Simulizi : Kisiwa Cha Majini
Sehemu Ya Nne (4)
Kwa kweli nilipomuona Yusira akiwa kwenye umbo lile huku akiwa anakuja kwangu niliogopa sana. Hata siku moja sikuamini kama mwanamke mzuri kama Yusira mwenye penzi moto moto alikuwa na sura ya kutisha kama ile. Niliwaza nitafanyaje ili kuweza kujiokoa tena kwenye mikono ile ya kijini. Kwa kweli bado nilikuwa na hamu sana ya kuendelea kubaki duniani. Pia bado nilikuwa na hamu ya kuendelea kuwepo na Maimuna kwani siyo mimi nilimsaliti bali nililazimishwa na mdogo wake. Yusira aliunguruma huku Mdomoni damu zikiwa zinamtoka utazani shingo ya ng'ombe imekatwa na damu zilikuwa zinatiririka. Ile hali ilimfanya Yusira kuwa na Sura ya kutisha zaidi. Tayari sasa alishanikaribia na kunyanyua CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/mikono yake ambayo ilikuwa na kucha ndefu na zakutisha. Nilishawahi kuona Mazombi mbali mbali kwenye picha ambayo yanakuwa na kucha ndefu na sura za kutisha ila kwa wakati yule Yusira alikuwa ametisha zaidi. Dalili ambayo alikuwa anaonesha Yusira ilikuwa inazihirisha tosha kuwa nilikuwa kwenye wakati mgumu sana. Yani uwezekano wa kufanyiwa unyambusi na yusira ulikuwa mkubwa sana. Yusira alinyanyua Mkono kisha akapanua Mdomo na kuachama tayari kwa kutaka kunishambulia. "subili kwanza kuna kitu nahitaji kumwambia Maimuna kabla sijafa"Niliongea kwa sauti kali na yenye hasira ambayo hata mimi nilijishangaa ule ujasiri nilikuwa nimeutoa wapi. Ile sauti ilimshitua Maimuna na kumwambia Yusira asitishe ili ananisikilize kwanza kuna kitu gani ambacho ningemwambia mimi. "Maimuna kwa kweli wewe mwenyewe unatambua ni kiasi gani nakupenda. Nakupenda sana Maimuna na nilikuwa nahitaji kuishi na wewe zaidi. Ila kwa kuwa umeamua kunitanguliza mbele ya haki basi sawa. Ila tambua kuwa unaniadhibu pasipo kufikilia. Mimi sijafanya hiki kitendo kwa kukubali mimi bali nimelazimishwa na mtu. Maimuna kumbuka siku tukiwa tunafunga ndoa yetu kwenye KISIWA CHA MAJINI ulitoa ahadi kuwa utanipenda mimi daima na milele na utanivumilia kwenye shida mbalimbali. Sasa mbona kwenye hii shida hutaki kunivumilia. Shida ambayo hata wewe unajua siyo kwamba mimi nilitaka kuifanya. Kwenye mapenzi yetu ulisema kamwe hutaniacha mimi labda mmoja wetu kupoteza maisha. Sasa mbona wewe mwenyewe unataka kuniua mimi. Ok mimi nimekubali kufa ila naomba unisamehe kwanza kile ambacho nimekifanya alafu uniahaidi siku na wewe ukifa na kunikuta huko kaburini naendelea kuishi utakubali kuliendeleza penzi letu"Niliongea haya maneno huku nikiwa siliasi mbaya. Haya Maneno yalimfanya kwanza Maimuna kubaki akiwa ananishangaa. Siyo Maimuna tu hata Yusira muda ule alibaki ameganda kwanza akishindwa la kufanya. "Kapopo utanisamehe kwa kukufanyia kitu kama hichi. Kwa kweli siwezi kuendelea kuishi na Mwanaume msaliti siku zote. Huwezi kunidanganya kuwa christina ati alikuzidi nguvu ukaamua kukubali. Mwanamke atakuzidije nguvu wewe mwanamme. Sema wewe mwenyewe ulikuwa umependa kufanya hivyo. Kwa hiki ambacho nakifanya naomba unisamehe"Aliongea Maimuna kisha alimwamlisha Yusira aniue ambae kwa muda ule alikuwa Amedua sana. "Maimuna mimi nimekubali sasa unie sina jinsi imeonesha ni kiasi gani umenichukie na kamwe huwezi kuendelea kuishi na mimi hapa duniani. Ila kuna kitu nataka nikuulize kabla sijafa. Maimuna nakuomba uniambie mama yangu bado mzima au amekufa. Nahitaji kujua hilo kama mama yangu ni mzima au amekufa Kama nitalijua hilo ndio mniue. Kama mama yangu atakuwa bado mzima basi ukamsalimie sana umwambie pia nilimisi vibaya mno. Pia ukienda Singida Msalimie Sana Rafiki yangu Mdete. Usimfiche kitu Mwambia kuwa wewe ndio uliyoniua. Mdete pia ndio yeye aliyonishawishi hadi mimi nilikubali kuwa na uhusiano na wewe. Pia msalimia baba yako na baba yangu kwani wote wale wamekuwa ni mwanga imara sana kwangu. Baba yako mwambie asante sana kwa vile vitu vyote alivyonifanyia. Ila hata kama mama yangu atakuwa amekufa na baba yako ndio alisema nimuue ili kukuoa wewe mwambie mimi nilimsamehe kwani ameonekana kunipenda sana"Niliongea tena haya Maneno huku Muda ule hadi machozi yalikuwa yananitoka na kusogea karibu kabsa na Uso wa Yusira ili aniue. "Dada Maimuna tafadhari naomba usimuue kapopo kwani hana kosa kabsa. Naomba uniue mimi dada yangu kwani mimi ndio nimesababisha hadi hiki kitu kitokee"Aliongea Tena Christina. "Pumbavu wewe malaya funga domo lako hivi unafikilia nimekusamehe atakufa kapopo na wewe utafuata"Aliongea Maimuna kwa sauti kali na yenye chuki ndani. "Kapopo kufa kupo pale pale tu haijalishi umeongea maneno gani ambayo yatanishawishi mimi. Wewe tayari ni mchafu maana umezini hivyo huwezi kuendelea kuwa na mimi kamwe"Aliongea Maimuna kisha alimwambia Yusira aniue. Kwa kweli hadi kufikia hapo nilikuwa sina tena neno la kuongea zaidi ya kupiga magoti na kutulia kimya tayari kwa kutaka kuuawa. Nilipopiga Magoti nilifanikiwa kuiona Miguu ya yusira kwani alikuwa amesimama karibu kabsa na kwangu. Ile miguu yani ilikuwa ya punda kabsa ingawa alikuwa na miguu miwili. Wakati nikiwa nashangaa ile miguu nilishangaa mikucha ikiingia Mwilini kwangu na kuanza kusikia baridi kali sana
Kwa kweli ile baridi ambayo nilikuwa naiona baada ya kucha kuzama kwenye mwili wangu ilikuwa inatisha sana. Yani tangia nizaliwe sikuwahi kuona baridi kama ile kwani ilikuwa baridi ya aina yake. Nilikuwa natetemeka sawa lakini cha ajabu mwili ulikuwa unatokwa na jasho mbaya. Kucha za Yusira ambazo ziliingia Mwilini kwangu zilianza kunipiga kitu kama shoti hivi kwani mwili wangu ulianza kubadilika rangi na kuwa mweusi kama mtu ambaye alikuwa amepakwa oil chafu. Kwa kweli sikuamini macho yangu kama Yusira binti ambaye alisababisha hadi mfanyakazi wake kufanya mapenzi na mimi ndio ambaye alikuwa ananiua. Nilinyanyua macho juu kumwangalia yusira cha ajabu pamoja na kuwa na sura ya kutisha lakini nilishangaa alikuwa anatokwa na machozi. Ile hali ya Yusira kulia ilizidi kunitia hasira ataliaje wakati yeye amesababisha haya mambo yote na bado yeye ndio amechukua jukumu la kuniua. Nilijitaidi kuamka ili nimzoe yusira lakini uwezo ule nilikuwa sina. Tayari mwili wangu wote ulishabadilika rangi na kuwa mweusi tii kama nimepakwa Masizi. Nguvu nazo mwilini kwangu zilikuwa zinakatika kwa kasi ya ajabu. Nilitamani kunyanyua Mdomo wangu ili kumwambia neno la Mwisho Maimuna ambaye alikuwa yupo kimya na kaangalia chini lakini nilishindwa. Taratibu macho yangu yalijaa ukungu hatimae usingizi mzito ulinipitia sikujua kile ambacho kilikuwa kimeendelea. "Sasa ndugu yangu naomba unisikilize kwa Makini yule pale ambapo ukifika nyumbani kwenu unamuona kama mama yako mdogo ndio mama yako mzazi. Mama yako hajafa kabsa ile siku ya msiba tulizika mgomba tu. Tena hakuna hata mtu mmoja ambaye alihudhuria kwenye ule msiba. Naomba nisikilize kwa Makini kapopo hapo najua nitakuacha round abaut usipokuwa makini kutega sikio. Ile siku ya Msiba ambayo wewe ulihisi mama yako amekufa mazingira ya msiba yote yalifanyika katika kisiwa cha majini ingawa yalibadilishwa na sisi tuliona kama mazingira yetu ya kwaida. Watu wote ambao wewe uliwaona wanalia walikuwa sio wenyewe bali ilikuwa ni vimvuli vyao. Hata wenyewe kesho yake waliposhituka waliota ndoto tu kuwa mama yako kafa na wamemzika yani mimi na wewe tu ndio tulihudhuria kwenye msiba wa kuzika mgomba tukiwa na miili yetu halisi ndio maana tuliamini kama mama yako amekufa. Ukitaka kuamini hiki mtafute mtu yeyote ambaye unamkumbuka kwenye msiba wa mama yako alikuwepo alafu umuulize kama aliota ndoto ya mama yako amekufa" Ilikuwa ni ndoto ambayo ilinishitua kwenye usingizi ambao nilikuwa nimelala. Kitu cha kwanza kukiongea niliposhituka nilisema Yusira usiniue. Nilishindwa kuelewa kwa nini niote tena ndoto kama hii ambayo ilikuwa maneno ambayo alinisimulia rafiki yangu Mdete CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ya kunisibitihia kama mama yangu ni mzima. Nilipoangaza vizuri kwenye kile chumba ambacho nilikuwepo nilijikuta nimelala kwenye kitanda changu tena kwenye nyumba yetu Singida. Ile hali ilinishitua kidogo maana nilichokumbuka nilikuwa nipo Saudi arabia tena kucha zilikuwa zimezama kwenye mwili wangu na mwili tayari ulikuwa umebadilika rangi na kuwa mweusi. "Inamaana Sijafa siyo, na kama sijafa huku Tanzania nimefikaje wakati nilikuwa nipo Saud Arabia"Niliongea haya maneno kwa Sauti bila kujielewa. Kwa kweli sikuamini kama nilikuwa Singida. Ilibidi Niamke pale kitandani nitoke nje ili kuhakikisha kweli nipo singida au naota. Niliamka taratibu na kuanza kutoka chumbani kwangu huku nikiwa nashangaa. Nilipofika sebureni nilimuona mfanyakazi wangu wa ndani na yeye akifanya usafi. Ile hali kweli ilianza kunifanya niamini kuwa nilikuwa nipo singida. "Shemeji pole sa Safari chai tayari nimekuandalia. Ila kabla hujanywa chai kunadawa Dada Maimuna kaniambia unywe kwanza ndio uje kunywa chai"Nilimsikia bint yule akinisemesha. Niliposikia jina Maimuna kwa kweli moyo wangu ulilipuka paa kwani nakumbuka Maimuna ndio ambaye aliamrisha kule niuawe sasa iweje bado nipo mzima. "Hivi nimekujali lini hapa nyumbani na nimekuja kwa usafiri gani vile Adela"Nilimuulize Mfanyakazi wangu huku nikicheka cheka kwani sikuwa najua kabsa nimefikaje Tanzania tena Singida kabsa nyumbani kwangu. "Jamani shemeji inamaana unataka kuniambia kuwa umesahau kabsa kama jana ndio ulikuja na dada. Sijajua kutoka dar hadi Singida mmekuja na nini. Ila Nyumbani mimi niliwaona mmeletwa na rafiki yako Mdete"Alinijibu mfanyakazi wangu. Yale majibu ya Adela yalinishitua Sana hasa aliponiambia kuwa rafiki yangu mdete ndio ambaye alinileta. "Wakati nimekuja nilikuwa natembea mwenyewe au nilikuwa nimelala wewe niambi.."Nilimuulizea Adela lakini kabla hata sijamaliza kumuuliza ili Anijibu nilihisi kama upepo mkali ulianza kuvuma pale. Cha ajabu ule upepo ulikuwa unavuma sehemu ambayo nilikuwepo tu. "Usimuulize sana Adela maswali ambayo atazidi kukushangaa. Ila kama unataka kujua umefikaje hapa naomba nenda kwenye kabati kuna kioo angali jinsi ulivyofika hadi hapa Tanzania. Pia ukimaliza kuangalia fanya kama Nilivyomuelekeza Adela kabla ya kunywa chai unywe hiyo dawa"Ilisikika Sauti ya Maimuna kwa nyuma yangu. Niligeuka nyuma kuangalia kama nitamuona Maimuna lakini sikuona kitu zaidi ya ule upepo kuacha kuvuma.
Kwa kweli ile hali ilizidi kuniogopesha sana ila sikuwa na jinsi niliamua kuondoka na kwenda hadi chumbani kwangu. Lengo nilitaka kufungua ile kabati na kutoa kile kioo kisha niangalie nimeokokaje kwenye kile kifo maana nilichokuwa nakumbuka mimi kucha za Yusira zilikuwa zimetinga kwenye mwili wangu na nilikuwa naona baridi kali sana. Baada ya baridi hiyo ambacho kilifuatiwa ilikuwa kupoteza fahamu sikujua kilichoendelea. Kitendo cha kushituka na kujikuta nipo singida tena nyumbani kwangu ndicho ambacho mimi kilinishangaza. Nilipofika chumbani wangu nilienda hadi kwenye kabati ya nguo na kwenda kufungua. Kweli nilipofungua kabati nilikutana na kioo saizi ya kati tu ambacho kilikuwa siyo kikubwa sana kilikuwa cha kawaida tu. Macho yangu yalipokiona tu kile kioo kwa kweli mapigo ya moyo wangu yalibadilika na kuanza kwenda haraka haraka. Ile dalili ilinifanya nibaini kuna jambo siyo zuri lipo kwenye kile kioo. Nililifikilia nichukue kile kioo niangalia au niache. Asilimia kubwa ya akili ya mwili wangu ili nicotrol niache kuangalia kwenye kile kioo kwani kama Najua bado nipo mzima haina haja ya kuangalia kitu ambacho kinaweza kunitia pressure. Ilibidi nifunge tena ule mlango wa kabati na kusitisha kuchukua kile kioo kuangalia namna gani nimefika hapa Tanzaniani wakati nilikuwa nipo Saud Arabia. Kitendo ch kufunga tu ile kabati nilishangaa kuona tena upepo mkali ukianza kuvuma. Ule upepo sikujua ulikuwa umetokea wapi kwani ulikuwa ni upepo mkali ambao ulikuwa umeambatana na Ngurumo. Ule upepo ulivuma kwa Muda kama wa dakika moja hivi kisha nilisikia sauti tena ya Maimuna ikiniamrisha nichukue kile kioo niangalie nimefikaje Tanzania. "Nimeacha kuangalia hicho kitu kwani hakina ulazima sana. Ili mradi nipo salama sitaki kujua nimefikaje hapa Tanzania"Nilimjibu Maimuna ingawa sikuwa namuona maana pale nilikuwa nasikia sauti tu. "Hebu acha kujidanganya kapopo hujafika kamili kutoka Saud Arabia kuna vitu vinatakiwa kurudi kwenye mwili wako kupitia hicho kioo. Ninachokuomba chukua hicho kioo uangalie kile ambacho kimeachana na mwili wako"Ilisikika tena Sauti ya Maimuna. Yale maneno ya Maimuna muda huu yalinishitua Kidogo. Kitendo cha kuniambia kuwa Mwili wangu haupo kamili kwa kweli nilishituka kidogo. Nilijichunguza Mwili wangu kuanzia juu hadi chini nilijikuta nipo full sikuwa na tatizo lolote. Hata hivyo bado niliamua kuchukua tu na kile kioo kuangalia kivipi maimuna anasema kuwa Mwili wangu haupo kamili. Nilienda nikafungua tena ile Kabati na Kutoa kile kioo. Kwanza kile kio kilinishangaza sana kwani kilikuwa kizito sana. Kioo kilikuwa na Udogo kama sahani tu ya Udongo lakini uzito wake kwa kweli ulinishitua. Kwa kuwa kile kioo kilikuwa kizito sana na uwezo wa kukishikilia niangalie ilikuwa hakuna niliamua kukiweka kwenye kitanda ili niweze kuangalia vizuri. Nilipokiweka tu kile kioo kwenye kitanda huku sehemu husika nikiiangaliza juu nilishangaa miale mikali sana ikitoka kwenye kile kioo. Ilibidi nisogee mbali kidogo huku nikiwa nashangaa ile hali kwani haikuwa hali ya kawaida kabsa. Nilipopiga hatua moja tu kurudi nyuma nilihisi kama mtu nyuma akinizuia huku akiniambia inatosha hapa hapa. Kwa kasi ya ajabu huku nikiwa nimeogopa niligeuka kuangalia alikuwa ni nani yule. Nilipogeuk cha ajabu sikuweza kumuona mtu wa aina yeyote yule. Ilibidi nikatulia na macho yangu niliyaelekeza kwenye kile kioo huku nikiwa natetemeka. Ghafla kwenye kile kioo miale iliacha kupiga na tukio ambalo Yusira aligeuka kuwa na Sura ya kutisha lilionekana kwenye kioo kile. Ile hali ilinifanya nishituke sana kwani muda ule kama Yusira alikuwa anatisha kuliko mwanzo. Taratibu Yusira alisogea hadi sehemu ambayo nilikuwepo na kunichoma na yale makucha
Baada ya Yusira kutia kucha kwenye Mwili wangu kisha mimi kupoteza fahamu ndipo mambo mengine kumbe yaliendelea. Kumbuka hapo kote matukio nilikuwa Naangalia kupitia kwenye kile kioo. Macho yangu yalikuwa yamekikodolea kile kioo ili kuweza kujua mambo kadha wa kadha. Jambo la kwanza ambalo nilitaka kuelewa ni nimefikaje Tanzania wakati nilikuwa nimepoteza fahamu Saud arabia. Pia Jambo jingine ambalo nilitaka kulifahamu ni kitu gani ambacho kiliendelea kwa yule Binti Christina baada ya Maimuna kugundua kuwa nilifanya naye mapenzi. "Inatosha usimfanyie kitu kingine kile chochote mwache nazani itakuwa imeshatosha. Hata rudia tena kwani nimebaini hata kufanya mapenzi atakuwa Amelazimishwa tu na huyu binti"Maimuna aliongea kumwambia Yusira ambaye alionekana bado alikuwa na hamu ya kutaka kunidhuru hata baada ya kufahamu kuwa tayari nilikuwa nimepoteza fahamu. Kwa kweli kile kitendo mimi kiliniuma sana ingawa nilikuwa naangalia kwenye kioo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Yusira yeye ndio alikuwa amesababisha hadi yule binti kupata nguvu za kufanya mapenzi na mimi baada ya kutuona tunafanya mapenzi naye lakini bado alionekana alikuwa anataka kuniua kabsa."Binti mimi wewe siwezi kukufanya kitu chochote ila iwe mwanzo na Mwisho kutembea na wanaume wa watu. Tena unabahati sana ningekugeuza kuwa swala sasa hivi ukatafunwe na simba ila nimeamua tu kukusamehe. Siku zingine hata kama unahisia kiasi gani jaribu kuzicontroll"aliongea Maimuna kumwambia Christina ambaye alikuwa anatetemeka mbaya. Baada ya kumwambia yale maneno Maimuna alianza kusogelea Mwili wangu pale chini. Alipoufikia alinyoosha kidole kuelekea kwenye sehemu ambao mwili wangu ulikuwa upo. Cha ajabu kile kidole ambacho alininyoshea kilitoa mwanga mkali sana kisha nilishangaa ule Mwili wangu ulibadilika na kuwa Mbwa. Tena mbwa mwenyewe alikuwa Mdogo sana mweupe na alikuwa mbwa ambao mara nyingi huwa nawaona wenzetu wa ulaya wanambwa kama wale na hutembea nae.. Baada ya kubadilika kuwa mbwa Maimuna alianza kukusanya Nguo zake na hatimae alinibeba mimi na kuelekea uwanja wa ndege. Hakutaka kabsa kuendelea kukaa pale kwa dalili ambazo alikuwa anaonyesha. Maana tiketi ambazo alikuwa amekata zilikuwa za kuondoka kesho yake ila muda ule ule baada ya kugundua tumefanya mapenzi na yule mfanyakazi alimamua kuondoka. Ndani ya Gari ambako alikuwepo Maimuna kuelekea uwanja wa ndege yusira na mimi ambaye niligeuzwa Mbwa pia nilikuwepo. "Kwa kweli dada yangu naomba unisamehe kwa hiki kitendo ambacho amekifanya mfanyakazi wangu. Mimi nahisi ni makosa yangu maana ndio mfanyakazi wangu yule. Vipi kuhusu huyu mume wako ndio utamgeuza mbwa hivi hivi mazima au"Nilimsikia yusira akimwambia Maimuna ambaye muda wote alionekana kuwa makini na gari. Baada ya Yusira kumwambia vile Maimuna hata Maimuna hakuongea maneno mengi bali alisema Atajua yeye mbele kwa mbele. Maimuna alipofika Uwanja wa ndege alikata Tiketi zingine kisha alipanda Ndege akiwa na mimi ambaye muda ule nilikuwa mbwa. Baada ya kupanda Ndege Maimuna hakuna tukio lolote ambalo liliendelea kwenye ndege ambalo lilionekana kwenye kioo. Tukio ambalo lilifuata lilinishitua maana nilijiona mimi nikiwa kwenye mwili wangu wa kawaida huku tukiwa kwenye basi. Cha ajabu kwenye lile basi nilikuwa naonekana mtu mwenye furaha Sana na muda wote nilikuwa natabasamu na kumlalia Maimuna. Hata Maimuna alionekana kuwa na furaha Sana na muda wote alikuwa ananipiga mabusu huku akiniambia Ananipenda. Kwa kweli ile hali iliniogopesha kwa kweli maana mimi sikukumbuka kabsa kama tulikuwa kwenye basi na tulikuwa tunafanya mambo hayo. Nilipochunguza vizuri ile gari niligundua ilikuwa ni Abc na tulikuwa tunarudi Singida kutoka Dsm. Hata tulipofika Stendi ya Singida Rafiki yangu Mdete ndio alikuja kutupokea na alionekana mtu wa Furaha sana. Ni kweli hata kile ambacho alikiongea Adela mfanyakazi wangu wa ndani kilikuwa cha Ukweli maana mdete ndio ambaye alitupakia kwenye Gari na kutupeleka hadi nyumbani kwetu. Tena ndani ya Gari tulikuwa tunapiga stori za kuchekesha sana na Mdete. Alipotufikisha tu mdete nyumbani kwetu ndio na kioo kile kilitoa miale mikali kisha hakikuonesha kitu cha aina yeyote tena. Kwa kweli nilibaki nikiwa natetemeka huku ile hali ikizidi kunishangaza sana. "Mbona unatetemeka wakati upo kwenye hali ya kawaida sana. Nenda kanywe ile dawa kisha kunywa chai mpenzi wangu tukamsalimia baba yako"Nilisikia sauti ikiwa inaongea kwa nyuma. Ile sauti mimi nilikuwa naifahamu sana ilibidi nigeuke kuangalia kweli kuna mtu alikuwa ananisemesha tena au bado ilikuwa sauti yake. Nilipogeuka kaungalia nilishangaa alikuwa ni mpenzi wangu Maimuna na alikuwa ametoka bafuni kuoga kabsa. Kwa kweli ile hali ilizidi kunishangaza sana, sikujua Maimuna aliingia Saa ngapi chumbani hadi akaenda na kuoga.
Kwa kweli kile nacho ilikuwa ni moja ya kitu kigeni sana kwangu maana nilichokuwa nakumbuka nilipoamka kitandani kwangu Maimuna alikuwa hayupo. Hata nilipotoka nje kwenda kumuulizia adela aliniambia tu kuwa Maimuna kaenda kazini ila amesema nikiamka kabla ya kunywa chai natakakiwa ninywe dawa flani. Nilimwangalia tena Maimuna kwa makini huenda alikuwa siyo Mwenyewe lakini alikuwa Mpenzi wangu kabsa Maimuna. Kwa kweli hapo ndio nilianza kuamini kuwa Maimuna hakuwa mtu wa mchezo kabsa na huenda ukawa unatembea nae bila wewe kujua. "Mbona kama unaonekana unashangaa sana kuna tatizo gani. Maana tangia nitoke bafuni unaniangalia unaonekana una wasiwasi. Kwanza ile dawa ambayo adela amekupa umekunywa"Maimuna alinisemesha. Kweli kile kitu ambacho aliniuliza Maimuna hakuwa amekosea. Kweli nilionekana mtu wa kushangaa sana tangia nilipomuona Maimuna ndani. "Bado sijanywa ile dawa Mke wangu. Kwanza kabsa mpenzi wangu nakuomba unisamehe kabsa na tusahau kabsa yale mambo ambayo yalitokea kwa nyuma. Nimegundua kama nimekufanyia kosa kubwa Sana ingawa hayakuwa malengo yangu. Ila hata hivyo naomba tu unisamehe kamwe hautakuja kuona kitu kama hiki tena kimetokea. Nakwambia ukweli kama atatokea mtu tena aniforce kimapenzi kama Christina basi nitamua na wewe utashuhudia hicho kitu. Ila pamoja na kukuomba msamaha kuna kitu nahitaji kukifahamu mpenzi wangu. Kitu cha kwanza nahitaji kujua ilikuwaje mimi wakati narudi Singida nilikuwa binadamu wa kawaida ila mambo yaliyotendeka mimi sikuyona wala sikuwa na kumbukumbu nayo. Mfano tuliporudi toka Dar kuja singida Rafiki yangu mdete alitupokea na ilionekana tumeongea mambo mengi sana lakini mimi sikuongea naye. Siwezi kukuulizia nimeondokaje Saud Maana Najua kule ulinigeuza mbwa. Kitu cha pili nahitaji kujua ni kweli ulikwepo ndani au uliende kazini maana Adela kaniambia ulikuwa kazini na kweli hata humu ndani hukwepo. Bafuni nilienda kukojoa siyo muda lakini hukwepo"Nilimueleza Maimuna kisha nimuuliza na swali. Yale Maswali ambayo nilimuuliza Maimuna yalimfanya kuanza kucheka hali iliyomfanya kuonekana kama amefurahishwa na kile ambacho nilikiongea. "Kwanza kabsa mimi nilikuwa nimeshakusamehe kutoka Saudi arabia. Kitendo cha kumzuia Yusira kukuua ndio Msamaha tosha kwako. Pia nimekugeuza mbwa kama adahabu tosha kwako. Pia nimekugeuza Mbwa kimakusudi kama utakuja kusubutu kufanya mapenzi tena na binadamu yeyote yule basi utakuja kugeuka mbwa mazima yani hakuna mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kukurudisha kuwa binadamu tena. Hata mimi jini sitakuwa na uwezo wa kukurudisha kuwa binadamu tena. Mimi bado nakupenda kapopo ndio maana hadi sasa bado upo hapa. Ila kama utakujua kurudia kufanya kitu kama hicho kwa kweli sitakuja kukusamehe tena. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Kuhusu wewe kujiona kwenye kioo ukiwa katika hali ya kawaida unacheka na rafiki yako lakini hukumbuki kama ulifanya hivyo hicho ni kitu cha kawaida sana. Kuna dawa ambayo mimi nilikunusisha ile dawa ukinusa kitu kikifanyika tu hazipiti dakika tano unakisahau. Hivyo haina maana ya kutaka kujua sana hiyo dawa maana haikuhusu ila elewa sasa upo mzima wala hauna shida yeyote. Kuhusu mimi kuambiwa nipo kazini alafu unanikuta nyumbani hicho kitu cha kawaida sana kwa sisi majini. Mfano mimi mwenyewe naweza nikajigawa mara nane hapa hapa ila mwili wangu mmoja ndio ambae utakuwa unacontrol miili mingine. Hivyo mimi wala sijaenda kazini ila nilitoka kama ninaenda kazini kwa mwili mwingine ambao nimejigawa. Ila hata sasa hivi adela ameniona kama nimerudi. Hivi ni vitu vya kijini na vigumu kuelewa wewe utakiwa kuzoe tu kwa kile ambacho unakiona"Alinijibu maimuna majibu ambayo yalizidi kunichanganya sana. Kwa kweli hadi hapo sikuwa na swali jingine la kuuliza zaidi nilitoka na kwenda sebureni nikachukua maji kwenye glassi na kunywa ile dawa ambayo Adela alinipa na kuniambiwa nimepewa na Maimuna. Baada ya kunywa ile dawa nilikunywa na chai kisha nilirudi chumbani kujiandaa kwa ajili ya Safari ya kwenda kumuona baba yangu. Ila kunakitu ambacho kila nilipokuwa nakumbuka furaha yangu ilikuwa inapotea ghafla. Kitu chenyewe ilikuwa juu ya Maimuna aliponiambia kama nitakuja kufanya mapenzi na mtu yeyote tofauti na yeye basi nitageuka Mbwa mazima. Niliwaza kama Maimuna atakuja kupotea ghafla au kufa maana hata majini yanakufa basi mimi nisingetakiwa kufanya mapenzi tena. Achana na kufa sisi wanaume tunavutiwa sana inaweza ikaja kutokea mtu akanilazimisha bila kupenda maana wanawake wanajia nyingi nikafanya mapenzi nako nitageuka Mbwa mazima. Kwa kweli ule ni msumari wa nchi tatu kabsa Maimuna aliupigilia. Hata hivyo niliapa kukaa mbali kabsa na wanawake ili kuweza kuyaweka maisha yangu kwenye hali ya Usalama. Baada ya kujiandaa wote mimi maimuna pamoja na Adela tulipanda kwenye Gari tayari kwa safari ya kwenda kwa wazazi wangu. Njiani ilikuwa ni furaha kila mtu alikuwa anajitaidi kuongea maneno ya kumfurahisha mwingine. Hata mimi sikujua ile furaha ilikuwa imetoka wapi. Tulipofika nyumbani kwa baba yangu kwa kweli kuna kitu nilikiona cha kushangaza sana. Nyumba ambayo ilikuwa ipo ya baba yangu ya tofali za kawaida kisha kuezekwa kwa bati ilikuwa hakuna bali kulikuwa na nyuma moja nzuri sana ambayo ilikuwa ipo ndani ya geti. Ilibidi niangalia kwa makini huenda nilifikilia labda nimekosea huenda tumeenda sehemu tofauti. Hata nilipochunguza kwa makini niligundua kuwa pale ndipo ilikuwa nyumbani kwa baba yangu. Wakati nikiwa nashangaa ile hali nilimuona baba yangu akiwa anatoka ndani ya lile geti huku wakiwa na rafiki yangu mdete wakiongea. "Hauna haja ya kushangaa sana hiyo ndio zawadi yangu kwa baba yako. Nilikupeleka kwenda Saud arabia ili ukija huku nikufanyia Surprise. Ulipoondoka tu huku nyuma ujenzi ulianza mara moja"Aliniambia Maimuna hali iliyonifanya kufurahi hadi nilianza kutetemeka.
Kwa kweli kile kitendo cha kukuta kwenye nyumba ambao alikuwa anaishi baba yangu kumejengwa nyumba nyingine nzuri kilinifanya kubaki hoi. Kweli ile ilikuwa ni Surprise ya nguvu ambayo alinifanyia Maimuna. Hapo kweli nilibaini maimuna alikuwa ananipenda kweli na kuapa kamwe sitakuja kumsaliti tena. Kwangu kumsaliti Maimuna ilikuwa vigumu tena ingawa nasikiaga watu wengi hupata bahati ya kuwa na uhusiano na majini ila wanakuja kuferi mashariti ila mimi muda huo nilikuwa sipo tayari kabsa kufanya ujinga tena. Kwanza kama ningemsaliti maimuna muda ule kwanza ningegeuka mbwa na pili kukosa furaha kama ya muda ule. Ile nyumba kwa kweli kila nilipokuwa naiangalia nilikuwa siimalizi. Nilimfuata Maimuna na kwenda kumkumbatia huku nikitoa Shukrani ambazo hazikuwa na kikoma. "Nashukuru sana Mpenzi wangu kwa kweli leo ndio nimeamini kama kweli unanipenda. Yani unanipenda mimi pamoja na wazazi wangu. Furaha ambayo nipo naye kwa kweli haipimiki. Basi baby nikufanyie nini basi na mimi kama malipo yako kwa mambo haya yote ambayo unanifanyia"Nilimwambia Maimuna huku nikizidi kumkumbatia. "Hata mimi nakupenda sana mpenzi wangu. Nakupenda wewe pia hata wazazi wako ni wangu ndio maana nawafanyia yote haya. Waswahili husema ukipenda boga basi upende na ua lake. Ambacho mimi nataka unifanyia kwa kunilipa haya yote ambayo nimekufanyia ni kunipenda kwa dhati tu mpenzi wangu. Sitaki unisaliti kamwe maana ukinisaliti lazima ugeuke mbwa kitu ambacho kitaniumiza mimi pamoja na wazazi wako"Aliniambia Maimuna. Nilichomwambia Maimuna muda ule kuwa neno usaliti naomba asahau kwani hilo hata mimi nilikuwa nimeliwekea kipao mbele. Baada ya kupongezana pale na Maimuna tulianza kutembea kuelekea sehemu ambapo alisimama mzee wangu na rafiki yangu mdete. Tulipomfikia mzee kwa kweli alinikimbilia kwa furaha na kuja kunikumbatia. Ile furaha ya muda ule mzee ambayo alikuwa ameionyesha kwa kweli ilikuwa siyo ya kawaida. Tangia anizae kwa kweli sikumuona mzee wangu akiwa na furaha kama ile. Baada ya kukumbatiana na mzee wangu aliniachia na kumsalimia na Maimuna kisha Maimuna aliingia ndani na kutuacha mimi mdete na mzee wangu nje. "Kwa kweli mwanangu jicho lako linaona mbali sana. Huyu mke ambaye umemuoa kwa kweli siyo wewe umemchagua bali moja kwa moja neema kutoka kwa mungu wangu. Kwa kweli mwanamke ameyafanya maisha yangu kuwa ya furaha tele na natamani mungu aniongezee miaka mia mbele kuishi. Kwa kweli mzee Ramadhani huyu ambaye maisha yake yalikuwa ya shida leo hii amekuwa mtu wa kutembea kwenye magari. Asante Mungu kwa kumpatia mwanangu mke mwema kama huyu. Yani huwezi Amini kuna baadhi ya watu wameanza kuongea maneno ya unafiki ati mwanangu ameoa jini mara mwanangu amekuwa free mason. Yani waswahili mtu akifanikiwa tu maneno yanakuwa kibao. Kweli wahenga hawakukosea waliposema pata pesa watu wajue tabia yako. Maana sasa hivi nakwambia waandishi wa habari kibao kila mmoja anataka nielezee siri ya mafanikio yangu"Aliongea baba yangu kisha aliniambia tuende ndani."Lazima watu waongee baba yangu hivyo. Kwani baba kwa mfano kweli ingetokea mimi ningekuwa nimemuoa mwanamke jini wewe ungefanyaje. Yani mfano ikatokea maimuna ni jini na mimi pamoja na wewe hatulijui hili ila tukaja kulijua baadae utafanyaje?"Nilimuuliza baba yangu huku tukiwa tunatembea kuelekea ndani. Nilimuuliza swali hilo baba yangu kimakusudi ili kuweza kujua angechukua hatua gani kama angebaini hivyo ili niweze kufanya maandalizi."Hata kama Maimuna atakuwa Zombi kwa haya mambo ambaye amenifanyia nitakuwa na furaha tu. Kwani nani ambae alikuwambia kuwa majini siyo binadamu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Huyu mtoto hata kama asiwe binadamu wa kawaida kwa kweli siwezi kukulaumu mwanangu. Yani achana na mwanae baba yake sasa anavyotujali yani sijawahi kuona. Twende ndani ukaone palivyo badilika pia nikupeleke kwenye biashara yangu yani acha mungu kweli anasikiliza shida za watu. Kila siku nilikuwa naomba na mimi kuwa tajiri hatimae mungu kasikia kilio changu. Hata kama utajiri wa kupewa lakini nashukuru hivyo hivyo"Aliongea baba yangu. Tulienda hadi getini tukafunguliwa na wote watatu tuliingia ndani. Nilipofika ndani ya uzio wa nyumba macho yangu yalitua kwenye gari nyingine ndogo aina ya mark two mpya. "Umeona hiyo gari, hiyo gari ni mke wako Maimuna amemnunulia mama yako mzazi hiyo gari. Tena hata yeye anahamu ya kukuona twende ukamsalimie" aliongea baba yangu maneno ambayo yalinishitua kidogo. Ambacho nilikuwa nafahamu mimi mama yangu mzazi alikuwa ameshakufa. Ilibidi nimuulize tena mzee anamaanisha mama yangu mdogo au ili kuweza kupata ukweli zaidi. "kapopo na wewe inamaana mama yako aliyekuzaa humjui au. Hii Gari amenunuliwa mama yako au mke wangu nikuambia hivyo ili unielewe zaidi"Aliniambia mzee wangu kisha alinishika mkono na kunivuta kunipeleka ndani nikamuone mama yangu. Yale maneno ya mzee wangu kwa kweli yalinichanganya kidogo maana nilichokuwa naelewa mama yangu alikuwa ameshakufa hata mzee alikuwa analielewa hilo
Kwa kweli sikuwa na jinsi huku nikiwa nashangaa niliamua kukubali kuelekea sehemu ambayo alikuwepo mama yangu kama baba yangu alivyokuwa anadai ili kwenda kumsalimia. Wote watatu mimi Mdete pamoja na baba yangu tulikuwa tumeongozana kwenda ndani kwenda kumsalimia mama yangu. Tulipoingia Mlangoni nilikuta mama yangu mdogo akiwa amekaa na maimuna huku wakiwa wanaongea. Kwa kweli ile nyumba sebure yake tu ilikuwa hadi raha. Baba yangu ambaye alizoe kukaa kwenye viti kama Vigoda huku chini kukiwa kunatimua Vumbi leo hii alikuwa anakaa nyumba ambayo ilikuwa na marumaru kuhu sofa za kifahari ambazo sikuwahi kuwaza kama familia yetu itakuja kulia zilikuwepo ndani. Nilipoona kwa jinsi kile sebure ambacho kilikuwa kimesheni vitu kama tv flat screen ya Ukatani, sofa safi viti na meza zakutosha nilisahau hata kama nilikuwa nimeenda ndani kwenda kumuona mama yangu. "Unashangaa nini baba yangu hii kazi ya Mwanangu Maimuna. Kwa kweli najivunia kupata mtoto wa kike kama huyu umeona kazi ambayo ameifanya. Wewe ulishazoea kila unapokuja kuniona lazima ukute vumbi. Sasa hivi subutu mafua na kikohozi bila mpangilio kwa heri"Aliongea Mzee wangu huku akiwa anatabasamu. Yale maneno ya mzee wetu yalitufanya wote pale sebureni tucheke hali iliyofanya kujua kama muda ule familia yetu ilikuwa ya raha sana. "Karibu mwanangu karibu sana nyumbani kwako maana tangia uondoke Kwenda Saud arabia kila siku nilikuwa natamani kukuona"Iliongea mama yangu mdogo ambaye alikuwa amekaa na Maimuna. Ile Sauti ya mama yangu mdogo kwa kweli ilinishitua sana. Kwani ile sauti ilikuwa inafanana na sauti ya mama yangu kabsa. Mama yangu Mdogo sauti yake mimi nilikuwa naifahamu ila sauti ya muda ule haikuwa sauti yake ilikuwa sauti ya mama yangu kabsa mzazi. "Mwambie labda mwenyewe mama kapopo, mimi nimemwambia mwanao kuwa ulipoondoka kila siku ulikuwa unamuulizia sasa mwambie mwenyewe labda ataamini"Aliongea baba yangu na kunifanya nizidi kushangaa. Kwani mama yangu mdogo alikuwa anaitwa mama hassani hivyo kitendo ha kumuita mama yangu mdogo jina la mama yangu mzazi kilinishangaza kweli. Kupitia sauti ambayo nilikuwa nimesikia pamoja na jina ambalo alimuita baba yangu mama yangu hapo niligundua kama yule huenda alikuwa mama yangu ila kuna mchezo tu maimuna alikuwa ananichezea. Kama Maimuna aliweza kunigeuza hadi mbwa na kusafiri nae kutoka Saud arabia hadi Tanzania atashindwake kumgeuza mama yangu sura nyingine. Sikutaka Kuonyesha Mshangao sana Muda ule zaidi nilimsalimia mama yangu vizuri na kuendelea kupiga stori mbali mbali huku tukicheka kwa furaha zaidi. Cha ajabu muda ule sauti ambayo ilikuwa inasikika kwa mama yangu ilikuwa sauti ya mama yangu mdogo na wala haikuwa sauti ya mama yangu. Muda ule kwa kweli nilitaka kwenda kumuulizia mtu mmoja ambaye nilimuona kwenye msiba wa mama yangu huyo ndio angeenda kunipa ukweli wa mambo kama mama yangu ni mzima au amekufa. Kwani Rafiki yangu mdete alishaniambia kama nataka kuamini kama kweli mama yangu alikuwa hajafa basi nitafute mtu yeyote ambaye alikuwa kwenye msiba kisha nimuulizie kama alishawahi kuota ndoto ya aina yeyote ile kuhusu mama yangu kufa. Baada ya stori za hapa na pale ilibidi nikamuaga mke wangu Maimuna kuwa nataka kutoka na rafiki yangu kwani kitambo sana. Maimuna wala hakuonyesha dalili yeyote ya kukataa zaidi aliniambia nichukue gari niende yeye atarudi na baba yangu hadi nyumbani kuna zawadi anaenda kumpa alimnunulia kutoka Saud Arabia. Ile kwangu ilikuwa ni nafasi tena nzuri kwangu kuweza kuongea mambo mengi na Mdete kisha kumtafuta Karimu kwani naye ni moja ya Mashekhe ambao walikuwepo kwenye msiba wa mama yangu. Tulitoka pale ndani na Mdete kisha tulienda kupanda kwenye gari yangu matata sana kisha tuliondoka kuelekea kwa shekhe Karimu. "Hivi mbona ndani ulikuwa kama unamshangaa sana mama yako kwani kulikuwa na tatizo gani"Aliniuliza Swali Mdete ambae sikujua alikuwa anamaanisha kitu gani. "Unajua pale rafiki yangu mdete kuna kitu kilinishangaza kweli. Baba yangu aliponiingiza ndani si unakumbuka alisema kuwa naenda kumuona Mama yangu. Kweli kabsa nilipofika mtu ambaye alikuwa ananisemesha sauti ilikuwa ya mama yangu lakini sura ilikuwa ya mama yangu mdogo hicho ndicho ambacho mimi kilikuwa kinanishangaza"Nilimjibu Mdete huku nikimkazia macho ili na yeye aniambie kama na yeye alikuwa ameisikia ile sauti. "Kaka yule ambaye alikuwa anaongea pale ni mama yako mzazi wala hakuwa mama yako mdogo. Hivi huoni hata Mzee wako alimuita mama kapopo. Yule ndio mama yako mimi nilikuwa namuona mama yako wa kawaida tu wala sijaona sura ya mama yako mdogo"Aliongea Mdete maneno ambayo yalinifanya hadi nilisimamisha gari na kushindwa kuendelea kukimbiza kabsa. Nilishindwa kuelewa ni kitu gani Maimuna alikuwa ananificha. Kama mama yangu alikuwa hajamua si angenifahamisha tu na mimi nianze kumuona ili furaha izidi zaidi na ndoa yetu iwe nzuri zaidi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
888888888888888888888888888888888888 Kwa kweli nilishindwa kuelewa kwa nini sasa maimuna ananificha mimi kujua kama mama yangu bado mzima au ameshakufa. Upande wangu sikuona faida kabsa ya Maimuna kulificha lile jambo maana lilikuwa linanifanya mimi kujisikia vibaya na yeye alikuwa hapati faida ya aina yeyote ile. "Mdete mimi narudi nataka nikamwambia baba yangu na mama yangu yule yule ambae mimi najua ni mama yangu mdogo. Nataka nikawaambia kama mimi nimeoa jini na mama yangu ndio nilimtoa kafala kama mahari ili niweze kujua watasemaje. Nafanya hivyo mbele ya maimuna kama mbwai na iwe mbwai barida"Nilimwambia Mdete huku nikifungua mlango wa Gari tayari kwa kutaka kuanza kushuka. Hata kabla sijatua mguu wangu mmoja chini mdete aliniwahi akanishika na kunivuta kunirudisha ndani ya gari. "Hapo ndipo huwa mnakosea unakuwaje na maamuzi ya kukurupuka Kapopo. Hivi Maimuna humjui kama yeye ni jini unataka kukurupuka tu kufanya maamuzi ya kijinga. Hivi ukimchokoza maimuna utakuwa unatembelea gari tena kama hili. Hebu kumbuka kwanza maisha mwanzo ambayo tulikuwa tunaishi ndio ufanye maamuzi. Watu sasa hivi tukipita mtaani unasikia boss mdete sasa unataka kutuharibia siyo. Hebu angalia baba yako raha aliyenae na amesema hata kama maimuna atakuwa jini yeye hajari hilo. Maimuna kumficha mama yako usimuone anamaana yake bwana hawezi kufanya tu kitu kama kile bira maana yake. Uzuri umeshaelewa mama yako hajafa bado mzima hizo chokochoko zingine unazitolea wapi. Hebu tulia twende kwa shekhe Karimu ukamuulizie wenzako tumezoea kutembelea magari usije ukatukimbizia ndege wetu"Aliongea Mdete. Yale maneno ambayo aliniambia Mdete nilihisi kama yanaukweli kidogo. Maana maimuna kweli asingeamua tu kumficha mama yangu bila sababu ya msingi. Nilichofanya nilirudi kwenye gari kisha tuliendelea na safari yetu ya kwenda kwa shekhe Karimu ili kwenda kumuulizia kama alishawahi kuota ndoto kuwa mama yangu amekufa. Maana huyu Ustadhi alikuwa ni moja ya watu ambae walikuwepo kwenye msiba wa mama yangu ambae ilisemekana wao walikuwa wanameota tu. Safari ya kwenda Nyumbani kwa Shekhe Karimu Misuna haikuwa ndefu sana na tulipofika pale uzuri tulimkuta shekhe yupo. Kwa kweli yule shekhe alipotuona alitupokea vizuri tulikaa na kuanza kupiga story za hapa na pale. Baadae tulimuomba apande kwenye gari ili tuende sehemu tukazungumze kwani pale ndani niliona siyo pazuri kuongelea kitu kama kile. Yule shekhe wala hakuwa Mgumu alimuaga Mke wake kisha tulitoka nje tulipanda kwenye gari na kuondoka. "Hebu niambieni siri ya mafanikio yenu maana vijana mmekua nawaona ghafla tu nashitukia mnamagari manyumba hata maisha ya mzee wako kapopo yamebadilika kabsa na sasa hivi tajiri mbaya. Maana nakumbuka nyinyi mlikuwa wanafunzi wangu madrasa nyie. Kuna watu Mungu anawajalia bwana"Aliuliza shekhe Karimu Swali ambalo kwangu lilikuwa gumu sana kulijibu maana nilishindwa ningemwambia kitu gani tumekifanya cha haraka sana hadi utajiri wetu ulikuwa vile maana tulikuwa matajiri sana. "Haya mambo ni kumuomba Mungu tu ndugu yangu ndio yametufanya hadi kufika hapa. Ila unajua baba yangu alikuwa na kiwanja kikubwa sana maeneo ya kitunda Dar ambacho aliachiwa na Marehemu baba yake ambaye ni babu kwangu. Hivyo kile kiwanja amekiuza kwa pesa nyingi sana kwani kunamtu amejenga sheri pamoja na nyumba. Hivyo kupitia zile pesa ndio unatuona leo hivi"Nilimwambia yule shekhe kwa kumdanganya. "Kwa kweli hongereni sana mmetumia akili za busara maana kama unakitu umeshindwa kukitumia bora ukibadilishe vile ili ukitumie kwa njia nyingine. Maana mlichokifanya kizuri sana kiwanja ambacho kilikuwepo tu mmekiuza kikawajengea nyumba pamoja kuyafanya maisha yenu kuwa mazuri. Ila nawaomba kitu kimoja naomba msimsahau mungu wenu. Maana watu wengi wakishapata pesa tu basi wao huwa wanamsahau sana mungu na kuanza kumuhasi"Aliongea Shekhe karimu. Dakika kama kumi mbele tayari tulishafika kwenye kiziwa Kindai ndicho ambacho tulikuwa tunakwenda kwa ajili ya kwenda kuumuliza yule shekhe. "Shekhe kuna kitu mimi nilikiota kwenye ndoto sasa na wewe nataka uniambie kweli na wewe uliota. Maana niliota kuwa mama yangu amekufa alafu na wewe ulikuwepo hiyo siku ya kumzika mama yangu. Sasa watu huwa wanasema kama utaota ndoto yenye uwezo wa kuelezea baadae huwa ya kweli hata ukienda kumuuliza na mwenzako uliyeota yupo kwenye lile tukio basi na yeye atakuwa ameota vilevile. Je ni kweli na wewe Ustadhi ulishawahi kuota kama mama yangu Amekufa"Nilimuuliza swali Shekhe Karimu baada ya kushuka tu kwenye gari. "Subuhhanah allah kijana unaongea nini wewe hivi unataka kuniambia kuwa mama yako hajafa. Kijana siyo kwamba ilikuwa ni ndoto ni ukweli mama yako kafa na wote tulimzika. Unataka kuniambia wewe hujui kama mama yako amekufa? Kweli kufiwa na mtu wa muhimu kwako kuna shida maana kijana wangu bado tu hujaamini kama mama yako ametangulia mbele ya haki. Kwanza unamaana gani kuniuliza swali kama hilo kwani mama yako wewe unamuona na unashinda naye maana unaniuliza swali linautata zaidi"Alijibu yule ustadhi huku akiwa ananishangaa. Yale majibu ya ustadhi naye yalizidi kunichanganya maana mimi nilihisi huenda yeye ndio ambae atanisibitishia kama mama yangu hajafa kama alivyokuwa amesema mdete. Niligeuka kumwangalia mdete kama inshara ya kumwambia kuwa umeona hiki ambacho shekhe amekiongea cha ajabu sikumuona mdete. Kwa kweli nilibaki nikishangaa huyu mdete kaenda wapi mbona tulishuka wote kwenye gari na hata dakika moja haijapita alikuwepo hapa leo kapotelea wapi.
Kwa kweli kile kitendo cha kumkosa Rafiki yangu Mdete wakati hata Muda wa dakika moja ulikuwa haujapita ulinishangaza sana. Ilibidi nianze kuita Mdete huku nikiwa najitaidi kusikiliza kwa makini kama angeitika sehemu yeyote ile. Cha ajabu nilishangaa Mdete akiitika pembeni yangu hali iliyonifanya nishituke zaidi kwani ile sehemu alikuwa hayupo. Kwa kweli kitendo cha kumuona tena mdete kwa ghafla pale nilianza kuhisi labda mdete alikuwa amebadilika kuwa Maimuna maana lile tukio sikulipatia picha. Nilipomwangalia Mdete hata yeye nilimkuta akitetemeka hali iliyonifanya nizidi kuogopa. "Kapopo twende bana tuondoke kwani muda umeshaisha hapa tulipo. Kuna kazi flani nataka kwenda kuifanya naomba tuondoke sasa hivi"aliongea Mdete na kuanza kutembea huku akiwa anageuka geuka nyuma kama vile alikuwa Ameona kitu cha kutisha. Ile hali kwa kweli ilizidi kuniogopesha maana hali ambayo alikuwa naye mdete ilikuwa siyo ya kawaida. Niligeuka nyuma kuangalia mdete alikuwa amekiona nini cha ajabu hadi alibadilika vile. Hata nilipogeuka sikuona mtu zaidi ya shekhe CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/karimu alikuwa anaangalia huku akicheka. Kitendo cha shekhe karimu kuanza kucheka nilianza kumshitukia kidogo maana tukio lile alitakiwa asicheke kwa shekhe kama yule zaidi ya kuuliza kuna nini mbona tumekuwa vile ghafla. Mimi sikutaka kushughulika sana na Karimu zaidi niliamua kumkimbilia mdete na kwenda kumshika shati. "Mdete niambi na wewe umekuwa jini, niambie rafiki yako ili nijue. Maana umepotea ghafla mara utokee tena niambie kama umekuwa jina na wewe"Nilimwambia mdete huku nikiwa namvuta. Cha ajabu mdete hakunijibu kitu chochote zaidi ya kugeuka geuke nyuma na kutulia. Wakati nikiwa naendelea kumbana mdete aniambie kuwa kuna kitu gani kilikuwa kinamsumbua mbona anaondoka kiajabu ajabu ndipo nilisikia ustadhi Karimu akiwa anakuja kwetu huku na yeye akinishangaa. "Jamani mmenileta huku ziwani kuja kuniambia kitu mbona sasa hamjaniambia kitu na mnataka kuondoka. Alafu kwa kweli nyie vijana mbona siwaelewi mlipotea ghafla mlikuwa mmeenda wapi"Alingea Shekhe karimu maneno ambayo yalinifanya nizidi kushangaa kabsa. Kwa kweli nilibaki nikimshangaa sana yule Ustadhi maana siyo muda nilikuwa nimemwambia aniambie kama alishwahi kuota ndoto ya mama yangu kama aliwahi kufa. Yeye alinijibu kuwa mama yangu ndio amekufa na wala siyo ndoto. Tena yeye ndio alinishangaa zaidi na kuniona mimi labda nimechanganyikiwa. Nilitamani kumziba kofi yule Ustadhi maana niliona kama ananikejeli vile lakini nilihisi siyo vizuri ngoja nimuache tu. Ilibidi nimuachie mdete na wote tuliongozana kwenye gari tukapanda na safari ya kumpeleka ustadhi kwao ilianza. Yani kwenye gari kila mmoja macho yalikuwa yameangalia mbele hakuna story yeyote ambayo ilikuwa inapigwa kama mwanzo wakati tunaenda kwenye ziwa kindai. Tulipomfikisha Ustadhi karimu tulimshusha mimi nikamuaga kwa shingo upande na kuondoka. "Kapopo rafiki yangu mimi nakuomba kama bado hujaamini kama mama yako ni mzima basi nakuomba amini kuwa amekufa. Naona sasa kuna kipindi unataka kuniua kabla muda wangu haujafika"Aliongea Mdete na cha ajabu hadi machozi yalianza kumtoka. Ile hali kwa kweli ilizidi kunishangaza sana kwani kitendo cha mdete kutokwa na machozi kilimanisha kuna kitu kibaya kimetokea. "Kapopo yule mtu ambaye ulikuwa unamuulizia Maswala ya kama aliwahi kuota kuwa mama yako alikufa hakuwa ustadhi karimu bali alikuwa ni mke wako Maimuna. Tulipofika pale ziwani kwa kweli mimi nilimuona maimuna akitokea ziwani huku akiwa amevaa nguo nyeupe zote. Alipofika pale aliposimama ustadhi nilishangaa yule ustadhi anapotea. Kwa kweli tena ulipokuwa unaongea na Maimuna alikuwa kwenye hali mbaya sana na alikuwa anatisha tangia nizaliwe sikuwahi kuona mtu au zombi ambalo lilikuwa linatisha kama Maimuna"Aliongea Mdete tena na kuanza kulia kabsa. "Kapopo mimi sitaki kufa tafadhari acha kupeleleza habari za mama yako amini tu kuwa yupo mzima. Kama utaendelea kupeleleza basi naomba usinishirikishe mimi"Aliongea mdete na kutulia wala hakuongea tena. Hata nilipojaribu kumpeleleza zaidi yeye alikuwa yupo kimya tu. Tulipofika karibu na dukani kwake Mdete aliniambia nimshushe. Sikutaka kubisha nilimshusha mdete nilitaka apumzike kwanza na mimi ningelikuja kupiga stori siku nyingine. Nilipomshusha Mdete moja kwa moja nilinyoosha hadi nyumbani kwangu. Nilipofika nyumbani kwangu nilikuta nyumba ipo wazi lakini kulikuwa na kimya cha ajabu sana. Nilimwita Mfanyakazi Adela lakini hata yeye hakuwepo. Ilibidi nilirudisha mlango wa sebureni na kuanza kwenda chumbani kwangu. Nilipofungua mlango wa chumbani kwa kweli nilishituka kidogo moyo utoke nilipomuona Maimuna akiwa amekaa kitandani huku akiwa anakula kama utumbo wa mtu. Nilipochunguza zaidi ndipo nilijikuta hadi nguvu zinaniishia nilipomuona baba yangu akiwa amelala kitandani huku tumbo lake likiwa kama limepasuliwa damu zinatoka na Utumbo wote ulikuwa nje.
Kwa kweli kitendo cha Kumkuta Maimuna akiwa kwenye hali ile huku baba yangu tumboni utumbo ukiwa nje kabsa nilipatwa na Mshituko ambae vigumu kukuelezea ukaniamini. "Hahaha hahaha hahaha naona wewe Unanichezea nimekwambia kuwa acha kufatilia mambo ambayo hayana umuhimu kwako lakini hutaki kunisikia. Hivi unapofuatilia kutaka kujua kama mama yako amekufa au laa unamaana gani. Hivi hukumbuki wakati tunafunga ndoa na mimi tulikubaliana kama mahari itakuwa mama yako. Sasa nini kinakuwasha hadi unaanza kupeleleza kama mama yako mzima au amekufa. Nimejaribu kukuonya lakini umeonekana Mgumu kuelewa sasa hiki unachokiona ndio zawadi yako kwako na ukiendelea kunifatilia hata wewe nitakutafuna"Aliongea maimuna kisha alipeleka Mkono kwenye tumbo la baba yangu na kutoka na utumbo akapeleka mdononi na kuanza kutafuna huku akicheka na damu zikitiririka mdomoni. Kwa kweli ile siku maimuna alikuwa anatisha mbaya maana hata macho yake tu yalikuwa mekunda kama kizinga cha moto. Ile hali ya Maimuna kuchukua utumbo wa baba yangu na kuanza kula huku akija sehemu ambayo nilikuwa nimekaa ndio ilifanya woga kuongeza hadi mikojo ilianza kunitoka kabsa. Kwa kweli nilishawahi kupatwa na mshituko wa kutisha hasa kipindi mara ya kwanza kujikuta nimelala juu ya mbuyu lakini mshituko ambaye niliupata nilipomuona maimuna anakuja kwangu ulikuwa hauelezeki. Hata maimuna aliposhuka Kitandani na kuanza kutembea chini kulikuwa kunatikisika kama mtu alikuwa anagonga nyundo kubwa chini. Kwa kweli nilikuwa natetemeka sana hata nguvu za kuongea kumuomba Maimuna msamaha nilikuwa sina kabsa. Pale kitandani hadi chini kulikuwa kumetapakaa damu ya baba yangu. Nilitamani sana kufungua Mdomo wangu na kumwambia Maimuna anisamehe sitarudia tena lakini kwa jinsi ambavyo nilikuwa nimeogopa hata kunyanyua Mdomo nilishindwa. Maimuna alitembea hadi alinifikia kisha alinishika kwa mkono mmoja tu na kuninyanyua juu. "Hahahaha hahaha nasema nakumeza leo umenichosha nakumezaaaaaaaaaa"Aliongea Maimuna kwa sauti kali na yenye kutisha kisha taratibu alinishusha kidogo na kufiki saizi ya mdomo wake kisha alipanua mdomo wake na kuanza kuniingiza. Kwa kweli kwenye ule mdomo wa Maimuna ulikuwa unatisha maana ulikuwa na meno manne mawili juu na mawili chini yalikuwa marefu na yakutisha sana. Nilipiga kelele huku nasema hapana Maimuna usifanye hivyo lakini taratibu nilishangaa kichwa changu kikiingia kwenye mdomo wa maimuna. Kilipoingia kichwa changu kwenye mdomo wa maimuna usingizi wa ajabu sana ulinipitia na sikujua kile ambacho kilikuwa kimeendelea....................CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/.......................................................................................................Nilipokuja kushituka nilijikuta nimelala kitandani kwangu. Ile hali kwa kweli ilishangaza na kutikisika huku kikifikicha macho. Nilikuwa natikisikika ili kuhakikisha kweli nilikuwa nimelala kitandani au tumboni kwa maimuna maana nilikuwa nakumbuka mara ya mwisho maimuna alikuwa ananimeza sasa iweje niwe kitandani . Hata nilipojitikisa nilijikuta bado nimelala kitandani kwangu. Wakati nikiwa nashangaa ile hali mara nilisikia kama sauti ya Maimuna akiwa anacheka mlangoni. Kile kicheko kilikuwa cha kawaida sana na alionekana kama mtu ambaye alikuwa na furaha sana. Baada ya kusikia kicheko cha Maimuna ndipo na kumbukumbu kama nilimkuta baba yangu tumbo likiwa wazi na utumbo unatoka ilinijia kichwani mwangu. Nilikumbuka hata kipindi maimuna alipokuwa anakula Utumbo wa baba yangu. Nilipokumbuka vile niliamka huku nikiwa napiga kelele za kutaja jina la baba yangu. Kitu kingine ambacho kilizidi kunichanganya pale ndani kipindi baba yangu akiwa amelala kitandani damu zilikuwa zimetapakaa chini ila muda ule kulikuwa hakuna damu hata robo. Niliamua kutoka chumbani kwangu huku nikiwa nimechanganyikiwa na kutaja jina la baba yangu. Kwa jinsi nilivyokuwa nimechanganyikiwa baba yangu nilikuwa namwangalia hadi mifukoni utafikilia nilikuwa nimemtumbukiza kwenye mifuko yangu ya suruali. Nilipofika Sebureni kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa nilipomuona Baba yangu mzazi wakiwa na Maimuna pamoja na baba yake na maimuna wapo sebureni wamekaa wanapiga story na kucheka kweli.
********************************************************************************************** Kwa kweli ile hali ya kumuona baba yangu akiwa na Maimuna alafu na baba yake na Maimuna akicheka tu bila shida kile kitendo kilinishangaza sana. Cha ajabu wao ilionekana hata ile Sauti ambayo nilikuwa napiga ya kumuita walikuwa hawajasikia maana walionekana hawana habari kabsa. Niliondoka kwa kasi kuelekea sehemu ambayo alikuwepo mzee wangu "Baba hebu niambie kweli ni mzima, niambie basi kweli ni mzima au umekufa na hapa ulipo ni mzimu"Niliongea baada ya kumfikia baba yangu na kuanza kumpapasa kabsa ili kuhakikisha kama kweli yule alikuwa ni baba yangu na wala siyo mzimu wa baba yangu. Nilipoweza kumpapasa ndipo niligundua kama yule alikuwa ni baba yangu kwani kama angelikuwa ni mzimu kamwe nisingweza kumshika. Sasa nilibaki nikitafakari na yule ambaye alikuwa amelala kitandani alikuwa ni nani mbona utumbo wake ulikuwa umetoka kitandani. "Ndoto hii mbaya sana ambae anaota mwanae ila mwache tu hivyo hata akitoka nje wewe muache. Alafu maimuna naomba usirudie kumfanyia hivi mume wako. Maana amelala chali umemuacha tu wakati mida ya saa kumi siyo vizuri mtu kulala chali"Aliongea baba yake na Maimuna. Kwanza baba yake na Maimuna naye alizidi kunishangaza alijuaje kama mimi nilikuwa nimelala chali. Alafu pili alikuwa anaongea uongo. "Kapopo yule mtu ambaye ulikuwa unamuuliza maswali kama alishawi kuota ndoto kama mama yako amekufa hakuwa karimu kama ulivyokuwa unadhani wewe bali alikuwa ni mke wako maimuna. Tulipofika pale ziwani kwa kweli mimi nilimuona maimuna akitokezea ziwani huku akiwa amevaa nguo nyeupe zote. Alipofika kwa ustadhi karimu cha ajabu ustadhi karimu yeye alipotea"Nilikumbuka moja ya maneno ambayo aliniambia rafiki yangu mdete nilizidi kuchanganyikiwa. Nilihisi huenda yule ambaye nilikuwa namuona baba yangu utumbo umemtoka alikuwa amebadilishwa tu kumbe alikuwa mdete ndio alikuwa analiwa. Maana nakumbuka siku mdete aliponiambia kuwa yeye anajua kuwa mama yangu mzima maimuna aliniambia kuwa Mdete amemsaliti hivyo lazima atamuua. " Kapopo rafiki yangu kama bado hujaamini kama mama yako atakuwa bado ni mzima basi nakuomba amini amekufa. Naona sasa kuna wakati unataka kuniua kabla ya muda wangu"Nilikumbuka pia Maneno ya rafiki yangu ambayo alikuwa anaongea huku akiwa analia na kuanza kuamini huenda lile tukio ambalo nilikuwa naona Maimuna amemfanyia baba yangu alikuwa anafanyiwa rafiki yangu. Nilichofanya nilitoka nduki kufuata mlango wa kutoka nje. Baba yangu alipotaka kunishika aliambiwa aniache kwani nilikuwa naota ndoto kali sana hivyo angenishika lazima ningekufa. Sikutaka kushangaa sana yale maneno ya baba yake na Maimuna nilichomoka nduki na kutoka nje. Nilipotoka nje nilitafuta boda boda na kumwambia Anipeleke sokoni singida kwani ndio maeneo mdete alipokuwa anafanyia kazi. Tena nilimwambia akimbize pikipiki kwa kasi sana. Kile ambacho nilimwambia dreva boda boda ndicho ambacho alikifanya kwani ndani ya dakika tano tayari nilikuwa kwenye duka la Mdete. Nilipofika kwa Mdete nako nilibaki nikiwa nashangaa nilipomkuta mdete akiwepo dukani kwake huku akihudumia wateja bila shida yeyote
Kwa kweli kitendo cha kumkuta Mdete Mzima ndo kwanza anawahudumia wateja dukani kiliniacha mdomo wazi. Niliwaza sasa yule alikuwa nani ambaye alikuwa anatafunwa utumbo na maimuna lakini sikupata jibu. Muda huo na Mdete alikuwa ameshaniona kuwa nipo nje ndukani kwake hivyo alitoka na kuja kunisikiliza. "Kapopo kwa kweli leo mimi siwezi kuongea sana na wewe naomba nenda yumbani kapumzike alafu ndio tafuta siku uje tuongee vizuri. Tena tuzungumzie mambo mengine na wala siyo jambo linalohusu kuwepo au kutokuwepo kwa mama yako"Aliongea mdete. Kwa kweli nilibaki namshangaa tu Mdete kwani yeye hakujua kama nimekuja na neno zito kuliko hata alivyokuwa anafikilia. "Mdete siyo kwamba nimekuja kwa ajili ya kuja kuongelea habari za mama yangu. Wala sijaja kuja kuongelea kitu chohote kuhusu yale ambayo yalitokea . Pia kuanzia sasa sitaki kabsa kuongelea mambo yanayomuhusu mama yangu. Awe mzima awe amekufa hiyo anjua mungu"Nilimwambia mdete maneno ambayo yalimfanya kunishangaa kidogo. "Sasa kitu gani ambacho kimekufanya hadi urudi kwangu wakati siyo muda tulikuwa wote"aliongea Mdete huku akinishangaa. Bila shaka nilibaini kuwa Mdete alikuwa na hamu sana yakuta kujua kitu ambacho kilinifanya kurudi kwake punde vile. "Hivi mdete inamaana sasa hivi hata kuonana na wewe tutakuwa tunaenda kila tiba. Kama tukionana mara moja inatosha hutaki tuonane tena. Hivi umeshasau kama Mwanzo nilikuwa nashinda kwako karibia hata siku nzima na kuna siku wewe ulikuwa unalala hadi kwetu. Basi hata hivyo siyo mbaya nilikuwa nimekuja kukuona maana nilikuwa na wasiwasi huenda utakuwa umekufa"Nilimwambia haya Maneno na kuanza kuondoka. Yale maneno kwa kweli yalimchanganya sana mdete na kuamua kunifuata. Wakati mdete akiwa ananifuata na kuniambia tukakae sehemu tuzungumze kidogo simu yangu ilianza kuita. Nilipoangalia simu yangu nilishangaa kuonaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ustadhi Karimu alikuwa ananipigia. Nilifikilia kwa Muda kama wa sekunde kumi hivi kisha niliamua kupokea tu ile simu. Nilibonyeza kitufe cha kijani kisha niliweka sikioni kusikiliza Shekhe karimu alikuwa na neno gani la kuniambia "Kwa kweli vijana wangu mimi sijafurahishwa na kitendo ambacho mlinionyesha. Hivi mlikuja kunipima imani na kujaribishia uchawi wenu wa mafanikio kwangu. Hata hivyo nawapa taarifa kuwa mimi hamniwezi natembea na mungu kamwe hamuwezi. Haiwezekani mnipeleke ziwani kwenda kuniambia kitu alafu mnapotea kimazingira ya kutatanisha na mnatokea tena. Inamaa uchawi wenu wa mafanikio mnaujaribisha kwangu. Bila shaka mlikuwa mnataka kunitoa na mimi kafara ila mmeshindwa. Mimi mtu wa mungu bwana labda tafuteni walevi wenzenu muwaotee ila siyo mimi"Aliongea Ustadhi kwa sauti kali iliyojaa hasira na kukata simu. Yale maneno ya shekhe Karimu kwa kweli yaliniumiza. Kama kweli yale ambayo alikuwa anasema aliyaona alikuwa na haki ya kukasilika. Nilikumbuka hata wakati tumepanda kwenye gari kumrudishe huku tukiwa tumevimbiana kwa hasira huenda alihisi kuwa tulikasirika kwa kushindwe kumtoa kafala. "Umeona sasa Kapopo jinsi tunavyo haribu. Hii yote kwa ajili ya wewe kutokuniamini. Unafikilia kama shekhe mzima alituona sisi tukipotea unafikili atatuchukuliaje. Kama siyo mtu kutuhisi kama haya ambayo anayesema"Aliongea Mdete kwani alisikia wakati nikiwa naongea na Yule Ustadhi simu yangu nilikuwe nimeweka loud speaker. Muda ule kwa kweli lawama zote zilikuwa kwangu hata mdete alisahau kama yeye ndio ambae alinisisitiza hata kutafuta mtu ambae nilimuona kwenye msiba wa mama yangu nimuulize. "Siyo muda wa kulaumiana huu mdete, kinachotakiwa ni kuwaza ni namna gani tunaweza kuyabadilisha mawazo ya huyu ustadhi asitufikilie kama anavyowaza"Nilimwambia Mdete huku nikibonyeza vitufe kazaa vya simu yangu kumpigia tena Ustadhi. Hata nilipompigia Ustadhi simu aliishia kukata tu. Baada ya kujaribu kupiga namba ya ustadhi bila mafanikio tuliondoka na Mdete na kwenda hadi Singida motel kwa ajili ya kula na kumueleza swala la kumkuta mzee wangu akiwa utumbo wazi. Tulipofika pale singida Motel tuliagiza mtori wa ndizi na nyama na kuanza kula huku tukipiga stori za hapa na pale. Tulipomaliza kula ndipo nilimuelezea Mdete kuanzia Mwanzo hadi mwisho hata sababu ya kuja kwake tena. Kwa kweli mdete alishangaa sana. Baada ya kushauriana mambo mengi ikiwepo kuacha kupeleleza kuhusu kama mama yangu amekufa au mzima tulienda hadi dukani kwa mdete na kuchukua gari yake tukaanza kwenda nyumbani. "Yani haya ndio mafanikio kutoka kwako na kwa shemeji yangu Maimuna. Kwani hata hili gari limetokana na pesa zenu ambazo mlinipa unajua kap..."Aliongea Mdete hata kabla ya kumalizia tulisikia kicheko kikali sana nyuma ya gari yetu. Nilipogeuka kuangalia nilishangaa kumuona Maimuna akiwa amekaa yuma ya gari. Kwa kweli kitendo cha mtu kucheka kwenye gari yetu alafu nilipogeuka nikakuta Maimuna akiwa Amekaa kwenye gari ile siti za nyuma kilinishangaza kweli. Maimuna mimi nilikuwa nimemuacha nyumbani na wazazi wangu sasa iweje muda ule yupo kwenye gari. Haadi hapo kwa kweli niliamini kumbe popote ninapoenda huenda natembea na Maimuna bila kujua. "Kapopo vipi mbona unageuka geuka nyuma kwenye gari au maimuna yupo humu nini. Maana huyo bwana hatabirika kama mvua ya kiangazi. Maana unaweza ukawa unaongea nae bila kujua kama yeye. Mfano pale nakwambia ulikazania kumuuliza Ustadhi karimu kumbe unamuuliza Maimuna"Aliongea Mdete huku akigeuka kwenye siti za nyuma. Cha ajabu kumbe mdete yeye hakusikia kile kicheko hata alipogeuka nyuma maimuna alikuwepo na mdete hakumuona. Hadi hapo niliamini nahitaji kazi kubwa sana kuweza kuishi na mwanamke wa kijini. Kama kila sehemu unayeenda na kila ambalo unaliongea analisikia basi ilikuwa haina siri. "Acha kumtania Mke wangu bwana mimi nampenda hivyo hivyo jinsi alivyo, so wewe kama shemeji yako unatakiwa umzoee na kumpenda"Nilimwambia Mdete kwa kujikaza ila asione dalili yeyote. "Mbona mimi nampenda sana maimuna, yani katika mashemeji wangu waukweli kwenye hii dunia Maimuna ndio kiboko yao. Yani mimi nampenda vile vile ingawa najua kuwa ni mtu hatari. Wewe huoni hata hapa nachezesha mguu mbala nashika break mara crach hii yote kwa ajili ya shemeji yangu Maimuna tena ngoja niongee kwa sauti ili Asikie huenda akwa around maana yeye anauwezo hata wa kupaaa. Maimuna Nakupenda shemeji yanguuuuuuuuuuuu"Aliongea Mdete kwa sauti ya juu na kucheka. Yale maneno ya mdete yalimfanya hadi maimuna kuanza kucheka. Nilipomuona Maimuna akiwa anacheka angalau kidogo pressure yangu ilianza kushuka na kuanza kusikia kawaida. "Kapopo nakuomba ukifika nyumbani fanya kama baba yangu atakavyokwambia ila baba yako ajue kama kweli ulikuwa unaota"Aliongea Maimuna kisha alipotea ghafla kwenye gari. Kile kitendo cha Maimuna kupotea ghafla mimi wala sikushituka kwani nilishazoe sana. Tuliendelea na safari huku mdete akipiga Story za hapa na pale na kunikumbusha hadi mambo ya shuleni. "Unajua mdete wakati unaongea mambo ya Maimuna sijui unampenda shemeji yako na yeye alikuwepo nyuma. Tena pale ulipoongea shemeji nakupenda kwa sauti ulimfanya hadi yeye amecheka"Nilimwambia Mdete na yeye kubaki akiwa anashangaa tu. "Ndio maana nakwambia ili kuishi vizuri na shemeji yetu tunatakiwa kufanya mambo ambayo ni mazuri na yanampenezesha yeye. Unajua kama umeshagundua maimuna popote unapoenda inawezekana yupo fanya mambo mazuri. Inawezekana hata unapoenda chooni kunya unafatiliwa na Maimuna hii hatari"Aliniambia rafiki yangu kisha wote tulicheka. Muda huo tayari tulifika hadi nyumbani. Nilichofanya nilimwambia mdete asiingie kwanza ndani niingie mwenyewe kwanza si mzee wangu anajua kama nilikuwa naota. Taratibu niliingia hadi sebureni huku nikiwa kama nashangaa hivi. "Hapo sasa bado anaota ila unaweza kumuita na asipate matatizo yeyote"Nilimsikia Baba yake na Maimuna kuongea tena vile. Kweli mzee wangu nilimuona akiniita na mimi nilijifanya kama nashituka na kuitika kisha kuanza kushangaa. "Jamani nimefikaje hapa mbona kama nilikuwa nimelala kitandani"Niliongea yale maneno na kujifanya kama nashangaa ili kumthibitishia baba yangu kuamini kama kweli nilikuwa naota. "Mwanangu ulikuwa unaota hivyo kawaida sana upo sehemu salama. Tena uzuri upo na wajuzi wa ndoto ingekuwa mimi ningekurupua na kukusababishia hatari kabsa"Aliniambia mzee wangu. Baada ya kuniambia hivyo mzee tulikaa huku mimi nikianza kulaumu ndoto mbaya hizi. Baadae mzee wangu Aliondoka pale nyumbani pamoja na baba yake na Maimuna tulibaki wawili na Maimuna. "Baby mbona nilikuta Baba yangu utumbo wake ukiwa nje na wewe ukiwa unakula iweje sasa awe mzima"Nilimuulizia CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Maimuna kwani hilo ndio swali ambalo nilikuwa naliwaza sana. Maimuna aliposikia lile swali yeye alianza tu kucheka na kuniambia mbona yeye alikuwa anakula tambi tu wala hakuwa anakula utumbo wa baba yangu. "Unajua sisi Kapopo ni watu ambae tunauwezo wa juu sana kufanya chochote ambacho kitakuwa kwenye hisia zangu wewe kukiona cha kweli. Mfano nikiwaza kama nataka huyu binadamu akija hapa anione nipo kama mbuzi kweli akija ananiona kama mbuzi. Yani hisia yeyote nikiwaza kwa mtu flani iwe hivyo inauwezo wa kutokea hivyo. Hata wewe uliponiuzi kule ili kukufundisha nizamu niliwaza kapopo akija kuniona nataka anione nikiwa natisha huku baba yake akiwa tumbo wazi na yeye akiniona aone kama nakula utumbo wa baba yake. Kweli ulipofika ndicho ulichokiona ingawa kilikuwa hakina ukweli wowote ule. Mimi siwezi kumua baba yako bwana kwani mimi siyo baba yangu"Aliongea Maimuna na kuja kunikumbatia. Ile hali kwa kweli ilinifanya kufurahi zaidi. Maisha yaliendelea pale singida huku tukizidi kuwa tajiri waliojulikana sana. Hadi tunamaliza miezi minne tangia Turudi Saud arabia kila Mtu alikuwa na gari yake mpya tulikuwa hatutumii tena gari ambayo baba yake na Maimuna alitununulia. Muda ule mapenzi yangu na Maimuna yalizidi kumea kwani nilishafahamu kuwa naisha na jini hivyo nilikuwa nafanya vitu vizuri tu. Muda ule habari ya kupeleleza mama yangu amekufa au laaa niliacha kabsa. Wanawake wengi waliokuwa wanajileta kwangu na kunitongoza wenyewe lakini niliwakataa. Wapo waliniganda wao waliishiwa kuchapwa vibao na maimuna kimazingara hadi waliponiona waliniogopa. Nakumbuka siku moja jioni Maimuna aliniita chumbani na kunifahamisha kitu ambacho kilinishitua sana. Kitu kile ilikuwa mdogo wake Yusira kuja Tanzania hususani Singida kuja kutusalimia. Tena mbaya zaidi Yusira alikuwa anakuja kufikia Kwetu. Ile hali kwa kweli ilinifanya kushituka. Nilichoamua ni kuunda safari na kumwambia Maimuna kuwa nahitaji kuondoka Tarehe flani kwenda kusalimia Mwanza. Nilitaja Tarehe ambayo yusira ndio angekuja singida. Nilipomwambia vile Maimuna alinikatalia na kuniambia lazima hadi shemeji yangu anikute akiondoka na mimi ndio naondoka. Tena Maimuna aliniambia kuwa Yusira alikuwa anatamani kuja kuniona. Kwa kweli sikuwa na jinsi niliamua kukubali ingawa nilijua itakuwa hatari. siku hiyo hiyo ambayo Yusira alikuwa anaondoka Saudi arabia tayari alinipigia Simu na kuniambia lengo kabsa la kuja singida ni kwa ajili yangu kwani ametokea kunimiss sana. Aliendelea kusema kuwa penzi ambalo nilikuwa nimempa alikuwa anataka nimpe zaidi kwani najua kuwatengeneza wanawake. Kwa kweli yale Maneno ya Yusira kwenye simu kusema kuwa alikuwa anakuja Tanzania kwa lengo la kuja kufanya mapenzi na mimi yalizidi kuniogopesha sana. Nilikumbuka Maneno ya Maimuna siku moja alishawahi kuniambia kuwa kama nitafanya mapenzi na Mwanamke yeyote yule nitageuka kuwa Mbwa ndio nilizidi kuchoka zaidi. Kwa dalili hiyo uwezekano sasa wa mimi kugeuka Mbwa ulikuwa Mkubwa sana. Nilitamani kutoroka na kwenda mbali kabsa maana sikutaka Kabsa yusira anikute nyumbani kwangu. Yusira kama angelikuwa wanawake wa kawaida na siyo jini ningebaki na ningeweza kumkabili. Lakini yeye ni jini hata ninapomkataa kuna nguvu huwa anazitumia na kunifanya nikubali kabsa. Nilichoamua kufanya ni kutoroka bila hata Kumuaga Maimuna. Kama Maimuna alishanizuia kuondoka kwa hiari basi nilipanga nitoroke tu hadi siku Yusira akiondoka ndio naondoka. Ilikuwa siku ya Juma pili ndio siku Yusira alikuwa anatoka Dar kuja Singida. Pale nyumbani yalikuwa yamefanywa maandalizi ya kufa mtu. Kwanza kuna sherehe ya sadaka ambae ingefanyikia kisiwa cha majini kama inshara ya kumkaribisha Yusira hilo mimi nilikuwa nalijua kwani taarifa alikuwa amenipa baba yake na Maimuna. Tayari mimi nilishaweka mambo yangu Safi kabsa kwa ajili ya kutoroka nyumbani. Nilipanga Maimuna angetoka tu kwenda sehemu yeyote ile na mimi ndio ningeanza safari yangu. Tulikaa pale nyumbani na Maimuna kutoka saa mbili Asubuhi hadi Saa tano bado Maimuna alikuwa hajatoka. Ile hali ilizidi kuniogopesha maana nilitaka Maimuna atoke ndio na mimi nipate Upenyo wa kusepa. Mungu nazani alisikia kilio changu kwani muda wa saa sita Maimuna aliniaga kuwa anatoka kwenda Super maketi. Hiyo ndio ilikuwa chance nzuri kwangu ya kuondoka. Nilipohakikisha Maimuna kapanda gari ndipo na mimi nilirudia begi yangu ya nguo ili niweze kuondoka. "Boss unaenda wapi mbona haraka hivi hata taarifa sina mbona kama unaondoka. Isitoshe kuna Mgeni anakuja hapa sasa inakuwaje unaondoka na mabegi. Pia hata dada Mai alipokuwa anatoka Amenimbia nipike haraka nikutengee chakula sasa inakuaje"Aliongea Mfanyakazi wangu Adela baada ya kuona nina begi. Nilichomwambia Adela kuwa natoka kimya kimya hata yeye anatakiwa kumwambia Maimuna kuwa hajui hata nilipoenda. Ila nilimwambia kuwa asiwe na wasiwasi nitarudi tena nyumbani. Adela hakuwa na kipingamizi tena kwangu aliniacha na mimi niliotoka ndani. Tayari nilikuwa nimempigia simu hata mtu wa Tax kuja kunichukua ili anipeleke stendi. Nilipotoka getini nilikuta tax tayari imeshafika hivyo nilipanda na safari ya kuelekea Stendi ilianza. "Boss unatakiwa uniongezee kidogo maana umeniweka sana. Unajua kuna deal zingine zilikuwa zinatokea nazipiga chini"Aliongea Dreva huku akiongeza kasi ya gari lake. Alichokiongea yule Dreba ilikuwa ni sahihi kabsa maana nilimwambia saa tatu ndio naondoka. Nilimwambia kuwa haina shida pesa nitamuongezea tu. Story za hapa na pale kwenye gari ziliendelea huku na safari ikizidi kusoga mbele. "Baby Utaondokaje bila kuniaga bwana. Alafu isitoshe nilisha kuzuia kusafiri hadi Yusira aje. Unajua sasa hivi unaanza kunitia wasiwasi kwa nini hutaki kuonana na mdogo wangu hadi unafikia hatua ya kutoroka"Ilikuwa sauti ya Mke wangu Maimuna ikisikika nyuma ya gari. Kwa kweli ile hali ilinishitua sana, hata nilipogeuka kweli nilimuona Maimuna akiwa ndani ya gari. Kwa kweli nilishindwa kumwambia nini maimuna na kubaki nikiwa nimechanganyikiwa sana. Yule dreva yeye alikuwa hajui hata maimuna alipokuwa anaongea yeye alikuwa hasikii kitu chochote kile. "Sasa wewe si utaki kumuona mdogo wangu, tutaondoka wote hadi stendi kisha tukaa tutamsubilia Yusira na tutampokea wote"Aliongea Maimuna maneno ambayo yalinifanya nibaki nikiwa nashangaa tu. Wakati nikiwa naendelea kushangaa pale nilimuona Maimuna ananisogelea na kuja kunifunika usoni. Aliponifunika tu usingizi mzito ulinipitia sikujua kilichokuwa kinaendelea. Nilipokuja kushituka nilibaki nikiwa nashangaa nilikuwa nipo kwenye gari ya Maimu stendi . Tena cha kushangaza Maimuna alikuwa amelala usingizi na gari ilikuwa imepakiwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kweli nilipojiona nipo kwenye gari ya maimuna huku mwenye gari yeye alikuwa anapiga tu usingizi nilibaki nikiwa nashangaa. Nilichokuwa nakumbuka mara ya mwisho tulikuwa kwenye tax na maimuna alikuja kunikumbatia usoni kisha usingizi ulinipitia. "Maimuna nimefikaje kwenye gari yako na yule kijana nani atakuwa amemlipa pesa yake. Mimi unajua nimeshakubali kumsubilia yusira, kwanza nilikuwa hata sitoroki ila nilikuwa nakupima je unauwezo wa kuniona kila ninapoenda. Sasa nataka uniambie yule kijana umemlipa pesa maana nilimpotezea muda"Nilimwambia Maimuna huku nikiwa namgeuzia ukweli niliokuwa nafanya kuwa uongo. Nilipoongea yale maneno maimuna yeye hakujibu kitu chochote. Alichofanya nakumbuka alinyanyua mkono wake akakunja ngumi kisha akaukunjua. Alipokunjua ule mkono wake nilishangaa kiganja chake cha mkono kilikuwa kinaongezeka ukubwa wake taratibu. Ile hali ilinishitua kidogo maana kiganja cha mkono wa Maimuna kiliongezeka ukubwa hadi vidole vikawa havionekana alafu kiganja kikawa cha mviringo kama Sinia la wali. Wakati lile tukio la kuongezeka mkono linafanyika cha ajabu yule ambae alikuwa anafanya lile tukio yeye alikuwa anapiga usingizi. Tena mbaya zaidi hadi alikuwa anakoroma hali iliyonifanya nizidi kushangaa. Niliendelea kuangalia kwenye kile kiganja cha mkono nini ilikuwa hatima yake. Kile Kiganja baada ya kuongezeka ukubwa wa kutosha nilishangaa kuanza kuona tukio la kwenye tax ya yule kijana. Tukio lilianzia pale maimuna aliponisogelea na kunifunika usoni na viganja vyake vya mkono. Kumbe baada ya maimuna kunifunika usoni aliniachia tena. Aliponiachia cha ajabu tuliendelea kupiga story za kawaida na yule Dreva hadi alinifikisha stendi nikashuka na kumkabidhi pesa yake. Ile hali kwa kweli mimi ilizidi kunishangaza maana mimi nilichokuwa nakijua baada ya Maimuna kunikumbatia sikujua kitu chochote ambacho kiliendelea. Baada ya kuona lile tukio la kumkabidhi kijana pesa yake baadae tuliondoka na Maimuna hadi sehemu flani tulikaa hadi mfanyakazi wa duka letu alipoleta gari ya maimuna kisha nilipanda nikiwa na Maimuna na kutuli kwenye gari. "Hadi hapo unaswali baby wewe subilia tu tumsubili Yusira huwezi kuondoka hapa wangu. Yani unapanga Safari za ghafla tu bila hata kuagana bhana"Aliongea Maimuna huku akiwa amefumba macho yake kama amelal hivi. Tena maneno ambayo aliongea maimuna yalikuwa mengi sana ila mdomo wake kufunguka kutamka maneno ulifunguka mara mbili tu. Kwa kweli hadi hapo nilikuwa sina jinsi niliamua kukubali matokeo tu na kuamini jini siyo kitu cha mchezo. Baada ya tukio zima kuonekana mkono wa maimuna ulianza kupungua kidogo kidogo ukubwa hatimae ukawa wa kawaida tu. ................................................................... Kwa kweli niliamua kutulia tu kubisa sikutaka hata kuuliza swali tena ilikuwaje hadi nilifanya yale matukio bila kujielewa maana nilikuwa najua kama yale yote yamefanyika kijini zaidi. Tulikaa pale stendi muda ule ilikuwa kama saa nane hivi hadi saa tisa ndipo Maimuna aliamka na bado Yusira alikuwa hajafika. Ndani ya gari tukawa tunapiga story za hapa na pale na maimuna. Kwa jinsi maimuna alivyokuwa mzuri kwa kweli hata kupiga nae story ilikuwa raha. Wakati tukiwa tupo pale tunapiga story mara maimuna alifungua mlango wa gari kwa kasi ya ajabu na kutoka nje. Ilibidi nimfuate maana alitoka ghafla sana. Nilipomfuata chini nilikuta Maimuna akiwa anatapika. Ila yale matapishi yake yalinishitua sana. Matapishi ambayo alikuwa anatapika maimuna yalikuwa mabonge mabonge ya damu kitu ambacho kilinifanya kushituka sana. "Baby vipi unatatizo gani, itabidi tuende hospitalini mara moja. Kama Yusira atakuja kupokelewa hata narafiki yangu mdete"Nilimwambia Maimuna baada ya kumaliza kutapika. "Wala usiwe na wasiwasi baby wangu, hii hali ni hali ya kawaida sana. Labda ngoja tu nikwambie kitu huenda ulikuwa hujui mimi nina mimba yako. Kwa kawaida majini tunatofautiana sana na binadamu pindi tunapobeba mimba. Sisi majini tukibeba mimba huwa tunatapika damu lakini binadamu huwa hatapiki damu. Hivyo hapa naomba wala usiwaze maana ni kitu cha kawaida sana"Aliongea Maimuna maneno ambayo yalinishitua sana.
********** Kwa kweli yale maneno ya maimuna yaliniacha nikiwa nimepigwa na butwaa. Kwanza nilikuwa nimefurahi sana kusikia kuwa maimuna alikuwa na mimba yangu. Pili upande mwingine nilikuwa nawaza je huyu mtoto ambae atazaliwa atakuwa binadamu wa kawaida au na yeye atakuwa jini kama mama yake. "Baby sijui nikupe zawadi gani, hebu chagua unataka nikupatie zawadi gani kama shukrani ya kuwa na mimba yangu. Naona kilio changu cha kuitwa baba kinaenda kukatika sasa. Alafu baby nahitaji kujua huyu mtoto ambae atazaliwa atakuwa binadamu wa kawaida kama mimi au atakuwa jini"Nilimwambia Maimuna huku nikiwa namsogelea na kwenda kumkumbatia kabsa sikujali hata kama muda ule ule alikuwa Ametoka kutapika mabonge ya damu. "Baby zawadi ambayo mimi nataka unipe ni wewe kunipenda tu milele hadi tuzeke pamoja. Mtoto ambae atazaliwa asilimia kubwa huwa binadamu wa kawaida. Ila ili azaliwe kuwa binadamu wa kawaida unatakiwa kufanya mambo ambayo yatamfurahisha huyo mtoto na kuyaiga. Ila sisi Majini mtu akiwa anafanya matendo mabaya na muda wote kuwa na huzuni mtoto ambae huzaliwa huwa jini. Tena tendo baya ambalo linafanya mtoto ambae atazaliwa kuwa jini ni wewe mwanaume ukiwa binadamu mke wako jini akapata mimba alafu wewe ukafanya mapenzi na mtu mwingine. Hivyo Mume wangu kama unataka Mtoto wako kuwa binadamu wa kawaida fanya mambo yalio mazuri ya kumpendezesha mtoto" Alinijibu maimuna. Kwa kweli yale maneno ambayo aliongea maimuna yalikuwa ya kawaida sana kwangu kuweza kuyatimiza. Neno ambalo lilikuwa gumu kwangu ni kutokufanya mapenzi nje. Nilikuwa najua kitendo cha Yusira kuja hicho kitu lazima kitatokea tu. Kwa kweli moyoni nilianza kulaumu ujio wa Yusira Tanzania maana umekuwa wa Mkosi huenda angefanya hata mwanangu kuwa jini. Hata hivyo sikutaka kukata tamaa niliamua kuja kupambana vilivyo na Yusira. Kwanza nilipanga sitampa nafasi yusira ya kukaa karibu nae. Pia ili kumuweza Yusira nilipanga Akija Muda wote mimi nitakuwa natembea na Maimuna tu. Hata kama Maimuna atatoka may be kwenda hata kichen party na mimi ningemfuata huko huko. Maana kukaa karibu na Yusira nilijua lazima kungekuwa na hatari. Nilimshika maimuna kiunoni taratibu na kuanza kutembea kurudi tena kwenye gari. Muda huo maimuna kwangu aligeuka kuwa Yai ghafla na nilikuwa namchunga mbaya. Maana tulimaliza kama mwaka hivi bado maimuna alikuwa hajapata mtoto. Tulipofika kwenye gari tulipanda na kuendelea kupiga story. Muda ule asilimia kubwa ya story yetu ilikuwa juu ya mtoto ambaye alikuwepo tumboni. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Muda wa saa kumi kamili ndio Basi Aina ya ABC ambaye alipanda Yusira iliingia. Abc kwa mimi ambaye naifahamu ni moja ya Gari za kifahari sana kwa Tanzania nzima. Hata wewe siku ukiwa unasafiri kutoka dar kuja Singida Jaribu kupanda hiyo basi. Baada ya Basi kwenda kupaki na sisi tayari tulikuwa tumeshuka kutoka kwenye gari yetu kwenda kumpokea Yusira. Tulipofika pale na Yusira aliponiona nilishangaa akinikimbilia na kuja kunikumbatia kisha alinipiga busu tano mfululizo tena Mdomoni hadi Maimuna alibaki akiwa anashangaa. Kwa kweli ile hali ilinifanya nibaki nikiwa nimechanganyikiwa maana zilikuwa siyo busu za kawaida kabsa. Mtu Shemeji yangu kuja kunipiga busu Mdomoni tena hadi aliacha vimate mate ilikuwa siyo kitu cha kawaida kabsa. "Wewe Yusira tabia gani hiyo ya kumpiga mume wangu busu namna hiyo tena na mimi nipo hapa hapa. Hata kama ni shemeji yako ndio umpige busu mdomoni kwake inamaana hujaona sehemu yeyote ya kumpiga busu zaidi ya Mdomoni. Kwa kweli hicho kitendo sijakifurahia kabsa"Aliongea Maimuna huku akiwa amekasirika kidogo. Yale maneno ambayo aliongea Maimuna upande Mwingine yalikuwa na ukweli maana ilikuwa siyo kitu kizuri kabsa kufanya lile tendo ambalo alifanya Yusira tena mbele ya mke wangu Maimuna. "Basi dada nisamehe unajua nina mzuka Mwingi sana maana kitambo sijawahi kumuona shemeji yangu. Alafu na nyie ubahiri wenu unazidi hata kunipigia simu kunisalimia hamtaki ndio maana tunawamisi hadi tunawapiga Busu Sehemu ambazo hazifai"Aliongea Yusira hali iliyomfanya Maimuna kutabasamu. Alipotabasamu Maimuna ilionyesha kama yupo sawa. Tulichukua mizigo ya Yusira kisha tuliondoka kuelekea ndani ya gari. Tulipofika kwenye gari maimuna alikaa mbele mimi na Yusira tulikaa nyuma. Sikutaka kukaa nyuma kabsa na yusira ila sema Maimuna aliponiambia nikae nyuma na shemeji yangu ndio niliamua kukaa naye. Wakati tukiwa tunaendelea na safari ya kuelekea nyumbani nilishangaa kuona yusira akileta mkono wake na kuanza kunibonyeza bonyeza kwenye mapaja yangu.
******** Kwa kweli kitendo cha Yusira kuanza kunibonyeza bonyeza kwenye mapaja yangu kama kipofu anatafuta fimbo yake imeanguka chini kilinifanya nishituke sana. Licha ya kushituka pia Msisimko mkali wa mapenzi ulinijia. Kwa kweli nilishindwa kuelewa hii hali inasababishwa na nini. Maana ninachokifahamu mimi kama mtu hauna Mzuka na Mwanamke flani mashine kusimama haiwezekani. Yusira mimi muda ule nilikuwa sina mzuka naye kabsa. Maana nilijua kama nitakuwa na ukaribu naye lazima ningefanya mapenzi na yeye na hatimae kugeuka mbwa kitu ambacho nilikuwa Sipendi kabsa kinitokee. Nilichofanya nilipeleka mkono wangu na kuutoa mkono wa Yusira kwenye pamaja yangu bila kuongea wala bila kumwangalia. Nilipotoa ule mkono wala hazikupita hata dakika mbili mkono wake tena ulianza kunipapasa. Ingawa nilikuwa nasikia raha ya ajabu pamoja na mashine yangu kusimama lakini moyoni nilikuwa nimechukia vibaya kile kitendo. Kwa kweli nilipanga kumwambia Yusira kwa sauti kabsa ili hata Maimuna akisikia basi nimueleze tu ukweli wote. Maana niligundua kama ningeendelea kukaa kimya ipo siku hili Jambo litakuja kunitokea puani. "Yusira mimi mchezo wako wa kunishika mapaja sitaki. Hivi hujui kama mimi ni shemeji yako jamani. Tabia gani sasa hii kwa kweli mimi nimechoka Maimuna hebu mwambie mdogo wako bwana ajiheshimu"Niliongea Kwa sauti lengo Maimuna Asikie ndio nipasuke yote. Yani nilipanga kuyatapika yote hata lengo la Yusira kuja huku. Pia nilipanga kimwambia Maimuna hata kipindi natoroka nilikuwa natoroka kwa ajili ya kumkwepa Yusira kwani alikuwa ananitaka kimapenzi. Nilipoongea yale maneno kwa sauti cha ajabu Maimuna wala hakugeuka hali iliyonifanya kuhisi huenda hajasikia. Bado Yusira alikuwa anaendelea kunipapasa kwenye mapaja yangu. Nilirudia tena kuongea kwa sauti ya juu sana hadi watu ambae walikuwepo nje ya gari wanatembea walisikia na kuanza kucheka. Wengine walimwambia Yusira aache kufanya hivyo. Lakini licha ya kuongea kwa sauti kubwa kama ile bado Maimuna alikuwa hajanisikia. Nilipomwangalia Yusira cha ajabu yeye nilimkuta akiwa anacheka tu. Ile hali kwa kweli ilizidi kunichanganya sana,nilishindwa kuelewa kwa nini maimuna alikuwa hanisikii kile ambacho nilikuwa nakiongea. Upande Mwingine nilihisi huenda Maimuna ananisikia ila anafanya kusudi tu. "Kapopo bwana kwa kweli unanichekesha sana, hivi unafikili mimi hadi kukufuata huku kimapenzi tena tunaenda kufanya ndani ya nyumba yenu na maimuna unafikilia mimi mpumbavu. Kuna vitu vingi sana namzidi Mkubwa wangu Maimuna. Kuna nguvu nyingi sana ninazo ambazo naweza kumcontrol Maimuna na kushindwa kuona chochote. Hata unapoongea Kuna nguvu Inaitwa NYAMSALE nimeitumia ambayo imemfanya maimuna kutokusikia kitu chochote. Hivyo wewe unatakiwa kutulia tu mimi nifanye yangu. Unajua sisi majini Mtoto wa Mwisho kuzaliwa ndio huwa anapewa nguvu kubwa kuliko watoto wote. Huyo ndio ambae hata Urithi huwagawia watoto wengine kama wazazi wao watakufa. Hivyo mimi kwenye familia yetu ndio Mwenye Nguvu kuliko ndugu zangu wote"Aliongea Yusira na kunifanya nizidi kumshangaa. Upande Mwingine nilianza kuamini yale maneno ya Yusira maana kweli Maimuna yeye alikuwa anaendesha tu gari wala hakunisikia kipindi napiga kelele za kulalamika Yusira ananibonyeza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ "Hata kama umemzidi nguvu siyo uanze kumfanyia hivyo dada yako. Kumbuka kuwa mimi ni shemeji yako na nimemuoa dada yako sasa kwa nini unafanya hivyo. Kwanini usitafute Mwanaume mwingine akuoe. Nachokuomba acha kupeleka mikono kwenye mapaja yangu la sivyo nitajiua kabsa maana mnanichosha"Nilimwambia Yusira kwa hasira kidogo. "Mapaja yako naacha kuyashika ila tambua Utamu lazima utanipa tu tena kwa tani yangu"Aliongea Yusira na kutoa Mikono kwenye mapaja yangu. Kwa kweli Muda ule nilitokea kumchukia sana yusira na kuwaza bora Ningeshamueleza Maimuna kabla ya Yusira kuja huenda angeniruhusu na kwenda mbali kabsa. "Baby mbona mmekaaa kimya hivi Na Shemeji yako inamaa hata story za kupiga mmeishiwa"Aliongea Maimuna huku akigeuka kutuangalia. Kwa kweli Yale Maneno ya Maimuna ndio yalizidi kunishangaza zaidi maana tulikuwa tunapiga mikelele ya kumwambia Yusira atoe mikono kwenye mapaja yeye ndo kwanza anatuambia kuwa tupo kimya. "Baby mbona mimi nilikuwa nakusemesha hata hukunisikia"Nilimwambia Maimuna. "Acha utani bwana umenisemesha wapi bwana. Inamaana baby sasa hivi umeniona sina masikio kabsa nisikusikie kama unanisemesha"Alinijibu Maimuna kisha kuniangalia na kutabasamu. Lile tabasamu la mpenzi wangu Maimuna kwa kweli lilinifanya nijisikie raha sana. Sikuwa na jinsi niligundua kweli Mke wangu NYAMSALE ilishafanya kazi kama Yusira alivyoniambia.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment