Search This Blog

MAITI YANGU - 4

 





    Simulizi : Maiti Yangu

    Sehemu Ya Nne (4)





    mara ghafla magembe alikumbukakuwa kaacha mkia wa ng'ombe ambao huwa anautumia katika mambo yake ya kichawi.... punde alitoweka kichawi bila kumuaga peto... magembe mbona unanikimbia rudi unisaidie nakuomba tafadhali....peto alijaribu kungana na kiwiliwili chake lakini hakufanikiwa...akatimua mbio kuelekea sebuleni... akatazama saa ya ukutani... zilikuwa zimebaki dakika nane.... uuuwi nakufa hivi hivi huku najiona.....yani masaa matatu yamekuwa kama karne alijisemea moyoni"""kisha akatimua mbio kuelekea upande wa nje... alipofika nje alitazamahuku na kule hakumuona magembe.... aliamua kutimua mbio na kurudi chumbani kwake.... kwanini utaki kuungana na nafsi yako eee eti wewe kiwiliwili changu"" tafadha embu sema na mimi!!!!! peto alisema maneno hayo akikiambia kiwiliwili chake.... dah!! mpaka umrbadilika rangi... mimi sio mweusi kiasi hicho... embu punguzaasihala unanichosha tazama siku ya tatu leo sijaoga wala sijala... peto alizidi kuongea akikiambia kiwiliwili chake.... aliona magembe anacbelewa..... peto. akatimua mbio kuelekea sebuleni... alipotazama saa ya ukutani zilikuwa zimebaki dakika tano(5) peto alizidi kuchanganyikiwa... macho yalimtoka akatimua mbio kurudi chumbani kwake.... ile anafika na magembe akatokea..... CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    magembe aligusa kiwiliwili cha peto kwa kutumia ule mkia wa ng'ombe... hivi magembe mbona unanichelewesha kuungana na kiwiliwili changu....maana yake sikuelewi kabisa!!!! alisema peto huku macho yake yakimtazama magembe kwa msisitizo..... magembe alisema haya panda juu yakiwiliwili chako... kabla magembe hajamaliza kuongea peto alikuwa kaisha panda....



    *******************



    magembe alistahajabu muona bado peto hawezi kuungana na kiwiliwili chake.... macho yaljmtoka magembe huku jasho likimtiririka.... mmmh!!! haiwezekani... magembe alijisemea moyoni" kisha anza kukizunguka kitanda cha peto.... wakati huo peto alikuwa akimtaza magembe...peto aliona kama muda unakwisha alinyanyuka na kutimua mbio kuelekea sevuleni akaitazama saa ya ukutani zilikuwa zimebaki dakika mbili... peto alizidi kuchanganyikiwa akatimua mbio kurudi chumbani....akapanda juu ya kiwiliwili chake... magembe alitoa kachupa kadogo akafungua na kumwa unga mweupe kwenye kiwiliwili cha peto....mara ghafla peto aliungana na kiwiliwi chake.... aisee peto alifurahi sana alinyanyuka kitandani kisha akaanza kucheza staili aina ya KIDUKU.....alimkumbatia magembe kwa kumsaidia.... aised wewe kiboko kweli wewe ni mkuu wa wachawi... alisema peto.... magembe alikuwa akimtazama peto wakati akiongea maneno hayo....... kisha magembe alikohoa kidogo..... akabaki kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamwambia peto.... kwa kuwa umeweza kuungana na kiwiliwili chako... itabidi utimize ahadi ya kumtoa kafara mtoto wako chales....peto alichanganyikiwa kisha akamwambia magembenakusihi tafadhali msimchukue mwangu chales sina mtoto mwingine zaidi yake..... magembe akasema haiwezekani ni lazima utoe kafara uzawa wa chimbuko la damu yako...kisha magembe akatoweka kichawi..... peto aliamua kutoka nje ili ahakikishe kama kweli ni yeye.... ile anatoka nje mara ghafla



    alihisi kama miguu yake haikanyagi chini.... aliogopa sana.... akasita kutoka nje akarudi ndani...

    mmmh!! jamani eee mbona kama bimemuona peto.. katokeza mlangoni kisha akarudi ndani.... alisema mtu mmoja kati ya watu waliobaki kwenye matanga....

    peto alichukua ndoo na kuchota maji kutoka kwenye diaba akayamimina kwenye ndoo.kisha akazipiga hatua kutoka nje.... watu walipomuona peto waliogopa sana.... ilikuwa kama sinema.... au mlipuko wa mabomu mbagala yani watu walitimua mbio kila mtu alipita njia yake na kutokomea kusikojulikana..... ndani ya dakika moja hapakuwepo mtu hata mmoja aliyebaki hapo.... peto alistahajabu kisha akajisemea moyoni kwenda zenu huko... kwanza mlitaka kunizika mzimamzima.... kisha akaendelea kuzipiga hatua kuelekea bafuni...

    baada ya kumaliza kuoga peto alirudi chumbani kwake...... akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi... ghafla wazo lilimjia... huenda akilala anaweza akapitiliza moja kwa moja aisiamke tena..alinyanyuka haraka kitandani...kisha akazipiga hatua kutoka nje ya nyumba.. na kuzipiga hatua kuelekea mjini.... kila alipokuwa akipita watu walitimua mbio......



    ***************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilipofika majira ya usiku......magembe alijiandaa mwenda kwenye shughuli zake za kichawi.......na ilipofika mida ya saa sita za usiku magembe alitoweka kichawi...alikwenda kwenye mti mkubwa wa m-buyu mti huo huwa anautumia na washirika wake kwenye vikao vyao vya kichawi.....alipofika alikuta tayari wale wachawi wengine wameshafika... kisha akasema leo ni siku maalumu ya kutimiza ahadi ya mwenzetu peto... hivyo inatakiwa chales aletwe usiku huu kwa ajili ya kafara.



    *****************



    ule upande mwingine alionekana peto akiwa nyumbani kwake.... alikuwa na wasiwasi kuhusu mwanae chales peto aliamua kuelekea mpaka kule kwenye mbuyu... alipofika alijipaka mafita ya binadamu... mafuta hayo ni ya kutoka kwenye mwili wa mtoto mchanga... upande wa katikati ya moyo..... baada ya peto kujipaka mafuta hayo punde alianza kuwaona wenzake alizipiga hatua mpaka pale walipokuwa.....alitoa salamu kwa ishara kisha akajumuika na wachawi wenzake..

    punde magembe sliamuru chales aletwe... peto alichanganyikiwa alianza kulia huku akimsihi magembe asimdhuru....hakuna namna hili ni agano la mungu wetu wa kuzimu""magembe alijibu""

    punde chales aliletwa...... chales alistahajabu kumkuta baba yake pale..... kisha magembe alimgusa kichani chales akawa hawezi kusema wala hakuweza kuona tena yale yanayoendelea...kisha magembe aliamuru chales alazwe juu ya gogo lililokuwa chini...... kisha peto apewe kisu amchinje mwanae ili kafara lifanyike.

    peto aliamua kutimua mbio akatokomea kusikojulikana.....



    peto alionekana akielekea kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KANGALA.....akaomba msaada... kangala amsaidie kumuokoa mwanae... kangala alikuwa ni moto wa kuotea mbali alikuwa ni mchawi kutoka SUMBAWANGA.....alikubali kumsaidia peto... kisha akampa kipande cha mkia wa FISI iwe kinga kwa peto..



    *****************



    ule upande mwingine kule alipokuwepo magembe na wachawi wenzake.. ilibidi wasitishe zoezi la kufanya kafara kwa sababu anayetakiwa afanye kafara hayupo hivyo haitowezekana mpaka peto awepo.. ili amchinje mwanae kwa mkono wake mwenyewe......

    taarifa hizo za peto kukimbilia kwa mchawi kangala. magembe alizipata... hivyo vita ikahamia kwa kangala..... magembe alijipanga kwenda kumkabili kangala.... kisha akatoweka kichawi..



    peto alionekana akitimua mbio kurudi nyumbani kwake...alipofika alichukua vitu vyake vyote alivyopewa na magembe ili kuvitumia katika shughuri zake za kichawi.....kisha akachukuwa kiberiti na kutoka nje akavichoma moto na kubakiza kile kipande cha mkia wa fisi alichopewa na Kangala mchawi kutoka sumbawanga.....CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    magembe alijitokeza kichawi nyumbani kwa peto.....alipofika alistahajabu kumuona peto akiwa tofauti na jinsi alivyomzoea....peto alionekana ananguvu za uchawi ambao magembe hakuwahi kuuwona....magembe alianza kuingiwa na wasiwasi.....wakati huo peto naye aliogopa baada ya kumuona magembe kaja nyumbani kwake...alijua kuwa huenda magembe kaja kumdhuru.....peto aliingiwa na wasiwasi mkubwa...kumbe kile kipande cha mkia wa fisi kilimfanya magembe amuogope peto...

    peto hakulijua hilo....aliona magembe akizipiga hatua kurudi nyuma na kutimua mbio kisha akapotea kichawi...pia peto alitimua mbio na kutokomea kusikojulikana..........



    ***************

    .ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog