Search This Blog

MAITI YANGU - 5

 





    Simulizi : Maiti Yangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    magembe alirudi kule kwa wachawi wenzake....alipofika alionekana kuwa na uwoga mkubwa"" wale wachawi wenzake walishangazwa na kitendo hicho.....kisha magembe akasema itabidi wafanye haraka iwezekanavyo ili kumbadilisha chales kutoka katika hali ya kibinadamu apelekwe katika gereza la kichawi lililokuwa GAMBUSHI..........kisha akaamuru chales avuliwe nguo zake zote ili achajwe na kupakwa dawa maalumu ili asionekane na kwenyeacho ya binadamu wa kawaida.....wale wachawi wengine walianza kumvua nguo chales.....na baada ya kumaliza.....magembe alizipiga hatua tatu na kuchukua unga mweusi kama mkaa...kisha akamlisha chales.......unga ule analishwa ili asiweze kuongea kitu chchote.....kisha chales akakalishwa chini.....kishamagembe akachukua kiwembe na kuanza kumchanja mwilini.....kisha akaamuru chales ageuzwe na kuangalia mashariki....punde chales aligeuzwa na mmoja kati ya wale wachawi....kisha magembe akachukuwa dawa ili ampake chales.....kabla ajaanza kumpaka dawa ile...punde alitokea Kangala na peto........mgembe akaacha kumpaka chales dawa ile....akajipanga kupambana na kangala.....

    peto alikaa pembeni...akisubiria kuona vita ya wachawi....kangala alizipiga hatua kumfuata magembe.....wale wachawi wengine walitimua mbio kwa sababu kangala alionekana kutisha hakuwa mtu wa kawaida........



    ******************



    Magembe alianza kuogopa...kisha akajaribu kurusha nguvu za kichawi..pale alipokuwa kasimama...nguvu zile zilidunda

    magembe alipo ona mambo yamekuwa magumu magembe alimgusa chales kichwani kisha akatoweka nae kichawi....kabla hajafika mbali kangala alimnasa magembe kichawi...akaanguka chini......kisha akaanza kuzipiga hatua kumfuatamagembe.....peto macho yalimtoka baada ya kuona magembe kadondoka lakini chales hakuonekana.......peto alimuona kangala akigusa mti uliokuwa pembeni kidogo...punde chales alionekana baada ya kangala kugusa mti huo......magembe aliingiwa na uwoga wa hali ya juu...

    kangala aligeuza shingo yake na kumtazama peto.......punde magembe alitoweka kichawi na kutokomea.......peto aliangua kicheko na kujisemea moyoni......kumbe kila mjanja ana

    mjanja wake!!!!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kangala alimsogelea chales na kumnyanyu bila kumgusa kisha akamtazama kwa umakini kangala aligundua kuwa chales alikuwa ameanza kubadilika kutoka katika hali ya kibinadamu....kumbe angepakwa dawa ile baada zile sehemu alizochanjwa basi asingeweza kuonekana tena......

    kangala alimwambia peto kuwa ili kumrudisha chales katika hali yake ni kazi kubwa......itabidi nimpeleke chales SUMBAWANGA nilipotoka.....hivyo itabidi twende usiku huu huu.



    macho yalimtoka peto kisha akahisemea moyoni. ""jamani mimi nimeacha uchawi sasa na huyu kangala anataka kunirudisha kwenye uchawi....peto aliogopa sana...ghafla kangala alimshika mkono chales kisha aka mfuata peto amshike ili waondoke kichawi kuelekea SUMBAWANGA..peto alijiandaa kutimua mbio...mara ghafla kangala akamuwahi peto kabla hajakimbia alipomgusa upande wa begani ghafla walitoweka kichawi " ni kitendo cha sekunde walitoka dar na kufika SUMBAWANGA"walitokezea njia panda kisha wakaanza kuzipiga hatua, wakati huo peto uwoga ulikua umemjaa alitembea huku akimwangalia kangala usoni kisha akamwangalia charles usoni.............. peto alimwonea huruma nwanae kisha akajisemea moyoni jaman mwanangu nakuonea huruma sana sijuiutapona: kangala aliweza kugundua kile alichokua akiwaza peto kwenye akili yake, kitendo hicho kilimchukiza sana kangala aligeuka na kumwangalia peto kwa macho ya mkazo, peto aliogopa akataka kutimua mbio kangala alisimaa!!! kisha akasema yakupasa uwe jasiri Kwa yale utakayoyaona: peto aliogopa sana, punde kangala alinyanyua mkono wake na kupeleka usoni kwa peto ghafla peto alianza kuona watu wengi alisitaajabu sana, kumbe walikua gambush; (kijiji cha wachawi) Aliona manesi na madaktali wakiwatibu watu, ,,watu hao waliokuwa wakutibiwa walionekana kuwa na nyuso za kutisha, nywelezao zilikua ni ndefu sana zilionekana kuchakaa, kucha za mikononi na miguuni zilikua ndefu pia. peto alimuuliza kangala hapa ni wapi??? kangala alijibu hapa ni kijijini kwetu na baba yangu ndiye mtemi wa kijiji hiki,,, peto alifurahi sana baada ya kusikia hivyo; kwa mbali peto aliona mtu kakaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mifupa ya binadamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****************



    ule upande mwingine alionekana magembe akijipanga upya alikwenda katikati ya shamba lake akaanza kuchumba....alichimba kisha akatoa irizi kumi zilizofungwa kwenye vipande vya kaniki nyekundu....kisha akazivaa shingoni mwake....akaanza kuzipiga hatua kurudi ndani....akafunua chini ya godoro na kutoa ngozi ya binadamu iliyokaushwa...ngozi hiyo ilionekana kama mkanda wa suruali...kisha akajifunga kiunoni......kisha akachukua jino moja la mamba aliyekufa miaka 50 iliyopita...akachukua kisu na kujikata kwenye paja kisha akaweka jino hilo ndani ya jeraha hilo na kujifunga kwa kipande cha kaniki nyeusi...... kisha akajikata kwa kutumia ksu kwenye sehemu ya kiganja chake.....na kuzipiga hatua kama mbili hivi....akanyunyiza damu ile kunako mdomo wa fuvu la binadamu lililokuwa juu ya mlango wake wa chumbani.....



    *****************



    kule SUMBAWANGA kangala alimuongoza peto pamoja na chales mpaka kwa MTEMI wa kijiji hicho aliyekuwa kaketi juu ya kiti kilichotengenezwa kwa mifupa ya binadamu...wwalipofika,,, kangala aliwatambulisha kwa MTEMI wa kijiji ambaye ni baba yake mzazi...

    walipokelewa vyema...kisha kangala akaeleza shida iliyomrudisha SUMBAWANGA...punde MTEMI aliamuru chales atibiwe ili arudi katika hali yake ya kawaida """kwa sababu alipolishwa yale madawa ya magembe....yalimfanya chales aanze kuwa ZEZETA....

    chales alianza kutibiwa haraka.......MTEMI aliamuru mbuzi aletwe....punde mbuzi aliletwa na kuchinjwa....wakati mbuzi anachinjwa damu zilipokuwa zinatoka...chales alianza kutapika vitu vyenye rangi nyeusi......mbuzi alipokata roho chales alirudi katika hali yake na kujitamvua.....peto alifurahi sana alimshukuru kangala pamoja na MTEMI kwa kuokoa maisha ya mwanae......kisha MTEMI alimuamuru kangala amrudishe peto na chales dar es salaam....kangala alitii amri ya baba yake...kisha akamshika mkono chales na peto wakatoweka kimiujiza.....ni kitendo cha sekunde walifika dar....



    ****************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande mwingine magembe alionekana akiatazama kwenye maji yaliyokuwa ndani ya chungu....aliweza kudundua peto na kangala ni wapi walipo.....alichukua kopo na kulifungua...alijipaka mafuta ya binadamu kisha akatoweka kichawi......



    wakati kangala na peto pamoja na chales wakiwa njiani wakizipiga hatua....ghafla magembe alijitikeza........peto alimshika mkono chales wakatimua mbio wakamuachia ugomvi kangala apambane na magembe""""

    kangala alipomtazama magembe aligundua kuwa kajipanga kikamilifu""" hivyo kangala alikuwa makini sana.....punde magembe alirusha nguvu za kichawi....lakini zilidunda kwa kangala pia kangala alirusha nguvu za kichawi zikadunda kwa magembe......kila mmoja alionesha kuwa yeye ni zaidi ya mwenzake...walipigana masaa saba mfululizo...magembe alianza kuzidiwa nguvu.....akataka kukimbia....kangala alimnasa magembe kisha akamgeuza magembe akawa kiatu...kisha kangala alikigusa kiatu kile kikajigawa vikawa viatu viwili.....akavivaa....

    palipokucha magembe alikutwa kaiaga dunia akiwa chumbani kwake...

    na wale wachawi wengine nguvu za kichawi ziliyayuka mwilini mwao.......na kuwa raia wema kama watu wengine.



    **********



    kule nyumbani kwa peto....alionekana akimsihi mwanae aisije akajaribu kujihusisha na mambo ya kichawi...mara ghafla...mlango uligongwa.. peto alistuka alijua magembe amekuja...peto alibaki kimya kisha akaanza kunyata yeye na chales ili wapitie mlango wa nyuma wakimbie....ghafla ikasikika sauti ikisema """"ni mimi KANGALA peto alifungua mlango haraka kisha kangala akasema magembe nimemuuwa usiku wa jana...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    peto alifurahi sana...alimshukuru sana kangala..



    maisha yaliendelea peto alirudi kazini kwake na kuendelea na shughuri zake za kubeba mizigo...

    aliamua kumrudia MUNGU.alikwenda kutubu zambi zake akatoa ushuhuda wa yale yote yaliyomtokea.....peto akaanza kuudhulia ibaada kila siku ya sabato.....watu walimpenda peto...na amani ikaongezeka ndani ya nyumba yake...aliishi maisha ya furaha na mwanae chales.



    ***********MWISHO WA SIMULIZI HII****

0 comments:

Post a Comment

Blog