Search This Blog

DAMU YA BABA - 4

 







    Simulizi : Damu Ya Baba

    Sehemu Ya Nne (4)



    Mdogo wangu akamwambia “kaka nisamee sina pesa ya nauli” konda akasema “kwanini ukusema mapema, hivi ujui na mimi nimeajiliwa naulizwa na bosi, ebu naomba ushuke dada”



    Dereva alisimamisha basi mdogo wangu akashushwa na kutelekezwa palepale kijijini kama mwizi jamani, watu walishangaa sana wakasema mbona huyu dada ameungua sura hivi labda alikuwa mwizi jamani, binti anatabia ya wizi ndiyo maana anapanda basi bila ata kusema kama hana nauli.Mimi nilimtafuta kila kona mdogo wangu sikumpata kabisa.Wakati mdogo wangu ametelekezwa mwenyewe na hajui atakula nini, hana ndugu yoyote pale alilala chini pembeni ya barabara akaanza kulia masikini!.



    Mdogo wangu alikata tamaa ya maisha kabisa, akatamani kufa maana alipatwa na njaa kali sana, sababu tangu atoke nyumbani alikuwa ajaweka chochote tumboni mwake.Aliamua kuamka na kuangalia kama anaweza kumuona mtu maeneo yale ili amsaidie ata maji ya kunywa tu.Kipindi anatembea kule kijijini akakutana na shamba lenye miti ya maembe na kulikuwa na mahindi pia mule shambani.



    Mdogo wangu hakutaka kujua kama ni shamba la mtu alienda moja kwa moja mpaka shambani kisha akapanda juu ya muembe, akaka vizuri ili aweze kuchuma maembe kupunguza njaa yake mdogo wangu kipindi anataka kuchuma embe kumbe kulikuwa na nyoka mwembamba wa kijani pembeni,Mdogo wangu alikuwa muoga sana alipo muona yule nyoka alidondoka chini mpaka paja lake likachomwa na miba akapiga kelele maana alidindoka mzima mzima, kale kanyoka pia kakakimbia na kuamia mti mwingine.



    Sasa kipindi anadondoka chini mwenye shamba alikuwa katikati ya shamba anakagua, Alivyo sikia mtu kaanguka kwa kishindo huku akipiga kelele shambani mwake, akajiuliza “huyo ni nani ngoja nimfate”



    Alipo fika akamuuliza wewe ni nani, mdogo wangu akasema “nilikuja kula maembe kumbe kwenye muembe kuna nyoka hivyo kidogo anin’gate ndipo nikadondoka chini”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Yule baba akasema “kwanini unaniibia maembe yangu”



    Mdogo wangu akasema mimi sikujua kama siruhusiwi kula maana nina njaa sana baba yangu”



    Yule baba akasema “nyie watoto mnaniibia sana matunda shambani mwangu sasa leo nimekupata wewe, na ndiyo utakuwa fundisho kwa wenzako”



    Mdogo wangu alikamatwa mikono na yule baba kisha akampeleka nyumbani kwake ili ampe adhabu.



    Kipindi mdogo wangu amefungwa kwenye mti ali aanze kuchapwa, maana yule baba alikuwa anapenda kufanya hivyo kwa mtu yoyote mwenye kosa.Ila siku hiyo yule baba alikuwa amechoka sana hivyo akamuita mwanae akamchape mwizi wake.



    Kipindi mwanae ameshika fimbo anaenda kumchapa akashangaa mdogo wangu anasema ” baba husinichape ni mimi mwanao”



    Yule mtoto wa yule baba akasema “mwanangu yupi tena” Ni mimi ulie niacha mjini na kaka yangu baada ya mke wako kufariki, ukaniacha mimi na kaka yangu mjini wewe ukaja na watoto wako kijijini.Kumbe alikuwa ni HANS masikini alie waacha mjini wakiwa wadogo sana hans akamuuliza..



    Hans akamuuliza, kaka yako yuko wapi? alafu mbona sura yako imeungua mpaka nikashindwa kukutambua? Na umefikaje fikaje huku maana sikuwambia nakuja kijiji gani.



    Mdogo wangu akasema, tulipata bahati ya kukaa kwa mama mmoja tajiri, tuliishi vizuri kwake,



    lakini alikuja mwanamke mwingine ambae kaka aliniambia ni mama yake wa kambo, Huyo mama alivyo kuja tu, yule mama mwenye nyumba akafa,kumbe yule mama akataka kuniua na mimi, mzimu wa marehemu mama yangu ukanisaidia mpaka nikatoroka nyumbani.



    ila nikapanda gari bila pesa yoyote mfukoni! sasa konda alipo kuwa anangalia tiketi  akanishusha tukiwa tumefika hichi kijiji,



    sikuwa na sehemu ya kula ndiyo maana nikaja shambani kula maembe yule mzee wako ila akanikamata.



    Hans akamuuliza na sura yako je,?



    kipindi nataka kukimbia yule mama akanimwagia maji ya moto usoni, yani hapa nilipo nahisi maumivu sana na kidonda bado kibichi bado kinatoa maji.



    Hans alimuonea huruma sana akamwambia” unabahati sana wewe na je konda asinge kushushia hapa au je usinge iba maembe ungefikaje hapa, alafu una bahati maana baba yangu anachapa sana leo ungekoma” Hans alimchukua mdogo wangu akampeleka kwa waganga ili wamtibu sura yake,



    mungu saidia alipewa dawa za kyenyeji mpaka akapona sura yake ikakaa vizuri kabisa.



    Ndipo akaanza maisha ya kijijini, mdogo wangu akawa analima na wale watoto wa hans, maana tayali walikuwa mabinti wakubwa tu pale kijijini.



    Mzimu wa mama dani uliendelea kumtesa sana mama yangu wa kambo ikafika hatua mama akaanza kulala nje ya nyumba kupunguza mateso, mama alikuwa ateseki mchana lakini usiku alikuwa akiangaika sana jamani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Siku moja kule kijijini mdogo wangu alitokewa na mzimu wa mama , ukamwambia “Mwanangu usione umefika hapa kwa hans, sio kwa ujanja wako, nimekusaidia mimi mwanangu kukufikisha kwa huyu kijana tena, maana mimi nilifariki mikononi mwake na mimi ndiye nilie mkabidhi yeye akulee, muheshimu kama baba yako na usirudi tena kwa mama dani, mpaka mama yenu wa kambo afe”Mdogo wangu akamuuliza mama “hivi baba yangu mzazi ni nani”



    Mama akamwambia “nilipo fukuzwa na baba yake kaka yako sikuwa na sehemu ya kulala usiku, ndipo nikabakwa  na vijana kama saba  mwanangu, ndipo mimba yako ikapatikana,….



    Mdogo wangu alisikitika sana mzimu wa mama ulipowambia kuwa baba yake ajulikani,



    Ila Maisha yake yaliendelea vizuri sana pale kijijini yani mdogo wangu akawa mzoefu sana kwa yale maisha, Na ikafika hatua akayapenda sana



    lakini mdogo wangu alikuwa ananikumbuka sana mimi kaka yake na alitamani  hata siku moja tuonane, lakini aliogopa kuja mjini maana tayari mzimu wa mama ulimwambia asiende kwa mama dani mpaka mama wa kambo akifa.



    Mimi niliendelea kuishi maisha ya wasiwasi na mama yangu wa kambo pale nyumbani lakini nilivumilia tu.Baada ya siku kwenda mbele, siku moja Hans akamuita mdogo wangu kisha akamwambia kwamba “Mwanangu nakumbuka ulisema kuwa kipindi upo mjini ulikuwa unasoma sekondari?” Mdogo wangu akajibu “ndiyo baba”



    Hans akasema “sasa sikiliza kuna mbunge mmoja amekuja kutafuta kura hapa kijijini kwetu, ili achaguliwe kwa mala ya pili, lakini amesema wasichana wote hapa kijijini wanaotaka kusoma yupo tayari kuwasomesha ili wasiolewe kwa umli mdogo”



    Mdogo wangu hakuamini akamuuliza Hans kwamba “baba hivi ya kweli unayo yasema au unatania,”



    Hans alimjibu,”kesho utaenda kuandika jina lako mtapewa pesa za matumizi na mtapelekwa mpaka jijini “dar es salaam” mpaka shuleni kusoma, ada ya shule na kila kitu anagharamia mbunge mwenyewe na hamtarudi tena kijijini mpaka mumalize masomo yenu”



    Mdogo wangu alifurahi sana akasema “ehh asante mungu ndoto zangu za kuwa mwanasheria zinatakamilika”. Kipindi mdogo wangu anaenda shule watoto wa hans na hans mwenyewe wakamsindikiza kisha wakamwambia kuwa “ukimaliza masomo yako usitusahau, utukumbuke na sisi kijijini”



    Mdogo wangu akawajibu kwamba siwezi kuwasahau ndugu zangu, na siwezi kukusahau baba yangu”



    Walibaki na majonzi kipindi anaondoka maana walikuwa wameisha mzoea sana mdogo wangu.



    Alipo fika shuleni alikuwa anafauru vizuri sana na alikuwa anashinda nafasi za juu kila mtihani,



    Mimi sikujua kama mdogo wangu yupo mjini maana ile shule walikuwa hawatoki nje ya geti mpaka wamalize masomo, hivyo ilikuwa ngumu kutambua kama yuko pale.



    Ila sasa siku moja kichwa kilikuwa kinaniuma sana hivyo nililala kwa tabu sana. Kipindi natafuta usingizi polepole, nilishangaa kusikia mama anapiga kelele kama anapigwa usiku…



    Mama alikuwa ameanza kuteswa na mizimu mitatu mida ya usiku,alipo enda chooni aliukuta mzimu wa mama danieli unalia.Na sebreni aliukuta mzimu wa mke wa hans unalia ukimwambia “ulitembea na  mme wangu hans, alafu ukaniua kwa kuniroga nimekufata lazima ufe pia we mwanamke”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama wa kambo alianza kulia na kwenda kukaa chumbani ndipo mzimu wa  mama ukamtokea na kumwambia “malipo ni hapa hapa duniani lazima ujutie yote uliyo yatenda



    “Maisha ya mama wa kambo yalikiwa magumu sana, tena sana sana nyakati za usiku,



    Mama wa kambo aliamua kwenda kwa wale wachawi ili wamsaidie, Asiweze kuangaika maana ile mizimu ilikuwa inataka kumtesa sana mama wa kambo mpaka apoteze maisha yake.



    Wale wachawi walimwambia mama “tulikwambia umuue yule binti ukashindwa sasa tukusaidieje tena”



    Mama akawambia “nipo tayari ata kumuua huyu nilie baki nae wa kiume pale nyumbani, au ata mtu yoyote jirani yangu nipo tayari kumuua ilimladi hii mizimu isinisumbue”



    Wale wachawi walimwambia “hauruhusiwi kumuua mtu mwingine zaidi ya yule binti”



    Mama wa kambo aliwambia “Naomba nimuue huyu kijana, maana mdogo wake alikimbia nimebaki na yeye mmoja tu”



    Walimwambia kuwa “huyu kijana auwezi kumuua maana alisha toa damu yake kwajili yako, kipindi kile umefumaniwa na mke wa hans, maana alitega mkono wake kile kisu kikamchoma yeye!hivyo ile damu inakufata bado nyuma ukimuua utateseka zaidi”



    Wale wachawi wakasema “ili hii mizimu ikapumzike na ikuache wewe unatakiwa kufanya mapenzi na huyo kijana”



    Mama alishtuka sana alipo ambiwa kufanya mapenzi na mimi.



    Mama hakuwa na jinsi akakubali kufanya mapenzi nami, ila aliwaza sana ni jinsi gani ataniambia mimi nifanye nae mapenzi. Alikuja nyumbani akiwa na furaha sana, nilipo muona nikamwambia mama kuwa “mama mwaka huu namaliza chuo,natakiwa kulipa ada ya shule”



    aliniambia “nitakuletea leo usiku chumbani kwako” Mama alikuja mida ya saa sita usiku akiwa amevaa nguo fupi ikionyesha mapaja yake na kitovu chumbani kwangu, aliniambia “mwanangu, tangia baba yako aniache sijawai kufanya mapenzi na mtu yoyote, Naomba tufanye mapenzi nina hamu sana, nisaidie mwanangu!huku akiwa ananivua shati langu polepole.



    Nilisikitika sana pale Mama yangu wa kambo alipo kuwa anataka kufanya mapenzi na mimi  ili mizimu iache kumsumbua, sikuamini kweli maana nilikuwa sitegemi kabisa tabia ile kama anaweza kuileta kwangu. Mama alisema kwamba “najua nilikuwa mke wa baba yako mzazi ndiyo, lakini ata tukifanya mapenzi hakialibiki kitu ebu angalia tunaishi wawili tu ndani unaniacha mimi nateseka hivi naomba unisaidie jamani, Mwanangu naomba  kubali nitakupa hiyo ada ya chuo na pesa zote za matumizi ilimladi unikubalie ombi langu ila usimwambie mtu yoyote itakuwa siri yangu mimi na wewe tu.” Nilikataa nikasema “hapana mama kumbuka wewe ni mke wa baba yangu mzazi! inakuwaje unanitesa hivi lakini ujue ata mungu hapendi mama yangu nitaanzaje kwanza kufanya mapenzi na wewe mama yangu”.



    Mimi naomba unisaidie nipate ada japo nimalizie elimu yangu tu, Maana ata sielewi tangu mama danieli afe umekuwa unatunyanyasa humu ndani. Angalia mdogo wangu tayari kaisha toroka sababu yako. Mama aliendelea kusisitiza akisema kwamba “sikiliza mwanangu naomba unisaidie mimi nateseka sana usiku nikiwa chumbani mwenyewe naomba tufanye japo mala moja tu inatosha”. Dah Sikujua kama anateseka na mizimu nilihisi mambo mengine tu ya ngono.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Yani mama alijaribu kunishikashika mwili wangu akiniambia “kwani ukinifanya mala moja utakufa, Ebu acha ushamba bhana, jaribu ata wewe utafurahia tu”, Aliamka akaenda kuzima taa ya chumba changu usiku huohuo. Niliogopa nika tetemeka sana mimi maana ata hisia japo kidogo sikuwa nayo kwake huyu mama jamani, na tabia zake mbaya nilikuwa nazifahamu hivyo nikajua mama anataka kuniharibia maisha ili na mimi niishi kwa matumaini. Mama akasema “nimezima taa nahisi ndiyo inakutia wewe aibu” nilimwambia “hapana mama siwezi kabisa kufanya hii dhambi maana najua ata kwa mungu haitasameewa”. Mama akasema kwani mungu unamjua? Alinilazimisha sana.



    Ndipo nikaanza kulia kama mtoto ili japo nimkubalie tufanye mapenzi mizimu iache kumtesa yule mama.  nikasema  “mama naomba tusifanye leo kesho njoo tutafanya”. Mama akasema hapana wewe utanitoroka mimi nataka leo nisaidie tu nitakuwa na wewe kila sehemu kwenye shida na raha zote za dunia. Nilimwambia mama kuwa “mama toka juu ya mwili wangu mimi siwezi kufanya tabia zako mbaya” Mama akasema jamani ebu angalia tayari nipo juu yako kwanini usivue nguo zako zote tu unisaidie japo kidogo tu, atukai sana mwanangu! Yani wewe haujui tu ila nateseka sana usiku. Mama alikataa kutoka juu ya mwili wangu huku akinibembeleza nivue nguo zangu zote ili nilale nae.



    Sikuuelewa ule mchezo kabisa, Niligoma ndipo mama akasema. Tambua mimi ni binadamu na ninatamani hiki kitu pia naomba unisaidie. Nilimwambia najua unahitaji ila sio kwangu maana mimi ni mwanano. Aliguna akasema acha ushamba bwana unaniuzi sasa kwani mimi ndiyo nilikuzaa wewe, mama yako alisha fariki. Mama akasema  sasa sikia “kama unaitaji msaada wowote kutoka kwangu naomba ukubali maana ata mimi naitaji kuishi kwa starehe pia. Au kama haupo tayari kusoma chuo sema? Maana ukikataa kufanya ata hiyo ada sitokupa kabisa nakwambia” Mama alijaribu sana kunishawishi nifanye nae hilo tendo ili mizimu iache kumtesa usiku. Ila nilikataa.



    Dooh ndipo nilishangaa mama ananivua mkanda wangu wa suruali kisha anaivuta suruali yangu chini tukiwa wote kizani, akisema nisadie mwanangu nisipo fanya na wewe basi nitakosa raha sana. Mama aliongea hivyo maana sharti la kumuua mdogo wangu alishindwa hivyo akaambiwa alale na mimi mizimu isimsumbue! ndiyo maana akalazimisha sana nilale nae alipo nivua nguo kabisa akasema subili kidogo ndipo mama akaenda kufunga mlango na komeo akasema “nitakuwa nakupa pesa na kukupa unachotaka naomba tufanye tu, ebu angalia nipo uchi sasa nakutegemea wewe hakuna atakae jua tunafanya hichi kitu maana tupo wawili tu humu ndani.. Nilipo anza kumuona mama ananifata tena kitandani Nywere zangu zilisisimka sana nikaogopa ndipo nikamwambia mama kuwa. Mama sikiliza mimi nipo tayari kufanya mapenzi na wewe lakini naomba tutumie kinga maana ata shuleni tunafundishwa kwamba, usimuamini mwenzako kwa kumtazama. Mama akasema sasa hiyo kinga unaipata wapi jamani. Maana mda umeenda sahivi.nilimjibu hapo nje kuna duka la madawa la masaa ishirini na nne nikitoka nje nachukua haraka narudi tufanye. Mama alikubaliana na mawazo yangu. Alipo niruhisu kutoka tu nje ndipo akawa amefanya kosa. niliamua kumkimbia pale kwake.



    Mama kipindi yupo chumbani ananisubilia kwa  hamu maana alihisi amenishawishi sana kumbe hapana. Alisubilia sana mpaka akaanza kijiuliza maswali kuwa… huyu mbona haji? Au amekuta kinga hazipo kwenye hilo duka, ngoja nimsubilie aje anisaidie nimeichoka mizimu ya kila siku inayo nitesa. Mimi niliamua kutoroka kwa mama danieli nikamuacha mama yangu wa kambo  mwenyewe ndani ya ile nyumba. Mdogo wangu wa kike kumbe alikuwa akiendelea na masomo yake na hakuna aliyekuwa hamfahamu shuleni kwao.



    Maana alikuwa anafanya vizuri katika masomo,  Nilipo toloka nyumbani usiku ule. sikuwa na sehemu yoyote ya kulala na kulikuwa na baridi sana siku hiyo maana nililala chini ya mti, mpaka nilitamani sana ningekuwa nyumbani lakini nilikuwa namuogopa sana mama wa kambo maana kwa jinsi alivyo lazimisha nilale nae kimapenzi iliniuma sana. Niliamua kulala nje siku hiyo ila nilitetemeka sana jamani. Mama alisubilia kama naweza kuja, ila sikurudi  tena nyumbani na nilimchukia mama sana maana niimuona ni mtu mbaya katika maisha yangu, sababu alikuwa mwasilika na alitaka kufanya mapenzi na mimi, wakati mimi nateseka sina pakulala jamani. Kumbe mama anateswa pia na mizimu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama aliendelea kuteswa zaidi maana Kipindi cha nyuma alikuwa akipigiwa kelele tu. hivyo walipo ona amezoea kupigiwa kelele. Mizimu pia ikabadilisha hadhabu, ilikuwa inakuja chumbani kwake imevaa sanda nyeupe kisha inaanza kumchapa sana mama na alichapwa na mizimu yote chumbani kwake ila mzimu wa mama daniel ulikuwa unamchapa uku unalia. Dah Mama akaanza kujiuliza afanyeje sasa. Mama yangu wa kambo aliamua kuwafata wale wachawi wenzake na kuwambia ukweli kuwa haja bahatika kufanya mapenzi na mimi na akawambia tayari mimi nimeisha mtoroka pale nyumbani. Mkuu wa wale wachawi akasema huyu mwanamke tangia tumempa uchawi hajawai kuleta damu ata zaidi ya mala tano alileta ya mme wake na ya mama danieli tu lakini anatusumbua,  na tangia awe mchawi hajawai kufanya agizo lolote likakubalika.



    hivyo kwanzia hivi sasa, kama unataka ile mizimu isikusumbue tena “unatakiwa kurudi nyumbani na kuchukua nguo zako zote alafu unatakiwa kuiacha nyumba ya mama dani  kama ilivyo pia usitoe pesa wala gari lolote ndani yani toka kama ulivyo ukatafute maisha mengine, ukifanya hivyo ndipo ile mizimu  itaacha kukusumbua. Kipindi mama anateseka na Mimi nilijaribu kutafuta pesa ili nisome ila ikawa ngumu ndipo nikaanza kujiushisha na kuosha magari ya watu ili nipate pesa ya kula. Mama wa kambo alipo ambiwa haache mali zote za mama dani ili mizimu isimsumbue alianza kulia akisema. “jamani naenda wapi mimi sahivi nikiacha hizo mali maana sina ata kazi.”Kweli mama yangu wa kambo aliacha ile nyumba kama alivyo ikuta ma magari yote akayacha kama yalivyo.



    Ndipo mama akaanza kuingia mtaani kutafuta tena maisha mapya. Mimi pia niliendelea na kuosha magari ya watu lakini sehemu ya kulala ilikuwa ni ngumu sana kwangu siku moja nilibahatika nikampata kaka mmoja yeye alikuwa amepanga  akanisaidia akasema njoo ukae kwangu kwa mda ila ukipata pesa zako utaama na upange kwako pia, nilimsimulia stori ya maisha yangu akawa amenionea sana huruma. akasema pole sana ila bila “damu ya baba yako” wewe usinge teseka hivi na mama yako mazazi asingekufa jamani ila mshukuru mungu. kisha nikaanza kukaa kwake nikifanya kazi yangu ya kuosha magari.



    Nyumba na Mali za mama danieli ziliachwa pekee bila mtu yoyote kuishi ndani maana ata mimi sikupenda kurudi kule nyumbani, mama wa kambo aliendelea kuangaika sana kwa kupata sehemu ya kula na kuishi lakini mizimu iliacha kumtesa sababu aliama pale kwa mama danieli kama alivyo ambiwa na wachawi wenzake,



    Mama danieli alimtesa sana mama maana mzimu haukupenda kabisa mama yangu wa kambo aendelee kuishi kwake, maana mama danieli aliangaika sana kutafuta mali zake, mama yangu wa kambo aliangaika ila siku moja alibahatika akapata kazi kwa mtu ili awe msaidizi wa kazi za ndani.



    Mimi kipindi hicho naendelea na kazi za kuosha magari ya watu ili kukidhi maitaji yangu ya kila siku. Siku moja niliosha gari la mama mmoja hivi alie kuwa na uwezo sana, nilijitahidi kulifanyia gari lake usafi likapendeza sana, alipo toka ofisini kwake alishangaa sana kuona gari lake limependeza zaidi ya alivyo kuwa anafikiri.



    Akasema, we kijana mbona umenifurahisha sana hivi,Tangia nianze kuwapa vijana wengine kuosha ili gari wamekuwa wakiosha ovyo ovyo tu,



    Nikasema , ahsante bosi wangu, mimi napenda kufanya kazi au kitu chochote kwa roho moja ata kama si changu



    Alivutiwa na maneno yangu akaniambia kuwa.



    Tafadhali kijana kwa siku unapata shingapi kwenye hizi kazi zako?



    Nikamjibu kuwa, Napata 6000 ila mda mwingine inakosekana kabisa sipati chochote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Yule mama Akasema, je upo tayari nikuajili uwe mfanyakazi wangu ukaishi kwangu niwe nakulipa kwa mwezi laki tatu na utaishi kwangu pia utakula hapohapo kwangu. Maana nimependa jinsi unavyo fanya kazi kwa roho yako safi.



    Sikuamini maneno yake kabisa nikahisi labda ananitania nikamuuliza kwa furaha tele usoni mwangu kwamba hivi nikweli utanipa kazi au unanidanganya tu?



    akasema kwamba,



    chukua namba yangu ya simu hii hapa kisha ndani ya hii wiki ukiwa tayari kufanya kazi niambie ili niweze kukuchukua na kukupeleka kwangu,



    sikuamini ujue maana aliniacha elfu hamsini kisha akasema kajiandae utaishi kwangu na usiniangushe naomba ukaishi kwangu unisaidie kazi zangu mwanangu.



    Kweli nilitoka yale maeneo ya kazi kisha nikaenda sehemu ninayo ishi ili niweze kumuelezea rafiki yangu ninae kaa nae bahati niliyo ipata.



    Nilipo fika nyumbani nikiwa na furaha kuwa lazima nitapata pesa niendeleze masomo yangu,



    kipindi nipo ndani namsubilia rafiki yangu aje,



    alikuja mtu akagonga mlango, ndipo nikaamka kwenda kumfungulia ila bahati mbaya nikaamka haraka maana nilikuwa na furaha sana dooh pale pale kichwa changu kiligonga kioo cha ukutani kikaanguka chini, nilipo kuwa nainama kuokota vipande vya kioo, wakati nasimama mguu ukagonga stendi ya Tv ikaanguka nayo chini tena vibaya na ikapasuka palepale pia kioo chake dah Kipindi nawaza mkosi gani huu najaribu kuinua ile stendi ya tv vizuri, nikaangusha ndoo ya unga wa ugali ambao tulikuwa tukipika pale nyumbani, wakati huohuo Yule mtu alikuwa anaendelea kugonga mlango nje ili nimfungulie, nilipo fungua nikizani ni rafiki yangu kaja ili nimwambie bahati iliyo nikuta, nikashangaa kumkuta mtu  mwingine akisema kuwa,



    “kaka mimi ni muuza laini za simu nimekuja kuuliza kama unaweza kununua hatalaini moja”.



    Nilishindwa ata kumjibu nikakaa kimya kwanza, akauliza kaka vipi mbona kimya ghafla,



    Nikamwambia kwamba “ hivi unajua asala niliyo ipata hapa kwajili yako? Nimealibu vitu vya watu ndani ata sijui navilipaje mimi dah”



    Yuke muuza laini za simu alipo ondoka,



    ndipo rafiki yangu mwenye kile chumba akawa amekuja, alipo ona vitu vyake vimealibika akasema,”kaka mbona unanialibia vitu vyangu hivi tatizo nini kwani jamani nimekukosea nini” akaanza kulia!



    Nikambwambia nimeangusha bahati mbaya kaka sijafanya makusudi kabisa. Akaniambia ulipo kuja kuomba msaada kwangu ulisema mama yako wa kambo kakufanyia mambo  sana  ukatoroka kwake na ndo maana nikakuruhusu ukae hapa kwangu, ila sahvi sikuamini tena nahisi wewe ndiyo sio mwaminifu na wewe ndo mwalibifu ndiyo maana umefukuzwa ata kwenu,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    nilimwambia kaka naomba unipe nafasi japo niongee, akasema nikupe nafasi ya nini wakati umeniharibia vitu vyangu ebu toka hapa, tena sikutaki kabisa kwangu,



    nikasema kaka nivumilie nitakulipa vitu vyako hivi karibun kaka.



    Alisema unilipe nini wakati mtu mwenyewe kazi zako za kubahatisha, nikajaribu kumwambia nimepata kazi nzuri lakini inayo lipa kwa Yule mama ila  hakunielewa kabisa, akasema kwa hii tabia uliyo fanya ya kunialibia vitu vyangu makusudi sikutaki tena kwangu ni bora uondoke kabisa.



    Niliamua kutoka kwake,  kisha mda huohuo nikampigia simu Yule mama alienipa namba ili niende kwake,



    kweli alinifata nikaenda nae mpaka kwake, ama kweli alikuwa na maisha mazuri yeye na mtoto wake wa kike.



    Kipindi nipo sebreni natazama TV



    Yule mama akamwambia binti yake  anionyeshe chumba changu cha kulala na kunizungusha maeneo ya pale nyumbani ili niwe msaidizi wa kazi na mazingila ya pale nyumbani.



    Tulipo maliza kuzunguka, na mda wa lanchi ukawa umefika pia, ndipo tukarudi sebreni ili twende sehemu ya kupatia chakula.



    Wakati tumekaa tunasubilia chakula kiletwe na dada wa kazi nilishangaa sana kumuona mama yangu wa kambo analeta chakula jamani.



    Dooh Nilishtuka sana  kidogo nikimbie kutoka pale nyumbani, ,mtoto wa boss wangu akasema, “ mbona unaogopa tatizo nini kaka huyu ndiye mfanyakazi wetu wa ndani. ni mpole sana hana shida kabisa anaongea na kila mtu” mama wa kambo alijua lazima nitamuumbua palepale kuwa na mfahamu akaweka sura ya upole sana jamani ila mimi nilinyamaza kimya sikuongea chochote kwanza.



    Nilikula chakula nikiwa na wasiwasi nikatamani ata kutoroka na kutoka kwenye ile nyumba,



    mtoto wa bosi akasema, “ jamani  mimi ngoja nikalie chakula sebreni kuna kipindi kwenye tv nakifatilia”



    hivyo Nikabaki na mama yangu wa kambo tu.



    Nikamuuliza maswali mengi sana pale.



    Hivi mama umekuja kuteketeza na hii familia kwa kujifanya mwema kama ulivyo fanya kwetu sio? Mama akaanza kulia, nikamuuliza tena, Na nyumba ya mama dani uliifanya yako je umemuacha nani kule?



    Ndipo mama akasema kwamba naomba usimwambie mtu yoyote kama tunafahamiana mimi nimeacha kuishi maisha ya ubaya kama ya zamani sahivi mimi naishi vizuri tu sina shida na mtu yoyote. Na ile nyumba nimeiacha kama ilivyo maana usiku nilikuwa siwezi kulala sababu mizumu ilikuwa inanitesa sana hivyo nikaona bora niache tu kuishi kule,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama alipo sema kuwa mizimu inasumbua kule nikakata kabisa tama ya kwenda kule kwa mama dani maana ata mimi nilikuwa naogopa sana mizimu.



    Tuliendelea kuishi tu vizuri kwa Yule mama pale nyumbani na nilifanya kazi zangu vizuri sana bila kuwa na kinyongo.



    Kumbe baba yangu mzazi baada ya kuona hari inakuwa ngumu, hivyo akaamua kuanza kuomba misaada kwenye nyumba za watu ili aweze kupata japo pesa ya kula.



    Hata hivyo Wengine waliokuwa na huruma walimsaidia pesa na wegine walio kuwa wachoyo walimtukana na kumzuia asije kuwasumbua tena kwao.



    Siku moja baba alienda mpaka kwa mama dani kwenda kuomba msaada bila kujua kama ni kwa mama dani au bila kujua kama sisi watoto wake tuliisha wai kuishi pale kwa mama danieli.



    Alipo fika aligonga geti la nje ila hakuna alikuja kufungua!



    aligonga sana mpaka akaamua kuingia ndani mwenyewe.



    Baba yangu alikuta magari mazuri, alishangaa sana pale nje alikuta uwanja mchafu sana kama haujafagiliwa siku nyingi,



    baba alienda mpaka mlango wa kuingia sebreni akagonga hakuna alie fungua baba akusita akaingia mpaka ndani pia ili aombe msaada maana alikuwa na njaa sana,



    alipo ingia akakuta hamna mtu yoyote pia.



    kumbe ulikuwa ni mzimu wa marehemu mama yangu unampeleka sehemu nzuri baba maana baba aliteseka vya kutosha na aliomba msamaa kaburini mwa mke wake na mama yake hivyo ule ndiyo ulikuwa msamaa kwake.



    Baba alipo ona hakuna mtu ndani alitaka kuondoka na kuacha nyumba ya mama danieli ikae bila mtu, ila wazo zuri likamuijia kwamba abaki mpaka wenyewe waje.



    akabaki palepale na alishangaa kuona inafika usiku mtu haji, wiki ikaisha mtu hajaja, mwezi ukakata akuna aliekuja.



    Ndipo baba akaanza kukagua nyumba



    Mungu saidia akakuta funguo za gari na pesa nyingi sana chumbani mwa mama danieli, zilikuwa kama miliioni 200 pesa za kitanzania na pesa zingine za kigeni kama dola elfu mbili, ndipo maisha ya baba yakonyooka sana akaanza biashara zake na kuishi vizuri pia.



    Maisha ya baba yangu mzazi yalikuwa mazuri, Alipendeza na kurudi katika hari yake ya zamani. Kipindi nipo kule kazini mimi na mama yangu wa kambo, Hatukujua kabisa kama kule kwa mama daniel ndipo baba mzazi yupo. Na hakuna ata mtu mmoja alikuwa anawaza kwenda kupaona kule kwa mama dani. Siku moja usiku tukiwa wote tumelala yani mimi, bosi wangu na mwanae mida ya saa nane na nusu usiku, Tulishangaa sana kusikia  mtu analia akipiga mayohe kama anapigwa sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Dooh ndipo tukaamka tukaenda nje kuangalia kunanini. Tulishangaa kumuona mama yangu wa kambo anajiviringisha chini kama anachapwa. Bosi wangu akauliza. Huyu katokaje ndani kuja nje? na mbona kama anachapwa jamani? na anae mchapa hatumuoni sisi! Mimi niliogopa sana kile kitu. bosi wangu akamuuliza mama yangu wa kambo swali kwamba “dada mbona unalia unapiga kelele tatizo nini” mama yangu wa kambo akajibu kuwa  “jamani nisaidieni napigwa na mizimu natweswa jamani” bosi akamuuliza “kwani umefikaje hapa nje wakati milango yote imefungwa kwa ndani” mama wa kambo akamwambia kuwa “nimebebwa kimzimu nisaidieni nachapwa mimi”.



    Hama kweli alikuwa anatia sana huruma, kitendo kilicho nifanya mpaka nitoe machozi palepale. Tulikuwa hatuna jinsi ya kumsaidia ikabidi tukae tukimtazama jinsi anavyo teswa. Tulijaribu kumshikiria ili asijivute sana chini maana alikuwa anapiga sana kichwa chake chini na alikuwa anajisugua sugua chini mpaka akachubuka mwili mzima. Bosi akasema “kijana wangu mbona hili balaa kubwa sana nyumbani kwangu maana hivi vitu havijawai kujitokeza kwangu kabisa ndo mala ya kwanza ” nilimwambia kuwa  “Bosi usijali labda ni mizimu ya nyumbani kwao, maana hii sio hari ya kawaida” Ilipo fika saa kumi alfajiri mzimu wa mama danieli ukawa umemuachia! ndipo mama akashtuka akishangaa akasema, “hee jamani bosi nimefikaje hapa, na mbona nimeumia hivi tatizo nini”  Kipindi mama anaamka kusimama nguo yake ikadondoka chini, aliona haibu sana pale maana tulikuwa tukimtazama na tulikuwa  tumeanza kumuogopa kabisa.



    Bosi wangu kile kitendo kilimkwaza sana, Hivyo akahisi ile mizimu inayo mtesa mama wa kambo inaweza tena kumtesa na yeye, hivyo basi, Bosi akamfata rafiki yake anaeitwa wastara. Bosi akamwambia “besti yangu uwezi amini, yani jana yalio nikuta nyumbani kwangu, nashindwa ata nianze vipi kukueleza” wastara akamwambia, usijali besti mimi tena we niambie tu anzia popote pale unapo pataka. Ndipo bosi akamwambia “yani jana pale kwangu yule dada msaidizi wangu wa kazi, alitolewa ndani na mizimu  bila milango kufunguliwa kisha akaanza kupiga makelele  sana kwa nje.



    Sasa nilivyo toka nje mimi na mwanangu pamoja na yule kijana wangu wa kazi unae msifiaga sana, tulishangaa kumuona anajiviringisha kama nyoka, Yani wastara shoga yangu  nashindwa ata nifanyeje maana ata nyumba yangu nimeisha iogopa nakosa amani” wastara akamwambia, “besti yangu mshukuru mungu kakuonyesha ili janga mapema, huyo dada hakufai nakwambia, yani mtoe hapo kwako mapema anaweza kukuletea matatizo makubwa, na mungu wako mkubwa sana”.



    Bosi akamwambia kuwa “lakini wastara besti yangu yule dada anapika chakula kitamu sana na anafanya kazi kama mashine alafu sio mwizi hajawai kuniibia hata shilingi mia yangu nikisahau hela nakuta kanitunzia” ndipo wastara akamwambia kuwa  “tayari nimeisha kwambia mtoe kwako au kama unaweza mwambie akupeleke hadi nyumbani kwao upajue na wazazi wake au ndugu zake uwajue wakuelezee kuhusu yeye na wala sio kukaa nae kiholelaholela tu” bosi wangu akamwambia sawa rafiki yangu.



    Kumbe kule nyumbani mama yangu wa kambo alipo ona anateseka sana akaamua kurudi kwa wale wachawi akawambia “jamani wakuu mimi mmeniambia niache mali zote za mama dani. Sasa mbona bado mzimu wake unanifata na unanitesa sana” mkuu wa wachawi walimwambia kwamba ” mzimu wa mama danieli umekufata tena sababu ya huyo mtoto wa mme wako alie lelewa na mama danieli, lakini huyo kijana akitoka hapo  mzimu haukufati tena” mama akawajibu “sawa nitajua cha kufanya”  mama alipo rudi nyumbani alianza kununa kila mda akisema “wewe ndiyo chanzo cha mimi kuteseka hivyo naomba uondoke uniache niishi kwa amani hapa”.



    Sikuelewa kabisa yale maneno ya mama nikamuuliza kwamba, “sasa nikiondoka hapa nitaenda kuishi wapi mimi” mama wa kambo akasema “sitaki kujua mimi naomba uondoke tu au kama upo tayari tufanye mapenzi ili nisiteswe na mizimu mimi”. Haaaa nilishituka sana jamani nikamuuliza kuwa mama kuwa “kumbe unataka kulala na mimi ili usiteswe, na hutaki kukaa hapa na mimi ili usiteswe sio, sasa kukaa hapa nitakaa na kufanya mapenzi ma wewe sifanyi”.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama wa kambo akasema “jamani mwanangu hivi unafurahia ninavyo teseka. Ebu angalia jinsi nilivyo umia.” Nilikataa kabisa  kumsikiliza mama yangu wa kambo mambo yake anayo niambia. Dooh Sitasahau mama wa kambo jamani, maana alienda akamwambia bosi wangu kuwa “mimi natembea kimapenzi na binti yake”.



    Bosi wangu alichukia  sana akasema “yani binti yangu natumia pesa nyingi sana kumsomesha alafu huyu kijana anataka kumualibia maisha” ila akasema siwezi kuamini mpaka nifanye uchunguzi. Siku moja usiku mtoto wa bosi akaja chumbani kwangu nimfundishe hesabu maana mimi nilikuwa najua sana hesabu, kuliko masomo yote, na hata kipindi sijaacha chuo nilikuwa nafauru sana hesabu, alikuja akasema “kaka nimekuja unifundishe hesabu kuna maswali magumu siyawezi alafu kesho nina mtihani”.



    Kumbe wakati anaingia chumbani kwangu mama yake ambae ni bosi wangu akawa amemuona anaingia!  Ndipo Mama yangu wa kambo akamwambia kuwa, “bosi unaona binti yako anajifanya anaingia na madaftali kusoma kwa huyo kijana kumbe wanafanya mapenzi tu ndani, mimi nataka mwanao asome mfukuze uyo kijana mnusuru mwanao bosi”. Bosi wangu alilia sana nje akasema yani huyu kijana nimemsaidia maisha yake kumbe mpuuzi kiasi hichi, yani ananialibia mwanangu tena ndani kwangu, siwezi kukubali.



    Wakati mama na bosi wapo mlangoni, mimi na mtoto wa bosi tulikuwa chumbani kwangu, nikamwambia yule binti kuwa “mdogo wangu unataka nikufundishe maswali gani”, alinionyesha maswali kisha akasogea karibu yangu, wakati naanza kumuelekeza maswali bahati mbaya taa yangu ikapata shoti! Dooh ikawa imeungua! ndipo tukakaa gizani. Mama yangu wa kambo akasema bosi unaona wamezima taa sasa. Bosi Kusoma gani huko gizani jamani, yani hawa Wanafanya mapenzi tu, na wenyewe wanajua wote tumeisha lala hivyo wanajua hatujui.



    Wakati huo mimi chumbani nikamwambia yule binti “nazani taa imepigwa shoti itatubili twende sebuleni nikuelekeze maswali” mtoto wa bosi akasema “sawa kaka”. Wakati bado sijaamka kwenda sebreni bosi akaja na mwiko wa ugali akanitwanga nao kichwani akasema yani nakusaidia kuishi kwangu kumbe ndiyo mnakaa karibu karibu na mwanangu mnafanya ushenzi ndani kwangu, bosi akasema “wewe mwanangu tabia hizi umeanza lini”, bosi alichanganyikiwa maana alijazwa maneno ya uongo akasema “wewe kijana panga vitu vyako uondoke sikutaki hapa”, nikamwambia bosi niruhusu niongee kidogo.



    Bosi wangu, akasema “wee kaa kimya, mpumbavu sana wewe, Uongee kwani we mme wangu, ebu toka hapa sikutaki, dooh mtoto wa bosi akasema “mama usimfukuze hana kosa”, mama yake akasema ” mwanangu unabishana na mimi unanivua nguo sio?  ndipo nikaamua kuchukua nguo zangu kisha nikatoka usiku huohuo bila kujua nitalala wapi huku kichwa kikiwa kinaniuma sana maana alinipiga vibaya na mwiko, mama yangu wa kambo alifurahi sana ndipo nikaamua kutafuta japo sehemu ya kujiegesha mwili wangu ili asubui nitafute sehemu ya kuishi.



    wakati nimelala chini ya mti wakaja vijana wanne wakiwa wameshikilia silaa waliniambia niwape begi langu la nguo na simu, nikakataa ndipo mmoja akanipiga na panga mgongoni likanikata kiubapa ingawa sikufa ila niliumia sana, niliwaachia mali zote wakakimbia, Ilipo fika asubui. Bosi wangu akaenda kumuelezea rafiki yake wastara mambo yaliyo mkuta kwake, ila wastara alisikitika sana kusikia nimefukuzwa. akasema “usinge mfukuza maana hukuwa na uwakika, na yule kijana ni mchapa kazi sana, mtoto wako ungemchunguza kwanza.



    Sasa taa imezima wewe ukaamini. Sio vizuri ulicho fanya. Kwani wewe binti yako umuamini, wastara akamwambia tena huyo mfanyakazi wako wa ndani ndiyo mbaya sana mimi simuamini hata kidogo. Mama yangu wa kambo akahisi kuwa awezi kusumbuliwa tena na mizimu, dooh kumbe mzimu wa mama yangu mzazi ulichachamaa na ukakasilika sana ukamfata mama yangu wa kambo usiku huohuo kumtesa zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama yangu wa kambo alihisi nikiondoka pale nyumbani basi ataendelea kuishi bila wasiwasi, kumbe mzimu wa mama yangu ulichukia kile kitendo alichonisingizia mpaka nikafukuzwa na bosi wangu nikaenda  kuteseka mitaani, tena chakushangaza nikafukuzwa nyakati za usiku nyumbani kitendo kilicho niliza maana nilikuwa sijafanya kosa mimi, mama yangu wa kambo aliendelea kusumbuka sana nyakati za usiku pia kwa kutokelewa na mzimu wa mama yangu mzazi tena mzimu ukiwa umevaa sanda yake nyeupe, hichi kitendo kilicho mkwazisha sana bosi pale nyumbani, maana mama wa kambo alikuwa ni mtu wa kupiga kelele usiku akiteswa na mama tu tena alikuwa  akijiviringisha kama nyoka uku akiongea maneno yasiyo eleweka kabisa yani, Mimi niliendelea kupata shida sana mtaani ila nashukuru mungu nilijitahidi kupambana mchana kutafuta pesa ya kula tu.



    Mungu saidia nikapata sehemu ya kulala usiku, ambapo ni kwenye magari ya daradara yalipokuwa yanapaki nyakati za usiku mimibaada ya shughuri zangu za mchana nilikuwa nikilala ndani ya gari na nilikuwa nikiamka saa 10 alfajiri kuendelea na kazi zangu ndogondogo tu.



    Baada ya mama wa kambo kuona nimetoka pale na matatizo yake ndiyo yakawa yanazidi kuongezeka, akaona ni bora akawambie wale washirikina wenzake ili wamsaidie maana alikuwa kaisha choka yale maisha sana, ikafika hatua akatamani kufa kabisa, na kweli maana alikuwa anakonda tu yani, yeye baada ya kunenepa anapungua. Washirikina Wenzake walimwambia kuwa “tunajua tulikwambia kuwa yule kijana aondoke na aliondoka sawa, lakini bahati mbaya alipigwa na panga mgongoni alivto toka pale kwa bosi wake, hivyo damu zikamtoka, ndiyo maana mzimu wa mama yake umechachamaaa na umekasilika sana maana uchungu wa mwana aujuae mzazi, na siku zote hii mizimu uwa inanguvu sana kutushinda sisi,



    Sasa unatakiwa kufanya kafara moja kubwa sana itakayo nusuru maisha yako yote na hautakuja kuteseka tena kamwe” mama akawauliza “kafara gani tena?” wakamjibu kuwa “unapaswa uondoe uhai wa bosi wako maana damu yake ikidondoka tu basi mizimu yetu itakulinda kama mfalme” mama yangu wa kambo hakuamini ujue akasema “yani hawa wachache tu nilio waua wananitesa hivi je akiongeza mwingine nikaua si nitateseka sana na mizimu yao ” dooh walimwambia kuwa  “kama uwezi kumuua acha lakini ukifanya hivyo utakuwa safi na utakuwa na amani kama sisi” dah mama yangu wa kambo akauliza “sasa naanzaje kumuua huyu bosi wangu jamani wakati ananisaidia na ananipenda sana isitoshe nimeishi nae vizuri na ananisikiliza sana mimi” walimwambia “usipo muua huyo utateseka maisha yako yote ya usiku na unatakiwa kufanya hivyo mapema kabla nyota yake haija mfungulia nuru ya kuhisi kuna baya lolote mbele yake” ndipo mama yangu wa kambo akaambiwa “unatakiwa kwenda chumbani kwa bosi wako mida ya saa tisa usiku, akiwa amelala sana, bila kuona wala kusikia chochote, kisha chukua nguo yake ya ndani yenye langi nyeusi alafu tuletee sisi tutajua cha kufanya” mama akashtuka akasema “jamani nguo ya ndani naona itakuwa ngumu maana mtamuua vibaya jamani nampenda yule bosi amenisaidia sana mimi” walimwambia kuwa “kafara nzuri nikwa mtu unae mpenda ndiyo yapaswa kumtoa kafara” mama yangu wa kambo hakuwa na jinsi aliamua kukubali tu maana hakuwa na cha kujitetea, ilipo fika saa tisa usiku akaenda kwa kunyatia  polepole ili aingie chumbani kwa bosi wake.



    Alipo chungulia mlangoni bosi wake akamkuta bosi anaongea bado na simu usiku! dah mama wa kambo akachukia kweli siku hiyo, kesho yake akafanya hivyo hivyo akaenda chumbani kwa bosi wake, tena  ileile mida ya saa tisa usiku. Alipo chungulia akakuta bosi wake amelala sana jamani akasukuma mlango wake polepole kisha akaingia akinyata taratibu ili akachukue ile nguo ya ndani nyeusi ya bosi wake kama alivyo ambiwa  apeleke waweze kumtoa bosi kafara. Kipindi ameingia ndani anafungua kabati alisikia mtu anakuja kumbe alikuwa ni mtoto wa yule mama anakuja kwa mama yake kuazima computer aina ya laptop ili aka andike kazi zake za shuleni. Kipindi mama wa kambo kaisha ishika ile nguo ya ndani ya yule bosi wake mlango ukafunguliwa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Dooh yule dada alipo fungua kabla hajaingia ndani vizuri kumfuma mama  akasikia  simu yake inaitia chumbani kwake akaacha kuingia ndani akarudi chumbani kwake kuipokea simu yake, ndipo mda huohuo mama yangu akatoka ameishika nguo ya bosi wake akiwa anataka kuipeleka kwa wale washirikina wenzake. Kulipo kucha yule bosi alikuwa amepanga kuvaa ileile nguo ya ndani lakini alishangaa hakuiona sehemu aliyo iweka ila akaachana nayo akihisi labda nguo zimechanganyikana humo ndani, ndipo mama yangu wa kambo akapeleka ile nguo mpaka sehemu usika ya wachawi. Kweli walianza kumfanyia vitu vya ajabu bosi kwa kutumia ile nguo yake jamani, bosi wangu alianza kupata hedhi isiyo kuwa na kikomo, mda mwingine tumbo lilimuuma sana ndani akawa analia kama mtoto mchanga kabisa, bosi akaamua kuacha kazi zake kwanza ili atazame afya yake itakuwaje, binti yake alikuwa analia sana pia maana mama yake aliacha  kazi sababu ya ugonjwa, maana tumbo lilikuwa linamuua kiasi ambacho alikuwa anashindwa kulielezea masikini.



    Ilifika hatua ikabidi amwambie yule rafiki yake wastara kuhusu tatizo lake dooh wastara aliumia sana maana walikuwa wanapendana sana, ikabidi bosi apelekwe hospital ili waangalie tatizo lake nini, wataharamu walishindwa kuutambua ugonjwa kabisa, dooh bosi aliogopa sana na alikuwa analia sana hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi alikaa siku saba  bila kula alafu akawa mzito sana kama jiwe yani kumnyanyua ni ngumu sana na ngozi yake ikawa laini kama vile nyoka. Wastara alilia sana tena alilia kama mtoto maana mtu wake wa karibu alikuwa ni yule bosi na ndiye alikuwa shoga yake wa karibu, hivyo alikosa sana raha masikini.baada siku tisa tangu alazwe hospitali wastara akaona kwamba akizubaa anampoteza rafiki yake maana tayari alikuwa kaisha anza kulishwa kwa milija, na bosi alikiwa aongei zaidi ya kufumbua macho kwanguvu sana akikodoa mpaka anatisha jamani. Kumbe hivyo vyote vilikuwa ni viini macho tu yani kumbe bosi ameisha chukuliwa na mizimu na wachawi wasubilia tu kumla nyama yake siku ya ijumaa. Ilipo fika alhamisi kabla ya ijumaa ili bosi aliwe nyama yake.



    Wastara aliota usiku kuwa bosi atakuwa amelogwa na wachawi maana ule ugongwa haukuwa wa kawaida, wastara alijiuliza maswali mengi kichwani kwamba, Hivi rafiki yangu atakuwa kachezewa na wafanyakazi wenzake ili afilisike au? Au majirani zake watakuwa wanamuonea wivu? Au ni huyu mfanyakazi wake? maana namuhisi vibaya sana huyo mtu! Wastara akasema lazima ninusuru maisha ya rafiki yangu “siwezi kumuacha afariki nikimtazama” wastara aliyasema maneno haya akiwa anatokwa na machozi masikini.



    Ndipo wastara akaamua kutafuta viongozi wa kidini ili wamfanyie maombi rafiki yake. Siku hiyo wakati anafanyiwa maombi ilikuwa ni alihamisi na ijumaa yake wastara angechelewa ndiyo alikuwa analiwa nyama yake. Bosi Alifanyiwa maombi sana, wastara alifunga, hakula chakula siku hiyo kwajili ya kumuomba mungu asaidie shoga yake apone. Maombi yalifanyika sana siku hiyo kipindi inafika jioni wakati wamefanya maombi sana bila kuona mafanikio walishangaa kuona, ghafla bosi anaamka akilitaja jina la rafiki yake  akisema, ‘wastara” na alilisema lile jina kwa unyonge sana maana alikuwa ananjaa.wale viongozi wa dini walisema kwamba chanzo kilikuwa ni nguo yake ya ndani na ilikuwa imebaki siku moja aliwe nyama yake.



    Hivyo wewe dada wastara usinge muhusisha mungu kwenye hili swala basi ungempoteza mwenzako. Wastara akawauliza sasa nguo yake ya ndani alifanyajefanyaje. Walimjibu kuwa mfanyakazi wake wa ndani ndiye alie chukua ile nguo akawapelekea wale wachawi ili huyu bosi wake afe kusudi mizimu ya watu alio waondoa maisha isimtese. Wastara alimwambia bosi unaona sasa nilikwambia hakufai huyu binti ukamgombania sana,tazama alichofanya yani kidogo ufe



    tusinge kuona tena jamani” mama yangu wa kambo baada ya kugundulika dooh ndipo….

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama wa kambo alipo gundulika kuwa alifanya mambo ya kishirikina kutaka kuondoa uhai wa bosi wake, kwa kuiba nguo ya ndani ya bosi wake yenye rangi nyeusi ili kumpandikizia kichawi magonjwa bosi wake, badae afe na mwili wake ubebwe kimizimu! Ndipo  Mama wa kambo aliamua kutoroka nyumbani maana alijua bosi wake kaisha mjua hivyo anaweza kumfanyia kitu kibaya sana. Bosi biashara zake ziliyumba sana maana alilazwa kwa mda mrefu na mambo yake ya kikazi pia yaka kwama, ila alijipanga upya na akafanya kazi zake zikapendeza zaidi, Bosi alimshukuru sana wastara akamwambia kuwa “kweli wewe ndiye rafiki wa kweli maana umeokoa maisha yangu sana” Na akamnunulia zawadi ya gari ishara ya furaha kuwa kamkomboa maisha yake. Mama wa kambo kipindi yupo mtaani hana mbele wala nyuma, hajui atakula nini na atakaa wapi jamani alianza kulia sana akisema “nilipata nafasi nzuri kwa bosi wangu nimeichezea kwa roho yangu mbaya hii, sijui nakaa wapi tena mimi” alishinda pale chini ya gogo akiwaza maana hakujua atalala wapi, ataoga wapi, na sehemu ya kula hakuwa nayo maana ata nguo aliziacha kwa bosi wake na ata mshahara hakuuchukua 

0 comments:

Post a Comment

Blog