu hivyo ata kuomba msaada ilikuwa ngumu, jamaa alipo angalia chini akahisi kama kuna mtu ila hakujali sana maana hakutegemea kukuta mtu mule chini isitoshe kulikuwa na giza sana, ibra alianza kulia machozi yakimtoka maana aliona kabisa hapa naweza nisisaidiwe, yule kijana alipo pata ufunguo akaanza kupanda kamba ili atoke mule chini na wakati huo ibra haoni wala hawezi kuomba msaada kusudi watu wamtoe mule shimoni........



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog