Search This Blog

PETE YA MVUVI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : LEICESTER PETRON



    *********************************************************************************



    Simulizi : Pete Ya Mvuvi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kawaida kwenye maisha tunakumbushwa kupenda kujituma kwa bidii zetu zote pale tufanyapo kazi zetu, Lakini pia tunahamasishwa kupenda kazi tunazozifanya, haijarishi ziwe ni za kipato cha chini au juu bila kujali ni kazi ya kuketi ofisini ukiwa umezungukwa na vitendea kazi vya kisasa kama Kompyuta, (Printer) kifaa cha kutolea kazi iliyoomo kwenye kompyuta na kuifanya ionekane kwenye karatasi n.k, Pia usijali kama kazi yako ni yakuzunguka mtaa kwa mtaa ukitembeza bidhaa zako au kazi ya kibandani kama kuuza genge, saluni, mgahawa n.k, Ndugu zangu wapendwa zote hizi ni kazi na inabidi tuzipende kwa moyo mmoja, Usidharau kazi yako kwani hata wateja wako na jamii yako kiujumla watakudharau. Kwa maisha ya hapa nchini kwetu Tanzania sidhani kama kuna mtu mwenye uelewa wa jinsi gani maisha yanavyoenda atakayeweza kuchagua au kubagua kazi fualni, Japokua kumekua na tabia ya kuchagua au kubagua kazi, Tabia hii imewaadhiri vijana wengi hususani vijana wa mijini kwa kuwa na msemo unaotamkwa na wengi wao ukisema, “Aaaaah!!!! Bwana eeeeh!!! Kijana mtanashati kama mimi (Au binti mrembo kama mimi) Kazi hii ni ya kike (Au kazi hii ni ya kiume) hivyo siwezi kufanya mimi yani bora nilale njaa, Jamii yangu nitaiyonea aibu au nitachekwa” Msemo huu umekua maarufu sana hususani maeneo ya mijini kwani vijana wengi wamekua ni Mabrazameni na Masistaduu hivyo kazi za kutembeza bidhaa au kazi za vibandani hawawezi kufanya kwani watajishusha thamani na pia wanaamini jamii yao itawacheka, Kazi wazipendazo wao ni zile za kuvaa Suti kali na tai huku mkononi wakiwa na funguo za magari mazuri tena ya kifahari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kwa uwelewa wa kawaida vijana kama hao ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya taifa letu kwani endapo wangejitolea kufanya kazi kwa wingi na kwa nguvu zao zote nina imani Tanzania yetu ingesonga mbele kwa kasi zaidi, ila badala yake utakuta vijana hao kwa upande wa mabinti utawakuta wapo teyari kuuza miili yao ili wapate pesa nyingi bila kufanya kazi yoyote ya msingi, huku upande wa wanaume wengi wao hujiiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kukosa kazi za kuwafanya wafikiri vitu vya maendeleo na badala yake wanaanza kuwa vibaka ili wapate pesa ya kwenda kununua Kete (Unga) au Ganja (Bangi). Hali hii inasikitisha sana kwani huwa tunapoteza vijana wengi kwenye umri ambao tunaamini wangeweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. Mnamo mwaka 1995, Katika kijiji cha “Luvile” yakiwa ni majira ya asubuhi sana nikiwa nimeketi na babu yangu nje ya nyumba yetu nzuriii!! ya udongo, Babu alinisimulia hadithi nzuri sana ambayo ilinifanya nipende kazi yake ya uvuvi kwani babu yangu alipenda sana kazi yake na hivyo alinisihi nijisikie wa bahati sana kujifunza kazi ile ya uvuvi kwani babu yangu alikua mvuvi mkongwe sana kwenye ziwa lilipo kijijini kwetu, kwa kuwa nilikua na umri mdogo (Miaka 15) Babu hakuwahi kunielezea historia ya wazazi wangu kwani sikuwahi kuwajua Baba na Mama yangu japo hata kwa sura na kila nilipokua nikimuuliza Babu hakuwa teyari kuniambia ila alichokua ananiambia ni, “Joshua mjukuu wangu wazazi wako walikua watu wema sana na walikupenda sana ila ni mipango ya Mungu walikuacha ukiwa mdogo sana, naomba uwaombee wapumzike mahali pema peponi”, Kauli ile ilikua ikinifanya niwe mwenye mawazo sana kwani nilitamani japo nikaone makaburi yao ila babu hakuwahi kuniambia walizikwa wapi wala sababu ya kifo chao. Nilijijengea tabia ya kabla ya kulala na kila niamkapo lazima nipige magoti mbele ya kitanda changu na kuwaombea marehemu Baba na Mama yangu. Siku moja, Ikiwa ni mida ya jioni saa 12 Babu alinituma niende ziwani nikaangalie kama rafiki zake walishaandaa nyavu za kwenda kuvulia samaki, Niliondoka huku nikikimbia na nikiimba nyimbo zangu za kuwinda ndege, kwakua muda ulikua umeshakwenda na ziwa lile lipo mbali na makazi ya watu niliongeza mbio. Nikiwa njiani niliona mfuko mweusi ukiwa umetupwa kati kati ya njia ile niliyokua nikipita, nilisimama na kuutizama mfuko ule kwani niliona kuna kitu kinacheza cheza ndani yake, nilivuta pumzi na kisha niliufata mfuko na nilijaribu kuufungua……… Loooooooh!!!!! Mungu wangu!!! Sikuamini macho yangu kwani niliona katoto kachanga kakiwa kamefumba macho yake na kwa haraka nilimtoa ndani ya mfuko ule na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Nilipokua njiani kachanga kale kalianza kulia na nilisimama na kutoa shati nililokua nimevaa na kumfunika kwani nilihisi mtoto yule anapigwa na upepo ndio maaana alikua analia, wakati namfunika mvua kubwa sanaa! Ilianza kupiga huku radi nazo zikigangamaa…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliogopa sana na nilimuonea huruma mtoto yule aliyekua hana kosa lolote la kumfanya apitie shida zote zile lakini kwa roho ya kijasili niliendelea kuongeza mbio na hatimaye nilifanikiwa kufika nyumbani huku nikiwa nimembeba mtoto yule na mwili wangu ukiwa umeloa chapa chapa!!!!. Nilipoingia ndani ya nyumba nilimkuta babu akiwa anakoka moto kwajili ya chakula cha jioni ambacho huwa alikua anapika kwanza ndio aelekee ziwani kuvua samaki, Babu alinishangaa sana kwani aliona nimebeba kitu kinachovuja damu ndipo babu aliinuka alipokua ameketi na kwa kuogopa aliniuliza, “Joshua mjukuu wangu umeiba wapi hako kachanga ka mbuzi?” Babu hakujua kuwa yule ni binadamu na sio kachanga ka mbuzi, Babu alinisogelea na alipofunua shati langu nililomfunika mtoto yule, Sauti nzuri ya furaha ilitoka ikilia, Ngaaa!! Ngaaa!!! Ngaaa!!! Ngaaa!!! Mtoto yule alitoa kilio kile ambacho kilimfanya babu anipokonye na kumsogeza karibu na moto. Kwakua sikua na uelewa wowpte juu ya kitendo kile nilimwambia babu, “Babuuuu!!!! Usimuue huyo ni malaika wa Mungu usimchome moto” Babu alinijibu, “Joshua huyu mtoto anahitaji joto hivyo namuweka karibu na huu moto apate joto kwani mwili wake una baridi, tena nahisi atakua na homa” Babu aliniomba nielekee nyuma ya nyumba yetu nikamchumie dawa iliyokua ni majani ya Roswa yaliokua yakipatikana kwa nadra sana, nilitoka nje na kumletea dawa ile ambayo aliitwanga kwenye kinu na kisha kuchuja maji yake na kumnywesha mtoto yule huku majani yake akimpakaa mwilini mwake. Babu yangu siku zote alipenda kuamini sana dawa za asili kwani hakuwahi kutumia hata Panadol, Na mtoto yule kupitia dawa zile za asili alianza kuendelea vizuri. Ilipokua asubuhi sana baada ya muda wa miezi 6 kupita babu aliniamsha na kuniambia, “Mjukuu wangu mimi natoka naelekea ziwani kutafuta riziki hivyo nakuomba ubaki na mdogo wako Neema na uhakikishe unanywesha uji na anashiba , Usimuache peke yake kitandani ataanguka na kuumia vibaya, Sawa babu?” Nilimjibu, “Sawa babu usijali pia naomba Mungu akuongoze uende salama na urudi salama” Babu alifurahi sana na ndipo aliondoka kuelekea ziwani. Nilimpenda sana mdogo wangu (Neema) kwani nilihakikisha tangu nilipomuokota mpaka asubuhi ile aendelee kuishi vizuri na pale atakapokua mtu mzima nilipanga kumueleza ukweli wa kila kitu. Majirani zetu hawakujua Neema ni mtoto wa nani wala kafika vipi pale kijijini na kila nilipokua naulizwa niliwajibu, “Neema ni mtoto wa Shangazi yangu yupo mjini kapatwa na tatizo kidogo hivyo kaniomba mimi na babu yangu tumsaidie kulea”. Kawaida ya Babu kurudi nyumbani ilizoeleka kuwa ni saa 10 jioni ila alipokua akichelewa sana pale alipokua akipitia kilabuni kupata chupa mbili tatu za kilevi alikua akifika nyumbani saa 12, Ila leo tangu alipoondoka asubuhi ile na mapema ikiwa ni saa 2 usiku hakuwa amerudi nyumbani, Niliogopa sana kwani muda ule upepo mkali na mvua kubwa Sanaa!! Ilianza kunyesha huku Neema akiwa analia njaa kwani tangu nimpe uji wa asubuhi nilikosa cha kupika kwani nilikuwa nikimsubiri babu arudi na unga nimpikie uji mdogo wangu. Hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya ila nilijaribu kumbembeleza Neema alale na alipolala nilitoka na kuelekea kwa jirani yetu wa karibu Mzee Magori ili nimuombe baiskeli yake nielekee ziwani kumuangalia babu yangu kwani nilihisi kuna kitu kibaya kimemtokea…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog