Search This Blog

MAITI YANGU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Maiti Yangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Alionekana Peto akiwa katika shughuri zake za kila siku.. peto alikuwa akifanya kazi bandarini kwenye upande wa kubeba mizigo(KULI) kwa kutumia toroli lake lililokuwa likimuingizia pesa ya kujikimu yeye na mtoto wake.... peto alifiwa na mkewe miaka miwili iliyopita.... mkewe alifariki baada ya kujaribu kumuuwa kichawi...jirani yake baada ya kuona jirani yake kafanikiwa kimaendeleo... na kila siku zilipozidi kwenda jirani huyo alizidi kuwa na maisha mazuri"""mke wa peto aliingiwa na wivu...kwa sababu alikuwa mchawi aliamua kumroga jirani yake ili afe... lakini hakufanikiwa kwa sababu jirani huyo,,,yeye pamoja na familia yake walikuwa wachamungu... walikuwa na imani kali juu ya kumjua na kumuabudu mungu...

    mke wapeto alipojaribu kumtupia madawa jirani yake ili afe... ilishindikana yakamrudia yeye mwenyewe.... mke wa peto alianza kuugua ugonjwa usiojulikana... peto alijitahidi kadri ya uwezo wake kumpeleka hospitali mbalimbali lakini CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alipofanyiwa vipimo haikugundulika anaumwa nini.. kadri siku zilivyozidi kusonga mke wa peto alizidi kuwa mgonjwa zaidi''alianza kutisha kwani ngozi yake ilianza kuota mapele makubwa... na baada ya mwaka mmoja.. mke wa peto aliiaga dunia.... aliacha mtoto mmoja wa kiume aitwae chales..



    peto aliishi na mwanae chales.. alimpenda sana mwanae kwa sababu alikuwa na nidhamu..msikivu na mtiifu... peto alikuwa na rafiki yake kipenzi aitwae Masanja.. sikumoja masanja alimshawishi peto kuwa ajiunge na chama chao cha wachawi.. peto alishawishika. naakakubali masanja ampeleke akajiunge kwenye chama hicho cha wachawi...



    ***************



    Kesho tunayo kazi moja tu ya kumkaribisha PETO kuwa mshirika mwenzetu.. ilisikika sauti ya mkuu wa wachawi aitwae MAGEMBE.. ikisema hivyo kisha wachawi walitawanyika katika mti huo mkubwa wa M-BUYU....kila mmoja aliondoka kwa njia yake kuelekea nyumbani kwake.....

    kesho yake majira ya saa nane za usiku peto alijiunga rasmi kwenye chama hicho cha wachawi.. akaanza kuwa anaroga watu hata wale ambao hawana hatia wala ugomvi na yeye..



    siku moja peto alimka usiku wa manane akaenda katika mambo yake ya KISHIRIKINA(UCHAWI) na kuacha kiwiliwili chake kitandani ndani ya chumba chake ikaondoka nafsi ambayo ni kimvuli chake..

    peto alikuwa anaishi na mtoto wake wa kiume aitwae Chales....."Chalesi aliamka usiku huo akaingia chumbani kwa baba yake ili amwambie kuna wezi wameingia ndani ya uzio wao... chales alimuita baba yake lakini hakuamka aliamua kukitukisa kiwiliwili hicho bila mafanikio...alipojaribu kumgeza baba yake chales aligundua kua baba yake kaiaga dunia.. aliita majirani. wakapeleka maiti hiyo mochwali..PETO alipomaliza mambo yake ya uchawi,,,"" nafsi ambayo ni kivuli chake ilirudi nyumbani ili iungane na kiwiliwili chake.... Peto alistahajabu baada ya kukuta kiwiliwili chake hakikuwepo pale alipokiacha..



    Peto alichanganyikiwa... alijiuliza ni nani aliyeingia chumbani kwake na kukitoa kiwiliwili chake... aliamua kwenda chumbani kwa mtoto wake... lakini hakumkuta chales... peto aliamua kutoka nje... ili akitafute kiwiliwili chake kiungane na nafsi yake alipitia mlango wa nyuma...alistahajabu kukuta umati wa watu wakiwa wamelala nje huku wametandika maturubai. watu hawa wamefata nini nyumbani kwangu...alijiuliza peto.... kisha akazipiga hatua kuelekea upande mwingine aliona watu wakicheza karata... alikwenda mpaka pale.. aliamua kuuliza kumetokea nini hapa nyumbani kwangu?? alistahajabu watu wale hawakumjibu kitu.. waliendelea kucheza karata.... akaamua kumgusa mmoja... inamaana hamuelewi swali nililouliza??? lakini hakujibiwa... aliamua kuondoka... na kuelekea upande wa ndani...aliingia kupitia mlango wa mbele... alipofika sebuleni alistahajabu kuona wanawake wengi wamekusanyika huku wakilia....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    peto alizidi kuchanganyikiwa.... akatoka nje haraka... alipo angaza angaza macho aliweza kumuona chales ameketi huku akionekana kuwa na huzuni kubwa..

    peto alizipiga hatua za harakaharaka kuelekea pale chales alipokuwa ameketi... alipofika alimuuliza chales...kumetokea nini hapa nyumbani!!! mbona watu wamekusanyika??? chales hakujibu chochote... peto alikasirika akaamua kumpiga kofi chales"""peto alistahajabu

    sana baada ya kuona chales kaketi vilevile bila kutikisika... inamaana hunisikii au ni dharau?? aliuliza peto""" chale hakujibu kitu alibaki kimya...

    ghafla alimuona mama mmoja akitokea uoande wa ndani... peto aliamua kuzipiga hatua kumfata mama yule...alipomkaribia.. alimuuliza hivi kumetokea nini hapa nyumbani kwangu??? mama yule hakujibu kitu chochote aliendelea kuzipiga hatua kuelekea upande wa chooni.. peto alimfata mama yule... kisha akabaki upande wa nje akimsubili mama yule atoke...

    inamaana watu wote hawa hawanioni au?? alijiuliza bila kupata majibu...



    yule mama alipotoka chooni peto aliendelea kumuuliza... lakini mama yule alibaki kimya... unaleta dharau eee?? aliamua kupaza sauti.. sitaki kumuona mtu yeyote hapa nyumbani kwangu ondokeni... lakini watu walibaki kimya... inamaana hamnisikii??? naingia ndani nitakapotoka nje sitaki kukuta mtu... peto alisema hivyo huku akiwa na jazba kubwa... alizipiga hatua za haraka haraka... akaingia chumbani kwake... akatoka na panga... alikwenda moja kwa moja mpaka kwa wale watu waliokuwa wameketi kando huku wakicheza karata... alipiga panda juu ya meza ile... peto alistahajabu kuona watu wale wakiendelea kucheza karata bila wasiwasi.. peto alikasirika akamkata mtu moja panga la kichwa lakini panga lile lilipita kama upepo... halikumkata mtu yule!!!! peto aligundua kuwa hayupo katika mwili wa kibinadamu...huenda watu hawa hawanioni wala hawanisikii!!! peto aliamua kuingia ndani... na kuendelea kutafuta kiwiliwili chake....alipokikosa kiwiliwili chake... alianza kulia...ilia kwa uchumgu mkubwa lakini hakuna mtu aliyemuona wala kumsikia..... peto alitoka nje alipoangaza angaza macho mara ghafla



    Mara ghafla alimuona yule rafiki yake aitwae masanja...peto alizipigahatua kuelekea kule alipokuwa amekaa masanja alipofika... alimuuliza...eti rafiki yangu hunioni??? masanja alibaki kimya....peto alijaribu kumtikisa masanja lakini masanja hakuonekana kumjali... jamani hata wewe rafiki yangu uliyenishawishi nijiunge na chama chenu cha uchawi... leo hutaki kusema nami!!!!? alisema peto" lakini bado masanja alibaki kimya... peto alizipiga hatua kutoka hapo alipokuwa ameketi masanja" alimuona chales akiingia upande wa ndani... peto alitimua mbio kumfuata mwanae chales..aliingia moja kwa moja mpaka chumbani kwa chales... kisha akauliza kwani kiwiliwili changu kimepelekwa wapi?? chale hakujibu... peto alijawa na jazba aliamua kumpiga mtama mwanae chales... peto alistahajabu kumuona chales hakuanguka... peto alizidi kuchanganyikiwa.....usiku aliowona ni mrefu kupita siku zote...



    **********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    asubuhi palipokucha watu walizidi kuongezeka.... aliwaona makuli wenzake wakija nyumbani kwake...aliwafuata na kuwauliza kwani leo sio siku ua kazi? mbona mmekuja wote nyumbani kwangu??? watu wale hawakujibu kitu chochote... peto alistahajabu kuona watu waliokuwa wakifika... wanakwenda kwenye meza kisha wanaweka pesa kwenye sahani na kiandika kwenue daftari lililokuwepo juu ya meza hiyo... peto alizipiga hatua za harakaharaka kuelekea kwenye meza ile ili aone ni nini kimeandikwa kwenue daftari hilo... alizipiga hatua nisu akimbie... alipofika kwenye meza hiyo""" alikuta kuna mtu anaandika jina lake..

    peto akauliza haya majina ya nini?? mtu yule hakujibu kitu... alipomaliza kuandika jina aliondoka zake kuelekea upande mwingine... peto aliamua kuchukua daftari lile na kuligeuza....alistuka baada ya kuona daftari hilo limeandikwa

    MCHANGO WA RAMBIRAMBI"" alafu jina lake limeandikwa nje ua Daftari hilo... peto alichanganyikiwa... akapaza sauti jamani mimi sijafa nipo hai.. lakini watu hawakumjali.. peto alizidi kuchanganyikiwa... wazo lilimjia aende hospitali kitafita kiwiliwili chake huenda walikipeleka mochwali kwa kudhani kuwa yeye amekufa...



    peto alianza kutimua mbio kuelekea hospital... alifika hospital ya mwananyamala.. akapitiliza moja kwa moja mpaka mochwali... alimuona muhudumu wa kuhifadhi maiti akiuandaa mwili wa mtu aliyekufa ili amuweke kunako jokofu""'peto alimfuata muhudumu yule.. akamuuliza hivi hujaona kiwiliwichangu kimeletwa hapa??? mtu yule hakumjali aliendelea na kazi yake... kisha peto akauliza... mbona unamchoma sindano ya kuhifadhi maiti mtu aliye hai??? muhudumu yule hakujibu kitu.... ghafla ile maiti iliyokuwa ikichomwa sindano ya kuhifadhi maiti...maiti ile ilimwambia peto mtu huyu hakusikii wewe ni mfu... hata mimi hapa ni mfu... na sina uwezo wa kunyanyuka wala kuongea... peto alistahajabu... wewe unasema mfu wakati unaongea!!!!!??? ndio naongea lakini binadamu wa kawaida hawezi kusikia nikisema... pole sana ndugu kwa kilichokukuta... yule muhudumu alimaliza kuichoma sindano maiti ile iliyokuwa ikiongea na peto.. kisha akaingiza maiti ile kunako nani ya jokofu... peto alistahajabu sana...alimkataza yule muhudumi asifanye hivyo.. lakini muhudumu yule hakumjali peto kwani alikuwa hamsikii wala kumuona peto.. kwa sababu peto alikuwa ni nafsi.

    maiti ile ilikuwa ikimuangalia peto kisha ikamwambia wewe ni mfu tu hata usisimbuke....peto aliogopa... yawezeka vipi binadamuhai anawekwa kwenye jokofu la kuhifadhia maiti!!!!! peto alianza kufungua jokofu mojabaada ya jingine kutafuta kiwiliwili chake.. alistahajabu kuona maiti zikiongea nae... alipofungua jokofu la mwisho... maiti ilimwambia mimi nipo hapa siku ya pili vipi unamtafuta nani??? peto alijibu kiwiliwili changu... maiti ile ilisema wewe ni mfu hata usihangaike... kwani hakuna anaekuona wala kukusikia... wewe ni mfu kama mimi.. peto alihisi kuchanganyikiwa.. alitoka mbio kuelekea muhimbili... wakati anatimua mbio alikuwa akikimbia katkati ya rami.. alistahajabu magari hayamgongi... yalipenya katikati yake kama upepo bila kumgusa. inamaana mimi ni mtu wa aina gani.. peto alijaribu kurijusha katika roli moja lililokuwa likienda kwa kasi... peto alistahajabu alipenya katikati ya gari hilo na kutokezea upande wa pili...alitimua mbio mpaka muhimbili.. ile anaingia getini alimuona mwanae chale na watu wengine wakiwa wamebeba jeneza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alitimua mbio kama mwanariadha kuelekea kule alipomuona chales pamoja na watu wengine wamebeba jeneza..alipofika alipaza sauti jamani mimi sijafa nipeni kiwiliwili changu.. lakini chales pamoja na wale watu hawakumjali peto"""" wala hawakuonekana kumsikiliza kabisa.. aisee peto alichanganyikiwa...watu wale walielekea kwenye gari na kuliweka jeneza ndani ya gari... kisha wote wakapanda ndani ya gari hilo.... aisee msinitanie acheni mchezo na kiwiliwili changu.. alisema peto kwa hasira... lakini bado watu wale hawakumjali.. peto aliamua na yeye kupanda ndani ya gari hilo.....alijaribu kufungua jeneza lakini hakuweza kulifungua... peto alianza kulia... hivi nyinyi watu mbona hamna huruma... jamani hata wewe mwanangu wa kumzaa mwenyewe unajifanya husikii kabisa ninacho ongea!!!! nakufukuza nyumbani kwangu....alisema peto huku akilia.. lakini chales hakumjali baba yake.. safari ileendelea na hatimae walifika nyumbani kwa peto.

    peto aliwashangaa wamama lilipokuwa wakilia baada ya maiti yake kuletwa nyumbani.. watu wote walishuka kutoka nadani ya gari na kulibeba jeneza kulipeleka upande wa ndani kunako nyumba.. peto alikuwa sambamba na jeneza lake... hakutaka kuwa mbali kabisa... kichwani mwake alikuwa na mpango mmoja tu... asubiri wakilifungua jeneza aungane na kiwiliwili chake""

    alipotazama upande wa nje kwa kupitia mlango wa sebuleni ulikuwa wazi... alimuona yule mkubwa wa wachawi aliyemkaribisha kwenye chama chake cha wachawi... peto alifuragi sana akapata matumaini...kisha peto akatoka nje huku akizipiga hatua za harakaharaka kuelekea kule alipokuwa ameketi yule mkubwa wa wachawi" peto alipofika alimwambia yule mkubwa wa wachawi...aisee ni bora nimekuona embu fanya mpango nirudi kwenye kiwiliwili changu.... yule mkubwa wa wachawi alikuwa na uwezo wa kumuona peto.....lakini alishindwa kumjibu peto kwa sababu alikuwa kwenye mkusanyiko wa watu.. hivyo wangemshangaa kuona anaongea peke yake...

    aliamua kutoka na kuelekea upande mwingine akajitenga peke yake.... ili peto amfuate ampe maelekezo jinsi ya kurudi kwenye kiwiliwili chake... peto alipo ona yule mkubwa wa wachawi akizipiga hatua kutoka hapo alipokuwa... peto aliamini hata kuwa hata huyo mkubwa wa wachawi hamsikii wala hamuoni.. peto alinyong'onyea.. akazipiga hatua kurudi kule lilipokuwepo jeneza lake... yule mkubwa wa wachawi alikasirika sana kwa kitendo kile cha peto kutomfuata kule alipojitenga.... huyu ni mtu mjinga sana anadharau kumbe... sasa ngoja nimuache wakizike kiwiliwili chake... alijisemea hivyo huyo mkubwa wa wachawi" kisha akazipiga hatua na kuondoka zake hilo eneo la nyumani kwa peto.. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    peto alikuwa akilitazama jeneza lake...huku akisikitika na kuonekana kuwa na wasiwasi mkubwa.. ilipofika majira ya saa saba za mchana jeneza la peto lilitolewa nje kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu... peto alizidi kuchanganyikiwa alipaza sauti.. jama mimi sijafa fungueni jeneza nirudi kwenye kiwiliwili changu... hakuna mtu aliye msikiliza peto wala kumjali.. jeneza lilitolewa nje na kuwekwa juu ya meza tayari kwa kuuaga mwili wa marehem... peto alimfuta mwanae chales na kumwambia ebu fungua jeneza mwanangu... nitakupa kila kitu unachokitaka.... chales hakumjali baba yake alibaki kimya""



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog