Search This Blog

KIBUYU CHA BABU - 3

 







    Simulizi : Kibuyu Cha Babu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    baada ya kuzika kila mtu alitawanyika wakabaki ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu...kipindi nipo njiani narudi nyumbani nilijiuliza maswsli mengi inamaana kumbe yule mtu aliyeliwa nyama jana usiku alikuwa ni baba wa mwanafunzi mwenzetu. ....nikaingiwa wasiwasi yawezekana hata wazazi wangu babu aliwala nyama..hivyo alinidanganya kuwa waliungulia mdani ya nyumba kwa ajali ya moto!!!!nilikasirika nikamchukia sana babu....

    nilizipiga hatua za haraka nikafika nyumbani...nilikaa kama dakika kadhaa hivi kisha nikamuona babu akija kwa hatua zake za kizee..

    aliponikaribia alisema amesikitishwa sana na kifo kile kuwa marehemu alikuwa rafiki yake...hapo ndipo nilipogundua kumbe wakiwa kwenye mambo yao ya kichawi huwa hawanioni bali mimi nawaona wao..





    babu hakukaa sana tangu alipofika.....aliingia ndani kisha akatoka na kuniaga kuwa anakwenda kwenye kahawa....nilijisemea moyoni babu akitoka tu...itakuwa ndio muda mzuri wa kuingia chumbani kwake nidadisi kibuyu kile...ghafla nikakumbuka kuwa jana niliingia chumbani kwake lakini sikuona kitu hata kimoja yani hata kitanda anacholalia...sijui leo pia itakuwa hivyohivyo?? alijisemea moyoni sudy...

    kisha baada ya dakika kadhaa kupita sudy aliamini kuwa babu yake atakuwa kafika mbali...

    aliingia chumbani""" lakini leo haikuwa kama jana sudy alikitafuta kile kibuyu cheusi chumbani mule mpaka akakiona lakini aliogopa kukishika kibuyu kile kisha akasema potelea mbali liwalo na liwe akatichukuwa kibuyu kile na kutoka chumbani kisha akaelekea nje...alizunguka nyuma ya nyumba kwa hatua za harakaharaka...wakati anazipiga hatua hizo huku akitazama huke na kule kushoto kulia ghafla alijikwaa kwenye kipande cha jiwe lililokuwa limezama chini ya aridhi na kutokeza kidogo upande wa juu ya aridhi sudy alidondoka chini Tiiiiiii""" alikiachia kibuyu kile ili mikono yake ishike aridhi asijigonge uso wake kwenye aridhi....

    kibuyu kilidondoka chini kikafunguka""" kilikuwa kimefungwa na kipande cha kaniki nyeusi.. ghafla. kilianza kufuka moshi"" moshi ule ulitoka kupitia upande wa juu ya kibuyu...sudy aliogopa sana akanyanyuka haraka pale chini...kisha akakimbia hatua kama kumi hivi akasimama na kugeuka kukitazama kibuyu kile....alistahajabu kuona vivuli vya binadamu vikitokea ndani ya kibuyu kile"" vivuli hivyo vilikuwa vingi sana havina idadi....sudi aliogopa sana mapigo yake ya moyo yalianza kwenda mbio...



    ***********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    upande mwingine nako alionekana babu kule kwenye kahawa baada ya kibuyu kile kudondoka kunakitu kilimuingia akastuka sana!!!! akakiachia kikombe cha kahawa kutoka mkononi mwake kikadondoka chini na kupasuka...wale watu wengine waliokuwepo pale kwenye kahawa walistahajabu kumuona Mzee Mkumbo yupo katika hali ile kwani uso wake ulionekana kuwa makini na jambo fulani...kisha alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi...walimsemesha lakini hakuwajibu kitu alibaki vilevile kama kapigwa shoti ya umeme...ghafla Mzee mkumbo alisimama kama roboti na kuanza kuzipiga hatua alijitahidi kutembea harakaharaka lakini kutokana na umri wake kuwa mkubwa alishindwa alijikuta anayumbayumba kisha akaendelea kuzipiga hatua zake za kizee""" ukimtazama mzee mkumbo uso wake ulionesha kuwa kunajambo linamtatiza kwa sababu alionekana kuwa na wasiwasi...."""

    mzee mkumbo uzee unamsumbua"" au presha imepanda kutokana na kahawa nyingi aliyokunywa leo...ohooo hilo ndio tatizo la kahawa ukinywa nyingi tu..mapigo ya moyo yanaanza kwenda mbio utadhani unakimbia..

    maneno hayo aliyasema kijana mmoja aliyekuwa miongoni mwa wale watu waliokuwa wanakunywa kahawa pale .



    *******



    kule nyumbani Sudy alizidi kuchanganyikiwa alistahajabu vivuli vile vya binadamu vilitoka kwa mfululizo...ghafla upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu utadhani kimbunga ulitokea pale kibuyu kilipokuwepo...alipotazama sehemu nyingine hakuona upepo huo isipokuwa pale nyumbani kwao pekee tena ile sehemu ambapo kibuyu kilidondoka."""",,,sudy aliogopa zaidi alipoona ule upepo unazidi kuwa mkubwa ukivuma kwa kuzunguka!!! kumfuata yeye....sudy alipoona hivyo aliamua kutimua mbio...alikimbia kama kawekewa mota miguuni....nadhani siku hiyo angeshindana na hunsen bolti basi sudy angeshinda shindano hilo la mbio....alikimbia bila kugeuka nyuma...

    ghafla aligeuka sudy alipiga kelele baada ya kuona upepo ule uko karibu yake tena ukiwa umebadilika na kuwa na rangi nyekundu mara ghafla..



    Sudy alikimbia sana hata pasipokujua anakoelekea....wakati anakimbia kwa lengo la kukimbia upepo ule mwekundu uliokuwa ukivuma kwa kasi ukiwa unazunguka huku ukimfata nyuma yake.. mara ghafla alikutana na babu yake njiani....

    sudy alipomuona babu yake alikimbilia ule upande aliokuwepo babu yake...ghafla babu yake alifungua mdomo kisha akanyoosha mikono yake juu macho yake yalibadilika na kuwa mekundu....upepo ule uliingia moja kwa moja mdomoni mwa mzee mkumbo......wakati upepo huo ukiendelea kuingia mdomoni mwa babu yake...sudy alistahajabu""",,,aliogopa sana kisha akaanza kutimua mbio kuelekea kusikojulikana....

    *********

    mzee mkumbo aliendelea kufumbua mdomo wake mpaka upepo ule uliishia mdomoni mwake....kisha kile kibuyu cheusi kilitokea angani kikadondokea mbele yake....macho ya mzee mkumbo yalirudi katika hali yake ya kawaida...kisha akakiokota kibuyu kile na kukiinua juu alisimama huku kakishika kibuyu kile kwa sekunde kadhaa kisha kibuyu kile kilitoweka ghafla....

    shwaini huyu mtoto angeniletea balaa laiti kama upepo ule ungemgusa angeiaga dunia na nafsi yake ikaingia ndani ya kibuyu....

    *******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine sudy alionekana akikimbia huku akigeuza shingo yake huku na kule...wakati anakimbia alipata wazo aende nyumbani kwao mbonde... alikimbia bila kusimama mpaka kwa kina mbonde wakati huo mbonde wakati huo ilikuwa kama majira ya saa moja jioni..

    mzee mkumbo alizipiga hatua na kuelekea nyumbani....alikasirika sana kwa kile kitendo cha sudy kuingia nda ya chumba chake bila ruhusa yake na kufanya yasiyomuhusu...kama kibuyu kimefunguka basi zile nafsi za watu niliowauwa kimazingala zitaniponza itakuwa balaa kubwa....alijisemea moyoni mzee mkumbo liwalo na liwe mimi ndio MKUMBO alijisemea moyoni"""

    alizipiga hatua na hatimae akafika nyumbani...alipitiliza moja kwa moja mpaka ndani kisha akaingia kwenye chumba chake"" aliinama haraka akachungulia uvunguni aliuvuta ungo wake kisha akahakikisha kama vitu vyake vya kichawi vitakuwa salama....""",,, aliona vitu vyake vyote vipo sawa isipokuwa kibuyu kile kilikuwa bado hakijafika....mara ghafla kilitokea kibuyu kile""",, hapo nafsi yake kidogo ikatulia....alikichukua kibiyu kile kisha akakipeleka moja kwa moja mpaka mdomoni...kisha upepo ule alioumeza aliuingiza ndani ya kibuyu kile kisha akakifunga na kipande cha kaniki nyeusi.....



    *********



    kijijini hapo balaa likaanza....walionekana watu wengi walio fariki miaka mingi iliyopita watu hao walitisha sana walikuwa na nywele ndefu....kucha ndefu walitembea kwa mwendo wa kizembe huku udenda ukiwatoka mdomoni...kumbe watu hao waliuwawa kichawi na mzee mkumbo kisha akazifungia nafsi zao ndani ya kibuyu kile....

    watu hao walionekana baada ya sudy kukidondosha kibuyu kile kikafunguka na nafsi zao zikatoka ndani ya kibuyu kile.......wakiwa MISUKULE tayari"""",,, wanakijiji walistahajabu sana....kuona ndugu zao waliofariki miaka mingi kumbe bado walikuwa hai,!!!..itakuwa kunamtu aliwauwa kichawi na kuzifungia nafsi zao....alisema hivyo mwanakiniji mmoja...

    wale watu misukule walienea kijijini hapo walikuwa wengi hakuna mfano.......walitapakaa huku na kule

    ilibidi aitwe mganga mkuu wa wachawi kutoka kijiji cha jilani ili kumtambua ni nani aliyesababisha hayo yote kisha auwawe hadhalani...alitumwa kijana mmoja kwenda huko kwenye hicho kijiji cha jilani kwa lengo la kumuita mganga yule mkuu wa wachawi...""" taarifa hizo alizipata mzee mkumbo....kwa njia ya kichawi kisha alicheka sana akajisemea moyoni nadhani hamjanitambua mimi ni nani yeyote atakayenifatilia nitamuonesha mimi ni nani......naanza na huyo mliomtuma...

    wakati kijana yule akiwa njiani kuelekea kijiji cha jilani... hana hili wala lile mara ghafla..



    Mara ghafla aliitokea kichawi mzee mkumbo mbele ya kijana yule..ni kitendo cha sekunde..

    kijana yule aliogopa sana aliamua kutimua mbio kwa sababu hakuona mzee mkimbo akizipiga hatua alistukia tu yupo mbele yake.....kijana yule alizichanja mbuga mara ghafla mzee mkumbo alijitokeza tena mbele ya kijana yule...kijana yule kutokana na kasi aliyokuwa kikimbia nayo kijana yule alidondoka chini baada ya kusimama ghafla. kisha mzee mkumbo akanyoosha kidole kuelekea pale alipodondoka kijana yule...mara ghafla kijana yule alikiwa kipofu pia hakuwa na uwezo wa kuongea tena mzee mkumbo alimfanya bubu...kisha mzee mkumbo akatoweka ghafla.



    ********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    kule nyumbani kwa kina Mbonde"""""....sudy aliamua kumueleza kila kitu rafiki yake....mbonde sliogopa sana kusikia yale aliyosimuliwa na sudy...sasa itakuwaje?aliuliza mbonde

    hata mimi sijui cha kufanya" alijibu sudy..kisha akasema naogopa kurudi nyumbani babu ataniuwa najua atakuwa amekasirika....mbonde alianza kumuogopa rafiki yake sudy....kutokana na yale mambo ya kichawi anayoyafanya Babu yake....aliuliza je babu yako akijua kuwa upo kwetu itakuaje si atatuuwa na sisi....aah mimi naogopa itabidi urudi tu nyumbani ukamuombe msamaha.....sudy alinyong'onyea sana baada ya mbonde kumwambia hivyo...aliamua kuondoka bila kusema kitu chochote....

    wakati sudy anazipiga hatua kuelekea kusikojulikana ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku....ghafla alikutana na MSUKULE mmoja njiani...msukule yule ni mmoja kati ya zile nafsi zilizotoka kwenye kibuyu zikiwa kama kimvuli cha binadamu..""sudy aliogopa akatimua mbio....kabla hajafika mbali alikuta tena na MSUKULE mwingine...sudy alizidi kuchanganyikiwa...



    *********



    mzee mkumbo alionekana chumbani kwake ni baada ya kumpofua na kumfanya bubu kijana yule kisha akatoweka kichawi....mzee mkumbo alipanga mikakati madhubuti ili kuhakikisha anawanasa misukule wale wote waliotoka ndani ya kibuyu...kazi hiyo nitaifanya usiku wa leo...alijisemea mzee mkumbo. kisha akaanza kuandaa vitu vyake vya kichawi....



    ********

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati sudy akiwa njiani aliamua kutimua mbio kuelekea nyumbani kutokana na uwoga baada ya kukutana njiani na misukule wale. alitimua mbio mpaka nyumbani alipofika jilani bisa na nyumbani kwao alipunguza kasi ya kukimbia hatimae akaanza kutembea...alizipiga hatua huku akigeuza shingo yake huku na kule...... slipotazama nyumbani kwao aliona mpaka muda huo taa haijawashwa.....alihisi huenda babu yake hayupo..alinyata akasogea kabisa mpaka kwenye mlango aliusukuma ukafunguka....alisita kuingia kisha akaamua kumuita babu...lakini babu yake hakuitika......mmmh!!!! sasa babu atakuwa kaenda wapi au ameuwawa na ule upepo uliovuma kwa kuzunguka huku ukiwa na rangi nyekundu.!!!!!! sudy aliogopa sana....alishindwa hata kuingia ndani...



    *********



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog