Search This Blog

NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 5

 





    Nusu Siku Ndani Ya Jeneza

    Sehemu Ya Tano (5)



    Hii tabia huku tulipo tunaichukulia kama ni kujinyima ndiyo maana mtu anakuwa hanenepi hata akila vipi kwa sababu kule kupindisha shingo ni sawa na kukilaumu chakula hiho hivyo unaondoa uwezo wake wa kufanya kazi vizuri mwilini!

    Wengine, wengi tu wapo wanaokula chakula huku wana amani. Watu hawa hata wakila mboga za majani kila siku, watanenepa tu kwa sababu wanakipa chakula uwezo wa kufanya kazi vizuri mwilini.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wengi wanaolaani chakula chao, utawaona wakiwa mfano baa au hata nyumbani, kikiwekwa tu mezani, anaanza kusema maneno ya kukilaani chakula, mfano kama ni kwa mgahawani a hotelini utamsikia mtu akisema:Huu wali mbona kama una mabongemabonge, halafu nyama mchuzi mwepesi sana. He! Mboga za majani umeokota au. Mimi nitakuwa silipi hiki chakula. Ona nyama zilivyo ngumu.'

    Hayo maneno ni ya laana kwa chakula, hata kama kipo vizuri lakini kwa maneno hayo lazima mtu huyo atakuwa kimbaumbau.

    Kwa wale wanaoumwa, kila dawa ni dawa ndani ya mwili wa binadamu, ila akili au mawazo ya binadamu wenyewe ndiyo yanasababisha kuwepo na tofauti.

    Mfano mzuri, utakuta binadamu anaumwa kichwa, lakini katika hizo dawa anachagua, kwamba dawa yenye jina fulani ndiyo inamponesha kuliko dawa nyingine.

    Kusema ule ukweli hapo hamna ishu ya dawa, ila akili za mtu. Na mtu akizoea kusema hivyo maana yake ni kwamba hata ugonjwa wenyewe utakuwa wa kwake. Kuna binadamu wanaumwa halafu wakiulizwa wanajibu:;Huu ndiyo ugonjwa wangu mwenzio.'

    Sasa turudi kwenye nyota kwanza, tumalize na kuendelea na mambo mengine. Nilikuwa naendelea kwenye nyota nyingine ambapo sasa tuiangalie nyota ya Ndoo au Aquaries kwa jina lingine.

    Kama binadamu amezaliwa baada ya tarehe 22 ya mwezi Desemba mpaka Januari 21 nyota hii ni sawa kwake. Ili abadili maisha yake kuwa mazuri, atatakiwa kufanya kazi ya umeme, kama vile mashirika ya umeme ya nchi zao, wawe mafundi wa kampyuta, lakini pia watu wenye nyota hii watafanikiwa sana kama watafanya kazi ya uchunguzi wa kisayansi, kazi za kujua elimu ya anga, hasa sayari na kazi ya kutunza mazingira.

    Hii kazi ya kutunza mazingira ina maana kwamba binadamu huyo hata kama ataamua kulima bustani za maua au mboga ataweza kuwa tajiri.

    Nataka kusema kwamba wapo binadamu wanaokimbia kazi fulani kwa sababu wameshawaona wenzao wamefanya na hawajafanikiwa. Binadamu hatakiwi kutembelea nyota ya mwenzake.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuna binadamu ni waalimu na maisha yao ni mazuri, makubwa na yanavutia, lakini wengine wanaamini hakuna kazi haina fedha kama ualimu. Kumbe yule aliyefanikiwa ni nyota yake inamruhusu kuwa mwalimu, mwingine haimruhusu.

    Kikubwa ni kila binadamu kufuata au kutafiti nyota yake ni nini na biashara gani afanye. Wengine wanakosa utajiri kwa sababu hawajui lolote. Unakuta binadamu anaanzisha

    duka halafu fremu za duka lake zinaangalia kusini au kaskazini, nani atakuja kununua wakati uwazi wa duka unaangalia upande ambao unakinzana na mzunguko wa dunia.

    Dunia yenu ipo na itaendelea kuwepo, maisha yenu duniani ni ya kubahatisha kwa sababu binadamu hawaombi au hawasali, ni kitu kibaya sana.

    Kuhusu hili la kusali naomba msiende kuwaambia kwa sababu huku tulipo, pamoja na himaya hii kubwa mnayoiona lakini hakuna kitu tunakiogopa kwa binadamu mwombaji. Ni hatari sana kwetu.

    Siku zote mwombaji ndiye anayetuumiza, anasababisha tunaungua, tunaingia vilema. Kwa kweli kila nikifikiria naumia sana. Hebu kwanza twendeni huku mkaone watenda kazi wetu walivyounguzwa, kupata ulemavu kwa sababu ya hao waombaji.

    "Wakati yule kiumbe anasema hayo, alishatoka eneo alilosimama na kutembea akituangalia ili tumfuate.

    "Tulitembea kama umbali wa dakika kumi tukafika kwenye banda moja la mabati, lakini si ya kuezekea nyumba. Tukaingia ndani na kusimama, kwa mbele yetu tuliweza kuwaona viumbe wa ajabu sana wakiwa wamelaliana, wengine wanalia, wengine wanaonesha sura zenye majonzi makubwa.

    "Wengi wao walikuwa wakituangalia, kasoro wachache tu ambao walionekana kama wamelaliwa zaidi na wenzao. Yule kiumbe akasema:

    "Hawa wote walikutwa na matatizo makubwa sana kutokana na wanadamu wanaojua kuomba au waombaji. Kuna yale maombi yenu mnamtaja jina bwana mmoja (akimaanisha Yesu). Lile jina linatuumiza sana sisi huku. Tena linatuumiza sana.

    Ila na sisi kati ya mambo ambayo tunayakeshea huku na watu wanaoomba. Mpango wetu mkubwa ni kuwatupia mashile waombaji wote, iwe mchana, usiku au muda mwingine.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama mtakumbuka sana, mtu anayeomba huwa ananyemelewa sana na usingizi hasa kama ni usiku au lazima tutampa kibarua cha kuwaza jambo lolote ambalo halihusiani na yale maombi anayofanya.

    Mfano mdogo, kama mmewahi kuchunguza ni kwamba, mara nyingi binadamu anaposali kwa kumaanisha, huwa anafuumba macho dakika chache baada ya kuanza sala.

    Kinachotokea ni kwamba, anaposali amefumbua macho sisi tunamwelekeza kuangalia kitu chochote pale alipo. Kama ni sebuleni tunaweza kumwelekeza aangalie hata picha za siku ya harusi yake ukutani.






    Baada ya kuangalia tunampa mawazo yule mwombaji. Kama alikuwa anaangalia picha za harusi, sisi tunampa mawazo ya kumwambia:

    Ile picha siku ya harusi yako, ulipendeza sana. Itabidi siku moja uchukue picha moja ukaitengenezee fremu kubwa, unajua ule ni ukumbusho mzuri sana?




    Au utakuta binadamu yupo kanisani, wakati wa kuomba yeye hafumbi macho. Tunachofanya tunampa mawazo, kama ni kwa mchungaji wake aliye mbele anaweza kujikuta akisikia sauti ikisema:

    Lakini mchungaji wako huyu anajua sana mafundisho, si eti? Binadamu bila kujua anaweza kusema moyoni ni kweli anajua'. Halafu tunaendelea kumpa mawazo mengine, tunamwambia:

    Leo ukitoka hapa ukamjulie hali dada'ko, si uliambiwa jana anaumwa sana. Atakuona humjali usipokwenda. Binadamu huyu ndani ya moyo wake atasema:

    Ni kweli, nikitoka tu naenda.'

    Hapa nataka kuwaambia jambo moja muhimu sana kwamba hali hiyo husababisha kuondoka kwa uwepo wa Mungu wenu katika maombi. Siku zote nguvu ya maombi ndiyo inayofanya kazi katika maisha yenu ya duniani.

    Binadamu kama mngejua kwamba maombi yanaweza kuwafanya mkawa juu basi mngekesha usiku na mchana mkiomba, lakini kwa sababu hamjui ndiyo maana mnalia kila siku na mnakumbwa na matatizo kila kukicha.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wapo binadamu ambao kuomba kwao ni kila siku asubuhi, usiku wakitaka kulala na wanapopatwa na matatizo lakini nataka kuwaambia nyie kwamba muda mzuri wa kuomba ambao huwa unatusumbua sisi hata katika utawala wetu ni usiku wa manane.

    Muda huo anga huwa jeupe, sisi watumishi wetu wanakuwa wamerudi kujipanga kwa mambo mengine. Muda huo maombi ya binadamu kwa Mungu wao yanaweza kupita na kufika kwa mhusika bila kukumbana na kizuizi chochote kile.

    Labda niwakumbushe kama mmesahau. Katika maandiko ya Mungu wenu kuna mahali palionekana mtu alikuwa akiomba (Daniel) lakini maombi yake yalizuiwa na mkuu wa anga ambaye ni wa huku kwetu, ikabidi mtumishi mmoja wa Mungu wenu (Malaika Mikaeli) ashuke na silaha (sime) ili kumpigania yule mtu maombi yake yapite.

    Sisi tuna uwezo wa kuzuia maombi yenu yasiwafikie kama Mungu wenu atakuwa amewajibu. Ndiyo maana yule mtu aliambiwa na yule mtumishi kwamba maombi yake yalishafika kule juu kwa Mungu wenu na alijibiwa, lakini majibu yalizuiwa angani kwa siku kadhaa.

    Sasa kama ni hivyo hapa tunajulishwa kwamba kumbe binadamu mnaweza kuomba na mkajibiwa lakini majibu hayo sisi wakuu wa anga tunaweza kuyazuia kwa siku kadhaa. Hapa kinachotakiwa kwa binadamu ni kuzidi kuomba kwa kupinga nguvu ya wakuu wa anga wanaozuia maombi.

    Wapo binadamu wakiomba shida zao zinaendelea kuwepo mpaka wanasema Mungu hanisikilizi au amenitenga lakini kumbe sababu kubwa ni hiyo majibu yamezuiwa angani.

    Leo nawafunulia siri hii nyie kwa sababu si wa kule tena na mkirudi mtafanya kazi chini ya sisi kwa kiapo kikuu, atakayekiuka atakuwa amejitabiria kifo kibaya mwenyewe.

    Aliposema hivyo tu nikajikuta nakosa nguvu ya mwili, nilijisemea moyoni kwamba ina maana mimi nitakuwa nikifanya kazi za kishetani? Ina maana mimi si binadamu tena? Nikataka kumuuliza swali, lakini yeye akawahi kwa kusema:

    Sasa tumalizie na nyota ya Samaki ambayo kwa jina lingine inaitwa Pisces. Hii nyota inawahusu watu wote waliozaliwa Januari 21 hadi Februari 20. Wenye nyota hii watakuwa wazuri sana kama watakuwa waigizaji, wanamuziki, kazi ya huduma ya matibabu, hasa unesi, ulinzi kama polisi wa majini na utumishi wa Mungu.

    Wako waigizaji wengi maarufu duniani ambao walianzia kwa kuwa chini wakapanda kwa sababu tu ni wenye nyota hii ya Samaki.

    Mtu mwenye nyota hii, siku moja akijaribu kazi ya sanaa atashangaa itakavyomtoa katika maisha yake yote.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyota zote nilizozitaja si rahisi mtu kujua zilivyo, lakini kama atafuatilia sana ataweza kubaini. Wale watu wasiopenda kwenda kwa wataalam wa kuangalia nyota, hao wanaweza kujua nyota zao kwa tabia ya kufanya jambo moja baada ya jingine.

    Kama watauza duka halafu ndani ya miezi sita hawoani mafanikio ni bora kubadili. Wengi wanazijua nyota si kwa kugundua bali katika kuhangaikia maisha tu wanajikuta wamebahatika kufanya mambo yanayoendana na nyota zao.

    Kuna kitu cha kujifunza mtakaporudi duniani kwa njia nyingine lakini si ile mliojia huku na kule mtatakiwa kutosema au kuanika lolote la huku, naamini hili nalizungumzia kama msisitizo kwani nimeshalisema awali.

    Kama atatokea binadamu kati yenu akaanza kuanika siri alizoziona na kujifunza huku huyo atakuwa ametangaza hali ya hatari kati yake na yetu sisi wakuu wa anga ya juu.

    Haya sasa inabidi kila mmoja apite mbele yangu na kukiri kwamba atakaporudi ulimwenguni atafanya kazi chini ya maelekezo yetu. Nataka kuwahakikishia kwamba kila mmoja wenu atakuwa akisikia maelekezo yetu pale ambapo patakuwa pagumu sana atasaidiwa kwani sisi hatushindwi na binadamu yeyote yule.

    "Alipomaliza kusema hivyo, alituamuru kila mmoja apite mbele yake ili amuwekee mikono kama kiapo chake. Hali ilikuwa sivyo kwangu sikutaka kabisa kukubaliana na tukio lile.

    "Sikuwa tayari kupita kwake na kuniwekea mkono au mikono kwani hilo nililiona kama ni kumsaliti Mungu wangu ambaye niliamini hata wao viumbe pia hawamuwezi.

      




    NIKAANZA kuangaza huku na kule, moyo ukawa unaenda kwa kasi ya ajabu sana. Moyoni nikajawa na wasiwasi mkubwa ambao sikujua ulitoka wapi.

    Nataka kila mmoja akae kwenye mstari kwa ajili ya kupita kwangu, ni kitendo cha haraka sana.

    Akazidi kutuamuru yule kiumbe, lakini safari hii alikuwa makini na siriaz sana, kwani alikunja sura kwa kumaanisha alichokizungumza.

    Wenzangu wote walijipanga mstari kwa ishara ya kukubaliana na amri ile, mimi na wenzangu wawili tulikuwa bado tukijikokota.

    Basi, yule kiumbe akaamka na kuja hadi mahali tulipokuwa tumekaa.

    Akatutaka sote tujipange mstarini kama alivyokuwa akielekeza.

    Kwa shingo upande, tukajipanga kwenye mstari na kuanza kumsogelea yule kiumbe ili tukiri kuwa tutafuatisha maagizo yake.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa baada ya zoezi hili, kuna nguvu kubwa na ya ajabu mno itakayoingia ndani yenu, na mtakuwa viumbe wapya kabisa na kuyafurahia maisha haya kwani mtakuwa mkifanya mambo yenu kwa uhuru mkubwa bila kipingamizi chochote kutoka kwa viumbe dhaifu kama bibadamu,” alisema.

    Akawa anasisitiza, lakini safari hii sauti yake ilitoka kwa juu sana huku ikiwa na kitetemeshi ndani yake, hali iliyomshitua kila mmoja wetu na kuanza kuingiwa na hofu kubwa ndani yetu.

    “Zoezi likaendelea hadi ilipofika zamu yangu. Hakika sikuwa tayari kabisa kukiri mbele ya huyo kiumbe kuwa nitafuata amri zake. Nilijiona kuwa na hatia kubwa mno kufanya jambo hilo kwani lilidhihirisha kuwa Mungu wangu wa Mbinguni alikuwa ameshindwa mbele ya viumbe wale.

    Wewe, sogea hapa muda umekwisha nataka tupangiane majukumu.

    “Aliniamuru yule kiumbe baada ya kuona nasitasita kusogea karibu yake.

    “Hapa naomba niseme jambo moja. Hakuna kitu ambacho viumbe wa aina hiyo huwakasirisha kama kuona binadamu wa kawaida anaonesha kiburi mbele yao.

    “Basi, akawa ananiita nami niliendelea kusimama bila hata kujisogeza. Nikageuka kuwaangalia wenzangu ambao walikuwa wamekwisha tawazwa, nikakuta wakinishangaa. Lakini walikuwa tofauti kidogo. Macho yao yalikuwa makubwa na maangavu sana. Hata maumbo yao yalikuwa yamebadilika na kuwa makubwa kuliko yale ya awali”.

    “Nikiwa naendelea kujiuliza, ghafla nikaanza kuona giza nene mbele yangu, kizunguzungu kikali kikanizingira na kuishiwa nguvu kabisa.”

    “Kwa jina la Yesu Kristo aliye hai, kwa jina la Yesu, shetani tokaaa.

    “Nilijikuta nikikemea kwa nguvu kubwa sana, sikuelewa ni wapi nilipata ujasiri huo, lakini nikazidi kukemea tena na tena.”

    “Nilipokemea kwa mara ya mwisho, nilijikuta niko ndani ya jeneza!

    “Jeneza lililokuwa limefunguliwa upande wa kichwa. Watu wengi walikuwa wakizunguka na wengine wakilia huku walikitaja jina langu, hali ilitisha.”

    “Wakati naangaza huku na kule, nilishangaa kuona watu wote wakikimbia huku wakipiga mayowe na kusema marehemu amefufuka. Watu wote walikimbia na kuniacha peke yangu pamoja na mzee ambaye kwa kumuangalia kwa haraka, alikuwa ni mchungaji kutokana na aina ya mavazi aliyokuwa amevalia.”

    “Mkononi alikuwa ameshika biblia. Akanitazama usoni na kukutanisha macho.

    “Bila hata kumsalimia nikamuuliza mahali nilipokuwa.”

    “Hapa ni kijijini kwenu Kilosa, tumekuja kukuzika,” alisema yule mzee huku akinisogelea kwa ujasiri mkubwa sana.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Akapiga magoti na kujiegemeza kwenye jeneza na kuuunyosha ule mkono uliokuwa na biblia kwa upande wangu.

    “Kunizika.”

    “Ndiyo,” akanijibu yule mzee huku akianza kukemea kwa sauti ya chini mno.

    “Sasa hivi ni saa ngapi,” nilimuuliza.

    “Ni saa kumi na mbili jioni, tulikusafirisha kutoka huko ulikokuwa ukiishi tangu saa moja asubuhi, sasa kutokana na ubovu wa barabara, tumefika huku saa kumi na moja, kutokana na shughuli za kuweka mwili wako hapa na kukuaga, hatimaye imetimu saa kumi na mbili,” akazidi kunifafanulia yule mzee.

    “Tulikuwa tumeamua kukuzika jioni hii kutokana na maamuzi ya kifamilia yaliyofikiwa na baadhi ya ndugu zako.”

    “Nilikufa lini?”

    “Ulikufa alifajiri, ilipotimu saa moja tukakuweka kwenye jeneza tayari kwa kukusafirisha,” akanijibu yule mzee ambaye alijawa na ujasiri wa ajabu mno.

    Hapa naomba niseme kitu kimoja. Watu wa Mungu huwa na ujasiri wa hali ya juu mno, hata kama watakumbana na maajabu kama yangu ya kufufuka.

    “Ina maana nimekaa nusu siku ndani ya jeneza?,” nikamhoji kwa huku nikiwa nimemkazia macho yule mzee.

    “Ndiyo kijana wangu, umekaa nusu siku ndani ya jeneza, hebu nieleze ulikuwa wapi?,” aliniuliza yule mzee na kunifanya nishtuke kwani sikutegemea kama angeniuliza swali kama lile.

      


    "Nilikokuwa siwezi kusema, naogopa ila cha msingi naomba niletewe mchungaji aniongoze sala ya toba ili niokoke. Hivi kweli nimerudi duniani? Niliuliza.

    "Umerudi duniani, mimi pia ni mchungaji na ndiye niliyekuwa naendesha sala ya kuuaga mwili wako kabla ya kupelekwa makaburini kuzikwa.

    "Sasa kama upo tayari toka ili nikutubishe," alisema mchungaji huku akiinama ili kunitoa kwenye jeneza. Nilijitahidi nikasimama, nikatoka huku nikipepesuka.

    Nilipiga magoti, sala ya toba ilipoanza tu, watu walirudi na kuingia ndani huku wakinishuhudia.

    Niliongozwa sala ya toba, nikaokoka rasmi siku hiyo. Watu walishangaa sana, wengi walipenda kujua nilikokuwa kulikuwa kunafananaje, lakini sikusema na hata mchungaji aliwaambia nilikataa kusema.

    Nilichoamua, ni kuwa mtumishi wa kanisa la mchungaji yuleyule pale Kilosa aliyeniongoza sala ya toba ambapo natumikia mpaka sasa. Dar nimekuwa nikija kama hivi na kurudi kule. Namshukuru sana Yesu wangu, aliniokoa kwa jina lake. Amina."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MWISHO. 




     

0 comments:

Post a Comment

Blog