Search This Blog

MAITI YANGU - 2

 





    Simulizi : Maiti Yangu

    Sehemu Ya Pili (2)



    ************



    jeneza lilifunguliwa upande wa kichwani... na watu wakajipanga kwenye mstari mmoja kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu peto... peto alipo ona jeneza limefunguliwa alifurahi sana alitimua mbio kuelekea pale jeneza lilipokuwepo ili aungane na kiwiwili chake.... alipofika alijaribu kuingia lakini alistahajabu sana.. kashindwa kuungana na kiwiliwili chake... kisha akasema ""jamani kiwiliwili changu mimi ni nafsi yako.....nihurumie""" mmh!! inamaana nazikwa huku najiona hivi hivi.... yani hata kiwiliwili changu kinanikana mimi nafsi yake.. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kumbe ili nafsi ya peto iungane na kiwiliwili ni lazima kiwiliwili kirudishwe pale kitandani kilipokuwa...

    peto alianza kulia kwa uchungu....baada ya watu waliohudhulia msiba wa peto walimaliza kuaga mwili wa marehem peto.... na kujiandaa kuelekea makaburini kwa ajili ya kuuzika.. peto alizidi kuchanganyikiwa.. baada ya kuona jeneza lake likibebwa kupelekwa ndani ya gari.



    Peto alianza kuangua kilio... alipiga mayowe ya kuomba msaada bila mafanikio yoyote... alimshi dereva... ili ahairishe kuendesha gari kuelekea makaburini.. dereva hakumjali peto... alibaki kimya huku akionesha wazi kutomsikia peto anaongea nini"" kisha dereva akazipiga hatua kuelekea upande mwingine... jamani mbona binadamu hamna huruma... alijisemea peto huku akilia kwa uchungu... peto hakukata tamaa aliendelea kuwasihi watu waliohudhuria msiba wale wasizike kiwilwili chake... aliamini huenda wakamsikia... peto aliamua kuchukuwa mawe mawili na kuyaweka chini ya matari ya gari ili lisiondoke.... kwa mbali alimuona chales akiingia upande wa ndani ya nyumba.... peto alitimua mbio kuelekea mule ndani alimoingia chales...peto alipofika alimwambia chales mwanangu tazama mimi baba yako ninavyoangaika!!!! nionee huruma mwanangu... ebu fikiria kama watazika kiwiliwili changu itakuwaje? ni nani atakaye kutunza zaidi ya mimi baba yako....ebu jaribu kuwaambia watu warudishe kiwiliwili changu kitandani kwangu hienda kikakubali kuungana na nafsi yangu" peto aliyasema maneno hayo huku akilia kwa uchumgu mkubwa.... wakati huo chales alikuwa kaketi chumbani kwake huku kashika tama akilia huku akimkumbuka marehemu baba yake.....hakika nilikupenda sana baba yangu lakini mungu kakupenda zaidi...alijisemea moyoni chales""huku akilia kwa uchungu... jamani mwanangu unalia nini mimi sijafa... alisema peto"" chales alionekana kuwa kimya bila kujibu chochote...

    kisha akanyanyuka pale alipokuwa ameketi na kuelekea upande wa nje... Peto alianza kuingiwa matumaini huwenda sasahivi mwanae kamsikia alichokuwa akimwambia ndio maana anatoka nje... asante mwangu kawaambie" peto alisema hivyo.. kisha akazipiga hatua kumfata chales kule upande wa nje.



    **************



    peto alipofika nje alistahajabu sana..kumuona chales akipitiliza na kwenda kuketi.... agh inamaana hakusikia yale yote niliyokuwa nikimwambia!!!! peto alijisemea moyoni""sasa hapo peto alianza kumkumbuka mungu aliamini mungu anao uwezo kuliko binadamu.......peto. alipiga magoti na kuanza kumuomba mungu huenda wakahairisha kizika kiwiliwili chake.... peto aliomba huku akilia kwa uchungu.. uso na macho yake yalionesha wazi kujutia..masanja umeniponza mimi laiti ningejua nisingekubaliana na wewe kunipeleka kujiunga na chama cha wachawi... tazama sasa hata nyinyi wachawi wenzangu mmeshindwa kunisaidia mimi mwenzenu!!!!! alisema peto huku akilia na kugalagala chini.....alipo ona hakuna msaada wowote aliamua kunyanyuka pale chini... aliona wakina mama wakilia kwa uchungu...hata yule jirani aliyetaka kuuliwa kichawi na mke wa peto naye alilia kwa uchungu mkubwa... pete alizidi kuchanganyikiwa alipo ona watu wengine walilia mpaka kuzimia.... peto aliweka mikono kichwani huku akiwatazama watu wakilia.... hivi hawa akinamama nahisi akili zao sio nzuri uani wanamlilia mtu ambaye hajafa!!!! alijisemea moyoni peto,,, kisha akapaza sauti jamani tusikilizane mimi sijafa embu acheni mchezo na kiwiliwili changu... watu hawakuonesha kumjali peto.... kisha akaona watu wakiingia ndani ya magari ili waelekee makaburini..... peto alizidi kuchanganyikiwa..watu wote waliingia ndani ya magari na wengine wakitembea kwa miguu kuelekea makaburini... alipotazama huku na kule aliona watu wanazidi kupungua.... aliamua kuzipiga hatua za haraka akaingia ndani ya gari lililobeba kiwiliwili chake.... na safari ya kuelekea makaburini ikaanza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alionekana derva akiingia ndani ya gari lililobeba kiwiliwili cha peto.. dereva alipoliwasha gari peto alichanganyikiwa... safari ikaanza"" makaburi hayakuwa mbali sana iliwachukuwa dakika 45 kufika makaburini... walipofika.. Peto alikuwa wa kwanza kushuka... kwa mbali aliona mafundi wajenzi wakiwa wanachanganya zege.... peto alizidi kuchanganyikiwa aliamini bila shaka mafundi wale walikuwa wakiandaa zege kwa ajili ya kaburi lake... alitimua mbio mpaka pale walipokuwepo mafundi.. alipofika alichungulia ndani ya shimo... jamani mbona hamna huruma inamaana ndio mnazika humu kiwiliwili changu... kisha akawatazama mafundi wale alimuona fundi mmoja aliyekuwa akimfahamu alimsogelea na kumsihi wasizike kiwiliwili chake""'" fundi eee kwani haunikumbuki??? mimi peto na sijafa....aliongea peto huku uso wake ukionekana kuwa na huzuni kubwa... fundi yule hakumjibu peto aliendelea kuchanganya simenti na mchanga vikiambatana na kokoto" huku akipiga stori na mafundi mwenzake.....yule fundi mwingine alisikika akisema ongeza simenti zege iwe kali...peto aliposikia hivyo alitamani amnyang'anye koleo fundi. alijaribu kufanya hivyo lakini alishindwa..... alipotazama upande wa kushoto aliona watu wakiwa wamebeba jeneza wakija huo upande aliokuwepo peto... peto alianza kulia.. alibaki akiwatazama watu wale... jamani hivi kweli hawanisikii au wanataka kunikomoa tu!!!! eti fundi hamnisikii??? alisema peto"" mafundi wale hawakumjibu kitu waliendelea kufanya kazi yao. nakuonekana kutomjali.. punde jeneza lililetwa likawekwa kando ya kaburi... peto aliweka mikono yake kichwani.... na kuangua kilio kwa kupiga mayowe.... lakini haikusaidia kisha alionekana mchungaji akija upande wa kaburi ili auwombee mwili wa marehem peto....... watu wote walifumba macho kisha mchumgaji akaendelea na maombi.. peto aliona huo ndio muda mzuri wa kufingua jeneza aingie kwenye kiwiwili chake. alipojaribu kulifungua jeneza alishindwa..



    ****************



    punde mchungaji alimali maombi.... peto aliona watu wanachukua kamba na kuziweka katijeneza kisha wakaanza kulishutaratibu kuliingiza nadani ya kaburi... aisee peto aliangua kilio...alijaribu kuwazuia watu wale wasiliingize jeneza kaburini lakini alishindwa.... punde walimaliza kuliingiza jeneza kisha mchungaji akasema mtoto wa marehemu ataanza kuweka mchanga kwenye kaburi la baba yake huku akifatiwa na ndugu na jamaa wa karibu na peto... chales alichota mchanga na kutupa ndani ya kabiri.. huku akilia kwa uchungu.. baba yangu inamaana sitokuona tena?? chales alisema huku analia""" peto alipaza sauti mwanangu mimi sijafa yani hata wewe unakubali kubali kunizika mzimamzima hivi najiona"""" chales aliendele kutupa mchanga ndani ya kaburi na kuondoka.. walifuta ndugu na jamaa pamoja na marafiki wa peto.... walipo maliza""" watu walianza kuchukua makoleo na kuanza kufukia kaburi la peto... mara ghafla....ilisikika sauti ya mngurumo mkubwa ikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu... watu walianza kuogopa hata peto iwoga ilianza kumuingia.... watu waliokuwa wakilifukia kaburi la peto waliacha kufukia... huku wakistahajabu upepo huo unaovuma kwa kasi isiyo ya kawaida... mara ghafla peto aliona watu wakija ule upande wa kaburi alipoangalia kwa umakini aligundua ni wale wachawi wenzake wakiongozwa na Magembe ambaye ni mkuu wa wachawi... walipokaribia mara ghafla jeneza la peto lilianza kutoka kunako ndani ya kabiri likija upande wajuu na kujiweka kando ya kaburi.... watu walitimua mbio hakibaki hata mtu mmoja""""hata yule mchungaji alitimua mbio kutokana imani yake kuwa ndogo... peto alipo ona mpaka mchungaji katimua mbio ilibidi na yeye atimue mbio peto alikimbia utadhani alishawahi kushiriki mashindano ya mbio za mita mia....

    magembe na wachawi wenzake walilifiata kaburi kisha wakasimama karibu na jeneza la peto... mara ghafla....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    peto alikimbia mara ghafla akasita kuendelea kukimbia.. akasimama... dah!! hivi mimi ni mjinga kiasi gani? huenda wamekuja kunisaidia... alipogeuka atazame ule upande lilipokuwepo kaburi lake... aliona Magembe...Masanja pamoja na wachawi wengine watatu wamelizunguka jeneza lake..... ghafla wakatoweka pamoja na jeneza....peto alichanganyikiwa akapaza sauti huku anakimbia kurudi kule lilipokuwepo jeneza lake... jamani eee mbona mmenisahau nipo huku"" Magembe unapeleka wapi kiwiliwili changu??peto alisema maneno hayo huku anakimbia kwa kasi kama kafungwa mota miguuni... alikata tamaa na kuamua kuondoka haraka aende nyumbani kwa magembe. ...akiwa njiani anazipiga hatua aliona mtu anasukuma mkokoteni huku kabeba mzigo..alipotazama vizuri aligundua ni mkokoteni wake .. alimfata mtu huyo... kisha akamwambia.... mbona unatumia kitendea kazi changu bila ruhusa yangu??? mtu yule alibaki kimya hakumjibu peto....peto alikasirika sana.. akaanza kukunja mikono ya shati yake ili aanzishe ugomvi... ghafla akakumbuka kiwiliwili chake... akaanza kutimua mbio kielekea kule nyumbani kwa magembe... alipofika hakumkuta magembe.... hivi hawa watu mbona wanafanya mchezo na kiwiliwili changu!!!? peto alijisemea moyoni"""" punde magembe ambaye ndiye mkuu wa wachawi alikuja nyumbani kwake.....huku akiwa amemuacha masanja na wale wachawi wengine wapeleke kiwiliwili cha peto nyumbani kwa peto pale juu ya kitanda ili peto aweze kuungana na kiwiliwili chake"""magembe alikuwa na iwezo wa kumuona peto... kisha akamwambia ndani ya masaa matatu.. inatakiwa uwe umeshaungana na kiwiliwili chako.... sharti... itabidi utoe kafara la damu ya mtoto wako.... peto alichanganyikiwa baada ya kusikia masharti ya magembe..... peto aliamua kukubali..... kisha akajisemea moyoni.....nikiungana na kiwiliwili changu tu.....naacha uchawi na sitoweza kumtoa mtoto wangu kafara...."""""" magembe alimwambia peto waweza kwenda.... peto alianza kutimua mbio kuelekea nyumbani kwake..



    *********



    uleupande mwingine.. Masanja na wale wachawi wengine waliwasili nyumbani kwa peto... wakatokezea upande wa nyuma ya nyumba ya peto...kisha masanja akaingia kichawi ndani ya nyumba ya peto ili aangalie mazingira yamekaaje.... alipoingia kwenye chumba cha peto masanja alistahajabu kukuta chumba cha peto hakuna kitu ndani hata kitanda ambacho inatakiwa iwekwe maiti ya peto...ili peto aweze kuungana na kiwiliwili chake...kumbe chales alikifungua kitanda hicho na kukiweka stoo ili atandike mkeka mkubwa ipatikane nafasi ya kulala wageni waliosafiri kuja msibani......

    wakati huohuo peto alikuwa njiani akitimua mbio kuja nyumbani kwake.. punde alifika.. alipitiliza moja kwa moja chumbani kwake ili aungane na kiwiliwili chake.... alikutana uso kwa uso na masanja... masanja hakuwa na uwezo wa kumuona peto isipokuwa Magembe pekee. ..peto alistahajabu kuona hakuna kitanda wa kitu chochote....kisha akamuuliza masanja kiwiliwili changu kikowapi?? masanja hakujibu kitu.. alitoweka kichawi....wee rudi hapa nipeni kiwiliwili changu""alisema peto kwa sauti ya ukali"""

    masanja alitokezea upande wa nyuma ya nyumba kule alipowaacha wachawi wenzake na kiwiliwili cha peto. .....na kusema hii kazi itakuwa ngumu sana kisha wakatoweka kichawi kuelekea kwa mkuu wa wachawi Magembe....huku wakiliacha hapo chini jeneza la peto...



    *********



    Peto alitoka mule chumbani na kuelea upande wa nje.. alimuona mwanae chales akamfata na kumwambia kitanda changu kikowapi??? chales alibaki kimya...peto alizidi kuchanganikiwa aliamua kurudi ndani na kutazama saa ya ukutani ilikiwa ni saa kumi na moja... lisaa limojs limshakwisha.....peto alianza kuingiwa na uwoga wa hali ya juu aliamua kutokea mlango wa nyuma... alistuka kuliona jeneza lake... akazipiga hatua za taratibu kulifiata jeneza lilipokuwa..... alipofikaara ghafla..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliona jeneza linafunguka peke yake bila kufunguliwa na mtu.... peto aliona kiwiliwili chake alipojaribu kurudi aungane na kiwiliwili chake alishindwa""" dah! yani hata wewe unanikataa mimi nafsi yako embu kuwa na huruma!!!! tazama yamebaki masaa mawili tu.... niliyopewa ili nirudi kwenye kiwiliwili changu""" alisema peto akikiambia kiwiliwili chake..... huku akionesha sura ya upole....na huzuni kubwa.. peto aliamua kutoka upande ule na kuelekea upande wa mbele ya nyumba...... alianza kupiga mayowe kwa sauti kubwa... jamani eee nimebakiza masaa mawili tu.....nyinyi ndio mtasababisha mimi nife!!!!! watu hawakumjali ndio kwanza waliendelea kunawa mikono na kula chakula....aisee inamaana nakufa hivihivi nikiona!!!!!? alijiuza kimoyoni kisha akakunja suruali akaanza kutimua mbio kurudi nyumbani kwa mkubwa wa wachawi ambae ni Magembe... peto alikimbia bila kugeuka nyuma"" alipofika alichanganyikiwa baada ya kutomkuta magembe.... Mbona mnaniangaisha hivi... haki naapa nikifanikiwa kurudi kwenye kiwiliwili changu.. naokona na kuanza kumtumikia Mungu""" Eee Mungu nisaidie tazama navyoteseka!!!!!!



    ***************



    ITAENDELEA
    Pseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

Blog