Search This Blog

THE NIGHTMARE - 4

 







    Simulizi : The Nightmare

    Sehemu Ya Nne (4)





    Maongezi yao yaliishia kwa furaha upande wao. Hasa kwa Karimu ambaye alikua ana hamu kubwa ya kumuona kutokana na sifa alizotajiwa.



    Kiza kilipoanza kuingia, watu wapatao kumi waliingia mule ndani. Walijigawa wasichana watano na wavulana watano. Walibeba mabegi yao kuashiria kuwa safari imeiva.

    Walipokelewa vizuri na wenyeji wao Karimu na mdogo wake Sharji.

    Vitu vilivyokua ndani vililetwa mbele. Makreti ya bia na pombe kali yalisogezwa tayari kwa part ndogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dakika kumi baadae lilikuja gari likiwa na wafanyakazi wanne walioshuka na majiko ya kuchomea nyama.

    Mziki mkubwa ulifunguliwa na watu wakaanza kuselebuka pale kati huku wakijisevia vinywaji na nyama choma za kila aina zilizokuwa zikichomwa bila idadi.



    Ilipotimia saa tano usiku. Sharji uzalendo ulimshinda kutokana na kutozoea makelele. Aliaga na kwenda chumbani kwake kulala.



    Mawazo juu ya safari aliyokua anaisubiri kwa hamu yalimfanya kukosa usingizi kwa muda mrefu. Baada ya masaa kadhaa, usingizi mzito ukamchukua na kushtushwa na Alarm yake iliyokua ikilia kwa nguvu. Aliamka na kuchungulia nje. Aliona jua la asubuhi likipanda taratibu.

    Aliamka na kuchukua mswaki na kuelekea bafuni. Baada ya kuoga, akaliendea kabati na kutoa nguo alizopanga kuvaa siku ile.



    Alisogea sebuleni na kuwakuta wale wasafiri wenzake wakiwa wanapata kifungua kinywa huku wakipiga stori zao huku wakicheka kila dakika.



    Aliungana nao na kunywa chai, baada ya hapo waliamua kutoka nje tayari kwa safari.

    “umeshapata?”

    Aliuliza mmoja kati ya wale wasafiri baada ya kumuona Karimu akirudi na gari lake.

    “anakuja nayo muda sio mrefu.” Alijibu Karimu.



    Dakika tano baadae, iliingia coster moja matata na wote wakatabasamu baada ya kuiona.

    “mpigie Balqis ili tujue kama anaenda au alikua anazingua.” Aliongea Karimu baada ya kuona kila kitu kipo tayari kwa ajili ya safari.

    “poa.”

    Alijibu Sharji na kuchukua simu yake na kuanza kuitafuta namba ya Balqis. Kabla hajabonyeza kitufe cha kupigia, inaingia marcides benz matata yenye rangi ya silver.



    Watu wote wakatoa macho baada ya kumuona mwanadada mrembo wa kiarabu mwenye nywele zilizowekwa brich na kuwa kama za kizungu akishuka kwenye ile benzi kwa madaha.. Alivaa gauni refu jekundu lenye mpasuo hadi kwenye mapaja yake.



    Karimu alipagawa kupita wote na kubaki ameachama kwa jinsi yule dada alivyokuwa mzuri. Mwendo wa kimiss ndio uliowafanya watu wote kuzihesabu hatua zake mpaka alipowafikia. Balqis aliwasalimia wote kwa kuwashika mikono. Alipofika kwa Karimu, alitumia dakika nzima kusimama kwakua tu karimu aliganda na mkono wake bila kumuachia. Alijitahidi kuutoa mkono wake na kuendelea kuwasalimia wengine kwa style hiyo hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipofika kwa Sharji, aliachia tabasamu na kumkumbatia. Harufu nzuri ya marashi aliyojipulizia Balqis ilipenya vizuri kwenye pua za Sharji.



    “tunaweza kuondoka sasa.” Aliongea Karimu na wote wakaingia kwenye ile coster.



    Siti aliyokaa Sharji ndio siti aliyokaa Balqis. Muda wote Balqis alikua anatabasamu na kujisika raha kukaa karibu na Sharji ambaye kimtazamo ni mdogo kwake. Na hata kama wakiwa wanatoka kimapenzi basi jamii ingemshangaa.



    Walifika feri ambapo bati yao ya kukodi ilikua inawasubiria.

    Waliingia kwenye ile boti kubwa iliyokuwa na floor moja. Ilikua na vyumba vya kulala sita na ukumbi mkubwa uliokuwa na viti juu kabisa ya boti ile.



    Ukubwa wa boti ile ulifanana na meli ndogo lakini yenyewe ilitengenezwa kwa ajili ya safari za kifamilia au kampuni.

    Kila chumba waliamua walale watatu watatu na na kikapatikana chumba kimoja ambacho kwa heshima na hadhi ya Balqis basi walimpa alale peke yake.



    Nahodha waliyepewa alianza kukiondoa chombo taratibu na kuanza safari yao.



    Masaa matatu baadae, tayari walikua wameshafika mbali sana na hakuna aliyekua anapaona nchi kavu tena. Kwakua walienda na music systerm, basi hawakuwa na budi kuweka miziki kwa sauti kubwa na kuanza kucheza huku wakipata vinywaji waliivyopanda navyo.

    Wakati boti inaendelea kukata mawimbi, mara ghafla injini ikasimama.

    “vipi tena?”

    Yalikua maswali yanayojirudia kwa kila mmoja wao akimuuliza nahodha.

    “hata mimi sijui. Maana nimeangalia kila kitu kipo sawa. Sasa sijui kwa nini imezima.” Aliongea nahodha wa boti hiyo baada ya kuikagua boti yake.

    “sasa tutafanyaje?” aliuliza Karim.

    “nitafanya mawasiliano na kampuni yetu ili walete boti nyingine, hakuna jinsi.” Aliongea nahodha na hoja yake ikapitishwa na kila mtu.





    Taarifa hizo ziliwafanya waache kucheza mziki na wote wakatulia tulii kungoja hatua zinazo fuata.



    Sharji alijiona anamkosi kwa kua ilikua ni mara yake ya kwanza kupanda chombo cha majini na ndio matatizo yanatokea.



    Wakati wote toka wanaingia kwenye ile boti, Balqis alikua habanduki kwa Sharji. Hali iliyowafanya wanaume wengine kumuonea donge Sharji kukumbatiwa vile na mtoto mzuri kama yule.

    Karim ndio kabisa, alikua anaumia ndani kwa ndani kwakua alishaanza kumuhusudu. Pia aliamini kua mdogo wake hamuwezi yule dada kwakua alikua mkubwa kwake, basi ni njia pekee ya kumyang`anya mdogo wake na kuwa naye yeye.

    --CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Masaa matatu yanapita bila matokeo yoyote yanayoridhisha. Uvumilivu unamshinda Karimu na kumfanya amfuate nahodha aliyekua kwenye chumba chake akihangaika kutafuta mawasiliano.



    “mbona sielewi na hutupi information yoyote?” aliongea Karimu kwa hasira.

    “eneo hili halina network kabisa… nimejaribu kupiga wapi, hakuna kitu.”

    Aliongea yule nahodha na kumfanya karimu ashushe pumzi ndefu na kuangalia chini. Aliponyanyua kichwa chake, sura ilikua imeondoa makunyanzi ya hasira na kuwa ya upole.

    “sasa tutafanyaje?” aliuliza Karim kwa sauti ya upole.

    “hatuna jinsi, zaidi tusubiri meli zitakazopita ili itupe msaada wa kuturudisha nchi kavu.” Aliongea yule nahodha na kumfanya Karimu atoke nje.



    “jamani hakuna kinachoendelea hapa, tunachokisubiri ni meli au boti yoyote ipite ndio tuombe msaada wa kuturudisha nchi kavu.”



    Aliongea Karimu na wote wakawa hawana jinsi zaidi ya kukubaliana na matokeo.



    Masaa yalizidi kukatika hadi kufikia saa kumi jioni ambapo walikula chakula walichokibeba na kuamua kusubiri labda kuna meli yoyote itakayo pita mida hiyo.



    Mpaka kiza kinaingia hakuna chombo chochote kilichopita. Wakakaa macho mpaka ilipotimia saa tano usiku.



    “jamani twendeni tukalale tu.” Alishauri Karimu baada ya kuchoka kusubiria.



    “sasa tutaendaje kulala wakati meli nyingi huwa zinapita usiku?.. tuvumilieni japo ifike saa saba au saa nane ndio tufikie hayo maamuzi.” Alishauri Balqis

    “hata mimi naona tuvute muda kidogo.” Sharji alionyesha kuungana na Balqis.



    Wazo la Balqis lilipita kwa kukubaliana kuvuta muda angalau ifike saa nane. Upepo uliendelea kuvuma kwa kasi huku watu wengi wakiwa kwenye nyuso za uoga kutokana na mazingira ya baharini yanavyotisha usiku.



    Hatimaye saa nane usiku iliwakutia pale pale bila chombo chochote cha majini kupita. Hapo wakaamua kwenda kulala na kusubiri kesho yake.



    “unaonaje ukilala na mimi Sharji, mwenzio naogopa kulala peke yangu.” Aliongea Balqis kwa sauti ya chini iliyosikika na Sharji peke yake kwakua alikua nae karibu.

    Sharji alifikiria kwa muda bila kujibu kitu kisha akamuonyeshea Barqis ishara ya kukubali kwa kumuonyeshea dole gumba.



    Sharji aliingia kwenye chumba alichopangiwa kulala na kaka yake, lakini baada ya muda aliamka na kumuacha mtu aliyekua analala naye na kwenda kwenye chumba cha Balqis.



    Aligonga mlango na kufunguliwa . alipoingia ndani, alishangaa kukutana na harufu nzuri ya marashi aliyokuwa akiisikia toka jana yake kwenye gari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Macho yake yalipata taharuki baada ya kumuona Balqis kwenye night dress nyepesi iliyoonyesha kila kitu kilichomo ndani. Hisia kali za kutamani kufanya mapenzi zikaingia fasta kichwani mwake. Na hata alipokaribishwa kitandani, alipanda haraka na kuchojoa nguo zake zote na kubaki na Boxer.



    Kwa madaha na maringo ya ajabu, Balqis alianza kuivua ile night dress na kubaki na nguo ya ndani tu aina ya bikini huku maziwa yake yaliyosimama vizuri yakionekana dhahiri kwenye macho ya Sharji.



    Ilikua zaidi ya utamu wa kawaida aliokuwa akiusikia Sharji baada ya kupata vitu adimu vilivyomzidi umri kutoka kwa Balqis aliyeamua kumpa penzi dogo huyo usiku ule.



    Game kali iliishia kwa kila mmoja kuchoka na kulala kwa muda usiojulikana.



    “mtafuteni Sharji yupo wapi jamani, mbona hafungui mlango?” aliongea Karimu baada ya kugonga mlango sana katika chumba alichokua amempangia kulala mdogo wake na jamaa mmoja kati ya wale aliowaalika.



    “mgongeeni na Balqis basi aamke.” Aliongea Karim na kuonyesha hali ya kuchanganyikiwa kidogo.



    Mlango wa Balqis uligongwa mara kadhaa bila majibu. Na baadae kelele za mlango ziliwaamsha Sharji na Balqis kutoka kwenye usingizi mzito uliochangiwa na uchovu wa mechi kali waliocheza usiku wa kuamkia siku hiyo.



    “kha!!!!”



    Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis. Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.



    “sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia mdogo wake kulala.

    “sasa mwenzako mbona haamki?....tumegonga sana tu.” Aliuliza Karimu huku akiendelea kugonga mlango na kuendelea kumuita kwa jina lake.



    Wasi wasi juu ya usalama wa mwenzao ulianza kuwatanda. Maana walikaa kwa masaa matatu lakini hakukua na dalili za mlango kufunguliwa.



    “tufanye nini jaamani?” aliuliza Karim baada ya kukaa muda mrefu.

    “tuvuunjeni tu mlango.” Aliongea mmoja wa watu waliokuwepo kwenye ile boti.



    Walikubaliana hivyo na kuchukua shoka lililokuwa kwenye boti hiyo na kuanza kuvunja mlango.

    “MUNGU WANGU!!!!”



    Wote walishika vichwa vyao kwa mshangao mkuu baada ya kumuona mwenzao akiwa chini ya kitanda huku katapakaa damu mwili mzima. Wasichana walianza kulia kwa uoga baaba ya kushuhudia kifo cha kutisha kilichompata mwenzao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kifo cha utata kilichotokea kwa mwenzao ndani ya boti kilileta taswira nyingine kwa wasafiri wote. Walichunguza bila kupata majibu yanayoridhisha. Wote wakaamini kuwa yule mtu alikufa kwa ajili ya majini yaliokuwa baharini.



    Furaha yote ilitoweka na huzuni ikachukua nafasi yake. Wanawake ndio kabisa walikuwa wakikaa karibu na wanaume kwa kuwa walijawa na uoga.



    “sasa nahodha , tufanye nini. Maana akili yangu haipo sawa muda huu.” Aliongea karimu na kumuangalia nahodha ambaye naye hakuwa na msaada kwa wakati hou.

    “kama hakuna mawasiliano unafikiri kuna maajabu gani zaidi ya kusubiri meli ije itupe msaada?” aliongea Nahodha na kuwakatisha tamaa kabisa.



    Masaa yalizidi kusogea bila dalili zozote za kutokea kwa meli au boti kuonekana maeneo hayo.

    Kiza kiliingia tena na wote kwakua walichoka, walienda kulala baada ya kula chakula ambacho kiliishia usiku huo. Kila mtu kwa imani yake aliomba ili kama kuna jini basi asije tena kuwaua.



    Sasa haikuwa siri tena, Balqis na Sharji walienda kulala chumba kimoja kwakua Balqis alitangaza kuogopa kulala peke yake na kumchagua Sharji kama mlinzi wake. Hata wanawake wengine waligoma kulala peke yao na kulala na wanaume.



    Asubuhi ya siku ya tatu toka wasafiri ilifika huku wakipatwa na msiba mwingine wa msichana mmoja ambaye alipotea kimaajabu na kukutwa mbele kabisa ya ile meli akiwa amekufa.

    Vifo hivyo mfululizo viliwafanya wakate tamaa ya maisha.



    “najuta kwa nini nimeikubali hii safari.” Aliongea Balqis akimwambia Sharji aliyekuwa pembeni yake lakini kwa sauti iliyosikika kwa kila mtu.

    “yaani mimi ndio sina hamu.” Aliongea Sharji



    Malalamiko yalichukua nafasi kwa kila mtu aliyekuwa pale, lakini ukweli ulibaki pale pale kuwa ndio washaingia kwenye boti na sasa wamekwama na mauaji yanatokea kila siku.



    Masaa yalizidi kusogea huku njaa ikianza kuwatesa kutokana na kuishiwa na chakula toka jana yake usiku. Mpaka kufikia saa kumi na mbili jioni, wote walilegea kwa njaa ya toka usiku wa jana yake.

    “jamani mimi na wazo, mnaonaje tukeshe ili kama jini linakuja basi tulione kwa macho yetu.” Balqis alishauri baada ya kugota saa tano usiku.

    “ni wazo zuri.” Alidakia Karim aliyekuwa pembeni huku akiwa amechoka kutokana na njaa aliyokuwa nayo.



    “mimi ndio nitakufa kwa njaa usiku huu hata kabla huyo jini kunitafuna.” Aliongea dada mmoja aliyekuwa anagala gala kutokana na kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.



    Wakakubaliana kukesha macho mpaka asubuhi. Zoezi hili lilifanikiwa kwa kukucha salama bila mtu yeyote kupoteza maisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kwa hii njia labda tutafaulu. Vipi kuhusu kukabiliana na njaa?” aliongea Sharji na kuungwa mkono na watu wote waliokuwa pale.



    “hapo hatuna jinsi, ndio tutakufa kama kuku wa mdondo.” Aliongea Dada mmoja ambaye naye alikuwa hoi kutokana na njaa aliyokuwa nayo.



    Dakikia kumi baadae walishuhudia mwenzao aliyekuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo akiaga dunia mbele yao.



    Hali hiyo iliwakatisha tamaa kabisa na kuwafanya wachanganyikiwe kupita kiasi. Kwa shida ya njaa na mateso hatimaye kiza kikaingia tena.



    “vipi na leo tunakesha?” aliuliza Juma ambaye alionekana kidogo ana uvumilivu wa njaa.

    “kama kufa tutakufa tu, haina haja ya kukesha.” Aliongea Sharji.

    “ kama kulala basi tulale wote hapa hapa.” Alishauri Balqis na wote wakakubaliana hiivyo.



    Usingizi wa mang`amu ng`amu ulipatikana kwa uchovu waliokuwa nao japo kuwa walikuwa na njaa ya ajabu.

    Maji kidogo waliyokuwa nayo ndio yalikuwa tegemeo lao. Hata hivyo nayo yaliisha usiku huo huo.



    Hatimye palikucha na kujikuta waliofanikiwa kuiiona asubuhi hiyo walikuwa watu wanne tu. Wengine wote walikufa kwa kuraruriwa vibaya kila sehemu na kufanya eneo hila kutapakaa damu. Hata wao pia walijikuta wamamwagikiwa na damu kiasi ya wenzao.



    Waliobakia ni Balqis, Sharji, Karimu na nahodha. Walipigwa na butwaa lakini hawakutishika sana kutokana na mioyo yao kujaa ganzi kwa matukio yale waliyokuwa wakiyashuhudia kila siku.



    Walijua zamu yao ilikuwa siku ile hata kama wasingeuliwa na huyo jini basi njaa na kiu vilitosha kuwapotezea uhai.



    “mi naenda kulala ndani,…. Kama kifo changu kinaniita basi itakuwa nimeandikiwa hivyo.” Aliongea Balqis na kuingia ndani ya ile boti.



    Cha ajabu alitokea upande wa pili na kujibadilisha kwa kutibua nywele zake na meno makali yenye urefu usio wa kawaida yakajitokeza.

    Alionyesha mkono kwenye bahari na boti dogo la uvuvi likajitokeza. Alijitoa photocopy na kuwa Balqis wawili wanaofanana, hapo Balqis mmoja akayeyuka na kutokea kwenye ile boti ndogo ya uvuvi.



    Hapo alijigeuza mvuvi na kutokea na vifaa vyote. Hapo Balqis alicheka na kujirudisha kama alivyokuwa awali na kurudi tena kwa wenzake aliowaacha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “usingizi hauji mamaa” aliongea Sharji baada ya kumuona Balqis pale.

    “kuna lalika basi na hii njaa niliyokuwa nayo?” aliongea Balqis .



    Baada ya dakika kumi kupita, kwa mbali waliona boti ndogo ikija upande wao. Waliipigia mluzi na yule mvuvi aliwafikia mpaka pale walipo.



    Walimuelezea shida iliyowapata. Yule mvuvi alisikitika kisha akaawaambia kama wakitaka msaada wake basi wawili wenye nguvu wapande boti yake wakamsaidie kuvua samaki kisha watawapitia wenzao na kurudi nao.

    Chakula alichokibeba na maji viliwafanya wagombanie kama mpira wa kona. Baada ya kumaliza kula. Walipata nguvu kidogo na Karim akiwa na nahodha walipanda ule mtumbwi na kuondoka zao na kuwaacha Sharji akiwa na Balqis.



    Walipofika mbali na pale walipokuwepo, yule mvuvi alisimamisha boti yake na kuwageukia Karim na yule nahodha wao.

    “mnanijua mimi ni nani?” aliuliza yule mvuvi na kuwaangalia huku akiwakazia macho.

    “hatukujui!” walijibu kwa pamoja huku wakiwa na mshangao kwakuwa hawakutegemea swali kama lile.



    Hapo hapo alibadilika na kuwa Balqis. Wote walitoa macho hali ya kutoamini walichokiona.

    Baiqis alibadilika na kutoa makucha na kumrarua yule nahodha huku Karimu akishuhudia.



    “aaaaaagh!!!!”



    Mlio huo wa uchungu ulisikika mpaka kwenye ile boti alilikuwemo Sharji na Balqis.



    Dakika mbili baadae, Sharji anaiona ile boti aliyopanda kaka yake na yule nahodha ikirudi ikiwa haina dalili zozote za kuwepo na watu mule ndani.

    Ile boti ilipokaribia maeneo yale, Shariji alishangaa kuona maiti ya kaka yake ikiwa imelala kwenye ile boti.



    “MUNGU WANGU????”



    Alishika kichwa Sharji baada ya kuona vile. Mara akaanza kusikia hatua za miguu zikimfata pale alipo.



    “MAMAAAAAAAAA!!!!!!”



    Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.



    “AAAAAAAAAAAGH”

    Sharji alipiga kelele na kukurupuka. Alipofungua macho yake alishangaa kumkuta kaka yake akiwa ameshika mswaki wake akimuamsha. Alitoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango baada ya kumuona kaka yake aliyempenda kuwa hai tena.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sharji, amka basi ujiandae. Unasubiriwa wewe tu.” Aliongea Karimu na kumuangalia mdogo wake ambaye muda huo moyo ulikua unamdunda kupita kiasi.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog