Search This Blog

SIRI ZA GIZANI - 5

 





    Simulizi : Siri Za Gizani

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ibra alikosa msaada kabisa, maana yule kijana alipo pata ufunguo alitoka mule shimoni na furaha sana kwamba amepata 10000 ya kula. Hivyo yule dereva alivyoo pewa ufunguo wa gari tu, akaenda kusogeza gari ili wamwage zile chupa mule ndani, na kipindi hicho hicho Ibra yumo bado shimoni amekata tamaa kabisa na maisha, dereva alivyo fikisha vile vipande vya chupa akawambia vijana waanze kuvimwaga shimoni. Kweli walikuwa wanavimwaga kwa kutumia koleo, chupa zilikuwa zina mdondokea Ibra kichwani, Ibra alichomwa sana kichwa, mikono, mwili mzima na uso ukatobolewa tobolewa akawa hatamananiki kabisa kaaribika uso sana, kwa bahati mbaya walivyo kuwa wanaendelea kumwaga zile chupa shimoni Ibra akawa amefariki mule mule ndani ya shimo maana alishindwa ata kuongea wenda wangemsikia na kumsaidia, hakuna ata mmoja alie jua kama ibra kafia mule ndani. Dereva alipo maliza kuzimwaga chupa akaondoka na ikasaulika hivyo hivyo. Mama Nasra alikosa kabisa sehemu ya kukaa maana kila alie muomba msaada alimkatalia kutokana na ule ugonjwa wake, sababu mama Nasra kiukweli alikuwa anatia kinyaaa, hivyo ata alipo enda kuomba kazi kwenye magenge japo aoshe vyombo apewe chakula, harufu yake ilimkosesha riziki kabisaa, kutokana na msongo wa mawazo na uchungu wa kugundua kuwa mama mkwe wake ndiye ameharibu maisha yake, alafu yale magonjwa yaliyo kuwa yamemuandama, mama Nasra alifunga kamba juu ya mti wa mpera kisha akajinyonga na kupoteza maisha yake kama mwanae Ibra, hivyo nyumbani kwao wakawa wamebaki, baba nasra, bibi nasra na msukule wa Nasra tu. Baba Nasra alipo letewa taarifa za kifo cha mke wake alisikitika sana maana wali ishi kwa mda mrefu sana ila hakuwa na jinsi maana baba nasra alikuwa anampenda mama yake mzazi kupita maelezo. Bibi nasra alienda kwenye msiba pamoja na baba Nasra, kisha wakarudi nyumbani. Maisha yaliendelea mule ndani sasa siku moja usiku, bibi Nasra aliamka kisha akaingia kwenye chumba cha mwanae alafu akapulizia dawa kisha akachukua maganda ya muhindi akamjaza nayo mdomoni alafu akarudi kulala. Asubui ilipo fika baba nasra alishangaa sana kukuta maganda ya muhindi mdomoni mwake aliyatema kisha akaenda kumuuliza mama yake kwamba, "mama jamani mbona naona vitu vya ajabu sana nimeshangaa kukuta maganda ya muhindi mdomoni na jana mimi ata sikula wala kuyaona mahindi" bibi nasra akasema "kijana wangu mimi sielewi ila ulikosea sana kuchagua mke nazani ukoo wao ndiyo unakutesa hivyo" baba nasra akaanza kuogopa kulala peke

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     yake akasema, "dahh sijui kwanini nilimfukuza mke wangu sahivi ata chumba nakiogopa ngoja nikalale na mama mzazi" kweli baba nasra akaenda kwenye chumba cha bibi nasra akiitaji alale humo eti anaogopa kulala peke yake. Bibi nasra akamfukuza akasema "mwanangu kuwa na adabu yaani unataka kulala na mimi kwanini au unataka kunibaka mtoto wa kiume usiwe muoga mbona mimi nalala peke yangu we kalale hakuna wa kukutesa leo" ikabidi akalale tu, bibi nasra aliamka tena usiku kisha akampulizia dawa baba nasra ili awe mnyonge sana amchezee anavyo weza. Kweli baba nasra alifungwa miguu na mikono kwa mashati yake mwenyewe kisha akapakwa michanga mwili mzima alafu akachanjwa na wembe kifuani. Asubui ilipo fika baba nasra anajikuta katika hali hiyo alilia mwenyewe akapiga yowe "uuuuwiiii uwiiiii, naombeni msaada" ndipo bibi nasra akaenda chumbani kwake, baba nasra akasema "mama sijui nani amenifunga mimi sijui ni nani huyu huu ni uchawi tu mama" bibi nasra akamfungua kisha akamwambia, "naona wamekuchanja na wembe kifuani mwanangu, yaani walimwengu wabaya jamani" baba nasra alilia kama mtoto, siku ya tatu hivyo hivyo bibi nasra alimfata mwanane usiku kisha akamtoa nje akampa jembe alafu akamwambia alime bustani zote za pale nyumbani maua na usafi wote, kisha alipo maliza akamrudisha, baba nasra alipo amka akakuta kachoka miguu inavumbi wakati alilala ameoga msafi tu. Dahh siku ya nne baba nasra akaogopa kulala ndani akakataa kabisa akasema hii nyumba siitaki tuiuze tu mimi ngoja nilale nje tu sitaki kulala ndani ata kidogo. Kweli baba nasra alikataa nyumba yake na akaanza kulala nje kila siku, mda mwingine analala kwa marafiki zake kwake hapataki kabisa, siku moja mama yake mzazi akamwambia kama ulali humu mimi naondoka kwako na hautaniona tena hapa maana tabia yako sijaipenda, baba nasra aliwaza sana masikini aliumia sana pia, ila akaamua kukubali tu kulala. Siku moja bibi nasra akiwa anajiandaa kwenda kumtesa baba nasra akashangaa kuona mzimu wa Ibra pamoja na mama nasra unamtokea na kumwambia kwamba "lazima ujutie kwa mabaya uliyo tufanyia kisha wakamwaga dawa zake zote chini akashindwa kwenda kumtesa baba nasra siku hiyo" bibi nasra alianza kuogopa kisha akaanza kutoa dawa mbali mbali za kujikinga lakini kwa hile mizimu miwili bibi alishindwa kabisa maana , mizimu miwili yote ilikuwa na asila sana" mzimu wa mama nasra ukasema, "wewe mama umetualibia maisha yetu umetutekeza kinyama lazima na wewe uteseke kama sisi" ndipo bibi akaanza kutafuta dawa za kujikinga ili asiweze kuteswa, akaenda kwa mganga ambae alikuwa na nguvu nyingi zaidi za kichawi, yule mganga akamwambia, "mama yangu ukitaka usiteswe na hao watu unatakiwa kukubali kubeba mateso yote waliyo kuwa wanayapata bibi nasra akauliza "mateso gani hayo" ndipo akaambiwa "unatakiwa kuwa kipofu na bubu, kama ulivyo mfanya mjukuu wako Ibra, sio hivyo tu unatakiwa kuwa na uvimbe sehemu zako za siri pia, alafu mtoto wako huyo baba nasra na yeye pia umfanye msukule kama ulivyo mfanya Nasra bila kufanya na kukubali hivyo ni lazima utakufa kifo kibaya sana mama yangu" sasa chagua moja, kufa au kupata adhabu. bibi akaanza kulia akasema....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Siwezi kukubali" alisema bibi Nasra akimwambia yule mganga. Dahh kweli bibi Nasra alishindwa kabisa kukubaliana na masharti ya yule mganga akaona ni bora atumie nguvu zake mwenyewe kujikinga na usumbufu wa mizimu, lakini alikataa katakata kuwa kipofu, kupata uvimbe na kumfanya baba Nasra mwanane wa damu, kuwa msukule ndipo bibi Nasra akaona haiwezekani kabisa kukubaliana na mawazo ya yule mganga, maana kwanza baba Nasra ndiye aliekuwa mtoto mwenye mchango mkubwa kwake, hivyo kama angemfanya msukule ina maana bibi nasra ange ishi maisha ya tabu sana. Mganga akamwambia, "kama umeshindwa amri na ushauri wangu, msaada mwingine wa mwisho ambao naweza kukupa mrudie muumba wa mbingu na dunia, yule mungu wa binadamu na uache kabisa mambo yako ya kishrikina, ya hii miungu yetu" bibi Nasra akasema, "nitaacha vipi ushirikina wakati ata wewe mwenyewe ni kama mshirikina tu" mganga akasema, "mimi ni mganga na tiba zote nazijua, ata kama nafanya hizi kazi ila najua kuna mungu duniani" bibi nasra alitoka pale na asila sana kisha akaondoka kurudi nyumbani. Alipo fika akamkuta baba Nasra sebreni akiwa na mawazo sana, baba Nasra akasema, "mama tangu umekuja hapa nyumbani matatizo yamekuwa yakijitokeza mala kwa mala alafu ni mengi sana mpaka mda mwingine nakuhisi vibaya mama yangu, natamani kuamini maneno waliyo kuwa wakiniambia kuwa wewe ni mchawi lakini nashindwa kabisa" bibi Nasra alichukia sana akasema, "mwanangu umenivua nguo leo, nakulaani kabisa, nimekuzaa mimi alafu unaniita mchawi, kwahiyo kipindi chote hicho upo mdogo nakulea ulisha wai kuniona mimi na uchawi wowote au na wewe umeisha nichoka" baba Nasra akasema "mama mimi sijawai kukuona kabisa kama una mambo ya kishirikina, lakini nakumbuka zamani baba yetu alipo fariki ghafla ndani, watu walikuwa wanasema umemuua wewe ingawa sikuwa naamini sababu ya upendo nilio kuwa nao kwako, sasa hivi familia yangu yote imepotea sina mke sina watoto, yaani wamepotea bila sababu maalumu" bibi nasra akasimama kisha akavua nguo zote mbele ya mtoto wake akasema, "nimekuzaa kupitia hapa mwanangu leo unaniita mchawi" baba nasra akafumba macho kwa uoga maana aliona aibu kumuona mama yake akiwa uchi, aliendelea kufumba macho hivyo hivyo akakimbia mpaka chumbani kwake na kumuacha bibi Nasra pekeyake, wakati huo bibi Nasra analia mwenyewe sebreni, kipindi baba nasra yupo ndani mzimu wa mama Nasra ukamtokea ghafla tu, ukamwambia, "usiogope mme wangu, najua hauna kosa ila mama mkwe wangu ndiye mkosaji na ndiye mualibifu wa familia nzima, chukua ili tawi baba Nasra utamsikia binti yako Nasra anavyo teseka kwa bibi yake lakini ujue kwamba mimi na mwanangu Ibra tumeisha fariki ila Nasra hajafa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    yeye yupo analishwa unga na bibi yake chumbani" baba Nasra akalipokea lile tawi, alipo lishika tu akaanza kusikia sauti ya Nasra ikilia ikisema, "bibi nitoe kwenye diaba, nimechoka kujikunja humu, nina njaa bibi" baba nasra akatoka haraka haraka mpaka sebreni kisha akamwambia mama yake, "mama unaona sasa kumbe kweli we ni mshirikina, kwanini unamuweka mwanangu kwenye diaba" bibi nasra aliogopa, akasema "mwanangu nitazame nipo uchi nakulaani, bado tu unanitusi" baba Nasra akasema, "sina uoga na laana zako mama, namtaka binti yangu maana ndio huyo tu nilie baki nae wengine wote umeisha wapoteza" bibi nasra aliendelea kulia akizani baba Nasra ataona huruma ila baba Nasra akaingia chumbani kwa bibi Nasra kisha akafungua diaba kumchukua nasra, ila cha kushangaza ni kwamba, alipo fungua diaba hakuweza kumuona nasra lakini nasra alikuwa humo humo ila baba yake hakuweza kumuona sababu ya zile dawa alizo kuwa amepakwa, baba Nasra alitoka nje akiwa amebeba shuka la mama yake akamfata na kumfunika maana alikuwa uchi, alafu akapiga magoti chini akilia ili mama yake amsamee kwa kumuita yeye mchawi, bibi Nasra akasema, "najua hunipendi mwanangu ndiyo maana umeniita hivyo ila kumbuka mimi ni mama yako na nimekuzaa kwa tabu sana, na kukulea kwa tabu pia, nashangaa leo nimezeeka unaniita mchawi" baba Nasra alisameewa na siku ikasha hivyo hivyo.



    Siku moja usiku bibi nasra akiwa anajiandaa kwenda kwenye nyumba za majirani kufanya uchawi ili kuwatesa kama kawaida yake, mzimu wa mama Nasra pamoja na Ibra ukamfatilia hukohuko, sasa wakati bibi nasra ameisha fika kwenye familia ile aliyo enda kuitesa, ile mizimu ikaingia ndani na kuwaamsha wenye nyumba kihisia, bibi Nasra alikamatwa na baba mwenye ile nyumba kisha akafungwa kamba mikononi na miguuni pia mpaka asubui, watu wenye hasila kali walipo gundua kuna mchawi kakamatwa walikuja na mapanga na marungu yao kisha wakaanza kumpiga bibi nasra, cha kushangaza watu hawakuweza kumtambua bibi Nasra maana alikuwa amejipaka vumbi ya mkaa usoni, sasa baada ya wale watu kumpiga sana wakaona ni bora wamuite mganga aje kumpa adhabu, mganga alie kuja alikuwa ni yuleyule ambae bibi Nasra alikuwa ameenda kwake ili ampe kinga ya mizimu, baada ya mganga kugundua kuwa yule bibi ndiye alie kuwa kwake, akaamua kumpulizia dawa kitaalamu ndipo bibi akapotea ghafla tu, watu wote walio kuwa katika yale mazingira wakakimbia, bibi alipo fika nyumbani alikuwa amejaa damu na mwili wote unamuuma, baba nasra alipo muona anachechemea akamuuliza, mama tatizo nini" bibi nasra akasema, mwanangu na mimi siku hizi wachawi wananifata sana usiku naangaika sana mtoto wangu" baba Nasra akampa pole kisha akampeleka hospitali. Sasa kutokana na hasila ya ile mizimu, kulipo kucha asubui, bibi nasra alishangaa sana kuona anapata uvimbe sehemu zake nyeti, kipindi anajitahidi kutafuta dawa ili apone alishangaa mwenyewe

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwamba badala ya kuona dawa kwa macho akawa anapapasa apate dawa kwa mikono yake maana bibi Nasra alipoteza macho kama alivyo mfanya Ibra, hivyo hakuweza kuona tena dawa ya kujitibu, alimfata baba nasra amuelezee tatizo lililo mkuta dahh bibi Nasra alishangaa zaidi maana hakuweza tena kusikia kama alivyo kuwa Ibra, sasa kipindi bibi Nasra analia huku akitamani kufa tu maana mateso yalimzidi sana, ndipo Nasra akatoka kwenye diaba na kukaa kwenye mgongo wa bibi yake bila kutoka maana alikuwa amenasa hapo hapo kwa sababu bibi nasra dawa zilimuishia na yeye ndiye alie mfanya Nasra msukule hivyo Nasra akawa ndiyo mzigo wake, Nasra alikaa mgongoni bila kutoka, lakini dawa au njia ambayo ingetumika kumtoa Nasra mgongoni ni kwamba bibi Nasra alipaswa kumlaza juu ya kaburi lake nje ya nyumba na kibaya zaidi bibi Nasra alikuwa kipofu hivyo alipaswa kuongozwa na baba Nasra mpaka kaburini na wakati huo bibi nasra alikuwa hataki kutoka nje ya chumba maana baba Nasra angemuona Nasra wake akiwa mgongoni...



    Bibi Nasra aliendelea kuteseka mule chumbani mwake bila baba Nasra kujua maana alikuwa katika miangaiko yake, ilipo fika usiku akajua kuwa baba Nasra anaweza kuja kumuona chumbani kwake na kumsalimia, hivyo akiingia tu atamkuta Nasra mgongoni, ndipo bibi Nasra akaanza kuwaza afanye nini ili baba Nasra asimkute Nasra mgongoni. Bibi nasra alijutia sana uchawi wake alio kuwa anafanya, alilia sana masikini, akajaribu kufanya kila alicho weza kumtoa Nasra mgongoni ila ikashindikana, kipindi bibi anawaza njia za ziada ili asigundulike, mzimu wa Ibra pamoja na mama Nasra ilimtokea bibi Nasra na kumwambia kwamba, "ulitutesa sana, ukatualibia maisha, na wewe leo ni zamu yako, utakaa na Nasra mgongoni mwako mpaka majirani wote na mwanao watakapo kuja kukuta nae na zile kuku ulizo zileta tumeisha zificha" dahhh kiukweli bibi Nasra aliomba msamaa akisema, "mkwe wangu na mjukuu wangu naombeni msamaa naombeni mnisaidie nisikamatwe, sitarudia hii tabia, nitaaibika sana nisaidieni jamani" Ibra na mama yake waliagana wakapotea kabisa kwenda kupumzika kwa amani na kumuacha bibi Nasra akilia, sasa ilipo fika mida ambayo baba Nasra angeweza kuja na kuingia ndani ili kumsalimia mama yake, bibi Nasra akaenda mlangoni na kufunga mlango, ili baba Nasra asiweze kuingia ndani, kweli baba Nasra alipo kuja akamtafuta mama yake sana mule ndani ili amsalimie ila hakuweza kumuona alipo enda kugonga mlango wake akakutwa mlango umefungwa, baba Nasra hakuelewa kabisa mama yake kaenda wapi maana hakuhisi kama mama yake angeweza kujifungia chumbani, ndipo akaenda kumuulizia kwa majirani, baba nasra alimtafuta siku tatu bila kumpata masikini dahh, na wakati huo bibi Nasra yupo chumbani njaa inamuuma hana msaada wowote ule wa chakula mpaka akaanza kuzidiwa na kuangukaanguka kila mala, siku moja alizidiwa zaidi maana alikuwa na njaa na anamzigo mgongoni, isitoshe alikiwa mzee hivyo ata kuamka kwenda kufungua mlango ilikuwa ngumu, sasa kutokana na kushindwa kutoka nje bibi Nasra akaanza kujisaidia kinyesi mwenyewe ndani ya mwili wake, hivyo harufu mule chumbani ikawa mbaya sana maana ata mkojo pia alikuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    anajikojolea mwenyewe, siku moja baba Nasra alitembelewa na rafiki yake pale kwake, ili ampe pole ya kupotelewa na mama yake mzazi, baba Nasra akamwambia rafiki yake kwamba, "mama yangu najua hajapotea, ila siku moja nilimtusi kuwa yeye ni mchawi nazani alichukia hivyo kaamua tu kuondoka maana ilo neno lilimuuma sana mpaka akavua nguo zake na kubaki uchi wa mnyama" rafiki yake akamwambia, "dahh kaka kweli ulikosea uta mtukunaje mama mzazi hivyo, kwamba yeye ni mchawi, kama angekuwa mchawi si ange kunyonga tangu ukiwa mdogo, jitahidi umtafute, umuombe msamaa, akusamee makosa yako hizo ndizo wanasema laana kutoka kwa wazazi". Walipo maliza kuongea wakati rafiki yake anaamka kurudi kwake wakati anatoka akawa amekatiza kwenye mlango wa chumba cha bibi, roho yake ikasita maana alihisi arufu mbaya sana inatoka mule ndani, akamuuliza baba Nasra, "kaka mbona hapa kuna harufu mbaya hivi, kama ya kinyesi, na mkojo wa mda mrefu" ndipo baba Nasra akaanza kuchungulia kwenye kitasa kuona nini kinanuka wakati anasogeza sura yake harufu ilizidi alafu akasikia kama kuna mtu anakema mule ndani, baba Nasra aliogopa mno, ndipo akamuuliza rafiki yake kwamba, "mbona nasikia kama kuna mtu anakema humo ndani" rafiki yake akaziba pua kisha akatega sikio kusikiliza kama ni kweli kuna mtu ndani, alipo sikia akasema, "dah kaka kuna mtu ndani alafu ni mchafu sana maana atakuwa anajisaidia humohumo ndani" baba Nasra machozi yakiwa yanamtoka akamwambia, "hichi ni chumba cha mama yangu nazani amejifungia ndani kaka, labda tubomoe mlango" ndipo wakabomoa ule mlango kwa tabu sana, walipo fanikiwa kubomoa ule mlango walishangaa sana kumuona bibi Nasra akiwa amembeba Nasra mlangoni, rafiki yake baba nasra akasema, "kaka huyo sini binti yako alie fariki na kaburi lake lipo hapo nyuma, inakuwaje tena anaishi na bibi yake ndani, alafu kwanini bibi anajisaidia mwilini mwake mwenyewe, angalia n'zi zilivyo mzunguka, baba Nasra akiwa analia akasema, "mama kumbe kweli wewe ni mchawi, kumbe mama wewe mshirikina kiasi hichi" bibi Nasra akiwa analia akaomba msamaa akisema, "mwanangu nisamee mimi ndiye nimesababisha vifo vya familia yako, naomba unibebe mpaka kaburini kwa nasra maana amekataa kutoka mgongoni, mpaka tutakapo mlaza kaburini na kaburi lake alitaonekana tena, maana sahivi siwezi tena kuona numekuwa kipofu kama Ibra nilivyo mfanya" watu walijaa sana kwenye ile nyumba majirani wa kila aina, mpaka waandishi wa habari zile taarifa zikavuma sana ndani na nje ya nchi, picha na kila kitu vikasambaa kila kona, ilikuwa ni aibu sana, Wakati baba Nasra anaomba watu wampeleke mama yake kaburini, hakuna ata mmoja alie kubali kumbeba maana bibi alikuwa mchafu sana, alafu alikuwa anaogopesha maana Nasra alikuwa tayari ni marehemu hivyo watu hawakuamini kama angeweza kuwepo tena duniani, kibaya zaidi Nasra alikuwa aongei chochote, maana baba yake alikuwa anamuita akisema "Nasra, Nasra mwanangu unanisikia" lakini nasra alikuwa akimtazama huku analia na kutoa machozi....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bibi Nasra aliona aibu sana maana kila mtu alikuwa anamtazama, Na msaada wake yeye kuona na kuweza kuongea kipindi chote hicho ni kwasababu Nasra alikuwa mgongoni mwake, hivyo angetoka tu, bibi angeendelea na ile hali ya kuwa kipofu na mateso mengine pia. Baba Nasra alikuwa analia tu maana aliona aibu sana kwasababu hakugemea kabisa kama mama yake mzazi angeweza kuwa na roho ya namna ile, kila mtu alikataa kumbeba bibi Nasra maana kwanza walimuogopa na baadhi ya watu wakasema, "dahh huyu bibi kweli mchawi, mtazame macho yake mekunduuu" wengine wakasema, "hii familia ilikuwa ya furaha sana lakini huyu mama ndiyo kaiteketeza, sasa angalia mwanaume kabaki mwenyewe ataishije sasa humu ndani" yale maneno ambayo raia walikuwa wanaongea mbele ya baba Nasra yalimtia uchungu sana, ndipo baba Nasra akamwambia rafiki yake kwamba, "kaka ngoja niingie chumbani kwangu mala moja nikachukue vitambaa ili tubembeleze raia wajifunge mikononi mwao kusudi wambebe mama yangu na kumpeleka kaburini" baba Nasra alipo ingia chumbani, akakuta baadhi ya dawa ambazo mke wake alizisahau chumbani kipindi anamfukuza maana hakuchukua zote kipindi kile, ndipo baba Nasra akachukua hivyo vidonge vyote kama 30 kisha akavimeza kwa pamoja, hakukaa ata dakika 30 watu wakasikilia sauti ya kilio kutoka chumbani walipo ingia kusaidia kwa bahati mbaya wakakuta tayari baba Nasra na yeye pia kafariki maana vile vidonge vilikuwa vingi hivyo vikageuka sumu. Yalikuwa ni maajabu sana siku hiyo, maana sisi kama ndugu yake ilituuma kutokana na msaada mkubwa ambao baba Nasra alikuwa akiutoa kwenye familia, ata majirani waliumia pia sababu baba nasra alikuwa ni mtu wa watu na familia yake ilipendwa mtaa mzima kwa busara walizo kuwa nazo. Bibi nasra alipo sikia mwanae kajiua aliishiwa nguvu kabisa akaanza kulia akisema, "bora na mimi nife, maana nimemuua mwanangu, niueni sitaki kuishi" walimwambia, "uchawi wako umekuponza sasa, angalia faida uliyo ipata, umekuwa ukifanya mambo yako kisiri tena gizani, angalia leo unavyo teketea kwenye mwanga kila mtu anakushangaa" mwenyekiti wa ule mtaa, akaamulu vijana wambebe bibi Nasra ili wampeleke kaburini, kweli bibi Nasra alibebwa mpaka kwenye kaburi la Nasra kuangalia kama kweli Nasra atatoka mgongoni, wakati huo baba Nasra ameenda kuandaliwa jeneza lake ili aweze kuzikwa. Daah ilikuwa ni historia kubwa sana ambayo ilizungumzwa kwa mda mrefu maana yale matukio hayakuwa ya kawaida, kipindi bibi Nasra amebebwa, n'zi nazo zilikuwa zinamfata! Alipo fikishwa kaburini kweli akalala juu ya kaburi ila cha kushangaza bibi alipotea ghafla alafu Nasra akabaki juu ya kaburi akiwa amechoka njaa imempiga mno analia tu, ndipo akapelekwa hospitali, ila kipindi Nasra anatibiwa kwa bahati mbaya akawa amepoteza maisha hivyo akafa upya kwa mala ya pili. Sasa kumbe bibi Nasra alipo potea alikuwa ameingia kwenye lilelile diaba ambalo Nasra alikuwa akikaa, watu wengi walipo muona bibi kapotea walikimbia maana wengi wao walikuwa wanasikia tu uchawi ila walikuwa hawajawai kuuona tangu wanazaliwa. Hakuna ata mmoja alie gundua kama bibi yupo ndani ya diaba. Mazishi yalifanyika ya Nasra pamoja baba yake, na watu walipo maliza wakaondoka na kutuacha ndugu tukiwa maeneo ya pale pale nyumbani, sasa hakuna ata ndugu mmoja alie kuwa anaweza kuingia ndani maana wote tulikuwa tunaogopa ushirikina. Tuliondoka na kuiacha nyumba kama ilivyo, ila kibaya zaidi bibi alikuwa bado yumo kwenye diaba na asinge weza kutoka mule ndani maana nguvu zake za kichawi zilikuwa zimepungua, alikaa kama siku tano akiwa kwenye diaba mpaka na yeye pia akafa na kuiaga dunia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutokana na bibi Nasra kufia ndani na hakukua na mtu ata mmoja kwenye ile nyumba, harufu ya mwili wa bibi Nasra ikaanza kutoka nje hivyo majirani na wapita njia wakaanza kuchafuliwa hewa kitu kilicho wakwaza sana maana mwili wa bibi ulioza pia mule ndani. Sasa watu wakajiuliza kwamba "hii nyumba ina nini, juzi juzi tu watu wamekufa wengine wakapotea na sahivi tena harufu zimeanza" wengine wakatamani kuingia ndani ila waliogopa labda kuna ushirikina wa yule bibi, ndipo kuna vijana wakorofi walipanga mipango yao usiku kisha wakaenda kuwasha ile nyumba moto ili iondoe gumzo na kero za pale mtaani, kweli nyumba ya kaka yangu ilichomwa moto vitu vya thamani vyote vikateketea, na hapo ndipo maisha ya kaka yangu pamoja na familia yake nzima akiwemo na mama yetu wakapotea.



    Baada ya baba kunisimulia hii story, akasema, "Awa binti yangu sisi tulikuwa hatumkumbuki mungu kabisa, na hatukujua mchango wa Mungu katika maisha yetu, na isitoshe wazazi wetu hawakutuimiza kabisa katika dini, lakini tangia haya matatizo yatukute kwenye ukoo wetu ndipo tukaufahamu mchango wa mungu na kutambua kuwa uchawi upo na bila mungu hakuna msaada" nikamuuliza baba kwamba, "baba kwanini hii stori ya baba mkubwa hukunisimulia kipindi chote hicho, leo ndiyo unanisimulia" baba Awa akasema, "wakati ulikuwa bado hujafika ila leo umefika" tangu kipindi hicho mimi na baba yangu Mr shaheem tunaswali sana na mwenyezi anatujali kwa kila tumuombacho kwa imani



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog