IMEANDIKWA NA : IRENE MWAMFUPE
*********************************************************************************
COMPLETE - IMEKAMILIKA YOTE
Simulizi : Padri Mla Nyama Za Watu
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mkasa huu unasimuliwa na Padri Moses au kwa kifupi Faza Moze lakini si jina lake halisi , akiweka bayana mambo aliyoyafanya mpaka kujutia. Padri Moses
hakutaka kuweka wazi ni wa kanisa gani kwani Mapdri hutumiwa na makanisa ya Anglikani na Romani. Anasema:
“Ilikuwa mwaka 1999, mwezi Desemba wakati wakristo wanajiandaa kwa sherehe ya Krismasi, kanisani walikuja wazee wawili ambao ni wageni machoni pangu
miongoni mwa waumini wa kanisa langu hilo .
Walikaa fomu moja na waumini wengine, lakini katika kukaa walitenganishwa na mzee mmoja. Nikiwa naendelea na ibada, kila wakati niliwaona wale wazee
wageni wakiangaliana kwa kupitia mgongoni kwa yule mzee aliyewatenganisha.
Kwa sababu moyo wangu ulikosa amani na wao, nikawa nawakazia macho hatua kwa hatua ili nione kila walichokuwa wakikifanya.
Kuna wakati nilishtuka sana kuona mmoja wao akibadilika sura na kuwa kama ya bundi, lakini nilipojiweka sawa kushangaa, akarudi katika sura ya kawaida,
na mwenzake akacheka kama vile alijua mwenzake amegeuka sura na mimi nimeogopa.
Ndipo nilipoanza kukumbuka ujaji wao kama ulifanana na mazingira ya kuwa waumini wangu.
Nikakumbuka kuwa, wakati wanaingia, walipitia njia zote za uumini, na pia walionekana ni wanyenyekevu kupita hata waumini wangu wa kila siku.
Wakati nikiwaza hayo, ghafla mmoja wa wale wazee alisimama mbele yangu bila kumwona akitoka kwenye fomu kuja mbele, nikashituka, lakini kumbe
waumini wengine waliniona nilivyoshituka, wakakaza macho kiwangu wakishangaa.
Nilikatisha maneno ya ibada na kuinua mikono juu kisha nikafanya ishara ya msalaba, kwa jina la baba, la mwana na la roho…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akapotea mbele ya macho yangu na kuonekana amekaa na mwezake kama mwanzoni, wakacheka sana lakini si kwa kutoa sauti.
“Nilishtuka sana , nikafikicha macho kuyaweka sawasawa kwani yalionekana kama yana ukungu wa moshi.
Yalipokaa sawasawa, nikaendelea na ibada lakini mwili wangu ukiwa umechoka sana, hauna nguvu tena mwilini kama kuna vitu vunatembeatembea.
Baadhi ya waumini walipata picha hiyo, kwamba sikuwa sawasawa, lakini walikuwa hawajui kama nilikuwa naona watu wa ajabu.
Nilipofika eneo la kuongea maneno ambayo ikawalazimu waumini wasimame, wale wazee wawili wakawa wa kwanza kusimama kabla sijamaliza maneno na
wakawa warefu kuliko waumini wangine.
Kurefuka kwao kama kuliambatana na moshi mkubwa wa moto wa kuni.
Nilipowaangalia waumini wengine walionekana hakuna wanalolijua kuhusu maono yangu kwani walisimama, wakafunga mikono kwa unyenyekevu mkubwa
wakinisikiliza.
Kama wangekuwa wamegundua kitu, basi hata wale waumini waliokaa jirani wangejua, kwani wao walikuwa wakinitazama tu wakati jirani yao kuna mambo
ya ajabu!
Nilikata maneno ya ibada na kuwaamuru waumini wakae, wakatii lakini mshangao:
“Humu ndani kuna watu wawili naona kama si wa imani yetu,” nilisema.
Waumini wote wakawa wanageukageuka na kutazamana wakiwatafuta wao watu wawili.
Walichokifanya wale wazee sasa, muumini aliyekaa katikati yao alipogeuka kumwangalia mmoja wao, wakaonekana wote wamekaa pamoja na yule muumini
akawa amekaa pembeni yao, kwa hiyo alipogeuka akawa anamwangalia muumini ambaye anamfahamu.
“Naamini hakuna atakayeweza kuwaona, maana wanatumika sana na ibilisi,” nilisema.
Ninawapa muda wa wao kujisema ni akina nani?” Nilisema huku nikiwaangalia kwa kuwakazia macho huku waumini nao wakinikazia macho mimi na
kuyafuatilia ninakoangalia.
Mara walipotea machoni pangu. Niliwaambia waumini kuwa, wametoweka na nikaonesha mahali walipokuwa wamekaa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule mzee aliyewekwa kati akasema, anachojua yeye ni kwamba, waumini waliokwenda kukaa kulia na kushoto kwake ni wanawake na alitaka kuwauliza kisa
cha kukaa upande ule wa wanaume.
Basi, niliendelea na ibada huku kila muumini akionekana hana amani moyoni. Hata pale alipoingia mtu na kuliza mlio wa viatu sakafuni, waumini wote
waligeuka kuangalia mpaka ikabidi mimi nisitishe kuendelea na ibada ili waumini wamalize kuangalia.
Ibada ilipokwisha, niliingia kwenye chumba nikavua mavazi ya utumishi, nikabaki na mavazi yangu ya kawaida. Nikiwa natoka nje ya chumba, ghafla nikaona giza nene mbele.
Nikawahi kushika flemu ya mlango huku nikiwa nahakikisha sianguki au kukanyaga sehemu ambayo siyo ardhi. Mpaka hapo nilikuwa siunganishi tatizo la
kuona giza na uwepo wa wale waumini wawili wa ajabu ajabu.
“Mtumishi wa Mungu kwema?” Nilisikia sauti ikiniuliza.
“Siyo kwema kabisa.”
“Unaona nini mbele?”
“Naona giza .”
“Fumba macho.”
Nilifumba.
“Haya fumbua sasa.”
Nilifumbua.
Nikaendelea kuona kama kawaida, lakini hakukuwepo na mtu yeyote aliyesimama mbele, nyuma, kulia wala kushoto kwangu.
Lakini pamoja na hali hiyo, niliisaka ile sauti akilini mwangu na kuigundua kuwa, ilikuwa ya yule mzee aliyekaa jirani na wale watu wa ajabu.
“Khaa!” Nilijikuta nikishangaa sasa.
Nilitembea kwa mwendo wa haraka hadi kwa waumini waliokuwa wamesimama nje ya kanisa wakiongea, wengine wakisalimiana na kuulizana maisha, kwani
waumini wengi huitumia Jumapili kuonana na kuongea mambo yao mbalimbali ya maisha.
Nilizungusha macho kumwangalia yule mzee, nikamwona katikati ya watu akicheka na kupiga soga na wazee wenzake, nikamfuata, lakini huku waumini
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ninaowapita wakinisalimia, wengine wakionekana kutaka kujua kile kisa cha ndani ya kanisa.
Wakati nakaribia kumfikia, nilijiuliza mwenyew, je, kweli kwa sauti ile kama angekuwa ni yeye angeshafika katikati ya watu?
“ Kama ni hivyo, mbona sasa wakati nafumbua macho sikumwona mbele yangu?”
“Faza pole na majukumu bwana,” yule mzee niliyekuwa namfuata alinisalimia na kuwawahi wenzake wote aliyosimama nao. Sauti yake niliikumbuka vizuri
sana, ndiyo ile iliyonielekeza mpaka nikafumbua macho.
“Nimeshapoa mzee wangu.”
Wazee wengine nao pia wakanisalimia huku wakinipa mikono.
“Eti mzee ulikuwa unasemaje?” Nilimuuliza yule mzee.
“Wapi?” Na yeye aliniuliza.
“Hukusimama na mimi pale mlangoni?”
“Mlangoni! Wapi?”
“Kule kwenye chumba?”
“Hata, hapana.”
Wazee wengine nao wakaonesha kunishangaa mimi, nikajisikia soni kwa nafasi yangu ya u-Padri.
“Oke, sawa basi.”
Nilitembea kwenda kwenye ofisi yangu, lakini nyuma nikamsikia mzee mmoja akisema.
“Kwani mzee Makwaya imekuwaje?”
“Sijui chochote,” mzee Makwaya alijibu, hali ya mshangao na minong’ono ya chini kwa chini iliendelea hadi ilipofika mahali nikawa siwasikii.
Kule ofisini nilikuwa peke yangu, nikainamia mezani na kuwaza ile hali mwanzo hadi pale ilipofikia nikaona giza nene mbele yangu.
“Hivi, wale ni akina nani?”
“Ni kwanini walinijia kanisani?”
“Wametumwa au?”
Nikiwa naendelea kuwaza hivyo, mara nikasikia sauti ndani ya ofisi.
“Unaendeleaje mtumishi wa Mungu?”
Ilikuwa ni sauti ya yule yule mzee Makwaya.
Nilishtuka sana , nikaangalia kila kona ya ofisi.
“Hakuwepo popote pale jambo lililonifanya nizidi kuogopa.
Nikiwa natafakari huku kijasho chembamba kikinichuruzika, mara nikasikia kishindo kikuu kwa nje kama vile kuna kitu kizito kinatua toka juu kwenda
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ardhini.
“Wewe ni nani?” Niliuliza lakini sauti yangu ikitoka kwa woga.
Sikusikia jibu wala sauti yoyote, ulipita ukimya, nikaendelea kutafakari huku kama nashikwa na usingizi mzito na macho yangu hayaoni.
Ghafla nilihisi kiumbe kusimama mbele yangu, nikajitahidi kufumbua macho.
Niliona binadamu mwenye mguu mmoja, sikio moja, mkono mmoja, tundu moja la pua, jicho moja amesimama mbele yangu akiachia tabasamu la kutisha.
“Kwa jina la baba na la mwana na la…”
Kabla sijamaliza kusema, alipotea mbele yangu, lakini bado macho yangu yakawa yana kivuli chake kwani alikuwa wa kutisha sana sijapata kuona mfanowe.
*********************************************************
Nilitamani waumini wangu, hata mmoja tu aje, lakini ajabu ni kwamba hakukuwa na dalili na si haikuwa kawaida yao, kwani mara zote, kila baada ya ibada
waumini walikuja ofisini kwangu na kueleza matatizo yao.
Ilifika mahali nikahisi labda siko mahali salama, labda mimi niliona nipo ofisini lakini kumbe sikuwa ofisini, ingawa nilipojaribu kutupa macho huku na kule,
akili yangu iliamini niko ofisini kwangu.
“Ngo ngo ngo.”
Mlango uligongwa.
“Karibu, ingia,” niliitikia haraka.
Waliingia wanawake wawili, wakiwa wamejitanda vitenge hadi kichwani na kubakiza uso tu. Walikuwa wageni machoni pangu, nikiwa na maana sijawahi
kuwaona hata siku moja katika maisha yangu ya utumishi.
“Karibuni sana akina mama.”
Hakuna aliyejibu hata kwa kutingisha kichwa.
Waliangalia wenyewe sehemu ya kuketi, wakaketi na kunikazia macho mimi.
Na mimi niliwaangalia kwa uso wa kuwauliza shida yao . Lakini hakuna aliyesema mpaka mimi nilipotoa sauti yangu.
“Niwasaidieni nini akina mama zangu?”
Ajabu iliyotokea hapo sijapata kuona wala kuisikia siku yoyote ile.
“Tuna shida na wewe Padri,” alisema mmoja, lakini kwa sauti nene na nzito, ya kiume.
Kwanza nilishtuka sana kusikia sauti ya kiume ikitoka kwenye mwili ule mwembamba.
“Shida gani mama zanguni?” Niliwauliza kwa sauti yenye woga woga kwani sasa nilianza kuyaona maisha yangu kama yanajaribiwa.
“Tunataka kuwa na wewe kazini kwetu,” alisema yule wa pili ambaye naye sauti yake ilikuwa nene zaidi kupita ya wa kwanza hadi nikajikuta nikitetemeka.
“Mna…mnanitaka kwe…kwenye kazi gani?” Niliuliza huku sauti yangu ikitetemeka kwa wasiwasi mkubwa moyoni, jasho jembamba lilizidi kuchuruzika licha
ya kwamba nilipoingia niliwasha pangaboi.
“Ina maana hutujui?” Wote walisema kwa wakati mmoja huku wakisimama na kujivua vitenge. Nilishangaa sana kuwaona wamebaki na suruali na mashati,
ina maana kumbe ni wanaume kama mimi na walivaa vile kike ili kinipoteza mawazo ya awali, niliwaza kwa wasiwasi huku nikiwakodolea macho pima.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mtumishi wa Mungu aliye hai, tunakutaka kwenye kazi yetu bwana, eee?”
Mmoja wao alisema akinisogelea nilipokuwa nimekaa mimi. Sasa niliibaini sauti yake, ndiyo ile ya yule mzee muumini wangu.
“Nyinyi si mliingia kanisani kwangu loe mkawa mnafanya maajabu?”
“Eee, ni sisi,” walinijibu huku yule wa pili naye akisimama, akanisogelea na kusimama sambamba na mwenzake.
“Sasa mnataka nikafanye kazi gani na nyinyi, ya maajabu kama nyinyi?”
“Eee, ndiyo,” walijibu wote.
“Mnatoka wapi?”
Mmoja wao akajibu:
“Tunatoka kwa Mungu.”
“Yupi?” Niliwauliza huku nikiwa nataka kusema ‘kwa jina la baba na la mwana…lakini wakaniwahi wao kwa kusema:
“Mungu kama wako, ametutuma kwako, amesema unatakiwa kupata nguvu ambayo na sisi tunayo, kwa hiyo na sisi tunakupa nguvu hii, POKEA!”
Waliposema ‘pokea’ walinigusa kwa pamoja kwenye paji la uso, nikaanguka chini na kupoteza fahamu.
Nilipokuja kuzinduka, nilikuwa katikati ya pori lenye miti minene, mirefu na matawi yakiwa juu sana .
Nililala kwenye nyasi, pembeni yangu nilizungukwa na watu wengi ambao niliwaona miguu tu. Kwa haraka haraka nilihesabu miguu ile na kupata idadi ya
ishirini na sita, ina maana watu waliosimama walikuwa kumi na watatu.
Niliinuka ili kukaa, lakini mmoja wa wale watu alinizuia nisikae, niendelee kulala, nikatii kwa vitendo na kurudi kujilaza majanini.
Ghafla nikasikia sauti nzito, yenye tetemeko.
“Umetakiwa kupokea nguvu ya kwetu,” ilisema ile sauti.
Yakapigwa makofi pale, halafu ukafuatia ukimya wa muda mrefu kama vile nililala peke yangu bila kuwepo mtu mwingine.
“Simama,” ile sauti ilisema kwa haraka na kwa amri.
Nilijikuta nasimama lakini nikiwa ndani ya ofisi yangu. Nilijiangalia na kujiona niko kama nilivyovaa awali, kila kitu ndani ya ofisi kilikuwa sawasawa, hakuna
hata kitu kimoja kilichoharibika au kutokuwepo.
Hofu ikaniingia kuhusu waumini wangu nje, kwamba kama walikuja wakakuta mazingira yenye utata wataelewaje?
Niliusogelea mlango na kushika kitasa, nikaufungua polepole na kuangalia nje. Hakukuwa na muumini hata mmoja, hata mtoto.
“Khaaa!” Nilishangaa.
“Ina maana nimetumia muda mwingi sana ?” Nilijiuliza.
Niliangalia saa ya ukutani na kugundua kuwa, wakati namaliza ibada ilikuwa saa nne na nusu, muda ule naangalia saa ilikuwa saa saba mchana, ina maana
kuingia kwa wale watu, kupoteza fahamu hadi kuzinduka ilipita saa tatu?!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mlango uligongwa, akaingia mtu mmoja, simfahamu. Nilimkaribisha, akakaa kwenye fomu.
“Nikusaidie?”
“Ee baba, mimi nimekuja uniombee,” alisema akijiweka sawasawa.
“Nikuombee nini?”
“Uniombee naumwa.”
“Unaumwa nini?”
“Huwa nikilala usiku naona watu wanakuja kunikaba.”
“Unaona au unaota?”
“Naona, wakati mwingine huwa napiga kelele kwa kuwaogopa.”
“Wewe ni muumini wangu?”
“Hapana, nasali mjini.”
“Sasa kwanini usiende kwa mtumishi wa Mungu wa kanisa lako?”
“Ameshaniombea sana lakini hakuna mafanikio.”
“Sasa unaamini nini kuja kwangu, kuna mafanikio?”
“Naamini yapo mtumishi.”
Nilihisi ni miongoni mwa wale watu walionijia na kunifanyia maajabu yao, lakini sijui ni nini, kwani ghafla nilijawa na ujasiri wa kutoogopa lolote na kuamua
kumwombea kweli.
Nilisimama, nikamtaka yeye apige magoti kisha nikamwekea mkono wangu wa kulia kichwani kwake na kuomba sana mpaka akaanguka chini.
Alipokuja kusimama, akasema anajisikia mwepesi, ana imani amepona kabisa.
“Usijali, nenda kwa amani lakini jilinde na dhambi.”
“Sawa Padri.”
Alipoondoka tu, mzee mmoja, aliyevaa shuka jeusi kuzunguka kiuno, chini akiwa hana kiatu wala sendoz, pekupeku, ju mabega wazi, mkononi alishika mkia wa mnyama, alisimama mbele yangu bila kujua aliingiaje?
“Karibu mzee wangu,” nilimkaribisha kwa ujasiri mkubwa sana, moyoni sikuwa na hofu wala wasiwasi. Pamoja na kuvaa kiajabu kama vile, lakini nilimwona kama mtu wa kawaida sana kwangu.
“Fumba kiganja cha mkononi,” aliniambia kwa amri.
Nikajikuta nafumba bila kuhoji yeye ni nani na ametoka wapi na kaja kwangu kufanya nini.
“Fumbua.”
Nilipofumbua, unga mweusi ulikijaza kiganja changu.
“Jipake kidogo usoni.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijipaka kidogo huku nikiwa nimeinama kuangalia chini.
“Unaona nini?”
“Sioni kitu.”
“Haya, hiyo dawa ndiyo tunayotumia kufanyia kazi, tunapotoka usiku kwenda kazini kila mmoja anakuwa na dawa hiyo, ndiyo inayosaidia watu wasituone…
“Fumba kiganja.”
Nikafumba.
“Fumbua.”
Nilipofumbua, sikuona ile dawa, kiganja kilikuwa cheupe kama mwanzo.
“Fumba tena kiganja.”
Nikafumba…
“Fumbua.”
Nilipofumbua mkononi, nusu kulikuwa na unga unga wa kijani nusu unga unga mweusi.
“Chota huo unga kisha changanya.”
Nilitii, kisha akaniambia nijipake kidogo usoni, nikafanya hivyo na kujikuta nakuwa mwepesi kuliko kawaida ya siku zote.
“Unaona nini?”
“Najiona mwepesi sana .”
“Unaweza kujaribu kupaa?”
“Nijaribu?”
“Jaribu basi.”
Niliinua mikono kama vile ndege anavyoinua mabawa, taratibu nilijiona napaa juu huku miguu ikiiacha ardhi taratibu bila ridhaa yangu.
“Unaonaje?”
“Napaa sasa.”
“Shusha mikono.”
Niliishusha, taratibu miguu ikakanyaga ardhi na kusimama kama mwanzo.
Baada ya hapo yule mtu akapotea machoni pangu na kuniacha nikiwa na maswali kibao.
Nilijiweka sawa, nikafunga madirisha ili kutoka, nikafunga mlango na kuondoka kabisa katika eneo la ofisi.
Nilikwenda kwenye makazi yangu, lakini kwa wakati huo nilijihisi mnyonge sana, mwili ulikuwa hauna nguvu, macho hayaoni vizuri mbele na miguu mizito.
Saa saba za usiku, nilishtuka kutoka usingizini baada ya kushikwa na kuvutwa kidole cha mguu wa kulia na mtu. Kulikuwa na giza kwa hiyo sikujua nani alifanya zoezi lile.
Swichi ya kuwashia taa haikuwa mbali na nilipolala, nikaiwasha chapchap, chumba kilipojaa mwanga sikuona kitu, nikaendelea kulala.
Baada ya muda nikawa katika ndoto.
“Wewe Padri, unadhani utafanya kazi mpaka lini?”
“Mungu apende,” nilijibu.
“Je, asipopenda?”
“Atapenda tu.”
“Kwanini unafanya kazi lakini huna nguvu.”
“Nguvu gani?”
“Ya kiroho.”
“Kwa sababu bado.”
“Bado nini?”
“Wakati wa kuwa na nguvu.”
“Ni sasa.”
“Kwa maana ipi?”
“Njoo.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimfuata huyo mtu, akanishika na kunivuta hadi mahali, akasimama na kuniambia.
“Nenda kaingie kwenye kanisa lile.”
Mbele yangu kulikuwa na kanisa, nikaenda kuingia.
Lilikuwa kanisa langu, waumini wangu, wake kwa waume wengine wamekaa wengine wamesimama. Walikuwa wengi sana.
Mimi nikapita hadi mbele kwenye madhabahu na kusimama pale.
“Wale wenye matatizo waje niwaombee.”
Karibu kanisa zima walipita mbele kuombewa.
Ule wingi wao, nikaanza kuogopa kwamba nitaweza kweli?
Wa kwanza nikamwekea mikono juu kichwani na kumwombea, pale pale aliposimama akaanza kupiga kelele na kuanguka chini kisha akasimama akiwa amepona na kurukaruka huku akimtukuza Mungu wake.
“Hee, hee nimekuwa mzima sasa.”
“Nenda usitende dhambi tena, sawa?”
“Sawa.”
Niliombea karibu kanisa zima, nilipomaliza nikawa natoka huku napigiwa makofi na waumini waliokuwa wamesimama kulia na kushoto kwangu.
“Padiri Padiri Padiri,” walisema wakipiga makofi, pwa pwa pwa.
Kufika nje, nikakutana na yule mtu aliyenichukua nyumbani.
“Umefanikiwa?”
“ Sana ,” nilimjibu.
“Umekubali?”
“Nini?”
“Kwamba wakati wa kuwa na nguvu ya kiroho ni sasa?”
“Nimekubali.”
“Haya, sasa twende kwa aliyekupa nguvu.”
“Kwa Mungu?”
“Wetu sisi.”
Tuliongozana hadi kwenye mti mmoja mkubwa, mrefu sana kwenda juu.
Chini walikaa watu wengi wakiwa kama wapo kwenye maongezi.
Kilichonishangaza miongoni mwa hao watu walikuwepo waumini wangu wa kanisani.
“Afadhali umekuja faza.”
“Faza nimefurahi sana kukuona.”
“Faza karibu sana .”
Wale waumini wangu wote walinikaribisha kwa furaha, amani na upendo wa hali ya juu.
Nilikaa sehemu ambayo kulikuwa na nafasi ya mtu mmoja, yule mtu niliyekwenda naye sikumwona tena alikopotelea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bwaba umekuja huku, uko tayari kwa lolote?” Aliniuliza mzee wa kanisani ambaye sikuwa na mazoea naye.
“Kwani hapa ni wapi?” Nilihoji.
“Hapa ni kwa wachawi.”
“Wachawi!”
“Eee, umekuja kwa wachawi, kazini kwetu, karibu.”
Alipomaliza kusema, alikaa chini, akasimama sasa yule mzee ambaye siku ile kanisani walipoingia wale watu wawili wa ajabu, yeye alikaa katikati yao.
“Eee, nina kila sababu ya kujisifu kwa kupewa heshima hii ya kumkuza kazini mtu mkubwa kama huyu,” alisema yule mzee.
Yakapigwa makofi kwa muda wa dakika tano nzima huku yule mzee akiwa amesimama tu akisubiri yaishe ili aendelee kuongea.
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namwangalia mimi, alikuwa anaongea kwa kujiamini sana na hakuonekana kujali kama mimi ni kiongozi wake wa kiroho.
“Kwa hiyo kuanzia leo mtumishi utakuwa chini yangu ukizitii na kuzifuata amri zangu, sawa bwana mdogo?”
Nilimjibu kwa sauti ya unyonge sana
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment