Search This Blog

UCHAWI WA KURITHI - 4

 





    Simulizi : Uchawi Wa Kurithi

    Sehemu Ya Nne (4)



    Pendo akawa ameamua kabisa kupambana na bibi yake, akakumbuka na maneno yote aliyoambia na bibi yake kuwa asiamini uchawi,

    "ananiambia nisiamini kama uchawi upo kumbe yeye ndio mchawi aliyekubuhu, nitapambana nae tu"

    Yusuphu alimsikiliza mjukuu wake na kumsikitikia kwani alimjua Nyuta ni taifa kubwa.

    YUSUPHU: Mjukuu wangu, nakuonea huruma sana yule bibi yako hafai kabisa.

    PENDO: Babu mateso tuliyopata ndio yananifanya niamue kupambana na bibi.

    YUSUPHU: Ila yule ni mtu hatari ni bora kumkimbia.

    PENDO: Babu hatatukimkimbia hawezi kuacha anayoyafanya na pia kukimbia tatizo sio suluhisho babu, suluhisho ni kulikabili tatizo.

    YUSUPHU: Sasa wewe utamkabili vipi bibi yako Pendo? Kama ameweza kumuua mtoto wake wa kumzaa itakuwa wewe mjukuu!!

    PENDO: Babu akili yangu bado inaendelea kuchanganua ila bibi lazima nimkabili.

    YUSUPHU: Sawa mjukuu wangu, nakutakia mafanikio tu.

    PENDO: Asante babu.

    Pendo alijikuta akiwa na uchungu sana na bibi yake, kila alipofikiria mateso aliyoyapata wakati anasoma, kifo cha baba yake na kaka yake. Akifikiria mateso waliyoyapata yeye na mama yake ndani ya nyumba ya misukule akazidi kupatwa na chuki dhidi ya bibi yake na akaamua kumkabili vilivyo.

    Pendo akamuaga mama yake kuwa ana safiri anaenda kumtembelea huyo bibi yake anayeogopewa mtaa mzima.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MARIUM: Pendo mwanangu, Pendo naogopa kukupoteza mwanangu.

    PENDO: Mama usijari ila mimi sirudi nyuma, itajulikana hukohuko nikiwa na bibi.

    MARIUM: Mwanangu jamani, bibi yako ni mtu hatari sana.

    PENDO: Ni bibi yangu ndiomana naenda kumkabili mama, atakuwa kama rafiki.

    MARIUM: Umesahau wakati unaumwa hadi ukarudishwa mwanangu.

    PENDO: Nakumbuka, na si ndio yeye mwenyewe akaniombea!! Mama, bibi yetu haepukiki cha msingi ni kumkabili tu. Usijari mama.

    Kwakweli Marium alimuhurumia sana binti yake, alikuwa amejawa na hofu ya kumpoteza kwani mtu anayeenda kupambana nae si wa kawaida. Pia aliwaza anaenda kupamba vipi na mtu anayetumia silaha zisizoonekana kwa macho ya kawaida. Kwakweli alimuhurumia sana binti yake, hata Amina nae alimuhurumia mdogo wake.

    AMINA: Ila Pendo jaribu kufikiria mara mbili, huko unakotaka kwenda hakufai.

    PENDO: Najua dada kama hapafai ila naimani Mungu atanisaidia.

    AMINA: Hayo ni matatizo ya kujitakia mdogo wangu.

    PENDO: Naelewa dada, ila nimehairisha hadi masomo yangu ili nikamkabili maana huyu bibi atatumaliza dada.

    AMINA: Sawa, naimani utarudi salama mdogo wangu.

    PENDO: Msiwe na shaka na mimi, kama mambo yameshaharibika mengi tu.

    Pendo akaendelea kujipanga kwaajili ya safari yake.

    Ila cha kwanza alipanga kufikia kwa shangazi yake Huruma ili akitoka hapo ndipo aende kwa bibi yake.

    Pendo alifika kwa shangazi yake, ambaye nae kwa kipindi hiko alikuwa na watoto wawili wadogo ambao walikuwa mapacha. Pendo hakujua kama huyo shangazi yake nae pia ni mchawi.

    Muda aliofika pale ilikuwa ni jioni ambapo alipokelewa vizuri tu na shangazi yake huyo, watoto wake walikuwa na miaka miwili na nusu.

    Usiku ulipofika, Pendo akawa ameandaliwa chumba cha watoto ambacho huwa wanacheza humo wakati wa mchana, kumbe na usiku huwa kina kazi yake ya ziada.

    Pendo hakujua kuwa hata wale watoto wadogo mapacho nao walikuwa wanafundishwa uchawi, aliwashangaa tu kuona watoto wadogo ila wameshupaa kama watu wazima.

    Hakuwaelewa watoto wale kwakweli.

    Pendo akiwa amelala, mara akasikia kama watu wanazungumza chumbani mule ila alikuwa haelewi wanazungumza mambo gani, akajaribu kuangaza huku na kule bila ya kuona chochote.

    Akiwa bado amelala pale, akaona kama wale watoto mapacha wamekaa pale kwenye kitanda chake wanamchekea, Pendo akaogopa. Akaona sasa kazi imeanza sasa, mara akasikia kama watu wanatembea akaanza kujiuliza kuwa au ile misukule ya ndani kwao imehamia kule.

    Pendo akajikunyata ukizingatia yupo mwenyewe humo chumbani. Ama kweli kuishi nyumba ya mchawi yataka moyo, kwanza unatakiwa usiwe na ule usingizi wa mang'amng'am, usingizi ambao mtu akikushtua tu unashtuka. Unatakiwa uwe na ule usingizi ambao ukilala umelala hadi kukuche hushtukishtuki hovyo.

    Sasa kwa Pendo aliyezoea kulala kwa machale ilikuwa ni tabu sana, alikuwa anaombea kukuche tu.

    Chumba kile kilikuwa kidogo ila kilikuwa na pilika pilika za kila aina.

    Mara vitu vingine vinatembea juu ya dari, mara watu wanaingia na kutoka. Kwakweli Pendo hakuelewa chochote, akajiuliza moyoni,

    "kama kwa mtoto mtu kupo hivi je kwa mama mtu kutakuwaje? Eeh Mungu nisaidie"

    Pendo hakuweza kulala hadi panakucha, alipoona mwanga tu akawa wa kwanza kutoka nje, shangazi yake alimkuta Pendo ameshaamka.

    HURUMA: Umelalaje shangazi?

    PENDO: (Huku akijibaraguza), salama tu shangazi.

    HURUMA: Mbona umewahi sana kuamka?

    PENDO: Nimezoea kuamka mapema tu shangazi si unajua mambo ya shule tena.

    HURUMA: Kweli kabisa shangazi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pendo hakuwa na furaha kama ile aliyofika nayo mwanzoni hapo kwa shangazi yake, akajiuliza kama aanze pale kwa shangazi au aende kwa bibi yake moja kwa moja, ila pale kwa shangazi yake palishamtisha akaogopa kulala kwa usiku mwingine zaidi.

    Siku ile wakati misukule inarudi kwa Nyuta, ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Nyuta kwani hakutegemea kurudishiwa ile misukule kwa staili ile, kwani misukule ilirudi na kufanya fujo sana pale nyumbani kwa Nyuta.

    Nyuta alichukizwa sana, na roho ikamuuma kuwa mwanae hakuwa tena miongoni mwa ile misukule kwa maana hiyo mwanae alikuwa amekufa kweli, roho ya Nyuta ilimuuma sana na akazidi kuwa na chuki na Marium mara dufu. Alimuona Marium kuwa ni mtu asiyefaa.

    Wakati Pendo anapanga kwenda kumkabili bibi yake, Nyuta nae alikuwa anapanga namna ya kuiteketeza familia ya Marium.



    Pendo akiwa anajipanga namna ya kumkabili bibi yake, kumbe Nyuta nae alikuwa anajipanga kwaajili ya kuteketeza familia ya Marium.

    Pendo akiwa pale kwa shangazi yake, akaamua kufanya maamuzi ya haraka sana.

    Akaamua kujitoa muhanga kuwa ataenda tu huko kwa bibi yake hata iweje.

    PENDO: Shangazi, leo sitalala hapa naenda kwa bibi.

    HURUMA: Unamaanisha bibi yako, mamaangu na mimi?

    PENDO: Ndio shangazi.

    HURUMA: Yamekusibu yapi hadi umeamua hivyo?

    PENDO: Nataka kwenda kumsalimia shangazi, na kama nikipapenda basi nikae huko kwa muda.

    HURUMA: Unajipenda wewe?

    PENDO: Ndio najipenda na kwanini waniuliza hivyo shangazi?

    HURUMA: Hamna kitu, nakutakia safari njema.

    Ingawa Huruma alikuwa ni mchawi ila alijikuta akimuhurumia Pendo kuhusu uamuzi anaouchukua wa kwenda kumsalimia mama yake.

    Pendo akajiandaa na kuanza safari ya kuelekea kwa bibi yake.

    Safari ikaanza na akiwa njiani akawaza mambo mengi sana. Akawaza namna itakavyokuwa kwake yeye na huyo bibi yake.

    Wakati akiwaza hayo wakatokea wanawake wamama wawili ambao walikuwa ni machizi, Pendo aliwahurumia ila hakujua kama ule uchizi wamepewa na bibi yake.

    Pendo hakuyajua mambo makubwa afanyayo bibi yake, aliyatambua yale madogo tu.

    Akajisemea moyoni kuwa anaamini Mungu ndiye atakaemsaidia katika maswaibu yake.

    Muda ukawa umeenda, Pendo akaona bora atafute nyumba ya kulala wageni apate kupumzika kwa usiku huo. Akaona kwenda kwa bibi yake usiku vile ndio anaweza asilale kabisa.

    Akiwa hapo kwenye nyumba ya kulala wageni akawasikia wadada wawili wakimzungumzia Nyuta na kusema hawamuamini na wanamuhisi kuwa ni mchawi.

    Pendo akaachana nao na kulala, alipoamka asubuhi, Pendo akapata taarifa kuwa kuna wadada wawili pale wamekutwa wamekufa.

    Pendo akashtuka, nae akajibeba kwenda kuwaona, mmh akasikitika sana kwa alichokiona kwani walikuwa ni walewale wadada wawili ambao usiku wake walikuwa wakimuongelea bibi yake. Akajiuliza maswali mengi kuwa ni kitu gani kimewaua wale wadada.

    Pendo hakujua kama hapo mtaani Nyuta hasemwi na watakaomsema tu lazima waende na maji.

    Pendo alisikitishwa tu na kifo cha wale wadada.

    Baada ya muda akajiandaa na kwenda kwa bibi yake.

    Alipokaribia karibu na kwa bibi yake, akamuona bibi yake akiwa nje anafagia uwanja.

    Nyuta alipomuona Pendo alishtuka kidogo na ubaya zaidi hakujua Pendo amefata kitu gani mahali hapo.

    Kwavile hakujiandaa na ujio wa Pendo kwa muda huo, ikabidi ampokee kwa mapokezi ya kawaida tu na kumkaribisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NYUTA: Vipi mbona nakuona na begi?

    PENDO: Nimekuja kukutembelea bibi halafu nataka kukaa kama siku mbili au tatu.

    NYUTA: Na mbona umekuja asubuhi?

    PENDO: Jana nilichelewa kufika bibi ndomana nimekuja leo.

    Nyuta akawaza sana kuwa mbona hakupewa taarifa rasmi za ujio wa Pendo mahali pale!! Akajiuliza kama vidubwana vyake vinachagua watu wa kumletea taarifa.

    Alikuwa akiwaza akiwa amesimama pale pale nje na Pendo.

    Akamkaribisha ndani na badae yeye akatoka nje kuendelea kujiuliza maswali mawili matatu.

    Nyuta akachanganua mawili matatu, akili yake haikukaa sawa akahisi kuna jambo tu ambalo huyu mtoto atakuwa amelifata.

    Akawaza pia, misukule yake imerudishwa kwa namna moja au nyingine wakina Pendo wamegundua kua yeye ni mchawi, na kama wamegundua iweje Pendo aende mahali pale? Bado hakupata jibu. Na pia akajiuliza, mpango wake ulikuwa ni kuiteketeza familia ya Marium iweje sasa huyu Pendo ajilete mwenyewe!!

    Nyuta akili haikumkaa sawa kabisa, akaamua kuwa kabla hajafanya chochote kuhusu Pendo lazima akamuulize kwanza kilichompeleka.

    Kwahiyo akaingia nae ndani na kuongea nae maneno ya faragha, alishajiweka sawa kuwa Pendo akijikanyaga kumjibu maswali yake basi kazi aliyoipanga dhidi ya Marium na itaanza kwa Pendo.

    Nyuta akaweka maongezi hayo na Pendo bila kupoteza wakati. Na akapanga kazi yake itaanza na Pendo na hatommalizia pale kwake ila atamngoja arudi kwao.

    NYUTA: Haya Pendo niambie mmegundua nini kuhusu mimi?

    PENDO: (Huku akili yake ikicheza na swali), kivipi bibi?

    NYUTA: Yani wewe na familia yako, mmenigundua mimi ni nani?

    PENDO: (Akagundua kuwa bibi yake alishajua kama wamemjua), tena afadhari umeniuliza bibi maana ndio kilichonileta.

    NYUTA: (Akashtuka), kivipi?

    PENDO: Bibi tumegundua kuwa wewe ni mchawi.

    NYUTA: (Huku sura yake ikibadilika), nini? Nani mchawi?

    PENDO: Bibi sina nia mbaya hapa, ila nakumbuka kuna siku uliniambia nisiamini uchawi na ukaniambia uchawi haupo duniani. Ndiomana mimi niliposikia kuwa wewe ni mchawi nikaamua kuja kukuuliza bibi yangu.

    NYUTA: Unataka kujua kama kweli ili iweje na itakusaidia nini?

    PENDO: Bibi, kwanza nilitaka kujua kama ni kweli. Pili kama ni ukweli nikupongeze bibi yangu kwani mambo uliyoyafanya sidhani kama wanasayansi wanayaweza.

    NYUTA: Unajielewa kweli wewe Pendo?

    PENDO: Najielewa kabisa bibi.

    NYUTA: Haya utafanya nini sasa baada ya kunipongeza?

    PENDO: (ikabidi atoe maamuzi ya haraka ili asije akadhuruka kabla hajafanya anachotaka kufanya), Nataka na mimi kuwa mchawi kwani kuna binadamu wanakera kweli, nataka niwe kama wewe bibi.

    NYUTA: (Sasa moyo wake ukajawa na furaha), kweli unataka kuwa mchawi kama mimi?

    PENDO: Ndio bibi.

    NYUTA: Nyumbani wanajua hayo uliyoamua?

    PENDO: Hawajui bibi, sikutaka kuzuiwa na mtu ndiomana sikuwaambia ila niliwadanganya vingine tu.

    NYUTA: Kwanza kabisa usiite uchawi bali sema ni ujuzi upitayo akili ya binadamu wa kawaida.

    PENDO: Kumbe bibi?

    NYUTA: Ndio hivyo, nitakurithisha mikoba yangu.

    PENDO: Sawa bibi.

    Nyuta alifurahi sana kuona mjukuu wake mmoja kaamua kwa roho safi kuwa mchawi.

    Pia akaona kazi imepungua kwani atamtumia huyo kuiteketeza familia yake.

    Alifurahi pia kuwa amempata mtu wa kumrithisha mikoba yake ya uchawi kwa urahisi kabisa.

    Kitu cha kwanza kabisa ni kumpeleka kwenye chama cha uchawi, familia ya kichawi inafurahi sana kuona mtu mmoja ameongezeka kwenye chama chao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakafanya sherehe ya kichawi ambapo Pendo akawa anashangaa na kuogopa mambo aliyoyaona huko kwenye chama. Na kimoyomoyo akajiita kuwa yeye ni mchawi wa kujitakia.

    Wakiwa pale kwenye chama, wakamtaka Pendo amtaje mtu wa kumtoa kafara ili aweze kujiaminisha kuwa ameanza kukomaa kwenye uchawi.

    Pendo akapatwa na wakati mgumu na kujilaumu moyoni kuwa kwanini ameamua kukubali kuingia kwenye mambo ya kichawi.



    Pendo akapatwa na wakati mgumu na kujilaumu kwanini ameingia kwenye uchawi. Ila bado akajitoa kupambana hadi ajue mwisho wake utakuwa ni kitu gani.

    Pendo hakuwa na jinsi zaidi ya kumsikiliza huyo bibi yake atakachomwambia.

    NYUTA: Sasa utamtoa nani Pendo?

    PENDO: Bibi inabidi kwanza unipe utaratibu wa kutosha ili nijue wa kumtoa.

    NYUTA: Unaweza ukamtoa hata mama yako au dada yako.

    Pendo akashuka sana.

    NYUTA: Tena nikwambie kuingia kwenye uchawi ni kitu rahisi sana ila kutoka yapasa kujipanga vilivyo.

    PENDO: Ila bibi sijasema kama nataka kutoka.

    NYUTA: Mbona umeshtuka sasa nilipokutajia hao?

    PENDO: Bibi nimeshtuka kikawaida tu, na wala sitaki nitoke bali nataka kuwa mzoefu tena wa kudumu.

    NYUTA: Nakufurahia sana Pendo, wewe ndio mrithi wangu.

    Nyuta akampeleka Pendo na kwenye ile nyumba aliyohifadhi misukule. Pendo alishangaa sana kuonyeshwa ile misukule ambayo mingi ilikuwa ni ndugu wa Nyuta. Akashangaa pia kuwaona wale wadada waliokuwa wakimteta Nyuta kwenye ile nyumba ya wageni na asubuhi wakakutwa wamekufa, akashangaa kuwaona wakiwa mule kwa bibi yake kama misukule.

    PENDO: Bibi na hawa walifanyaje?

    NYUTA: Walikuwa wananiteta.

    PENDO: Ulijuaje kama wanakuteta?

    NYUTA: Unajua nini Penda! Hiki kitongoji chote nina antena zangu kwahiyo watu wakinisema tu nawajua haraka sana, napata taarifa kwa wepesi na kufanya kazi yangu. Ndiomana nakwambia mimi itakuwa vigumu sana kudhurika kwani nimejikamilisha.

    Jambo hilo lilimfanya Pendo awe anafanya vitu kimoyomoyo kwani akiropoka kwa mtu yoyote atajulikana, akashukuru pia kuwa bora aliacha simu nyumbani.

    NYUTA: Kuna wamama wengine wawili nimewapa ukichaa sababu ya tabia yao ya kunisema.

    PENDO: Au ndio wale niliokutana nao wakati nakuja?

    NYUTA: Itakuwa ni hao hao.

    Hapo Pendo aliweza kuona kuwa bibi yake ni mtu katili wa kiasi gani, hata akisemwa anammaliza mtu.

    Pendo akaendelea kutafakari cha kufanya ili asije akashtukiwa mapema vile ambavyo amepanga na moyo wake.

    Kwanza kabisa akataka kushuhudia wafanyavyo.

    PENDO: Bibi nataka japo nijifunze unachofanya hadi kunakuwa na misukule kama ile.

    NYUTA: Utajua tu, kila kitu ni taratibu utajua. Wewe ni mrithi wangu kwahiyo nitakujulisha mambo mengi.

    Nyuta akamfundisha Pendo namna ya kutengeneza dawa za kuwapa watu magonjawa yasiyo na tiba hospitali, pia dawa za kuua mtu na kuwa msukule, na dawa za kuua kabisa. Zote alimfundisha Pendo namna ya kuzitengeneza.

    Pendo aliona mambo mengi na ya kusikitisha mule kwenye uchawi.

    Pia alimshangaa bibi yake kutunza misukule mingi kiasi kile.

    Akajaribu kufanya dawa tofauti tofauti ambazo zilimpa majibu mazuri.

    Nyuta akamjaribisha Pendo kama anaweza kumuua mtu, akamlengesha kwa mtu mmoja ambapo Pendo alitakiwa kumuua mtu huyo.

    Pendo akiwa hajui hili wala lile, akapewa dawa mkononi aliyoitengeneza yeye mwenyewe. Halafu Yeye na bibi yake wakaondoka kichawi, wakafika mahali ambapo yule dada atapita, Pendo akaamriwa aiweke ile dawa.

    Alipoiweka tu yule dada akapita na kuikanyaga, mara akatapatapa na kufa.

    Pendo akashangaa sana, Nyuta akamgeukia na kumpongeza.

    NYUTA: Hongera sana, umeweza kuua mtu.

    PENDO: Sielewi bibi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NYUTA: Unapokuwa mchawi unatakiwa uwe na uwezo wa kuua na ukifanikiwa basi unakuwa shujaa na nguvu zako zinaongezeka. Kama mimi sitetereshwi na chochote na wala mtu yeyote hanibabaishi sababu nina siri kubwa sana ya maisha.

    Pendo ikabidi afanye kitu cha kumchunguza bibi yake kwanza, alitaka ajue ni kitu gani ambacho bibi yake anajivunia nacho.

    Alitaka aijue hiyo siri aliyonayo bibi yake kwani ndio ilikuwa kitu pekee cha kumuangamiza bibi huyo.

    PENDO: Bibi tulipomuua yule mdada, ulisema una siri kubwa sana. Ni siri gani hiyo.?

    NYUTA: Taratibu mjukuu wangu, tunapozidi kuwa pamoja itakuwa rahisi kukwambia kwani wewe ndio utakuwa mrithi wa kazi yangu.

    PENDO: Na mbona bibi wewe ni katili sana?

    NYUTA: Unapokuwa mchawi unatakiwa uwe katili, ila mimi ukatili ulianza tangia nikiwa mtoto mdogo.

    PENDO: Kivipi bibi?

    NYUTA: Nilipokuwa mdogo, nilikufa kwa siku kadhaa kiuchawi. Nilienda moja kwa moja kuzimu.

    PENDO: (Akashtuka), ulienda kuzimu kule kwa shetani bibi?

    NYUTA: Ndio, na nilipokuwa huko nikakabidhiwa kitu cha kunikinga, ndiomana naweza nikajifanya mtu wa aina yoyote hapa duniani silogeki wala sidhuriki labda nijitengenezee dawa mwenyewe.

    PENDO: Duh bibi hiyo ni hatari, sasa hicho kitu ulichopewa ukakiweka wapi?

    NYUTA: Nililishwa, labda nikitapike.

    PENDO: Huwa inawezekana kukitapika?

    NYUTA: Kuna dawa zake, na tena labda nitengeneze mwenyewe.

    Mimi sio kama Kisu aliyerogeka kirahisi namna ile. Ila mjukuu wangu nitakurithisha vyote hivi.

    PENDO: Wale wanaoombea pia hawawezi kukupata bibi?

    NYUTA: (Akacheka sana), mara ngapi wanaomba huko kwaajili yangu? Mimi ndio Nyuta, na mara nyingine mimi mwenyewe hujifanya mwanamaombi. Kuna kitu hukijui mjukuu wangu kuhusu hii dunia.

    PENDO: Kitu gani bibi?

    NYUTA: Wanadamu ni waoga sana, kwahiyo sisi wachawi hutumia udhaifu huo kuwaangamiza. Hata sisi tunatambua uwepo wa Mungu.

    PENDO: (AKashangaa sana), kumbe mnatambua bibi duh!!

    Pendo akatafakari sana namna ya kumkabili bibi yake ila bado akajipa matumaini.

    Nyuta akaendelea kumsisitiza Pendo kuhusu swala la kafara.

    Pendo akafikiria sana na akawaza kujaribu bahati yake kwa mtindo huo.

    PENDO: Bibi kabla sijatoa kafara kuna kitu nataka kufanya.

    NYUTA: Kitu gani?

    PENDO: Nataka nimloge mama, halafu dada yangu nitamtoa kafara.

    NYUTA: (Akafurahi sana kusikia hivyo), umenifurahisha sana mjukuu wangu, na sasa utakuwa mchawi shujaa.

    PENDO: Ila kuna kitu ningependa unisaidie hapo.

    NYUTA: Nitakusaidia chochote mjukuu wangu, sema tu nini unataka.

    PENDO: Nataka unitengenezee dawa za kukamilisha mambo hayo.

    NYUTA: Ila si nimeshakufundisha namna ya kutengeneza dawa?

    PENDO: Ndio bibi ila mimi ningependa nitumie dawa uliyotengeneza wewe kwasababu mama yangu ni mgumu sana yule. Mimi naweza nikakosea.

    NYUTA: Na kweli mjukuu wangu, mama yako ni mgumu sana. Basi nitakutengenezea hiyo dawa.

    PENDO: Ndio nitengenezee bibi halafu nitaenda kukamilisha mambo yote mimi mwenyewe. Na pia unipe na ile dawa ya kujificha ili mchawi mwingine asinione.

    NYUTA: Nitakupa kwani umenionyesha ujasiri mkubwa sana.

    PENDO: Nawachukia sana wale bibi, bora niwamalize tu.

    NYUTA: Sawa sawa mjukuu wangu.

    Siku iliyofatia ilikuwa ni siku ya kutengeneza hiyo dawa ili Pendo akakamilishe kazi na aweze kuwa mchawi mzoefu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo ikawa ni siku ya kutengeneza dawa.

    Nyuta alikuwa makini sana kwani anajua jinsi ilivyo ngumu kumkabili Marium ambaye ana vitu vinavyomlinda.

    Ila Nyuta alifurahi moyoni kuwa lazima safari hii atampata Marium na kumfanya atakavyo hadi mauti itakapomchukua huyo Marium kwani mwanae mwenyewe alijitoa kumteketeza mama yake. Nyuta alifurahi sana na kumpenda sana Pendo. Akawa anampongeza kila wazo alilompa.

    PENDO: Bibi, hivi wewe huna ndugu wa karibu?

    NYUTA: Ninao ila watoto wa baba kama watatu hivi nimewatoa misukule.

    PENDO: Kwanini bibi?

    NYUTA: Sitaki baba aishi na mwanamke yeyote yule, napenda wanavyomkimbia.

    Nyuta alifanya vingi sana kwa baba yake bwana Kisu hadi baba yake akajuta kuwa na binti kama kisu.

    PENDO: Ila bibi, unaowachukia ndio wametenda haya?

    NYUTA: Hapana, walionitenda vibaya walikuwa kule kijijini kwa bibi yangu na karibia wote nimewamaliza.

    PENDO: Upo juu sana bibi yangu.

    NYUTA: Hawaniwezi kabisa mimi.

    Kwasababu kwenye ile nyumba ya Nyuta alikuwa anaishi mwenyewe na sasa yupo na Pendo, Nyuta hakuwa na shaka la kufanya kitu chochote mule ndani kwani anajua Pendo ndiye mrithi wake.

    PENDO: Bibi nipake hiyo dawa ambayo sitaonekana na mchawi wala mtu wa kawaida.

    NYUTA: Sasa mjukuu wangu na mimi sitakuona ujue!

    PENDO: Sawa bibi, basi nipe mimi niwe napaka halafu nikirudi najifuta.

    NYUTA: (Akawa kama mtu mwenye machale kidogo), kwani wewe unataka ya nini?

    PENDO: Bibi kule kwenye kikao cha wachawi kuna siku zingine watakuwa wanakusema tu.

    NYUTA: Inawezekana eeh!!

    PENDO: Ndio bibi na kama hivyo leo utakuwa huku ukiendelea kutengeneza dawa basi ndio watazidi kukusema kwavile umewashinda. Sasa mimi nataka nikawasikilize bibi.

    NYUTA: Kweli nimempata mjukuu mwenye akili sana. Basi nitakupa kidogo mjukuu wangu. Ila dawa yenyewe ukiipaka inawasha kwanza, utaweza?

    PENDO: Nitaweza bibi.

    NYUTA: Sawa mjukuu wangu, nitakupa badae na kukuelekeza pia.

    PENDO: Sawa bibi, nakupenda sana.

    NYUTA: Hata mimi nakupenda mjukuu wangu.

    Nyuta na Pendo wakawa ni marafiki wa karibu sana kwani walipatana sana na kuambizana mambo tofauti tofauti.

    Ila urafiki wao ulikuwa na unafki ndani yake na Nyuta hakulijua hilo, laiti angewahi kuwa na marafiki angeweza kutambua udhaifu wao.

    Usiku Nyuta akampa dawa hiyo Pendo, kama alivyopanga, akaenda kujaribu kama kweli hatoweza kuonekana.

    Alipopaka tu, akapatwa na muwasho wa ajabu ukiambatana na maumivu ila ikabidi avumilie tu. Akaenda hadi kule kwenye kikao cha wachawi, na kweli walikuwa wakimsema Nyuta.

    MCHAWI 1: Huyu Nyuta ana majivuno sana kwanza siku za kuja kikaoni anachagua sijui kwavile anajua hatumuwezi.

    MCHAWI WA PILI: Hapa ni kufanya mkakati tu kila mmoja ajitegemee, maana wengine hawana ushirikiano mzuri.

    MCHAWI 3: Kujitegemea haiwezekani jamani tutashindwa kufanya kazi vizuri.

    Waliendelea na maongezi na wala hakuna aliyemuona Pendo kama yupo mahali pale.

    Hakutaka kupoteza muda mahali hapo alitaka bibi yake awasikie ili ajue atakachowafanya kwamaana Nyuta hapendi kutetwatetwa hovyo.

    Badae Pendo akarudi na kumpa taarifa bibi yake.

    NYUTA: Kweli wananisema?

    PENDO: Ndio bibi nimewasikia kwa masikio yangu.

    NYUTA: Basi watajuta.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda huo huo Nyuta na Pendo wakapaka ile dawa na kuondoka kichawi hadi kikaoni. Ile dawa mkipaka wote mnaonana ila asiyepaka hawezi kukuona.

    Wakaanza kuwasikiliza, na bado waliendelea kumteta Nyuta.

    MCHAWI 1: Jamani tufanye mpango wa kumteketeza Nyuta ana majivuno sana.

    MCHAWI 2: Nani atamuweza Nyuta unadhani!!

    Nyuta akachukizwa sana na akajisemea,

    "kabla hawajaniteketeza mimi, naanza na wao"

    Pendo akawa anamuangalia tu bibi yake ambapo Nyuta alichukua dawa na kuisambaza kikaoni hapo. Halafu yeye na Pendo wakaondoka kiuchawi.

    Kesho yake akapata habari kuwa kila mchawi aliyekuwa pale kikaoni ni mgonjwa mahututi, Nyuta akafurahi sana na kusema, "mimi ndio Nyuta bwana, hakuna kinachonishinda chini ya jua"

    PENDO: Duh bibi kweli wewe ni noma jamani, wote chaliii.

    Pendo na bibi yake wakawa wanacheka.

    NYUTA: Na wewe mjukuu wangu utakuwa noma kama mimi nakwambia.

    PENDO: Ndio nanachokitaka hicho bibi yangu.

    NYUTA: Usijari mjukuu wangu utapata, wewe ndiye unanifaa. Wote wamenikimbia lakini wewe umenipenda mjukuu wangu.

    PENDO: Tena nakupenda sana bibi.

    NYUTA: Na leo ndio ile kazi yako ya kafara na kumloga mama yako.

    PENDO: Ndio bibi nilikuwa naingoja kwa hamu.

    NYUTA: Leo hawezi kukwepa hii dawa, lazima aikanyage tu.

    PENDO: Tena mimi si nazijua nyendo zake, lazima nimroge tu atake asitake.

    Pendo na bibi yake wakawa wanajipongeza sana kwa kazi zao.

    NYUTA: Vipi utataka nikusaidie au?

    PENDO: Hapana bibi, hii kazi niachie mwenyewe.

    Muda ulipofika Nyuta akamkabidhi Pendo zile dawa,

    NYUTA: Kuwa makini na hii dawa, anatakiwa aikanyage Marium tu. Akikanyaga mtu mwingine amekwisha.

    PENDO: Bibi niaminie, mimi nazijua nyendo zote za mama. Kwahiyo hapa lazima ajute.

    NYUTA: Au nikusindikize mjukuu wangu?

    PENDO: Hapana bibi, tukienda wote nitajiona sifanyi kazi. Ila itabidi niende mwenyewe bibi nione ujuzi nilioupata.

    NYUTA: Sawa mjukuu wangu.

    PENDO: Sawa bibi.

    NYUTA: Na hii ya kafara mjukuu wangu uwe makini nayo, kwani ukiikosea tu basi huyo mtu mwingine anakuwa kichaa.

    PENDO: Nimekuelewa bibi, nakuahidi kuwa siwezi kuikosea kamwe.

    Nyuta akawa amemaliza kazi yake kwa hapo.

    Muda wa kufanya hizo dawa ukafika kwa Pendo, akatoka na dawa na kuondoka kichawi.

    Kufika mbele akapaka ile dawa ya kutokuonekana na mchawi yeyote.

    Baada ya kupaka hiyo dawa sasa, akaanza safari ya kwenda kwa shangazi yake, akaweka ile dawa ya kafara mlangoni na baada ya hapo akagonga mlango na akajua kwa vyovyote tu shangazi yake atashtuka na kwenda kufungua mlango.

    Akuchukua muda hapo akarudi kwa bibi yake.

    Akamtegeshea ile dawa ya kumroga mama yake mlangoni, na alijua tu kuwa lazima kuna muda bibi yake atatoka.

    Kwavile bibi yake alikuwa ni mchawi tena wa kudumu ikabidi aichanganye na dawa ya kutokuonekana na mchawi, halafu akajifuta ile dawa yake na kwenda kugonga dirishani kwa bibi yake.

    PENDO: Bibi bibi.

    NYUTA: Nini Pendo, hujaondoka tu?

    PENDO: Bado bibi, kuna kitu nimesahau?

    NYUTA: Kitu gani?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    PENDO: Ile dawa ya kutoonekana bibi.

    NYUTA: Ulivyokadhana na hiyo dawa kama vile mama yako nae ni mchawi.

    PENDO: Halafu hapa nje kuna kitu sikielewi.

    NYUTA: Kitu gani?

    PENDO: Njoo ukione bibi.

    Ni kweli Pendo hakuelewa, kwani aliona mti wa hapo nje ukilia na kutoa machozi, ni jambo lililomshangaza sana.

    Nyuta akaanza kufungua mlango ili atoke nje kumbe ule mti ulikuwa unamlilia yeye.





    Nyuta akafungua mlango na kuanza kutoka nje, kumbe ule mti ulikuwa unamlilia yeye.

    Laiti kama Pendo angemwambia kuwa ni mti unalia basi Nyuta angejua mapema cha kufanya kwani angetambua kuwa kuna hatari ya kuikabili huko nje.

    Ila Nyuta hakuwa na shaka ya aina yoyote ile na wala hakufikiria kama Pendo angemuwekea mtego pale mlangoni.

    Nyuta hakuamini kabisa kama angetendwa na Pendo siku ile kwani ilikuwa ni siku ya furaha kwake kummaliza adui yake ambaye ni Marium, mama yake na Pendo. Na alikuwa na furaha siku hiyo kwani Amina angetolewa kafara na nyama yake ingeliwa kwahiyo ingekuwa ni siku ya kwanza kwa Pendo kula nyama ya mtu tena nyama ya dada yake. Kwahiyo Nyuta hakujua kama adui yako yupo nyumbani mwako.

    Nyuta alikuwa ni mtu wa kujiamini sana na alijua kuwa hawezi kutetereshwa na chochote na wala mtu yeyote.

    Alipopita tu pale mlangoni, akakanyaga kitu ambacho kilimrusha kama vile amepigwa na shoti ya umeme.

    Akajikuta tu ametupwa chini, Nyuta akawa anagalagala kwa maumivu, maumivu ya dawa aliyoitengeneza mwenyewe.

    Nyuta aliugulia sana, huku Pendo akiwa anamuangalia tu.

    Nyuta alipotulia, alishindwa kunyanyuka kabisa pale alipoanguka, ikabidi Pendo aende kumnyanyua na kumpeleka ndani, akamlaza kitandani.

    Nyuta alikuwa na hali mbaya sana kwani alijikuta amepooza mwili wake wote, ni kichwa pekee kilichoweza kuzunguka na mdomo kuzungumza.

    NYUTA: (Huku chozi likimdondoka), umenimaliza Pendo.

    PENDO: Nisamehe bibi sikujua.

    NYUTA: Hukujua kitu gani wakati umedhamiria?

    PENDO: Kweli bibi, sikudhamiria. Ni bahati mbaya tu bibi yangu.

    Nyuta alitambua kuwa Pendo alidhamiria kuyatenda yote hayo ila hakuwa na la kufanya kwa muda huo kwani alishawahiwa na Pendo.

    Nyuta na ujanja wake aliwezwa na binti mdogo tu, kwakweli alijisikitikia sana.

    Nyuta akaamua amtume Pendo kwa mwanae Huruma ili akamuite na amsaidie cha kufanya.

    Pendo akaondoka na kwenda hadi kwa shangazi yake.

    Alipofika akawakuta wale watoto mapacha wako peke yao, alipowauliza kuwa mama yao yuko wapi hawakuwa na jibu la kueleweka. Jirani mmoja wa Huruma ndio akamwambia kuwa Huruma ameondoka hapo kama kichaa. Pendo akaelewa kuwa dawa ile imeenda kumtenda shangazi yake.

    Pendo akaamua kuwachukua wale watoto mapacha na kuondoka nao kuelekea kwa bibi yake bi.Nyuta.

    Wale watoto mapacha nao walikuwa ni wachawi kwani walifundishwa kila siku na mama yao. Kwakweli Pendo aliwahurumia sana watoto wale.

    Wakiwa njiani, walipishana na nyumba nyingi zikiwa na misiba, alipojaribu kuuliza ni wale wachawi waliokuwa kikaoni wakimteta Nyuta.

    Hapo ndipo Pendo akagundua jinsi dawa za Nyuta zilivyokuwa na nguvu kubwa na kwa ubaya sasa zimeenda kumdhuru mwenyewe.

    Nyuta huwa akidhamiria kitu kinafanyika kweli, sasa mambo yamemgeukia yeye mwenyewe.

    Walipofika pale kwa Nyuta, Pendo alizidi kushangaa kwani miti na maua yote hapo nje vilionyesha kunyong'onyea mno.

    Walipoingia ndani, swali la kwanza Nyuta aliuliza kuwa mwanae yuko wapi, na Pendo akamjibu kuwa amekuwa chizi.

    Nyuta alisikitika sana.

    NYUTA: Yani Pendo umedhamiria kutuangamiza kweli?

    PENDO: Hapana bibi nilikuwa najaribisha dawa tu.

    Nyuta alisononeka sana na hakuamini kama mjukuu aliyempenda na kumuamini ndiye aliyemtenda vile alivyomtenda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyuta alijikuta akimuelezea Pendo kuhusu kifo cha mama yake.

    NYUTA: Walimuua mama yangu bila hata ya hatia, kwakweli nilifadhaishwa sana nilipoambiwa ukweli ndiomana nimekuwa na chuki hadi leo.

    PENDO: Na mbona ulitaka na mimi nimuue mama yangu?

    NYUTA: Nilitaka utawaliwe na chuki kama ilivyokuwa kwangu kwani hali hiyo ingesumbua akili yako.

    PENDO: Bibi nakupenda ila mama yangu nampenda zaidi.

    NYUTA: Ndiomana ukaamua kunitenda hivi?

    PENDO: Hapana bibi ila nilitaka nijaribishe kwako kwanza kabla ya kufika kwa mama yangu.

    Nyuta alisikitika sana na pia akajilaumu kuwa kwanini alimuamini Pendo kiasi kile. Ila ndio hivyo, alikuwa kitandani na kuinuka tena haiwezekani.

    Pendo alijiuliza sana kuwa kwanini miti na maua isononeke, hakupata jibu ikabidi amuulize huyo huyo Nyuta.

    PENDO: Bibi, mbona miti na maua imenyong'onyea? Na mbona ule mti mwingine ukalia.

    NYUTA: Kwanza tambua kabisa kuwa nje ya nyumba yangu hakuna mti wala ua.

    PENDO: (Akashtuka), bali kuna nini bibi?

    NYUTA: Wale wote ni watu, wanasononeka kuona nateseka. Wale ndio walinzi wangu.

    PENDO: Kivipi bibi?

    NYUTA: Wale ni watu wa kawaida kabisa kama wewe na mimi ila niliwageuza kuwa miti na maua.

    Pendo akabaki akishangaa na kustaajabu maneno ya bibi yake.

    NYUTA: Mimi ni mchawi mkubwa ndiomana nina ulinzi wa kutosha hata nimeshangaa wameshindwa vipi kuniambia kuhusu wewe.

    Hapo Pendo akatambua kuwa kama angeondoka na kutegemea kuwa bibi yake angetoka isingekuwa rahisi vile kwani angekuwa ameshapata taarifa kutoka kwenye wale watu wake wa nje.

    Kwakweli Pendo hakuamini kama ile miti na maua pale nje ni watu, akaamua kutoka nje ili akaiangalie kwa makini zaidi.

    Pendo akiwa nje anaishangaa ile miti na maua huku akiendelea kutafakari kauli ya bibi yake kuwa pale nje hakuna mti wala ua.

    Mara gafla akasikia kelele za juu kutoka ndani, Pendo alijikuta akitetemeka pale nje.



    Mara gafla akasikia kelele za juu kutoka ndani Pendo akawa anatetemeka pale nje.

    Akaamua kusikiliza kwa makini, akagundua ile ni sauti ya bibi yake.

    Pendo akafanya haraka sana kuingia ndani ili aweze kuona nini kinaendelea.

    Alipoingia ndani sasa, akawakuta wale watoto mapacha wameshika visindano vinavyowaka moto wakawa wanamchoma choma Nyuta. Kwanza kabisa Pendo akashangaa sana na kujiuliza wamevitoa wapi vile visindano vyenye moto ila hapo hapakuwa pa kujiuliza sana kwani vile vitoto vilikuwa ni vichawi.

    Pendo akachukizwa sana kwa mambo wanayofanya pale wale watoto.

    PENDO: (Akiongea kwa ukali), acheni!! Mnamfanya nini?

    DOTO: Tunataka kujaribu kumtibia.

    PENDO: Mjaribu kumtibia kwakuwa nyie ni kama nani?

    DOTO: Sisi ni wajukuu zake.

    PENDO: Mnadhani mtaweza?

    KULWA: (Akiongea kwa dharau), unadhani ni jambo la kutushinda hili? Tushafanya mengi sana.

    Mapacha wale wakawa wanacheka.

    Pendo akachukizwa zaidi kwani hawa watoto ni wadogo ila mambo yao na maneno yao ni kama ya watu wazima.

    PENDO: Hivi nyie watoto mna wazimu? Nimewahurumia kumbe na nyie hamfai.

    KULWA: Hata wewe hufai, hujui kuwa huyu bibi ndio kila kitu kwetu?

    PENDO: Mbona msimtibie mama yenu? Hapa ndio mnafanya shobo.

    DOTO: Unaonyesha kutudharau dada, sisi tunajua mambo mengi kushinda wewe.

    Wakaanza tena kumcheka Pendo,

    PENDO: Sio kosa lenu, tatizo uchawi ushakula mifupa yenu. Nitawabadilisha tu ili muwe watoto wa kawaida kama wenzenu.

    DOTO: Sisi sio watoto bwana, kwanza hata wewe tumekuzidi.

    PENDO: Hamfai kabisa nyie.

    KULWA: Unajifanya mjanja sasa wakati siku ile nyumbani tulikuenyesha hadi ukaona nyumba chungu.

    Pendo akakumbuka na kufikiria yaliyompata siku ile alipokuwa kwa shangazi yake, akastaajabu kusikia kuwa yale yote alifanyiwa na watoto wale, kwakweli akaona ubaya wa wale watoto na kugundua kuwa wale watoto ni hatari tena hawafai kabisa. Ingawa mwanzo aliwahurumia ila akaona kwamba wale watoto wanaweza wakamgeukia yeye muda si mrefu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pendo akaona hawa dawa yao ni kuwawahi kwa madawa kabla hawajamuwahi yeye.

    Akachukua dawa na kuwamwagia kwamuda mfupi tu wakawa kama mazezeta, aliwafanyia hivyo ili kumaliza kwanza tatizo la Nyuta.

    Akaona sasa anaweza kushughulikia mambo mengine baada ya kuwatuliza wale watoto mapacha.

    Wakati Pendo anaongea na wale watoto, Nyuta alikuwa kama vile mtu aliyezimia.

    Mara alipozinduka, Pendo akashangaa kumuona Nyuta ameweza kukaa hapo akaelewa kuwa visindano vya wale watoto vilianza kufanya kazi.

    Pendo hakutaka kupoteza muda tena mahali hapo, alienda haraka chumbani kwa Nyuta na kuchukua dawa aliyotengeneza Nyuta kwaajili ya kuwafanya watu mazezeta. Akaenda na kumpaka mgongoni.

    Ikawa ni muda mfupi tu, Nyuta amekaa lakini ni kama zezeta.

    Wale watoto waliweza kumuokoa mikono ila miguu ilikuwa bado kwahiyo Nyuta hakuweza kusimama.

    Nyuta akawa anaongea kama mtu zezeta.

    NYUTA: Yani ndio umeamua kunimaliza kabisa Pendo?

    PENDO: Bibi nataka upumzike kwa unayopenda kufanya.

    NYUTA: Ila hapa unanitesa tu kwani mimi kufa hivi ni ngumu sana kutokana na kitu nilicholishwa nikiwa mtoto labda hadi nitapishwe.

    Pendo akaona kuwa mtihani mwingine umefatia sasa. Kwani ni ngumu sana kumtapisha huyo Nyuta.

    PENDO: Basi bibi kubali nikakutoe uchawi.

    NYUTA: Siwezi kuacha uchawi kwani upo ndani ya damu.

    PENDO: Na je hicho kidude ulichomeza unaweza kutapishwa kweli?

    NYUTA: Yani Pendo nia yako nife ndio uridhike ila ni ngumu sana kwangu kwani dawa ya kunitapisha anayo bibi yangu tu. Wa kule nilipokupeleka na kukwambia tutaenda tena ili ukamilishe uchawi.

    Pendo akakumbuka sura ya yule mbibi inavyotisha, akawaza kama anaweza kumkabili ili apate hiyo dawa.

    Akakumbuka jinsi alivyoenda na bibi yake kule na kulazimishwa kuwa lazima atoe kafara ili arudi kukabidhiwa mikoba ya kichawi vizuri ili awe kama Nyuta.

    Kwakweli Pendo akimfikiria yule bibi anajawa na hofu zaidi bila ya kujua cha kufanya, na hapo akagundua kuwa uchawi umetawala sana na pia upo kama mnyororo ambao umeanzia kizazi hadi kizazi ndiomana kuna wachawi wenye uchawi wa kununua na wale wenye uchawi wa kurithi na wale walioingizwa kwenye uchawi bila kutegemea. Pendo akafikiria mambo mengi bila ya kupata jibu la moja kwa moja.

    Nia ya Pendo ilikuwa ni kumuangamiza kabisa Nyuta na anajua wazi kama Nyuta akiweza kuinuka mahali hapo basi yeye atakuwa mashakani na maisha yake pamoja na nduguze.

    Pendo akawaza sana bila ya kupata jibu la moja kwa moja, sura ya yule mbibi bado ilimtembelea kichwani mwake.

    Akaona ni vyema kama akiweza kujibadilisha na kuvaa mwili wa Nyuta kiuchawi ili aweze kumkabili yule bibi, na uzuri ni kuwa Nyuta mwenyewe amewahi kumfundisha Pendo namna ya kuvaa sura ya mtu kichawi ili ukafanye jambo fulani.

    Ila njia aliyofundishwa ikawa inamsumbua sana akili yake.

    Pendo hakujielewa kwakweli ukizingatia Nyuta ana vibaraka wengi.

    Pendo akajifikiria mambo mengi sana, akaona kama maji ameyavulia nguo basi aamue tu kuyaoga.

    Akajisemea sasa,

    "siogopi kitu, nitasonga mbele hadi kieleweke"

    Pendo alishadhamiria toka mwanzo kuwa lazima amuangamize bibi yake kwani anajua kitendo cha kumuacha kitafanya wazidi kuteketea watu wengi wasio na hatia.

    Siku hiyo akaiweka kuwa rasmi kwa yeye kujifanya ndio Nyuta. Akamuwekea Nyuta dawa zake za usingizi na kuvaa sura ya Nyuta kichawi. Huku akiwa amejawa na uoga na ujasiri pia, akaondoka kichawi na kuelekea kwa yule bibi.

    Akiwa kwenye ngome ya yule bibi sasa, hakujua aanze na njia gani kupata dawa ya kumtapisha Nyuta.

    Akiwa anashangaa shangaa pale, mara akatokea shangazi yake na Nyuta.

    SHANGAZI: Nilijua tu kuwa Nyuta utarudi hapa, yani wewe kila siku unaishia kwa bibi yako tu.

    Kumbe Pendo alikuwa amekosea njia, badala ya kwenda kwa bibi yake na Nyuta akajikuta ameenda kwa shangazi yake na Nyuta.

    PENDO: Nisamehe.

    SHANGAZI: Maajabu haya, toka lini Nyuta umeanza kuomba msamaha?? Inamaana umekuwa wa tofauti siku hizi?

    Pendo hakuwa na jibu kwani hakuweza kuongea kwa ukali kama bibi yake afanyavyo.

    Akawa anajikaza tu kuongea.

    PENDO: Tuachane na hayo, nina shida kidogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SHANGAZI: Una shida? Nyuta wewe uwe na shida!! Maajabu, kuna mtu anayekuweza wewe kweli? Ndiomana nikakupa jina la Nyuta, nilitaka wajue kwamba usipoziba ufa utajenga ukuta. Ushamaliza watu karibia wote hapa kijijini, vipi leo zamu yangu nini?

    PENDO: Hapana, sio hivyo kabisa bali nina shida nyingine.

    SHANGAZI: Mbona umekuwa mpole sana, hadi umeanza kunipa wasiwasi sasa.

    Pendo akajihisi kutetemeka, na akajua wazi wakimgundua tu hapo kama anaigiza basi atakuwa kwenye matatizo makubwa sana.



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog