Search This Blog

UCHAWI WA KURITHI - 5





    Simulizi : Uchawi Wa Kurithi

    Sehemu Ya Tano (5)



    Mara gafla likatokea joka kubwa na kuanza kumfata Pendo huku likitematema mate.

    Lile joka lilikuwa linawaka kama taa, likasogea taratibu hadi kumfikia Pendo, likaanza kujiviringisha kwenye mwili wa Pendo. Likajiviringa hadi kichwani huku likimuangalia Pendo na kutoa toa ulimi wake kila mara. Pendo akawa anatetemeka tu, mara akamsikia mtu akicheka. Alipomsikilizia vizuri akagundua kuwa ni sauti ya bibi wa Nyuta.

    Na mara lile joka likayeyuka na kumuacha Pendo akitetemeka mahali pale, ni hapo ambapo Pendo akagundua ubaya wa bibi huyu kuwa ni zaidi ya alivyofikiria.

    BIBI: Kumbe bado una uoga binti?

    Pendo akabaki kumuangalia tu.

    BIBI: Nilikuwa nakujaribisha ili kupima ujasiri wako, ila wewe bado muoga.

    PENDO: Sio sana ni kiasi tu.

    BIBI: Nilitaka kupima ujanja wako.

    PENDO: (Huku akiendelea kutetemeka), hapana mimi sio mjanja.

    BIBI: Mbona sijapata taarifa yoyote kuhusu kafara, bado hujatoa kwanini??

    Mara shangazi wa Nyuta akadakia,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SHANGAZI: Ila kilichomleta leo si kafara, ametumwa na Nyuta huyo kufata dawa.

    BIBI: (Akahamaki), ametumwa na Nyuta? Kwanini huyo Nyuta asije mwenyewe?

    SHANGAZI: Alikuja jana mama na hukuwepo.

    BIBI: Haya, nitaamini vipi kama ametumwa na Nyuta?

    SHANGAZI: Mama, unakosaje imani kwa binti mdogo kama huyu?

    BIBI: Ni wajanja sana hawa mabinti mwanangu. Haya Pendo nithibitishie kama kweli umetumwa na Nyuta.

    Pendo akatoa kile kibuyu cha bibi yake. Kitendo hicho kilimfanya yule bibi atikise kichwa kuonyesha kwamba amekubali kuwa Pendo kweli ametumwa na Nyuta.

    BIBI: Haya sasa niambie alichokutuma.

    Pendo akamueleza yule bibi kama alivyoelezwa shangazi wa Nyuta jana yake.

    Baada ya hapo shangazi wa Nyuta akatoweka na kurudi kwenye ngome yake. Kwahiyo pale alimwacha Pendo na yule bibi. Pendo akawaza kuwa utetezi mwingine ataupata kwa nani, ila aliendelea kuwa jasiri tu.

    Bibi wa Nyuta akaingia kwenye ngome yake ili kuleta hiyo dawa ya kumkabidhi Pendo.

    Pendo alijihisi ushindi moyoni ingawa hofu kubwa ilikuwa imemjaa.

    Bibi akachukua hiyo dawa na kumpelekea Pendo.

    BIBI: Anayetaka kutapishwa si ndio wewe?

    PENDO: Ndio ni mimi.

    BIBI: Sasa kwanini nisikunyweshe tu hapahapa ili utapike?

    PENDO: Bibi alisema kuwa itakuwa vyema kama hii dawa ataninywesha yeye.

    BIBI: Hataki kusaidiwa? Nyuta hajawahi kuitumia hii dawa ataiweza kweli?

    PENDO: Alisema nielekeze mimi tu.

    BIBI: Hii dawa mwambie akologe uji achanganye nayo halafu unywe na nyingine akupake kifuani hadi tumboni.

    PENDO: Sawa nitamwambia.

    BIBI: Kwani amekulisha kitu gani?

    PENDO: Sijui, ni bibi mwenyewe ndio anajua.

    Pendo akaona kuwa kuendelea kukaa hapo ni sawa na kugundulika anachopanga kwenye akili yake.

    Yule bibi akaingia kwenye ngome yake na Pendo akawa anajiandaa kuondoka kichawi ili arudi kwa bibi yake. Mara kuna mjusi akamuangukia Pendo kwenye bega, alikuwa na mjusi mkubwa sana tena ni mjusi wa ajabu kwani aliweza kuongea.

    MJUSI: Mimi ni mtu, ni wewe pekee unayeweza kuniokoa.

    PENDO: (Huku akitetemeka), kivipi?

    MJUSI: Nisaidie tafadhari, mimi na mwanangu tunateseka huku.

    Pendo akawa anaogopa bila ya kuyaelewa mambo yale. Yule mjusi nae akaendelea kumsisitiza kuwa amsaidie.

    Pendo akajiuliza kuwa atamsaidiaje huyo mjusi.

    Yule mjusi akamuomba Pendo aingie kwenye ngome ya bibi wa Nyuta na kuitoa fimbo ya mlangoni kwani ndio uzima wao.

    Pendo akawaza sana, akaona sasa kazi itakuwa ngumu.

    Akamuhurumia yule mjusi aliyekuwa akilalamika kuwa anahitaji msaada.

    Ikabidi afanye ujanja wa kuweza kuipata hiyo fimbo aliyoambiwa.

    Akiwa na ile dawa yake mkononi, akahisi kuipoteza akiingia nayo kwenye kutafuta hiyo fimbo.

    Ikabidi atafute sehemu ya mbali na hapo na kuificha ile dawa kichawi.

    Akaanza kujipanga sasa namna ya kuipata hiyo fimbo aliyoambiwa.

    Kuingia tu kwenye mlango wa yule bibi, akakutana na fuvu la mtu. Pendo akaogopa sana, kwakweli huyu bibi alionyesha kuwa ni hatari zaidi ya Nyuta.

    Pendo akaanza kupapasa ili apate hiyo fimbo, akaona fimbo moja chini ile kuigusa tu ikageuka nyoka. Pendo akaitupa pale chini nayo ikageuka kuwa fimbo tena, Pendo uoga ukamjaa. Akajiuliza kama fimbo yenyewe ndio hiyo au kuna nyingine.

    Akajiuliza maswali mengi bila ya kupata jibu, ikabidi atoke na kukimbilia kwa yule mjusi.

    PENDO: Mbona fimbo yenyewe nikiishika inageuka nyoka? Ndio hiyo kweli?

    MJUSI: Ndio ni hiyo, huyo bibi ni mchawi sana tena ni mtu hatari sana unatakiwa uwe na tahadhari.

    PENDO: Nitaibeba vipi wakati inageuka nyoka.

    MJUSI: Wewe ibebe tu kuna muda itageuka kuwa fimbo tena cha muhimu uwe jasiri tu.

    Pendo akajipanga kwenda tena kuchukua ile fimbo.

    Akiwa anakaribia kuelekea, akamuona yule bibi akiwa pale nje ya ngome akizungukazunguka.

    Pendo akaogopa, akaamua kumuuliza yule mjusi.

    PENDO: Itakuwaje sasa?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MJUSI: Subiri ataondoka tu, yule bibi usimuone ni mzee vile. Ana machale sana yule bibi.

    Pendo akazidi kushangazwa na mambo ya ajabu ya yule bibi.

    Baada ya muda yule bibi akaondoka, Pendo akaenda tena ndani ya ngome.

    Kuinua ile fimbo akageuka ngoka na kadri alivyozidi kumshika ndivyo alivyozidi kuwa mkubwa. Pendo akazidi akajawa na uoga, akatamani amtupe ila akajipa ujasiri na kuendelea kumbeba.

    Alipotoka nae nje tu akageuka na kuwa fimbo tena na hapo Pendo akawa na uhuru zaidi wa kuibeba ile fimbo.

    Akaenda nayo mpaka kwa yule mjusi, na kuuliza cha kufanya ili amsaidie. Yule mjusi akamuomba Pendo amchape na ile fimbo kichwani, Pendo akafanya hivyo mara gafla yule mjusi akageuka na kuwa mama wa makamo.

    Pendo akashangaa sana na kustaajabu yale mambo.

    Yule mama akamwambia Pendo kuwa waondoke eneo lile haraka kwani yule bibi akishtuka watakuwa na hali ngumu sana mahali hapo.

    Pendo na yule mmama wakaondoka kiuchawi na kwenda hadi eneo aliloweka dawa huku ameshika ile fimbo mkononi.

    Walipochukua ile dawa wakaondoka hapo hadi nyumbani kwa Nyuta ili wakaongee vizuri.

    Walipofika pale kwa Nyuta, yule mmama akamwambia kuwa ile miti na mauwa pale nje kwa Nyuta ni watu kwahiyo hata hao wanaweza kuokolewa na ile fimbo aliyoishika Pendo.

    Wakiwa bado wanashangaa, mara gafla kikatokea kitu kinachowaka kama mbalamwezi na kuanguka pale kwenye uwanja wa Nyuta.

    Pendo na yule mmama wakaanza kujawa na mashaka.



    Mara gafla kikatokea kitu kinachowaka kama mbalamwezi na kuanguka kwenye uwanja wa Nyuta.

    Pendo na yule mmama wakaanza kuogopa na kutetemeka.

    Ile kitu ikawa inatoa mwanga mkali zaidi kila muda unavyozidi kwenda, Pendo na yule mmama walijikuta wakiumizwa macho sana na ule mwanga hadi wakajaribu kuchukua mikono yao ili kuziba ule mwanga.

    Wakati Pendo anafanya kitendo kile cha kujiziba sura, mara akajikuta kama ameinua ile fimbo ambayo ikaelekea kwenye ule mwanga.

    Na gafla ule mwanga ukapungua na kuzima kabisa.

    Pendo akashangaa sana kile kitendo, wakabaki wakiangaliana na yule mmama.

    MMAMA: Inaonyesha kuwa hiyo fimbo ina nguvu sana.

    PENDO: Nadhani hivyo ila ni nini kile?

    MMAMA: Itakuwa ni makombora ya yule bibi ndio yameanza kutufatilia.

    PENDO: Tutafanyaje sasa?

    MMAMA: Ilimradi hiyo fimbo inauwezo wa kutuliza basi tusijari sana.

    Pendo aliona kuwa haya mambo ni miujiza tu.

    Wakaingia ndani, Pendo hakutaka kuiweka hata chini ile fimbo ila vilevile hakutaka bibi yake aione ile fimbo.

    Akamuomba yule mmama aishike ili yeye akazungumze na bibi yake ila yule mmama akagoma.

    MMAMA: Sikia binti, mimi sihusiki kwenye huyu bibi, hiyo fimbo itanidhuru tu. Bora wewe.

    Pendo hakujua aiweke vipi ile fimbo. Ikabidi aendelee kuishikiria.

    Ila akamuomba yule mmama amsaidie kukoleza moto ili wapike uji.

    Ila alihisi kuchelewa pia.

    Akaamua kwenda kumtazama kwanza bibi yake wakati yule mmama akikoleza huo moto.

    Pendo akaingia chumbani na kumkuta bibi yake amejilaza kama alivyomuacha.

    Akainama chini na kuiweka ile fimbo ili bibi yake asimuone nayo. Halafu ndio akamsogelea ili kuzungumza nae.

    PENDO: Pole bibi.

    NYUTA: Asante, umepata dawa lakini?

    Nyuta alionekana mpole sana yani kama sio yule Nyuta machachali.

    PENDO: Ndio nimepata bibi.

    NYUTA: Nipe basi ninywe.

    PENDO: Inapaswa nikuchanganyie na uji, basi ngoja nikakoroge uji bibi.

    NYUTA: Sawa nangoja Pendo.

    Pendo akatoka na kuiacha ile fimbo palepale chini alipoiweka.

    Aliporudi jikoni alikuta moto umekolea na akabandika chungu cha uji kwenye moto.

    Ndipo yule mmama akaanza kumuuliza Pendo.

    MMAMA: Nyuta ndio bibi yako?

    PENDO: Ndio, kwani vipi?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MMAMA: Chanzo cha mimi kuwa vile nilivyo ni huyo huyo Nyuta.

    PENDO: Kwani alifanyaje?

    Yule mmama akaamua kumueleza Pendo yaliyomtokea kabla.

    MMAMA: Ni muda mrefu sana tangu nimegeuzwa kuwa mjusi.

    Nyuta alipokuwa mtoto mchanga wakati mama yake ndio amekuja kule kijijini nilimuhurumia sana yule dada, nikaona kuwa hana hatia. Nikamwambia dada yangu kuwa tumsaidie yule dada.

    Dada yangu ndio yule aliyekuleta pale kwa yule bibi.

    Yule ni dada yangu ambaye tumechangia baba na yule bibi ni mama yangu wa kambo.

    Dada akamwambia ukweli halisi mama wa Nyuta. Na ni hapo walipojua kuwa nimemwambia mimi kumbe sio mimi.

    Hilo halikuwa tatizo sana kwani nilipewa onyo tu, ila tatizo lilikuja pale Nyuta alipotambua ukweli juu ya kuuwawa kwa mama yake.

    Aliyemwambia ni dada yangu ila nikasingiziwa mimi si unajua tena siku zote mnyonge anaonewa.

    Ni hapo mama na kundi lake wakachukia na wakaamua kunipa adhabu, wakanifungia kwenye chumba cha giza. Kuna kipindi nikajaribu kutoroka, Nyuta akanikamata, alikuwa mdogo kwangu ila na nguvu kubwa ya kichawi.

    Aliponikamata akanirudisha kwa bibi yake na ndio hapo nilipopewa adhabu ya milele kwani niligeuzwa na kuwa mjusi.

    Nilifurahi sana kusikia maongezi yenu kwani nilijua wewe ndio ukombozi wangu.

    PENDO: Pole sana, kwahiyo wewe jina lako halisi ni nani?

    MMAMA: Naitwa Maria.

    PENDO: (Pendo akapatwa na hofu kidogo), ulirudishwa huko kipindi gani? Yani Nyuta alipokukamata.

    MMAMA: Nilishangaa kwanini Nyuta alinikamata wakati sijawahi kumkosea, alinikamata kipindi alipokaribia kuolewa kwani ndio kipindi nilichotoroka.

    PENDO: Inaonyesha bibi anachukizwa sana na hilo jina, pole sana.

    MMAMA: Asante, yani kule lazima uwe mchawi kwanza.

    PENDO: Kwahiyo hata wewe ni mchawi?

    MMAMA: Ndio nilikuwa mchawi ila ni uchawi wa kulazimishwa.

    Wakazungumza ya hapa na pale.

    Ni hapo ambapo ule uji ukawa tayari, na Pendo akamuomba yule bibi asitoke kule jikoni ili Nyuta asishtuke kumuona mtu yule.

    Pendo akachukua ile dawa na kuikoroga kwenye uji halafu akampelekea bibi yake.

    NYUTA: Mbona umechelewa sana Pendo, hutaki nipone jamani.

    PENDO: Usijari bibi yangu, nataka sana upone.

    Akachukua ule uji na kuanza kumnywesha bibi yake.

    Alipomaliza kunywa, akachukua na ya kumpaka kifuani hadi tuponi akampaka.

    Akainuka na kukaa mara akaiona ile fimbo ambayo Pendo aliiweka chini.

    Nyuta akashtuka sana na kuanza kuuliza,

    NYUTA: Umeitoa wapi ile fimbo Pendo? Umeitoa wapi? Wewe ni binti muuaji!

    Nyuta aliunganisha maswali mengi mengi bila ya majibu, hadi Pendo akamshangaa.

    Mara sura ya Nyuta ikaanza kubadilika, sauti yake ikawa ya kukoroma.



    Sura ya Nyuta ikabadilika na akaanza kukoroma.

    Pendo alikuwa pembeni yake akimuangalia tu na kikubwa ni kuwa alikuwa akimngoja atapike kile alicholishwa utotoni. Ila alimuona Nyuta akikaa vizuri huku akiweka mikono yake shingoni na kuanza kutapatapa kama mtu anayetaka kutapika.

    Ila hakutapika, kitendo hicho kilimshangaza Pendo kwani alingoja na kungoja ila Nyuta hakutapika.

    Ndipo Pendo akaamua kurudi jikoni na kwenda kuzungumza na yule mmama.

    Pendo akaamua kumweleza ukweli halisi na kwanini ameamua kufanya ayafanyayo.

    PENDO: Nia yangu atapike kile alicholishwa utotoni.

    MMAMA: Ila dawa si umeshampa?

    PENDO: Ndio, nilimpa pamoja na ule uji ila nashangaa hadi sasa hatapiki. Kwani unaweza kutambua ni nini tatizo?

    MMAMA: Tatizo ni kuwa, kitu alicholishwa Nyuta ni cha kurithi. Sasa inatakiwa apatikane mtu wa kukirithi.

    PENDO: Itakuwaje sasa?

    MMAMA: Unatakiwa wewe ukubali kukirithi.

    PENDO: kwani hakina madhara?

    MMAMA: Hakina madhara ila humfanya mtu ateseke sana pale muda wake wa kufa unapofika.

    PENDO: Bibi hapana mimi sitaki kurithi hicho kitu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MMAMA: Asante kwa kunipa heshima ya ubibi Pendo.

    PENDO: Usijari wewe ni kama bibi yangu, nakuomba tutafute njia nyingine ila sio ya mimi kurithi. Sitaki matatizo zaidi maishani.

    MMAMA: Njia nyingine ni kuwa tumbebe Nyuta hadi mtoni ili akatapikie huko kwani kile kitu huwa kinataka kikitoka kiweze kutembea na kwenda kwingine.

    PENDO: Tufanye hivyo basi ili tuwahi.

    Basi Pendo na yule mmama wakaamua kufanya mpango wa kumbeba Nyuta ili kumpeleka huko mtoni.

    Wakaingia chumbani kwa Nyuta, na Nyuta alipomuona yule mmama alichukia sana alitamani kusema kitu ila alishindwa sababu ya kile kitu kilichomkaba kooni.

    Yule mmama ndiye aliyeamua kumbeba Nyuta mgongoni, na kumwambia Pendo aibebe ile fimbo ili waende nayo pamoja.

    Pendo alipoibeba ile fimbo ikageuka kuwa nyoka yani ikafanya kama ilivyofanya wakati wapo kule kwa bibi wa Nyuta, kwakweli kwa mtu asiye na ujasiri hawezi kuibeba ile fimbo kama Pendo afanyavyo.

    Pendo alikuwa ni mtu jasiri sana kwani aliweza kufanya mambo mengi kwa ujasiri alionao.

    Safari ya kuelekea mtoni ikaanza na Pendo akijihesabia ushindi moyoni kwani hapo atakuwa amekamilisha lile lililompeleka pale nyumbani kwa Nyuta.

    Walipofika mtoni, wakaingia katikati ya maji na kumshusha Nyuta, yule mmama akamwambia Pendo kuwa amchape Nyuta na ile fimbo mgongoni ili awe kama anamshtua. Na kweli baada ya kufanya hivyo Nyuta alishtuka na kuanza kutapika.

    Akatapika kitu kisicho na rangi yani kipo kama maji ila ni cha mviringo na kinalepweta. Kikaangukia kwenye maji na kuondoka kikifata uelekeo wa maji yale.

    Pendo na yule mmama wakamchukua Nyuta na kutoka ndani ya yale maji.

    PENDO: Kwahiyo kile kitu ndio kimeondoka?

    Yule mmama akamzuia Pendo kama ishara kuwa hawatakiwi kuongea chochote mahali hapo. Pendo akawa anamshangaa kwani hakujua masharti hayo kabla.

    Tangu Nyuta atapike kile kitu akawa amezimia kwa muda na hakuona chochote kilichoendelea mahali pale.

    Wakati wanataka kuondoka, mara kikatokea kitu na kuanguka mbele yao. Ilikuwa ni sanamu ila yenye umbo la mnyama.

    Sanamu ile ikaanza kuwafata, Pendo na yule mmama wakawa wanaogopa. Pendo akataka tena kusema kitu ila yule mmama akamzuia Pendo kusema kwa kidole bali alimuonyesha ishara kuwa anyanyue ile fimbo na kuielekeza kwa sanamu yule, naye Pendo akafanya kama alivyoamriwa na hapo hapo ile sanamu ikatoweka. Yule mama hakutaka wajadili jambo lolote mahali hapo bali waanze safari ya kurudi na wakafanya kama walivyokwenda yule mmama akambeba Nyuta na Pendo nae akaishika ile fimbo vilevile hadi wakafika tena nyumbani kwa Nyuta.

    Wakiwa nyumbani kwa Nyuta wakampeleka Nyuta chumbani kwake na kumlaza.

    Pendo akaamua kuhoji kwanini alikuwa anazuiliwa kuongea.

    PENDO: Mbona ulikuwa unanikataza kuzungumza?

    MMAMA: Hairuhusiwi kabisa kuongea, unaona ukataka kuzua tatizo lingine!

    PENDO: Kwahiyo lile sanamu lingetudhuru?

    MMAMA: Ndio lingetudhuru.

    PENDO: Asante bibi kwa kunisaidia mambo haya.

    Pendo akaenda kumuonyesha yule mmama wale watoto mapacha walioonekana kulegea sana.

    Ikabidi wawape ule uji uliobaki ili kuwatia nguvu.

    MMAMA: Usijari kuhusu hawa watoto, kumtoa mtoto uchawi si kazi ngumu kama ilivyo kwa mtu mzima.

    PENDO: Tena mtu mzima mwenye moyo kama wa Nyuta.

    MMAMA: Ni kweli, si rahisi kwa mtu kama Nyuta kuacha uchawi.

    Pendo akaendelea kuwaza namna ya kumteketeza Nyuta kwani kila kitu kilikamilika kilichobaki ilikuwa mauti ya Nyuta pekee.

    Pendo na yule mmama wakiwa kwenye chumba cha Nyuta.

    NYUTA: Pendo umeamua kunimaliza mimi ila tambua kwamba kuna watu kama mimi wengi sana.

    PENDO: Ila wewe ni zaidi kwani umetutesa sana.

    Pendo aliongea kwa ujasiri mkubwa sasa.

    NYUTA: Na wewe Maria hata sijui na nani aliyekutoa.

    MMAMA: Umenichukia bila sababu ya msingi Nyuta.

    NYUTA: Yupo Maria mwenzako kwenye jeneza, ni miaka na miaka sasa.

    Pendo akashtuka sana na kugundua kuwa mtu aliyemuona kwenye jeneza kuwa nae ni Maria.

    PENDO: Bibi kwanini unawachukia?

    NYUTA: Maria alipendwa na Yusuphu sitaacha kumchukia Maria kwani alifanya Yusuphu asinipende mimi kabisa.

    PENDO: Hata kama bibi, ila Maria aliyekuchukiza ni mmoja iweje sasa uwachukie wote wakina Maria? Nakumbuka hata rafiki yangu aliyeitwa Maria ni wewe uliyemuua bibi, kwanini ufanye hivyo?

    NYUTA: Maria alifanya nisipendwe, na kama angekuwa anaitwa Pendo basi ningewachukia Pendo wote duniani.

    Ni hapo ambapo Pendo akagundua kuwa bibi yake anakisasi cha kudumu moyoni mwake.

    Ni hapo akauliza kwa yule mmama.

    PENDO: Na mbona bado inakuwa ngumu kummaliza Nyuta.

    MMAMA: Kumbuka Nyuta ni mchawi wa muda mrefu tena uchawi wake ni wa kurithi inatakiwa kuwa makini sana katika kumuangamiza.

    PENDO: Tutafanyaje sasa?

    MMAMA: Nadhani hilo jeneza lenye mtu ni kiashirio tosha cha mauti ya Nyuta.

    Yule mmama na Pendo wakapanga mkakati wa kumuokoa Maria aliyewekwa kwenye jeneza kwani uzima wa Maria huyo ndio itakuwa mauti ya Nyuta.

    Wakajiandaa kutoka ili kwenda kutimiza mipango yao.

    Wakati wanatoka nje wakakutana na bonge la joka lenye asili ya chatu yani ni lile joka lililomviringa Pendo akiwa kwa bibi wa Nyuta.

    Sasa Pendo alihisi mpambano mkali kwani lile joka lilikuwa ni kiashirio kikubwa cha yule bibi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati wanatoka nje wakakutana na bonge la joka lenye asili ya chatu yani ni lile joka lililomviringisha Pendo alipokuwa kwa bibi wa Nyuta.

    Sasa Pendo akahisi mpambano mkali kwani lile joka lilikuwa ni kiashiria kikubwa cha yule bibi.

    Pendo na yule mmama wakaanza kurudi nyuma kwa uoga mwingi, wakahofia maisha yao kwa hofu kubwa sana.

    Lile joka lilizidi kuwasogelea, mmama akamwambia Pendo amnyooshee fimbo lile joka, naye Pendo akafanya kama alivyoambiwa ile kunyoosha tu ile fimbo lile joka likatoweka. Pendo hakuamini macho yake kama lile joka limetoweka kweli mahali pale.

    MMAMA: Hiyo fimbo ndio ukombozi wetu Pendo.

    PENDO: Natumaini itatusaidia hadi mwisho.

    MMAMA: Hata mimi natumaini hivyo Pendo.

    PENDO: Basi tufanye haraka katika kumteketeza Nyuta.

    Pendo na yule mmama wakaondoka eneo lile na kwenda kwenye ile nyumba iliyohifadhiwa misukule.

    Wakaingia ndani na kuona kuwa hali ni mbaya sana, kulikuwa na harufu mbaya tena za ajabu ajabu. Hapakueleweka kama ni nyumba waliyoishi watu mwanyoni.

    Kila siku ndivyo ile nyumba ilivyodhidi kuwa na hali mbaya. Hawakutaka kupoteza muda wakishangaa wakaamua kufanya walichofata mahali pale. Wakaenda moja kwa moja kwenye kile chumba ambacho Nyuta amehifadhi vitu vyake.

    Kuangalia huku na kule Pendo akashangaa bila kuona tena lile jeneza.

    PENDO: Mbona halipo tena? Inamaana Nyuta ameweza kufanya hivyo akiwa na hali mbaya kiasi kile?

    MMAMA: Pendo, hapa kazi ipo. Lazima kuna kitu tumekosea hebu jaribu kukumbuka.

    PENDO: Sasa nitakumbuka nini bibi?

    MMAMA: Kwani mara ya mwisho ulifata nini humu?

    PENDO: Nilikuja kuchukua kibuyu cha bibi.

    MMAMA: Kiko wapi?

    PENDO: Nimekiacha kule kwa bibi.

    MMAMA: Hilo ni tatizo, katika uchawi hata kibuyu hufanya kazi kama ya binadamu cha msingi ukakilete hapa.

    PENDO: Basi twende tukakifatilie hicho kibuyu kwa sasa.

    Ikabidi warudi tena nyumbani kwa Nyuta kufata kile kibuyu.

    Wakiwa pale kwa Nyuta, Pendo akijaribu kutafuta kile kibuyu wakamuona Nyuta akicheka, Pendo akapatwa na hasira sana kwani mambo ya bibi yake hayakumpendeza hata kidogo.

    PENDO: (Akimuangalia Nyuta kwa jicho la chuki), unacheka nini sasa?

    NYUTA: Nakucheka unavyohangaika kukazana kuniua mimi.

    PENDO: Na kwataarifa yako si mimi nitakayekumaliza, bali utamalizwa na hao watu uliowatesa.

    NYUTA: Sasa wewe inakuuma nini wakati sijakutesa wewe?

    PENDO: Usitake kunikumbusha machungu, nina hasira sana na wewe Nyuta.

    NYUTA: Yani mimi si bibi yako tena?

    PENDO: Sikupendi na nachukizwa kuwa na bibi kama wewe, umenipotezea baba yangu na nimebaki yatima sina baba kwajili yako. Ukaona haitoshi ukammaliza na kaka na bado ukataka kummaliza mama sasa nakuwahi kabla hujaniacha mtupu kabisa. Najua huna ujanja tena hapo, ngoja kifo chako tu.

    Nyuta akajihisi kunywea na kujihisi kuwa na hatia kubwa moyoni mwake kwa yote aliyoyafanya.

    Mara kibuyu kikaonekana, Pendo akachukua kile kibuyu na kuondoka nacho.

    Kwakweli Pendo alishangazwa sana na uchawi wa Nyuta na wala hakuhisi kama ingekuwa ngumu kiasi hicho katika kumuangamiza.

    PENDO: Sikufikiria kama ni vigumu kiasi hiki.

    MMAMA: Nyuta ni mkongwe wa uchawi, elewa hivyo Pendo na ubaya zaidi ana vingi vya kumsaidia.

    PENDO: Ila naamini tutashinda tu bibi.

    MMAMA: Hata mimi nategemea hivyo.

    Wakaendelea na safari yao ya kwenda kwenye ile nyumba.

    Wakaenda tena kwenye ile nyumba hadi kwenye kile chumba, wakakuta lile jeneza na maiti yake ndani kama kawaida. Hapa ndio Pendo akaona jinsi uchawi na vinyamkera vyake vinavyosaidiana katika kazi zao.

    PENDO: Sasa ndio tunafanyaje?

    MMAMA: Ipige hiyo maiti kichwani na mgongoni na hiyo fimbo. Halafu mwenyewe atarudi.

    PENDO: Inamaana huyu sio mwenyewe?

    MMAMA: Huo ni mwili wake tu ila mwenyewe hayupo hapo.

    Basi Pendo akachukua ile fimbo na kuipiga ile maiti kama alivyoambiwa kwakweli ni kitendo cha ujasiri sana kukifanya, Pendo alikuwa ni binti jasiri.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ya ile maiti ikaanza kubadilika, hata rangi yake nayo ikaanza kubadilika mara akainuka na kukaa pale kwenye lile jeneza, kitu kilichowashangaza wote ni kuwa ile maiti pia ilishtuka kujiona ndani ya jeneza, ila sasa haikuwa maiti tena bali alikuwa ni mtu mzima kabisa.

    Aliposhtuka pale kwenye jeneza alitoka kwa hofu huku akitaka kukimbia, Pendo na yule mmama ndio waliomshikiria na kumtuliza kwani alikuwa ni mtu asiyejielewa kabisa.

    Wakamtuliza kwa dawa zao kwanza.

    Wakamfata na yule paka mwenye sura ya binadamu naye wakamchapa akageuka kuwa mtu, huyu alikuwa akishangaashangaa na kustaajabu tu.

    Pendo na yule mmama wakaona kuwa sasa inatosha. Na wakaona kuwa hao wawili ndio wanafaa kummaliza Nyuta.

    Wakarudi nyumbani kwa Nyuta na watu wale.

    Wakaenda nao hadi chumbani kwa Nyuta, alipowaona alishtuka sana. Nyuta hakuamini macho yake kuwaona watu wale alishangaa sana.

    Wakiwa pale ndani wakashangaa kusikia upepo ukivuma kwa kasi sana nje.

    Pendo na yule mmama wakaenda kuangalia wakaliona lile joka la mwanzo likija tena.

    Pendo akanyoosha ile fimbo kama mwanzoni lakini safari hii mambo yakawa tofauti kwani lile joka liliendelea kuwafata.

    Wakapatwa na uoga wa hali ya juu, kikasikika kicheko nyumba nzima, walipoisikiliza vizuri wakagundua kuwa ni sauti ya yule bibi wa Nyuta. Sasa mpambano kamili ukawa kwenye kikaango katika kuanza.



    Kikasikika kicheko nyumba nzima, waliposikiliza vizuri wakagundua kuwa ni sauti ya bibi wa Nyuta.

    Sasa mpambano kamili ukawa katika kikaango kuanza.

    Sauti ya yule bibi ikaendelea kusikika na hakuna aliyejua cha kufanya.

    Pendo akafanya kitu cha haraka sana na hakuna aliyefikiria kwa muda ule kuwa Pendo yuko wapi, kwani walimuona Pendo akiwa amelala kwenye kitanda alicholala Nyuta.

    Kwakweli yule mmama alishangaa sana kwani walipokuwa wamekimbilia chumbani kwa Nyuta, alimuona Pendo akiwa pale kitandani, alishangaa kwavile alipoangalia huku na kule hakumuona Pendo wakati walikimbia wote, alijiuliza maswali mengi kuwa Pendo ameelekea wapi na Nyuta je ameenda wapi.

    Yule mmama hakuelewa kitu, kwakweli akakodoa macho tu wala asijue kinachoendelea.

    Mara yule bibi wa Nyuta akatokeza sasa, yule mmama akiwa mwenyewe na wale watu waliopumbazika akazidi kuogopa, akaanza kulia kwa hofu huku akitetemeka.

    Yule bibi alienda moja kwa moja pale kitandani na kuanza kumkaba mtu wa pale kitandani, yule mama hakuelewa kama anayekabwa pale ni Nyuta au ni Pendo.

    Yule bibi alimkaba yule mtu hadi akammaliza na alipommaliza tu sura ya yule mtu ikabadilika na kuwa ya Nyuta ni hapo yule mmama alipomuona Pendo akiwa nyuma ya yule bibi na upanga halafu akamfyeka nao shingoni.

    Chumba chote kilitapakaa damu, Pendo alitetemeka sana kwa jambo alilofanya akamkimbilia yule mmama na kumkumbatia kwa hofu.

    Hali ilikuwa mbaya sana mule chumbani.

    Hakuna aliyeweza kukitazama chumba kile mara mbili mbili.

    Pendo hakuamini kuwa ni yeye aliyefanya kitendo cha ujasiri namna ile.

    Lilikuwa ni jambo la kustaajabisha sana, yule mmama akamuuliza Pendo alichofanya kwani alitokea kimaajabu.

    Kumbe Pendo aliamua kuibadili sura ya Nyuta na kuweka sura yake ili Nyuta amalizwe na bibi yake mwenyewe ila Pendo hakuweza tena kupambana na huyo bibi kichawi ndiomana akaamua kuchukua upanga na kummaliza.

    PENDO: Sikuwa na jinsi yoyote, ilinibidi nifanye hivi.

    MMAMA: Wewe Pendo ni binti shupavu, hongera sana.

    Kwakweli yule mmama aliushangaa sana ujasiri wa Pendo.

    Wakaona wasipoteze wakati mahali hapo, wakaamua kumbeba Nyuta na bibi yake kichawi na kwenda kuwaweka nje ya pango la shangazi wa Nyuta. Walifanya hivyo huku wakijipanga kwa shambulizi lolote litakalotokea mbele yao kwani walijua fika kuwa bibi wa Nyuta ni mtu mwenye jeshi kubwa sana.

    Mara shangazi wa Nyuta akatokea, Pendo akiwa na hasira na ghadhabu.

    PENDO: Na wewe amua moja unaacha uchawi au huachi?

    SHANGAZI: (Huku akijawa na hofu), niko tayari kuacha.

    Basi Pendo na yule mmama na shangazi wakarudi nyumbani kwa Nyuta lengo likiwa moja tu kuacha uchawi na kurekebisha vyote vilivyokosewa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ilikuwa bado ni mbaya sana pale nyumbani kwa Nyuta. Ikabidi wamtumie huyu shangazi wa Nyuta kuweza kuwafungulie wale misukule wa Nyuta kwani huyu alikuwa na uwezo mkubwa wa kichawi kushinda wao.

    Walipoenda kuwafungulia hao misukule ndio huko wakawakuta na wale wamama vichaa wawili wakiwa nje ya nyumba hiyo, hapo hapo wakaamua kuwazindua, wale wamama wakajishangaa sana kujiona katika hali halisi hawakutegemea kuwa vile walivyo.

    Wakafanya pia kazi ya kurudisha misukule wazima na wale waliokufa basi wakafa kweli.

    Kitu kilichomshangaza Pendo ni kuwa baada ya kuzindua wale misukule ile miti iliyokuwa nyumbani kwa Nyuta karibia yote haikuwepo.

    Kwakweli Pendo alishangaa sana namna ambavyo uchawi unavyoweza kutafuna dunia, na kuona jinsi gani Nyuta aliwafumba watu macho kwa uchawi wake.

    Wakaenda pia kumchukua yule Huruma kichaa na kumtoa uchizi huku wakimpa sharti moja la kuacha uchawi naye akakubali kufanya hivyo.

    Na wale watoto mapacha pia wakawatoa ile hali ya uzezeta. Na ni hapo walipomuita mganga kuwatoa wote, watoto wale kwa wakubwa wakatolea alama za kiuchawi.

    Wakatoa vitu vyao vyote vya uchawi na kuvichoma moto.

    Watu wote waliozinduliwa walibaki kushangaa tu, hakuna aliyeelewa kitu kwa wakati huo. Mama Huruma na mama Yusuphu hawakujielewa kabisa kwani hawakufikiria kupona na kupata uzima wao.

    Pendo alikuwa ni binti jasiri sana.

    Watu wote waliozinduliwa walikuwa ndani ya nyumba ya Nyuta.

    Shangazi wa Nyuta na watu wote wakasaidiana kuzisafisa zile nyumba ile ya Nyuta na ile aliyohifadhi misukule. Walitoa uchawi wote uliotapakaa humo.

    SHANGAZI: Hata mimi nilikuwa nauchukia uchawi ila sikuweza kukataa ili nimridhishe mama yangu.

    PENDO: Ningependa mambo yote ya kichawi tuachane nayo na tumrudie Mungu kwa sasa.

    SHANGAZI: Nakubaliana nawe Pendo, Mungu ndio kila kitu.

    Basi Pendo, Huruma na watoto wake, yule mmama na shangazi wa Nyuta wakaenda kwenye maombi na kukiri kuwa wanaachana na mambo yote ya uchawi. Na kuwa wameamua kumrudia Mungu kwani Mungu ndio kila kitu katika maisha.

    Ni hapo ambapo wale waliokuwa misukule waliopona wakatakiwa warudi kwa ndugu zao.

    Na Pendo akaita familia yake yote, ambapo walifikia ile nyumba ya misukule ambayo sasa haikuwa na misukule wala uchawi tena.

    Familia ya Pendo ikafikia hapo.

    Wote walifurahi sana, Yusuphu na Nina walifurahi kumuona mama yao mama Yusuphu, na kwa bahati mtoto mmoja wa mama Huruma aitwaye Rehema alipona katika wale misukule naye alifurahi sana kuwa katika maisha halisi. Kwakweli ilikuwa ni furaha, ingawa Yusuphu alipoteza watoto karibia wote ila alibakiwa na huyu Huruma ambaye kwa sasa alikuwa Huruma safi asiye na uchawi tena.

    Ilikuwa ni furaha sana, Maria akiwa mzima kabisa ni Maria yule yule aliyependwa na Yusuphu.

    Waliwakumbuka pia Mussa na Abra, wakawaombea wapumzishwe kwa amani.

    Yusuphu na Maria wakakumbatiana kwa furaha, huku Pendo akiwa mshindi wao katika vita vile.

    Familia nzima ilikumbatiana kwa furaha.

    MARIUM: Asante sana Pendo kwa kuokoa hili jahazi.

    PENDO: Yote yaliyotokea nyuma ni madhara ya UCHAWI WA KURITHI aliokuwa nao bibi yangu Nyuta.

    Nitauchukia uchawi siku zote za maisha yangu, uchawi wa aina zote duniani ninauchukia milele.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ~~MWISHO~~





0 comments:

Post a Comment

Blog