Search This Blog

MTOTO WA MCHAWI WA KIJIJI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : YONA FUNDI

    *********************************************************************************



    Simulizi : Mtoto Wa Mchawi Wa Kijiji

    Sehem Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Toka! Toka! Toka! Leo ndio mwisho wenu. Tumewavumilia vya kutosha sasa basi, Basi!” Zilisika nje ya nyumba ya Mzee Shabani Mlakwama. Sauti za ghadhabu zilizochanganyika na hisia kali vinywani vya baadhi ya vijana katika kijiji cha Tangeni miongoni mwa vijana waliofika kuumaliza utawala wa Mzee Shabani Mlamkwama kama walivyoamini kuwa mwisho wake umefika.



    Kelele nyingi zilisikika kama vile watu wanapomkimbiza mwizi, kwa nia tu kukomesha hali ile. Uchungu wa kila kijana uliongezeka maradufu, yote visa na matukio ya kutisha ya ndani ya kijiji chao. Vijana kupotea, vifo vya kukutatanisha vikihusishwa na mazingira ya kichawi tena wa kutisha sana. Muhusika wa yote akiwa Mzee Shabani na familia yake.

    Tangia kuhamia kwake muda mfupi tu, Tangeni ilikumbwa na balaa. Hali ilikuwa mbaya zaidi, matukio ya kutisha yalitawala. Ushirikina wa hali ya juu, wanakijiji kupotea, mazao hayapatikani shambani, kila ukionesha juhudi unaambulia robo tatu tu ndani ya hekari nzima. Haijalishi iwe ya mahindi au mchele, tabu tu!



    Suala hili liliwapa wakati mgumu sana viongozi wa kijiji pamoja na wanakijiji wenyewe. Hapo sasa ndipo walipoamua kutafuta suluhisho na nini chanzo cha yote hayo. Waganga na waganguzi kutoka katika kila pembe ya kijiji walitafutwa ila waligonga mwamba. Hawakujua nini tatizo linalowatafuna watu wa Tangeni ila walichojua kuwa ni pazito na si pa masikhara, inahitaji mganga tofauti kabisa wa kutoka nje ya Tangeni. Hivyo juhudi za kumsaka mganga zilianza na kwa bahati nzuri walimpata Bwana Mzanzu Wa Wazanzu, kiboko ya wachawi katika kila pembe ya Dunia. Kupatikana kwa bwana huyo, kidogo ilileta matumaini ndani ya kijiji cha Tangeni.

    Ujio wa Mzanzu wa Wazanzu, kiboko ya wachawi ulikuwa si ujio wa masikhara ndani ya kijiji cha Tangeni. Kila Mwanakijiji alipata habari zake wakiamini sasa tatizo linaweza kuwa bayana kila Mwanakijiji akajua ninikinachokisibu kijiji chao.

    Kuwasili kwa Mzanzu Wazanzu, kiboko ya wachawi ndani ya kijiji ilikuwa tumaini jipya. Waliteuliwa vijana wachache, kama kumi na wawili ilikuweza kumsaidia na kumpa mahitaji wakati wa shughuli yake itakapoanza. Mzanzu aliagiza mahitaji yote ikiwemo mtama, uwele, ufuta, pamoja na kondoo dume kwa ajili ya kazi hiyo ambayo alipanga kuifanya majira ya saa saba za usiku wakati dunia ikiwa inajibadili kama waaminiavyo Wachawi katika ulimwengu wa giza.

    Vifaa vyote muhimu vilikamilika, ilibakia muda wakuanza shughuli yake Mzanzu Wazanzu, kiboko ya wachawi. Muda ulienda kwa kasi na hatimaye wakati wenyewe wa shughuli ulitimia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzanzu Wazanzu akiongonzwa na wale vijana kumi na wawili, aliaanza kazi huku akionesha kujiaamini kwa kiasi kikubwa sana. Alichukua mtama, uwele, ufuta akavichanganya kwa pamoja huku akiongea maneno fulani hivi kwa taratibu sana. Mwanzoni hata wale vijana hawakuyasikia ila baadae kidogo yalipita vizuri kwenye ngoma za masikio yao.

    “Mzilli... Mzilli... Cha cha mziliii” “Uwaano... Uwano kazi mziliiii” “Uuutuu mziilli… Cha chaa”

    Alizidi kutamka maneno yale huku akiwa anachanganya vile vitu kwa dakika hivi. Huku akiwa anaendelea kuchanganya, hali ya hewa ilianza kubadiika. Wingu jeusi lilitanda juu ya anga, mungurumo wa radi ulipiga, ulifanya vijana waliokuwa wakimsaidia Mzanzu Wazanzu kuogopa sana.

    Yeye akiendelea na kazi yake, mara alinyamaza ghafla. “Piteni hapa.” Kwa sauti ya kutisha iliyojaa utetemesho, mganga aliwaita wale vijana na kuanza kuwapa ule mchanganyiko. Wote waliokuwepo pale hali yao ilibadilika, wakaanza kuona vituko vya kichawi sasa mbele ya mboni zao.

    Mzanzu Wazanzu aliagiza aletewe kondoo yule halafu akanena, "Kazi imeisha. Mimi sitowatajia nani anayesumbua kijiji chenu, ila mtamuona wenyewe. Kitu kimoja tu! Msishangae. Mkishaangaa tu! Hata mmoja wenu, litakalowakuta tusilaumiane nadhani tumeelewana vijana". Kwa sauti ya kuonesha msisitizo.



    Haraka Mzanzu alipitisha kisu shingoni kwa yule kondoo, damu zilimwagika na umwagikaji ule ulifanya sehemu ile ibadilike. Vijana wakajikuta wapo katikati ya mkutano wa Wachawi ukiongonzwa na Mzee Shabani. Mandhari ya pale yalitisha sana. Maneno makali na ya Mzee Shabani yaliwatisha sana. Vijana waliona kama vile wanaonekana na Wachawi hao, la hasha hata punje ya taswira zao hazikuweza kuonekana mbele ya macho yao.

    Huku wakiongonzwa na Mzanzu Wazanzu, vijana walizidi kuoneshwa ukatili na unyama wa Mzee Shabani, kiongozi wa Wachawi. Watu walipotea, ilizidi kuwatisha vijana hao na kuwaongezea machungu ndani yao. Mzanzu aliwaonesha kila kitu.

    Hatimaye Mzanzu Wanzanzu, kiboko ya Wachawi, aliwaambia sasa kazi imekwisha na yeye hatoweza kulala pale kwa hali ilivyo. Ila wale vijana ndio watawapa majibu viongozi na Wanakijiji wengine juu ya kinachoikumba Tangeni. Walikubali na kila moja alirudi kwao huku wakiwa hawamini walichokiona. Ila mganga Mzazu, hakuondoka hivihivi, aliwaachia dawa vijana wale.

    Asubuhi na mapema, la mgambo lililia na kama unavyojua la mgambo likilia huwa lina jambo athirani. Hivyo jioni waliitisha mkutano wakijiji na Wanakijiji wote walidhuria kwa wingi tofauti na mikutano mingine inayotokea ndani ya kijiji cha Tangeni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Ajenda kila mtu alifahamu, nini tofauti na kawaida kabisa. Mara nyingi Mzee Shabani huwa ni mhudhuriaji mzuri wa Mikutano, ila siku hiyo hakufika na watu walibaini kuwa hakufika kwenye eneo lile. Japo haikushangaza, na kwa wengine waliamini tu hatakuwa labda tangazo halijamfikia kutokana mkutano wenyewe kuitishwa ghafla, na kibaya zaidi nyumba yake ilijitenga kivyake.

    Mkutano ulifunguliwa mapema kabisa. Mwenyekiti wa kijiji aliongea kwakina mchakato uliofanyika juu ya jambo lile. Kila mmoja alielewa vizuri tu! Kutokana na mganga Mzanzu alivyowachia maagizo, vijana wale ilibidi awape fursa ya kuongea iliwaweze kubaini nini walichokuwa nacho vijana hao.



    Siri, miongoni mwa vijana hao ndio alipewa jukumu la kunzungumza kwaniaba ya vijana wale kumi na wawili. Alinyanyuka na kuanza kuzungumza mambo waliyoyaona mwanzo hadi mwisho. Sasa ikafika muda wakumtaja mhusika kuwa ni Mzee Shabani na wenzake. Siri alikuwa kama amepigwa na ububu, ghafla hali yake ilibadilika, jasho lilimtoka kwa hali ya juu kitendo kilichowafanya wanakijiji waogope sana, macho Siri aliyatumbua. Hali yake ilibadilika sana, harakaharaka vijana walimbeba Siri. Hata hawakufika mbali, Siri alipoteza maisha mikononi mwao. Kikao kiliahirishwa, na sasa watu wakajiandaa kufanya mipango ya mazishi. Kifo cha Siri kiliwatatanisha sana, kuogopesha miongoni mwa vijana wale.

    Hali ilikuwa mbaya sana ndani ya kijiji. Maziko ya Siri yalifanyika huku ikifatiwa na vifo vya wale vijana. Wengine walikuwa miongoni waliteuliwa moja moja walipoteza maisha. Hali iitisha zaidi ndani ya kijiji cha Tangeni.



    Ni mmoja tu! Ndiye aliyebaki. Ndio aliweza kuwaambia kinachowamaliza. Watu hawakuamini kuwa unyama wote unaotokea ndani ya kijiji chao ni Mzee Shabani. Ndipo hapo baadhi ya vijana walikusanyika wakiwa na majembe, wengine mapanga kwa hasira na chuki iliyosababishwa na vitendo vya unyama wa Mzee huyo.

    Vijana walizidi kupiga mayowe, lakini hakuna mtu aliyejibu si Mzee Shabani wala mwanae Mwajabu, hata mkewe. Ndani kulikuwa kimya tu.

    _______________

    Urembo wa Mwajabu Bint Shabani ulikuwa tishio. Kila mtu alivutiwa nao. Umbo lake la wastani, macho yakulegea, tabasamu lake, rangi nzuri ya maji ya kunde, ni vitu adimu sana. Wasichana wengi hawana tofauti na Mwajabu. Tangia nimjue ndani ya kijiji chetu cha Sitakishari, imeniletea shida ndani ya mtima wangu. Jack mimi, tatizo la moyo acheni tu!

    Sikujua nilizoeana naye vipi, ila nilijikuta tumekuwa marafiki ndani ya muda mfupi tu. Japo ulikuwa ni urafiki wa kawaida, ila nilikuwa naamini ipo siku utazaa matunda, na Mwajabu bint Shabani atakuwa wangu siku moja. Sikuwa na mzaha hata kidogo, nilichohitaji siku moja nikuwa Baba na yeye Mama wa watoto wetu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mazoea kati yangu na Mwajabu, yaliongezeka siku hadi siku mpaka kuna baadhi ya watu zangu wa karibu walianza kuhisi uenda kunakitu kinaendelea baina yangu na binti huyo. Vijiutani utani vilikuwa haviishi, wengine mpaka waridiliki kuniita Baba Mwajabu. Ila mimi niliona sawa tu, wananivimbisha kichwa. Kwa jinsi ya uzuri alionao Mwajabu, kila mvulana ndani ya kijiji chetu, tangia ahamie pale, hakuna mtu aliyetaka kucheza mbali. Kila mtu alikaba nafasi yake, ila mimi nilionekana nikojuu zaidi ya vijana wenzangu wengine.



    Namna mambo yalivyozidi kwenda, ndio ukaribu ulizidi. Nakumbuka jana nilikuwa na Mwajabu kisimani tukiongea mambo mawili matatu, dah! Kuna jambo aliniambia lilinishitua sana. Kwajinsi ambavyo Mwajabu alivyokuwa akiniambia, nilizidi kuogopa. Niliogopa sana na moyo wangu ulikuwa kama umepigwa msumali ndani yake, na sasa Mwajabu maneno yake kwangu yalikuwa kama kuuchomoa au kuchoma zaidi moyo wangu. Namna alivyokuwa akiendelea kunena, alizidi kiniumiza. Kadiri alivyokuwa akiyatamka ndani ya kinywa chake hali yangu ilikuwa ikibadilika kwa muda mfupi tu.



    Kwa jinsi moyo wangu ulivyozama kwake, sikupenda hata kidogo maneno yale yalivyokuwa yakipenya ndani ya masikio yangu yote mawili. Yalichoma choma ngome zangu za masikio na kuipoteza kabisa furaha yangu. Si mimi tu! Niliyekuwa nikuumia na maneno yale, la hasha! Kwa muonekano wake Mwajabu uliashiria kuwa maneno yale yalimchoma ijapokuwa yeye ndio alikuwa akiyatoa kwenye kinywa chake

    "Sikia Jack. Moyo wangu haupo, hii wazi haupo kabisa na jambo ambalo Mzee analitaka. Hawezi kunichagulia mtu wa kuishi naye mimi. Sijambo nzuri kabisa. Jack moyo wangu haupo kwake kabisa, labda nikwambie ukweli tu. Mapenzi si yakulazimishana, ni tendo la kuridhiana baina ya pande mbili. Naomba unisikilize Jack, huo ndio ukweli. Sipo tayari." Aliongea Mwajabu namna alivyokuwa akiyanena maneno yale kwa hisia kali kabisa yalizidi kunichanganya nisijue cha kufanya kabisa. Nilihisi kama naota kumbe ndio ukweli.

    Nilitafakari kwa kina jambo lile bichi kabisa ndani ya kichwa changu. Ni jana tu ndio Mwajabu aliniambia kule kisimani tulipokutana tukizungumza na mara nyingi sehemu hiyo ndio huwa tunapataga fursa ya kuonana tofauti na sehemu nyingine ndani ya kijiji chetu. Kwa mara ya kwanza ndipo nilipoanzisha mazoea na mdada yule na tangia hapo moyo wangu ulipodondoka ndani ya penzi lake bila mimi kujua kuwa ndio nishapenda, uwiiiii!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimfahamu vyema Mzee wake kuwa ni mkali si masihara, kama pilipili. hana utani

0 comments:

Post a Comment

Blog