Search This Blog

NILITAFUNA MAITI YA MWANANGU NIWE TAJIRI - 5

 







    Simulizi : Nilitafuna Maiti Ya Mwanangu Niwe Tajiri

    Sehemu Ya  Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    .kuajiri dereva, kufanya manunuzi ya nguo za thamani kwa ajili yake ya mkewe, kutafuta nyumba ya kifahari ya kupanga maeneo ya Mikocheni.

    “Mpenziiiii!” Galos aliita, Rita akageuka kuangalia.

    “Hee!”

    Rita alipayuka kwa mshangao, kumwona Galos katika hali tofauti kabisa na aliyoondoka nayo asubuhi. Alikuwa ameng’ara, uzuri wa sura yake ambayo kwa muda mrefu ulikuwa umefunikwa na umaskini mkubwa sasa ulikuwa umechomoza na kumfanya Galos awe kama ambavyo Rita alimwona siku za mwanzo wa uhusiano wao.

    “Galos!” aliita akimkimbilia.

    “Yes baby.”

    “Nini kimekutokea wewe mwanaume?”

    “Mungu ametuona.” Aliitikia Galos akimkumbatia mkewe.

    “Si umeondoka hapa asubuhi ukiwa na nguo zako?”

    “Ndiyo.”

    “Sasa?”

    “Wewe acha tu, nitakueleza baadaye, twende zetu!”

    “Wapi?”

    “Tunahama.”

    “Kwenda wapi?”

    “Mikocheni.”

    “Mh! Mbona ghafla hivi?”

    “Punguza maswali mke wangu, ze taimu tu-tesa iz nao!” aliongea Galos akichanganya na Kiingereza kibovu kuthibitisha lile lisemwalo kwamba, ukitaka kumgundua mwanadamu tabia yake, mpe fedha! Tayari Galos alishaanza kuonyesha mikogo ya mafanikio kwa kujaribu kuongea Kiingereza.

    “Niache basi hata nikachukue vitu vyangu.”

    “Vitu gani? Una vitu humo ndani au takataka? Sitaki uingie humo, kilichomo atachukuwa atakayetaka.”

    Rita hakuwa na la kusema, akiwa katika mshangao huo huo aliingia ndani ya gari baada ya Galos kumfungulia mlango, kichwani mwake alikuwa na maswali mengi mno yaliyohitaji kujibiwa na mume wake.

    Gari likaanza kuondoka, Rita akibubujikwa na machozi si ya huzuni bali furaha, kila kitu kwake kilionekana ni ndoto na kwamba muda si mrefu angezinduka na kujikuta amelala kwenda kitanda chao cha mbao kisicho na godoro bali jamvi.

    “Tunaelekea wapi?”

    “Wewe twende”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva akaendesha gari kwa mwendo wa taratibu, Galos na Rita wakiwa wemeketi kiti cha nyuma, kwa mara ya kwanza maishani mwake Rita akimshuhudia mumewe akimfanyia mambo ambayo aliwahi kuyaona kwenye sinema za Kihindi, hakuamini kama ni Galos aliyekuwa akifanya mambo hayo, gari likasimama mbele ya jumba kubwa la kifahari.

    “Tumefika.”

    “Kwa nani hapa?”

    “Kwetu.”

    “Kwetuuu? Mbona unazidi kunichanganya mume wangu? Au umejiunga na…”

    “Nini?”

    “Fre…ma…!”

    “Ah wapi, hapa bongo kila mtu akifanikiwa maishani anaambiwa amejiunga na Freemason,” Galos aliongea akifungua mlango wa mbele ya nyumba.

    Macho ya Rita yalionyesha mshangao mkubwa alipoitazama sebule, ilikuwa nzuri mno, yenye samani za thamani kubwa ambazo hakika hakuwahi kuziona maishani mwake.

    Galos akamsaidia kuketi kwenye moja ya makochi makubwa ya sufi nyeupe, mbele yake kukiwa na runinga ya nchi sabini na mbili.

    “Unataka chaneli gani mpenzi?” Galos aliuliza akiwa ameshikilia rimoti mkononi mwake.

    “Galos acha utani, hebu nieleze umepata wapi fedha za kufanya mambo yote haya?”

    “Madini.”

    “Madini? Umeanza lini biashara ya madini mume wangu?”

    “Nilikutana na watu wakanifundisha, kwa mara ya kwanza tukapata kipande kikubwa cha Almasi ambacho tumekiuza na kupata kiasi kikubwa cha fedha, ndiyo maana tuko hapa, punguza maswali mke wangu, huu ni wakati wa wewe kula bata badala ya kugeuza nyumba yetu Bunge la Katiba.”

    Rita alikuwa akilia kwa furaha, alipopelekwa chumbani ndiyo alichanganyikiwa kabisa, kulikuwa na kitanda pamoja na kabati iliyoundwa kwa miundo ya Kiarabu, kiyoyozi kikiwa kazini, hakika yalikuwa mabadiliko ya haraka mno ambayo hakuyatarajia jana yake wakati anaingia kitandani kulala kwenye kibanda chao cha mbavu za mbwa.

    “Hii siyo ndoto kweli?” alimuuliza Galos.

    “Subiri kama ni ndoto utaamka!” Galos aliitikia huku akicheka.

    Usiku wa siku hiyo hata tendo la ndoa lilikuwa tofauti na siku nyingine zote, waligundua kumbe joto la uswahili liliwasumbua sana.

    Kila mtu alikiri mwenzake alikuwa mtaalam wakati walikuwa ni watu walewale, ingawa mioyo yao ilikuwa imejawa furaha na kuridhika, wote kwa pamoja wakakubali penzi bila mawazo kichwani, lilikuwa zuri na la kuvutia.

    Hayo ndiyo yakawa maisha yao, mara kwa mara Galos akawa analetewa na majini kipande cha Almasi na kwenda kuuza, fedha zilizopatikana alizitumia kununua nyumba na magari ya kifahari, watu wote wakakiri kwamba “tajiri mpya” alikuwa ameingia mjini, ambaye chanzo chake cha mapato hakikueleweka vizuri lakini ndiye aliyeendesha magari ya kifahari kuliko mtu mwingine yeyote.

    Ndani ya miaka miwili ya mafanikio hayo, uani kwa Galos kulikuwa na Ferarri mbili, Buggatti moja, Range rover mbili na Lamborghini moja ambayo alipenda sana kuitumia mwishoni mwa wiki, mke wake akiendesha Buggatti! Kila mtu alimzungumzia Galos, maana kwa watu wengi waishio mjini hasa katika nchi za Kiafrika utajiri wa mtu ni gari analoliendesha, ndiyo vijana wengi huwa radhi wakati mwingine kuendesha gari la mamilioni ya fedha, lakini wakiwa wamepanga chumba kimoja uswahilini.

    Pamoja na maisha hayo ya kifahari Rita hakumwacha Mungu wake, bado aliamini kulikuwa na jambo lisilo la kawaida nyuma ya mafanikio ya mume wake, alikuwa mtu wa kanisani mara tatu kwa wiki, mara nyingi akifunga na kuomba ili Mungu amsaidie. Kadiri siku zilivyozidi kusonga ndiyo amani moyoni mwake ilivyozidi kutoweka, hasa pale alipojaribu kumdadisi mume wake juu ya utajiri waliokuwa nao, lakini akaishia kuambiwa “tulia kula bata.”

    Kwa miaka mitatu Galos hakuwahi kwenda tena kwenye ulimwengu wa wachawi, kiasi cha kuanza kuhisi kwamba huenda mchezo huo ulikuwa umekwisha, wachawi waliachana naye ili afaidi utajiri. Katikati ya mwaka huo wa tatu, Galos akiwa usingizini, alijikuta tena mbele ya Mukulungu kwenye sherehe ya wachawi chini ya mti mkubwa wa Mbuyu, kila mtu akiwa utupu.

    “Enheee Galos!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo Mukulungu.”

    “Umeona raha ya kuwa na utajiri?”

    “Ndiyo Mukulu.”

    “Sasa nataka kuuchukuwa utajiri wangu, urejee kwenye maisha yako ya zamani.”

    “Kwa nini?”

    “Imetosha tu,”

    “Tafadhali usifanye hivyo, watu watanicheka, heshima yangu itapotea.”

    “Nitauacha tu kama utatimiza sharti langu.”

    “Lipi tena?”

    “Nataka damu ya mkeo!”

    “Mke wangu?”

    “Ndiyo, umtoe kafara, wazee wanywe damu, nenda kafikirie, kesho utakuja kunipa jibu.”

    Galos akainamisha kichwa na kuanza kulia, alikuwa njia panda, ghafla akazinduka usingizini na kumkuta mkewe akimtingisha na kumbembeleza aache kulia.

    “Mbona umelia sana? Ndoto gani hiyo?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Galos alibaki kimya, machozi yakiendelea kumbubujika. Moyo wake ulitamani kufunguka na kumweleza mke wake ukweli wa yaliyokuwa yakimtokea na hasa juu ya siri ya utajiri wao usio wa kawaida. Alishindwa kufanya hivyo pamoja na Rita kumshawishi aeleze kilichomfanya alie akiwa usingizini.



    “Mh! Galos, hebu nieleze ni nini kilikuwa kinakuliza usingizini tena ukisema maneno sitaki kumuua mke wangu?” Rita aliuliza akimwangalia Galos usoni.

    Akainamisha kichwa chake chini, alipokinyanyua dakika kama kumi hivi baadaye, alifuta machozi, akamwangalia mke wake machoni, kisha kushusha pumzi ndefu.

    “Rita!” Galos akaita.

    “Bee!”

    “Nikikuambia ukweli hutaniacha?”

    “Siwezi.”

    “Wanataka nikutoe kafara!”

    “Mh!” Rita aliguna kwa mshangao, maneno hayo yalithibitisha kabisa alichokisikia wakati Galos akilia usingizini.

    “Ni kweli.”

    “Akina nani?”



    “Baba yangu alikuwa mchawi kabla ya kifo chake…” Galos alijaribu kuzungumza lakini alishindwa, kwikwi ya kulia ikamkaba.Alichokifanya Rita pamoja na hofu iliyokuwa imemwingia, ni kuwa mvumilivu, akimbembeleza mume wake mpaka aseme ili ajue ni kitu gani kilikuwa kikimsumbua.



    Alipotulia, Galos aliamua kufunguka na kuweka kila kitu bayana, kuanzia historia ya baba yake na uchawi, kulazimishwa arithi mikoba jambo ambalo alilikataa, adhabu ya kutopata mtoto aliyekuwa amepewa, hatimaye kula maiti ya mwanaye ili apate utajiri.

    “Kwa hiyo mimba zinazotoka ni adhabu Galos?”

    “Ndiyo mke wangu.”

    “Na hiyo maiti uliyokula ni ipi?”

    “Ya mimba ya mwisho.”



    “Mungu wangu!” Rita alisema kwa mshtuko akiwa ameshikilia midomo yake.

    “Ndiyo hivyo, leo wamenichukua tena nikiwa usingizini na kunipeleka kwenye ulimwengu wao ambako wameniambia wanataka nikutoe wewe kama kafara, ufe mke wangu, nimekataa kwa sababu ninakupenda, wameniachia mpaka kesho ndiyo nitarejea tena kuwapa jibu, kama

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nitakataa, watachukua kila kilicho chao na tutarejea tena kwenye umaskini.”

    “Hawawezi, Mungu wetu ana nguvu kuliko wao na kila kitu tulichonacho ni halali yetu, hawana uwezo wa kutunyang’anya.”

    “Ni wachawi mke wangu.”

    “Mimi namwamini sana Mungu!”

    “Sasa tutafanyaje?”



    “Nitafunga, kumwomba Mungu apambane nao badala ya sisi, kisha tuone hiyo kesho!”

    “Kweli Mungu atawaweza?”

    “Galos! Huu ni wakati wa wewe kuamini kwamba Mungu wetu ana nguvu kuliko miungu mingine yote.”

    “Naogopa!”



    “Huhitaji kuogopa, acha tusubirie hiyo kesho tuone.”

    Hawakulala tena mpaka asubuhi, Rita akisali, huku Galos akiwa kando yake. baadaye alimwongoza sala ya toba, kama aliyoongozwa yeye kanisani, Galos akawa amempokea Kristo kama Mwokozi wa maisha yake. saa kumi na mbili alfajiri, walianza rasmi mfungo wakimwomba Mungu awalinde na kuwaepusha na nguvu za giza.



    Hawakutoka ndani siku hiyo mpaka jioni ya saa kumi na mbili, Rita akatoka chumbani kwenda jikoni kuandaa chakula, kilipokuwa tayari wote walijumuika mezani kula, Galos akionekana mwenye nguvu na matumaini, hofu yote ya mkono wa Mukulungu ikiwa imemtoka, alijisikia yu tayari kwa lolote kwani imani yake ilikuwa imepanda juu.



    Baada ya chakula wote walijitupa kitandani, wakaendelea na mazungumzo mbalimbali kuhusu maisha, saa tano na dakika arobaini na tano, Galos akapitiwa na usingizi, muda huo huo akajikuta yuko kwenye ulimwengu wa kichawi. Rita akanyanyuka kitandani na kuanza kusali akimwomba Mungu ajibu kwa mapigo dhidi ya Mukulungu na jeshi lake.



    Kwenye ulimwengu wa giza Galos hakuwa wa kawaida, alikuwa na nguvu mno, Mukulungu na jeshi lake walishindwa kumtuliza na kujikuta wakipokea vipigo na wengi kuchomwa moto, mwisho wakasalimu amri na kulala chini kifudifudi kutii amri ya Galos.

    “Ufalme wako Mukulungu umefika mwisho, nguvu ya Mungu iko mahali hapa kusambaratisha kila kitu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo Galos.”“Ni wakati wa wewe na watu wako kutubu, mkamrejee Bwana, kwani mmetenda maovu kwa muda mrefu, mmeharibu maisha ya watu na kuwaua wengi, tubuni sasa mkapate kusamehewa.”

    “Tuko tayari!” watu wote wakaitikia.

    “Basi simameni kwa miguu yenu.”



    Wote wakanyanyuka na kusimama wima, Galos akawaongoza sala ya toba, wakaapa wasingeshiriki uchawi tena maisha yao yote yaliyobaki, alipowaeleza juu ya ubatizo wote walitamani kubatizwa lakini Galos aligundua hakuwa na uwezo wa kufanya jambo hilo, akawataka wafike kanisani Word



    Alive, Sinza Mori ambako wangefundishwa Neno la Mungu na baadaye kubatizwa.

    Galos akafumbua macho na kumkuta Rita bado akisali na kunena kwa lugha mpya, akakiacha kitanda na kumkumbatia mke wake, wakalia kwa furaha sababu ya ushindi waliokuwa wameupata.

    Siku ya Jumapili Kanisa la Word Alive lilijaa idadi kubwa sana ya watu kuliko kawaida, wengi wakiwa



    ni watu maarufu lakini kumbe walikuwa wakishiriki mambo ya ushirikina, wote wakakabidhi maisha yao kwa Mungu, na Galos hakudiriki kufungua mdomo wake kutoboa siri ya yaliyotokea usiku, kila kitu alikiacha mikononi mwa Mungu.



    Yeye na watu hao wasiopungua mia mbili na ishirini walibatizwa wiki mbili baadaye mafundisho yalipokamilika, ukawa mwanzo mpya wa maisha kwa Galos na mke wake Rita, ambaye mwaka mmoja baadaye wakiwa na utajiri wao alijifungua mtoto wa kike, wakampa jina Genesis.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog