Search This Blog

NYUMBA YA MISUKULE - 1

 







    IMEANDIKWA NA : ATUGANILE MWAKALILE





    *********************************************************************************





    Simulizi : Nyumba Ya Misukule

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Wakiwa wamejiinamia kwenye benchi la hospitali waliyompeleka baba yao, Amina na mdogo wake Pendo walikosa raha kabisa kwani baba yao alianguka gafla tu na hakuna ajuaye alianguka kwa sababu ya nini.

    Daktari akamuita Amina na kumuuliza,

    DAKTARI: Kwani ni kitu gani kimemuangusha mzee wenu?

    AMINA: Kwakweli hatujui kwani baba alikwenda kuoga ndio hivyo akaanguka bafuni.

    DAKTARI: Mama yenu yuko wapi?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    AMINA: Mama amesafiri na nyumbani tumebaki sisi wawili tu na baba.

    DAKTARI: Vipi hakuna mtoto wa kiume kwenu?

    AMINA: Yupo kaka yetu mkubwa ila kwa sasa yupo masomoni nje ya nchi.

    Daktari akaishia hapo kuuliza maswali.

    Baada ya siku mbili yule mzee aliyejulikana kwa jina la Mussa akapewa ruhusa ya kurudi nyumbani lakini alikuwa amepalalaizi, hakuweza kuongea tena wala kutamka neno lolote, watoto wake Amina na Pendo wakamsaidia baba yao hadi nyumbani.

    Maisha ya kuishi na mtu aliyepalalaizi ndani yakawa magumu kwao kwani hawakuwahi kumuhudumia mgonjwa yeyote yule.

    Mama yao, bi.Marium alikuwa sehemu ambayo hata mawasiliano yalikuwa tatizo kwahiyo hakuweza kupata taarifa yoyote kuhusu ugonjwa wa mumewe, hadi pale alipoamua kurudi nyumbani na kukutana na ile hali ya mumewe kupalalaizi.

    BI.MARIUM: Kwani baba kafanyaje? (aliwauliza binti zake).

    AMINA: Mama, hata haijulikani vizuri kwani baba alianguka gafla bafuni, tumempeleka hospitali ndio hivyo tumerudi nae amepalalaizi.

    BI.MARIUM: jamani, mume wangu mbona imekuwa hivyo wakati sipo?

    Akiwa na majonzi mengi baada ya kumwangalia mumewe asiyeweza kutamka jambo lolote, alijikuta machozi yakimtoka.

    Siku moja wakati mama huyo amemaliza kumuhudumia mumewe, akamuona kama akifurukuta pale kitandani huku mipande ya damu ikimtoka mdomoni, yule mama alijikuta akitetemeka sana na kuamua kuwaita wanae, nao pia wakabaki wakistaajabu ile mipande ya damu, wakaamua kuomba msaada ili kumnyanyua baba yao na kumpeleka hospitali.

    Walipofika hospitali, yule mgonjwa akawaishwa kwenye matibabu ila gafla daktari akaja na taarifa mbaya.

    Aliwapa taarifa ya kifo cha bwana Mussa, kwavile walikuwa wote wanawake hakuonekana mwenye moyo wa ujasiri pale, ikabidi wapate msaada kwa majirani waliowapeleka pale hospitali.

    Wakarudi nyumbani wakiwa na majonzi mengi, kilio kikatawala kwenye nyumba yao, kila mmoja alilia kwa namna yake ya alivyompenda mzee huyo.

    Mara nyingi kwenye misiba ndio hutokea vitu vingi vya ajabu ajabu, kwanza kabisa ukatokea mtafaruku wa mahari watakapomzika yule mzee, ndugu wakasema akazikwe kwao alipozaliwa, mke na watoto wakataka aizikwe pale pale karibu na wanapoishi. Basi mtafaruku ukawa mkubwa sana, hakuna anayekubali. Mama mkwe wa bi.Marium akiongea kwenye simu na bi.Marium huku kavimba kwa hasira juu ya mazishi ya mwanae,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MAMA MKWE: Hivi unang'ang'ania mwanangu azikwe huko wewe kama nani?

    Bi.MARIUM: Mama, hata mimi pia nina haki kwani huyu ni mume wangu na nimeishi naye muda mrefu sana. Napenda azikwe karibu na tunapoishi ili iwe rahisi kutembelea kaburi lake.

    MAMA MKWE: Hivi mama na mke nani mwenye mamlaka? Unajua usinichanganyishie mada wewe, huyo ni mwanangu na inabidi aje huku kwanza afanyiwe mila ndipo azikwe.

    Bi.MARIUM: Mama, nimetuma gari ikufate ila umegoma kuja, hata mila inawezekana kabisa kufanyiwa huku. Mbona baba amekubali jamani.

    MAMA MKWE: Wee endelea kung'ang'ania usivyovijua na vitakutokea puani mwehu wewe.

    Yule mama mkwe akakata simu.

    Bi.Marium akiwa na mawazo mengi, ikabidi akaongee na baba mkwe ambaye naye alikuwepo pale msibani.

    BI.MARIUM: Baba, wewe umeturuhusu mazishi tufanyie hapa, mbona mama anafoka sana?

    BABA MKWE: Achana nae, hapa tupo kwenye majonzi. Nyie pangeni taratibu za mazishi vizuri twende tukazike.

    BI.MARIUM: Asante baba.

    Siku ya mazishi ikapangwa na wote wakawa katika mazishi ya mzee yule huku wakibaki na majonzi. Taratibu zote zikafanyika na wakamaliza kuzika.

    Ila Hawakumtaarifu mtoto wa kiume wa ile familia aliyekuwa masomoni kwani alikuwa kwenye mitihani wakahofia kumpa mvurugo wa mawazo.

    Usiku wa siku hiyo ya mazishi, ndani ya nyumba wakiwa wamebaki bi.Marium, Amina, Pendo na ndugu zao wengine wa karibu, mvua kubwa ikaanza kunyesha huku radi zikipiga mfululizo mara umeme nao ukakatika, kila mmoja akashindwa kwenda kutafuta kiberiti ili wawashe mshumaa kwani kila mmoja alikuwa na hofu kwenye moyo.

    Amina na Pendo na mama yao walijikuta wakiwa wamekumbatiana kwa uoga, na hali ikazidi kuwa mbaya kadri mvua ilivyozidi kunyesha kwani kuna sauti ambazo zilianza kusikika mule ndani bila kujua zinapotokea. Kila aliyekuwemo kwenye nyumba hiyo alijawa na hofu na mashaka. Mara wakashangaa milango ya pale sebleni ikifunguliwa, kila mmoja hofu ilizidi kumtanda kwani hakuna aliyepata ujasiri wa kufanya chochote, wote walijawa na uoga.

    Mara kukawa na watu kama wanatembea na kuongea ila hakuna hata mmoja mule ndani aliyeelewa kuwa waliongea vitu gani.

    Hali ikazidi kuwa mbaya kila dakika iliposonga na miguu ya watu kutembea mule ndani ilisikika kwa kishindo kikubwa, hakuna aliyeelewa kuwa ni kitu gani kinatembea.



    Wakiwa wote hawajielewi mule ndani, mara wakapitiwa na usingizi na hakuna aliyeshtuka hadi kunakucha.

    Baada ya kuamka, kila mtu akawa anashangaa tu na hakuna aliyeweza kumweleza mwenzie juu ya tukio la usiku wa siku ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya siku mbili kukaa na kufanya maongezi mbali mbali wale ndugu wa karibu wakaaga na kuondoka, kwahiyo ikabiki familia tu mama na binti zake wawili. Kutokana na uoga, mama huyo akawa akilala pamoja na binti zake hao.

    Wakiwa kwenye maongezi ya hapa na pale,

    AMINA: Ila mama hii nyumba yetu inatisha kweli siku hizi.

    BH.MARIUM: Ni kweli mwanangu, ila hapa ni nyumbani hatuwezi kupakimbia.

    PENDO: Kweli kabisa mama, ila karibia nitakuacheni hapa kwani mie nitaenda kukaa hostel za chuo.

    BI.MARIUM: Aaah Pendo! Usiende kukaa hukohuko bhana, mtaniacha mpweke hapa. Itabidi uwe unaenda na kurudi mwanangu.

    PENDO: Na Mariana atarudi lini? Maana nimeshachoshwa na kazi za hapa.

    BI.MARIUM: Atarudi hivi karibuni, nimeshaongea nae.

    Mariana ni mfanyakazi wa ndani kwenye hii familia, na kama ilivyoada kuna watu wengine hawatajwi. Yani ile kumuulizia tu, naye akawa mlangoni amerudi. Wakampokea na kumkaribisha, huku akizidi kuwapa pole kwani hakuwepo kwenye msiba wa mzee Mussa.

    Baada ya wiki mbili kupita, mtoto wao aliyekuwa masomoni akawa amerejea.

    Walipokaa na kumpa taarifa ya msiba wa baba yake akajikuta akichukia sana.

    ABRA: Mama, kwanini mlinificha juu ya msiba wa baba yangu mwenyewe?

    BI.MARIUM: Tusamehe baba ila hatukutaka tukuchanganya na mitihani mwanangu.

    ABRA: Mama, unaweza kuniambia mitihani na baba yangu kipi bora?

    BI.MARIUM: Tafadhari mwanangu, naomba msamaha.

    Kijana yule akawa amejawa na hasira tena kupita maelezo.

    Nae mama yake akazidi kumbembeleza na kumsihi kuwa awasamehe.

    Ila hakuonekana kuwaelewa kabisa.

    Akaenda chumbani kwa mama yao na kuchukua funguo ya gari, akaenda nje na kupanda gari na kuondoka zake.

    Baada ya muda kidogo, akaja mtu ndani ya nyumba yao huku jasho likimtoka, yule mtu alisikika akisema

    "mama Amina, mwanao kapata ajari"

    Bi.Marium akapagawa kabisa na huo ujumbe, akajikuta akitoka mbio mbio hadi eneo la tukio.

    Kufika eneo la tukio, anakuta ajali aliyopata mwanae ni kuwa amegonga mpapai, ila gari haikuharibika popote na cha kustaajabisha ni yule kijana kukutwa ndani ya gari damu zikimtoka.

    Watu wakamtoa mule kwenye gari na kumuwaisha hospitali, na mashuhuda wa lile tukio walisema kuwa ile gari haikuwa na mwendo kasi sana ila hata wao walishangaa imeenda kugonga mpapai.

    Wakiwa hospitalini, daktari anawaletea taarifa kuwa yule kijana amekufa.

    Kwakweli bi.Marium alihisi kurukwa na akili, alitamani ardhi ifunguke ajifukie humo.

    Wakiwa na hudhuni na majonzi kwa kifo cha Abra, kila mmoja alijiuliza kivipi afe kwa kugonga mpapai tena mpapai ambao hata haujakomaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuna mwenye jibu la moja kwa moja juu ya msiba ule.

    Wote wakawa na hudhuni huku mawazo mengi yakitawala. Ndipo bi.Marium akapigiwa simu na mkwe wake.

    MAMA MKWE: Usiniambie kuwa hata mjukuu wangu utamkatazia kuzikiwa huku.

    BI.MARIUM: Mama, tupo kwenye majonzi, si vizuri kuanza kugombea maiti.

    MAMA MKWE: Kama unatambua hilo basi acha maiti ya mjukuu wangu ije kuzikiwa huku.

    BI.MARIUM: Mama sikuelewi kwakweli, kwanini wapenda tushindane kwenye misiba? Huyu inapaswa azikwe karibu na baba yake.

    MAMA MKWE: Niliyajua yote hayo kabla ndiomana nikasema mwanangu aje azikiwe huku.

    BI.MARIUM: Acha marumbano mama, tuwaache marehemu wapumzike kwa amani.

    Akaamua akate ile simu, huku akiwa haelewi kwanini mama mkwe wake anafanya vile.

    Akakaa na ndugu wa karibu na kupanga taratibu za mazishi.

    Siku ya mazishi ndio balaa lilipoanza.

    Wakati wapo makaburini kuzika, mara gafla ikaonekana lile kaburi ni dogo.

    Mama wa marehemu akazidi kulia huku wachimbaji wakiongezea upana wa kaburi.

    Walipomaliza, wakataka kuzika, wakaona lile kaburi limejaa maji. Kwakweli kila mtu alistaajabu yale matukio. Mara baba mkwe akamuita bi.Marium pembeni.

    BABA MKWE: Kwani kuna tatizo gani hadi inashindikana kuzika?

    BI.MARIUM: Baba, hata na mimi nashangaa kwakweli. Sijui nini kinaendelea!

    BABA MKWE: Uliongea na bibi yake?

    BI.MARIUM: Ndio na akasema msiba tupeleke kule.

    BABA MKWE: Nilijua tu.

    Wakiwa wanaendelea kujadili namna ya kuzika, mvua kubwa ikaanza kunyesha pale makuburini, kitu kilichofanya watu wasambaratike kwenye makaburi yale. Kila mtu alikimbilia eneo atakalojikinga na mvua ile.

    Vijana wenye nguvu wakaenda ili kulibeba jeneza na kulitoa pale kwenye mvua ila kila walipojitahidi ilishindikana kwani lilikuwa zito sana, hakuna aliyeweza kulinyanyua lile jeneza.

    Ikabidi na wao wakimbie kwenye maeneo ya kujikinga na ile mvua.

    Bi.Marium alizidi kulia, alitamani abaki pale makaburini karibu na lile jeneza la mtoto wake ila watu wakamtoa eneo lile na kumuingiza kwenye gari.

    Mvua ilizidi kunyesha huku na maradi yakipiga katika eneo lile.



    Ile mvua ikasababisha kuwe na baridi kali sana eneo lile, mara gafla walipoangalia lile jeneza waliloacha pale makaburini likawa limetoweka. Wakiwa katika kustaajabu yale, ikawa kufumba na kufumbua jeneza limerudi ila likiwa tofauti na lile la mwanzo, na mvua nayo ikakatika muda huo huo.

    Kila mtu alishangaa na kustaajabu yale matukio ila hakukuwa na jinsi zaidi ya kuzika kwani ndio kitu walichoenda kufanya pale makaburini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikabidi vijana hodari wasogee eneo lile kwaajili ya kuendelea na mazishi.

    Mara akasikika bi.Marium akilia,

    "hapana jamani, huyo mnayemzika sio mwanangu jamani"

    Ila watu wakaamua kumpotezea kwani washapoteza muda mwingi katika mazishi yale, walijua yule mama anasema vile kwakuwa bado haamini kama mtoto wake amekufa, kwahiyo wakaamua kuzika kinguvu tu na cha kushangaza muda huo lile kaburi lililokuwa limejaa maji mwanzo kwa muda huo lilikuwa kavu kabisa.

    Baada ya mazishi yale watu wakasambaratika hata hivyo hawakuwa wengi sana kwani baadhi yao walikimbizwa na ile mvua kwahiyo wakarudi majumbani mwao.

    Wakiwa nyumbani, kila mmoja alionekana kutafakari lile tukio la pale makaburini. Mara, Pendo akamsogelea mama yake,

    PENDO: Mama, unajua bado sielewi kabisa.

    BI.MARIUM: Hata mimi sielewi mwanangu, yani moyo wangu unaniambia kuwa mwanangu hajafa.

    PENDO: Kwanini mama?

    BI.MARIUM: Kwanini jeneza lilibadilishwa wakati mvua inanyesha? Na je lilibadilishwa na wakina nani?

    PENDO: Mama, hali hii inatisha na kuogopesha kwakweli. Maana hata ukimsimulia mtu atadhani unamwambia mambo ya kwenye sinema.

    BI.MARIUM: Yani mwanangu, lile tukio limefanya machozi yanikauke kabisa. Hadi sasa sielewi kitu.

    Baada ya msiba na matanga kuisha, watu walisambaratika kwani kila mmoja alirudi kwenye familia yake. Na wanafamilia wakabaki pale kwao.

    Siku moja bi.Marium akatembelewa na rafiki yake mama Sarah.

    Akamkaribisha vizuri na wakaongea mambo ya hapa na pale.

    MAMA SARAH: mama Amina ndugu yangu, siku zote mtu atakunyima chakula lakini si maneno.

    BI.MARIUM: Kivipi tena ndugu?

    MAMA SARAH: Ndugu yangu wee, haya matukio ya kwenye misiba hapa kwako umeyaonaje?

    BI.MARIUM: Ni ya ajabu sana hata nashindwa kuyaelewa.

    MAMA SARAH: Bibi weee kuna mkono wa mtu hapa si bure.

    BI.MARIUM: Kivipi? Hebu nieleweshe.

    MAMA SARAH: Kwanza kabisa elewa kwamba matukio ya kuanguka bafuni sijui mara chooni mara nyingi huwa ni mambo ya kishirikina.

    Mara gafla wakati akiendelea kuongea, wakasikia kishindo kikubwa kutoka kwenye paa na wote wakashtuka na kujikuta wakiangaliana na kuulizana "nini??"

    kila mmoja alimwangalia mwenzie kwa mshangao,

    MAMA SARAH: (Huku akiinuka), mmh mama Amina kwaheri.

    BI.MARIUM: Mbona hivyo tena?

    MAMA SARAH: Hapana mwenzangu siwezi sema tena, hiko kishindo kimenitisha.

    BI.MARIUM: Hapana ndugu usiondoke.

    MAMA SARAH: Kama wewe mwenye nyumba kishindo cha nyumbani kwako unaniuliza mimi nini, mmh nimepatwa na uoga wa gafla.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara, Mariana akaja pale sebleni akitokea jikoni,

    BI.MARIUM: (Akimuuliza Mariana), eti na wewe umesikia hiko kishindo mwanangu?

    MARIANA: ndio nimesikia mama ila itakuwa mipanya hiyo.

    MAMA SARAH: Mmh! Nyumba nzuri hivi iwe na panya kwenye darini? Wanapitia wapi??

    MARIANA: Mmh! Mama Sarah na wewe kama hujui jinsi panya walivyowajanja? Hapa cha msingi ni kuwawekea sumu tu.

    Mara kishindo kikasikika tena. Safari hii wote wakatoka nje ya nyumba, walipofika nje wakaanza kuchekana kwa uoga,

    MARIANA: Loh! Kumbe mama ndio muoga namna hiyo? (huku akicheka)

    BI.MARIUM: Hata wewe ni muoga, mbona nawe umekimbia.

    Wote wakachekana pale nje, ikawa muda huo Amina na Pendo wakaingia getini.

    Basi wakawashangaa tu wale pale nje na wakazidi kuchekana,

    AMINA: Kwahiyo ndio wote nyie mmekimbia panya ndani? Loh watu wengine ni watu wazima hovyo kweli. (huku akiwacheka).

    Basi Amina, Pendo na Mariana wakaingia tena ndani na kuendelea na shughuli zao kama kawaida, pale nje wakamwacha mama yao na rafiki yake wakisindikizana.

    MAMA SARAH: Basi ndio hivyo ndugu, ila ukitaka msaada niambie mimi nitakusaidia. Kwani kuna mganga maarufu yupo Sumbawanga namfahamu.

    BI.MARIUM: Sawa ndugu, nimekuelewa.

    Siku zikawa zinapita, ila kukawa na mambo ambayo yalikuwa yakiwashangaza mule ndani, ikabidi bi.Marium awaite wote Amina, Pendo na Mariana ili aongee nao.

    BI.MARIUM: Mnajua mchezo mnaofanya siku hizi sio mzuri.

    PENDO: Mchezo gani mama?

    BI.MARIUM: Yani nanunua mchele, unga, maharage na mboga karibu zote ila kidogo tu eti vimeisha, au mnabeba na kuwapelekea mabwana zenu nyinyi.

    AMINA: Mama, siwezi kufanya hivyo hata siku moja.

    Na wote wakakataa madai hayo.

    BI.MARIUM: Kwamaana hiyo, chakula chote huwa kinapikwa?

    MARIANA: Tena mama bora umeongea, maana hata mimi nashangaa. Usiku utakuta wali umebakia kwenye sufuria ukija asubuhi eti umeliwa wote. Hata sielewi nani mwenye tabia hiyo.

    PENDO: Kuhusu kiporo tukuulize wewe mwenyewe Mariana maana hakuna anayehusudi kiporo humu ndani zaidi yako.

    BI.MARIUM: Jamani, tuache hayo marumbano ila ninachoomba ni kila mmoja kuwa mwangalifu na mwingine na mwisho wa siku tutajua tu kuwa huu mchezo unafanywa na nani kati yetu.

    Ila karibia wote wakamuhisi Mariana kuwa anagawa chakula nje kwavile hajui uchungu wa kukisaka.

    Siku moja, Pendo akiwa kwenye harakati zake za kula ila awahi kwenda kwenye semina.

    Akachukua chakula na kuweka mezani ili kiwe kinapoa na yeye akaenda kuvaa.

    Alivyotoka chumbani, anaangalia mezani chakula hakipo, yani kimeliwa chote na sahani kuwa tupu kabisa. Ikabidi amuite Mariana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    PENDO: Jamani Mariana, ndio mchezo gani huu wa kula chakula changu wakati jikoni kipo?

    MARIANA: Jamani, Pendo unanisingizia bure tu, mie hata sijala chakula chako hata hivyo nimeshiba na siwezi fanya hivyo.

    PENDO: Sasa nani amekula? Maana mama amelala na dada Amina hayupo, hapa ni mimi na wewe, nani amekula sasa?

    MARIANA: Hata na mie sijui, labda mbwa kaingia ndani kala.

    PENDO: Mariana ni wewe umekula maana unaleta maneno hata ambayo hayawezekani, maana huyo mbwa aingilie wapi wakati amefungiwa kwenye banda lake.

    MARIANA: Tuache kubishana basi, lete sahani nikakuwekee chakula kingine.

    Pendo akawa amekaa pale mezani kwa hasira na Mariana akaenda jikoni kumwekea Pendo chakula kingine.

    Mara gafla Mariana akaanza kupiga kelele kwa nguvu huku akimuita Pendo, hadi mama yao aliyekuwa amejipumzisha kwa muda huo akashtuka





    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog