Search This Blog

KIBUYU CHA BABU - 4

 







    Simulizi : Kibuyu Cha Babu

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee mkumbo alikuwa tayari kwa ajili ya kazi aliyopanga kuifanya usiku huo alionekana akiizungukia mitaa kwaajili ya kuikusanya MISUKULE ile airudishe ndani ya kibuyu... kumbe taarifa zile zilimfikia yule mganga mkuu """ na yeye pia muda huo alikuwa akijipanga ili kwenda kumkabili huyo mchawi anayesumbua kijiji cha jilani ambaye ni Mzee mkumbo...



    wakati mzee Mkumbo akiwa anazunguka zunguka kwenye mitaa ya kijiji hicho..... alihisi harufu ya jambo la hatari...alistahajabu arufu hiyo ilizidi kuongezeka...hiyo ilimaanisha kunajambo la hatari litatokea muda si mrefu.....alikasirika sana akajisemea ni nani hiyo anayetaka kuingilia himaya yangu......mzee mkumbo alianza kuingiwa wasiwasi....huenda kunamtu mchawi zaidi kuliko yeye...



    *********



    kumbe yule mganga mkuu kutoka kijiji cha jilani alikuwa ameisha ingia kwenye kijiji anachoishi mzee mkumbo......kisha akaanza kutega mitego ya kumnasa mzee mkumbo kwa kutumia madawa ya kichawi... mzee mkumbo akiwa hana hili wala lile mara ghafla..



    Mara ghafla mzee mkumbo aliona..mwanga mweupe unakuja kwa kasi kumfata pale alipo....alipoona hivyo aligundua kuwa hizo ni nguvu za kichawi zimerushwa ili zidhibiti....macho yalimtoka.....kisha akanyanyua kibuyu chake ili kuzikabili nguvu hizo za kichawi....alijibu mashabulizi"" nguvu zile zilivyokutana zilishambalatika na kuyayuka.....yule mganga alistuka sana hakuamini kama kunamtu anayeweza kukabilia na yeye....yule mganga alipo ona hivyo aliamua kuongeza nguvu za kichawi mara mbili ya zile alizozirusha....zilimfata mzee mkumbo alikwepa kisha na yeye akajibu shambulizi.....uchawi wa mzee mkumbo zilionekana kuwa na nguvu kuliko uchawi wa mganga yule aitwaye MAZIKU...

    zile nguvu zilikwenda moja kwa moja kumfata pale alipokuwa....maziku na yeye alirusha nguvu za kichawi ili kuzikabili zile skadi alizozirusha mzee mkumbo.....lakini haikusaidia chochote nguvu za kichawi za mzee mkumbo zilipenya katikati ya zile nguvu za mganga na kumpata...skadi ile ilimpiga kifuani yule mganga na kumrusha mbali sana.....kisha akatuwa na kudondoka chini.....

    mzee mkumbo alicheka kwa saiti kubwa.....kwa kweli sauti hiyo ilitisha....kisha akasema Hakuna wa kupambana na mimi....

    mimi ndio MKUMBO mkuu wa wachawi..

    yule mganga alipata majeraha ni baada ya kupigwa na zile skadi za nguvu za kichawi alizozirusha mzee mkumbo..



    ************



    kule nyumbani Sudy aliamua kuingia ndani aliogopa sana kuona misukule ile alifunga mlango kisha akaingia chumbani kwake....alipanda kitandani....aliwaza sana juu ya yale aliyoyaona"" hivi ni kweli au nilikuwa naota ndoto za chanamchana!!!!!!! aliamua kuutafuta usingizi kwa sababu alikuwa kachoka sana..hivyo ndani ya sekunde kadhaa alikuwa kashasingia kabisa...



    ********



    Ule upande mwingine yule mganga mkuu alivyoona kajeruhiwa alitoweka akayeyuka kichawi..."""mzee mkumbo alitoa macho kutazama ni wapi alipoelekea lakini hakumuona...shwaini huyu anataka kunijaribu eee haya jitokeze tena nikuoneshe kazi ya kibuyu changu....

    yule mganga mkuu alikwenda kijijini kwao kujipanga upya ili kumkabili mzee mkumbo...

    mzeemkumbo alipojaribu kutazama kwa kutumia nguvu za kichawi aligundua kuwa mganga yule MAZIKU kwamba hayupo tena maeneo hayo...kisha akaendelea na ile kazi aliyokuwa ameipanga kuifanya usiku huo....ni kazi ya kuwakusanya misukule wale na kuwarudisha ndani ya kibuyu chake ili aendelee kuwatumia katika shughuli zake mbalimbali....kumbe mzee mkumbo alikuwa akiwatumia misukule wale kuwalimisha mashamba yake...wengine aliwatumia kuwaibia watu pesa kichawi(CHUMAULETE) alizungukia maeneo yote lakini hakuweza kufanikiwa kupata hata msukule mmoja kwa sababu walikiwa tayari wameshatoka ndani ya kibiyu kile hivyo haiwezekani tena kuwarudisha kwa namna yoyote ile"" mzee mkumbo alihisi kuchanganyikiwa....alijaribu kadri ya uwezo wake lakini ilishindikana kila akikutana na msukule akijaribu kumrudisha kichawi ndani ya kibuyu kile ilishindika......alijaribu mpaka ikafika usiku wa manane bila mafanikio....hakuamini macho yeke kama ameshindwa kuwarudisha misukule wale ndani ya kibuyu.....alikata tamaa akaamua kuondoka zake alistuka""""kumbe yule mganga karudi na nguvu mpya mara ghafla..



    Mzee mkumbo hakuamini macho yake...shaabashi!!! huyu mwanaharamu karudi tena kwani anataka nini!!!!? alijiuliza mzee mkumbo kisha uso wake ukaonekana kujaa jazba na hasira za hali ya juu ukizingatia alikuwa ameshahisi kuchanganyikiwa baada ya kishindwa kufanikisha kazi aliyokuwa ameipanga kuifanya usiku huo kurudisha zile nafsi za watu aliowauwa kichawi misukule..."""" alinyanyua kibuyuchake kisha akarusha nguvu za kichawi kuelekea pale kwa yule mganga Maziku....mzee mkumbo alistahajabu sana shambulizi lile halikumfanya chochote mganga maziku...."""" mzee mkimbo alitoa macho kama mjusi kabanwa na mlango...

    Mganga maziku alicheka sana hahahahah"" kitendo hicho cha maziku kucheka kilimfanya mzee mkumbo hasira zimpande kichwani mara tatu zaidi...alianza kuzunguruka kama jogoo anapomvizia jike.....kisha akanyanyua kibuyu chake juu.... ulitokea mwanga kama radi kisha mwanga huo ukafuata moja kwa moja mpaka pale alipokuwa amesimama mganga maziku.....hiyo ilikuwa balaa hatari sana.....maziku alitoa macho kisha na yeye akarusha nguvu zake za kichawi ili zizuie zile nguvu za mzee mkumbo lakini alikuwa amechelewa zilikwenda moja kwa moja mpaka katikati ya kifua cha mganga maziku...na kumrusha juu kisha mzee mkumbo akafungua kibiyu ili amnase mganga maziku aichukue nafsi yake aifungie ndani ya kibuyu..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********



    kule nyumbani sudy alistuka kutoka usingizini..ni baada ya kuhisi kiu ya maji ya kunywa.. alinyanyuka kitandani akaelekea sebuleni aliwasha koberiti na kuchoma utambi wa chemli kisha ikawaka alifungua mtungi wenye maji ya kunywa kisha akaondoka zake kurudi chumbani kuendelea kulala...



    ************



    kule kwenye vita ya kichawi kati ya mzee mkumbo na mganga maziku iliendelea...baada ya mzee mkimbo kufungua kibuyu ili amnase maziku.... mara ghafla zile nguvu za kichawi zilimuachia mganga maziku akiwa bado yupo juu kabla hajatua chini...kisha akatua chini bila kupata madhara yoyote..mzee mkumbo alistahajabu sana akajiuliza nini kimetokea???? mbona nimepoteza nguvu zangu ghafla..

    kumbe wakati sudy anakunywa maji alisahau kuufunika mtungi akauwacha wazi bila kuufunika...hivyo ni kosa kubwa sana inapofika usiku wa manane kisha ukafungua mtungi kwenye nyumba ya mzee mkumbo kwani endapo mtungi ukifunuliwa mda wa usiku wa manane basi unazizuia nguvu zake kufanya kazi.......

    mzee mkumbo alijaribu kurusha skadi za kichawi lakini ilishindikana"" ndipo mzee mkumbo akagundua kuwa kunatatizo nyumbani kwake bila shaka mtungi umefunuliwa majira hayo. ndio maana nguvu zake hazifanyi kazi!!!!! wakati akiwaza hivyo mara ghafla...alistuka amepigwa na skadi kifiani kwake akaanguka chini....kabla hajafanya kiitu chochote akapigwa tena na skadi nguvu hizo za kichawi zilitoka kwa mganga maziku....mzee mkumbo alipo ona kazidiwa aliamia kutoweka aliyayuka kichawi akatokomea kisikojulikana ni kitendo cha sekunse akafika nyumbani kwake....alipotazama ule mtungi wa maji ya kunywa ulikuwa wazi...... ilibidi amuite mjukuu wake sudy aje afunike mtungi ule...kwani ni mwiko kwa mzee mkumbo kushika au kugusa mtungi majira ya usiku wa manane.....emdapo angefanya hivyo angeweza kupoteza uhai wake papo hapo...aliita lakini sudy hakuitika ghafla alisikia harufu harufu hiyo ilimaanisha hatari inatokea muda si mrefu.....kumbe ni yule mganga maziku anakuja akiwa angani juu ya ungo kwa kasii ya ajabu.. ....aliitambua harufu hiyo kichawi""" mzee mkumbo ilibidi aingie haraka chumbani kwa sudy ili amuamshe sudy afunike mtumgi ule ili nguvu za kichawi za mzee mkumbo zirejee haraka kumkabili mganga maziku.....mzee mkumbo alipagawa alipoingia chumbani kwa sudy lakini hakumkuta sudy...nimekwisha""" alijisemea moyoni huku jasho likimtoka kama kamwagiwa maji.. kumbe sudy alijificha uvunguni kwa kuhofia huenda babu yake alikuwa anataka kumuadhibu...mzee mkumbo alitoka chumbani kwa sudy haraka ili aangalie namna ya kufanya"" ile amefika sebuleni mara ghafla..



    Mara ghafla mganga maziku alirusha nguvu za kichawi zilikwenda moja kwa moja mpaka pale alipo simama mzee mkumbo mlangoni mzee mkumbo alikwepa... kisha akayayuka akatoweka kichawi ilibidia aingie chumbani kwa sudy alipojaribu kuangalia kichawi akamuona sudy yupo chini ya uvungu... alimbalidisha ufahamu akampachika mawazo kichawi...ghafla sudy alinyanyuka kutoka mvunguni haraka akaelekea sebuleni... alifunika mtungi haraka.... wakati huo sudy hakutambua alicho kifanya kwa sababu haikuwa akili yake.... alibadilishwa mawazo kichawi na babu yake... mzee mkumbo nguvu zake za kichawi zirirudi muda huohuo... alinyanyua kibuyu kisha akarusha nguvu za kichawi kuelekea pale alipo kuwepo Mganga maziku.... skadi ile ilikwenda moja kwa moja mpaka kifuani kwa mganga maziku... zilimrusha mbali sana huku akiwa anawaka moto.... sudy akuweza kushuhudia vita ile kutokana alifumbwa kimiujiza na babu yake...

    mganga maziku alipotua chini alikuwa akiwaka moto kama mtu aliyemwagiwa mafuta aina ya petroli. "" alipo ona mambo yamekuwa magumu aliamua kutoweka kichawi""" lakini mzee mkumbo alimuona aliamua kumfuata....baada ya mzee kumbo kuona ameanza kuingia kwenye mpaka wa kijiji cha jirani alikata tamaa ya kumpata mganga maziku.... aliamua kurudi kijijini kwao kutokana ilikuwa inaelekea majira ya saa kumi na moja alfajiri....ni kitendo cha sekunde tayari alikuwa ameshafika nyumbani kwake....



    ***********

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    palipokucha sudy alistahajabu babu yake hajadamka mpaka muda huwo ilikuwa saa mbili kasoro.... za asubuhi. na si kawaida yake... kwani alizoea kumuona babu yake akidamka mapema wakati mwingine yeye ndiye huwa anamuamsha sudy aende shule aliingiwa na uwoga akaamua kwenda kugonga mlango wa babu yake""""mzee mkumbo alistuka kutoka usingizini...akaitika alipojaribu kuamka alihisi maumivu mwili mzima hii ni kutokana na ile vita ya kichawi aliyopambana jana usiku...alijikongoja mpaka mlangoni kisha akafungua mlango.. sudy alimsalimia babu yake na baada ya kumuona babu yupo salama sudy aliamua kuondoka na kuelekea shuleni.... alizipiga hatua na hatimae alifika sguleni.. alikuta wanafunzi wenzake wamo darasani wameshaanza vipindi vya masomo...aliingia darasani na kuanza kumsikiliza mwalimu akifundisha... mara ghafla walionekana misukule wakilandalanda shuleni hapo misukule hao walikuwa wengi sana walitembeatembea huku na kule kwenye eneo hilo la shule""" wanafunzi baada ya kuona hivyo waliogopa wakatoka madarasani wakakimbia kila mtu na njia yake... hata walimu walijiunga pamoja na wanafunzi kutimua mbio... sudy alistahajabu aliumia sana moyoni kwa kuwa alikuwa anajua misukule wale walitokea wapi!!!!! misukule hao walianza kuonekana baada ya sudy kudondosha kibuyu cha babu yake kikafunguka upande wa juu kilipofungwa na kipande cha kaniki nyeusi""" nafsi za watu wale zilitoka ndani ya kibuyu kile kisha zikawa huru....



    ***********



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog