Search This Blog

KIBUYU CHA BABU - 2

 







    Simulizi : Kibuyu Cha Babu

    Sehemu Ya Pili (2)





    baada ya yule mwalimu wetu kumuweka yule mtoto mchanga ndani ya kinu...alichukuwa mwichi...eeeeh nilipoona hivyo nilisimama haraka huku mapigo yangu ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu....ghafla nikaona anatwanga ndani ya kinu kile...nilipoona hivyo nilitimua mbio kurudi nyumbani.....ingawa kulikuwa na giza nene lakini nilikimbia pasipo kujikwaa wala kuanguka....nilikimbia kwa kasi sana na nilipokaribia maeneo ya nyumbani nilipunguza mwendo kisha nikaanza kutembea",, CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwa mbali nilimuona babu akiwa peke yake alikuwa amekaa chini"",, palepale nilipomuona kakaa jana...huku moto unawaka....nilipotazama kwa mbele yake kulikuwa na kibuyu kile cheusi.....niliogopa sana nikaanza kuzipiga hatua za harakaharaka....nilipoanza kuingia kwenye kiwanja cha nyumnani kwetu..nilisita kutembea nikachchumaa huku nikitazama ule upande aliokaa babu..ghafla niliwaona watu wawili wakitokea angani wamevalia kaniki nyekundu huku wapo juu ya ungo...kisha wakatua chini...

    kitendo kile kilinifanya niogope kiasi ambacho haja kubwa ilinitoka...pia nikashusha vijampo vya mfululizo......uwoga ulitanda juu yangu nilikuwa nikisimuliwa kuhusi wachawi wakipaa na ungo usiku nilikuwa siamini lakini leo nimeshuhudia kwa macho yangu....nilijikaza nisipige kelele...niliendelea kukodoa macho mara ghafla waliomgezeka watu wawili wengine...wakitokea angani wakiwa juu ya ungo kisha wakatuwa chini watu wale walikuwa wamejipaka unga mweupe kwenye nyuso zao hivyo sikuweza kuzitambua sura zao...ghafla babu alitoweka...sikuona alipoelekea kwa sababu kilikuwa ni kitendo cha sekunde... baada ya sekunde kadhaa alijitokeza tena.....niliona mtu mwingine akiongezeka lakini mtu huyu sikumuona akitua kutokea angani"" ila mtu huyu alikuja kama upepo nilistukia tu namuona""",, alikuja kambeba mtu lakini nilipotazama vizuri niliona mtu yule aliyekujanae alikuwa kafungwa kamba...kisha akamlaza chini....niliogopa sana nilimuonea huruma mtu yule alikuwa akilia kwa uchungu lakini haikusikika sauti yake... kisha nikamuona babu anakitoa kisu chake kwenye kiuno..



    kisha akakishika baraabara..niliona babu akisimama kisha akapiga hatua mbili kielekea pale alipokuwa amelazwa yule mtu aliyeletwa.....akakipeleka kisu kile moja kwa moja mpaka kwenye shingo ya mtu yule"" ,,nilimuonea huruma sana lakini sikuwa na uwezo wa kwenda kumsaidia...babu alikata shingo ya mtu yule kisha akapiga magoti na kuanza kufyonza damu ya mtu yule kupitia ile sehemu aliyo ikata kwa kisu"" ,,mtu yule alirusha rusha miguu kutetea pumzi yake ghafla mtu yule alitulia tuli"" baada ya babu kumaliza kifyonza damu aliinua kisu chake na kukidunga kwenye tumbo la mtu yule. kisha akapasua tumbo lile na kuingiza mkono wake niliona ametoa moyo akauweka pembeni..kisha akaingiza mkono tena"" alipouchomoa mkono alitoka na maini kisha akasimama na kuanza kula maini yale yakiwa mabichi...



    niliogopa sana..nikafumba macho....wale watu wengine walianza kuimba nyimbo zisizoeleweka huku wakicheza kwa kushangilia ushindi wa kazi waliyoifanya isiku huo....nilipofumbua macho niliona watu wale pia wakila nyama ya mtu yule...."" kwa mbali niliona mwanga"" ,, mwanga ule ulikuwa ukimulika kuelekea upande wangu!!! niliogopa nikaamua kula chini...nilipotazama vizuri niligundua ni taa ya baiskeli hivyo nikajua kuwa kunamtu anaendesha baiskeli ile...sikumjali nikageuza shingo kuendelea kutazama kule walipokuwepo akinaBabu na washirika wake.....ghafla waliacha kuimba nikakodoa macho kuona nini kitatokea...ghafla babu alitoweka....CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ni kitendo cha sekunde."" ,, nikazidi kuogopa huku naangaza angaza macho kushoto kulia...ghafla nilisikia mtu yule akipiga kelele!!! nilipotazama upande ule ambo kelele hizo zilitokea niliona baiskeli iko chini...kisha nikaona mtu yule akitimua mbio na kutokomea kabisa...mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda kasi huku jasho likinitoka... nilipotazama kule walipokuwepo watu wale nikamuona babu sikujua alirudi vipi pale...walikaa kimya kwa muda wakimsikiliza babu anachoongea...kiukweli sikusikia maneno yale kutokana na umbali niliokuwepo..ndipo watu wale wakasimama kila mmoja kwenye ungo wake..nakuanza kupaa angani....nakutoweka kusikojulikana



    ***********



    alibaki babu peke yake yeye na kibuyu chake....ghafla na yeye akatoweka kisha kikafatia kibuyu chake....na ule moto uliokuwa ukiwaka ukazimika ghafla pakawa na giza nilizidi kuogopa..nikajiuliza sijui mlango utakuwa umefungwa?? aah kwa baridi hili siwezi kulala nje nilinyanyuka pale chini...kisha nikaanza kuzipiga hatua za kunyata.. ghafla wingu kubwa lilitanda likazifunika mbaramwezi na nyota pakawa na giza nene ikiambatana na ngurumo radi"" punde mvua ikaanza kunyesha....



    ilianza mvia ya manyunyu na baada ya muda ilianza kunuesha mvua kubwa sana...niliogopa sana baada ya ngurumo za radi kuzidi niliamua kukimbia kuufata mlango..nilipojaribu kuusukuma.. kumbe mlango ulikuwa wazi..nilijiuliza sana inamaana babu hakugundua kuwa mlango upo wazi?? je alipitia wapi? nilisita kuingia ndani ghafla radi ilipiga nikaogopa nikaingia ndani na kufunga mlango



    niingia moja kwa moja mpaka chumbani kwangu

    nikapanda moja kwa moja kitandani kwangu.. sikuweza kupata usingizi usiku huo...nilibaki macho mpaka kukakuchacha...



    *********



    niliamka na kujiandaa kwenda shule...."" mara kwa mbali nilisikia tangazo"" niligundua tangazo lile ni la msiba nilistuka sana nikawaza msiba huu itakuwa yule mtu aliyechinjwa na babu yangu usiku wa jana kisha wakala nyama ya mtu yule babu na washirika wake....



    punde babu aliamka kisha akaniambia anajiandaa kwenda msibani baada ya kusikia taarifa hiyo ya msiba iliyotangazwa namjumbe wa nyumba kumi.



    nilimtazama babu kwa macho ya mshangao...sikuamini kama ndiye huyu babu niliyemuona jana usiku..akinywa damu na kula maini ya binadamu"",, kisha nikaendelea kujiandaa ili niende shule....babu alimaliza kujiandaa kabla yangu kisha akatoka chumbani kwake... alinikuta niko sebuleni navaa viatu vyangu...alitoa noti ya shilingi mia tano kisha akanikabidhi akasema utakunywa chai huko shuleni..kisha akatoka na kuondokazake",, nilimchungulia dirishani ili nihakikishe kama atakuwa amefika mbali..niingie chumbani kwake nikaangalie kibuyu kile cheusi kina nini ndani yake.....nilipoona katokomea kabisa yupo mbali na nyumbani niliingia chumbani kwake..nilistahajabu sikukuya kitu hata kimoja chumbani mule yani hata kitanda chake sikukiona!!! chumba kilikuwa wazi utadhani labda hakai mtu ndani yake...niliogopa nikatoka haraka chumbani mule kisha nikachukua begi langu haraka nikatoka nje.....nilirudishia mlango kama kawaida nilivyozoea tangu nilipokuwa mtoto mdogo...nakumbuka babu alishawahi kuniambia kuwa hakuna mtu anayeweza kuja kuiba kitu chochote pale nyumbani yani hata kipande cha kuni......

    *********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nikaanza kuzipiga hatua kuelekea shule....wakati nikiwa njiani alitokea mwalimu wetu wa kiume alikuwa anafundisha somo la kiswahili..alikuwa akiendesha baiskeli kuelekea shule...alisimamisha baiskeli na kuniambia nipande kwa sababu na yeye anaelekea hukohuko shuleni..nilipanda na tuianza safari...

    nilipofika shule nilihesabu namba ghafla kengele iligongwa wanafunzi wote tukakusanyika...kisha mwalimu mkuu akasema wanafunzi wote wa darasa la saba mnatakiwa kwenda msibani kwani mwanafunzi mwenzenu kafiwa na baba yake mzazi.."""" kisha akaamuru tutawanyike na ikawa hivyo kama mwalimumkuu alivyoamuru

    ********

    Sudy......sudy ilisikika sauti ya rafiki ysngu mbonde kisha nikageuka nilimuona anakuja akikimbia ule upande niliokuwepo....mambo vipi mbona sikuizi umekuwa zobazoba hata mpirani hutaki kuhudhulia au babu yako kakukataza usicheze mpira?? aliuliza hivyo mbonde....

    sikumjibu kitu nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nikaamua kumdanganya ili asijue kinachonitatiza....nikamwambia sikuizi ule muda wa jioni huwa najisomea kwa ajili ua kujiandaa na mtihani wa Taifa.. basi sawa rafiki yangu ni jambo jema alisema mbonde.. kisha tukaanza safari ua kuelekea msibani...



    ********



    Tulipofika msibani tulikuta mkusanyiko wa wanakijiji...wanafunzi tulikaa upande wetu...lakini mimi na mbonde tulijitenga tulikaa peke yetu..ghafla nilimuona babu nikastahajabu sana jinsi alivyoondoka asubuhi alikuwa amevaa suluali na shati alafu kavalia koti la suti ya kizamani...alafu namkuta huku kavaa mavazi mengine tena yale anayoyavaa usiku akiwa na washirika wake kwenye vikao vyao vya kichawi...

    alikuwa kavalia kaniki yake nyekundu....nilostahajabu sana sikuwahi hata sikumoja kumuona kavaa hivyo mchana kweupe.. alionekana kutisha kutokana na sura yake ya kizee iliyokunjamana ikiambatana na madevu yake marefu meupe kidevuni......sikutazama sehemu yoyote zaidi ya ule upande aliokuwa amesimama babu....ghafla waliongezeka watu wawili sikujua wametokea wapi niliwatazama watu wale sikuwatambua...lakini nilipovuta kumbukumbu niwakumbuka watu wale"""" ni wale wanaokuja kila siku nyumbani wanakula nyama za binadamu pamoja na babu....watu wale walikuwa uchi...nikamtikisa mbonde...alipogeuka nikamnongoneza ona watu wale wapo uchi.....mbonde alipotazama hakuona kitu chochote aksema mbona sioni kitu!!!!! nikagundua kuwa watu wale pamoja na babu naona mimi pekee..niiliogopa sana..



    *******



    ulipofika muda wa kuaga maiti...watu wakijiandaa kupanga mstari..nilimuona babu akinyoosha mkono wake mmoja juu"""ghafla nikaona kibuyu kile kinatua kwenye mkono wa babu!!!! kisha akasogea mpaka kwenye jeneza na wale watu wawili waliokuwa uchi wa mnya walimfuata...babu alisimama upande wa kichwani kwenye jeneza kisha wale watu wawili ambao wako uchi walisimama pembeni mwa jeneza....nilistahajabu ule umati wote wa watu...hakuna hata mmoja aliyeweza kuona jambo hilo ila ni mimi pekee..



    ********

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wanakiniji waanza kupita moja baada ya mwingine wakaaga mwili ule wa marehemu...walipomaliza watu wote kuuaga mwili wa marehemu...nikamuona babu akiweka kibuyu chake kwenye paji la uso wa marehemu kisha maiti ile iligeuka kuwa gogo la mti....niliogopa sana...nilisikitika nilipoona mke na mtoto wa marehemu wakilia kwa uchungu huku wakigusa mwili wa marehemu....nikajiuliza inamaana watu wote hawa hawaoni kuwa hiyo siyo maiti bali ni gogo la mti....nilimuonesha mbonde lakinj hakuona kitu chochote...

    kaka mkubwa wa marehemu alifunga jeneza kwaajili ya maziko...



    ********

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog