Search This Blog

NILILALA NA MAITI 20 ILI NIOLEWE NA RAIS - 1




      IMEANDIKWA NA : ANDREW CARLOS
      *********************************************************************************
      Simulizi : Nililala Na Maiti 20 Ili Niolewe Na Rais
      Sehemu Ya Kwanza (1)

      Machozi yangu yaliendelea kunibubujika katika paji la uso wangu mithili ya maji yakifuata mkondo wake. Niliendelea kugalagala chini huku nikiwa sijitambui. Kwikwi ya ajabu ilioambatana na kukohoa pasipo na mpangilio ilikuwa imenibana vilivyo. Sikuweza kuamini macho yangu kwa kile nilichokuwa nikikishuhudia mpaka pale niliposhikwa mkono na jirani zangu niweze kumwaga mchanga wa mwisho katika kaburi kubwa. Kaburi refu lililokuwa limechimbwa na majirani wema kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa mama yangu mpendwa, mama Adela. Mama aliokuwa ameniacha mimi mtoto pekee tangu alipofariki baba miaka mitatu iliopita na kutuacha katika kipindi kigumu cha kutegemea milo miwili kwa siku. 

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Umeniacha mkiwa mama, Niacheniii…?” Watu kibao waliokuwa wakionesha sura za huzuni walikuwa wamenizunguka. Ni mchungaji pekee ambaye alikuwa mbele ya uso wangu akiwa ameshikilia biblia. Nilianza kutapatapa kwa uchungu. Kutapatapa kwa kuendelea kumlilia mama yangu.Ghafla nilitekwa na nguvu za ajabu katika mwili wangu. Nikajikuta nimeyatoa macho ya ukali kuwaangalia wale wakina mama waliokuwa wamenishika. Mmoja wapo alionekana kuwa na ukali dhidi yangu. Hilo sikulistaajabu, kwa kutumia meno yangu niliweza kuwang’ata wote wawili mikononi mwao na ndio ukawa mwanya wa mimi kuchoropoka na kudumbukia katika kaburi la mama yangu. ‘Tiii’ nikasimama juu ya jeneza. Kamwe sikutaka kuyabinua macho yangu kutazama juu nilipotoka. Nguvu ya ajabu ikanishika na kuendelea kunitawala katika mwili wangu, nilijikuta nikifungua lile jeneza lililoupumzisha mwili wa marehemu mama yangu kipenzi, mama Adela pasipo woga wowote. “Mama? Mama? Amka mama yangu japo nikuone tena kwa mara ya mwisho mama?”Niliendelea kulia kwa uchungu huku mikono yangu miwili ilikuwa imeng’ang’ania uso wa mama yangu sambamba na kichwa chake kikikaribiana kabisa na cha kwangu.“Mama? Hutaki kuamka? Mie nitaishi na nani tena mama yangu?”Hasira ilinizidia mara mbili ya awali. Ilinibidi niutoe ulimi wangu nakuudumbukiza katika mdomo wa mama yangu. Nilichukua mikono yangu nikaisogeza mpaka masikioni mwa mama kisha nikamtoa pamba masikioni mwake nakudumbukiza vidole vyangu. Nilivuta pumzi yangu kwa kasi nikidhani huenda atashtuka. Hola! Kadri nilivyozidisha kuvuta pumzi ndivyo na harufu kali ilikuwa ikinirudia kutoka mdomoni mwa mama. Nikajihisi mwili wangu unabadilika kwa haraka zaidi. Ile mikono ambayo niliitumia kumuingizia vidole masikioni mwa mama yangu sasa ikawa imebadilika rangi na kuwa na maji maji mithili ya rangi ya kijani kijani. 

      *******“Hapa ni wapi? Na mama yangu yuko wapi?”“Nyamaza na utulie kimya Adela wewe?”Woga ulianza kunitanda kwa ghafla. Sauti kali ya kike ilikuwa imetingisha ngome ya masikio yangu baada ya kunitaja jina langu.Mwili wote ukaendelea kulowana si kwa maji bali kwa jasho langu mwenyewe. Sikujua sababu ilionifanya kufika katika eneo hili. Eneo lililokuwa limejaa maajabu ya kila aina. Hakukuwa na nyumba hata moja bali watu walikuwa wakipishana wenyewe tena walitembea wakiwa hewani. Si magari wala nyumba la hasha! hazikuwepo. Hakuna hata mmoja aliokuwa amevaa nguo zaidi yangu japokuwa nguo nilizovaa zilikuwa zimenipauka na kuchakaa kwa vumbi na damu damu lililogandia. Nilijihisi mwili wote kuishiwa na nguvu sambamba na kizungu zungu huku macho yangu yakionesha kutoshirikiana katika kumsikiliza mama aliyekuwa mbele ya macho yangu.“Adela unakumbuka mara ya mwisho ulichokuwa ukikifanya?”Alirudia jina langu kiufasaha hali iliyonitia woga mara mbili yake huku nikijiuma uma kwa kujibu.“Hapana sikumbuki”“Hukumbuki?”“Ndio sikumbuki na niambieni kwani nilifanya nini na hapa ni wapi mbona sielewi?”“Unawaona wasichana wenzako kule na kule wanaozunguka wakiwa uchi?”Haraka haraka niliyazungusha macho yangu kutazamana kinachoongelewa na huyu Mmama.“Ndio nimewaona”“Hawa wote hawana wazazi kama ulivyokuwa wewe na hapa unapowaona mchana huu wote tupo nao na ikifika usiku kila mmoja anaenda kazini”“Kazini? Ndio wapi na ofisi gani hizo za usiku?”“Eeeh he heee!! Embu wacha kunichekesha Adela. Wewe ulikuwa umeshapoteza uhai ukiwa ndani ya kaburi la mama yako pindi ulipokuwa unamlilia. Na hapa ninavyoongea na wewe si mtu hai bali ni mfu”“Mfu? Inamaana nilishakufa nikazikwa?”“Ndio Adela, wewe ni mfu. Mjini kote wanajua kuwa ulishakufa toka kipindi kile ulichodumbukia katika kaburi la mama yako na leo ni siku ya tano umezinduka hapa kwetu. Na ni sisi ndio tuliokupa nguvu za ajabu na kuweza kuishawishi akili yako ifanye vile mpaka kufikia hatua ya kumnyonya mama yako ndimi huku ukimdumbukiza vidole vyake katika masikio yake. Wale wadada unaowaona kule ndio waliofanikisha zoezi zima la kufanya mpaka upo hapa.”“Miiimi?”“Ndio wewe Adela na hapa ninavyokwambia wamezika gogo tu tena pembeni ya kaburi la mama yako wakidhani wamekuzika wewe!”Machozi ya uchungu yalianza kunitoka. Nilijitahidi japo kurudisha kumbukumbu lakini kichwa changu kiliishiwa na uwezo wa kufikiri kabisa. Nilijihisi akili na macho kukosa ushirikiano kabisa. Nilitumia mikono yangu kujipangusa machozi lakini nilistaajabu mikono yangu kuwa na damu damu.“Adela?”“Abee!!”“Umeingia kwenye himaya yetu huku na ni lazima ufuate mila na tamaduni za huku kwetu hayo mengine ya duniani yaache kama yalivyo sawa? Huna mama huna baba wala mume na hata watoto huna hilo tunalitambua na ndio maana siku zote tulitamani kuwa na mtu kama wewe na leo hii upo mikononi mwetu.”“Hapana mie nataka kurudi nilipotoka nirudisheni tafadhali, nirudisheniii?

      ”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Hasira zilifika kikomo lakini hazikusaidia chochote ndani ya himaya hii ya kufikirika. Nilijiangalia mara mbili mbili umbo langu kwa jinsi lilivyokuwa la kuvutia. Weupe wangu uliokuwa ukiwakosesha usingizi wanaume wengi waliokuwa wakiishi maeneo ya karibu na nyumbani sasa nilikuwa nikiushuhudia ukiharibika. nilijutia hata kwanini nilikataa kuolewa wakati nilipokuwa nikiishi na mama. Maneno ya mara ya mwisho ya mama yangu kuwa nitulie tu nitapata mume mwema sasa nikawa nikiyajutia nakuona dunia chungu. Posa ambazo nilizikataa kwa wanaume zaidi ya watatu waliokuja nyumbani kutaka kunioa ndizo ziliniongezea hasira zaidi. “Mama nataka unirudishe duniani, nakuomba tafadhali?”“Unajua Adela wewe ni mwanamke ambaye karibu kila kitu tumefanana na hata mimi nililetwa na hawa wachawi wenzangu pasipo kujijua mpaka huku na uzuri wangu niliokuwa nao. Tena wewe una bahati sana wamekuleta wanawake wenzako ukiwa tayari umeshakufa duniani. Mimi walinileta wazee kabisa na siku ya kwanza nilipofika nilichezewa sana mwili wangu ikiwa ni pamoja na kubakwa mfululizo na wazee. Kila ilipofika usiku ilinibidi ni lazima nilalae na wazee zaidi ya kumi na tano kwa usiku mmoja. Mwanzoni nilipata sana shida lakini kwa sasa nimezoea mwenzako na mpaka nimekuwa kiongozi wa wasichana wote wanaoletwa huku na mimi ndio wazee wamenipa uongozi wa kuhakikisha nawapa kazi za kufanya wasichana wapya kila inapofika usiku sambamba na kuwajaza nguvu zetu za kichawi. Kwanza niambie upo tayari kufanya nitakayokupa kisha nikufanyie mpango urudi duniani?”“Ndio mama nipo tayari hata sasa hivi”“Unatakiwa ulale na maiti ishirini huku kila moja ukiivua na kuichezea viungo vyake vya siri ikiwa ni pamoja na kuzinyonya, kuzilamba masikioni na midomoni kama wafanyavyo wapenzi wanaopendana huko duniani, sawa?”“Hapana, hilo siwezi, siwezi nibadilishie adhabu”“Mwanangu Adela hiyo siyo adhabu hiyo ni njia ya wewe kurudi katika mazingira ya kawaida ili usiwe mfu tena. Adela umenielewa mwanangu?”***************************************“Hapana mama bado sijakuelewa kabisa!” “Sasa muda wa kubembeleza umeshapita, cha kufanya wewe subiri muda ukifika utaona kitakachokutokea na kama maagizo tayari nimeshakupatia, tumeelewana Adela?” ******

      * Milio ya sauti za ndege wa porini kama bundi ndio ilihamsha zaidi hisia za mwili wangu kupitia masikioni. Woga wa ajabu uliendelea kunitanda katika halmashauri ya kichwa changu. Macho yangu yalizidi kustaajabu mazingira niliopo. Hakukuwa hata na mtu aliyeniongelesha zaidi ya kila mmoja kunitazama nakisha kuendelea na shughuli zake. Ninaweza kusema kuwa wengine hawakuwa hata na sehemu za siri japokuwa kila mmoja alikuwa akipita uchi. Yale maneno ambayo nilikuwa nikiyasikia kwa watu kuwa kuna uchawi. Kuwa wachawi huwa wana sheria zao na tamaduni zao kamwe nilikuwa siyaamini lakini leo hii nayatazama kwa macho yangu mwenyewe tena nikiwa kama mchawi mchanga. Mchanga kwa kutofundishwa bado uchawi haswaa! Niliye katika mazoezi ya kulazimishwa kuujua na kuufanya uchawi kama sehemu ya maisha yangu. Hatua mbili tatu nilijikuta nikiinuka nakuanza kuzunguka zunguka mwenyewe. Nikajiwekea ujasiri wa kiume katika mwili wangu. Ujasiri wa kupambana na chochote mbele yangu kwa kutumia nguvu zangu. Baada ya hatua chache huku nikitembea nikasikia minong’ono ikitokea upande wa pembeni yangu. Haraka haraka nikageuza macho yangu lakini sikushuhudia kitu chochote. Nikatoa sonyo kali lakini nikastaajabu masonyo zaidi ya kumi yakinirudia katika masikio yangu. “Alaaaah!!” Nikastaajabu!. Nikiwa bado katika hali ya kustaajabu mazingira na sauti zilipotokea mara macho yangu yakakutana tena na rundo la wasichana wadogo wadogo wakiwa wamezunguka huku wakionekana kwa mbali kama wakicheza ngoma. Taaratibu niliwasogelea mpaka katika eneo lile nami nikajiweka mstari mmoja nao kwa shauku ya kutaka kujua kitu gani walichokizunguka wakicheza. “ooohhhhh!! Ohhh!!” Mapigo yangu ya moyo yalianza kunibadilika kwa kile nilichokuwa nikikishuhudia mbele yangu. Walikuwa ni wazee wawili wakiwa uchi wa mnyama wakiuchezea mwili wa mtoto mdogo alioonekana kama ni maiti huku wakiing’ata ng’ata na kisha kutafuna nyama zake na kuzitapika papo hapo na midomoni mwao wakibakiwa na damu damu. Woga ulinizidia, ule ujasiri wa kiume niliojijaza kwa muda mfupi ulinitoka ghafla na kuingiwa na huruma ya kike. Huruma kama ya mwanamke aliyetoka kujifungua.Nikatamani sana kuingilia kati kwenda kuwazuia lakini nikaogopa huenda ningefanyiwa kitu kibaya kwa kuharibu mila zao hivyo nikabaki nikiwaangalia huku machozi ya uchungu yakiendelea kunidondoka kwa huruma. Niliendelea kupatwa na hasira kali haswa kwa jinsi mabinti walivyokuwa wakifurahia kwa kupiga makofi. “Adela? Adela njoo hapa kati?” Mmoja kati ya wale wazee aliniita jina langu la Adela. Sikutaka kuamini kama anayeitwa ni Adela mimi. Niliyageuza macho yangu kuwaangalia wale mabinti huenda mmojawapo anaitwa Adela.

       Cha kustaajabu kila mmoja alikuwa akinitolea macho mimi kana kwamba anayeitwa ni mimi. Nilijihisi mwili kunitetemeka sambamba na mkojo kunichuruzika huku nikirudi nyuma nyuma nikihema juju. Kwakuwa nilikuwa eneo kama hewani sikuweza kujua wapi pa kutokea na wapi pa kuingilia hivyo nilibaki nikirudi nyuma nyuma nisijue naelekea wapi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Sitaki niacheni jamani, niacheniii?” Nilijitahidi kutoa sauti lakini haikusaidia kuwanyamazisha wale wazee kwani ndio kwanza waliendelea kunisogelea kwa ukaribu huku lile rundo la mabinti wakiwasindikiza kwa nyuma yao. Hatua chache nyuma nilishangaa kama nimejikwaa, kwani nilijikuta nikidondoika mpaka chini nakulala kifudifudi kisha viungo vya binadamu vilidondoka kwa kunizunguka. Vipande vipande kuanzia mikono, miguu na viungo vya sehemu za siri za wanaume ambazo vilikuwa vikitoa harufu kali sana. Haraka haraka nilivuta kiungo kimojawapo na kutaka kuwarushia wale wazee waliokuwa wakinifuata mbele yangu. “Weee!! Wee!! Weeee!! Thubuutuuu!!? Mpumbavu kabisa wewe!. Unajua thamani yake hivyo vitu ulivyovishika?” Nilibaki nimeyakodoa macho yangu kwa kustaajabu maneno ya mzee aliokuwa akiniongelesha. Nilijihisi kutetemeka zaidi mwili wangu. Wale wazee wakainama hadi chini nilipokuwepo na kisha wakaanza kuniingiza vidole katika sehemu zangu za siri huku yule mzee mmoja akininyonya papi zangu huku akinimwagia damu nyingi ndani ya mdomo wangu. Damu damu ambazo bado zilikuwa zimebaki kwenye mdomo wa yule mzee zote kwa kula nyama za yule mtoto zote zikahamia mdomoni kwangu. Aliufanya mdomo wangu atakavyo huku mzee mwingine na yeye akichezea sehemu zangu za siri sambamba na maziwa yangu atakavyo. Niliumia sana moyo wangu. Nilipingana na akili yangu chafu iliyoshinikizwa na nguvu za kichawi kuingia kaburi la mama yangu mpaka kufika huku. nilibaki nalia kwa vikwifukwifu. “Jamila?” Yule mzee aliokuwa akinichezea sehemu zangu za siri aliita kwa sauti ya juu huku akiwaangalia wale mabinti. Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakugundua kuwa kumbe mmojawapo kati ya wale mabinti anaitwa jamila. Punde huyo jamila alijitokeza. ”Abee baba!” “Nenda kule kwa mama yako kanitafutie lile panga langu” Niliposkia tu panga nikajihisi mapigo ya moyo kukosa ushirikiano. Nikajua hata kama mfu nauliwa tena sasa sijui ndio nitakuwa mfu wa kweli ama mfu wa pili baada ya kufa mara mbili. Mwili wangu ukawa hauwezi kunyanyuka wala kufurukuta zaidi ya kuukabidhi kwa wale wazee waufanye watakavyo. Wakiwa bado wanamsubiri |Jamila.Yule mzee aliokuwa akininyonya mdomo wangu akaendelea tena kuniyonya mpaka mdomo wake ukabadilika rangi nakuwa nyekundu si nyekundu na hata bluu si bluu. “Hili hapa baba!” Sauti ya Jamila nikaisikia kwa mbali kama ikikabdihi hilo panga aliokuwa ametumwa. Macho yangu yakawa hodari kwa kuangalia ni panga kweli au la!. “Mhh!! ama kweli?” Nilibaki nausemea moyo baada ya kuona mfupa mkubwa sana ukiwa umekaa mithili ya panga Jamila akimkabidhi baba yake. “Adela?” “Abee baba!”

       “Unawaona wenzako wote hao waliokuzunguka hapa?” “Ndio nawaona” “Embu jaribu kuwaangalia vifuani mwao?” Nilianza kuyatoa macho yangu kwa kuaangaza wale mabinti waliokuwa wamenizunguka. Japokuwa walikuwa uchi wa mnyama. Niliweza kugundua kuwa hawakuwa na maziwa vifuani mwao. “Nimewaona tayari” “Umegundua tofauti yao na yako ipi?” “Hapana baba sijagundua chochote” Ilinibidi kuwaongopea kwa makusudi ili niepukane na kukatwa kwani nilijua wazi wanataka kunitoa maziwa yangu nifanane na hawa mabinti.Yule mzee alichukuwa lile panga na kuanza kunikata nalo ziwa moja baada ya jingine. Sikuwa na nguvu ya aina yeyote tena na wala sikusikia maumivu zaidi ya kuhisi kama natekenywa. Ni dhahiri kuwa lile panga lilikuwa na dawa zao za kuweza kumpumbaza mtu anapokatwa asisikie maumivu yeyote. Alipomaliza kunitoa maziwa yangu yote mawili akawarushia wale mabinti wakaanza kugombania kwa kuyala bila kujali limbi la damu zake. Nilitamani sana kutoa sauti kwa ukali ya kuwatukana lakini nilishindwa. Tayari nilikuwa kama nimefanyiwa dawa za kutokutoa sauti kwa kipindi. Nilibaki kuwa kama mtu aliyefungwa mdomo kwa kutokuwa na uwezo wa kutoa sauti. ”Adela, sasa umekamilika mwanetu, inuka?” Nilidhani utani kuwa nisingeweza kuinuka. Nilishangaa nguvu za ajabu zikinirudia na kuweza kuinuka kutoka pale chini. Maswali mengi yalibaki kichwani mwangu ikiwa ni pamoja na kuyatoa maziwa yangu, pili sijaona damu zozote wala maumivu ya aina yeyote na tatu nilishangaa kuishiwa nguvu zote na baada ya kukatwa nilipata nguvu ya kuinuka. “Sasa waweza kwenda pale ukakutane na kiongozi wako uanze kazi leo leo,sawa Adela?” “Sawa baba!” Niliondoka kiunyonge huku nikijihisi kama aibu kubwa imenitawala Adela mimi. Kwa mwendo wa taratibu huku nisielewe mazingira ya chini yapoje poje kwani hayakuwa na vumbi wala ardhi yaani yalikuwa ni kama angani tu. Ndani ya muda mchache nikawa tayari nimeshafika kama nilivyoelekezwa na wale wazee walionitoa maziwa yangu na kuwapa wale mabinti wagawane kwa kuyatafuna. “Adela mwanangu umekuja?” Aliongea yule mama wa kwanza kabisa. yule alioniambia kuwa ni kiongozi wao na atanipangia kazi ya kulala na maiti ishirini. “Ndio mama” “Umependeza mwanangu! Hivyo ndivyo mabinti wakike wanavyoishi huku kwetu. Si umeniona hata mimi sima maziwa? Yaani huku hayana kazi maana kama mimba hatupati, watoto wanaliwa na wazee na hawaruhusiwi kuishi sasa miziwa niwe nayo inafanya kazi gani?” ****************************

      Nilijiangalia mara mbili mbili kifuani mwangu kwa hasira ya hali ya juu. Yale maziwa madogo dogo na ya kumvutia kila mwanaume sasa yakawa hayapo tena katika kifua changu. Yametolewa na wale wazee wachawi wenzangu. Niliumia sana lakini kwa kuwa tayari nilishakubaliana na nguvu ya kiuchawi ilinibidi yatolewe. “Adela?” “Abee mama!” “Kuanzia sasa usiniite mama, mimi siyo mama yako sawa? Mbona mimi sikuiti mwanangu nakuita Adela? Nataka uniite Sophia ama sophy, tumeelewana Adela?” “Ndio maama nimekuelewa” “Haya sogea karibu yangu hapa nilipo kisha nikumbatie kwa nguvu” Aliongea yule Sophy kwa sauti ya ukali akinisisitizia kwa mkazo. Nilitahamaki maneno yake ya ukali lakini nilijikuta naingiwa na moyo wa subira. Moyo wa kuvumilia yote nionayo na nisikiayo. Mwili wangu bado ulikuwa haujakamilika kabisa kwa uchawi kwani nilianza kuhisi woga woga ukininyemelea kila muda niliokuwa nikiongea na Sophy. Hata aliponisihi nimsogelee na kumkumbatia bado nilikuwa nikimuogopa. “Hivi unanisikia Adela ninachokuambia? Au unataka nikurudishe kule kwa wazee ulipokuwepo wakakuchezee tena mwili wako?” “Hapana mama, anhh nisamehe!!. Hapana Sophy!” Kwa uoga uliochanganyikana na aibu kwa mbali ilinibidi nimsogelee na kisha nichukue mikono yangu na kupitisha mabegani mwake kwa lengo la kumkumbatia kama alivyohitaji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-*******Baridi kali lilikuwa likiendelea kuusumbua mwili wangu. Kiza kinene kiliyashinda macho yangu angavu.Macho yenye nguvu ya kuangaza popote sasa yakawa hafifu. Hafifu kwa kutoweza kuona vizuri mbele wala nyuma.Nikajikuta nikiwa juu ya mti mkubwa sana. Mti aina ya mbuyu uliopukutika majani yake na kuwa mkavu. Nafsi yangu iliuliza moyo lakini akili ilibaki kutokujua na kukataa kuujibu moyo juu ya kinachoendelea.Sauti za ndege aina ya popo na bundi ndizo zilienea zaidi. Mwili wangu haukuwa mwili wa kawaida tena kutokana na kujikuta nimezungushiwa shanga na hirizi karibu mwili mzima na mikononi nikiwa nimefungwa vitambaa vyekundu.Pembeni yangu alikuwepo Sophy akiwa amebebelea ungo mkubwa uliokuwa umejaa vibuyu,vidole vya watoto,masikio ya watu wazima pamoja na mikia. Sikuelewa vizuri ilikuwa ni mikia ya mnyama gani kutokana na mikia kuwa mirefu sana. Sophy alionesha kufurahi jambo huku akinitazama usoni mwangu. “Adela sasa kazi yetu inaanza rasmi sasa hivi. 

      Na hapa nilipo nipo kwa ajili ya kukuonesha tu utakavyokuwa unafanya na siku nyingine utakuwa unakuja peke yako mpaka utakapomaliza zoezi la kulala na maiti zote ishirini, umenielewa Adela?”“Nimekuelewa Sophy”Nilijibu kwa kujiamini kana kwamba tayari ni mchawi aliyekamilika.Baada ya hapo Sophy akachukuwa Mikia miwili na mmoja wapo akanikabidhi kisha akaniamuru ule mkia niwe nauchovya kwenye kibuyu kuna nguvu zetu za kutulinda tusionekane na wala tusikamatwe na mtu yeyote na hata tukikutana na mchawi ambaye hayupo katika himaya yetu asiweze kutudhuru. Nilifanya hivyo pamoja na Sophy naye alikuwa akifanya hivyo hivyo huku tukishuka kwa kuteleza chini ya mbuyu taratibu, na tulipofika chini kabisa nilishangaa kukutana na makaburi mengi yakiwa yamejipanga.“Adela?”“Abee Sophy?”“Haya ni makaburi ya Mwananyamala, na kwa kuanza chukua hiki kibuyu kitakuwa kinakuongoza. Unapita mstari huu wa makaburi uku ukiyapandia juu yake mpaka kule mwisho na ukijiona mzito unashindwa kwenda mbele ujue hilo ni kaburi la mwanaume ambaye amezikwa leo leo. Haya tuanze mimi nipo nyuma yako taratibu”Nilijikuta nauvaa moyo wa kijasiri na wakiuchawi. Woga uliniyeyuka ghafla na kuvaa ngozi ya kichawi tena yule mchawi aliyekubuhu kwa uchawi. Nilianza kupiga hatua huku nikifuata mstari wa makaburi kwa kuyakanyaga juu yake. Nilifanya hivyo kwa zaidi ya makaburi sita lakini nilipolikaribia kaburi la saba nilishangaa mwili wangu kama kutetemeshwa. Ganzi! Ndio ganzi mithili ya shoti ya umeme ilikuwa imeninyuka katika miguu yangu vilivyo. Nilitetemeka nakutaka kuanguka mpaka chini.“Adela? Nini tena unafanya? ““Sophy nashindwa kutembea, nashindwa nivute?”“Hivi unajua kuwa ilo sio kaburi unalotakiwa kulichimba leo. Na kaburi hilo uliokanyaga ni la zamani sana. Na ukionea miguu inatetemeshwa ujue hilo kaburi litakuwa la mchungaji ama kiongozi wa kanisa au msikiti. Na mara nyingi huwa inatutokea tukiwa katika mawindo yetu haya. Sasa si unaona na maua kabisa yanaonekana yamewekwa leo. Watakuwa walikuja kulisafisha na kuliombea mchana au asubuhi”“Ndio”“Lazima utakuta waliweka maji yao ya Baraka sambamba na kuliombea lakini usijali Adela, dawa zetu zina nguvu zaidi yao twende.”Nilishangaa nakuwa mwepesi kwa mara nyingine

      .Sophy alinivuta mkono wangu sambamba nakunipokonya kile kibuyu nilichokuwa nacho nakubakiwa na mkia pekee. Niliongozana naye kwa zaidi ya makaburi kumi na moja akasimama.“Adela umepaona hapa?”“Ndio”“Hapa kibuyu kimekataa kusogea na hata mkia pamoja na shanga zangu za kiunoni nilizokuwa nazo zinacheza cheza sana. Na wewe umehisi hilo?”“Mimi zinaniwasha sana na mkia nilioushika unajitingisha wenyewe”“Basi hapa ndipo penyewe.Kama ukiona kibuyu kinacheza peke yake ujue hilo ni kaburi la mwanamke achana nalo. Lakini kama utaona kibuyu paoja na mkia na hizo shanga ulizonazo zote zinacheza cheza ujue hilo ni la kiume na hata si unaona kaburi lilivyo jepesi pamoja na mchanga wake uliofukiwa inaonyesha dhahiri kuna maiti ya kiume tena imefukiwa leo leo. Haya unatakiwa uweke kibuyu hapo pembeni ya msalaba wao hili nguvu yetu ya kichawi iweze kushinda na baada ya hapo utatumia mikono yako kuchimba hili kaburi”Ule woga wote niliokuwa nao ulishafutika toka nimekatwa maziwa yangu nakuwa mchawi kamili. Roho ngumu na ya kichawi ndio ilionitawala katika halmashauri ya kichwa changu. Kwa haraka zaidi nilifanya kama nilivyoelekezwa na Sophy. Nilichimba kaburi kwa kutumia mikono yangu. Nilishangaa nguvu za ajabu nilizokuwa nazo za kuweza kulifukuwa kaburi refu kwa muda mchache nilijikuta nimeshafika umbali mrefu sana. Niligeuza macho yangu kuangalia juu nilipotoka lakini sikuweza kumuona Sophy japokuwa kulikuwa na mwanga wetu wakichawi uliosaidiana na mbalamwezi. Nikaendelea na kilichonileta hapa kaburini.Baada ya kuendelea kuchimba kwa muda kidogo nilikutana na mbao mbao. Akili yangu ikajibizana na mdomo nakutambua kuwa ilikuwa ni jeneza. Nilishika mbao zake kwa nguvu zote nakuanza kulifungua. Nilifanikiwa kulifungua japokuwa nilikutana na harufu kali sana. Mara nyingi harufu za kichawi hufanana sana na zile pafyumu za kupulizia maiti hivyo hazikuniathiri pua zangu ama mimi mwenyewe. “Umependeza!!”Nilijikuta natoa mdomo wangu nakuusemea moyo huku nikiangalia ile maiti kwa jinsi ilivyokuwa imevalishwa suti nzuri na ya kuvutia. Nikalitoa bao lote lililokuwa limefunikiwa kwa juu. Nikaanza kumvua nguo zake taaratibu kuanzia tai, koti la suti na kisha nikamalizia suruali yake mpaka akabakiwa uchi kabisa. Mwili wake ulikuwa umesinyaa sana nadhani ilitokana na kukaa mochwari kwa muda mrefu ama alikuwa akiugua sana hilo sikulijali Adela mimi zaidi ya kuendelea kumvua nguo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“ Mlambe lambe kuanzia kifuani, mdomoni, na kisha umnyonye sehemu zake za siri. Ukimaliza ufanye naye mapenzi kwa kumlala juu yake kama wafanyavyo wapenda nao huko duniani!

      ”Sauti mbili mbili zilizochanganyikana na sauti ya Sophy zilikuwa zikitikisa ngome ya masikio yangu.Nikataharuki! nikaanza kuzubaa sasa. Kadri nilivyokuwa nikizubaa kwa kuzisikiliza sauti zile zilipotokea ndipo nazo zilikuwa zinaongezeka na kurudia maneno yale yale. Kwa takribani dakika tano nzima zile sauti ziliongezeka mara kumi ya pale kwani niihisi watu wengi sana wananiambia maneno yale. Mwili wangu ulishtuka kama vile ulipigwa na radi.Nilijikuta ghafla nikisisimka sambamba na furaha. Nikaanza taratibu kulamba usoni ile maiti na mikono yangu nikiitumia kumtoa pamba zake puani na masikioni mwake. Niliendelea kumnyonya mdomoni mwake huku ulimi wangu nikiutelezesha mpaka kifuani mwake.Nikiwa bado katika hali ya kumnyonya ghafla nikashangaa ile maiti kushtuka. Nikataharuki! nikainuka nakuiangalia, nikashangaa jicho moja la maiti hii likifumbua nakunitazama. Nikabaki nimetulia kama mtu aliyegongewa misumari katika mbao.“Sophhhhhyyyyy??”Uzalendo ulinishinda kabisa nikabaki nikitoa sauti ya ukali na ya juu kabisa kumuita Sophy. Sophy yule niliekuja naye huenda nilikosea masharti au nguvu za kichawi zimeniishia. Lakini sikuambulia msaada wowote zaidi ya ile sauti nilioitoa kumuita Sophy ikinirudia mwenyewe mithili ya mwangi wa sauti katika mapango marefu na yenye giza.*************************** Unavyodhani Adela atanusurika hapo na hiyo maiti? Vipi kuhusu Sophy?, atakuwa wapi au amerudi kule kwa wachawi wenzake akamuacha Adela? Nini hatma ya maisha ya Adela?

      ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog