Search This Blog

VAMPIRE NUSRATY - 5

 







    Simulizi : Vampire Nusraty

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulipoishia

    “Kuhusu swala la Shekhe Yusuf tuseme alijisahau hakika Shetani ana vitimbi vya kila aina,

    Kwahiyo yule Jinni akaona njia pekee ya kumteka Shekhe Yusuf ni kupitia mkewe

    Akaenda kumuingia mwilini

    Usiku Shekhe akafanya tendo la ndoa na mkewe akajisahau au kusahaulishwa kwenda kuoga kwa ajili ya kuondoa Janaba,

    Akalala ndipo yule Jinni akatumia nafasi hiyo kumdhuru.

    Kumbuka unapokuwa huna

    Hudhu Qur'an inakuwa mbali nawe

    unakuwa hauna ulinzi wowote,

    Cha umuhimu tudumishe kuwa na hudhu kila sekunde kila dakika na masaa yaendayo kwa

    Allah (s.w.t)!"

    Baada kuniambia vile tukawa tayari tushafika nyumbani kwake

    Akasema kazi ianze,"

    Songa nayo

    Sasa

    Baada Shekhe milongo kusema

    Kazi ianze tukatia hudhu, baada kusali kama rakaa mbili hivi

    Kisha Shekhe milongo akaniambia hivi

    “Hafidhi kijana wangu.

    Au Shekhe wangu tambua kitu kimoja huyu Shetani ni kiumbe mjanja sana kwanza kabisa amejijengea kwenye akili yake ya kwamba binaadamu ni viumbe waoga mno,

    Yani utakuta mtu anapandisha mashetani na kuongea sijui nataka mtindi au Pete sijui furani

    Mchawi tambua huo ni uwongo yani anachotaka ni kuwapima imani

    Embu nikuulize swali kijana kwa mfano Mkeo akapandisha Mashetani na kusema Mama yako ni Mchawi utaamini au?"

    Nikatikisa kichwa kukataa yani siwezi kuamini kamwe,"

    “vizuri sana kijana siku zote dawa ya moto ni?,,,,,,

    Nikadakia kwa kujibu

    “ni moto"

    Akasema

    “Ehee ewaa kumbe kijana unaakili sana mi nilijuwa utasema maji wakati maji yatachemka tu, sasa ukimuona mtu anapandisha Mashetani cha kufanya msomee kisomo cha Ruqiya hakika huyo Shetani au Mashetani yatakimbia kabisa kwenye kichwa cha huyo mtu kamwe hawatoweza kuja tena

    Maana utakuta mtu anapandisha na kuanza kutaja vitu vya gharama sijui Pete cheni za dhahabu mtu kama huyo mchape makofi tena ya nguvu

    Huwenda Shetani wake anataka kuwa Sharobaro,,,,,,"

    Nikajikuta nacheka mbavu sina,

    “Ha!ha!ha!ha!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    tehe,,,tehe!

    Shekhe akaniambia huku akinishika begani

    “ohoo kijana basi usicheke sana matokeo yake ukajamba hapa!"

    Hakika Shekhe milongo alikuwa na maneno yenye utani mwingi sana nikamuuliza",

    “kwani Shekhe Majinni wapo ambao ni Masharobaro?"

    Akatabasamu kwa kunijibu

    “ndio wapo tena wengi tu tambua kitu kimoja Jinni siku zote anapenda kufanya kile ambacho binaadamu hupenda kufanya

    tukianzia katika Kula kulala kufanya mapenzi

    Yani hadi kwenye hiyo mitandao ya kijamii majinni wapo!"

    Nikabaki kusema

    “Duhuu kumbe Majinni noma ehee

    Yani kila kona wapo"......

    “ndio kila kona wapo tena Majinni ni wengi kuliko binaadamu

    Maana wengine tunaishi nao kwenye Majumba yetu wengine wapo Baharini wengine kwenye miti kwa mfano ukitaka kumkamata jinni subiri nitakufundisha Yani jinni anakatika kama kifaranga cha kuku,"

    Nikawa na shahuku ya kutaka kujuwa jinsi ya Kumkamata Jinni sema Shekhe akaniambia nisiwe na haraka

    Atanifundisha tu

    Basi kisomo kikaanza tulisoma mpakaa saa nane Usiku ndipo tukapumzika na kupitiwa na Usingizi

    Ghafla nikahisi maumivi makali sana mwilini mwangu

    Baada kuchapwa bakora sijui ina miba au vipi nikastuka,,,,"

    Mama yangu weee sikuweza kufahamu nipo wapi yani sehemu niliyokuwepo inatisha vibaya mno

    Kibaya zaidi nilikuwa nimelalia mafuvu ya watu nikajikuta natoka mbio yani nilikimbia huku nikiita

    “Shekhe milongo nisaidie msaada tafadhali yani kukimbia kote kule ajabu nikajikuta nipo pale pale.

    Dahaa mbona majanga, nikazidi kutandikwa bakora tu mpaka nikahisi mwili wangu kuchanika chanika vibaya sana.

    Nikiwa sijui huku nimefikaje kwani

    Ghafla ile fimbo ikadakwa kile kiumbe kilichokuwa hakina nyama hata moja mwilini yani mifupa mitupu

    Kikageuka kuangalia nani kaidaka ile fimbo. Akastukia anapigwa zinga la kofi akarushwa hewani

    kumbe alikuwa

    Nusraty basi akanifata pale nilipokuwa nimejikunyata nikiugulia maumivu akaniambia

    “Hafidhi nisamehe Mimi sikutaka wakuadhibu hivi niliwatuma tu waje kukuchukuwa na kukuleta huku!"

    Unajuwa kitu ukikizoea bwana huwezi kuwa na hofu kubwa ndio mimi kwa Nusraty sikuwa namuhofia sana

    Kingine ukishajuwa unapendwa

    lazima ulinge basi nikamkazia macho na kumuuliza

    “kwani Shekhe milongo yupo wapi?"

    Akanionyeshea kiganja chake cha mkono nikaona Eti nyumbani kuna msiba tena aliyekufa ni mimi.

    Nikapiga kelele kwa kusema

    “Hapanaa,,,,,,,"

    Nilipiga kelele kama mwehu vile sikutegemea kuona eti nimekufa dahaa

    Nusraty akaniambia

    “kuanzia leo wewe ni Mume wangu Mimi huwezi kurudi tena duniani utabaki huku katika dunia yetu mpaka siku utakayo kufa",

    Nikamwambia

    “hata kama utanifanyia kitu gani siwezi kuwa Mumeo kamwe bora nife tu,

    Nikaokota kimfupa kimoja wapo kilicho chongoka na kutaka kujiuwa

    Huku nikisema

    “ni bora kufa tu kuliko kuwa huku

    Nusraty sikupendi sikutaki mbona husikii,"

    Nae akaniambia

    “tafadhali mpenzi wangu usijiuwe ukijiuwa unafikilia nitaishi na nani Mimi niambie kitu gani unataka nikufanyie ili usijiuwe?,,,,,

    Nikamwambia

    “Nirudishe nyumbani,,,

    Ghafla nikasikia naitwa kwa mbaali na

    Shekhe Milongo

    “Hafidhi!!!,,,,,hafidhi,,,amka Shekhe wangu muda wa kwenda kuswali nikastuka kumbe khaa nipo kwenye kile chumba cha Shekhe Milongo,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada Shekhe milongo kuniamsha kwanza nikabaki kushangaa huku nikigeuza shingo yangu huku na kule kukitizama chumba kile.

    Kisha nikamtizama Shekhe usoni

    Na kumuuliza swali ambaro jibu lake ninalo Mimi mwenyewe,

    “kwani niko wapi hapa?"

    Shekhe milongo hakujibu kitu zaidi ya kunisaidia kunyanyuka tukaongozana kwenda msikitini,

    Njia nzima nikawa naona nyota nyota tu miguu ilikuwa mizito kutembea yani nilikuwa kama vile nimebebeshwa mifuko ya Cement kama sita hivi kichwani arafu niambiwe kimbia nayo.

    Shekhe alikuwa kimya tu

    Mpaka tukafika msikitini tukatia Hudhu

    akaniambia niadhini kiukweli nikamwambia hapana sitoweza maana kichwa changu hakipo sawa kabisa,

    Baada kuswali

    Shekhe akasimama na kusema kitu kimoja tu yani ifikapo saa tatu Asubuhi Mashekhe wote mnaitajika kufika hapa msikitini kutakuwa na kisomo kizito sana, hakuna aliyeuliza kila mmoja akatawanyika kimpango wake.

    Nikarudi nyumbani,

    Dada akaniuliza

    “Kaka Hafidhi usiku wa jana ulikuwa wapi?",,,,maana kuna mgeni wako alikuja jana usiku akakusubiri wee akijuwa labda utakuwa msikitini"

    Nikamuuliza

    “huyo mgeni jinsia gani na anaitwa nani?"

    “ni Mwanamke kasema anaitwa Nusraty!"

    Nikajishika kichwa huku nikisema

    “Mungu wangu wee!!!

    unasema ni Nusraty ndio kaja hapa jana usiku?",,,,,

    “ndio tena kaniachia ujumbe nikupe"

    Dada akingia ndani na kutoka na bahasha kisha akanikabizi kwa kusema

    “ujumbe wenyewe huu hapa!"

    Kwanza nikapokea huku mikono ikinitetemeka yani kama vile unanipa kaa la moto nikijuwa kabisa nitaungua.

    Nikaipokea Fatuma akaondoka nikaenda kukaa kibarazani nikaifungua kiumakini sana.

    Kisha nikakutana na barua hii yenye maajabu kwanza haikuandikwa kitu chochote kile, yani karatasi nyeupee

    Nikawa naigeuza huku na kule kisha nikasema

    Nusraty ghafla akatokea kwenye ile karatasi mmh!

    Nikataka kuitupa chini ajabu haikutoka mikononi mwangu,

    Nusraty akabaki kucheka tu kisha akaanza kulia huku akisema maneno yenye kusikitisha sana,

    “Hafidhi ni lipi kosa langu Mimi....yani kukupenda wewe kwangu imekuwa tatizo,

    Hafidhi unataka kuniuwa sio please usinifanyie hivyo tafadhali nisamehe Mimi najuwa nimekukosea sana kukupenda binaadamu wewe rudisha moyo nyuma usiende.

    Msikitini kwenye hiko kisomo hakika nitakufa mimi,

    Hafidhi nitamkie neno moja tu ya kwamba unanipenda hata kama utaenda nikifa nife kwa amani tu,

    Niambie basi unanipenda au,

    Maneno ya Nusraty yakaniacha njia panda nikajikuta namjibu

    “nakupenda"

    Nusraty alifurahi sana

    Na kuniambia

    “Nashukuru sana kusikia hivyo naweza kulala kwa amani sasa Mama yako

    Shekhe Yusuf na Mama mjumbe nitawaachia.

    Najuwa mtawaogopa baada kujuwa ya kwamba wamekufa bye kipenzi changu,"

    Nusraty akapotea ghafla kuna mtu akaja kunipora ile barua akakimbia nayo. Hakuwa mwingine aliyefanya hivyo ni Hasina, baada kukimbia

    hatua kazaa akasimama na kuikunjua ile barua eti asome akabaki kuigeuza tu mara aiyangalie utasema pesa ya bandia vile kisha akacheka sana na kusema

    “hakika wewe

    Hafidhi ushaanza kuwa mwehu yani tokea natokea kule nilikuona unasoma mwenyewe mpaka unalia.

    Nikajuwa labda mpenzi wako kakuacha

    Ghafla kila mmoja wetu akatoka mbio"

    Nilipofika mlangoni nikampiga kikumbo Shangazi wote tuakenda chini puhuu

    Sijui alikuwa ndio anatoka kwendaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kupiga mswaki au vipi?....

    maana kopo la maji

    likadondoka maji mwahaa akabaki kuuliza

    “wee Hafidhi nini kwani?"

    Sikumjibu kitu nikaingia ndani haraka na kufunga mlango huku yeye nikimuacha nnje,

    kwa upande wa Hasina kitambo tu kashaingia ndani kwetu utasema kwao vile

    nikawakuta wakiulizana yeye na Dada

    “wee Hasina nini kwani?"

    Hasina hakuwa na jibu kulia alitaka kusema alitaka akabaki kunyooshea mikono nnje

    Mie nikapita mbio na kwenda kujifungia chumbani kwangu kimyaa



    Nikiwa ndani nikasikia sauti ya shangazi huko nnje akipiga kelele tu,

    “jamanii...nakufaa!!!

    Jinni,,,,,"nifungulieni ghafla kishindo kikasikika tii, akawa kimya

    Sauti ya Mama akiita

    Wifi ikasikika na kunichanganya zaidi

    “Wifi",,,,,wifi!!!,,,embu Amka imekuwaje tena, Mume wangu,,,Baba Hafidhi wee njoo umuone huku Dada yako!!!,,,

    Fatuma sijui Hasina ndio aliyefungua mlango wakatoka mbio

    Maana hata kukaa ndani wakaona hakuna usalama tena, nikasikia

    Surat mudathir

    pale Mtume wetu Muhammad (S.a.w)

    Alipoambiwa na malaika Jibrilu (A.s)

    “Ewe uliojifunika minguo. Simama na uonye. Na mola wako umtukuze. Na nguo zako uzisafishe. Wala usitoe kidogo kwa kutaka kingi.

    Nikajikuta nafungua mlango na kutoka zangu nnje, baada kufika ukumbini ni kweli alikuwa Mama yangu kwa wakati huo alikuwa katika pilika pilika za kumfanyia huduma ya kwanza Shangazi baada kuniona Mimi

    Akashituka hivi na kuniambia kitu ambacho kilinishangaza kidogo kwa kusema

    “Nusraty anakusalimia sana hakika bado anakupenda,

    Kwanza nikatabasamu huku mchozi ukinidondoka

    Watu wakajazana eti wakidai Mama aliwekwa ndondocha,

    Baba nae akafika haraka hakujali nini wala kitu gani akaja kumkumbatia mkewe

    mama mjumbe nae akaonekana kupita eneo lile watu wakatawanyika kwa kutimua mbio yani ikawa mkanyage mkanyage tu familia yake yote wakamkimbia,

    Na kuiyacha nyumba tupu!"

    hakika ilikuwa shida juu ya balaa

    Mpaka Shekhe milongo alipokuja na kuanza kutoa Mawaidha,

    kwa kusema,"

    “ndugu zangu Waislamu na wale ambao sio Waislamu hakika dunia ina mambo ya kushangaza sana tena sana kwanza kabisa wote tunatambu ya kwamba kila nafsi itaonja umauti kwa wakati uleule uliopangwa na Allah (s.w.t)

    Sema kuna vifo vingine ni vyakujitakia,

    Ndio maana ukaambiwa kujiuwa ni dhambi kubwa sana

    yani unakunywa sumu au kujinyonga

    kisha wewe mfiwa unasema tu

    Inna lillahi wainna ilahi rajiun,,kwa mfano Mwizi katoka nyumbani kwake haliyakuwa anafahamu fika Mimi naenda kuiba nikikamatwa nitauwawa, huyu tuseme kajitakia kifo yeye Mwenyewe, usitake kusema Allah amepanga

    tofautisha mwizi na mwenye kupata ajari ya ghafla.

    Kwanza mwizi hana tofauti na yule mzinifu mwisho wa ziku akafa kwa ukimwi,

    Ndugu zangu naomba tutambuwe ya kwamba

    sio kila kifo ni kifo vingine ni

    Viini macho tu

    tunachezewa na viumbe vyenye uadui nasi

    yani Majinni tunaenda kuzika vitu ambavyo sivyo

    Mfano ni hawa wenzetuCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama yake Hafidhi na huyu pamoja na Shekhe wetu pale,

    yote sababu ya Jinn Nusraty kumtaka kimapenzi kijana Hafidhi kijana mmoja mchamungu

    Kijana akagoma kuwa nae ndipo sekeseke likaanzia hapo kwa kumchukuwa mmoja baada mwingine,,,"kama tungefanya masikhara

    Tungezika kila mtu kumbe wenzetu wapo ujinini wakifanyishwa kazi

    Ngumu na mateso.,

    Ninacho waomba kuanzia sasa tuwapokee binaadamu wenzetu tuwe nao tusiwaogope,

    Alfatiha

    Basi ikasomwa surat lfatiha

    Shekhe akatoa duwa kila familia ikaondoka na ndugu yake.

    Shekhe milongo akanifata na kuniambia

    “Shekhe wangu kazi imeisha kwa baraka zake

    Allah sema kuna kazi moja tu"

    Nikamuuliza kazi gani hiyo tena?"

    “unatakiwa umuowe yule binti anaeitwa

    Hasina"

    Baada kusema hivyo kama nilivyokwambia

    Shekhe ni mtu wa matani sana akaniambia

    “hapana bwana Shekhe wangu nakutania tu

    maana nyie vijana hamchelewi kusema ohoo maswala ya kuchaguliana wake imepitwa na wakati!"

    Basi tukacheka

    Kuanzia siku hiyo sikuweza kumuona tena Nusraty wala kuisikia sauti yake unyonge ukanishika nikatamani kumuona japo kwa mara moja tu, niweze kucheka nae nifurahi nae nilikuwa na kawaida nikipita pale mbuyuni nasimama zaidi ya nusu saa nikijuwa

    Nusraty atatokea tu

    hakika ikabaki kama history tu nililala na kutamani aje hata ndotoni.

    Nusraty hakuja. Nikaanza kukonda kimawazo kutwa kucha kumuwaza

    Nusraty sijui yuko wapi nini kilichomfikia,

    Hata kula nikawa siwezi hakika nilitokea kumpenda hata kama ni

    Vampire,

    Baba baada kuniona nazidi kukondeana siku hadi siku

    Wakaenda kwa kina

    Hasina na kuitaji nimuowe binti yule basi ndoa ikapita,

    Baba yake Hasina akatupatia Nyumba kubwa tu ya kwenda kuishi Mimi na mwanae

    Maeneo ya kwa Tegeta kibaoni,

    Hii ndio siku niliyoweza kucheka na kufurahi

    Baada kutoka msikitini kufika nyumbani kwangu nikamkuta mke wangu hayupo

    Nikaingia chumbani nipumzike kidogo ghafla nikaanza kuhisi nashikwa miguu nikashituka

    Amini usiamini nikamuona

    Nusraty akitoka uvunguni mwa kitanda

    Akiwa kakenua meno

    Minjino yake miwili ya juu imechongoka vibaya mno nikabaki kuweweseka huku nikirudi nyuma kwa uoga.

    Akaniambia kwa sauti ya besi

    “Wewe Hafidhi kwanini umenisaliti yani umefikia hatua ya kutembea na mdogo wangu sasa leo nakutafunaa!!!

    Yani nikajikuta najamba puhuu,,,

    Ajabu

    Nusraty akaanza kucheka kisha akatoa Yale meno Kudadeki kumbe alikuwa

    Mke wangu Hasina

    Pumbavu sana huyu, dahaaa

    Akacheka na kuniambia

    “Kumbe Mume wangu muoga hivyo mpaka unajamba embu katie hudhu!"

    Nikatoka huku nikimlaani

    wakati huo Hasina tayari ana mimba....

    Kumbe kile kisomo kilicho somwa

    Siku ileCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nusraty aliteseka sana mwishoe akafariki

    kumbuka tambua Majinni wanakufa

    Qur'an ni siraha kari sana kwa Wachawi na Majinni



    ****MWISHO***



    SINA BUDI KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUNIJAALIA PUMZI MPAKA LEO HII NAHITIMISHA STORY HII NI UBUNIFU TU HAIHUSIANI NA TUKIO LOLOTE LA KWELI

0 comments:

Post a Comment

Blog