IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS
*********************************************************************************
Simulizi : Niliolewa Na Mganga Kwa Tamaa Ya Cheo Kazini
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ukimuangalia unaweza kusema ni bibi wamiaka 60 lakini ni mwanamke wa miaka 37 msomi mwenye shahada ya Uchumi aliyochukulia nchini Marekani. Kwa umri wake wa miaka 37 amepata watoto sita wa mganga huyo wa jadi.Akisimulia mkasa wake kwa mwandishi sababu iliyomfanya kuwa mke wa mganga wa jadi na kuacha kazi yake ya uhasibu. Ni kisa kitakachokusikitisha na kukuacha mdomo wazi pia kina mafunzo mengi. Alianza kukielezea kisa chake kama ifuatavyo:Naitwa Eflazia ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita, wa kike tukiwa wanne waliobaki ni wanaume. Naweza kusema namshukuru Mungu kutujalia familia yenye uwezo pia inayojali elimu. Katika familia yetu aliyesoma elimu ya chini aliishia kidato cha sita.Naweza kusema taa ya bahati iliniangaziamimi kwa kufanya vizuri katika masomo yangu yote na kufanikiwa kufikia ndoto yangu ya tangu utotoni ya kufika chuo kikuu. Kweli Mungu alisikia maombi yangu na kufanikiwa kuingia chuo kikuu.
Nilisoma kwa umakini mkubwa huku nikizingatia yote niliyoelezwa na wazazi wangu kuhusu kuzingatia masomo niliyoyafuata na si kujichanganya na starehe na kusahau kilichonipeleka pale.Sikatai sikuwa mtawa nilikuwa na rafiki yangu wa kiume ambaye hakuwa mwanafunzi wa chuo, alikuwa mtu mzima kidogo mwenye mke wakati ule alikuwa na watoto watatu. Sifahamu sasa hivi yupo wapi na ameongeza watoto au la.Penzi langu na mtu mzima yule ambaye alikuwa ni meneja wa kampuni moja kubwa nchini, halikuniumiza sana akili japo kuna siku nilipomkosa nilipatwa na presha. Lakini nilipokutana naye alinituliza kama ujuavyo mtu mzima alikuwa na busara tofauti na kijana mwenzako.Nilishuhudia mapenzi ya wanafunzi kwa wanafunzi wakipigana na kudhalilishana mbele za watu, hilo sikupenda kwangu litokee kutokana na heshima ya familia yangu. Kama ingenitokea ningeweka wapisura yangu mbele ya wazazi wangu. Mzeemzima alinilea mapenzi ya baba na mtoto wake kutokana na kunitekelezea mengi niliyomuomba.Sikuwa mtu wa tamaa sana hata yeye alinisifia kwa tabia yangu ya kutokuwa na tamaa pia heshima na unyenyekevu. Ahadi aliyonipa ni kunipatia kazi nimalizapo chuo kikuu kwa upande wangu niliona ni bahati ya pekee niliyopata.Niliendelea kusoma huku tukiendelea na mapenzi yetu ya siri na mzee wangu ambaye muda wote alipenda kuniita “Bebii” kwangu ilikuwa faraja moyoni mwangu mpaka nilipokaribia kumaliza chuo kikuu baba shangazi wangu ambayealipenda nimwite Sam ikiwa kifupi cha majina yake matatu.Mzee Sam aliniletea habari njema kuwa rafiki yake amempa ofa ya mimi kwenda kusoma nchini Marekani kwa miaka miwilina nikirudi nitakuwa mhasibu mkuu kwenye moja ya shirika kubwa la serikali. Nilimshukuru sana mzee Sam kwa upendo na kutimiza kila aliloniahidi.
***Baada ya kumaliza chuo kikuu sikusubiri hata maafali niliondoka wiki moja kabla na kwenda kwenye chuo cha uchumi nchini Marekani. Kwa kweli nilijiona ni kiumbe niliyezaliwa na bahati. Niliamini kumbe hata mwili wako ukiutumia vizuri unaweza kukusaidia katika maisha yako, vilevile ukiutumia vibaya unaweza kuyachukua maisha yako.Niliyasoma masomo yangu kwa furaha naamani ya moyo, huku nikijifikiria nitakapoajiriwa kwenye kampuni ile yenyejina kubwa na mishahara minono inayoongoza katika makampuni makubwanchini. Pamoja na kusoma sikufikiria kufanya kazi kwenye kampuni kubwa kama ile.Miaka ilikatika huku mtoto wa kike nikizidikupendeza na kutakata asikuambie mtu Ulaya ni ulaya hii ngozi unayoiona kama ya bibi kizee ilikuwa kama mtoto wa miaka miwili jinsi ilivyokuwa laini na kung’aa.
Mzee Sam alikuwa akija Marekani kwa mwezi zaidi ya mara mbili na kutumbua naye maraha, sikumnyima kitu mzee wa watu kwa kujitoa muhanga kwa ajili yangu. Ilikuwa kama mke na mume na kuniahidi nikirudi na kuanza kazi ananihamisha nyumbani na kunijengea jumba la kifahari ili niwe nyumba yake ndogo.Japo katika maisha yangu sikukipenda kitendo cha mwanamke kugeuzwa nyumba ndogo, lakini kwa yote aliyonifanyia nilikubali kuwa nyumba yakendogo pia kuwa muaminifu kwake. Kwa mzee Sam ilikuwa tofauti na wanaume wengi wenye umri kama wake tena wenyewake zao huwageuza watoto wa kike chombo chao cha starehe hasa wanafunzi wa sekondari na vyuoni kwa kutumia matatizo yao kama fimbo ya kuwapigia.Nilifanikiwa kumaliza masomo yangu chuo cha uchumi na kupata cheti changu ambacho kingeniwezesha kufanya kazi sehemu yoyote duniani. Kama asingekuwa mzee Sam nilikuwa nifanye kazi Marekani, naamini yote ya kuzalishwa kama totoleo la vifaranga vya kuku wa kisasa yasingenikuta
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
.***Baada ya kurudi nyumbani Tanzania nilikaa nyumbani kwa mwezi mmoja tu na kuitwa kwenye shirika hilo kubwa na kufanyiwa usahili ambao niliufanya vizuri na kuajiriwa kama kaimu mhasibu mkuu. Mhasibu mkuu alikuwa jamaa mmoja ambaye elimu yake ilikuwa kidato cha sitana kufanyia kazi uzoefu.
Nilielezwa kuwa baada ya miezi mitatu nitapewa nafasi ile ya uhasibu mkuu, kauli ile ilinifanya niote ndoto za kumiliki nyumba na gari bila msaada wa mzee Sam, pia kuwasaidia wazazi wangu ambao nao walitegemea kula matunda yao ya kunilea na kunisomesha.
Kazi niliifanya kwa ufanisi mkubwa kila mmoja alinisifia kwa uwezo wangu wa kufanya kazi kisomi zaidi. Wengi walishangaa elimu yangu na uwezo wangu wa kazi kuwa nilitakiwa mimi niwe mhasibu mkuu. Maneno yale japo yalinifanya nijisikie vibaya lakini muda ulikuwa bado ila mwezi wa tano ulikuwa ukikatika bila kusikia taarifa zozote kutoka kwenye bodi juu ya kupewa nafasi yangu ya uhasibu mkuu.
Taarifa zile nilimfikishia Mister ambaye alinieleza niwe mvumilivu suala langu linashughulikiwa, nilivumilia wakati huo nilikuwa nimepangiwa nyumba nzima maeneo ya Mikocheni B na kunipa moja ya gari zake nilitumie kwa kunipeleka kazini na kunirudisha nyumbani.
Maisha kila kukicha yalizidi kuniangazia na kujiona mwenye bahati ya mtende kwanza kupata kazi yenye mshahara mzuri pia kuwa na mwanaume anayenijali zaidi ya mkewe na wanaye. Yote niliyafurahia kasoro kitu kimoja kilinikera sana cha kuwa chini ya mtu niliyemzidi elimu mara kumi.
Mwaka ulikatika hakukuwa na mabadiliko yoyote kitu kilichonikosesha raha, ilifikia hatua hata bwana yangu kuniambia niachane nalo kutokana na kunipatia kila nilichokitaka na pesa iliyozidi mshahara wangu mara moja na nusu. Pamoja na kunipatia pesa zile niliamini zile sio zangu kwa vile ana maamuzi ya kusema sasa basi au kufariki.
Niliamini kipindi hicho nitakuwa kwenye wakati mgumu bora nipate changu mapema cha kwake kiwe cha kujazilizia. Nilijikuta nikifanya kazi kwa kinyongo kwa kuona kama hawakunitendea haki. Siku zote sehemu yoyote huwezi kukosa shoga yako ambaye mmeshibana.
Siku moja nilimweleza dukuduku langu lililokuwa likiutesa moyo wangu, shoga yangu alinieleza kitu ambacho kwanza kulinishtua na kuhisi presha kunipanda kwa kunieleza:
“Shoga hata sisi tunashangaa kwa elimu yako kuwa chini ya huyo bwana ambaye elimu yake haikupati hata kidogo, lakini kuna tetesi za juujuu kuwa bwana huyo yupo pale kwa nguvu za giza.”
“Etii?” Kauli ile ilinishtua na kubakia kinywa wazi.
“Una uhakika na usemalo Rose?”
“Kweli kabisa, unajua wewe ni mtu wa sita kuwa chini ya yule bwana wenye elimu kumshinda yeye. Lakini bwana yule nasikia amejidhatiti wote waliopita waliahidiwa kama wewe lakini asikia wakubwa wote kawaziba midomo hawaongei lolote. Kwa hiyo shoga bila kuhangaika nafasi ile utaiona vilevile na zaidi utaondoka bila kuaga kama walivyofanya wenzako.”
Mmh! Ilikuwa kali ya mwaka upande wangu yaani kumbe kuna watu wanategemea nguvu za kiza na si elimu, nilijiuliza kuna umuhimu gani basi mtu kumaliza muda mwingi katika elimu kama kuna njia ya mkato ya nguvu za giza. Nilijikuta njia panda nisijue nifanye nini nikitaka msaada wa Rose.
“Sasa Rose, shoga yangu utanisaidiaje?”
“Hakuna msaada wowote zaidi ya kuhangaika.”
“Kuhangaika kivipi zaidi ya elimu niliyonayo au nikamuone mkurugenzi?”
“Mmh, wala usijisumbue kuna msichana mmoja alimaliza chuo cha fedha na kuajiliwa kama msaidizi wa mhasibu mkuu alikwenda kulalamika kwenye bodi ya wakurugenzi ambao waliona kabisa ana haki ya kuwa mhasibu mkuu na kumuahidi kulifanyia kazi tatizo lake.
“Wengi tuliamini Mbwana Tensa amekwisha, taarifa zile zilipomfikia aliaga kazini ruhusa ya siku mbili na kwenda kwao Tanga aliporudi siku ya pili yule dada badala ya kuongezwa cheo alipewa barua ya kufukuzwa kazi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huwezi amini kila mtu alichanganyikiwa na kuamini kabisa Mbwana ni mshirikina mkubwa. Si huyo tu kuna kaka mmoja naye baada ya kuahidiwa na uongozi kuwa anatakiwa kuwa mhasibu mkuu na Mbwana kutaarifiwa kumuachia madaraka.
“Ilikuwa jambo la ajabu kukubali bila jambo lolote kumtokea, yule kaka alifanya kazi kwa wiki moja tu siku ya Jumatatu tuliletewa taarifa kuwa amekutwa amekufa bafuni wakati akijiandaa kuja kazini.
“Tukio lile lilizidi kuwachanganya watu na kuamini kabisa Mbwana ndiye mhusika mkuu lakini hakuna aliyemwambia live zaidi ya kunung’unikia pembeni.
“Matukio kama hayo hayakuishia hapo kuna dada mmoja ambaye naweza sema kweli alijidhatiti alipofika tu alikaa wiki moja alichukua nafasi ya uhasibu mkuu, yule dada alidumu miezi sita. Ilikuwa lazima kila wiki mbili aombe ruhusa ya siku mbili na kuondoka tena alikuwa akitoka siku ya Alhamisi na kurudi Jumatatu.
Ndiye dada pekee aliyeweza kudumu kwenye kiti hicho.”
“Ilikuwaje akaacha kazi?” nilimuuliza baada ya kumsikiliza kwa muda mrefu huku presha ikinipanda kutokana na mtihani uliokuwa mbele yangu.
“Mmh sijui alipata kazi sehemu nyingine alipotea ghafla bila hata kuaga tulipata taarifa yupo kampuni moja ya wazungu. Lakini tetesi zisizo rasmi anasema mauzauza aliyokutana nayo ofisini yalimfanya awe kwenye wakati mgumu wa kuhangaika kupambana na adui yake.
“Na baada ya kupata kazi hakuwa na haja ya kuaga kutokana na bomu alilokuwa ametegewa. Lakini alisema kama asingepata kazi sehemu nyingine lazima angemfunza adabu kwa kumkaushia ofisini na vibomu vyake.”
“Sasa kama hao wenye uwezo wa kupambana naye wameshindwa mimi nitawezaje, yaani hapa haja kubwa na ndogo zote zinataka kutoka kwa pamoja hata hamu ya kazi imenipotea. Hebu fikiria Rose mimi mweupe siku zangu za kuishi duniani si zinahesabika?” nilimuuliza huku nikisikia utumbo ukinitetemeka.
“Ndiyo maana nikasema maisha ya sasa ni kuhangaika hata hao mawaziri na wabunge usiwaone wako vile wamehangaika bila kuhangaika mambo yako hayawezi kwenda. Hata viongozi ya dini pamoja na kusimama mbele ya waumini kutangaza neno la Mungu kuwa watu wamche Mungu lakini wakitoka pale nao wanaingia kuhaingaikia maisha.”
“Sasa utanisaidia nini maana hapa nilipo nimepoteza mwelekeo hata kuiogopa ofisi yangu pia kumwona Mbwana kama mtoa roho.”
“Ngoja nikupe siri ya Mbwana kama ukiwa mkimya ni mtu mzuri tena mwenye kusikiliza watu hata kutoa pesa za mfukoni mwake. Lakini ukitaka kupambana naye hapo ndipo hugeuka na kuwa na roho ya shetani, anapotetea ugali wake yupo radhi kupoteza maisha hata ya mwanaye ili kuhakikisha nafasi yake haipotei.
“Na sasa hivi amejidhatiti si rahisi kumtoa pale kutokana na bodi ya wakurugenzi kumuamini kwenye kazi zake japo hazipo katika ubora kama ufanyazo wewe pindi anapokuwa amesafiri.”
“Mmh!”
Niliguna huku nikifikiria nitawezaje kukabiliana na Mbwana kazi naitaka na cheo changu nakitaka vilevile, lakini ubabe wa nguvu za kiza za Mbwana zilinitisha. Baada ya kutulia kwa muda nilimuuliza Rose anaweza kunisaidia vipi.
“Kwa hiyo Rose kwa hili utanisaidia vipi?”
“Kuna mzee mmoja yupo Mbagala alinisaidia katika tatizo moja la kufukuzwa kazi, si unajua stoo kulipotea vitu ambavyo wakati naondoka vilikuwepo kumbe kuna watu walinizunguka, kesho yake katika kufanya mahesabu ilionekana kuna mapungufu kitu kilichosababisha niwe kwenye wakati mgumu.
“Sikuwa na ujanja kwa vile funguo nilikuwa nazo mimi na mimi ndiye mtu wa mwisho kufunga, kufukuzwa kazi kulikuwa njenje. Lakini alikuja dada mmoja aliyeniuma sikio na kunipeleka Mbagala Charambe kwa babu mmoja ambaye alifanya mambo.
“Huwezi kuamini soo lile liliisha kimyakimya huku wezi wakinifuta na kunishukuru eti bila mimi nao lazima wangefukuzwa kazi. Nilishukuru walinipatia kifuta jasho si haba…Lakini kabla ya kukupeleka Mbagala kwa nini tusimtafute yule mama aliyetoana jasho na Mbwana ili atupe siri ya mafanikio ya kuweza kumdhibiti.”
“Tena kweli, sasa tutampataje?” Nilijikuta nikiwa na shauku ya kumuona mama huyo ambaye katika historia ya watu waliopita pale yeye ni kiboko.
“Hebu ngoja nimuulizie Fatuma ndiye aliyekuwa na mahusiano naye ya karibu.”
Rose alimpigia simu Fatuma ambaye alitupatia namba ya simu ya huyo mama kiboko ya Mbwana. Baada ya kupata tulimpigia simu yule mama aliyefahamika kwa jina la mama Sabuni. Alipokea na Rose alijitambulisha, cha kwanza kabla ya salamu aliuliza kama Mbwana yupo na ameua wangapi pia kujinadi ana bahati safari hii angekimbia ofisi yeye Mbwana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rose alimuomba tukutane naye kuna jambo muhimu alilotaka kuzungumza naye. Kutokana na tabia yake ya ucheshi alikubali tuonane naye jioni ya siku ile baada ya muda wa kazi.
***
Baada ya muda wa kazi tulimfuata mama Sabuni kwake kwa mazungumzo ya kina na kwa uhuru mkubwa. Alikuwa anakaa Kiwalani ambako mume wake alikuwa amejenga, tulifika Kiwalani majira ya saa kumi na mbili kwa kutumia gari nililopewa nitumie na Mister wangu wakati huo nilikuwa naendesha mwenyewe.
Nyumba yake ilikuwa ya kisasa iliyokuwa umejengwa na kuzungushwa na uzio wa matofari. Tulipofika tulipiga honi geti tulifunguliwa na kuingiza gari ndani, mwenyeji wetu muda huo alikuwa ameisha toka nje kutupokea.
“Ooh, jamani karibuni sana,” alikuwa mama mcheshi sana.
“Asante mpenzi,” tuliitikia kwa pamoja.
Alitupokea na kutuingiza sebuleni ambako ndipo tulipoanza mazungumzo yetu baada ya kutupatia vinywaji.
“Mhu, Rose wewe nakufahamu sijui mgeni wetu unaitwa nani?”
“Naitwa Eflazia.”
“Ooh, dada karibu sana.”
“Asante.”
“Mm’hu Rose, nilikusikiliza kijuujuu sikukuelewa vizuri, ehe leteni habari.”
“Kama tulivyo kueleza kwenye mazungumzo ya awali, mtu wako bado anasumbua.”
“Kwani tatizo nini?”
Ilibidi nijielezee mzunguko wangu kuwa mrefu wa kukamata madaraka pia na vitisho nilivyovisikia kuhusiana na tabia za Mbwana.
“Mdogo wangu umeisha wahi kufika kwa waganga wa kienyeji?”
“Bado.”
“Toka uzaliwe?”
“Ndiyo.”
“Na pale ndiyo sehemu yako ya kwanza kufanya kazi?”
“Ndiyo.”
“Ndiyo maana, sasa mdogo wangu upo tayari kimapambano?” “Ndiyo dada yangu,” nilijibu kwa kujiamini.
“Kwa vile wewe ni mwanamke mwenzangu na tabia za Mbwana nazijua vizuri nitakusaidia kumkomesha.”
“Nitashukuru dada yangu.”
“Tena ana bahati kama ningekuwepo angekimbia yeye, nakuhakikishia lazima utamtia adabu tena wewe ndiye atakaye mfanya aikimbie kampuni.”
Baada ya mazungumzo ambayo yalipata muafaka tulihamia mazungumzo mengine ambayo yalitufanya tuzungumze kwa kucheka na kugongeana mikono kisha tulikubalia siku ya mimi kupelekwa kwa mtaalamu ili niipate nafasi yangu ya Mhasibu mkuu.
Nilimpitisha Rose nyumbani kwake Kinondoni na mimi kurudi nyumbani kwangu kujipanga kwa ajili ya kwenda kwa mtaalamu ili niipate nafasi niliyoitafuta kwa udi na uvumba.
Siku ilipofika kama tulivyokubaliana nilikutana na mama Sabuni ambaye alinipeleka kwa mganga aliyekuwa akikaa mpakani mwa Tanga na Pwani baada ya kuvuka vijiji viwili ndani ya Mkoa wa Tanga, tuliingia mkono wa kushoto na kuifuata njia isiyo kuwa na lami kwa mwendo wa dakika 20 kwa gari mpaka kufika kwa huyo mganga.
Tulifika saa kumi jioni na kupokewa na mganga ambaye alionekana ni mtu mzima lakini mwenye nguvu, baada ya kutupokea tuliingia kilingeni kutusikiliza. Mama Sabuni mwenyeji wangu alimweleza sababu iliyotupeleka pale baada ya kutusikiliza aliuliza;
“Bado tu unawasumbua?”
“Bado babu.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lakini si nilikuambia uje nikupe funga kazi.”
“Babu umesahau pale nilihama na wewe ndiye uliyenitengenezea upupu ule wa kuitwa ile kampuni.”
“Mjukuu wangu uzee huo, napoteza mpaka kumbukumbu.”
“Kwa hiyo babu mjukuu mwingine huyu, nina imani ile funga kazi utampatia yeye.”
“Hilo halina tatizo nafikiri unanijua vizuri.”
“Kazi kwako.”
“Lakini kwa vile mmekuja muda mbaya nilikuwa nakuombeni leo muondoke ila Jumapili njooni mapema kila kitu kitakwenda vizuri mtakuta nimeandaa kabisa.”
Baada ya kuelezwa vile hatukutaka kupoteza muda. Tulirudi mjini kwa ajili ya kujipanga kurudi tena Jumapili huku nikimuahidi mama Sabuni kama nitafanikiwa kumng’oa Mbwana kwenye kile kiti, lazima nimpe zawadi kubwa.
***
Siku ya pili ambayo ndiyo ilikuwa Jumapili nilimpitia mama Sabuni ambaye siku hiyo alikuwa na udhuru kwa kupata wageni. Kwa vile sehemu ile nilikuwa naijua na uwezo wa kuendesha gari peke yangu nilikuwa nao, nilienda peke yangu.
Niliendesha gari kwa shida kwa vile sikuwahi kuendesha kwa safari ndefu, muda mwingi nilisimamisha nilipokutana na gari kubwa. Nilitumia muda mwingi na kujikuta nimeingia kwa mganga saa tisa alasiri. Aliponiona alifurahi sana, siku ile hakukuwa na wagonjwa kabisa.
Wakeze walinipokea kwa furaha, kilichonishangaza kukuta wake wa yule mzee watatu ni umri wangu, tena wazuri wakiwa katika mavazi ya kaniki migongo nje. Kilichonifariji walikuwa wakarimu sana na kujikuta nikitokwa na ugeni. Nilijiuliza mbona yule mzee ana wake bado vijana tena warembo.
Mmoja alikuwa na watoto wawili wa pili alikuwa na mtoto mdogo wa miezi minne na wa tatu ambaye kwa kweli alikuwa bado kabisa kigori alikuwa mjamzito wa kujifungua leo, la kesho.
Suala la nguvu za kiume halikunipa shida, zaidi ya kujiuliza kitu gani kilichowavutia hasa wanawake wale kuacha kuolewa na vijana wenye hadhi na maisha mazuri na kukimbilia kuolewa na kizee kama kile tena kiganga cha kienyeji kisicho na uwezo mkubwa zaidi ya mashamba na mifugo na kulala kwenye nyumba isiyo na hadhi.
Mganga alinikaribisha kwa uchangamfu mkubwa.
“Ooh, mjukuu karibu.”
“Asante babu.”
“Mbona peke yako?”
“Mwenzangu amepata udhuru.”
“Karibu sana.”
“Asante.”
Nilikaribishwa katika chumba cha uganga, niliingia ndani na kukaa kwenye mkeka ulioanza kuisha. Baada ya mganga kukaa na kutulia alinigeukia na kuniuliza.
“Eti mama mlikuwa na shida gani vile?”
“Babu nawe umesahau uzee kweli unakunyemelea,” nilimtania.
“Mambo mengi mjukuu wangu, bibi zako nao wananisumbua kila siku hawaishi kugombana wivu unawasumbua.”
Kauli ile ilinifanya nijiulize maswali mengi huo wivu wanamuonea kwa kipi cha mno alichonacho. Lakini sikutaka kuingilia kisichonihusu.
“Babu kuhusu kumtoa yule mwanaume aliyekalia nafasi yangu kazini.”
“Ooh, nimekumbuka, sasa unataka tumfanyeje?”
“Ujuavyo babu wewe si ndiye mtaalamu utakavyoona inafaa wewe fanya.”
“Tumuulie mbali?”
“Hapana, aondoke mwenyewe kwenye kiti changu,” sikutaka kuua niliiogopa dhambi yake.
“Kumbe unacho unachokitaka.”
“Ni kweli babu mtu kama yule niliambiwa unaweza kumfanya mwenyewe aache kazi.”
“Hiyo ni kazi ndogo mjukuu wangu, sasa fanya hivi leo nitakupa dawa ya kuoga kuondoa nuksi na nyingine utajifukiza kabla ya kulala na ya kuweka chini ya mto uilalie mpaka asubuhi, kisha utanitafutia jogoo mwekundu mmoja, shuka nyeupe, nazi zipo hukuhuku, mishumaa minane na kama utafanikiwa kuniletea kalamu au karatasi aliloandika niletee vyote Ijumaa.
“Pia itakuwa vizuri kama utachukua mchanga sehemu aliyokanyaga au sehemu iliyokuwa na kivuli chake hiyo itatusaidia kuifanya kazi kwa urahisi.”
“Nimekuelewa babu, lakini huoni kama baadhi ya vitu ni vigumu kupatikana?”
“Tena katika masharti wewe nimekupa madogo kutokana na jinsi ulivyo si mzoefu wa mambo haya. Siamini kama utakosa karatasi aliloandika hata siku za nyuma, pia kukanyaga sehemu siyo lazima uchukue kwa muda ule.
“Wewe ni kuangalia amesimama wapi au wapi kivuli chake kimeelekea. Kwa wakati wako chukua mchanga hata kwa kujifanya unaokota kitu ulicho kidondosha ili mtu asijue unafanya nini.”
“Mmh, nitajitahidi.”
“Nakuhakikishia ndani ya wiki lazima ataomba kuacha kazi mwenyewe, asivyofanya hivyo njoo uchome vikapu vyangu vya uganga kwani nitakuwa nimeshindwa kuifanya kazi niliyorithishwa na babu yangu ambaye enzi za uhai wake alisifika sana kwa kuwasaidia watu wenye matatizo,” mganga alijigamba.
“Yaani nitashukuru, nakuhakikishia kukupa zawadi kubwa sana babu.”
“Mimi ndiye mzee Sionjwi, tena nilitaka kusahau ukiisha maliza kutengeneza dawa nilizokupa usiku wakati wa kulala usilale na nguo ya ndani, pia usilale na mwanaume kwa siku zote tatu za kutumia dawa.”
“Hakuna tatizo.”
Babu Sionjwi kama jina lake alivyonitamkia alinipa dawa zote na kunielekeza jinsi ya kutumia kisha tuliagana na kurudi mjini huku nikiwa na matumaini makubwa ya kumng’oa Mbwana.
***
Nilipofika nyumbani nilimpigia simu Rose na kumweleza hatua niliyofikia, Rose alinipa moyo na kuniahidi kunisaidia hasa katika kuchukua mchanga wa nyayo na kivuli cha Mbwana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Eflazia nakuhakikishia nitakuwa bega kwa bega na wewe kuhakikisha tunamng’oa mchawi yule.”
“Nitashukuru sana shoga yangu si unajua mimi bado mgeni kwenye mambo haya!”
“Usihofu nitakusaidia kwa kila kitu.”
“Nitashukuru, basi kesho kazini kama kawaida.”
“Wewe tu.”
Nilikata simu na kujiandaa kufanya ile kazi niliyoagizwa na mganga, baada ya kuoga dawa na kujiandaa na dawa nyingine ya kujifukiza mlango uligongwa, nilishtuka kwa vile ‘mister’ wangu pamoja na kuwa naye kipindi chote hakuwahi kulala nje ya kwake kama yupo Dar.
Alikuwa akiiheshimu sana ndoa yake ambayo waliifunga kwa sheria zote za dini, nami japo nilimkosa usiku na kujikunja peke yangu kitandani bado sikumlaumu kwa vile alivyonifanyia ni zaidi ya nikitakacho. Nilikwenda hadi mlangoni na kuuliza.
“Haloo nani mwenzangu?”
“Mimi dear,” ilikuwa sauti ya mister wangu, kabla ya kumfungulia nilishtuka kidogo na kujifikiria usiku ule wa saa nne amekuja kufanya nini.
“Nakuja dear.”
Nilirudi haraka ndani na kuviweka vizuri vitu vyangu ambavyo nilikuwa nimeviweka hovyo kwa kuamini nipo peke yangu muda ule. Baada ya kuwa na uhakika nimeviweka vizuri nilirudi hadi sebuleni na kufungua mlango. Nilipomuona nilimrukia kwa furaha.
“Wawooo my darling.”
Mister hakujibu alionekana kukunja uso wake kitu kilichonitisha na kunifanya nihoji kuwa katika hali ile.
“Vipi mpenzi mbona hivyo?”
“Ulikuwa na nani?”
“Una maana gani?”
“Hujanijibu, ulikuwa na nani?”
“Nilikuwa peke yangu.”
“Kweli?”
“Mbona umeniuliza hivyo? Kipi cha ajabu umekiona?”
“Mbona uliposikia sauti yangu ulirudi ndani kwanza.”
“Mmh, kumbe hilo mpenzi, kwanza sikuamini kama ni wewe pia huwa siingizi mtu ndani nikishafunga mlango. Wakati unagonga nilikuwa ndiyo nataka kujipaka mafuta ili nipande kitandani, hivyo niliona kazi kuchukua kitu nilitoka kama nilivyozaliwa kwa kuamini kama mazungumzo tungemaliza yeye akiwa nje na mimi ndani.
Lakini kumbe ulikuwa mume wangu na kunifanya nirudi ndani kujifunga khanga, ningeweza kukupokea hata bila ya nguo lakini sikujua umeongozana na nani au ulitaka niwe kituko mbele ya mgeni. Huuoni mwili wangu bado una maji na sina kitu ndani,” nilijitetea mtoto wa kike.
Nilisema huku nikiitoa khanga yangu mwilini na kumuonesha umbile langu ambao niliamini litamchanganya akili.
“Mpenzi siwezi kufanya uchafu wowote kwa vile kila nikitakacho unanipa kwa nini niwe mwizi wa fadhila umenifanyia mazuri mangapi. Naomba uniamini kama una wasiwasi japo dini hairuhusu nioe niwe mkeo wa pili ili muda wote niwe pembeni yako.”
“Basi...basi mpenzi inatosha, vipi uliniambia ulienda Kibaha kwa bibi hajambo?”
“Hajambo anakusalimu.”
“Mmh! Ananijua?”
“Hivi unafikiri kuna siri basi familia yangu yote wanakufahamu hata wazazi wangu, ndiyo maana hawajaingilia katika suala la kuolewa.”
“Mmh, makubwa.”
“Madogo yana nafuu.”
“Najua utashangaa kuniona muda huu?” aliniuliza, muda huo nilikuwa bado sijaokota nguo.
“Ni kweli lakini sishangai kwa vile hapa ni kwako,” nilijibaraguza japo moyoni donge lilinikaba la hasira la kumwona muda ule kwangu.
“Basi leo nitakuwa mgeni wako, mke wangu nilimpeleka Kibaha kwenye msiba hivi ndivyo narudi hapa nitalala mpaka saa kumi usiku kisha nitaondoka na kurudi nyumbani.”
“Hakuna tatizo mpenzi wangu jisikie furaha kulala katika nyumba yako.”
Baada ya kuingia alikwenda kuoga kisha tulipanda kitandani huku nikiwa nimechanganyikiwa kwa kuamini mister lazima atataka mchezo tu usiku ule. Nilijiuliza nitaanzia wapi kumnyima mtu sina tatizo lolote na sijawahi kumfanyia kitu kama kile. Wasiwasi wangu kama nitasingizia ugonjwa lazima angejua nimemfanyia makusudi ni kweli nilikuwa na mwanaume.
Nikiwa njia panda kipindi hicho mzee alikuwa anataka haki yake, nilijikuta nikikubali kama mbwa kwa chatu bila kupenda. Alfajiri mister aliondoka na kuniacha nimechanganyikiwa alfajiri ileile nilimpigia simu Rose kumuomba ushauri kwa kukiuka masharti ya mganga. Rose alishangaa kumpigia simu asubuhi sana.
“Vipi Efrazia mbona simu alfajiri?”
“Ndugu yangu kuna mambo yamenitatiza.”
“Yapi tena hayo?”
Ilibidi nimweleze ukweli kuhusiana na masharti niliyopewa na mganga na makosa niliyofanya. Rose kabla ya kunijibu alishusha pumzi ndefu kisha alisema.
“Mmh, shoga mbona mapya tena hayo, lakini kwa nini hukutumia uongo? Efrazia umeshindwa kutunga uongo hata tumbo linakuuma ili tu ufikishe siku hizo?”
“Shoga yaani sijui nikuambie nini, wakati namalizia kufanya uwanga wangu si ndiyo Mister akaja nyumbani kwangu ghafla na si kawaida yake kwa vile moja ya masharti aliyonipa ni kulala nyumbani kwake na mkewe.
“Hata sijui ni kitu gani siku zote asitokee atokee siku nina kazi yangu muhimu, na kilichonichanganya ni kuchelewa kwangu kufungua mlango. Mister alijua nina mtu ndani kitu kilichonichanganya hata aliponiomba nikashindwa kumnyima.”
“Mmh, hilo nalo neno.”
“Sasa utanisaidiaje?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi ninavyojua kila kitu kimeharibika ni wewe kufunga tena safari mpaka kwa mganga ili kumweleza ukweli juu ya kosa lililotokea.”
“Yaani najuta, mganga aliniahidi wiki hii asipoacha kazi mwenyewe basi nikachome mikoba yake.”
“Mungu wangu, Efuuu! Emeharibu kila kitu yaani kumbe si muda mrefu tungekuwa tunakula bata.”
“Yaani we acha, japo kaniudhi lakini siwezi kumlaumu sana kwa vile ndiye mtu aliyenifikisha hapa. Kwanza hapendi nifanye kazi zaidi ya kunihudumia kila kitu. Lakini shoga kuna leo na kesho leo yupo kesho hayupo ndiyo nianze kuhangaika.”
“Kweli usemalo.”
“Sasa unanishauri nini?”
“Kuna la kukushauri zaidi ya kurudi kwa mganga?”
“Sasa itakuwaje ikiwa siku ya kurudi ni wiki moja nzima?”
“Efrazia hakuna haja ya kufanya kazi, leo ukifika kazini omba ruhusa kuwa unakwenda hospitali ujisikii vizuri. Ukichukua mapumziko yako ya siku mbili unamaliza kila kitu.”
“Kweli umenipa wazo ambalo halikuwa akilini mwangu, nimeamini kidole kimoja hakivunji chawa.”
“Basi hivyo jiandae asubuhi tu ukifika usifanye kazi yoyote kachukue sick sheet na kwenda hospitali utajua ya kuzungumza upate mapumziko ya siku mbili.”
“Hakuna tatizo acha nami nijiandae kwa ajili ya kuja kazini.”
“Sawa tutakutana hiyo asubuhi.”
Baada ya kuzungumza na Rose nilikwenda bafuni kuoga na kuchukua kila kilicho muhimu ili nikitoka hospitali nipitie moja kwa moja kwa mganga. Baada ya kujiandaa nilikwenda hadi kazini ambapo sikushika kitu chochote zaidi ya kuchukua sick sheet na kuelekea hospitali.
Nilipofika nilimweleza daktari kuwa sijisikii vizuri hivyo nilikuwa naomba mapumziko ya siku mbili ambayo niliyapata. Sikutaka kupoteza muda nilijaza mafuta kwenye gari langu na safari ya Kibaha ilianza mara moja. Kwa vile ilikuwa bado muda nilitembea kwa mwendo mkali kwa vile nilikuwa nimeshaanza kuzoea barabara, kutokana na mwendo niliokwenda nilifika kwa mganga saa tano na nusu.
Kama kawaida wakeze walinipokea kwa furaha utafikiri tulikuwa tukijuana muda mrefu na furaha yao ilijionesha wazi kwangu. Nami siku ile nilikuwa nimejiandaa kwani nilikwenda na miche mitano ya sabuni, sukari na mchele mfuko wa kilo 50 na kindoo cha mafuta cha lita 20.
Kweli nilipokelewa kama mfalme na kunifanya hata kuondoa wasiwasi wa kumweleza mganga kosa nililofanya la kukosea masharti. Kabla ya kuingia katika kilinge cha mganga nilizungumza mawili matatu. Kubwa kabla ya yote nilitaka kuwachimba ilikuwaje wakaolewa na mganga yule kufikia hatua ya kuwaonea wivu.
Lakini kabla sijapata nilichodhamiria mganga aliniita kilingeni kwa vile alikuwa anataka kutoka.
“Samahani mjukuu ninataka kutoka kwenda kutafuta dawa tena wewe ndiye uliyenifunga miguu, kila nilipotaka kuondoka niliona miguu mizito basi nilijua kuna ugeni.”
“Nakuja babu nilikuwa nazungumza na shoga zangu.”
“Basi fanya haraka ili niweze kukimbia porini kabla jua halijawa kali.”
Niliingia kilingeni kwa babu ambaye alionekana bado mkakamavu.
“Mhu, karibu mjukuu.”
“Asante.”
“Mbona ghafla kulikoni?”
“Babu nimechanganya madawa.”
“Kuchanganya madawa una maana gani?”
Nilimuhadithia hali ilivyokuwa, baada ya kunisikiliza alishusha pumzi na kusema.
“Pole sana, najua ugumu wa tatizo lilivyokutokea, lakini usijali nitakusaidia hilo, la muhimu jitahidi kuwa makini dawa nitakazokupa leo. Kwa vile ndiyo nilikuwa naelekea porini naomba ubakie na bibi zako mpaka nitakaporudi kuleta dawa za kazi yako.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali kubaki na kina bibi zake mganga, kabla ya kuondoka alinichinjia kuku kwa ajili ya kitoweo cha chakula cha mchana ambapo mke mkubwa ambaye alikuwa rika langu aliingia jikoni kuandaa chakula.
Baada ya chakula tuliingia kwenye mazungumzo na shoga zangu ambao tulizungumza mengi zaidi kuhusiana na maisha huku tukitaniana kuvuta muda wa mganga kurudi.
Muda ulizidi kukatika bila kumuona mganga kitu kilichonishtua na kujiuliza atakuwa umechelewa wapi.
Ilipotimu saa kumi na mbili nilitaka kuaga ili nirudi kesho bahati nzuri mganga alirejea akiwa na rundo la miti na majani, wakeze walimpokea kwa furaha na bashasha kila mmoja alimpokea cha kwake. Nilijikuta nikivutiwa na nidhamu waliyoonesha wanawake wale.
Kitu kama kile kilikuwa adimu sana katika dunia ya sasa kwa wanawake kumpokea mume wao kwa furaha hasa wakiwa matara, wengi hununiana na kuishi kama chui na paka.
Nilijikuta nikisubiri mpaka alipomaliza kula muda nao ulikuwa umepiga hatua na kuingia saa mbili. Kuaga nilishindwa nilibakia kusubiri mganga ataniambia vipi. Lakini nilijiambia kama atanipa dawa nitafika Dar saa sita usiku, nilimsubiri mpaka aoge ndipo aanze kunipatia huduma.
Nilijikuta nikijilaumu bora ningekuja siku ya pili na kukuta dawa tayari. Niliamua kusubiri kwa vile maji nilikuwa nimeshayavulia nguo sikuwa na budi kuyaoga, baada ya mganga kuoga na kula ndipo aliponiita nilipokuwa nimejilaza kwenye mkeka kutokana na uchovu huku usingizi ukianza kunichukua.
Nilijinyanyua na kwenda kukaa kwenye mkeka alipokuwa amekaa yeye, nilikaa pembeni yake.
“Vipi mjukuu?”
“Safi tu babu,”
“Naona leo umekosa raha kukuweka mpaka muda huu kijijini?”
“Hakuna babu kawaida muda bado nitawahi tu kama utamaliza shughuli mapema hata saa tano usiku nitaondoka.”
“Vizuri, sasa mjukuu kutokana na kukosea masharti nimeonelea nibadili dawa, inabidi upate dawa ya kuoga ili kuondoa nuksi ambayo inaonekana bado inakunyemelea na ukiiacha ina mwisho mbaya.
Inaonesha kabisa adui yako naye ameanza kukuzunguka kukuharibia usipokuwa makini utakimbia wewe umuache yeye.”
“Babu sasa utanisaidiaje?” Kauli ya babu mzee Sionjwi ilinitisha na kujiona tayari nimeingia kwenye vita na Mbwana ambayo wengi wamechemsha.
“Kimoja kilichonifanya nichelewe kurudi ni pamoja na kuifuata mbali dawa hiyo, umbali wake ni sawa kutembea kwa miguu toka Kariakoo mpaka pugu.“
“Ooh, pole babu” nilijikuta nikimuonea huruma babu wa watu, kutokana na umri wake na safari aliyotembea.
“Aah, kawaida tu mjukuu wangu ndiyo kazi yetu…kwa vile umefanya makosa na dawa yenyewe ya kuoga ambayo itawekwa kwenye beseni lenye maji na kupigwa na ubaridi wa usiku kisha uioge dawa alfajiri kabla ya adhana.”
“Mmh, babu mimi mkiristo nitajuaje mambo ya adhana na wakati kuyaoga pia kuyaweka nje yapigwe na baridi, wasiwasi wangu yanaweza kumwagwa na kufanya kosa lingine.”
“Hilo nalijua ndiyo maana nikaamua kazi hii kuifanya mimi.”
“Utaifanyaje babu wakati tutakuwa mbali mbali?” nilimuuliza.
“Kutokana na kazi hii kuisimamia itakubidi ulale hapa ili kazi hii tuifanye alfajiri kama masharti yanavyotaka.”
Mmh, kauli ya kulala nje na nyumbani kwangu tena sehemu duni kama ile ilinishtua sana, lakini nilificha hofu yangu na kujifanya nimekubaliana naye ili nisiharibu maana nzima.
“Hakuna tatizo babu, vipi kuhusu usalama wa gari langu?”
“Hilo usihofu, hakuna kiumbe chochote kibaya kitakachoweza kuingia hapa kwangu.”
Baada ya makubaliano nilipewa maji ya moto ambayo yaliandaliwa kwa ajili yangu kisha nilipewa chakula cha usiku ambacho tulikula wote, baadaye nilioneshwa chumba cha kulala ambacho kilikuwa kina kitanda cha mbao kilichokuwa na godoro na shuka nzuri za maua ya kufuma ambazo zilizidi hata za kwangu mimi niliyejiona bora kuishi mjini na kuishi maisha mazuri.
Ilionesha jinsi gani mzee yule pamoja na kuishi kijijini sehemu iliyokuwa haina hadhi lakini alikuwa akijithamini hasa katika malazi. Baada ya kuoneshwa chumba na kitanda changu nilipanda kitandani. Kutokana na uchovu nilipitiwa usingizi mzito.
Usiku wa manane sikuwa na kumbukumbu kama nilikuwa naota au ni kweli kitu kile kilinitokea, usiku wa manane niliota kama kuna mtu juu ya mwili wangu. Alikuwa kama yule mzee lakini mwili wote haukuwa na nguvu na kumuacha afanye atakavyo.
Nakumbuka kama nilihisi raha ya ajabu ya kufurahia penzi tamu la babu ambalo sikuwahi kulipata katika maisha yangu. Lakini ajabu usingizi ulinipitia na kushtushwa na mkono wa mtu ukiniamsha.
“Bibie amka tufanye kazi ili uwahi kuondoka.”
Nilipofumbua macho nilimkuta mke mkubwa wa mzee Sionjwi akiwa amesimama kitandani kwangu.
“Kwani saa ngapi?”
“Saa kumi na nusu.”
Mmh, kibaridi cha alfajiri kilikuwa kikali sana, kama ningekuwa naishi kule basi ningechelewa kazini kila siku. Nilinyanyuka kitandani nikiwa natetemeka kwa kibaridi kikali. Nilitoka hadi nje ya nyumba ambako baridi ilizidi mara dufu.
Nilishangaa kuwaona wenyeji wangu hawaoneshi chochote kuhusiana na ubaridi ule ilionesha wameshaizoea. Baada ya kutoka nje nilielezwa nimfuate mmoja wa wakeze aliyekuwa amebeba beseni la maji lililokuwa na dawa ya unga na majani mabichi yaliyokuwa yamelazwa kwenye maji yale.
Nikiwa natetemeka kwa kibaridi cha alfajiri nilimfuata mke wa mganga hadi nyuma ya nyumba, baada ya kufika aliniomba nivue nguo zangu zote na kuziweka pembeni kisha aliniambia nichutame nami nilifanya hivyo. Alichota maji na kuanza kunimwagia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nusra nigande kwa baridi maji yalikuwa kama yametoka kwenye friji alinimwagia maji taratibu huku akisema maneno ya chinichini ambayo sikuyasikia. Baada ya kunimwagia makopo kama matano, aliniacha nimalizie mwenyewe kwa kujisugua na majani yaliyokuwa kwenye maji.
Baada ya kumaliza kuoga alinipa kipande cha kaniki nijifunge, baada ya kujifunga tulirudi hadi mbele ya nyumba. Baadaye nilipewa nguo ya kujifuta maji na kuvaa nguo zangu. Sikupewa kitu kingine zaidi ya kuzingatia maagizo ya mwanzo ya kupeleka vitu alivyonituma mwanzo, mchanga wa kimvuli na nyayo za Mbwana pia karatasi au kalamu aliyokwishatumia.
Ila alinieleza zoezi la kujifukiza usiku kwa siku tano halikuwa na muhimu baada ya kuifanya ile dawa. Aliniomba nivifikishe vile vitu siku ya Jumapili mapema ili niwahi kuondoka.
“Vipi kukutana na mzee?” nilimuuliza nisije rudia tena makosa niliyoyafanya mwanzo.
“Hakuna tatizo wee akija mpe tu haki yake.”
“Nashukuru babu.”
Nilishukuru maana nilijua ni mtihani kumnyima mtu ambaye ananijua vizuri nilivyo, uongo wowote ungefanya anifikirie vibaya kuwa nina mwanaume mwingine.
Baada ya kumaliza kila kitu niliondoka kurudi Dar majira ya saa kumi na mbili na nusu. Nilitembea kwa mwendo wa kasi ulioniwezesha kufika nyumbani majira ya saa nne. Niliingia ndani na kujitupa kitandani kutokana na uchovu na usingizi nilipitiwa usingizi mzito.
Nilishtuka majira ya saa kumi jioni nikiwa mchovu na kuamua kwenda kuoga kabla ya kutafuta chakula kutokana na njaa kali iliyokuwa imenibana. Nilikula chakula na kurudi kitandani kujilaza mwili kama haukuwa wangu.
Siku ya pili nilikwenda kazini kama kawaida, wa kwanza kunifuata alikuwa rafiki yangu Rose.
“Shosti vipi umefanikiwa.”
“Namshukuru Mungu mambo hayakwenda vibaya.”
“Mm’hu, nini kinaendelea?”
“Shoga naomba msaada mmoja wa kunitafutia mchanga wa kivuli cha mbwana na nyayo zake nitakupa zawadi nzuri.”
“Hiyo kazi nyepesi mpaka muda wa kuondoka nitakuwa nimekukamilishia usikonde.”
“Nitashukuru.”
Rose aliondoka na kuniacha nikiendelea na kazi kama kawaida, baada ya muda nilikwenda kwenye mafaili na kuchomoa karatasi zilizokuwa na mwandiko wa Mbwana ambao ulikuwa ukijulikana. Nilichukua na kuiweka ndani ya mkoba wangu na kutulia kusubiri mchanga niliomtuma Rose.
Jioni kabla ya kuondoka Rose aliniletea vikaratasi viwili alivyokuwa amefunga mchanga, kimoja alikiandika kimvuli na kingine nyayo.
Nilimshukuru kwa msaada wake nilifungua pochi ili nimpe elfu 20 lakini Rose alikataa.
“Hapana Efrazia, msaada wangu kwako hauhitaji malipo ndiyo maana nimeamua kujitolea.”
“Mmh, nashukuru.”
Baada ya Rose kuondoka niliviweka vitu vyangu vizuri mpaka muda wa kurudi nyumbani ulipotimia. Nilirudi nyumbani nikiwa na furaha tele nikiisubiri siku ifike na kwenda kumaliza kazi.
Nilishukuru kipindi chote kile mume wangu hakuwepo alikuwa amesafiri nje ya nchi kikazi, ile ilinifanya nifanye mambo yangu bila kuingiliwa na mtu.
***
Siku ya Jumapili ilipofika niliondoka nyumbani na kila kitu nilichotumwa majira ya saa kumi alfajiri, nilifika kwa mganga saa moja kasoro kutokana na mwendo niliokuwa nikienda.
Mganga aliponiona alishangaa kuwahi namna ile lakini hakuchelewa aliponiona tu, aliingia ndani na kutoka na vitu vyake vya kazi na kuniita kilingeni. Niliingia na kukaa kwenye mkeka aliniomba vitu alivyonituma nilimpa vyote, baada ya kuvipokea alisema:
“Sasa kazi itafanyika.”
Alivichukua vikaratasi vyote na kuvisoma na kuweka kila mchanga sehemu yake, mmoja aliuweka katika kikopo kilichokuwa na moto na mwingine aliuchanganya na dawa kisha kwenda kuutupa nje kwa kuumwaga angani ambao ulipeperushwa na upepo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kumaliza zoezi lake alisema:
“Kazi imekwisha.”
Mganga alinipatia kikaratasi kilichokuwa na maandishi ya Kiarabu na kunieleza kuwa nikiweke chini ya godoro upande wa kichwani na nibadili ulalaji wangu.
“Naona haya ni zaidi ya yote uliyouliza.”
“Bahati mbaya leo mizimu haifanyi kazi imepumzika leo ni siku ya kutoa dawa si ya kuwasikiliza wazee.”
“Babu suala langu linahitaji ufumbuzi wa kina bila hivyo litanitia uchizi.”
“Ni tatizo gani tena hilo?”
Tulisogea mpaka chini ya mti wa Mkorosho na kukaa kwenye mkeka, baada ya kukaa babu alinigeukia na kuniuliza.
“Mmh, mjukuu wangu una tatizo gani?”
“Babu kuna kitu kimekuwa kikinitokea kwa kweli sijui ni nini?”
“Kitu hicho?”
Ilibidi nimweleze ukweli babu japo nilikuwa naona aibu kuyasema yale, baada ya kumweleza yale alicheka kidogo na kuchimba chini na kijiti kisha alisema kwa sauti ya chini.
“Mmh, kwa nini usiiache tu hiyo mimba?”
“Hapana babu, bwana wangu nitamwambia nini?”
“Mwambie hii mimba ni yake hawezi kukataa.”
“Babu shida yangu si kuzaa bali kuitoa nilikuja kupata ushauri wako nawe unaniambia eti nizae. Mtoto baba yake atakuwa nani au unataka nizae kiumbe cha ajabu?”
“Baba yake nitakuwa miye.”
“Etiiii?” Kauli ya mzee Sionjwi ilinishtua.
“Babu hutani huo kwa nini mtoto baba yake uwe wewe kwani wewe ndiye uliyeniingilia?”
“Siyo mimi niliyekuingilia kwa vile kila ulipoota unaingiliwa uliiota sura yangu, basi acha mtoto awe wangu pengine hata sura yake itafanana na mimi.”
Kauli ile ilinitisha na kujikuta nikiwatazama watoto wa mzee Sionjwi utafikiri wamepigwa fotokopi. Nilijiuliza sura mbaya kama ile na jinsi mister wangu alivyo handsome nitawaeleza nini walimwengu. Ni sawa na Waswahili wazae mtoto Mchina lazima watu watakunyooshea vidole.
“Hapana babu ujauzito huu nakwenda kuutoa.”
“Usiutoe mjukuu wangu utakuletea madhara.”
“Bora nife kuliko kuzaa mtoto asiye na baba.”
“Mjukuu wangu wote unaowaona hapa wapo wengine walipata tatizo hilo walipokataliwa na waume zao niliwapokea na wanafurahia maisha.”
Kauli ile ya babu Sionjwi ilinivunja nguvu, lakini sikuwa tayari kuzaa mtoto wa kimiujiza ambaye atakuwa kituko. Niliona bora ningekuwa nimebakwa nikajua moja lakini si kupata ujauzito kwa njia ile.
“Babu hakuna msaada mwingine wa kunisaidia juu ya ujauzito huu?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmh, hakuna hiyo ni mizimu iliyokusaidia kufanikisha mambo yako, asante yako ni kuizalia mtoto.”
“Ina maana mlifanya vile makusudi?”
“Hiyo sijui labda uje uiulize yenyewe.”
“Siwezi na sasa hivi naondoka na kwenda kuutoa ujauzito huu na liwalo na liwe Mungu atanilinda.”
Nilinyanyuka kwa hasira na kuingia kwenye gari langu na kuondoka kwa kasi bila kuaga. Njia nzima nilijikuta nimechanganyikiwa juu ya ujauzito ule ambao ulionekana kuingia kimiujiza. Bado sikukubali kuzaa mtoto asiye na baba pia mazingira yake ya kumpata yalikuwa ya utata mkubwa.
Kutokana na kuchanganyikiwa nilkijikuta nikikosa kuanguka kwenye mtaro baada ya kulivaa tuta la barabarani. Nilitetemeka kwa kukanyaga breni huku gari likisota na kwenda kusimama pembeni kabisa ya barabara na mtaro mrefu.
Kama ningeangukia mle mtaroni nisingetoka salama.
Baada ya kutulia dakika tano bila kunyanyuka kwenye uskani huku mapigo ya moyo kunienda kwa kasi na mwili kukosa nguvu. Nilisali kimoyomoyo kabla ya kuwasha gari muda huo watu walikuwa wamekusanyika nje ya gari langu wakinipa pole na wengine kunilaumu kwa uendeshaji wangu wa rafu kwa kasi na kushindwa kulimudu gari.
“Wengine magari ya baba zao hawajui uchungu wao,” jamaa mmoja alisema.
“Baba zao si ndiyo mafisadi wanaokula nchi hii,” mwingine aliongezea.
Kauli zile zilinichafua na kuamua kuliondoa gari kwa kasi bila kuzungumza na mtu. Njia nzima nilihisi kuchanganyikiwa ujauzito ulinikosesha raha, majibu ya mzee Sionjwi yalinikatisha tamaa kwa kusema eti baba wa mtoto atakuwa yeye kwa vile amenitokea ndotoni wakati wa tendo la ndoa.
Pia alizidi kunichanganya kwa kunieleza kuwa nisiitoe mimba naweza kutokewa na jambo baya. Nilijiuliza kama nitaiacha ile mimba nitamweleza nini bwana wangu mtu niliyemtegemea kwa asilimia kubwa na kuamini sina mwanaume zaidi yake.
Japo sikuhofia sana kuachwa kwa kuamini bado nilikuwa msichana ambaye wanaume wengi walikuwa wakinitaka kimapenzi lakini nililinda heshima yake kwani ni mtu aliyechangia maendeleo yangu kwa kiasi kikubwa. Wasiwasi mwingine niliamini kama atanipiga chini lazima ataniundia fitina kwa rafiki yake ili nifukuzwe kazi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kingine kilichonikosesha raha ni kuzaa mtoto asiyejulikana aliingiaje nilijua huo ndiyo mwanzo wa kuzaa kiumbe wa ajabu na kunifanya niwe mtu wa kuandikwa katika vyombo vya habari. Lakini wasiwasi mwingine niliamini kauli za Rose kuwa huenda ni njama za Mbwana za kutaka kunikosanisha na mganga wangu, mpenzi wangu hata bosi wangu wa kazi ili nami nikose kazi. Lakini mbona mganga hakuonesha ushirikiano zaidi ya kuweka mzaha mbele.
Kabla ya kufika nyumbani nilimpigia simu Rose tukutane kwangu baada ya muda wa kazi ili nimweleze niliyokutana nayo kwa mzee Sionjwi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment