Search This Blog

NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 3

 







    Nusu Siku Ndani Ya Jeneza

    Sehemu Ya Tatu (3)



    "Unajijua?" yule kiumbe aliniuliza.

    "Ndiyo."

    "Unajijuaje?"

    "Mimi ni binadamu."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Siyo kweli."

    "Siyo kweli kivipi?"

    "Kuna ubinadamu baada ya kifo?" aliniuliza.

    Nilibaki kimya. Yeye akaendelea:

    "Binadamu ni uhai, ukishakufa si binadamu tena unakuwa maiti, mfu au marehemu. Wewe umewahi kusikia watu wakisema binadamu huyo atazikwa kesho?"

    Nilitingisha kichwa kuashiria kwamba alichosema ni kweli, akaendelea:

    "Je, umewahi kusikia wakisema binadamu huyo atasafirishwa kwenda mahali kwa mazishi?"

    Pia nilitingisha kichwa kukataa kwamba sijawahi kusikia.

    "Kwa hiyo ubinadamu ni uhai, baada ya kifo hakuna ubinadamu?"

    "Ndiyo," nilimjibu.

    "Ndiyo maana nilikuuliza unajitambua? Ukanijibu ndiyo, wewe ni nani ukasema ni binadamu. Wewe si binadamu kule si ulishakufa au hujaambiwa?"

    "Nimeambiwa."

    "Kwa hiyo wewe ni maiti?"

    Nilisita kumkubalia, lakini mwishowe niliamua kukubali tu. Nilisita si kwa sababu si kweli bali kwa vile niliona ni jambo zito sana mimi kuitwa maiti. Maiti inatisha, maiti inaogopwa, huwezi kulala na maiti hivihivi tu hata kama marehemu alikuwa mke au mumeo.

    Yeye kama alijua, akasema:

    "Nyinyi binadamu mna jambo moja la ajabu sana. Huwa hamuamini maandiko yenu wenyewe. Ukiitwa maiti unaogopa, lakini si ukweli kwamba baada ya kifo ni

    Mimi nikadakia nikasema hukumu. Nikiwa na maana kwamba baada ya kifo hukumu ndiyo andiko nililoanza kulijua mapema sana kwenye maandiko.

    "Siyo mauti. Baada ya kifo ni maiti. Mtu ukishakufa tu unakuwa maiti."

    "Sisi kwenye maandiko yetu tunajua baada ya kifo hukumu."

    "Ni sawa kabisa. Lakini sisi huku tunajua hukumu ipo tangu kuzaliwa kwako maana maisha yameshajulikana hata hujaanza kuishi, ila baada ya kifo ni maiti. Na mtu akishakufa hajui kitu."

    "Hajui kitu kivipi?" nilimuuliza.

    "Hajui kitu kwa maana kinachoendelea."

    "Ha! Mbona kuna elimu kule duniani inasema mtu akishakufa anasikia kila kitu ila kusema ndiyo hawezi?"

    "Umewahi kulala usingizi wa fofofo?"

    Nilimkubalia kwamba nimewahi.

    "Unaweza kusikia kitu?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana."

    "Sasa kufa ni mara mia zaidi ya kulala usingizi mzito. Jifunzeni sana. Roho ikishatoka kinachobaki ni mwili na ubinadamu haupo tena."

    "Kwani roho ni nini?" nilimuuliza.

    "Roho ndiyo nafsi."

    "Na nafsi ni nini?"

    "Uhai."

    "Uhai ni nini?"

    "Unajua uhai wa binadamu upo kwenye damu. Humo ndimo mwenye nafsi. Ndiyo maana mtu akimwaga damu nyingi hawezi kuishi tena."

    Yule kiumbe aliyeonekana mwenye uwezo mkubwa wa kuzungumza aliendelea kusema:

    "Maandiko yenu yanaweka wazi kila kitu kwamba damu ndiyo nafsi, damu ndiyo pumzi. Moyo unaporusha damu mwilini na kuvuta ndipo mtu anapopumua au mnasema kuhema.

    "Mungu wenu katika maandiko ameweka wazi mambo mengi sana kuhusu damu na uhai au nafsi. Ukisoma kwenye sheria za vyakula, kuna wakati Mungu wenu alikataza watu wasile nyama fulani, halafu baadaye akaruhusu wale.

    "Alikuwa akikataza na kuruhusu kwa misimu, lakini wakati wote Mungu wenu amekataza ninadamu msinywe damu kwa kuwa humo ndimo mwenye nafsi ya mtu."

    Aliposema hivyo nilishtuka kidogo kwani ninavyojua mimi kuna kabila nchini mwangu linakula damu ya wanyama. Nilishindwa kuuliza, lakini yule mtu akaendelea kusema:

    "Ukikuta mtu anapenda kunywa damu hata ya mnyama, mara nyingi katika maisha atakumbwa na tabia ya kufanya maamuzi ya ajabu yenye vitendo visivyokubalika."

      




    "Kama vitendo gani?"

    "Vingi tu. Kama vile kuua, kudhuru, kuharibu, kutukana. Mara nyingi kutukana huku kunakuwa hadharani. Pia unaweza kushangaa mtu anakuwa na tabia ya kupenda sana kitu fulani."

    "Da! Nimejifunza mengi sana."

    "Bado hujajifunza, hapa umeletwa ili ujifunze mbinu inayotumika kuua watu duniani. Hii mbinu tunataka wewe ndiyo uende ukaisambaze kwa dunia ukiwa mwalimu wa mbinu hiyo lakini nguvu yote itatoka kwetu.

    "Sasa hivi niliposema kaa lengo langu nianze kukupa hiyo mbinu ili sisi tuweze kuvuna wanadamu wengi katika kipindi hiki ambacho dunia itafikia mwisho wakati wowote ule."

    "Kwani hata wewe hujui mwisho wa dunia ni lini?"

    "Najua."

    "Ni lini?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kha! Mbona hata wewe unajua ni lini!"

    "Mimi sijui, kwenye vitabu vyetu tuliambiwa hakuna anayejua siku ya mwisho wa dunia, hata malaika wa mbinguni."

    "Ni kweli lakini maandiko hayohayo yameweka wazi ishara ya siku za mwisho na ishara hizo zote zinaonekana sasa au nasema uongo?"

    "Ni kweli."

    "Kwa hiyo unakubali kwamba hata wewe unajua kuwa dunia imefikia mwisho?"

    "Kweli nimejua."

    "Sasa tunataka kukutuma duniani, kazi utakayotakiwa kuifanya ni pamoja na kuhakikisha kila siku unaua binadamu zaidi ya mia moja."

    "Hee! Niue binadamu wenzangu?" niliuliza kwa mshtuko nikataka kusimama.

    "Kijana tulia. Unatakiwa kufuata maagizo yetu."

    "Sijawahi kuua na kuua ni dhambi kubwa sana."

    "Kwani kuna dhambi ndogo?" aliniuliuza kwa sauti ya ukali.

    "Najua hakuna, lakini kuua mtu dhamira inauma sana kuliko nikimwibia mtu."

    Aliniangalia kwa karibu dakika moja halafu akageuka pembeni na kumwangalia kiumbe mwenzake mmoja ambaye alikuwa kama msaidizi wake, akasimama na kunisogelea.

    Aliponifikia aliweka mkono wake juu ya kichwa changu, palepale nikajikuta niko kwenye kundi la viumbe wengi lakini kuna kiongozi mmoja mkubwa ambaye alikuwa akitoa maagizo fulani.

    Alikuwa amesimama akamnyooshea kidole kiumbe mmoja akimwambia:

    "Wewe lazima ukamuue kwa ajali leo hii Alia, yule mfanyakazi wa kampuni ya madini, muda huu yupo kazini. Halafu si unajua yule wakati wa kulala au akiamka huwa hasali kwa Mungu wake? Kwa hiyo ni mwepesi sana.

    "Unachotakiwa kufanya, nenda nyumbani kwake kampige ugonjwa wa ghafla mkewe na umwangushe chini halafu ashindwe kusema. Yule mtoto wake mkubwa atampigia simu baba yake.

    "Sasa baba akiambiwa mkewe kaanguka na hawezi kuongea, itabidi atoke ofisini haraka na ataendesha gari kwa spidi sana.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Halafu uende pale Kituo cha Mabasi cha Faya, mwamuru dereva mmoja wa daladala aondoe basi kwa kasi ukimpiga upofu asione vizuri mbele, akifika kwenye makutano ya Barabara ya Faya na Morogoro apite bila kuangalia taa, Alia naye atakuwa ameshafika pale na taa zitamruhusu apite, watakutana na ajali itatokea, Alia atakata roho palepale, sawa?"

    Kile kiumbe hakikujibu sawa, ila kilisimama wima kikainamia mbele kama ishara ya kumtii kiongozi wake, akafutika mbele yetu. Niliogopa sana kusikia mpangilio ule.

    Kumbe ilimaanisha kwamba, ajali inapotokea inakuwa imepangwa na pepo wachafu tena kwa mpangilio wa ajabu, kwamba ajali ianzie wapi na kuishia wapi! Ina maana Alia hakujua kama kule kupigiwa simu kuwa mke wake kashikwa na ugonjwa wa ghafla ndiyo ilikuwa tiketi ya sababu ya kufa kwake.

    Kama angejua angetoa amri akimbizwe hospitalini halafu yeye atafuata huko polepole.

    Baada ya yule kufutika, yule kiongozi akiwa bado amesimama akamnyooshea kidole kiumbe mwingine, akamwambia:

    "Wewe! Kwanza simama."

    Yule kiumbe akasimama kwa utii wote huku akimwangalia yule mtoa amri. Mtoa amri akaendelea:

    "Nataka ukasababishe ajali mbaya ya lori na basi. Ajali hii nataka itokee Barabara ya Chalinze-Morogoro. Unachotakiwa kufanya, wakati basi linatokea Morogoro kwenda Dar es Salaam, wewe toa malori mawili Chalinze kwenda Morogoro.

    "Yale malori yataanza kufukuzana mpaka yanapokaribia kukutana na lile basi, mpige upofu dereva wa lori la nyuma, aamue kumpita mwenzake bila kuangalia mbele na wakati huohuo mfanye dereva wa basi aongeze spidi mpaka kukutana uso kwa uso na ajali itokee.

    Utakachotakiwa kukifanya baada ya ajali ni kukusanya damu za watu watakaoumia, lakini usiue maana leo letu ni damu ya binadamu, si mnajua tuna sherehe mwisho wa mwezi huu?

    "Basi harakisha ili kitengo cha damu kiwe na akiba ya kutosha, watu waumie sana, wavunjike miguu, mikono, wapasuke vichwa lakini usitoe roho ya hata mmoja wao.

    Yule kiumbe naye akainama kwa ishara ya unyenyekevu na kufutika mbele ya macho yangu. Nilianza kujiuliza ina maana katika maelekezo yale itafika zamu yangu?

    Kisha yule mkubwa wao akaangalia huku na kule mpaka mimi akanipitia na jicho lake moja tu lililo kwenye paji la uso, akaniambia:

    "Wewe, simama kwanza."

    Nikasimama huku nikitetemeka moyoni nikijiambia sitakubali kutumwa kwenda kuua wala kusababisha ajali. 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule kiumbe aliniangalia kwa muda wa kama dakika moja nzima, haongei kitu wala hapanui kinywa. Baadaye akasema:

    "Nitakupa kazi. Kaa kwanza."

    Nilikaa huku macho yangu yote yakiwa kwake.

    Akamsimamisha mwingine akisema wewe pale, simama haraka sana.

    Niligeukia kule alikoelekeza kidole yule kiumbe mkubwa nikamwona kiumbe mwingine akisimama kwa utii wote.

    "Nenda kasambaze uwezo mdogo kwa wanawake wajawazito kujifungua wenyewe hadi wafanyiwe upasuaji. Naona kuna kampeni ya wajawazito kujifungua salama, mimi sikubaliani nayo, lazima katika kila wanawake wajawazito kumi, wanane wajifungue kwa kupasuliwa ndiyo lengo letu la mwaka huu. Hakikisha mikono ya madaktari inakuwa na uharaka wa kufanya kazi hiyo."

    Bado nilikuwa nimemkazia macho yule kiumbe aliyekuwa akipewa mwongozo, aliinamisha kichwa kwa utii, akapotea mbele ya macho yetu. Sasa nilijua inakuja zamu yangu ingawa bado mle ndani mlikuwa na viumbe wengi.

    Aliniangalia kwa kupitisha macho yake kwangu lakini mwisho yakaenda kutua kwa kiumbe aliyekaa pembeni yangu, akamwambia asimame. Yule kiumbe akasimama.

    "Ile meli uliipinduaje?"

    "Ile iliyoua abiria wengi?" yule kiumbe alimuuliza mkubwa wake.

    "Unataka nikujibu nini?"

    "Nilipeleka mawimbi makubwa baharini, bahari ikasukwasukwa na upepo mkali hadi meli ikapinduka na kuzama."

    "Serikali ikasemaje?"

    "Serikali ilitoa tamko kwamba kuchafuka kwa bahari ndiyo kulisababisha ajali na watu, hasa wavuvi wakatakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hicho,."

    "Ohoo! Kwa hiyo serikali haikujua kama sisi ndiyo tulisababisha?"

    "Haikujua mkuu, ilijua ni upepo mkali wenye mawimbi makubwa."

    "Safi sana, kaa nitakupa kazi."

    Akakaa kwa heshima zote.

    Nilijiuliza maswali mengi. Hiyo meli wanayoisema ni ipi, ni ya Tanzania au? Maana Tanzania nayo kuna ajali za meli kama tatu zilitikisa. Kuna MV Bukoba, MV Skagit na MV Spice Islanders.

    "Vurata," aliita yule kiumbe mkubwa. Ndiyo nikajua kumbe nao wana majina. Sikuwahi kusikia. Alisimama kiumbe mmoja wa ajabu kuliko wenzake wote. Yeye masikio yalipita kichwa hata ya sungura hayaoni ndani, alikuwa mweusi sana, ni sehemu za macho tu ndiyo alionekana vyema. Midomo yake ilikuwa ya duara kama sehumu wa juu ya kikombe cha chai.

    Shingo yake ilikuwa ndefu kama vile mtu alitundika kichwa chake kwenye mti ulionyooka. Aliposimama akawa anajibinuabinua shingo na kutoa ulimi mweupe kama karatasi na mrefu mfano wa kujiko kikubwa.

    Nilimwogopa sana, maana kama alinijua vile, kila wakati alikuwa akiniangalia mimi na kuachia tabasamu ambalo lilizidisha ubaya wake kuliko alipokuwa hatabasamu. Huyo ndiye Vurata. Mkuu wake akamwangalia kisha akauliza:


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Umerudi lini Vurata?"

    "Jana usiku," alijibu kwa haraka sana.

    "Safi sana. Nipe matokeo," alisema mkuu wao kisha akacheka na kuniangalia mimi huku akijitapa:

    "Sisi huku tunashughulika na vitu vingi sana vingine kama havina maana lakini kwetu vina maana. Enhe, nipe matokeo."

    "Matokeo timu ya Yanga imeifunga Simba bao moja kwa bila."

    "Mfungaji nani?"

    "Anaitwa Tegete."

    "Dakika ya ngapi?"

    "Ileile ya sabini kama ulivyotaka mkuu."

    "Ulifanyaje?"

    "Ile timu nyekundu ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kushinda maana mtaalam wao alikuwa mzuri, lakini nilipofika uwanjani niliwanyong'onyesha miguu ikawa mizito."

    "Vurugu ulizituliza?"

    "Ndiyo mkuu."

    "Sasa hakikisha kila mwaka upinzani unakuwa mkali kwa timu hizi. Sitaki moja iwe juu ya mwenzake kwa sababu ikitokea hivyo mashabiki watapungua na sisi lengo letu mpira uendelee kuwa na mashabiki wengi kuliko wanaokwenda kanisani."

    "Hilo halina shida mkuu."




    "PIA nafikiria kwamba ili ushindani uwe mkubwa wachezaji wa timu ya kijani waende kwenye timu ya rangi nyekundu na wa nyekundu waende ya kijani, kusiwepo madhara lakini."

    "Sawa mkuu."

    "Kaa chini, simama Shubiraa."



    Niligeuka kuangalia nikamwona kiumbe mwingine kasimama, huyu hakuwa anatisha, unaweza kusema ni binadamu kama sisi. Aliposimama akainamisha kichwa, akakiinua mkuu akamuuliza:

    "Makahaba wameongezeka kama nilivyoelekeza siku unakwenda?"

    "Ndiyo mkuu."

    "Umefanyaje?"



    "Nilichofanya mkuu, nimehakikisha wanaume wenye kupenda kulala na makahaba wanaongezeka, pia wanawake wengi, hata wa maofisini, wanafunzi na wake za watu nimewatia kiu ya kupenda kuwa makahaba.



    "Pia nilihakikisha nafanya juu chini ili warembo wengi nao watamani kazi hiyo. Ndiyo maana hata mavazi yao siku hizi ni ya kikahaba tu. Msichana anavaa kisketi kifupi sana."

    "Sawa, lakini kuna jambo la kukuongezeahapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nitafanya hivyo siku nyingine. Kwa leo kapange mikakati yako halafu utaniambia kwenye ufunguzi," alisema yule mkuu. Sikujua ni ufunguzi gani. Hakuishia hapo, akaangaza kulia na kushoto akaita:



    "Wewe Balozeti, simama." Aliyesimama safari hii ambaye ni Balozeti alisimama mbele yangu. Nikamwangalia kwa umakini wa hali ya juu maana alikuwa mrefu sana, kama binadamu wawili mmoja apande na kusimama juu ya kichwa cha mwenzake. Halafu mweusi tii.

    "Balozeti nilikupa mkakati gani?"



    "Nakumbuka mkuu. Ulisema nihakikishe watu wanapenda mikusanyiko isiyokuwa na maana kuliko kupenda kwenda kanisani."

    "Sasa mbona makanisa yanajaza sana siku hizi?"

    "Mkuu nilitumia mbinu moja kubwa na nzuri."



    "Hebu nisimulie hiyo mbinu Balozeti maana nakuaminia sana wewe."

    "Mkuu niliamua kuwapotosha baadhi ya wachungaji wapenda pesa kwa kuweka kipaumbele kwenye fedha badala ya kuhubiri neno la Mungu wao."

    "Hali ikawaje au ikoje?"

    "Kwa sasa wachungaji wengi wakisimama hawalizungumzi sana neno la

    Mungu wao, wanatanguliza shida za mwili za binadamu."

    "Mfano?"

    "Mfano, tumewafanya wachungaji watoe matangazo redioni wakiuliza watu kama wanasumbuliwa na magonjwa sugu kama kansa, ukimwi, presha na mengine mengi.



    "Lakini pia tumewafanya wachungaji haohao wakitoa matangazo yao waulize watu kama hawana kazi, wanatafuta watoto lakini hawapati, wanawake wanatafuta wanaume wa kuwaoa lakini hawapo.



    "Matangazo haya yanasaidia kuwafanya watu wamiminike kwenye makanisa yao ambako neno linakuwa adimu. Kwa sababu hiyo siku hizi baadhi ya makanisa ya kilokole yana waumini wenye tabia kama za waumini wa makanisa ya kimwili."



    "Sijapenda unaposema baadhi ya makanisa, mimi nataka makanisa yote yawe hivyo. Niahidi hapahapa Balozeti."



    "Mkuu kwa heshima kubwa na nzito kwako na kwa kuzingatia hivi vita na kwa kuwa siku zimekwisha, ulimwengu umefikia ukingoni tayari na kwa kuwa mkakati wetu ni kuvuna wengi zaidi ili lile neno lao waingiao upotevuni

    ni wengi nakuahidi kwamba makanisa yote yatakuwa hivyo."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwamba?"

    "Kwamba watasimama zaidi kwenye kuwapa waumini wao mambo ya kimwili na kusahau ya kiroho."

    "Sawa. Mwaka elfu moja mia tisa na sitini tuliweka mkakati wa kuhakikisha makanisa yanakuwa mengi sana, wachungaji wanyang'anyane waumini lakini makanisa yote yakose nguvu, ilifanyika?"



    "Ndiyo mkuu. Makanisa kwa sasa ulimwenguni kote ni mengi sana.

    Tumejitahidi kuhakikisha baadhi ya maeneo kunakuwa na makanisa hata kwa umbali wa mita hamsini."



    "Una maanisha nini?"

    "Namaanisha kuna maeneo ambayo ukitembea umbali wa mita hamsini unakutana na kanisa. Wengine wanasali kama familia tu."



    "Sawa. Vipi ule mpango wa kuwaingizia wachungaji roho za uzinzi, wizi, masengenyo, ubakaji, ulawiti na kupenda fedha kuliko kumpenda



    Mungu?"

    "Mkuu hilo lipo vizuri kwani kama utaangalia kwenye kumbukumbu zako za mwaka huu, wachungaji wengi siku hizi wanakumbwa na skendo hizo ulizozitaja licha ya kwamba waumini nao wameonekana hawapotezi imani kwa wachungaji hao licha ya vitendo viovu.



    "Kwa hiyo?"



    "Tunaendelea mkuu. Lakini kuna wachungaji waliosimama katika kuomba kila siku usiku na mchana wamekuwa wagumu kuwaingilia.
    na kuwapandikizia roho chafu.”

    Nilimwona yule mkuu wao akikunja sura na kukasirika.

    “Balozeti una maanisha sisi tunashindwa?”

    “Mkuu ukweli hatuwezi kushindwa lakini ni kweli kwamba kuna wachungaji wamesimama kwenye neno. Kila tukiwafuata tunawakuta wanaomba au wametoka kuomba kwa hiyo bado wanakuwa na moto wa kutuunguza.”




    Siwezi kukubali kusikia hivyo unavyoongea wewe. Unataka twende na mimi kwa hao wachungaji nikaone huo moto wao kama utamudu kuniunguza?”

    “Mkuu itakuwa vyema, lakini sipendi uende kwa sababu tunatafuta udhaifu wao ndiyo tuwaingie.”

    Yule mkuu alimwangalia Balozeti kwa macho yaliyojaa hasira huku midomo ikimtetemeka. Nilitamani kumwambia Balozeti amruhusu mkuu wao aende ili na yeye akakumbane na huo moto maana alikuwa haamini kama upo kwa wachungaji wenye kuomba sana.

    “Ni muda gani mnakwenda?”

    “Usiku sana.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lakini lile zoezi nililowaagiza kwamba hakikisheni waumini wa makanisa wanaingiwa na uvivu wa kuamka na kumwomba Mungu wao linafanyika?”

    “Mkuu linafanyika tena kwa kasi nzuri.”

    “Halio ikoje?”

    “Yaani hali iko hivi, katika kila waumini kumi, ni mmoja au wawili ndiyo wanaoweza kupata muda wa kuushinda uvivu na kuamka kusali.”

    “Wengine?”

    “Hao wengine tisa au nane wao ukifika muda wa kuamka kusali wanasikia uvivu. Lakini wana uwezo wa kuamka na kufanya mambo mengine yasiyo ya kumpendeza Mungu. Wapo akina mama wanaamka saa kumi kuwahi kununua samaki, wapo wanaume wanaamka saa kumi kufanya shughuli nyingine.”

    “Safi sana. Hilo ndilo tatizo la wanadamu, hawajui kama maombi ya usiku mwingi yana nguvu sana kuliko muda mwingine wowote ule.”

    “Haya, ondoka sana. Wewe simama,” yule mkuu aliniambia mimi nisimame. Nikasimama wima kama askari.

    “Wewe nataka kukupa mmoja wa viumbe wangu uende naye duniani kufanya kazi nitakayowaagiza, uwe uko tayari au hauko tayari si swala la kujieleza. Sumumu, upo?”

    Sumumu alisimama na kusema yupo kwa sauti nzito sana.

    “Wewe ulikwenda kufanya nini duniani? Maana sijakuona siku nyingi sana huku.”

    “Mkuu ulinipa kazi ya kuhakikisha mitandao ya kijamii inaenea kwa kasi sana na binadamu kupoteza muda humo.”

    “Umeifanya?”

    “Kwa asilimia mia moja mkuu.”

    “Nakumbuka nilisema wanafaunzi mashuleni wajue matumizi ya teknolojia mapema ili akili zao zizoee hivyo na kila jambo walifanya kwa kutumia teknolojia, wao watajua wameendelea kumbe akili zao zinadumaa. Ni sawa?”

    “Ndivyo ilivyo mkuu.”

    “Sasa toka na huyu, nataka mkahakikishe uchawi unatawala, wazee wanauawa sana kwa tuhuma za uchawi. Mzee akiwa na macho mekundu tu watu wajue ni mchawi, wamuue.”

    Aliposema hivyo akamwangalia kiumbe mwingine kama aliyeachana na sisi, yaani mimi na Sumumu. Mimi nikanyoosha mkono, akaniuliza:

    “Unasemaje? Zingatia kabla hujasema lolote kwamba nilishakuelekeza hoja zangu si za kukataa ni utekelezaji tu.”

    “Sawa mkuu. Lakini mimi siwezi kwenda.”

    “Haa!” viumbe wengine wote walishtuka na kusema hivyo.

    “Unasemaje?” mkuu aliniuliza.

    “Nasema siwezi kwenda.”

    “Unanijua mimi ni nani?”

    “Nakujua.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni nani?”

    “Mkuu wa hawa.”

    “Haa!” wale viumbe wengine walishtuka tena.

    “Wewe unataka kucheza na moto?”

    Nilijiuliza nitachezaje na moto wakati tayari niko kwenye eneo la moto.

    “Mimi sichezi na moto.”

    “Bali?”

    “Bali nipo kwenye moto tayari.”

    “Kingereza,” aliita.

    “Naam mkuu.”

    “Chukua huyu, mtumbukize kwenye wakorofi wenzake, akapate ile dawa yao kisha mlete hapa.”

    Kingereza alinibeba juu kwa juu hadi kwenye ukumbi mmoja ambao kwa nje ulionekana moja kwa moja kwamba ndani kuna giza nene.

    “Ingia,” Kingereza alinisukuma kwa mikono yake yenye nywele kama za kichwani.

    Nilizama kwenye chumba hicho, nikawa sijui nitembee au nikae maana nilikuwa sioni mbele, kulia wala kushoto. Ghafla mwanga ulioonekana unatoka kwenye taa ya kibatali uliwaka ukiwa hafifu sana.

    Niliwona wanadamu kama mimi wamesimama mstari mbele yangu, mtu wa kwanza kabisa mbele alikuwa anaingia kwenye mlango mwingine.

    Baada ya kuingia ghafla kikasikika kilio huku akisema:

    “Basi sirudii, sirudii jamani.”



    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog