Search This Blog

MWANAFUNZI MCHAWI - 4

 







    Simulizi : Mwanafunzi Mchawi

    Sehemu Ya Nne (4)



    "Amka mama Pamela kuna jambo nataka nikuambie"

    "Bwana utaniambia asubuhi"

    "Huu ndo muda mzuri wa kukuambia lakini kama hutaki basi.. " Alisema baba Pamela kwa sauti ya utulivu sana . Licha ya ubishi aliokuwa nao mama Pamela katika suala la kuamka lakini ilimbidi tu aamke ili amsikilize mume wake. Kwani alijua huenda ana jambo muhimu anataka kumueleza wakati ule.

    "Niambie basi mume wangu!" Alisema mama Pamela huku akipiga miayo ya uchovu wa usingizi.

    "Asubuhi ya Leo nina safari kikazi.."

    "Unaenda wapi?" Aliuliza mama Pamela.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Naenda Arusha mke wangu... Nilitemea nikuambie Jana ila uliniudhi mpaka nikashindwa kukuambia"

    "Mmh! Utakaa muda gani?"

    "Mwezi mmoja!"

    "Mwezi mzima? Mbona mrefu hivyo?"

    "Ndio hivyo mke wangu ni masuala ya kazi tu, sina jinsi"

    "Imekuwa ghafla!"

    "Ndio nimepewa taarifa juzi jioni, lakini...."

    "Lakini nini?" Alishtuka mama Pamela

    "Nikiondoka tu, na huyo mgeni wako atoke hapa nyumbani kwangu"



    Alisema Baba Pamela kwa sauti ya msisitizo sana akidhihirisha kuwa alimaanisha kile alichokisema.

    "Baba Pamela utaniudhi.. Sitaki maudhi yako na hiyo roho mbaya yako"

    "IPO siku utafahamu kwanini nasema hivo.. Kaa vizuri na Mungu utafahamu mengi!" Alisema Baba Pamela kisha akajifunika vizuri na kulala ili aamke baada ya nusu saa.



    Mama Pamela alibaki na mawazo mengi sana ila katu hakuwa tayari kumwacha Doreen aende zake. Alimwonea huruma binti yule kwani alishamwambia historian nzima ya maisha yake.' Mime wangu sijui yukoje siku hizi.. Ana roho mbaya.. Simfukuzi ng'oo Doreen. Mtoto ana adabu tena mstaarabu' aliwaza Bi Carolina.



    Asubuhi na Mapema Baba Pamela alijiandaa na kuwahi uwanja wa ndege, Bi Carolina alimsindikiza mumewe hadi uwanja wa Songwe Airport Kisha akamuaga.

    "Ila tekeleza nilichokuambia"

    "Sawa !" Alijibu Bi Carolina kisha akaingia kwenye gari na kuondoa gari kuelekea nyumbani kwake.

    Haukupita muda mrefu Bi Carolina alitia timu nyimbani kwake, akapaki gari na kuingia ndani. Lakini alipoingia ndani alikutana na hali ya utofauti.



    .BI CAROLINA alipiga hatua za taratibu kuelekea sebuleni lakini hali iliyokuwemo ndani mle ilizidi kumshangaza kwani alisikia harufu Kali na mbaya ya kitu kuungulia. Alifika sebuleni lakini hakukuta Mtu yeyote, akaamua kwenda jikoni.



    Alipoingia jikoni tu, alipiga chafya tatu mfululizo kutokana na moshi mzito ulioambatana na harufu Kali sana uliotawala jikoni mle. Aliisogelea mpaka sehemu ya kupikia akagundua moto uliwashwa na kuna kitu kilichomwa. Akaangalia sufuria zote lakini hakukuta kitu chochote, akabaki na mshangao.

    "Doreen!" Aliita Bi Carolina akiwa ameshika mkono kiunoni.

    "Abee mama!" Sauti ya Doreen ilisikika kutoka chumbani.

    "Njoo huku jikoni"



    Bila ya kuchelewa Doreen alifika jikoni kule na kumkuta Bi Carolina akiwa ameshika kiuno akimsubiri kwa hamu amuulize kilichotokea.

    "Abee mama" aliitikia Doreen kwa adabu sana.

    "Nini kimetokea huku jikoni?"

    "Nisamehe mama... Nilitaka kupika.. Ila kwa bahati mbaya nikaunguza kwani sijui kutumia jiko la gesi." Alijitetea Doreen huku akitia huruma sana.



    "Ulitaka upike nini asubuhi yote hii?"

    "Nili...nilikuta maziwa.. Nyama kwenye friji nikataka nipike.."

    "Mara maziwa mara nyama.. Mbona sikuelewi? Haya ulipikia sufuria gani?" Bi Carolina alishindwa kumuelewa Doreen ila kutokana na ugeni aliokuwa nao hakuweza kumfokea sana kwa kuhofu kuwa atajisikia vibaya.

    "Nilichukua nyama... Sufuria ilipoungua sana nikaamua kuiosha.." Alisema Doreen akidai kutetemeka kwa woga.

    "Sawa ila usirudie tena.. Nitakufundisha jinsi ya kupikia jiko la gesi.."

    "Sawa mama" alisema Doreen kwa sauti ya upole iliyojaa hekima ya viwango vya juu.

    "Sawa mwanangu nenda kaendelee na kazi zako"



    Doreen alitoka jikoni mle na kuelekea chumbani kwake. Alichukua kimfuko cheusi kidogodogo kisha akafungua na kuutoa ungaunga mweusi. Kisha akaweka kiganjani na kusogelea kila kona ya chumba kile na kuupuliza kwa midomo yake. Alifanya hivyo mpaka unga ule ilipoisha, akasogelea kitanda chake na kukaa.



    "Hapa sasa nimemaliza kazi... Mpaka huo moshi uishe nitakuwa nimefanikiwa kabisa." Alisema Doreen akitabasamu kwani ule moshi uliotapakaa ndani mle ulisababishwa na Doreen. Alikuwa amechoma dawa ambayo ingewafanya wakaaji wa nyumba ile kumpenda Doreen kupita kiasi, na wasingeweza kumfukuza hata iweje mpaka pale atakapoamua kuondoka yeye mwenyewe.



    Aliangalia SAA yake ya mkononi ilikuwa tayari ni saa nne na nusu asubuhi. Doreen alisikia sauti ya Bi Carolina ikimwita. Akatii wito na kumfuata Bi Carolina.

    "Abee mama" aliitikia kwa heshima.

    "Umeoga?"

    "Bado"

    "Kaoge unywe chai."

    "Sawa mama"

    Doreen alitoka sebuleni pale na kwenda bafuni kuoga. Alipomaliza alipaka mafuta na kuvaa tena nguo alizokuwa amevaa kabla ya kuoga kisha akaenda sebuleni. Akamkuta Bi Carolina akiwa amekaa huku akitazama televisheni.

    "Mbona umevaa nguo chafu?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sina zingine"



    "OK.. Baadae tutaenda Mwanjelwa ukatafute nguo za kuvaa.. Sasa hivi nenda ukanywe chai.." Alisema Bi Carolina.

    "Sawa mama.. Vipi kuhusu Dada Pamela?" Aliuliza Doreen.

    "Atakuja si muda mrefu.. Ameniambia yupo njiani. Baada ya kumwambia hivyo ghafla mlango ukagongwa . Akaingia msichana mmoja mrefu kiasi, mweupe, matiti yenye ukubwa kiasi, kiuno chembamba kama sindano na makalio makubwa kama milima miwili iliyopangana vyema. Wote walishtuka kidogo.

    "Ah Pamela kumbr ulikuwa jirani tu.. Tumekuongelea sasa hivi hapa.."



    "Sikuwa mbali"

    "Karibu sana" alisema Bi Carolina wakati huo Pamela alikuwa akiketi sofani na kuweka pembeni mkoba wake. Kwa muda wote huo Doreen alikuwa akimtazama Pamela katika maeneo ya kifuani.

    "Shkamoo Dada Pamela" alisalimia Doreen

    "Marhaba hujambo? Wewe ndo Doreen?"

    "Ndio.." Aliitikia Doreen huku akimgeukia mama Pamela "kumbe una mtoto mzuri namna hii?" Alisema.

    Bi Carolina na Pamela walicheka tu.

    "Huyu ndo mwanangu mpenzi... Yuko peke yake kama Tanzanite..." Alisema Mama Pamela huku akicheka.

    Doreen aliwaacha wakiendelea na mazungumzo kisha yeye akaenda chumba cha kulia chakula (dinning). Moyoni mwake alifurahi sana kwani kwa uzuri aliokuwa nao Pamela titi lake lilifaa sana kwa kazi ya Doreen.



    ********



    Dorice aliitazama Pete ya Mansoor kwa mshangao kwani hakujua lengo kamili la Mansoor kutaka kuitazama Pete ile.

    "Umeitazama vizuri Pete hiyo?"

    "Ndio"

    "Hii Pete, si kama Pete za kawaida, ina nguvu nyingi sana ambayo inazidi nguvu za kaeaida." Alisema Mansoor kisha akakohoa kidogo ili kusafisha koo lake kisha akaendelea.



    "Pete hii nilipewa na babu yangu ambaye anaishi mbali sana katika sayari nyingine kabisa, alinipa kwaajili ya ulinzi wangu binafsi kwasababu alikuwa ananipenda. Na Mimi nitakupa wewe pete hii kwasababu nakupenda sana, ili ikusaidie katika kumuokoa mtu umpendae sana." Alisema Mansoor huku akimtazama Dorice. Dorice aliendelelea kumsikiliza kwa umakini sana Mansoor.

    "Pete hii ni ya ufalme wangu pale nitakapopewa ufalme na mama yangu... Wewe kwasababu ni mke wangu utakuwa malkia..."

    "Nini?"



    "Unashangaa nini? Sina njia nyingine ya kukusaidia mbali na hii.. Kama upon tayari nitakupa pete hii na utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kijini... Utarudi duniani na utafanya kila unalotaka..." Alisema Mansoor. Maneno yake yalikuwa mazuri masikoni mwa Dorice ingawa yalimpa utata wa kiwango cha juu alijiuliza maswali mengi kichwani mwake juu ya suala la umalkia. Lakini akayapotezea maswali yake kwani alitamani sana kurudi duniani kumuokoa mpenzi wake Eddy na kwenda kwa wazazi wake ambao hakuwaona kwa muda mrefu.

    "Sawa... Nipe tu..!" Alisema Dorice akionesha kukubali masharti ya Mansoor.



    "Nitakupa Mke wangu lakini kuna jambo muhimu unalotakiwa kuzingatia pindi utakapokuwa na hii pete"

    "Jambo Gani?" Dorice alishtuka.

    "Hii ni pete ys heshma sana, ambayo haihitaju uchafu wa aina yoyote.. Kwahiyo ukiivaa na kwenda Nayo duniani hutakiwi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi yangu Mimi!" Alisema Mansoor huku akimtazama mkewe kwa macho yaliyoonesha msisitizo kwa kile alichokizungumza.



    "Mmh!" Aliguna Dorice kwani alikuwa na wazo la kumsaliti Mansoor pindi atakaporudi duniani. Na alikuwa na lengo la kutorudi tena katika himaya ile ya majini. Hivyo basi masharti ya pete ile yalikuwa magumu sana kwake na kumuweka katika wakati mgumu sana.

    "Mbona unaguna?"

    "Kwani hakuna msaada mwingine mbali na hiyo pete" aliuliza Doreen

    "Upo!"

    "UPI.. Nipe msaada mwingine Mansoor tafadhali"

    "Unataka njia nyingine?"

    "Ndio.." Alijibu Dorice haraka.



    **********



    Mr Aloyce alitembeatembea katika eneo lile akimsubiri mkewe atokeze lakini muda ukazidi kwenda Vila kuona dalili yoyote. Mr Aloyce alianza kukata tamaa ya kumpata mkewe akahisi huenda alikuwa anadanganywa tu. Akataka kuondoka lakini moyo wake ulisita sana baada ya kuumbuka msemo usemao "atafutaye hachoki, akichoka keshapata" akaamua kuwa mvumilivu kwani siku zote mvumilivu hula mbivu.



    Ajasogelea eneo tulivu lenye nyasi fupi kisha akaketi pale. Mawazo mengi yalifurika kichwani mwake, "nimekuwa mtumwa... Mtumwa wa nguvu za giza hii hali mpaka lini? Kila siku yanaibuka mapya... Mmh! Yote hii ni kwasababu ya Eddy.. Ila sipaswi kumlaumu" alijiwazia Mr Alloyce huku machozi yakimtiririka.



    Ghafla upepo mkali ulianza kupuliza eneo lile na kumwondoa mawazoni Mr Aloyce. Alinyanyuka pale chini na kutazama juu lakini hakuona chochote.



    Upepo ukazidi kupuliza kwa kasi sana mpaka miti ikaanza kuyumbayumba. Miti iliyumba kwa kasi sana na ile isiyo na nguvu ikaanguka. Mr Aloyce aliogopa sana.

    Baada ya upepo ule radi Kali zikapiga mfululizo, zikazidi kumtisha Mr Aloyce. Alipiga hatua kuelekea kwenye gari yake ili akajifiche mle maana hali ilitishs lakini ghafla akasikia sauti ya kilio kikali.



    "Nisaidie mume wangu.. Nisaidiee!" Mr Aloyce alishtuka sana kwani sauti ile aliijua fika. Ilikuwa ni sauti ya mkewe mpenzi. Akabaki amesimama wima kama mlingoti ili asubiri kitakachoendelea.

    Akiwa bado amesimama alishtushwa na kitu kikipita miguuni mwake, akatulia kimya huku akipiga jicho kutazama kilikuwa kitu gani.



    "Mamaaa" mr Aloyce alipiga ukunga kwa woga na hofu baada ya kuonana uso kwa uso na chatu aliyekuwa akijiviringa kwa kasi mwilini mwake.





    ...... MR ALOYCE alibaki kimya akiwa ametulia kimya kama vile amegandishwa na gundi ngumu. Haja ndogo ilipita taratibu katikati ya mapaja yake na kushuka chini ardhini. Alitamani ardhi ipasuke ili walau akajifiche chini ya ardhi kuliko kuendelea kushuhudia tukio lililokuwa linaendelea kwa wakati ule. Akili ilisimama, mwili ulinyong'onyea kwani hakuwa na lolote la kuweza kufikikiria kwa wakati ule. "Nimekamatika kwenye mtego" ndilo wazo pekee lililomjia akilini mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chatu yule aliendelea kujiviringisha kwa madaha na mbwembwe nyingi mwilini mwa Mr Aloyce na kumfanya mwanaume yule ajihisi mfu aliyebakisha roho yake tu kabla ya mazishi. "Nisaidie Mungu wangu" Mr Aloyce alisali kimoyo moyo akiamini kwamba huenda Mungu atasikia maombi yake na kumkumkumbuka katika Mateso yake. Machozi hayakumtoka hata chembe kwani hofu ilimzidia mpaka chozi lilimkauka.

    Akiwa katika hali hiyo ngumu isiyoelezeka Mr Alloyce hakuona mtu yeyote wala dalili ya kiumbe chochote katika eneo lile. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, ulikuwa kama kimbunga kinachoweza kuleta maafa kwa makazi ya watu. Mr Aloyce alijishangaa sana kuona mwili wake ukiwa mwepesi sana tena umejiachia kupita kiasi. Moyo wake ukafurahi na akatumia nafasi hiyo kujitazama mwilini mwake, akagundua yule chatu hayupo tena mwilini mwake Bali amesogea pembeni kidogo na kujituliza kama gogo.



    Macho yalimtoka kama njugu akimtazama yule Chatu, ghafla akapigwa na mshangao wa ajabu baada yule chatu kubadilika umbile na kuwa na umbo la mtu. Mr Alloyce akamkazia macho MTU yule aliyetokana na chatu. Hakuamini macho yake pale alipogundua mtu yule alikuwa mkewe, Aloyce alitetemeka sana. Ndipo mwanamke yule alipoachia kicheko kikali sana huku akimsogelea Mr Aloyce. "Nilikukumbuka sana mume wangu.. Ila nasikitika unaniogopa" alisema mwanamke yule mwenye sura na umbile la mama Eddy. Mr Aloyce alitetemeka sana, akapiga hatua za kinyumenyume kumkwepa mwanamke yule.

    "Mume wangu! Mbona unaniogopa?" Alisema mwanamke yule.



    ****



    Dorice alimtazama Mansoor na kumsikiliza kwa umakini huku akiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua njia nyingine ya kuweza kuondoka katika himaya ile ya kijini na kurudi duniani ili kumkomboa Eddy mpenzi wake wa dhati.

    Mansoor alimtazama Dorice kwa unyonge sana, sura yake ilidhihirisha huzuni aliyokuwa nayo moyoni mwake. Akasogeza mkono wake na kuushika mkono wa Dorice kisha akausogeza karibu kabisa na midomo yake mizuri. Akaachia mabusu mazito mfululizo huku chozi likimdondoka. Kisha akainua macho yake na kumtazama Dorice.

    "Dorice kwanini hunipendi?" Aliuliza Mansoor. Dorice alimtazama Mansoor bila kujibu chochote.

    "Kwanini hunipendi?" Aliuliza tena Mansoor huku macho yake yakizidi kuwa mekundu kama pilipili. Kisha taratibu machozi yake yalianza kubadilika rangi na kuwa kama damu.

    "Dorice! Naumia sana moyoni mwangu kumpenda mtu asiyenipenda! Najilaumu sana ingawa sio kosa language ila ni kosa la moyo wangu ambao haukumchagua yeyote ila wewe.. Natamani ungejua thamani ya upendo wangu kabla haujaenda duniani ili unikumbuke moyoni mwako" alisema Mansoor huku machozi mekundu yakizidi kudondokea kwenye mikono mizuri na laini ya Dorice. Maneno Yale yaliugusa moyo wa Dorice, akahisi ni mkosaji sana kwa kuutesa moyo wa Mansoor. Machozi yalimlengalenga machoni mwake akajikuta anamkumbatia Mansoor na kumtakia maneno ambayo hakuwahi kumtamkia hata Mara moja.

    "NAKUPENDA SANA MANSOOR" alisema Dorice huku midomo yake ikibusu shingo ya Mansoor kwa huba, na mikono yake ilitembea taratibu mgongoni kwa Mansoor na macho yake yalikuwa yamefumba na kumpa nafasi zaidi ya kuzitafakari kwa kina hisia za mapenzi zilizokuwa kichwani mwake.

    "Asante sana mpenzi wangu... Nakupenda na nitazidi kukupenda milele.." Ilisikika sauti iliyojaa huba na mahaba mazito ya Mansoor.

    "Asante mpenzi... Lakini naomba unisaidie kwa lile suala langu.. Na umesema kwamba kuna njia nyingine.." Alisema Dorice akiwa bado amemkumbatia Mansoor.

    Swali lile lilikuwa kero kwa Mabsoor kwani alijua Dorice hatozungumzia tens suala lile baada ya kumpa maneno matamu zaidi ya asali.

    "Mh! Nitakusaidia... " alisema Mansoor.

    "Lini?"

    "Kuwa na subira... Wala usijali... " Mansoor alimwondoa shaka Dorice. Baada ya muda mfupi Mansoor alimuaga Dorice kisha akatoweka machoni pake huku akimuahidi kuwa atarudi baada ya muda mfupi tu.

    Hazikupita dakika nyingi Mansoor alijitokeza tena kwa Doreen lakini alikuwa na kitu kilichomshtua Doreen na kumfanya aogope sana.



    ******

    Siku ya kwanza ndani ya nyumba ya mama Pamela iliisha vizuri sana wakiwa na Doreen. Usiku majira ya SAA NNE baada ya kula na kutazama televisheni huku wakipiga soga za hapa na pale wakaagana na kila mmoja alienda kulala kwenye chumba chake.

    Usiku ule Mama Pamela alihisi kuna utofauti ambao hakuuzoea kabisa.

    Paka walilia Mfululizo na kumfanya Mama Pamela ahamaki kidogo, sauti ya paka kutoka batini ilisikika ikilia kama mtoto mchanga jambo ambalo lilimtisha mama Pamela. Na haikuwa hivyo kwa mama Pamela tu bali pia hata kwa Pamela kwani alikuwa anaogopa kupita kiasi.

    Ghafla usingizi wa ajabu ukampitia Mama Pamela, macho yalikuwa mazito kiasi kwamba alishindwa hata kuyafumbua ingawa akili yake bado ilikuwa inaendelea kuwaza . akajishangaa na kujiuliza usingizi ule ulikuwa wa aina gani kwani kwa kawaida mtu akilala hata akili pia inalala. Ghafla kitu kizito militia juu yake, akashindwa kupumua vizuri na kila alipojaribu kujiinua alishindwa. Akahisi anakabwa sana shingoni na kila alipojaribu kuinua mkono wake ili ajiokoe alishindwa. Akazidi kuhema kwa nguvu.

    Nusu SAA nzima hali ile ilizidi kumsumbua mpaka aliposhtuka na kukaa kitandani huku jasho likimtoka kwa kasi kana vile yupo jijini Dar kumbe yupo Mbeya kwenye baridi Kali. Alikaa kitandani huku akihema sana ghafla akasikia kishindo kikali sana kilichomshtua na kumfanya atahamaki.

    "Mamaaaa! Mamaa " sauti ya Pamela ilimshtua sana Bi Carolina. Akatamani ainuke kitandani pale ili akamtazame mwanaye, Mara taa ikazimwa. Akajua umeme umekatika lakini kilichomshangaza .........





    .... Leyla alikuwa amechanganyikiwa sana baada ya mumewe kuwa katika Hali ile. Alishindwa kuelewa atafanyaje ili kujimudu katika familia yake kwani Mwalimu John ambaye ni mumewe asingeweza kurudi tena kazini. Kilichomfanya anyong'onyee zaidi ni hali ya Judith kwani hakuweza kuongea wala kusikia. Leyla alikosa raha sana, akakaa kitini akiwa na mawazo mengi sana. Alijiuliza afanye nini ili aweze kuwaokoa wahanga wa tatizo asilojua limetona na nini.



    Akiwa katika kutafakari hayo yote ghafla wazo muhimu lilimjia kichwani mwake. Leyla alichukua simu yake na kutafutw namba fulani kisha akapiga. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa kisha ikakakata. Leyla hakukata tamaa akapiga tena lakini majibu yakabaki Yale Yale, simu haikupokelewa akajaribu tena na tens simu ikapokelewa.



    "Bwana asifiwe mchungaji.." Alizungumza Leyla kwa sauti ya unyenyekevu sana kwani aliyempigia alikuwa ni mchungaji wake.

    "Amen.. Unasemaje?" Alijibu mchungaji yule kama vile hataki kuzungumza.

    "Samahani mchungaji nina shida... Naomba msaada wako!" Alisema Leyla.

    "Shida gani"

    "Kuhusu familia yangu!".



    "Kama ni mumeo mama... Chukua imani hapo ulipoanza maombi Mimi sina muda... Nina mambo mengi ya kufanya.." Alisema mchungaji yule kwa ukali kiasi jambo lililomtisha sana Leyla kwani hakutegemea kama mchungaji wake angemjibu vile.



    "Pastor! Tafadhali nisaidie.." Leyla alimbembeleza mchungaji lakini hakumuelewa. Na mchungaji huyu ndiye aliyefanya mazishi ya mwalimu John.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Kwasasa sipo nyumbani.. Nipo mbali kikazi..." Alisema Mchungaji yule. Kiukweli ilikuwa vigumu kwa Leyla kuamini maneno ya mchungaji wake kwani Siku zote aliamini mchungaji wake angekuwa ndiye mfariji lakini haikuwa hivyo.

    "Cha kukusaidia labda nitawaita wanamaombi waje kukusaidia" alisema mchungaji na kukata simu.



    Leyla alishindwa afanye nini kwani hata ndugu zake walimtenga. Ilipita nusu SAA nzima , mlango wake ukagongwa. Alifurahi sana kwani alijua tayari mchungaji amewasiliana na wanamaombi ili waje kuombea familia yake. Alinyanyuka kitini na kwenda moja kwa moja kufungua mlango.



    *****



    Mama Pamela alizidi kutetemeka kwa woga sana, alijikunyata kama mgonjwa kitandani kwake. Lakini alizidi kuisikia sauti ya mwanae ikiendelea kumwita. Mama Pamela akazidi kupata hofu, japo aliogopa sana lakini aliamua kuinuka kitandani na kunyata taratibu kuelekea chumbani kwa Pamela. Na hii ni kwa sababu damu nzito kuliko maji .



    Nyumba ilitawaliwa na kiza kizito sana, hivyo ilimpa shida sana Mama Pamela kuelekea chumbani kwa mwanae. Aliingia chumbani kwa Pamela na kuita taratibu "Pamela! Pamela!" Lakini Pamela hakuitikia. Mama Pamela alisogelea kitanda cha Pamela na kuanza kupapasa papasa lakini cha ajabu hakuona dalili zozote za uwepo wa mtu kitandani pale. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa sana.



    Akaita tena "Pamela! Pamela!" Lakini bado hakukuwa na sauti yoyote iliyoitikia. Mama Pamela alihisi akili yake inavurugika. Akauvua woga wake na kumuita Pamela kwa sauti kubwa lakini bado hakuitikia.



    Mama Pamela alirudi chumbanu kwake na kupapada sehemu ilipokuwepo simu yake na baada ya kuipata alimshukuru Mungu. Kisha akawasha tochi na kuanza kumulika kila chumba.



    Aliingia chumba cha kwanza akamulika lakini hakuona MTU, akamulika, cha pili, cha tatu na kisha akaingia jikoni lakini bado hakumuona Pamela. Roho ya Mama Pamela iliingiwa simanzi, akajua mwanaye amepotea kwa mazingira ya kutatanisha . akaingia bafuni na kumulika lakini Hakumkuta Pamela. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa zaidi.



    "We Mungu bora wangenichukua Mimi sio mwanangu Pamela," alisema Mama Pamela akiingia chooni.

    Mama Pamela alistaajabu sana alichokutana nacho. Alimkuta Pamela akiwa amelala chooni huku kajifunika blanketi lake vizuri."

    "Pamelaa!" Aliita mama Pamela kwa mshangao na mpaka wakati huo mama Pamela hakujua Doreen anaendeleaje.



    ****



    Mr Alloyce alibaki njia panda, alikuwa haelewi cha kufanya juu ya mwanamke yule. Alijiuliza amkubalie kama mkewe au asimwamini? Mawazo yake hayo mawili yalimezwa na ukarimu wa mwanamke yule kwa jinsi alivyoonesha kumjali Mr Aloyce.



    "Mime wangu... Mbona hunichangamkii? Baba Eddy jamani" alisema mwanamke yule na kumsogelea Mr Aloyce "hivi kweli we ni Mke wangu? Mama Eddy?" Aliuliza Mr Alloyce kwa wasiwasi.



    "Kha! Kumbe huniamini mume wangu?" Alisema

    "Mbona ulitokea kama Chatu?"

    "Hahahah unatakiwa kuniamini mume wangu!" Alisema mwanake yule na kumsogelea Baba Eddy kisha akamkumbatia.



    Mr Aloyce alitamani kumwamini mwanamke yule kama ndo mkewe lakini moyo wake ulisita. Alimsogelea na kumkumbatia lakini moyoni make alikuwa na mashaka sana.

    "Nakupenda mume wangu.. Naomba tuwahi nyumbani ili nikamwone mwanangu" alisema mama Eddy.



    "Sawa" alisema Baba Eddy huku akifungua mlango wa gari.

    "Lakini unanishangaza mume wangu?"

    "Nakushangaza na nini?"

    "Huna amani moyoni mwako.. Kwanini?"

    "Usijali Niko sawa..."



    Wallingia kwenye gari kisha Mr Aloyce aliwasha gari na kuanza kuendesha. Aligeuka kumtazama mkewe yule aliyekuwa ameketi pembeni yake, lakini kuna kitu kilimshangaza.....



    .MR Aloyce alizidi kumkazia macho mkewe akahisi ni mrembo zaidi ya Mama Eddy yule anayemfahamu yeye. Halafu alikuwa na madaha sana kuzidi vile alivyomzoea. Wasiwasi ukamtanda akilini make na kumfanya asimwamini sana mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi.



    "Mbona unaniangalia sana? Umemisi busu langu nini?" Aliuliza Mama Eddy.

    "Hapana wala usijali"

    "Ok kama wewe hukumiss basi Mimi nilimisi sana kiss lako mpenzi".



    Alisema Mama Eddy huku akimsogelea Mr Aloyce kwa ukaribu zaidi na kumshikashika kidevu kwa mahaba. Mr Aloyce alionesha kutojali mguso ule aliopapaswa na mikono laini ya mkewe. Hakuelewa ni sababu zipi zilizomfanya asimjali mwanamke yule kwa kiasi kile ila moyo wake ulikuwa mzito sana.



    "Baby mbona hivyo...? Embu usiwashe gari kwanza mpaka unibusu" alisema Mama Eddy kwa sauti iliyojaa mdeko wa kimahaba. Mr Aloyce hakutaka kukiri udhaifu, akaachia usukani na kusogeza mdomo wake karibu na mdomo wa mkewe kisha akambusu.



    Busu lile lilimpa nafasi nzuri sana Mama Eddy ya kupenyezapenyeza mpaka kuingiza ulimi wake mdomoni kwa Mr Aloyce. Kisha wakabadilishana mate yao kwa mahaba. Lakini wakati tendon hilo likiendelea, Mwanamke yule alimwachia vitu Fulani Mr Aloyce bila yeye mwenyewe kujua. Na ilikuwa ni dawa Kali ya kumfanya Mr Aloyce amwamini mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi wakati hakuwa yeye. Alikuwa ni mwanamke kutoka himaya ya akina Doreen na alitumwa nyumbani kwa Mr Aloyce ili afanye kazi muhimu sana aliyotumwa.



    Kwa vile alivyomfanyia Mr Aloyce, alifanikiwa kuziteka akili za Mwanaume yule. Baada tu ya busu lile la huba, Mr Aloyce alijkuta akimpenda sana mwanamke yule akijua ndie Mkewe halisi na kumbe haikuwa hivyo. Wasiwasi wake ulifutika kichwani mwake, pendo la dhati likatawala moyoni mwake.



    "Tuondoke mume wangu" alisema mama Eddy kwa sauti ya upole iliyojaa huba huku akiwa ameachia tabasamu pana usoni mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Usijali mke wangu.. Nilikukumbuka sana... Nina imani hata mwanetu anakusubiri kwa hamu sana." Alisema Mr Aloyce huku akishikilia vizuri usukanu na kuondoa gari kwa kasi sana.



    Mr Aloyce aliendesha gari kwa kasi ya ajabu na baada ya masaa machache tu waliwasili eneo la Ipogoro Iringa kisha wakaelekea nyumbani kwao.



    Walifika getini wakapiga honi geti lilifunguliwa. Mr Aloyce aliegesha gari pembeni kisha akashuka kwa furaha kubwa, na baada ya hapo akaelekea upande wa pili wa gari yake na kumfungulia mkewe huku tabasamu mwanana likiwa limechanua mdomoni mwake.



    "Shuka malkia wangu... Tumeshafika kwetu.." Alisema Mr Aloyce huku mwanamke yule anayefanana kwa kila kitu na Mama Eddy akishuka kwa madaha kisha akamkumbatia Mr Aloyce na kumbusu. Wakati yote hayo yakiendelea Mlinzi alikuwa pembeni yao akishuhudia penzi la zamani lililochipua upya tena kwa kasi ya ajabu.



    "Mh bosi naona mama Amerejea.." Alisema mlinzi kimzaha.

    "Ndio.."alijibu Mr Aloyce kwa furaha.

    "Baby nataka kuongea jambo na mlinzi wetu naomba utuache kidogo.." Alisema Mama Eddy.

    "Ok ila kuwa makini tu nisije kupinduliwa na houseboy.." Alisema Mr Aloyce na kuondoka zake huku akimsisitiza mkewe asichelewe.



    Baada ya Mr Aloyce kuondoka pale, Mwanamke yule alimsogelea mlinzi na kumtazama kwa ghadhabu Kali. Hali hiyo ilimtisha sana mlinzi na kumfanya ajiulize maswali mengi ambayo alishindwa kujijibu mwenyewe.



    ****



    Mama Pamela aliishiwa nguvu kabisa. Alijiuliza sana ni kwanini mwanaye amelala chooni kule ilhali ana kitanda kizuri cha kumfaa? Maswali yake hayakuwa na majibu akajikuta anaishia kupiga makofi kwa mshangao.



    "Pamela!" Alimwamsha mwanae ambaye bado alionekana ana usingizi mzito sana. Alimtikisa tikisa mpaka alipofanikiwa kumwamsha kabisa. Pamela aliinuka, lakini alibaki mdomo wazi baada kuona mazingira aliyopo si ya kitandani kwake.



    "Mama nipo wapi hapa? Mbona kama chooni?" Aliuliza Pamela kwa mshangao.

    "Nikuulize wewe mwanangu.. Umefikafikafikaje mpaka ukalala chooni?" Aliuliza Mama Pamela.

    "Mbona sielewi mama" alisema Pamela.

    "Haya chukua hilo shuka lako twende chumbani.. Hayo mengine tutajua huko huko.."



    Walitoka chooni mle na kuelekea chumbani kwa mama Pamela. Pamela alitoa nguo aliyokuwa amevaa kwaajili ya kulalia kisha akavaa nyingine kwani ile tayari ilishapata unyevunyevu wa chooni.

    "Lakini mama mbona Doreen hatujaenda kumwangalia si atahisi tunamtenga.." Alisema Pamela.

    "Ila kweli"



    "Tumfate basi.." Alisema Pamela kisha wakainuka na kwenda chumbani kwa Doreen. Kulikuwa na Giza totoro ambalo bila msaada wa tochi basi wasingeona chochote. Walimulika kitandani kwa Doreen na kumwona Doreen akiwa amelala fofofo. Walimsogelea kwa ukaribu na kumwamsha lakini Doreen hakuitikia. Pamela na mama yake walitazamana mshangao.



    "Mbona haamki?" Walinong'ona taratibu.

    "Isije ikawa ndo amek.. Amepata matatizo mengine" alisema Pamela.

    "Doreen! Doreen" Mama Pamela aliita kwa sauti kubwa lakini Doreen bado hakuamka.



    "Tumuache basi tutamkuta kesho yawezekana mwenzetu hajakumbwa na mauzauza" alisema Pamela kisha wakarudi chumbani kwa Mama Pamela kupumzika kidogo maana Pamela asingeweza kulala peke yake kutokans na woga aliokuwa nao kwa usiku ule.



    *****



    "Umeshika nini hicho Mansoor" aliuliza Dorice kwa woga .

    "Nimeshika Pete" alijibu Mansoor. Jibu hilo lilimshangaza Dorice kwani alichokiona mkononi kwa Mansoor haikuwa Pete Bali alikuwa nyoka mkubwa aliyejiviringisha kama Duara kiganjani kwa Mansoor.



    "Pete gani hiyo?" Dorice alizidi kuogopa.

    "Ni pete ya kukupa wewe ili uwe na nguvu ya kurudi duniani na kufanya lolote utakalo..."

    "Mbona namuona Nyoka?"

    "Fumba macho kisha ufumbue nikikuruhusu" alisema Mansoor kisha Dorice alifanya kama alivyoambiwa.

    Mansoor alisogeza mkono wa Dorice kisha akchuku kidole Chanda na kumwambia Dorice afumbue macho yake.

    Dorice alifumbua macho yake na kutazama kidole chake. Alishtuka kuona pete inayong'aa sana kidoleni mwake.



    "Umenivisha SAA ngapi?" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nimekuvisha ulipofumba macho"

    "Mbona sikuhisi chochote? Na je yule nyoka yuko wapi?"

    "Sikushika nyoka.. Nilishika pete" alisema Mansoor.



    Ghafla Dorice alijiona wa tofauti sana. Kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi sana, akaanza kulalamika. Na kadri alivyolalamika ndivyo kadri maumivu yalivyomzidia.



    Machozi yalianza kuchuruzika lakini cha ajabu, matone ya machozi yake hayakuwa ya kawaida kwani kila tone alilodondosha lilikuwa damu. Dorice alijishangaa sana lakini Mansoor akaangua kicheko kikali kilichomshangaza Dorice.





    .Dorice aliendelea Julia huku matone yake ya machozi yakiwa damu. Ghafla akajikuta ana uwezo wa ajabu ambao hajawahi kuufikiria kuwa nao hata siku moja. Alijibadilisha sura na kuwa kiumbe wa kutisha, macho yalikuwa kama ya paka, uso wake ukawa mweusi tii kama mkaa, kucha zake zikawa ndefu sana na meno yake mawili yalichomoza nje ya kinywa chake. Mansoor alicheka kicheko kikali cha kutisha huku sauti ya kicheko chake ikiambatana na mwangwi. Radio zikapiga mfululizo Dorice akatoweka ghafla na kumuacha Mansoor.



    Pete aliyokuwa amevalishwa Dorice ilimpa uwezo mkubwa na wa ajabu. Alipata uwezo wa kupotea na kujibadilisha kadri atakavyo lakini sharti kubwa alilotakiwa kufanya ilikuwa ni lazima arudi tena kwa Mansoor baada tu ya kumaliza kazi yake inayompeleka duniani.



    Dorice alikuwa ametokeza katika eneo lenye Giza Giza lilitawaliwa sauti za wadudu. Palikuwa na utulivu mkubwa sana , kwani eneo lile halikukaliwa na mtu yeyote zaidi ya ndege, wadudu na wanyama wadogo wadogo. Dorice alibaki anajishangaa, alijiuliza amefika vipi eneo lile akiwa peke yake bila Mansoor.



    "Ina maana nimekuwa na nguvu za kijini?" Alijiuliza Dorice. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, Dorice alitazama huku na kule ili kujua nani alikuwa mgeni wake kwa wakati ule. Ghafla Mansoor akajitokeza akiwa anacheka kicheko cha kutisha sana kisha akapiga hatua za taratibu kumsogelea Dorice.



    "Kwanini umefika huku?" Aliuliza Mansoor kwa ghadhabu.

    "Sijui nimefikaje" alijibu Dorice.

    "Muda wako wa kuondoka kwenye himaya yangu bado Dorice, nilikuwa na jaribu kukupa ladha ya vile utakavyokuwa baada ya wakati kutimia" alisema Mansoor.

    "Kwahiyo unataka nirudi?"

    "Ndio.. Tunarudi wote".



    "Hapana Mansoor sitaki kurudi tena Kule" alisema Dorice.

    "Ni lazima urudi maana bado sijakupa maelekezo"

    "Hayo maelekezo nipe hapa hapa"

    "Haraka haraka ilimfanya chura apate ngozi ya mabaka"

    "Hata hivyo siwezi kurudi".



    Yalizuka mabishano makali baina ya Dorice na Mansoor kwani Dorice hakutaka kurudi kwenye himaya ya Mansoor tena. Alitaka aachwe huru na arudi kwao, lakini mkongwe ni mkongwe tu licha ya mabishano Yale Mansoor aliibuka mshindi baada ya kumchukua Dorice kinguvu kwa kutumia uwezo mkubwa wa kijini alionao. Katika eneo walilokuwepo ukatokea upepo mkali na kuwavuta wote wawili kisha ndani ya muda mfupi walijikuta wametokea katika himaya ya akina Mansoor. Dorice alikasirika sana.



    *****



    "Mama mbona sikuelewi" aliuliza mlinzi kwa hofu huku akimtazama Mama Eddy kwa woga.

    "Wewe!" Alisema mama Eddy akiwa amevimba kama mbogo huku akimsonta mlinzi yule kwa kidole chake na kumfanya mlinzi yule atawaliwe na hali ya sintofahamu.

    "Nimefanya nini mama?".



    "Kaa mbali na Eddy... Nakusisitiza Tena kaa mbali na Eddy la sivyo utakiona cha mtema kuni paka shume wewe!"alisema Mama Eddy huku akipiga hatua na kutaka kuondoka.



    Alitembea kwa hatua chache tu kisha akamgeukia tena mlinzi na kumuonya vikali kuwa asiwe karibu na Eddy. Mlinzi yule hakuelewa mwanamke yule ana maana gani kumwambia vile. Alibaki na maswali mengi kichwani mwake huku akimsindikiza kwa macho mwanamke yule aliyejongea taratibu machoni mwake baada ya kuingia ndani ya jumba la kifahari la Mr Alloyce. Mlinzi aliachana na mwanamke yule kisha akaendelea na kazi zake za kupunguza maua.



    Mama Eddy aliingia ndani na kumkuta Mr Aloyce akiwa ameketi kwenye sofa huku uso wake ukidhihirisha furaha kubwa aliyonayo moyoni mwake. Alifurahia sana kurudi kwa mkewe katika familia yao ili waendelee kuijenga na kuidumisha furaha yao ikiwa ni pamoja na kutafuta tiba ya tatizo la mtoto wao wa pekee.



    "Mwanangu yuko wapi?" Aliuliza Mama Eddy huku akitabasamu. Baba Eddy alinyanyua kichwa chake na kupaza sauti yake akimwita mwanaye. Bila kuchelewa Eddy alirudi sebuleni na kumkumbatia mwanamke yule aliyedhani ni mama yake.



    "Mama bora umerudi.. Tulikuwa wapweke sana humu ndani!" Alisema Eddy na kumfanya mwanamke yule atabasamu kwa furaha.

    "Nimerudi mwanangu" alisema mwanamke yule. Familia ile ikarejewa na furaha iliyokuwa imepotea ndani ya muda mfupi uliopita.



    Wakiwa wameketi sebuleni pale kwa utulivu wa hali ya juu, ghafla simu ya Mr Aloyce iliita, akaitoa mfukoni na kuangalia nani alimpigia. Alipotazama tu akaona namba aliyoisevu "Shem Dar" akashtuka kidogo kisha akapokea.



    "Ndio..ndio shemeji!" Alisema.

    "Nipo njiani na sio muda nafika hapo nyumbani" ilisikika sauti ya Dada yake Mama Eddy.

    "Unakuja hapa kwangu?"

    "Ndio.. Si ulisema kuna matatizo!"

    "Mh Haya karibu"



    Baada ya mazungumzo hayo simu ikakatika ndipo Mr Aloyce akaona si vyema kumficha mkewe kuhusu jambo lile. Akamweleza kila kitu kuhusu chanzo cha Dada yake kufika nyumbani kwao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ulimwambia kuna tatizo gani?" Alisema mama Eddy kwa mshangao.

    "Nilimwambia tu kuna tatizo na sikumweleza ni tatizo gani. "

    "Vizuri! Akija hapa usimweleze chochote kuhusu suala la Eddy" alisema Mama Eddy. Kauli hiyo ilimshtua Mr Aloyce kwani hakuona haja ya kumficha shemeji yake kuhusu jambo lile.



    "Kwanini nisimwambie? Hujui kama anaweza kutusaidia.. Pengine hata kwa ushauri..." Alisema Baba Eddy.

    "Nimesema usimwambie chochote.." Alisema Mama Eddy na kuinuka kitini kisha akaondoka sebuleni pale na kuwaacha Mr Aloyce na Eddy.



    Mr Aloyce alibaki na mshangao sana kwani alikumbuka jinsi ambavyo Mama Eddy wanavyopatana na kuelewana kama mapacha iweje Leo amfiche matatizo yake?. Alishindwa kuelewa sababu akabaki kimya kitini pale.



    *****



    Mama Pamela na mwanaye waliendelea kuusubiri usingizi uwachukue ili kupambazuke haraka. Usingizi ulichelewa sana kuwachukua lakini haukuwaacha kabisa. Baada ya kuusubiri kwa muda mrefu wakiwa na hofu kupita kiasi hatimaye usingizi ukawapitia. Kila mmoja alilala fofofo kutokana na uchovu pamoja na mihangaiko mingi iliyosababishwa na mauzauza ya usiku ule.



    Hatimaye kukapambazuka lakini bado wanafamilia ile walikuwa wapo katikati ya usingizi. Mlango wa chumba iligongwa na kumfanya mama Pamela ashtuke usingizini na kusikiliza nani aligonga.



    "Mama" sauti nyororo ya Doreen ilipenya masikioni mwa Mama Pamela ikiwa na wingi wa adabu na upole uliokithiri. Bila kusita mama Pamela Aliitikia wito na kumsikiliza Doreen anahitaji nini.



    "Hauendi kazini? Pia Dada Pamela haendi shule?" Aliuliza Doreen.

    "Hatuendi... Wote tupo likizo.." Alijibu Mama Pamela .

    "Sawa mama.. Nilifikiri mmesahau.. Ngoja niendelee na kazi"

    "Hebu njoo kwanza.." Mama Pamela alimwita Doreen na kutaka aingie chumbani.

    "Abee mama" Doreen aliitika kwa heshima na kusogelea karibu kabisa na kitanda cha Mama Pamela.



    "Hivi usiku ulilala salama?"

    "Ndio kwani vipi?" Aliuliza Doreen kwa mshangao.

    "Mh! Kweli?"

    "Ndio.. Kwani nini kilitokea"

    "Duh basi kama ulikuwa salama sawa... Hakuna tatizo!" Alisema mama Pamela.



    Doreen alijifanya kushangaa kupita kiasi, lakini hakuuliza zaidi. Aliachana nao na kwenda jikoni kuandaa chai.Alichemsha maji na kuweka majani ya chai. Na baada ya kuhakikisha imechemka vizuri akaiipua vizuri kisha akatemea mate halafu akaiweka kwenye chupa ya chai huku akicheka.



    "Mtakoma mwaka huu..." Alijisemea Doreen kisha akapeleka chai mezani. Akarudi jikoni na kuchemsha maini ya ng'ombe lakini alipokuwa akichemsha maini yale alichanganya na maji Fulani yaliyokuwa kwenye kichupa Fulani kidogo.



    "Na mtakula sana uchafu wangu... Huu mkojo tu! Bado vingine vinakuja" alisema Doreen kwa sauti ya chini.Maini Yale yalichemka vizuri na kutoa harufu ya kuvutia sana. Baada ya kuyaivisha vizuri akachukua mayai ns kuyakaanga vizuri kisha akapeleka mezani na kuandaa vizuri.



    Majira ya saa tatu asubuhi Mama Pamela na mwanae waliamka. Wakaoga na kwenda chumba cha kulia chakula.

    "Doreen kumbe umeshaandaa kila kitu" alishangaa Mama Pamela.

    "Ndio mama! Karibuni" Aliitikia Doreen.

    "Asante.." Alisema mama Doreen huku akiketi na kusogeza karibu mikate, akaipaka blueband.



    "Mbona wewe huji kula?" Alimuuliza Doreen.

    "Mimi tayari.. Hivyo ni kwaajili yako na dada Pamela"

    "Oh sawa.. Mwite Dada yako aje kula maana ni mvivu kweli" alisema mama Pamela huku akianza kukishughulikia chakula kile. Punde tu Pamela naye akaenda mezani pale na kuanza kula.



    Wakati huo Doreen alikuwa pembeni yao akiwatazama jinsi wanavyokula chakula kile kichafu. Aliwasikitikia sana moyoni mwake lakini wao walimmwagia sifa tele kwa utamu wa chakula kile. Kila mmoja alimsifu Doreen kwa kumwambia ni fundi wa Mapishi.



    "Doreen mwanangu.. Nataka nikuulize kitu" alisema Mama Pamela huku akimeza funda moja la chai na kutua kikombe taratibu kwenye meza nzuri na safi ya kioo. Kauli ile ilimshtua kidogo Doreen na kumfanya amuulize vizuri mama Pamela.

    "Kitu gani mama?"



    ..Doreen alimsikiliza kwa Umakini mama Pamela ili ajue ni swali gani analotaka kuuliza. Mama Pamela alikaa vyema kisha akakohoa kidogo na kumtazama Kwa makini Doreen.

    "Niulize Tu mama" alisema Doreen.



    "Hivi ni kitu gani unapenda nikufanyie ili moyo wako ufurahi? Maana nimependa sana heshima na adabu uliyojaaliwa." Alisema mama Pamela.



    "Kiukweli mama Mimi napenda sana unitafutie shule.. Ili niweze kusoma na kufikia malengo yangu" alisema Doreen.

    "Shule tu? Wala usijali wiki ijayo nitakuwa tayari nimetafuta shule kwa ajili yako.."



    "Nitafurahi sana mama..."

    "Unapenda shule ya kutwa au bweni?"

    "Yoyote tu itanifaa" alisema Doreen.

    Suala lile lilimfurahisha sana Doreen, aliendelea kuishi kwa kunyenyekea sana ndani ya nyumba ile, lakini katika ulimwengu mwingine alikuwa ni mtu jeuri na katili kwa familia ile. Kila Mara aliliwinda sana titi la Pamela, alitamani kulipata kwa udi na uvumba lakini kwa bahati mbaya ilikuwa vigumu kulipata. Alitumia kila namna lakini bado hakuelewa sababu ya kushindwa kulipata titi la Pamela.



    Hasira zilimuwaka sana Doreen pale alipoingia chumbani kwa Pamela usiku na kutaka kumkata titi lake. Alikuta Pamela amelala usingizi mzito sana, akampulizia dawa ili usingizi ule uzidi kuwa mzito zaidi kisha akamsogelea taratibu akiwa ameshikilia panga Kali lililofungwa kaniki nyeusi na nyekundu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Doreen alitamka maneno ambayo aliyajua mwenyewe kisha akamfunua shuka Pamela na kusogeza kisu chake karibu na titi la Pamela. Hakuwa na hofu kama kazi yake haitofanikiwa kwani alikuwa anajiamini na alikiamini kile alichokifanya. Lakini kwa bahati mbaya sana kila alipotaka kumgusa Pamela na upanga ule, Doreen hakuona chochote kitandani pale. Alijaribu tena na tena lakini bado hali ikaendelea kuwa vile vile. Doreen alikasirika sana, akatupa chini upanga ule mlio wake ukamshtua Pamela usingizini.



    Doreen alishtuka sana baada ya Pamela kushtuka usingizini, akakimbia haraka na kujibanza kwenye kona moja ya chumba kile kisha akatamka maneno Fulani ya kichawi halafu akatulia kimya.



    Pamela aliangaza macho huku na kule chumbani mle lakini hakuona kitu, akainuka kitandani na kuwasha taa kisha akaangalia kila sehemu ya chumba kile lakini hakuona chochote. Akatoka na kwenda msalani, alipokuwa anajisaidia haja ndogo akahisi kuna mtu anamfuata nyuma yake Pamela alishtuka na kuogopa sana kisha akakumbuka jambo muhimu la kufanya kama alivyoambiwa na baba yake. Pamela akasali kwa sauti ya chini na kwa imani kubwa sana kisha akajisaidia na kurudi kitandani, akalala bila kuzima taa.

    Doreen alikasirika sana baada ya kumkosa Pamela kwa Mara nyingine. Akaamua kurudi chumbani kwake kupitia kona ile ile aliyokuwa amejibanza.



    Doreen alitokea chumbani kwake akiwa na hasira sana. Alijituliza kimya akiwa amekaa chini sakafuni huku akiwa ameshika tunguli na hirizi mkononi mwake. Aliamua kuita mizimu ya kwao ili iweze kumsaidia katika hali ngumu aliyonayo.



    Ndani ya sekunde chache alitokea mwanamke mmoja Mzee sana. Kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi lakini hakuvaa nguo yoyote isipokuwa kaniki nyeusi aliyovaa kiunoni pamoja na shanga nyingi sana alizokuwa amevaa kiunoni mwake na shingoni. USO wake ulikuwa na makunyanzi mengi sana yaliyokuwa yametawaliwa na vitu kama unga unga mweupe. Alipotua tu chumbani kwa Doreen, nyumba nzima ilitikisika kwani alikuwa ni mtu mkubwa sana katika himaya ya uchawi ya akina Doreen.



    "Karibu! Karibu! Mama mtukufu! Mkuu wa wachawi wote! Mwenye nguvu kuliko wote duniani!" Doreen alimkaribisha mgeni wake yule kwa heshima kubwa sana. Yule bibi hakutoa sauti yoyote zaidi ya Kuitikia kwa kichwa tu huku akimsogelea Doreen kwa kutumia makalio yake.



    "Doreen! Tangu tumekutuma huku duniani hujawahi kuniita isipokuwa Leo.. Najua una jambo zito linalokusumbua"

    "Ndio! Ndio! Mtukufu"

    "Sasa inabidi tutoke humu maana si mahali sahihi"

    "Sina pingamizi Bi Tatile! Kipenzi cha wachawi wote" yule Bibi alimshika mkono Doreen kisha taratibu kwa kutumia makalio yao wakasogelea kona ya kushoto kwao. Kisha wakatoweka ndani ya jumba lile. Lakini kitandani kwa Doreen waliacha mwili wa Doreen pekee na hata kama angeamshwa kwa kipindi kile basi asingeweza kuamka .



    Safari ya wawili wale kwa kutumia usafiri wa ungo huku dereva akiwa Bi Tatile iliwafikisha mpaka eneo la makaburini ambapo walitua na wakaketi hapo kisha wakaendelea na kikao chao kifupi kilichotokea kwa dharula.



    "Sema mjukuu wangu.. Mimi ndo Tatile binti Matatila mwenye uwezo wa kubadili nyasi za kijani zikawa nyeupe.."

    "Mtukufu lile suala la kupata titi naona linakuwa gumu sana kwangu.. Nimekamilisha kila kitu lakini bado hilo tu.. Tafadhali naomba unisaidie kwa hili..."



    "Ha ha ha hah Doreen wewe una uwezo mkubwa sana wa kukamilisha hilo.. Unaweza ukafanya hivyo haraka sana ila kuna jambo moja tu! Unatakiwa ufanye."

    "Jambo gani mtukufu? Niambie tu maana nimechoka kuhangaika" alisema Doreen.



    ****



    Majira ya saa kumi na moja jioni Dada wa Mama Eddy aliwasili nyumbani kwa Mr Aloyce. Alipokelewa vizuri sana na Bwana Aloyce pamoja na Eddy lakini ilikuwa tofauti sana kwa mama Eddy kwani alimkaribisha Dada yake kama vile alimkaribisha adui yake ndani ya nyumba. Suala hilo liliibua maswali mengi sana kwa Mr Aloyce pamoja na mgeni wao.



    "Mama Eddy.. Nakuomba chumbani Mara moja..." Alisema Baba Eddy kisha akaingia chumbani. Mama Eddy alimfuata mumewe ili amsikilize kile anachotaka kumweleza.

    "Mke wangu... Mbona unaniabisha kwa shemeji yangu?"

    "Kivipi?"

    "Dada yako amekuja lakini unamsalimia kama hutaki vile.. kwanini?" Aliuliza baba Eddy kwa mshangao.



    "Nimejisikia tu.."

    "Hapana mke wangu usiwe hivyo... Nakuomba basi onesha kumjali mgeni tena nduguyo wa damu.."

    "Siwezi kumjali mchawi mkubwa yule..." Alisema mama Eddy akiwa anajishumburua midomo yake kwa dharau.

    "Unasemaje? Dada yako mchawi kivipi?"

    "Amemroga mwanangu..."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Umejuaje au nawewe mchawi? Maana haiwezekani umtuhumu mwenzio mchawi wakati huna uhakika?" Alisema Baba Eddy kwa hamaki. Hakutaka kuamini kile alichokisa mkewe.

    "Leo hii unaniambia mimi mchawi? OK sawa... " alisema Mama Eddy na kwenda sebuleni kwa hasira.



    Alisimama wima akiwa ameshika mkono kiunoni huku akimtazama dada yake kwa dharau.

    Dada yake alipigwa na butwaa sana, alibaki anamshangaa mdogo wake kwa vitendo vya dharau anavyomfanyia.

    "Wewe!" Alisema Mama Eddy.

    "Naomba utoke kwenye nyumba yangu.. Ulichomfanyia Eddy kinatosha..."

    "Mimi?"



    "Kumbe naongea na nani kama sio wewe mpumbavu..." Alisema Mama Eddy akidhihirisha chuki kubwa aliyonayo moyoni mwake. Eddy alimtazama mama yake kwa mshangao sana akiwa haelewi sababu ya mama yake kumfanyia unyama ule dada yake wa damu. Hakuna aliyefahamu ukweli kuwa yule hakuwa mama Eddy halisi.



    "Mama... Mama mkubwa amekosa nini?"

    "Hebu kelele huko na wewe.. Hujui kama huyu ndo aliyekuroga?"

    "Sio huyu mama..." Eddy alimtetea.

    "Hebu ondoka hapa.. Kwanza hayakuhusu.." Alifoka Mama Eddy.

    "Sasa na mimi naondoka na mamkubwa.. Sibaki hapa?" Alisema Eddy.

    Wakati huo Mr Aloyce alifika sebuleni pale na kuanza kumuomba msamaha mgeni yule asiye na hatia....



    .... Shule ya sekondari Mabango ilikuwa na utulivu wa hali ya juu tangu Doreen alipoondoka shuleni pale. Licha ya kwamba kulikuwa na upungufu wa walimu lakini hali ilikuwa shwari kabisa. Wanafunzi waliendelea na masomo yao kama kawaida huku wakimshukuru Mungu kwa kuwaondolea mbaya wao aliyeisumbua shule ndani ya muda mfupi tu.





    Majira ya saa saba mchana katika shule ile alifika Mwanaume mmoja wa makamo akiwa ameambatana na mwanamke mmoja mwembamba mrefu. Wanafunzi wa shule waliokuwa karibu waliweza kugundua kuwa mwanamke yule bila shaka alikuwa ni mama yake Dorice kwa jinsi walivyofanana. Nadia Joseph aliyekuwa anapita eneo lile la ofisi aliwasalimia kwa heshima kisha akasimama kidogo huku akitafakari jambo alilotaka kuzungumza.



    "Samahani mama.. We ni ndugu yake Dorice.." Aliuliza Nadia huku akitabasamu.







    "Ndio.. Ni mama yake mzazi.." Alijibu mama yule.



    "Oh mmefanana sana... Vipi lakini hajambo?" Aliuliza Nadia akiwa anatabasamu lakini swali lile lilikuwa kama mwiba mkali moyoni mwa Mama Dorice kwani ujio wake pale shuleni ilikuwa ni kumfuata Dorice na kupata taarifa zake kwani ulipita muda mrefu sana bila mawasiliano yoyote.



    "Kwani Dorice hayupo hapa shule?" Aliuliza Mwanaume aliyeambatana na Mama Dorice kwa mshangao. Na huyo alikuwa ni mjomba wa Dorice.







    "Ah! Unataka kuniambia hayupo nyumbani?" Alishangaa Nadia lakini ndani ya muda mfupi alitokea madam Amina eneo lile hivyo Nadia aliamua kuondoka ili kukwepa adhabu.



    Madam Amina aliwasogelea wageni wale na kuwasalimu. Kisha akawakaribisha ofisini. Bila kuchelewa wageni wale waliambatana na Mwalimu Na kuingia ofisini.



    "Karibuni sana.. "



    "Asante.. Sisi ni wazazi wa Dorice na tumekuja hapa kuuliza binti yetu anaendeleaje?"



    "Dorice.. Alikuwa kidato cha nne?" Aliuliza mwalimu.



    "Ndio!"







    "Mmh! Mbona aliacha shule na tuliwapigia simu mkasema amefika" alisema Mwalimu Amina kwa mshangao. Kauli ile iliularua moyo wa mama Dorice na kumfanya achanganyikiwe sana, maana hakuna simu aliyopigiwa wala Kuambiwa chochote kuhusu mwanae.



    "We mwalimu umechanganyikiwa? Mbona kama hujielewi eti?" Mama yule wa kinyaturu aliinuka kitini na kuanza kumfokea mwalimu.



    Mwalim Amina aliamua kujitetea kwani hali ya hewa ilianza kuchafuka ofisini mle. "Tunamtaka mwanetu.. Mmemtorosha nyie? Au mmemuua?" Alizidi kucharuka mama Dorice.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwalimu Amina alikumbuka mbali, akakumbuka siku ambayo Dorice alipotea kisha wakapewa taarifa za upotevu wa mwanafunzi huyo. Barua ya maelezo iliandikwa kisha walimu wakapiga simu kwa wazazi wa Dorice. Lakini kwa bahati mbaya sana simu ilipokelewa na jini Mansoor kwa namna ya ajabu sana. Na jini huyo aliongea sauti ya Mama Dorice na kuwafanya walimu wajiaminishe vizuri kuwa waliongea na mama Dorice lakini kumbe haikuwa hivyo na hakuna aliyejua siri hiyo zaidi ya Mansoor pekee.







    "Mama tena nilipiga simu Mimi.. Na ulikubali mwanao aache shule.." Alijitetea madam Amina lakini hakueleweka.



    Wazazi wa Dorice waliondoka kwa hasira sana shuleni pale huku wakiwa hawajui binti yao alienda wapi. Roho iliwauma sana lakini hawakuwa na jinsi. Waliondoka na gari yao waliokuwa wamekodi ikawafikisha kituo cha mabasi Iringa mjini.



    Walishuka ili watafute sehemu ya kula chakula kwani hawakula chochote tangu asubuhi kisha wakate tiketi, ghafla kwa mbali sana Mama Dorice alimwona msichana kama Dorice. Alijifuta macho yake na kutazama vizuri akamtazama vizuri binti yule.



    "Kaka Dorice yule pale"



    "Yuko wapi?" Kaka yake alishtuka sana.



    "Pale mbele kwenye watu wengi.. Tumfate haraka.." Alisema Mama Dorice akiwa tayari ameanza kupiga hatua kuelekea kule alipo msichana yule.





    ********



    "Chukua hii" Bi Tatile alimpa hirizi moja Doreen. Doreen aliipokea kwa mkono wake wa kushoto na kusikiliza maelekezo kwa umakini kutoka kwa Bi Tatile.



    "Hii umeze sasa hivi.... Haraka sana.." Aliamrisha Bi Tatile na Doreen alifanya hivyo haraka. Akaibugia mdomoni na kuimeza. Alihisi maumivu makali sana ya Tumbo, akapiga kelele kwa kulalama.



    "Hapa inabidi urudi haraka nyumbani... Ukajisaidie haja kubwa sebuleni kwenye sahani safi.. Kisha uzunguke sebuleni Mara Saba kutokea kona moja hadi nyingine huku akitamka jina la msichana yule... Umenielewa?"



    "Nimekuelewa mtukufu.." Alijibu Doreen kwa woga kiasi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Haya ondoka haraka.." Aliamrisha Bi Tatile huku akimalizia na kicheko kikali cha kutisha.







    Bila kuchelewa Doreen aliopotea eneo lile na kutokea nyumbani kwa Mama Pamela. Pindi alipokuwa anaingia ndani kilisikika kishindo kizito sana. Doreen aliingia ndani na kupulizia dawa ya kuwalaza usingizi wote waliokuwa ndani kisha akaenda sebuleni. Akachukua sahani nzuri sana Kabatini, akaiweka chini na kujisadia haja kubwa yenye harufu Kali sana kwenye sahani ile. Kisha akaenda kwenye kona ya kwanza na kuanza mzunguko wa kwanza huku akitamka jina la Pamela.







    Akamaliza mizunguko saba kama alivyoambiwa punde Pamela alitokea sebuleni pale. Doreen alicheka kicheko kikali sana cha kutisha, huku akimsogelea Pamela aliyekuwa ameinamisha kichwa chino bila kumtamzama Doreen.





    Doreen alisigeza mkono wake na kuusogeza kifuani kwa Doreen kwenye titi lake la kushoto. Akalishika titi lile huku akitamka maneno Fulani kisha titi lile likapotea kifuani kwa Pamela akabakiwa na titi moja tu. Pamela alikuwa hajielewi kabisa akiwa pale. Baada ya titi kuchukuliwa akapotea. Na Doreen pia akapotea huku moyoni mwake akifurahia ushindi alioupata kwani tayari kazi iliyomleta ilikuwa imekamilika.





    Asubuhi na Mapema, Mama Pamela aliamka usingizini akiwa mchovu sana. Alijikongoja na kwenda chumbani kwa mwanaye alikuta amelala fofofo, akamshtua.



    "Mbona umelala sana Leo?"



    "Mama naumwa sana." Alisema Pamela kwa sauti ya kichovu.



    "Unaumwa? Unaumwa nini? " mama Pamela alishangaa.



    "Kifua kinaniuma sana.. Titi linauma balaa.."



    "Titi?" Alishtuka mama Pamela.



    "Ndio.."



    "Pole sana.. Halafu kuna harufu naisikia humu ndani.. Sijui pua zangu.." Alisema mama Pamela na kulipuuza suala la binti yake kwani alihisi ni ugonjwa wa kawaida tu.



    "Hata Mimi naisikia..." Alisema Pamela.







    "Ngoja niangalie angalie basi huko sebuleni." Alisema Mama Pamela na kwenda sebuleni. Alipoingia tu alikaribishwa na harufu mbaya sana iliyomfanya apige chafya. Na kwa ukali wa harufu ile alitamani atapike. Macho yalitua moja kwa moja mpaka kwenye sahani yake iliyokuwa imejaa kinyesi pale sebuleni kwake.



    "Oh My God!" Alishtuka Mama Pamela huku macho yamemtoka kama yai la kisasa.



    "Ama kweli dunia ina mambo.. Pamelaaa! Njoo!" Alisikika mama Pamela.



    Pamela aliitika na ndani ya sekunde chache alifika sebuleni pale.







    "Oh gash! Nani kafanya ivi?" Alishangaa Pamela baada ya kushuhudia tukio lile pale sebuleni.



    "Shangaa wewe! Maana mie nimeishiwa nguvu kabisa!" Alisema mama Pamela. Walishangaa kupita kiasi na muda si muda Doreen alifika sebuleni sebuleni pale na kuungana na wenye nyumba kushangaa tukio zima.



    "Alaaniwe sana aliyefanya tukio hili.." Alisema Doreen huku akipiga makofi ya mshangao.



    "Halafu Dada Pamela hapo kifuani pakoje?" Aliuliza Doreen.



    Pamela alishtuka kusikia swali lile. Akajiangalia kifuani kwake na kugundua kifua chake kimetuna upande mmoja lakini upande mwingine hauna kitu. Hofu kuu na mshangao vikamvamia akajifunua shati na kujikagua zaidi.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog