Simulizi : Niliolewa Na Mganga Kwa Tamaa Ya Cheo Kazini
Sehemu Ya Pili (2)
ILIPOISHIA:
Kingine kilichonikosesha raha ni kuzaa mtoto asiyejulikana aliingiaje nilijua huo ndiyo mwanzo wa kuzaa kiumbe wa ajabu na kunifanya niwe mtu wa kuandikwa katika vyombo vya habari. Lakini wasiwasi mwingine niliamini kauli za Rose kuwa huenda ni njama za Mbwana za kutaka kunikosanisha na mganga wangu, mpenzi wangu hata bosi wangu wa kazi ili nami nikose kazi. Lakini mbona mganga hakuonesha ushirikiano zaidi ya kuweka mzaha mbele?
Kabla ya kufika nyumbani nilimpigia simu Rose tukutane kwangu baada ya muda wa kazi ili nimweleze niliyokutana nayo kwa mzee Sionjwi.
SASA ENDELEA…
Rose alinieleza kuwa atafika kwa muda tuliopanga.
Nilipofika nyumbani baada ya kuingia ndani hata bila kuvua nguo nilizotokanazo safari, nilijilaza kichwa kilikuwa kimechanganyikiwa na kushindwa nifanye nini kila nililolifikiria lilikuwa mzigo kichwani mwangu.
Mwili ulikuwa umechoka vibaya hata usingizi ulivyonipitia sikujua, nilishtushwa na sauti ya simu iliyokuwa ikiita. Nilipoangalia nilikuta ni Rose niliipokea.
“Haloo Rose vipi upo wapi?”
“Shosti nimepiga kengele zaidi ya mara kumi hakuna jibu vipi umetoka?”
“Wapi shoga! Nimo ndani, dada wee acha tu tutazungumza, ngoja nije nikufungulie mlango.”
Nilinyanyuka mwili ukiwa umechoka kama mgonjwa wa malaria hadi mlango mkubwa na kumfungulia Rose, baada ya kufungua alinishangaa.
“Vipi shoga ulilala muda mrefu mbona macho yamevimba?”
“Tangu nilipokupigia simu mpaka sasa hivi, yaani wee acha tu hata sijui nifanyeje?” Nilisema kwa kukata tamaa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwani vipi?” Rose aliniuliza kwa kunishangaa.
“Kwa vile umefika nitakueleza masaibu yaliyonifika hili naona ni zito kuliko yote.”
Nilimkaribisha ndani Rose ambaye alionesha kunishangaa kwa jinsi nilivyokuwa na maneno yangu. Baada ya kuketi nilimletea kinywaji kisha nilikwenda kuoga kabla ya mazungumzo kutokana na mwili wangu kuwa mchovu sana.
Baada ya kuoga nilikaa kwenye kochi lililotazamana na Rose na kuanza kumuelezea nilichomuitia. Nilimuhadithia yote niliyokutana nayo katika safari yangu nzima juu ya majibu ya mzee Sionjwi yaliyonikatisha tamaa. Baada ya kunisikiliza alishusha pumzi ndefu na kusema kwa sauti ya chini.
“Mmh, ipo shughuli shoga yangu lakini kwa nini usiutoe ujauzito huo?”
“Mmh, nilisahau mzee Siojwi amesema nisithubutu kuutoa ujauzito ule eti nitakutana na balaa.”
“Sasa itakuwaje nawe unasema bwana wako hataki mtoto na anaujua mzunguko wako vizuri?”
“Rose kukuita hapa nimepoteza uwezo wa kufikiri nahitaji msaada wako.”
“Msaada wangu mkubwa ni kwenda kuutoa hata kama kasema mtoto atafanana na yeye na pia mpenzio hatang’amua bado ni doa, kama yeye haoni marafiki zake watamweleza tu…
“Mmh, najiuliza mtoto azaliwe afanane na mzee Sionjwi japo siamini mtu akutokee ndotoni ukifanya naye mapenzi mtoto afanane naye mbona nasi tunafanya mapenzi na watu ndotoni haijatokea. Halafu bado siamini kama hiyo ni mimba kweli japo vipimo vinaonesha ujauzito wa mtoto wa ukweli.”
Mwenzangu hapo ndipo nachanganyikiwa au mzee Sionjwi kaniingilia kimazingara, halafu huwezi kuamini penzi la ndotoni lilikuwa likinikata kiu kuliko la bwana wangu ambaye niliona alinipaka shombo tu.”
“Mmh! Makubwa kama ulilifurahia penzi la mzee Sionjwi la ndotoni basi furahia mlelee ujauzito wake na umzalie mtoto.”
“Mmmh! Makubwa sura kama ngedere nitaiweka wapi?”
“Lakini mimi nakushauri ukaitoe hii mimba ili tujipange upya.”
“Lakini kabla ya kuitoa hebu nipeleke kwa mtaalamu mwingine ili niangalie atanisaidia vipi.”
“Hilo nalo neno niachie leo kesho ukija kazini nitakujulisha au nitakupigia simu.”
Baada ya mazungumzo yaliyochukua zaidi ya saa tatu niliagana na Rose ambaye aliondoka hata kabla sijaingia ndani bwana wangu aliingia. Ajabu nilijikuta nikimchukia sana tofauti na zamani, sikupenda kumuona pale siku ile.
Bila kunielewa nilimuuliza swali hata sijui nililitoa wapi na kupitia mdomoni mwangu.
“Mhu, unasemaje?” nilimuuliza bila kumkaribisha ndani.
“Niseme nini mbele yako kipenzi changu.”
“Lakini wewe si una mkeo?”
“Swali gani hilo sweet?”
“Nataka jibu wewe si una mke?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo sweet kwani ulikuwa hujui?”
“Basi kama una mkeo hapa unafuata nini?”
“Efrazia unatania au upo serious?”
“Bado hujanijibu umekuja kufanya nini?”
“Hebu acha utani, utani huo si mzuri wakati huu, si unajua mwenzio amesafiri leo nitakuwepo mpaka asubuhi.”
“Koma tena ukome ujana ule wapi uniletee uzee wako, nimechoka kugeuzwa kibanda cha kupumzikia, kama una shida na mimi nenda kwa wazazi wangu utoe posa ili unioe.”
“Kwani tatizo nini?”
“Sitaki maelezo nasema tokaaa,” nilimfukuza.
“Sweet vipi?”
“Sweet mkeo.”
Nilimsukuma nje na kufunga mlango kwa ndani, sikumsikiliza alivyokuwa akinibembeleza nilikaa chini na kuangua kilio niliona yote yale yametokana na kutaka maisha kwa njia ya mkato.
Nilijiuliza ujauzito ule nitaupeleka wapi, wazo la kutoa lilikuwa la kwanza lakini nilijifikilia kama umeingia kichawi ni vigumu kutoka kizungu.
Kila nilipofika hapo nilizidi kuchanganyikiwa nililia mpaka sauti ikakatika huku nikijipigiza chini.
Hata usingizi ulivyonipitia sikujua nilishtukia siku ya pili asubuhi nimelala mlango wa kutokea nje. Nilikwenda hadi bafuni kuoga kitumbo kilichoanza kuvimba kilizidi kuumiza moyo wangu.
Wakati mwingine niliona kama vile mchezo wa kuigiza lakini dalili zote za ujauzito wa kuchagua vyakula kichefuchefu nilikuwa nazo kitumbo nacho kilianza kuvimba.
Baada ya kuoga hata bila kunywa chai nilimpigia simu Rose anipeleke kwa mtaalamu wa miti shamba ili kujua hatima ya ujauzito ule. Niliposhika simu yangu nilikuta zaidi ya ‘missed calls’ 30 na ujumbe mfupi zaidi ya SMS kumi, zote zikiwa za bwana wangu za kuniomba msamaha na kuniahidi yupo tayari nimpe muda ili arekebishe suala letu la ndoa.
Sikutaka kumjibu kwa vile sikutaka kuchanganya madawa, akili yangu yote ilikuwa kwenye tumbo la muujiza. Niliapa siku ya kuitoa sitakanyaga tena kwa mzee Sionjwi pengine kuachana na kujihusisha na ushirikina na kurudi kuungama kanisani.
Nilimpitia Rose tulipokubaliana na kuelekea maeneo ya Mbagala- Kibonde Maji kuna mtaalamu toka Muheza. Tulifika kwa mtaalamu majira ya saa mbili na nusu asubuhi.
Watu hawakuwa wengi hatukuchukua muda mrefu kufika kwa mganga ambaye alikuwa mwanamke wa umri wa kati, hakuwa kijana sana wala mtu mzima sana.
Baada ya kukaa alituuliza:
“Mnataka kuzungumza na walimu?”
“Ndiyo” alijibu Rose naye alikuwa havumi lakini yumo.
“Alichukua udi kwenye boksi na kuuwasha kisha akiuweka pembeni ya pua na kuuvuta taratibu akiwa amejifunika shuka jeupe kichwani baada ya muda alianza kutikisa kichwa.
“Asalamu aleykumu walimwengu,” mganga alitoa salamu kwa sauti nyembamba.
“Waleykum salamu,” tuliitikia wote.
“Haya walimwengu mna shida gani?”
“Mwenzangu kuna kitu kinamsumbua.”
Alinishika mkono kichwani kwa muda kisha aliniachia na kusema kwa sauti ya chini.
“Wewe nafanyiwa mchezo mbaya na fundi iliyokusaidia, nakuingilia usiku si ndoto ni kweli kabisa na kiumbe si jini ni kiumbe ya kweli kabisa.”
“Sasa mwalimu utatusaidia vipi tulitaka utusaidie kuitoa.”
“Yule fundi naifunga kama naitoa inaondoka na mtu.”
“Sasa tufanye nini?”
“Ni kurudi kuiomba inaweza kukubalieni na kuitoa.”
“Wewe huwezi?”
“Kama nitaitoa na mama yake itafuata.”
“Una maana gani mama yake kuifuata?” Rose alimuuliza mimi nilikuwa kimya nimechanganyikiwa na kitendo alichonifanyia mganga.
“Kumfuata si kufa?”
“Mungu wangu, kwa hiyo?”
“Ni kuitunza mpaka azae au kumuomba mwenyewe awaruhusu kuitoa”
Mmmh kisu kiligusa mfupa tulirudi njia nzima nilikuwa naendesha gari nikilia kwa uchungu wa kubakwa kichawi na mganga.
“Efrazia usilie, tujaribu kurudi kwa mganga kumuomba huenda akakusikiliza na kukuondolea tatizo.”
“Mmh, sidhani acha twende kwa vile muda unaruhusu.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************
**********************
*******************************
“Marahaba, samahani kwa kukuchelewesheni kwa vile jana mlikuja ghafla sikuwa na dawa hivyo nilidamka alfajiri bado kiza.”
“Hakuna tatizo babu.”
“Pumzikeni kazi itakuwa jioni baada ya jua kuzama, kazi yako inafanyika kabla ya jua kuchomoza na baada ya jua kuzama.”
Tulitazamana na tusipate jibu kwa vile muda ule ilikuwa ndiyo saa saba mchana, hatukuwa na jinsi ilibidi tuwe wapole kusubiri muda huo. Nikiwa nimekaa na Rose nilishangaa aliponieleza.
“Eflazia nakuja,” alisema huku akinyanyuka.
“Unakwenda wapi?”
“Aah, nakuja.”
Sikutaka kubishana naye kwa vile ni mtu mzima japo sehemu ile alikuwa ni mgeni. Nilimuona akielekea kwenye shamba la mzee Sionjwi lililokuwa na mazao na miti mingi ya aina mbalimbali.Sikuelewa alikuwa anakwenda wapi, nilisubiri kwa muda huku nikijilaza kwenye jamvi. Baada ya nusu saa kupita niliingiwa na wasiwasi juu ya Rose kuondoka na kuchelewa kurudi, huku akiwa mgeni maeneo yale.
Nilinyanyuka taratibu na kuifuata njia aliyopita, nilitembea taratibu huku nikipepesa macho. Nami sehemu ile sikuwahi kufika zaidi ya kuishia kwake.Njiani nilikutana na embe mbichi zilizoning’inia na mapera yaliyoiva, niliangua mawili na kula kisha niliendelea na safari yangu, njia yote sikubahatika kumuona mtu kitu kilichonitia wasiwasi na kujiuliza Rose atakuwa amekwenda wapi.
Shauku ya kuingia zaidi iliniingia na kusogea mbele huku ujasiri wa kumtafuta Rose ukiongezeka kwa kuhofia kumpoteza rafiki yangu kimuujiza. Baada ya kusogea mbele zaidi kwenye miti na majani mengi nilisikia sauti ya watu wawili wakizungumza. Niliposikiliza vizuri niligundua sauti ya kike ni ya Rose na ya kiume ni ya mzee Sionjwi.
Nilijiuliza wanafanya nini kule, wazo lilikuwa labda wanachimba dawa, lakini sauti ya Rose ilinishtua pale nilipomsikia akisema:
“Babu inatosha na siku nyingine.”
“Basi mjukuu namalizia.”
Mmh, sauti zile sikuzielewa zilikuwa zinamaanisha nini japo ziliniweka njia panda. Wazo kuwa huenda wanachimba dawa, sikutaka kuwashtua nilinyata mpaka kwenye zile sauti na kufanikiwa kuwaona.
Japo ilikuwa kweli lakini bado macho yangu hayakukubali, mzee Sionjwi na Rose walikuwa wakifanya mapenzi. Japo ni jambo la kawaida kwa wanadamu kufanya hivyo lakini kwa Rose na mzee Sionjwi kwangu ilikuwa sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano.
Kwa kweli sikufanya lolote zaidi ya kujirudisha taratibu ili wasinione hadi nyumbani na kukaa kwenye mkeka kama nilikuwa naona mazingaombwe enzi nikisoma shule ya msingi.Kila swali nililojiuliza juu ya Rose kufanya mapenzi na mzee Sionjwi nilikosa jibu. Bado sikuelewa Rose na mzee Sionjwi walikuwa na mahusiano ya mapenzi tangu zamani au vipi. Sikuamini kwa mara moja vile mtu kukubaliana na mtu na kuweza kwenda sehemu kufanya mapenzi.
Pia umri wa mzee Sionjwi ambaye sisi wote tulikuwa sawa na wajukuu zake lakini bado alionekana mwanaume mwenye uwezo wa kufanya mapenzi kwa uwezo mkubwa. Nilikiwa bado nipo kwenye lindi la mawazo nilimuona Rose akirudi akijikausha, nilimuangalia sikummaliza.
“Vipi shoga ulikwenda wapi?”
“Nilikuwa na hamu na mapera nikaenda kuchuma.”
“Mmh, sawa.”
“Kwani vipi mbona unaguna?”
“Hata, kawaida.”
“Muongo au unadhania kitu.”
“Walaa, kitu gani?”
“Aaah, basi.”
“Mbona hukuniletea nami mapera?”
“Sikujua kama nawe unayapenda.”
“Shoga na hali hii vitu vya ugwadu navitaka sana.”
“Basi baadaye nitakufuatia.”
“Eflazia nahisi joto acha nikaoge.”
“Hakuna tatizo.”
SIKUTAKA kumuuliza mara moja nilimuacha ili aamini kuwa jambo alilofanya lilikuwa la siri. Baada ya kuoga alirudi na kujilaza pembeni yangu hakuchelewa alipitiwa na usingizi mzito.Mara alipita mzee Sionjwi na kapu lake la dawa alilokuwa anakwenda kutwanga kwenye kinu, nilimtazama yule mzee nisimmalize, nilimpandisha na kumshusha bila kupata jibu. Kila nilipouangalia umri wake na vitendo vyake vichafu nilikuwa sipati jibu.
Niliamini si sisi tu ambao katembea na sisi hata wateja wazuri waliofika kwake nao alitembea nao. Wasiwasi wangu niliamini maisha yetu yapo hatarini kama atakuwa na ugonjwa ambukizi unaopatikana kwa njia ya kujamiiana.
Sikuamini hata wakati akifanya mapenzi na Rose kinga ilitumika zaidi ya kwenda peku tu. Nilishindwa kujilaumu sana kwa kosa nililofanya la kutumia ushirikina kutaka madaraka na matokeo yake ni hayo ya kupewa ujauzito na mganga ambaye hana mbele wala nyuma.
Niliamini kabisa nimetumbukia shimoni na dalili za kutoka zilitoweka, nilibakia nikisubiri maajabu sikutaka kumshirikisha Mungu katika uchafu ule. Wasiwasi wangu mkubwa japo alikuwa amenitoka moyoni ni bwana wangu. Bora ningefanya lolote ningeweza kumdanganya lakini si ujauzito ambao anajua kabisa si wake.
Sikuwa na jinsi zaidi ya kusubiri muujiza wa shetani wa kuitoa ile mimba au huruma ya mzee Sionjwi. Rose aliamka jioni kutokana na uchovu wa mbilingembilinge ya mzee Sionjwi.Usiku ulipoingia mzee Sionjwi aliniita pembeni na kukaa kwenye mkeka wawili na kuanza kunieleza alichoniitia pembeni.
“Mjukuu wangu nimejaribu kila aina ya dawa ili kuitoa mimba lakini mizimu imekataa.”
Kauli ile ilinikata maini na kuona si bora angetuacha turudi nyumbani kuliko kutuweka, wazo lilikuwa labda alituweka vile ili wafanye uchafu wao na Rose.
“Babu mbona unanikata maini,” nilisema kwa masikitiko.
“Si kwamba hakuna njia nyingine.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama ipo nifanyie tu babu nipo katika wakati mgumu sana.”
“Njia yenyewe sikuipenda sana kwa vile huenda usiipende.”
“Njia ipi tena hivyo?” Kauli yake ilinishitua.
“Hii inatakiwa iingizwe dawa kwa ndani ili ikasafishe ndani na baadaye ujauzito huo utatoka.”
“Sasa kwa nini usifanye?”
“Lakini inatakiwa dawa ipakwe kwenye uume wa mtu kisha uwe kama unafanya naye mapenzi, dawa ile ikichanganyikana na mbegu za kiume basi utakuwa umemaliza tatizo na muda wake saa sita usiku ikizidi na dakika tano.”
“Mmh, mbona mtihani,” ulikuwa mtihani mwingine.
“Ndiyo maana nilisema dawa hii imenisumbua sana nimeiomba mizimu ibadili lakini hakuna kilichoendelea zaidi ya kusisitiza hii ndiyo dawa inakayofaa kuutoa huo ujauzito zaidi ya hapo itakubidi ukubali kuzaa tu.”
Mmh ulikuwa mtihani mwingine ambao niliona sina ujanja zaidi ya kukubali kwa vile mtu mwenyewe kashafanya mapenzi na mimi kwa njia za kishirikina mpaka kunipa mimba kukataa ungekuwa ujinga.
“Sawa babu nimekubali.”
“Vizuri kazi itakuwa saa sita ya usiku.”
“Hakuna tatizo babu.”
Niliachana na babu na kurudi kujumuika na wenzangu kwa vile chakula kilikuwa kimeiva tulijumuika wote kupata chakula cha usiku. Baada ya chakula tuliingia kwenye mazungumzo ya usiku mpaka saa tano walipoamuriwa wote waende wakalale na sisi wageni tuliingia chumbani kwetu.
Majira ya saa sita usiku mzee Sionjwi alinifuata kuniamsha kama tulivyokubaliana. Niliamka na kumuaga Rose aliyekuwa bado hajalala.
“Shoga ngoja nikapate tiba.”
“Hakuna tatizo, sijui utanikuta nimelala au?”
“Vyovyote.”
Nilitoka nje ya nyumba yetu na kumfuata mzee Sionjwi aliyenipeleka mbali kidogo na nyumbani kwenye mti mmoja ambao yeye aliuita wa mizimu. Tulipofika pale alinieleza nivue nguo zote na kusimama kuutazama mbuyu, nilifanya vile huku aibu nikiiweka pembeni.
Mzee Sionjwi naye alisimama mbele naye akiwa mtupu kama mimi macho yake yakitazama kwenye mbuyu na kuanza kusema.
‘Mizimu leo hii ni siku ya kutimiza yale mliyoniagiza, leo hii nawarudishieni zawadi yetu mliyompa binti huyu bila ridhaa yake naomba muipokee.”Baada ya kusema vile eneo lile lote lilitetemeka na kutamani kukimbia. Baada ya muda sehemu ile ilitulia mzee Sionjwi alinigeukia na kunisemesha.
“Sasa mjukuu wangu tuifanye hii kazi.”
Alitandika mkeka kisha alinieleza nitangulie chini na yeye alitoa kikopo na kutoa dawa nyeupe ya mafuta. Nilimuona akiipaka sehemu zake za siri, moyo ulinishtuka na kumuuliza.
“Babu ina maana tunafanya bila kinga?”
“Hii dawa inatakiwa upate joto halisi la mwanaume na mbegu zake ndizo huenda kuubomoa mji wa mimba.”
Mmh sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali kila alichokifanya mganga, baada ya kupaka dawa zake aliniingilia kimwili, japo sikupenda tiba ile kwa msisimko nilioupata sikutaka mzee Sionjwi atoke upesi alipotaka kunyanyuka nilimkamata shingoni na kumrudisha huku nikimuomba nami anisindikize nifike safari kwa vile muhemko ulikuwa mkubwa.
Tulijikuta tumeacha kilichotupeleka na kuingia kwenye mapenzi ambayo kwa mara ya kwanza tangu nivunje ungo nilikutana na mwanaume ambaye kila akikugusa unasisimkwa na mwili na kutamani kuwa naye muda wote.
Baada ya kumaliza alinipa dawa ya kuoga na kunywa kisha tulirudi nyumbani, kutokana na mshikemshike wa kufa mtu wakati wa kutengua amri ya sita nilitumia nguvu nyingi nilipofika kitandani nilijitupa bila kujijua na usingizi mzito ulinichukua.
“Eflaziaaa.”
Sauti ya mshtuko ya Rose ilinishitua katikati ya usingizi mwili ukiwa umechoka kama umetwangwa katika kinu, nilifumbua macho lakini yalikuwa mazito kufumbuka kutokana na kuzidiwa na usingizi.
“Eflazia hii nini hebu amka.”
“Rose nimechoka niache nilale,” nilijibu bila kufumbua macho.
“Hapana Eflazia umejichafua damu nyingi zimekutoka.”
“Damu?” Kauli ile ilinishtua na kunifanya nikurupuke nilipokuwa nimelala na kukuta nimelalia damu. Damu ilikuwa nyingi kitu kilichonishtua, nilijishangaa baada ya kukuta kanga niliyojifunga wakati wa kulala imelowa damu sehemu kubwa.
“Ha, nini hii?” Nilishtuka japo ilionekana kama damu ya hedhi lakini ilikuwa nyingi.
“Ni kama mimba imetoka,” alisema Rose.
“Mungu wangu mbona damu ni nyingi si nitakufa mie jamani!” niliingiwa woga.
“Sidhani, ngoja nimfuate mzee Sionjwi.”
Rose alitoka na kuniacha nikiwa bado sijaivua ile kanga yenye damu huku nikiendelea kuishangaa damu nyingi iliyokuwa kitandani sehemu niliyokuwa nimelala. Mara aliingia Rose akiwa ameongozana na mzee Sionjwi, alipoingia niliona aibu kutokana na hali aliyonikuta nayo.
“Vipi kulikoni?” Aliuliza bila kushangaa.
“Nimeamka na kukuta hali hii,” nilimuonesha ile damu japokuwa alikuwa akiiona.
“Sasa kipi cha ajabu,” mzee Sionjwi aliuliza bila kuonesha kushtushwa na kwa kile alichokiona.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ina maana huoni hii ni damu ya kawaida?”
“Mjukuu, kwani hii dawa ina tofauti gani na damu uliyoizoea?”
“Hii ni nyingi sana kama kachinjwa mbuzi,” Rose alisema.
“Sasa si ulitaka iwe hivi unashangaa nini?”
“Ina maana hivi ndiyo mimba inatoka?”
“Binti acha kunichanganya nini kilikuleta au tuirudishe.”
“Ha…ha…pana.”
“Sasa?”
“Naogopa damu imetoka nyingi sana naweza kufa.”
“Kutoa roho ya kiumbe mchezo.”
“Sasa itakuwaje?”
“Usihofu, nenda ukaoge nikupe dawa kila kitu kitakwenda vizuri.”
Baada ya kusema yale alitoka na kuniacha na Rose chumbani, niliitoa ile nguo yenye damu na kujifunga nyingine kisha nilitoka nje kwenda kuoga. Nilipopiga hatua tumbo lilinikata kama mtu ameukata utumbo kwa mkono. Nilipiga kelele za maumivu na kukaa chini.
“Eflazia, nini tena?” Rose aliniuliza.
“Tumbo…Tumbo, Rose nakufa.”
Tumbo lilinikata na kuhisi kama utumbo wote umekatika tumboni, maumivu yalikuwa makali sana, nilianza kulia huku nimeshikilia tumbo ambalo maumivu yake sikuweza kufananisha na kitu chochote. Wakati huo damu zilianza kutoka tena.
Nguvu ziliniishia na kuanza kuona kizunguzungu kikali na kuiona dunia ikizunguka niliamini kabisa kifo kilikuwa kikinisubiri. Nilimsikia kwa mbali Rose akitaharuki na kumwita mzee Sionjwi.
“Mzee Sionjwi njoo umuone Eflazia.”
Baada ya kuja nilimsikia akiuliza.
“Kuna nini tena?”
“Alikuwa anatoka ndani akaanza kulalamika tumbo kisha akakaa chini, baada ya kukaa chini na damu nazo zinamtoka.”
“Sasa cha ajabu nini?”
“Mzee Sionjwi huoni ajabu mtu yupo kwenye hali gani unasema hakuna cha ajabu.”
“Hivi kukitoa kiumbe tumboni ni mchezo, huu ni mwanzo bado kuna mzoga unatakiwa kutolewa.”
“Mungu wangu si atakufa?”
“Kufa hafi ila cha moto atakiona.”
Walinibeba juujuu hadi kwenye kijumba kilichokuwa pembeni baada ya muda ililetwa dawa iliyokuwa imechemshwa na kunyweshwa. Mmh, haikupita muda nilisikia kitu kama haja kubwa na kuanza kusukuma. Kumbe nilikuwa nakitoa kiumbe kilichokuwa tumboni. Baada ya kutoka nilipoteza fahamu sikujua kinacho endelea.
****
Niliposhtuka nilijikuta nimelala kwenye mkeka, pembeni yangu alikuwepo Rose ambaye alionekana yupo mbali kimawazo hata nilipoamka hakuniona, nilimshitua kwa kumwita.
“Rose…Rose,” aligeuka na kunishangaa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ha! Eflazima upo salama mpenzi, siamini niliamini kabisa umekufa japo mzee Sionjwi alinieleza kuwa utarudi katika hali yako, unajisikiaje?”
“Mmh, sijambo japo sijui nimekuwaje kuwa katika hali hii?”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment