Search This Blog

JINI HUSNAT - 3

 







    Simulizi : Jini Husnat

    Sehemu Ya Tatu (3)



    "siyo mmmh lakin si wakijinga jinga kama wa uku kwenu wa kule kwetu kuna matabaka mawili kuna tabaka la himaya ya vibwengo au himaya nyeusi na himaya yetu hiitwayo himaya ya jini MUKRAIYA.wachawi wa himaya ya jini WEUSI uvamia kwetu katika misheni mbalimbali katika maabara kuiba ugunduzi flani ulogunduliwa.

    "kah!".

    .

    **********

    Majini hao nyie muwaitwao vibwengo wanaoishi katika himaya yenye giza jeusi utuma wachawi wao kuja kwetu wachawi wao uwanga kwa kuiba ugunduzi wa kisayansi tiba mbalimbali tulizogundua.ndo uchawi wa kwetu huo uchawi wa kuzidiana maharifa.kama viumbe weupe wa bara ulaya wafanyavyo tofauti na nyinyi...mrudishanao nyuma.

    "basi mke wangu tulale...tutaendelea na story kesho."

    wakakatisha mazungumzo wakakumbatiana na kuusaka usingizi ulowapitia kwa pamoja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwanza alianza kwa kupapasa mbele ya mikono yake akiazimia kumpapasa mtu! aka ambulia patupu...bado alikuwa amefumba macho akayalazimisha kufunguka nayo yakagoma.akashtuka kwa kujilazimisha.akata hayari milango ilikuwa imefungwa HUSNA akuwepo."ndo tatizo la kuishi na majini humu ndani wanaondoka bila taharifa."

    alilaani VERGAN akajibwaga katika kitanda chake kabla mvurumuko wa simu yake ya kiganjani aijaita.naam akaikwapua na bila kuangalia aliyepiga akaweka maskion

    "unasema maiti wamekutwa katika maporomoko?"

    "ooh MY GOD ZUBER na kipara?"

    "sawa! sawa naja saiv"



    MOURINE moyo ulimwenda mbio,hasira chuki kwa VERGAN zikaongezeka! mbinu zake zote mbili zilishindikanika kwanza kumshawishi MOURINE halisi kuwa na VERGAN kimapenz ili HUSNAT asipate nafasi hiyo ilishindikanika pili kumwangamizi VERGAN pia ilishindikanika na tatu kuwatenganisha wawili wale pia ilikuwa ngumu akamkumbuka heshima ambayo angeipata kwao kama angefanikisha ili.wazo ili likapingana na lile akabaki katika mawazo yalo changanya ubongo wake.mwisho akapata jibu ni kucheza na akili za VERGAN kama JINI HUSNAT.wazo hilo akaliafiki.akatabasamu.majini kama majini wana muda wao na wana tofautiana ki uwezo.tayari alishaisoma ratiba ya JINI HUSNAT juu ya safari zake katika dunia.akautumia udhaifu huo kujifanya ni JINI HUSNAT...Kete yake ya kwanza aliirusha wakati VERGAN akipata chakula cha mchana na marafiki zake.MOURINE akiwa na sura ya JINI HUSNAT kAtika meza ya pembeni mwanaume shabibu alikaa pembeni yake wakilishana kimapenzi.mikao ya kimah



    ***********

    Moyo wa VERGAN ukapasuka paaa! akutaka kabisa kuya amini macho yake! bumbuwazi likautawala uso wake akaweka kijiko cha chakula chini.akasimama wafanyakaz wake alokuwa anakula nao wakabaki wanamshangaa bosi wao bila kumwelewa.ilo yeye akulijali alitaka kuyadhibitishia macho yake kwa kile akionacho akazidi kujongea eneo lile alokwepo mpenz wake feki na hawara wake.jibu alilolipata likadhibitisha fikra zake baada ya macho yake na ya JINI HUSNAT kugongana.mwanadada yule akapata mshtuko ambao ni wa kufoji ulo tafsiriwa vingine na JOHN mshtuko ule wa JINI ZAIDATU au mourine au husnat wa bandia haukudumu akawa kawaida.JOHN akawafikia Wawili wale akiwa na uso wa hasira na ghadhabu

    "unafanya nini hapa? na huyu ni nani?" VEGAN akauliza

    "HUSNAT huyu ni nani?" kijana yule alokuwa na MOURINE akazidi kupigilia msumari wa moto katikati ya moyo wa VERGAN kwa kulitaja jina la HUSNA maksudi "sijui beby! ntamjuaje?" Mourine alijibu huku akiwa amemlalia yule jamaa kifuani.

    "HUSNA! mi naondoka nashkuru sana...."

    "babu weee tupishe katika starehe zetu!"

    "husna! husna wakunifanyia hivi!"

    "nakuomba tokaaaaa"

    jini yule alipiga ukelele huku katika macho ya VERGAN akionekana kiumbe wa ajabu kitendo kilicho mfanya aanze kukimbia na kuparamia viti.akadondoka baadhi ya watu walimcheka wengine wakimsikitikia kwani kile alichokiona wenzake awakukiona akajipakia ndani ya gari lake na kuliondoa kwa speed huku akisindikizwa na vicheko....wafanyakazi wake wakabaki katika hali ya simtofahamu.MOURINE alifrah baada ya kumaliza kula akaelekea chooni na kutoweka akitokea kazini kama MOURINE

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kama ni kazi akuweza kuendelea kuzifanya moyo ulimuuma alijuta kumpa nafasi jini yule alomsaliti ukiona mtu mzima analia basi ujue kuna jambo JOHN VERGAN alilia mapenzi yalimliza.akachukua mkonga wa simu na kupiga namba kadhaa "naomba nletee bia!"

    ili kupunguza mawazo akanywa bia na kulewa chakari kila MOURINE alipoingia kumpelekea chupa alizidi kumuona yule binti ni mrembo akaitaji kingine......



    ******



    Hisia kali za mapenzi ziliuvuta moyo wa VERGAN! na kuitaji kingine kwa Moureen.aliitaji penzi lake...



    Moureen naye alizidisha hisia zile za kijana wa watu! alitaka kujua hasimu wake yule "JINI HUSNAT" alifaidika na nini kwa binadamu yule...kile alichokipata jin mwenzake naye aliitaji kukipata.



    je kingearibu kazi yake?

    kazi ya hatari lakini yenye heshima katika maisha yake?

    kazi ilomtoa ujinini na kumleta duniani kuifanya kwa umakini ulotukuka?



    akatabasamu baada ya kugundua kwamba ata kama angempa penz binadamu yule asingeiaribu kaz yake!

    kwanza akuwa na mpz hata ujinini kwao useme kwamba angekuwa kamsaliti...

    wakati akiwaza ayo akasikia akiitwa.akujiuliza akachukua chupa ya bia na kuingia nayo.akamsogelea bosi wake na kumwekea mikono katika miguu yake huku akiwa kachuchumaa

    "bosi una matatizo gani leo? mbona si kawaida yako?"

    "maisha yenyewe mafupi nachen mi nile ujana,kujirusha kila wikendi nakula ujana!..."

    baada ya kujibu VERGAN akaanza kuimba.huku akiupeleka mdomo wake katika mdomo wa Moureen.mdada yule akaupokea dakika chache badaye wakazama katika mapenzi kule kule ofisini..,.

    -....-....-.....-

    Moureen alinogewa na penzi la VERGAN alijilaumu moyoni mwake kwa kitendo cha kutaka kumuua kijana mtamu namna ile...alionja asali alitaka achongeshe mzinga....alijua kwa vyovyote vile kijana yule ni haki yake kutokana na sababu alizozijua yeye zilizomkosesha JINI HUSNAT nafasi ya kuwa na kijana yule.kwa fikra zake yakinifu lakini.alitamani kumuua HUSNAT ila ilo lilipingana na kazi yake.akala kiapo kitakatifu! kiapo cha kumtawala mwanaume yule....katika himaya ya mahaba yake....... Kwa upande wa VERGAN kama maranda yateketeavyo katika moto moyo wake uliteketea kwa binti MOUREEN,ni binti alompenda ata kabla ajakutana na HUSNA akajipa tumaini.penzi lake lilikuwa tamu zaidi ya ata la HUSNA...ghafla moyo wake ukanyongonyea baada ya kukumbuka machungu ya usaliti alosalitiwa na jini yule./.sidhani kama atakuja tena kwangu/...

    Zuberi Musa Maruma's photo.



    *********



    UPANDE WA PILI WA SHILINGI



    NJE YA TUFE LA DUNIA

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilikuwa ni kiumbe kilichokaa juu ya mnyama mfano wa farasi,farasi yule alokuwa na mabawa pia mwenye speed zaidi ya upepo,kiumbe yule alokb juu ya mnyama mkononi alishika upanga ulowaka waka nywele zake ndefu zilipepea kukinziana na upepo wa eneo lile.awakuwa kwenye kasi ya kawaida! huyo kiumbe alikuwa ni JINI HUSNAT katika moja ya safari zake zakuelekea katika sayari ya marz walokuwepo viumbe wenye asili kama yao lakini wenye nguvu zaidi yao.lengo la kwenda kule ni kuitaji idhini ya kumpa nguvu za kijini mpz wake VERGAN ili akienda nae ujinini asipate tabu.moyo ulimuuma kuondoka bila kumuaga mpz wak yule lakini akuwa na budi ilikuwa ni safari ngumu ambayo ilimlazimu kupoteza mawasiliano na duniani na ujinini.nafas hiyo ndiyo MOURINE aloitumia kumuadaa kijana yule na kumuweka katika himaya yake.



    usiku na mchana ndani ya wiki moja akiwa katika faras wake alikata mbuga mara chache akiingia katika ardhi ilotokota moto yenye shaba na joto kali ilimlazimu wapae hewani.jini husnat alikuwa ni kiumbe mwenye hasira za karibu kwa viumbe walojitokeza mbele ya macho yake kwa lengo la kuizuia safar yake aliviteketeza kwa upanga wake damu yao akiifanya ndo chakula katika safari ile alotegemea kuchukua wiki moja.atimaye ndani ya siku tatu na nusu aliifikia sayar ile na kupokelewa kwa shangwe na viumbe wale.akafikishwa mpaka kwa babu zake.

    baada ya salamu za hapa na pale story na vionjo vya vyakula akaeleza shida yake.babu yake alimsikitikia sana

    "mziwanda wangu nshakukataza mara ngapi kuwa na binadamu?"

    "siwezi muu nampenda sana yule nsaidie babu nkamwongezee nguvu nataka nkamtambulishe nyumbani!"

    "achana na binadamu olewa na jini mwenzako!"

    "hapana babu muu cwezi nampenda mbona wewe ulimuoa binadamu?"

    ghafla babu muu akanyongonyea ni kweli yeye kabla awaja amia huku aliwah kumuoa binadamu enzi za ujana wake miaka elfu na kitu ambaye alishakufa siku nyingi sana.ndo akamuoa jini mwenzake ambaye ndo bibi yake HUSN



    *******

    Babu muu alikumbuka mbali sana! ila kwa mjukuu wake huyu alimsikitikia! sana.akainua kiganja cha mkono wake

    "hivi unajua kinachoendelea duniani saivi kwa mpz wako?"

    jini HUSNAT akatingisha kichwa kukataa kutokujua kilichoendelea duniani akiwa na shauku la kujua kulikoni macho akiyakaza katika kiganja cha babu yule.ghafla kiganja kile kikaanza kumuonesha VERGAN akiwa na MOUREEN katika matokeo mbalimbali kama wapenzi,moyo wa HUSNA ulimpasuka.na bila kuaga aliondoka kwa speed kali aki hema kwa hasira baadh ya majini walijaribu kumzuia bila mafanikio hasira zilimzidi akuitaji tena kuongezewa nguvu alichoitaji ni kufika duniani na kumwangamiza tu Mourine.



    DUNIANI



    Kama mapenzi ni ukichaa wao sasa walikuwa ni machizi katika ofis ya secretary VERGAN aliketi akimchombeza mpenz wake yule.ghafla upepo mkali ulivuma na vitu vikaanza kurushwa rushwa madirisha yakajifunga na milango pia...tayari MOUREEN alishajua huo ni ujio wa HUSNAT ivyo akawa tayari kwa kukimbia alipoufikia mlango ukajifunga na kutupwa mpaka katika meza ile....akanyanyuliwa kidogo na kimbunga kilichoingia mule ndani kimaajabu na kubwagwa chini jini ZAIDATU akukubali kwa spidi kali akajinyanyua mkononi akiwa na upanga.VERGAN akashtushwa kwa ilo lakini akukuwa na muda wa kutafakari yalokuwa yakitokea jini HUSNAT Alikuwa katikati ya kimbunga kile akiunguruma kwa hasira.waka angaliana ana kwa ana na zaidatu.

    "naomba niambie wewe ni jini wa wapi? na kwa nini uingie kwenye himaya yangu?"

    HUSNA alimuuliza jini mwenzake uku akiwa kamgandisha na upanga wake....

    "sema kabla sijakutenganisha kichwa!" HUSNA alizidi kusisitiza

    "mimi natoka katika himaya yetu ya MUKRAIYA"

    "Nini?" HUSNA akuamini kama jini yule anatoka nyumbani kwao.

    "nawe umetumwa?" akaendelea kumuuliza huku akiwa kamkaba

    "nd..i..io"

    "unasema? ina maana umetumwa na mshenzi ZULUWALADI?"

    "NDiyooo usiniuwe shoga..."

    "utansamehe shetani mkubwa wewe!"

    akampulizia moto uloanza kumteketeza kisha wote 3 WAKATOWEKA.....



    HUSNAT Alikuwa katikati ya kimbunga kile akiunguruma kwa hasira.waka angaliana ana kwa ana na zaidatu.

    "naomba niambie wewe ni jini wa wapi? na kwa nini uingie kwenye himaya yangu?"

    HUSNA alimuuliza jini mwenzake uku akiwa kamgandisha na upanga wake....

    "sema kabla sijakutenganisha kichwa!" HUSNA alizidi kusisitiza

    "mimi natoka katika himaya yetu ya MUKRAIYA"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nini?" HUSNA akuamini kama jini yule anatoka nyumbani kwao.

    "nawe umetumwa?" akaendelea kumuuliza huku akiwa kamkaba

    "nd..i..io"

    "unasema? ina maana umetumwa na mshenzi ZULUWALADI?"

    "NDiyooo usiniuwe shoga..."

    "utansamehe shetani mkubwa wewe!"

    akampulizia moto uloanza kumteketeza kisha wote 3 WAKATOWEKA.....



    *********

    CHINI YA BAHARI



    HIMAYA YA JINI MUKRAIYA



    Kulikuwa na mabishano makali! kati ya mtoto kipenzi! mtoto pekee wa jini mkuu MUKRAIYAH aliyeitwa ZULUWALAD na baba yake jini mukraiyah

    "baba siwezi kuishi bila yeye baba lazima nimfate duniani nampenda sana JINI HUSNAT..." aliongea ZULUWALAD kwa hisia machozi yakitoka kila kingo za macho yake baba yake ambaye ndo mfalme akaufungua mdomo wake kwa sauti ndogo ya kushawishi

    "mwanangu! nishakwambia ilo swala tuachie sisi mimi kama baba yako na mama yako malkia SUMAIYAH tuta akikisha HUSNAT anakuwa wako!"

    "aswaaa mme wangu! na jambo zuri zaidi kijakazi tulomtuma dunia jini ZAIDATU akamwangamize yule binadamu wake tumewasiliana naye anaendelea na kazi vizuri na ameshamteka kimapenz kijana yule.sasa akasema bora awe naye kwa kuwa HUSNA atakuwa kasalitiwa lazima arudi huku awe na mwenetu."

    ZULUWALAD kusikia hivyo aka achia kicheko ishara ya furaha.

    "na je ikiwa mipango yote ikagoma pengine ZAIDAT aka uwawa itakuwaje?" ZULU akaoji...

    "ZAIDAT ni msichana tunayemwamini na kama ikitokea akashindwa angetoa taharifa lakin mama yako kasema amewasiliana naye na mambo yapo fresh...."

    wakati MFALME MUKRAIYA akiendelea kuongea ghafla kijakazi mleta taharifa akaingia huku akiwa ana hema.akafungua mdomo kusema maneno yalovunja mioyo ya wanafamilia wote

    "mfalme! habar nlotumwa nkufikishie ni kwamba JINI HUSNAT na binadamu wake pamoja na mwili uso na uhai wa jini ZAIDATU wamerudi himayani"

    "nini?" watatu wale wakauliza kwa pamoja wakitegemea jibu lingebadilishwa tofauti na mategemeo yao walipewa majibu yaleyale.

    "naitaji walinzi wawili muende popote mtakapo waona waletwe mbele ya macho yangu haraka!"

    "sawa mfalme." kijana yule akatoweka.na kuwa acha wahusika wakiwa katika dhamira ya majonzi makuu.

    -.....-......-......-

    katika nyumba hii kulitawala majonzi! aikuwa ni nyumba ya kifahari ila ni nyumba ya kawaida mama mwenye nyumba ile kwa mara ya pili sasa akiongeza sauti yake kidogo akauliza swali lile lile



    **********

    mama HUSNAT akiwa na uso wa majonzi alimwangalia mme wake na kurudia swali lake lile kwa mara ya pili "mme wangu siku zinazidi kukatika bila mwanetu HUSNA kurudi nyumbani toka akimbilie duniani! unafanya jitihada gan tumpate mwanet....."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "shataaaaaap!" akakatishwa na sauti kali iloambatana na radi! eneo lote likazizima.mama HUSNA akazid kunyongonyea akimwacha mwanaume yule kuendelea kufoka.kibabe

    "nimesha sema HUSNAT si mwanangu kakataa kuolewa na jini mwenzake? tena mtoto wa mfalme MUKRAIYA linaenda kupendana na lijibinadamu sijui! sasa kwanzia sasa simtambui na sitaki kusikia habari za HUSNA katika kizazi changu! ndo nimesem....."

    kabla ajamalizia JINI HUSNAT,VERGAN,na jini ZAIDATU akiwa mweusi tii kutokana na kombora alilopigwa wakatokea maeneo yale.VERGAN alikuwa ana fahamu,JINI HUSNAT hasira zilikuwa zimempanda,akiwa kaushikilia upanga wake ulowakawaka mkononi akikoroma kama simba,urembo wote ulitoweka alikuwa akitisha,meno yalochongoka,kucha ndefu zenye ncha mwili wake ulijengeka kimazoezi.hakuwa yule binti mrembo mwenye uzuri wa kiindi alowatoa udenda wanaume wamwangaliaye! huyu alikuwa ni HUSNAT mwingine.akainama ishara ya kutoa heshima wakati huo huo akimtupia jicho la kumtaadharisha baba yake juu ya alichokuwa akifikiria.mzee yule akanywea alimjua vizur mwanae akiwa katka hali ile

    "baba,mama huyu anithi,fedhuli jini ZULUWALAD anantafuta nini lakini? anatuma vibaraka zake kunchezea nao wanaingia hadi kwenye moyo wangu....."

    hasira za uchungu zikamzidi akaanza kulia akiendelea kumwadhibu maiti ya MOURINE kwa kuicharanga charanga na kucha zake kama vile mwili ule una uhai.

    "nipo tayari nifukuzwe IMAYANI lakini si kumpoteza VERGAN hata babu muu nimemwambia nampenda sana huyu kiumbe akuna wa kututenganisha nay....."

    "NYAMAZZZAAAAA!!!"

    Baba HUSNA akapayuka wote wakakaa kimya kwa dakika chache kupunguza hasira katika mioyo yao mikono ya HUSNA na mdomo wake ulikuwa ukitetema kwa hasira upanga wake ukiwa mkononi

    tayari kwa chochote mdaa wowote.



    ********

    "NYAMAZAAA!!!"

    Wote wakakaa kimya kila mtu akihema kwa hasira! hasira kuu!,mdomo wa jini HUSNAT ulimtetema kwa hasira zilizokidhiri! upanga unaowaka waka ukiwa mkononi! kabla baba akaendelea kuongea vibaraka watatu walotumwa na mfalme MUKRAIYA wakatokea......

    kwa uwepesi wa ajabu JINI HUSNAT akaurusha upanga wake kule kwa adui alokuwa anamfata VERGAN na wakati huo huo naye akiruka kwa yule mtu wa pili alokuwa akimwendea akampokea kwa ugoko wa sehemu za siri kibaraka yule akatoa kilio cha maumivu kilichopokewa na yule kibaraka mwingine alotembelewa na upanga ulokifyeka kichwa chake.kichwa kile kikadondoka chini na upanga ukarudi mkononi mwa JINI HUSNAT kwa maajabu kichwa kile kilichokuwa pale chini mara kikapata uhai na kupaa kumfata yule alokatwa alokuwa chini akigugumia kwa maumivu.kichwa kile kikarudi katika muunganiko wake pale shingoni.na ghafla kijana yule akawa kama awali.haya yote yalitendeka kwa wepesi wa ajabu ndani ya sekunde za kibinadamu.yule kibaraka aliyepigwa sehemu za siri huku akiwa na tabasamu la dharau usoni akamnyooshea HUSNA mkono short za umeme zilizoambatana na makombora vikaanza kutoka! na kumwendea HUSNAT aliyekuwa na kazi ya kuzikinga kwa mikono yake.baada ya jambo ilo kushindikanika vibaraka wote watatu wakaunganisha kwa maajabu nguvu pamoja na kuanza kutupa makombora ambayo JINI HUSNAT alishindwa kuyazuia yakamlevya na kumdondosha.akapoteza fahamu hakika yalikuwa ni majonzi katika familia ya jini husnat aliye na uchungu na mwana ni mama ni kweli.mama HUSNA alilia lakini aikusaidia miili ile mitatu ikatoweka ikielelea nyumbani kwa mfalme MUKRAIYAH

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    RAHA ya MAPENZI ni pale upendo unapopatikana pande mbili

    ZULUWALAD mtoto wa jini mkuu alitokea kumpenda sana JINI HUSNAT ila moyo wake hukuwa na nafasi kwa binti yule alotoka kwenye familia ya umasikini wa kutupwa.ZULUWALAD alikuwa ni kijana mzuri ambaye alijaliwa umbo mukhtari kwa kila kiumbe kimwangaliacho wajihi wa umbo lake lilimpelelea

    wanawake mbalimbali(majini) kumpend



    *******



    Raha ya mapenzi ni pale upendo unapokuwa pande mbili,ZULUWALAD mtoto wa jini mkuu MUKRAIYAH alitokea kumpenda sana JINI HUSNAT ila mrembo yule katu akuwa na upendo kwa prinsi yule.

    JINI HUSNAT alitoka katika familia yenye umasikini wa kutupwa.

    zuluwalad alikuwa ni kijana mzuri! ambaye alijaliwa umbo muhtari! kwa kila kiumbe kimwangaliacho wajihi wa umbo lake matata! lilipelekea wanawake mbalimbali kumpenda ila moyo wake ulitweka na HUSNA tu! jini yule wa kiume akuruhusiwa kutoka nje ya himaya ya baba yake kuofia kudhuriwa na maadui,na hata kama pale ikitokea akitembea baadh ya maeneo ndani ya himaya ile alikuwa katika ulinzi mkali!.kitendo icho kilimkosesha amani! ila alikula nadhiri ya kumpata JINI HUSNAT kwa namna yeyote ile ndipo alipomwita jini ZAIDATU msichana wao wa kazi aliyeaminiwa kazi ya kwenda duniani na kuchunguza nyendo za jini husnat! zaidatu akawasili duniani na kuutumia mwili wa MOURINE na kuangukia kwenye penzi la binadamu yule kabla ajafumwa na jini husnat na kuambulia kuangamizwa kikatili! na msichana yule mpole mwenye hasira za karibu(JINI HUSNAT)



    Ni wakati kikao kile cha watatu wale ambao ni MFALME MUKRAIYA,MALKIA SUMAIYAH,na MTOTO WAO ZULUWALAD kikiendelea ghafla vibaraka wale watatu ambao ni DENASI.OBISHI na ZINDUNA wakatokea! hapo hapo jini husnat,vergan na mourine au jini zaidatu nao wakatokea! vergan na jin husna wakiwa wamefungwa kamba madhubuti mikononi na miguuni! Zuluwalad kwa mshtuko!! na mshangao!!! machozi yakimtoka akamrukia husna na kumwagia mvua ya mabusu zulu kwa husna alikuwa ni kichaa.hama kweli mapenz ni uchizi kwa zuluwalad ili lilidhibitika wazaz wake walimwangalia kwa huruma

    "Husnat amka mpz wangu...amka husna,HUSNAAAAAA!"

    ZULUWALAD akaita kwa ukelele mkali ardhi yote ikatetema,nuru ikatoweka....

    "nani kamuua mpz wangu?!"

    zuluwalad akauliza mda huo huo akanyoosha mkono wake upanga ukatua akaushikilia vizuri na kujongea kwa vibaraka wale watatu walokuwa wakitetemeka.kwa khofu mioyo yao ikiwapeleka mpwe



    ******



    Mioyo yao ikaanza kwenda mpwetapweta! "nauliza tena nani kamuua mpz wangu? nliwatuma mkamuue?!"

    bado ZULU aliuliza hasira zikiwa zimekijaza kifua chake macho akayanatisha kwa ZINDUNA.ambaye huku akitetemeka akajitutumua na kuufungua mdomo wake "yaah mtukufu wa himaya hii tusamehe sisi vijakaz wako husna ajafa! ajafa prinsi kazimia tu!"

    "la! kama ni kweli msemacho mfungueni haraka mumpeleka chumba cha matibabu! akifa mpz wangu mtaisoma namba! akuna hata mmoja ntakayemwacha mzima"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    vijakazi wale wakainama ishara ya heshima na haraka wakambeba husna na kutoweka naye.wakati wote mfalme MUKRAIYAH na malkia sumaiyah awakuwa na cha kusema walimpenda sana mtoto wao.baada ya zuluwalad naye kutoweka khusni labda alielekea hospitalini au laa! katika eneo lile wakabaki mme na mke yani mfalme na malkia wake wakiangaliana.yamkini mfalme alikuwa mbali kimawazo akashtuka na kuhema kwa nguvu! malkia wake sumaiya akimwangalia ishara ya kumuuliza kiendeleacho?! macho yake yakatua katika miili ilobaki pale ndipo akaukumbuka wadhifa wake! kama kichwa cha familia! mke wake alisubiria aambiwe na mme wake kipi kifanyike kwa sauti ya upole jini MUKRAIYAH akamwambia mke wake....



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog