Search This Blog

NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 4

 





    Nusu Siku Ndani Ya Jeneza

    Sehemu Ya Nne (4)



    "Sawasawa Humuli. Je, kuna dalili ya mafanikio kwa kiwango kikubwa?"

    "Sana mkuu. Nchi kubwa na tajiri zote zinatetea wanawake, taasisi mbalimbali zimeanzishwa kwa ajili ya kuwatetea wanawake, baadhi ya nchi kwa sasa duniani zinatawaliwa na wanawake, yapo makanisa ambayo wanawake ndiyo viongozi, lakini pia tumehakikisha kwamba kila serikali inaweka wizara ya kutetea wanawake."

    "Je, mmefanyaje ili serikali zisishtuke kwamba ni mkakati wetu?"

    "Tumehakikisha tunaongeza, mfano wizara ikiwa ya wanawake tunaongeza na watoto au jinsia au walemavu."

    "Je, mkakati mpya mnaokwenda nao mkiwa na huyo binadamu ni upi?"

    "Huyu tutamtumia katika maeneo ambayo akifika yeye wanadamu watalainika kuliko sisi tukijifanya wanadamu."

    "Sawa. Lakini huyu bado sijakubaliana naye kurudi huko, napenda sana akakae kwenye chumba cha tabia za wanadamu na sifa za nyota ili ajifunze, nataka akiondoka ame amejifunza kazi hiyo akawasaidie wenzake kule."

    Aliposema hivyo, kiumbe mmoja alinishika mkono tukaondoka eneo hilo. Tulitembea umbali wa kama nusu saa tena kwa miguu lakini sikutokwa na jasho wala kuhusu joto maana kama nilivyosema, kule kuna mwanga mkubwa lakini hautokani na jua.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tunakwenda wapi?" nilimuuliza yule kiumbe, akanijibu kwa mkato:

    "Chumba cha tabia na sifa za nyota."

    "Ndiyo nini?"

    "Utakwenda kuona."

    Nilifunga mdomo, tukatembea mpaka kwenye jumba kubwa sana kama godauni, tukaingia ndani yake. Mle ndani nilikuta wanadamu wenzangu wamekaa kwenye madawati halafu kuna kiumbe kama anawafundisha bila kutumia ubao.

    Nilipoingia tu, yule kiumbe aliyenipeleka akageuza na kurudi alikotoka. Yule kiumbe aliyekuwa akifundisha aliponiona alisimama kufundisha akanionesha sehemu ya kukaa.

    "Una bahati somo letu ndiyo kwanza linaanza."

    Nilikaa mkao wa kusikiliza.

    "Karibu sana bwana, hiki ni chumba cha tabia za wanadamu na sifa za nyota zao. Eee, mara zote binadamu anakuwa na tabia ya kubadilika kutokana na siku aliyozaliwa. Binadamu aliyezaliwa mwezi wa Januari hawezi kuwa na tabia moja na yule aliyezaliwa mwezi wa Novemba.

    Kila mwezi unatawaliwa na nyota yake. Ndiyo maana katika kuishi au kufanya kazi zenu mnatakiwa sana kuhakikisha zinalingana na nyota.

    "Ziko nyota kumi na mbili na zote hizi zinatawaliwa na mkuu wa huku mliko. Sisi tunazijua nyota hizi kwa majina ya huku ambayo nyie hamuwezi kuyajua, ila kwenu mnaita hivi: Nyota ya kwanza, Punda au Aries kwa lugha ya kigeni.

    "Hii nyota kama wewe unajijua unayo au unajua mwanao anayo ni nzuri kumkuza au kumuandaa kwa kazi kama za jeshini, uokoaji wa majanga mbalimbali, michezo, mfanyabiashara, ualimu na mambo yote yanayohusu usimamizi wa fedha kwa ujumla.

    "Binadamu mwenye nyota hii akifanya moja ya kazi hizo atatajirika, atang'ara na atavuma sana. Kama ni mpira ndiyo binadamu wenzake husema f'lani ana kipaji. Huwezi kumkuta mhasibu mwenye nyota ya Punda anapata shoti kazini au anafungwa kwa wizi wa fedha.

    "Mfanyabiashara mwenye nyota ya Punda mafanikio yake ni makubwa mno. Anaweza kutajirika mpaka watu wakasema ameroga au anafanya biashara na misukule. Lakini si kweli bali ameongozwa kwenye kazi ambayo ina nyota yake.

    "Huwezi kumkuta mfanyabishara ana nyota ya Punda halafu anafilisika. Ile nyota peke yake inalinda fedha zake za kazi. Kwa wanajeshi, wengi wao hufikia kiwango cha kuwa mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi, mkuu wa magereza na mambo mengine yenye mazingira hayo.

    "Hata hivyo, wanajeshi wenye nyota hii ni rahisi kupindua nchi kwa mafanikio makubwa endapo hakutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na serikali iliyopo madarakani.

    "Pia wengi wenye nyota ya Punda hupenda kimiliki silaha lakini matumizi yao hayaendi kinyume na sheria ya nchi kama wengine. Ila akilenga mahali lazima apige. Wana shabaha sana.






    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "KABLA sijaendelea na somo langu la uhusiano wa nyota na maisha yenu binadamu, kuna jambo moja nataka niwaambie," alisema yule kiumbe huku akituangalia kwa zamu sote tuliokuwemo chumbani humo.

    Alipofika kwangu , alinikazia sana macho na kuanza kunisogelea huku akinitazama kwa umakini kama aliyenifananisha.

    "Unajua ninyi binadamu mnatushangaza sana, yaani mnasumbuliwa na vitu vidogovidogo sana wakati uwezo wenu ni mkubwa kuliko kiumbe yoyote huko duniani na hata huku kwetu!" aliendelea kufafanua huyo kiumbe baada ya kurudi kwenye eneo lake la awali na kutufanya tukae kimya sana na kuendelea kumsikiliza kwa umakini wa hali ya juu mno. Akaendelea



    "Kitu kikubwa ambacho ni kidogo lakini kinawasumbua sana, ni kutokuwa na uamuzi wenye msimamo au kufanya mambo hata ambayo hayakuwa kwenye mipangilio maalumu."

    Alipofikia hapo, akanyamaza kidogo na kuanza kutuangalia tena kama awali.

    "Hamjawahi kumuona au kumsikia mtu akisema kuanzia leo sitaki kufanya jambo fulani lakini muda mfupi tu baadaye, unasikia au kuona akikifanya?" akatulia tena na kuendelea;

    "Mfano unakuta mtu anasema, kuanzia leo sinywi tena pombe, nitatunza sana pesa zangu hadi nikamilishe lengo fulani.

    "Lakini, saa chache mtu huyohuyo unamkuta baa akiwa na rafiki zake akizungusha raundi za bia hadi anaishiwa kabisa pesa, lakini akiamka asubuhi akiwa hana pesa anajuta sana, anajilaumu sana na kujiapiza kutorudia tena lakini atakapopata pesa tena anaendelea kufanya jambo lilelile la kunywa pombe na kupoteza pesa!"

    Kila mmoja wetu alitingisha kichwa kuashiria kukubaliana na kiumbe huyo.

    "Hapo inakuwa hivi, mtu huyo anakuwa na roho ya umasikini ambayo kila akipata pesa au kitu chochote cha thamani, inamuingia na kuanza kumpelekesha na baada ya kutimiza dhamira hiyo inamtoka na ndiyo hapo mtu anaanza kujilaumu ni kwa nini alifanya ufujaji wa namna hiyo.

    "Au unakuta mtu amekaa mahali fulani, anapita mtu akiuza kitu ambacho hata hukuwaza kukinunua kabisa. Lakini anamaliza pesa yote na wakati mwingine kitu hicho hakina umuhimu hata kidogo.

    "Hiyo yote ni kutokuwa na msimamo wa maamuzi hali ambayo hupandikizwa na roho hiyo niliyoitaja huko nyuma.

    "Lakini watu wenye imani kubwa kabisa na mungu wenu, huwa hawakutani na mambo kama hayo. Ndiyo maana baadhi yenu wenye imani kubwa hata kama vipato vyao ni vya kawaida, maendeleo yao huwa yako juu sana kwa sababu hawana roho huyo mchafu, fuatilieni sana."

    Kila mtu alikuwa kimya, tukimsikiliza kiumbe huyo. Ilikuwa ni elimu ambayo sikuwahi kuisikia mahali popote duniani!

    "Ninyi binadamu mna uwezo mkubwa sana, ndiyo maana hata mungu wenu kabla hajawaumba, alisema aumbe watu wa kufanana naye! Kwa maneno mengine ninyi ni mfano wake! Si kwa sura bali kiuwezo japo si kwa asilimia zote.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sasa mbona mnayumbishwa na mambo madogo kama hayo? Ndiyo maana kutokana na imani yenu ndogo wengi wenu hukimbilia kwa waganga bila kujua kabisa kuwa hata hao waganga huongozwa na roho wachafu juu ya nyota zenu.

    "Huko mbele nitafafanua zaidi kuhusu waganga wenu wa kienyeji na jinsi wanavyowaibia kwa kutumia nyota zenu, ila kwa sasa nilitaka niwagusie kidogo kuhusu imani kabla sijaendelea na somo hili la nyota.

    "Angalia hata sisi, japo tuliasi, lakini tunawazidi mambo mengi sana kwa sababu tunakuwa na imani kwa mambo tuyatendayo.

    "Mfano, kiumbe yoyote akiwa na imani pasipokuwa na shaka, anaweza kutembea hata juu ya maji! Lakini akiwa na mashaka kidogo tu, lazima azame.

    "Ndiyo maana hata yule Petro, alipokuwa na yule nabii wenu alijawa na imani na akaweza kutembea juu ya maji lakini alipoanza kuwa na mashaka kidogo tu alianza kuzama!" alisema yule kiumbe na kutulia kidogo.

    Alitoa mfano wa Petro kwa kutaja jina nabii wetu, akiwa na maana Yesu ila asingeweza kutaja jina Yesu kwani ni mwiko mkubwa sana kule kulitaja.

     




    Yule kiumbe alituangalie wote kwa zamu, akatulia kwa muda wa kama dakika moja nzima halafu akaendelea kusema:

    Tuachane na habari hizo, sasa tuangalie nyota ya Mapacha ambayo hujulikana kwa lugha ya kigeni kwamba ni Gemini.

    Nyota hii ni ya tatu katika orodha ya nyota zinazomgubika binadamu ulimwenguni. Wengi wenye nyota hii wakitaka kufanikiwa na maisha yao kuwa mazuri lazima wawe watangazaji, wafungue ofisi ya kutoa ushauri nasaha, hasa wa watu waligombana kwa mapenzi.

    Wakiamua kufanya kazi ya kuchapisha vitabu pia hufika mbali sana. Lakini kama wana mitaji hata midogo wakaamua kufanya biashara ya kusafirisha bidhaa huwa matajiri wakubwa baada ya muda mfupi.

    Kama mtu anajijua ana nyota ya Kaa ambayo kwa lugha nyingine inaitwa Cancer, mafanikio yake makubwa yapo kwenye kufanya kazi benki mbalimbali, kuwa baharia kutoka nchi moja kwenda nyingine na uandishi wa habari.

    Mara nyingi watu hawa wakifanya kazi hizo huwa na vyeo vikubwa na kulipwa marupurupu makubwa hali inayowafanya wabadili maisha yao. Ndiyo maana hata kama mtu akiwa na nyota hii halafu asifanye kazi maeneo hayo, lakini atakuwa msimamizi mahali pake.

    Hebu tuiangalie nyota ya Simba au kwa lugha ya kigeni Leo. Hii ndiyo nyota yenye machafuko na umaarufu duniani pote. Ni nyota inayaosumbua wengi bila kujua. Ni ya Julai 22 hadi Agosti 22.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Viongozi wote duniani waliowahi kuvuma na kutawala kisha wakasikika walikuwa na nyota ya Simba.

    Wenye nyota hii lazima wawe watawala katika eneo lolote lile. Kama ni mtoto ndani ya familia basi atakuwa na sauti yenye mamlaka hata kama wako waliozaliwa kabla yake.

    Watu wengi maarufu duniani walizaliwa mwezi huu tena walivuma sana na wanaendelea kuvuma. Mtoto mwenye nyota hii akikuzwa vizuri akaangaliwa kipaji chake lazima aje kuwa mtu maarufu.

    Labda niwape mfano wa watu maarufu duniani wenye nyota hii.

    Kuna Bill Clinton yeye aliwahi kuwa Rais wa Marekani (alizaliwa Agosti 19). Barak Obama (Agosti 4), Napoleon Bonaparte (Agosti 15), Neil Armstrong (Agosti 5), Kobe Bryant (Agosti 23), Michael Jackson (Agosti 29), Lady Madonna (Agosti 16).

    Wengine ni kama Halle Berry (Agosti 14),

    Magic Johnson (Agosti 14), Mama Teresa (Agosti 26), Fidel Castro (Agosti 13),

    Malkia Elizabeth (Agosti 4), Yassar Arafat (Agosti 24) na wengine wangi sana.

    Kifupi wengi wenye nyota hii huwa watawala, maarufu au wasumbufu katika jamii.

    Kwa upande wa ndoa, mwanamke mwenye nyota hii huwa mtawala kwenye ndoa yake labda kama ataolewa na mwanaume mwenye nyota ya Mshale kwa lugha ya kitaalam Sagittarius.

    Kwa kawaida watu wenye nyota ya Mshale wana kinga kubwa kutoka kwenye nyota mbalimbali.

    Hapa nataka kusema wazi kwamba binadamu wengi hamjui kuishi kwa kutumia maisha ya nyota. Hasa nyie watu weusi ndiyo kabisa.

    Lakini kama binadamu mngekuwa mnajua kuishi kwa kufuata nyota mngeepuka mambo mengi sana. Mwanaume mwenye nyota ya Mbuzi au kitaalam Capricorn asije akafunga ndoa na mwanamke mwenye nyota ya Simba kwa sababu hawatawezana.

    Ndoa zenu siku hizi zinavunjika sana kwa sababu wanandoa hawakubaliani nyota zao. Hili suala la nyota za wanandoa kutokubaliana ndiyo husababisha ndoa kuingiliwa na ushetani na kuvunjika haraka.

    Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya nyota na wanandoa, hata siku ya kufunga ndoa pia lazima ihusiane na nyota. Ndoa za kufungwa mwezi wa Oktoba si imara sana kama za mwezi Novemba.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini mwezi wenye ndoa zinazodumu maisha ni Januari, ingawa tunawaona kule kwenu duniani mwezi Januari hawafungi ndoa kwa kisingizio cha mwezi mgumu una mambo mengi.

    Yale mambo mengi tunayatawanya sisi ili watu waishi wakiwa wanajua hivyo lakini ukweli ni kwamba sisi hatupendi watu mfunge ndoa mwezi wa Januari kwa sababu hatutaki ndoa zidumu.

    Kwa upande mwingine, nguvu ya nyota hii katika utawala huonekana pale ambapo mtu mwenye nyota ya Simba anatawaliwa na mtu mwenye nyota ya Samaki, hapo hapatakalika. Migogoro na uasi hutokea.

    Baadhi ya viongozi duniani waliwahi kupinduliwa na watu wenye nyota ya Siimba kwa sababu wao hawakuwa na nyota hiyo. Waliwatawala wakiwa na nyota dhaifu sana.

    Tukiachana na yote, namalizia na nyota ya Simba kwa kusema kuwa wengi wenye nyota hii ni wanamichezo, masonara, wanamitindo, wacheza sinema na kazi zinazohusiana na mambo ya vijana.

     




    Kabla sijaendelea mbele na lile darasa nililolikuta kule kwa viumbe napenda kuwajulisha kwamba, kila binadamu ana nyota yake inayoambatana na maisha yake ya kila siku.

    Nasema hivi kwa sababu nilimsikia yule kiumbe akisema hivi:

    "Unajua kama binadamu wote kule duniani wangejua uwezo wa nyota zao wangekuwa wanafanya makubwa sana. Lakini hamna kitu kwa sababu hawajui lolote lile. Kila binadamu anayezaliwa na mwanamke ana nyota yake inayomwangazia, hata yule nabii wenu (Yesu) naye alizaliwa akiwa na nyota yake ndiyo maana kwenye maandiko yenu mmeandika kwamba nyota yake ilionekana kutoka upande wa Mashariki.

    "Ile yenyewe inadhihirisha kwamba kila binadamu ana nyota yake. Na nyota kwa kawaida inaonesha tabia ya mtu, karama yake au kule duniani mnasema kipaji au kwa nini binadamu alizaliwa.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini wapo binadamu ambao nyota zao huchukuliwa na inapotokea hivyo yale yote yanayohusu nyota yake yanakuwa hayapo tena katika maisha yake.

    Kuna tofauti kubwa sana kati ya elimu ya kawaida na nyota kila kukicha, suala la elimu si la nyota na nyota ya binadamu haipatikani shuleni au vyuoni ndiyo sababu wapo binadamu hawana elimu kabisa lakini wana mafanikio makubwa katika maisha.

    Nyota pekee ndiyo inayoweza kumfanya binadamu kuwa mzuri au mtaalam wa jambo fulani, kama wanamuziki, wacheza mpira, madereva au mambo mengine mengi yenye kutaka kufanywa na watu mbalimbali.

    Nyota huweza kumpa akili ya ziada ndani ya akili yake akaweza kufanya jambo ambalo wengine walilishindwa kwa kutokuwa na akili hiyo.

    Lakini nyota hiyohiyo ndiyo inayoweza kumfanya mtu ang'ae na kuonekana zaidi mbele ya watu, au tuseme mtu anakuwa na mvuto.

    Siku hizi binadamu wengi kule duniani wanahangaika kuanzisha biashara mbalimbali tena kubwa tu, wanakopa mikopo mikubwa tu, lakini hawaoni maendeleo yoyote zaidi ya kudidimia kwa sababu nyota zao zinazowaongoza zimezolewa na wabaya wao ili wateseke au ili wakawape watu wengine.

    Wapo binadamu wenye utaalam wa kumpoka mtu nyota yake yenye mafanikio ya kibiashara na kwenda kuwapa watu wengine ambao wanateseka kusaka maisha mazuri yenye mafanikio.

    Kuna mwenye swali kabla sijaendelea? aliuliza yule kiumbe. Mimi nilinyoosha mkono, akaniuliza wewe unasemaje? Halafu unajua kule duniani wanadamu, nduguzo bado wanaomboleza kifo chako?

    "Sijui," nilimjibu.

    Ndiyo hivyo nilivyokwambia. Leo mchana wa kule jeneza lako linaandaliwa ili ukazikwe.

    "Mimi?"

    Wewe ndiyo. Lakini sidhani kama utazikwa kwa muda huu tunaouendea wa nusu siku. Haya uliza swali.

    Nilibabaika kidogo kutokana na mazingira ya kauli ya yule kiumbe, lakini nikajitutumua na kuuliza:


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sasa binadamu atajuaje kuwa nyota yake imechukuliwa na wabaya wake?"

    Aliniangalia kwa macho yaliyoonesha kuwa swali langu lilikuwa na umakini wa hali ya juu, akasema: Binadamu akiwa hana nyota inayomwangazia maisha yake hata kama atakuwa ana elimu ya juu ya vyuo vikuu lazima atakosa dira ya maisha yake. Kama ni mfanyabiashara haitakwenda vizuri, atakuwa anadaiwa na mabenki na taasisi za fedha.

    Au angalia mtu anayefanya kazi kubwa, muda mwingi yupo kazini analipwa mshahara mkubwa tu lakini hana msingi wa maisha kwa kuwa nyota yake imepokwa na wabaya wake.

    "Katika hili kazi ipo, siwezi kushauri hasa nini cha kufanya kwani nafasi hainiruhusu hapa lakini kuna kitu cha kufanya."

    Basi, yule kiumbe akaendelea kufundisha kuhusu nyota sasa.

    Nyota nyingine ni ya sita, inaitwa Mashuke au lugha ya kigeni inaitwa Virgo. Binadamu kama nyota yake haijapokwa na wabaya wake, mwenye nyota hii ambayo inamhusu aliyezaliwa Agosti 23 hadi Septemba 22, mafanikio yao makubwa ni kwenye kazi ya uchapishaji, uongozi wa mahali, kazi ya afya, biashara mbalimbali na ukatibu (secretary).

    Nyota hii haina watu maarufu sana kama ya simba kwa sababu mashuka huweza kufunikwa na nyota nyingine mbalimbali nyingi, haina nguvu kubwa ya kupambana.

    Nyota nyingine ni ya saba ambayo ni Mizani au kwa lugha ya kigeni ni Libra. Watu wa Libra walizaliwa Septemba 23 mpaka Oktoba 23, hawa ndiyo wanahusika.

    Kazi zao zenye kuwapa mafanikio ni uhusiano katika jamii, ushauri wa masuala ya ndoa. Wengi waliotaka kupeana talaka waliposuluhishwa na wenye nyota hii walirudiana na ndoa kudumu.

    Pia ni wafanyabishara wakubwa sana hasa ya mambo ya sanaa, mambo ya sheria au uhakimu. Mtu mwenye nyota hii akiwa wakili anashinda sana kesi na wateja kwake hawapungui. Kama atakuwa hakimu atakuwa anatoa hukumu ya haki kwenye kesi ngumu.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa wale wanaoamua kufanya biashara ya sanaa hufanikiwa sana, mfano ni kama wanamuziki akina Lil Wayne, Bella Thorne, Eminem, Kim Kardashian, Will Smith, Ushar Raymond na Snoop Dogg.

    Wapo marais wenye nyota hii na waliongoza mataifa makaubwa, mfano ni Jimmy Carter wa Marekani. Marais wengi wenye nyota hii hufanya kazi zao kwa busara sana na utulivu, hawakurupuki, si wapenda vita wala udikteta.

    Wanapoachia madaraka wengi huishi maisha ya heshima sana na jamii huwatambua miaka na miaka.

    Wacheza mpira wenye nyota hii pia hung'ara sana ulimwenguni, kama akina George Opong Weah, Muset Ozil, Ibrahimovic, Vidoc, Defoe na wengine kibao ambao nyota zao ni Libra na wakafanya vizuri kwenye mpira wa miguu.

    Ipo nyota inaitwa Nge, lugha ya kigeni inaitwa Scorpio. Hii ni nyota ya nane kati ya kumi na mbili za duniani. Hiii ni nyota yenye majukumu mengi sana, dunia imeendelea kupitia watu wenye nyota hii. Kama wanadamu wangejua wangefanya juu chini kuzaa kipindi cha nyota hii ya Scorpio.

    Mtu mwenye nyota hii ili afinikiwe anatakuwa kufanya kazi za madawa, upelelezi na uchunguzi. Hata wavumbuzi wengi wa mambo ya kihistoria wapo kwenye kundi la nyota hii.

    Watu waliogundua vitu vingi vya kisayansi, kama ndege, meli nakadhalika wanatoka kwenye nyota hii.

    Lakini kuna binadamu wanasumbuliwa sana na mambo ya mapenzi, washauri wao wakubwa wanatakiwa watu wenye nyota hii.

    Kuna nyota inaitwa Sagittarius au Mshale. Hii nyota inawafaa sana watu ambao watafanya kazi za kusafiri, kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupeleka bidhaa au kuchukua, lakini wanasheria wazuri sana wanatokea kwenye nyota ya Mshale. Wakiwa waandishi wa habari wanakuwa mahiri zaidi na huvuma muda wote.

    Ili wawe na mafanikio makubwa, wenye nyota hii wanatakuwa pia kufanya kazi ya ualimu, wachungaji wa makanisa wanaweza kujikuta wanavuta waumini wengi sana kama wana nyota ya Mshale. Wachungaji wenye nyota hii, wanakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kutenda miujiza mingi ya kuwashangaza wengi.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pia wenye nyota hii wana uwezo mkubwa wa akili, kufikiri na kukwamuka kutoka katika matatizo. Mwanamke yeyote, hata kama ana nyota ya Simba, akiolewa na mwenye nyota ya Mshale atakuwa chini yake tu.

    Nizungumzie nyota ya Capricorn au Mbuzi kwa jina la kujulikana kule duniani mnakotokea nyinyi. Hii nyota huwa ya utajiri mkubwa kama wahusika watafanya shughuli zifuatazo:

    Uinjinia, uchoraji wa ramani za majengo, watafiti wa ardhi, kuajiriwa serikalini. Mara nyingi mwenye nyota hii akiajiriwa serikalini hupanda cheo kwa kasi sana, anaweza kuanzia chini akapanda hadi kuwa waziri na watu wakamshangaa.

    Lakini wanasiasa wengi mahiri mkiwachunguza kwa karibu wana nyota hii ya Mbuzi. Tena wengi wanapopanda majukwaani hupigiwa makofi sana, hushangiliwa. Wana uwezo wa kuwashawishi watu kufanya jambo fulani, mfano kupigiwa kura.

    Mtu akiwa na nyota ya Mbuzi na akataka kugombea nafasi ya siasa huwashinda wenzake kwa kura nyingi sana, ni mahiri wa kujibu maswali ya watu kama ataulizwa.

    Kabla sijaendelea napenda kuwaambia kuwa maskini wengi au fukara wengi ni wale wanaofanya shughuli ambazo nyota z
    ao zinakataa. Mtu nyota yake anatakiwa kuwa mwalimu, anaamua kuwa mfugaji, huyu lazima atalia. Kama atakopa mkopo kwa ajili ya kununua ng'ombe ili afuge atajikuta ng'ombe wote wanakufa kwa sababu nyota yake inakataa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pia kuna jambo moja ambalo binadamu wengi linawaingiza katika umaskini bila wenyewe kujua. Mfano, ni vibaya sana mtu kuishi kwenye nyumba ambayo, ukienda kazini, jua linakupiga usoni, ukirudi nyumbani jioni pia jua linakupiga usoni.

    Hapa sidhani kama kuna sababu ya kufafanua sana, ni uelewa mdogo tu. Ni vizuri mtu anapoishi iwe sehemu ambayo akienda kazini anapigwa na jua kisogoni, akirudi jioni hivyohivyo.

    "Yule kiumbe aliposema hivyo tu mimi nikawaza kwamba, mfano mtu anaishi Kimara, kazi anafanyia Kariakoo, kwa hiyo asubuhi anapokwenda kazini jua linamuwakia usoni, jioni pia kwa sababu jua linakwenda kwenye kutua sasa.

    "Nikamwelewa kuwa, ana faida sana mfano, mtu anayeishi Magomeni halafu kazi anafanyia Ubungo, akienda kazini jua linampiga kisogoni, akirudi jioni jua linakuwa limeshageuka, pia litampiga kisogoni.

    Akaendelea kusema:

    Pia watu waogope sana kulala kwenye vyumba ambavyo madirisha yake yanatazama upande unaotokea jua au mlango unaoingilia chumbani unatazamana na karo la maji au sehemu ya kuoshea vyombo.

    Vyombo vya kupikia, wengi wanasema wamekula vyakula vibaya wameendesha, lakini ukweli ni kwamba kupika chakula halafu ukatoka jikoni huku umechukizwa na jambo fulani husababisha anayekula matumbo kuendesha.

    Wapo binadamu wanakula sana lakini hawanenepeshwi na chakula hicho, sababu kubwa ni tabia ya kula chakula huku mtu anayekula shingo yake imepindia upande mmoja, uwe wa kulia au kushoto na si nyuma wala mbele.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog