Search This Blog

KITABU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kitabu

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walionekana wanafunzi wa wakitoka chuo na kuelekea HOSTEL....walijitenga kwa makundi makundi...wengine wakiwa mbele waengine wakiwa nyuma ya wanafinzi wenzao...kwa mbali alionekana Mwanafunzi mmoja wa kike aitwae CHERY akiwa na marafiki zake watatu wakizipiga hatua huku wakipiga story na kucheka.chery alisema""napenda sana siku moja niwe mtu maarufu duniani na ipo siku ndoto yangu itakuwa kweli....marafiki zake hoa wawili walimcheka na kimwamvia aache kuota ndoto za mchana mchana.....waliendelea kuzipiga hatua baada ya dakika kadhaa walifika hostel...chery alipoingia katika chumba alichokuwa akilala alifungua kabati na kutoa daftari kubwa alilolitumia kuandika kitabu alichokuwa anakitinga kila alipokuwa akilata muda....siku ya leo chery alikuwa kadhamilia kuandika muendelezo wa hadithi ya kitabu alichokuwa akikitunga....alichukua karamu akavuta kiti pamoja na meza kisha akaanza kuandika kitabu hicho.....wale wenzake watatu walikwenda kuoga na kumuacha chery akiandika kitabu....leo chery aliandika tukio lililosimulia mauwaji ya kikatili yaliyofanywa na binti mwenye roho ya kikatili......marafiki zake na watu wengi walipenda kusoma kitabu hicho alichokuwa akitunga na kukiandika katika daftari hilo kubwa....watu wengi walimfuata chery kwenye chimba anacholala ili kusoma muendelezo wa hadithi hiyo aliyokuwa akiitunga...chery hakuwanyima aliwapa kitabu hicho wasome kila alipokuwa akimaliza kutunga muendelezo mmoja.....



    siku zilisonga hatimaemiaka miwili ikapita... siku ya leo chery anauanza mwaka wa mwisho chuoni hapo ili amalize deplomar ya Utangazaji...chery aliendelea kuandika muendelezo wa kitabu chake hatimae hadithi aliyokuwa akiitunga ilifika mwisho....ilipofika mwezi wa kumi mwaka 2005 chery alifanya mtihani wa kuhitimu deplomar...

    wiki hiyohiyo chery alichukua kila kilichomuhusu kisha akaandaa safari yakurudi nyumbani kwao...

    kabla hajaondoka aliamua kumkabidhi rafiki yake kipenzi aitwae Lattifa kile kitabu alichokitunga ndani ya miaka mitatu....kisha akasema """sidhani kama tutaonana tena...kwaheri ya kuonana rafiki yangu kipenzi tunza kitabu hiki ishara ya kunikumbuka popote uendapo......lattifa alikipokea kitabu kile kisha akamkumbatia cherry huku machozi yakimtoka kwa sababu walizoeana walisaidiana waliishi kama ndugu wa damu humo HOSTEL kisha chery akachukua begi lake na kuondoka..........haikujulikana ni wapi chery alipoelekea hata wazazi wake hawakuwahi kumuona tena chery.......tangu alipohitimu chuo.



    ****BAADA YA MIAKA KUMI NAMBILI KUPITA***



    sasa yapata miaka kumi na mbili tangu 2005-2017.....bado hajajulikana ni wapi chery alipo..wazazi wake walisikitika sanampaka walikata tamaa ya kumuona tena mtoto wao chery....Matukio na michoro iliyoitungwa katika hadithi ya kitabu cha chery yalianza kutokea tena yanafanana na michoro na kile alichokiandika chery...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    lattifa alimtafuta sana chery kwa anuani lakini kila alipopiga simu ya nyumbani kwa kina cherybado aliambiwa kuwa chery bado hajaonekana.....

    latiffa alikisoma kitabu kile alichokitunga chery kwa sababu kilikuwa na kurasa nyingi sana lattifa aliamua kuwa anakisoma pale anapopata muda wa kupumzika......tena nyakati za mchana kwa sababu hadithi hiyo ilikuwa inatisha ilieleza matukio ya mauwaji ya kutisha kwa maandishi na michoro..

    latifa alipata kazi miaka mitatu iliyopita aliajiliwa katika kituo cha habari kiitwacho TBC FM sikumoja ililetwa habari na muandishi wa kituo hicho kuwa kuna mtu kakutwa kauwawa na kukatwa nyeti zake pamoja na mikono na miguu na itumbo ulikuwa umetolewa....kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na vyombo vya dola inasemekana muuwaji baada ya kufanya tukio hilo la mauwaji alikata nyeti za mwanaume huyo pamoja na miguu na mikono na utumbo kisha akaondokanavyo.....lakini haikufahamika ni nani aliyefanya mauwaji hayo....

    latifa alistahajabu sana baada ya kuona tukio hilo linafanana kabisa na tukio la sehemu ya kwanza ya hadithi ya kitabu cha chery



    Lattifa alishtuka sana akaipokea habari ile na kuitangaza kwenye radio.....

    baada ya sikumbili kupita lilitokea tukio jingine la kikatili kutisha....ilikuwa hivi mwanamke mmoja alitoka kazini majira ya saa moja za usiku akiwa njiani alitokewa na mtu wa kutisha aliyekuwa na umbile la mmbwa lakini mwili wa binadamu...kiumbe huyo alimvamia na kumuuwa mwanamke huyo kisha akapeleka katika mlango wa nyumbani kwake akalazwa upande wa nje.....

    maiti hiyo ilionekana kuraruliwa vibaya....ilikutwa haina macho utumbo pamoja na miguu na mikono........taarifa zile alizipata latifa kupitia mitandao ya kijamii Facebook....latifa alistuka sana tukio hilo lilifanana kabisa na sehemu ya pili ya hadithi ya kitabu cha chery....latifa akaanza kukgopa"""akahisemea moyoni """mbona hadithi aliyoitunga chery inafanana na michoro na matukio yanayojitikeza kwa sasa....je ni nani anayefanya mauwaji haya!!!?? latiffa aliendelea kukisoma kitabu hicho...alipoianza sehemu ya tatu ilikuwa inasimulia matukio matano ya mauwaji ya kikatili tukio la kwanza lilionesha mauwaji ya kutisha ya askari mpelelezi aliyepewa kazi ya kumtafuta muuwaji...

    latifa alijiuliza lakini hakupata jibu...vyombo vya dola viliendelea kufanya uchunguzi ili kubaini muuwaji ni nani....

    baada ya wiki moja kupita mkuu wa upelelezi aliamuru aitwe mpelelezi professional kutoka Amerca aje nchini Tanzania kufanya uchunguzi na amnase muuwaji...

    mpelelezi huyo alipofika alipewa nyumba na gari la kutembelea ili limsaidie katika shughuli za upelelezi......baada ya wiki mbili kupita mpelelezi huyo alikutwa kauwawa ndani ya nyumba aliyopewa.....maiti yake ilikutwa imekatwa katwa vipande vingi...bila kufahamika nani kafanya mauwaji hayo.

    tukio hilo lilikuwa la aina yake....lilistua Taifa zima...latifa aliogopa sana baada ya kupata taarifa hizo....ni moja ya tukio alilolisoma wiki iliyoisha kwenye sehemu ya tatu ya kitabu cha Chery....tukio hilo lilikuwa hivyohivyo katika mchoro wa kwenye kitabu.....latiffa alizidi kuchanganyikiwa alijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu.....akatoka kazini haraka akarudi nyumbani kwake...alipofija alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani...akafungua kabati na kutoa kile kitabu cha chery.....akafunua ukurasa mpaka akaipata sehemu ya tatu...akaangalia tukio linalofuata kati ya yale matukio matano ya sehemu ya tatu... akaanza kusoma alistuka akaogopa sana...hadithi ilisimulia""familia moja iliyokuwa inaishi mikocheni siku hiyo waliamua kwenda kutembea katika hifadhi ya vitu na mambo ya kale huko BAGAMOYO..........alikumbuka kuwa kuna baba yake mdogo anaishi mikocheni...huwa anapenda kuipeleka familia yake mara kwa mara kutembelea mbuga za wanyama na na hifadhi ya makumbusho ya kale.. latiffa alichukuwa simu yake na kumpigia baba yake mdogo...... alipoipokea simu latifa aliuliza ""ukowapi?????

    baba yake mdogo alijibu"""sasa hivi tumeingia Bagamoyo nimewaleta ndugu zako waje kutembea...ghafla simu ya baba yake mdogo ilizimika chaji....kabla latiffa hajaingea neno lingine..



    walipofika waliingia kutalii katika katika makaburi ya watu viongozi wa kale(wakoroni) walipoingia wakaanza kupouwawa mmoja moja kwa kukatwa shingo na kutolewa utumbo wakakatwa mikono na miguu kisha maiti zao zikatelekezwa hapohapo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************



    latiffa alijaribu kupiga simu ya baba yake mdogo siku nzima lakinj haikupatikana hewani...ilipofika majira ya saambili za usiku latiffa akiwa nyumbani kwake akiangalia taarifa ya habari...alistuka kusikia taarifa kuwa kuna familia moja wamekutwa wameuwawa katika hifadhi ya mambo ya kale(makumbusho) huko Bagamoyo.

    latiffa alihisi kuchanganyikiwa.....

    akatoka nyumbani kwake na kuelekea Mikocheni kwa baba yake mdogo...alipofika alistuka kukuta watu wamekusanyika kwa ajili ya msiba...latifa aliangua kilio huku akise Chery umeuwa ndugu zangu.....



    *************



    baada ya wiki moja kupita latiffa aliendelea na kazi yake ya utangazaji....siku hiyo alitoka kazini na kurudi moja kwa moja mpaka nyumbani kwake...alipoingia chumbani aliwasha simu yake....kuna ujumbe mfupi wa maneno(SMS) ukaingia.....latiffa alistuka sana baada ya kusoma SMS hiyo kisha akakurupuka haraka kutoka pale alipokuwa ameketi akafungua mlango wa kabati na kukitoa kitabu cha chery akafunua mpaka sehemu ya tatu akaanza kusoma tukio la tatu kati ya yale matukio matano yaliyopo sehemu ya tatu

    marra ghafla alistuka kuona tukio lililotisha ambalo limetokea muda si mrefu......





    akaendelea kusoma kitabu cha chery alipofika kwenye tukio la nne hadithi ilisimulia....kuna mtu mmoj alikuwa akiendesha gari...mtu huyo ni dereva wa gari la kusafirisha mizigo...siku hiyo majira ya alfajiri aliianza safari akitokea Mwanza kuelekea Dar es salaam...ilipofika majira ya saa nne za usiku alikuwa amekaribia kuingia Mji wa Morogoro....akiwa njiani aliona kiumbe wa kutisha akiwa anakimbia nyuma ya gari...mara ya kwanza alihisi huenda ni msongo wa mawazo aliyokuwanayo....aalipoendelea kukitazama kioo kilichoonyesha pembeni na nyuma ya gari....aliona kiumbe kile kinazidi kusogea kisha kikatoweka..aliogopa sana akaongeza kasi ya mwendo wa gari.....alipotazama upande wa mbele alistahajabu kukiona kiumbe kile mbele yake kimesimama katikati ya barabara alkawasha taa za gari mwanga mwingi zaidi(full light) ghafla akamparamia kiumbe ye na kumgonga...ikatokea ajali kubwa utadhani magari mawili yamegongana uso kwa uso... roli lile liliharibika vibaya sana upande wa mbele....dereva alikuwa kaumia kupita kiasi..damu nyingi zilimtoka....kisha kiumbe yule akamfuata dereva akamtoa ndani ya gari akamtupa upande wa nje....dereva alikuwa hoi..hakuweza hata kunyanyua mkono...alibaki akimtazama kiumbe yule...

    baada ya sekunde kadhaa kiumbe yule alivuta kichwa cha dereva na kukitenganisha na shingo kisha akanyofoa miguu na mikono akatoweka navyo.......



    latifa aliogopa sana akakifunika kitabu haraka...huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu...aliona ndani hapakaliki akaamua kutoka upande wa nje....



    ****************



    kesho yake alidamka na kujiandaa aende kazini alipomaliza alifunga mlango wa chumbani kwake na kuondoka kuelekea kazini....alipofika aliletewa habari aitangaze kwenye radio...alipoisoma habari ile ilikuwa ni taarifa ya ajali ya roli lililopinduka huko morogoro alafu dereva amekutwa amelala upande wa nje huku maiti yake ikiwa haina kichwa miguu pamoja na mikono.....latifa alistuka akaogopa sana.....akaamua kuwaambia watangazaji wenzake kuhusu kitabu alichotunga chery....miaka kumi na mbili iliyopita(12) kwa sasa matukio na michoro iliyochorwa kwenye kitabu ndio haya yanayojitokeza kwa sasa!!!

    watu waliokuwemo kwenye kipindi walistahajabu sana wakawa na shauku ya kutaka kikiona na kukisoma kitabu hicho.....CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilipofika saa kumi za jioni..latiffa alitoka kazini na kurudi nyumbani......akiwa njiani simu yake iliita...alipoitazama aliona mfanyakazi mwenzake aitwae BENJAMINI anampigia...alipoipokea simu hiyo.....benjamini aliomba watoke pamoja kwa ajili ya chakula cha usiku...latifa alikubali akasema"sawa ngoja nifike nyumbani nikabadilishe nguo... nitakujulisha nikiwa tayari....kisha akakata simu....latifa alipofika nyumbani kwake aliingia bafuni kuoga kisha akarudi chumbani kwake....akavaa nguo nyingine tofauti na alizokuwa amevaa kazini...kisha akatoka na kuzipiga hatua za taratibu huku akichezea simu yake.....alipofika barabara kuu..aliamua kumpigia Benjamini amfuate.....kisha akajisogeza kwenye mgahawa uliokuwa pembeni ya barabara akaketi na kuagiza soda....akaanza kunywa huku akimsubiri Benjamini..



    **********



    baada ya dakika kumi kupita.Benjamini alifika, Latiffa aliweza kumuona Benjamini kwa urahisi kwa sababu alikuwa ameketi jirani kabisa na barabara kuu...akanyanyuka na kulifuata gari la benjamini akafungua mlango na kuingia upande wa ndani...benjamini aliliwasha gari na kuliendesha mpaka SIX PARK HOTEL. walipofika waliagiza chakula na baada ya muda chakula kililetwa wakaanza kula.....benjamini akasema "kunajambo nataka nikwambie lakini naomba ulipokee kwa moyo mkunjufu...kwa sababu ni muda mrefu nimekaa nalo moyoni..lakini leo nimeamua nikwambie..benjamini aliyasema maneno hayo huku akitafuna nyama ya kuku...

    kabla hajamaliza kuongea simu yake iliita""sory naomba niongee na simu mara moja...kisha akanyanyuka na kusogea kando kidogo....akaipokea simu ile.....alistuka baada ya kupata taarifa ya msiba wa baba yake pamoja na mama yake wamekutwa wameuwawa kikatiri ndani ya nyumba yao na kukatwa katwa vipande vingi....benjamini alichanganyikiwa akakata simu akarudi haraka mpaka pale mezani alipokuwa amekati akamshika mkono latiffa na kuondokanae...latiffa alishangaa akauliza"" kwani vipi!!!!!kuna tatizo gani sikuelewi""""

    benjaminj alibaki kimya hakujibu kitu...ghfla muhudumu aliwafata mpaka kwenye gari akasema"" mbona mnaondoka bila kulipa pesa ya chakula mlichoagiza?????

    latiffa akadakia akauliza shilingi ngapi??

    yule muhudumu akajibu elfu arobaini..benjamini alitoa pesa kwenye mfuko wa suruali akamlipa yule muhudumu kisha akaliwasha gari na kuliondo kwa kasi...wakati huo latifa alikuwa anamshangaa benjamini...aliliendesha gari mpaka pale alipo mkuta latiffa kisha akamwambia ninamsiba wazazi wangu wameuwawa na mtu asiyejulikana muda mchache uliopita...kisha benjamini akaliendesha gari kwa kasi ya ajabu...macho yalimtoka lattifa...akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea nyumbani kwake..alipofika alipitiliza mpaka chimbani..akafungua kabati na kukitoa kitabu cha chery...akafunua kurasa mpaka sehemu ya tatu akasoma ili aone tukio lililotokea je linafanana tukio la kwenye kitabu!!

    aliposoma alistuka kusona mchoro wa mauwaji ya kikatili aliposoma ilikuwa hivi"watu wawili mke na mume walivamiwa na kiumbe wa ajabu na kuwauwa kikatiri kisha kiumbe huyi alikatakata vipande vingi maiti hizo na kutokomea kusikojulikana...

    latifa alipoendelea kusoma hadithi ilieleza kuwa kijana mkubwa wa wazazi hao waliouwawa alikwenda nyumbani haraka baada ya kupata taarifa hizo..alipofika aliogopa sana kukuta wazaziwake wameuwawa kikatiri....akiwa anatahamaki mara ghafla kiumbe yule alijitokeza na kumuuwa kijana huyo....latifa alistuka akaogopa sana alihisi kuchanganyikiwa alijua wazi kuwa anayefuata kuuwawa ni Benjamini...

    akachukua simu na kumpigia benjamini ili asiende nyumbani kwao....simu ya benjamini iliita lakini haikupokelewa.....



    *************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    upande mwingine alionekana benjamini akiitazama simu yake ikiita lakini alishindwa kuipokea kwa sababu alikuwa amechanganyikiwa na taarifa ya vifo vy wazazi wake..

    baada ya muda kidogo alifika akiingia nyumbani kwao akalipaki gari akashuka haraka na kutimua mbio kuingia upande wa ndani.....alipoingia mara ghafla.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog