Search This Blog

DAMU YA BABA - 3

 







    Simulizi : Damu Ya Baba

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Mama,,akasema rafiki yangu mimi nina wazo moja, Ebu angalia dunia ya sasa ilivyo chafuka! Yani namaanisha kuwa  sisi wote tayari ni waathirika wa virusi vya ukimwi, kwanini tusifanye biashara isiyo itaji mtaji mkubwa yani kujirembua, kuvaa na kupendeza usiku.

    Dada,,nini? Yani unamaanisha tujiuze au?

    Mama,,ndiyo!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    maana tayali sisi tumeisha pata maambukizi inatupasa tule na tuishi kwa furaha ili tuishi maisha marefu.

    Dada,,hapana rafiki! mimi nimesoma lazima nitumie elimu yangu kuchanganua mambo, kujiuza sio biashara nzuri ata kama ina pesa bora tu tufe njaa humu ndani.

    Mama,, basi sawa kama umeamua hivyo

    Dada,,poa rafiki.

    Mama,,lakini best mimi haya maisha nayajua yameisha nipiga sana tutafute njia nyingine angalau nyepes

    Dada,,njia gani rafiki yangu.

    Mama,,rafik mungu katujalia wote makalio makubwa! je unaweza kucheza muziki?

    Dada,, ndiyo naweza!

    Mama akasema, sasa sikia rafiki yangu kuna bar moja kubwa sana ina matajili wa kila aina

    sisi tutakuwa tunaenda bar wakiwa mezani wanakunywa tukifika tunawakalia wanaume juu kisha tunaanza kukatika makalio yetu juu ya mapaja yao!

    wakisha pata hisia tunarembua macho kisha tunawaomba hela huku tukishikashika vifua vyao vizuri kimahaba.



    Yule dada aliamua kukubaliana na mawazo ya mama wa kambo akasema “sawa shoga yangu tutajaribu tu ila naona haibu sana kufanya hiyo kazi, maana kukatikia wanaume wakiwa wanakunywa vinywaji baani mi naona ni aibu sana”Mama akamwambia “acha tabia za aibu usiku nani anakujua wewe tufanye hii kazi tukipata pesa tunaacha”Ndipo wakaanza kujipanga kwenye mavazi na kununua nguo za utupu ili wakianza kazi waweze kuvutia wanaume wengi wakiwa kazini.Mama alinunua nguo za kuachia mapaja yao wazi na zingine za kuonyesha vitovu vyao na maziwa yao kubinuka pia.



    Ilipo fika jioni kipindi yule dada kajisahau, mama akamwambia, “shoga yangu mda umefika kaoge tuondoke zetu kazini”Wote wakajiandaa lakini wakaona aibu kuvaa zile nguo palepale nyumbani, maana zilikuwa za aibu sana na walikuwa hawajazoeleka kuvaa hivyo.Hivyo zile nguo wakazibeba kwenye mifuko ya plasitiki. Walipofika kwenye ile baa wakaenda nyuma na magari yalipo pakiwa kisha wakabadilisha nguo, mama alikuwa kavaa nguo za utupu sana mpaka yule dada akaona aibu akasema “mimi sijafundishwa kuvaa hivi nimehairisha kufanya hii kazi fanya peke yako”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    mama kidogo amumeze mzima mzima akamwambia “tutakosana sana usipo vaa, yani tufike hapa afu nifanye kazi mwenyewe na tumenunua nguo kwa pesa” ndipo yule dada pia akavaa nguo!



    Mama akamwambia “rafiki yangu umependeza sana ebu angalia ilo guu lako la bia tazama makalio yako pia lazima tupige pesa umo ndani” yule dada aliguna tu maana akuwa na jinsi ila mama alimwambia “ukiwa mule uwe shapu shapu usizubae nakuomba”



    Walipo ingia walionekana wapya pale maana wazamani walikuwa wameisha zoeleka, mama alikuwa aogopi alienda kwa mwanaume wa kwanza akamzungushia kiuno chake akilishika shingo la yule baba! alivyo anza kuzabaa mama yangu wa kambo akamlembulia macho kisha akamwambia”jamani mpenzi naomba hela ya bia” kisha akambusu yule baba alikuwa na kitambi akachukua waleti yake kisha akamchomolea elfu hamsini akampatia mama alifurahi sana kisha akaanza kumchezea akikatikia makalio juu yake yule baba kanogewa mama akaamka na kuondoka na kwenda kwa mwanaume mwingine.



    Dah Yule dada pia alishangaa kuona mama anapewa hela, akatamani na yeye apate japo hela kiasi ndipo…



    Yule dada alijikaza akamfata baba mmoja kisha akamwambia “kaka mimi naweza kucheza” yule baba akacheka kwa tabasamu akasema “naona una umbo zuri la kucheza, basi cheza nione” ndipo yule dada akapanda juu yake kisha akashika meza akaanza kucheza juu yake maana mule baa kulikuwa na redio kubwa sana hivyo muziki mda wote unaimba tu. Kipindi yule kaka anafurahia kuchezewa juu ndipo yule dada akamwambia “naomba hela ya bia mpenzi”yule baba akasema nimeacha pesa zote nje kwenye gari langu hivyo naomba twende nikakupe, kipindi hicho mama yangu wa kambo yupo upande mwingine anacheza na wababa,wazee,vijana waliopo mule bar,



    hivyo yule dada hakuwa wa wasiwasi maana aliona mwenzake anapata tu pesa akakubali kwenda kwenye gari nje.



    Walipo fika kwenye gari waliingia ndani yule kaka akabadilisha kauli kisha akafunga na kuloki milango na madilisha ya gari lake, wakawa wawili tu mule ndani ndipo akamwambia “we dada nimependa sana mwili wako hivyo ili nikupe pesa naomba kiustahalabu vua nguo zako tufanye mapenzi” dada alianza kulia akasema mimi nimekuja kucheza muziki sio kujiuza yule kaka akatoa bastola yake kisha akasema usipo vua nakuua mzima mzima! Yule dada alipo ona bastola akaona bora afanye kuliko kufa ndipo akamwambia “kaka mimi nimeathirika sitaki kukuathiri na wewe” yule kaka akasema hapana sitaki kujua!



    Masikini yule dada akavua nguo na kulala kwenye viti vya nyuma yule kaka akafanya yake kisha akampa yule dada elfu 60 na akamwambia amefurahia ushirikiano wake.



    Yule dada alivyo pata pesa akafurahi sana maana alihisi anaweza kuibiwa akavaa nguo na kurudi ndani akarudia tena kuwachezea watu kama mwenzake walipo rudi nyumbani walishangaa sana maana mama yangu wa kambo alikuwa na laki mbili na nusu na yule dada akawa na laki moja na sitini.



    Yule dada alifurahi akasema “best mala ya kwanza nilikuwa na idharau hii biashara ila nimeipenda sana inalipa naomba kesho tena twende” mama akamwambia “mimi nilikwambia ukawa unachukulia masiala”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kesho yake pia wakarudi palepale wakiwa wamependeza sana zaidi ya jana kila mtu akiwa mzoefu sasa hakuna wa kumtazama mwenzake



    Mama aliendelea kama alivyo zoea, ila yule dada akaenda upande wake pia………..



    Kipindi mama yangu wa kambo na yule dada wanafanya kazi zao mule baa, mama alienda kwa baba mmoja hivi umli wake mkubwa tu,



    mama akaanza  kufanya kazi yake kama alivyo zoea,



    kiukweli yule baba alikuwa hajitambui kabisa jamani maana alikuwa amekunywa pombe sana, hata hivyo kipindi mama yangu wa kambo yupo juu yake akikata mauno ili baadae amrembulie macho kisha amuombe pesa ya bia yule baba alifurahia sana kukatikiwa huku akisema, “asante mke wangu unacheza vizuri leo zaidi ya siku zote tangu nikuoe”



    Mama akamwambia “asante mme wangu naomba hela ya bia mpenzi”



    Wakati huo yule dada rafiki yake mama alikuwa hajapata mtu maana karibia wanaume wote walikuwa wameisha palamiwa na wakinadada mule baa



    ila kwenye ile baa kulikuwa na baba mmoja hivi kutoka nchi za kigeni “mzungu”. sasa wale wa dada mule ndani waliogopa kumfata mzungu ili kumuomba pesa maana waliogopa kuongea nae lugha ya kiingereza!



    Lakini yule dada rafiki wa mama alikuwa kasoma na alikuwa na elimu tu ingawa alikuwa hapati kazi!  hivyo akatumia elimu yake kuongea na yule mzungu.



    Dada Alifika akamwambia kwa kiingereza,”naomba tucheze” huku akimsogelea sehemu aliyo kaa akapanda juu ya yule mzungu na kuanza kucheza muziki, mzungu alikuwa anacheka kwa furaha huku akisema “una mwili mzuri msichana wa kiafrika! unaitwa nani?”



    yule dada alimjibu lugha vizuri na wakaelewana sana na yule mzungu akatokea kumpenda dada! alimuelezea yule dada hisia zake kisha akamwambia wataondoka kutoka tanzania wakaishi wote”Germany”yule dada alikubali kwa moyo mmoja na wakatoka wote baa kwenda kulala.



    Mda huo Mama yangu wa kambo anaendelea kukata mauno yake juu ya yule baba huku akisema “naomba pesa ya bia”



    yule baba akasema “nakupa pesa mke wangu usijali”



    Kipindi yule baba anatoa pesa kwenye waleti yake! Kumbe mke wake alikuwa ametoka nje kidogo kuongea na simu! Hakuamini kukuta mme wake amebeba mwanamke juu yake, Akamwambia”Mme wangu jamani yani nimetoka nje kidogo tu umeanza kushikana na awa malaya wa hapa bar” mme wake hakujibu maana alikuwa amelewa sana haelewi kabisa.Yule mama akachukua chupa ya bia kisha akampiga kichwani mama yangu wa kambo kipindi mama anaamka yule mama akamchana na chupa usoni.



    Mama alichanika shavu lake maana alichanwa na kipande cha chupa cha ile bia aliyo pigwa nayo kichwani,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    mama alijikaza akiwa kajaa damu mwili mzima kisha akakimbia mpaka alipo kuwa anaishi na rafiki yake.Mama yangu wa kambo Alipo fika hakumkuta rafiki yake maana aliitaji msaada japo wa kuoshwa zile damu maana zilikuwa zinamtoka sana jamani.Mama alilia akisema, “besti yangu uko wapi nimepigwa sana natoka damu jamani nisaidie”



    Na mda huo nyama za shavuni zilikuwa zimenin’ginia maana zilichanwa na chupa



    hivyo aliitajika kuwaishwa hospitali ziweze kushonwa ili apone kidonda masikini.Lakini bahati mbaya rafiki yake mama yangu wa kambo alikuwa hayupo, alikuwa kwa yule mzungu wake wakijivinjali usiku huo maana yule mzungu alimpenda sana na alikuwa kaisha amua kumpeleka yule dada nchini “Germany” kufunga nae ndoa kabisa.Mama yangu wa kambo alilia usiku huo sana alisikia maumivu sana mpaka akapoteza fahamu kabisa,



    kipindi mama anazinduka na kupata fahamu akakuta vijana wawili wakubwa sana wamekuja ndani mwake.



    Wakiwa wameshika panga, mama aliogopa sana kuwaona wale watu usiku ule maana walikuwa wanaume na walikuwa na silaa na hakukua na mtu wa kumsaidia mama usiku ule.Kumbe wale vijana walikuwa wametumwa na yule mwanamke aliye mkuta mama anakatika juu ya mmewe baa.



    Alibakwa na wale vijana kisha wakamvua nguo ya juu na kumvua sidiria yake! mama akasema kwanini mnanifanya hivi.



    Walimfunga mikono na miguu kisha wakamkata matiti yake na kuyaweka kwenye ndoo alafu wakapanda pikipiki na kuondoka usiku huohuo mida ya saa nane na nusu.Mama alipatwa na maumivu sana maana matiti yake yote yalikatwa jamani,alilia mpaka sauti ikakauka.



    Rafiki yake mama alipo kuja mida ya asubui akiwa amebeba pesa aina ya Dola alizo pewa na mpenzi wake wa kizungu.



    Alishangaa kukuta damu mlangoni kidogo akimbie alivyo ingia ndani akakuta mama anapumua ya mwisho mwisho. Alimpeleka hosipital mda huohuo ili asiweze kupoteza maisha yake.



    Alipo fika hospital alipokelewa vizuri lakini dakitari alisema “hali ya mama mbaya sana hivyo inaitajika pesa nyingi sana ili aweze kupona, maana amekatwa matiti na pia amechanika shavu lake na amepigwa na chupa imemchana nyama kichwani.”





    Kipindi kile dokta anamueleza yule dada hali ya mama yangu wa kambo, mama alikuwa na hali mbaya sana iliyo muogopesha kila mtu aliye kuwa mahali pale ata wagonjwa wengine walipata na nafuu kabisa baada ya kumuona mama katika hali ile, maana walijiona hawaumwi kabisa sababu matiti ya mama yalikuwa yamekatwa yani ni damu tu zilikuwa zinatoka, na damu zilipungua kumtililika mama baada ya kupata huduma ya kwanza, Doctor akamuuliza yule dada kuwa “kama mnaweza kulipa hizo gharama zote zilizopo kwenye hiyo risti basi tuanze matibabu ili ndugu yenu asipoteze maisha”.Mama alianza kulia akisema”eh mungu wangu nimetesa watu wengi sana wasio na atia na wanyonge, nimekualibia ndoa yako mpaka mmeo kupoteza maisha yake jamani. Rafiki yangu wewe ondoka tu niache nife sina thamani tena maana urembo wangu umeisha potea,tazama shavu langu vilevile maziwa yangu hamna tena nitakuwa mgeni wa nani mimi”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Yule dada alikumbuka jinsi mama alivyo mualibia ndoa yake akasababisha akafungwa akasababisha mpaka mme wake kujiua”Dada akasema”rafiki yangu umenifanyia mambo  mabaya sana lakini siwezi kukutupa”Yule dada akamwambia doctor naomba atibiwe pesa nitalipa Mama akamuuliza wewe utalipaje hela umetoa wapi hizo milioni za pesa mimi kutibiwaYule dada akasema doctor wewe mtibu tu apone pesa ninayo.Mama alianza kutibiwa.



    kipindi yupo anatibiwa yule dada akamfata mzungu wake na kumuelezea hali ya rafiki yake.Yule mzungu akamuonea  sana mama huruma kisha akasema atalipa pesa zote hizo za matibabu maana yule dada alimtetea sana mama kuwa ni mtu mwema na ni kama ndugu yake.Kipindi mama anapata matibabu alihudumiwa vizuri mpaka akaanza kupata nafuu,Kumbe yule mzungu na mama yangu mlezi (mama Danieli) walikuwa marafiki!Na yule mzungu alikuwa akija afrika ili kufanya biashala na mama daniel maana wote walikuwa wafanya biashala.Yule mzungu akamtambulisha yule dada kwa mama danieli kuwa ndiyo mke wake! yule dada na mama Daniel wakaanza kuitana wifi.siku moja ikabidi mama yangu mlezi, yule dada, pamoja na mzungu waende hospital kumjulia hali mama yangu wa kambo, na wakati huo mimi sina taarifa kama mama danieli anaekwenda  kumuangalia hospitari ni mama yangu wa kambo jamani.



    Mama Danieli na wenzake walipo fika hospitalini walimuonea huruma sana mama yangu wa kambo maana alikuwa katika hali mbaya sana kiafya.



    Mama danieli alipo mtazama vizuri mama akakuta kawekewa bandeji hivyo akauliza “hii bandeji kwenye maziwa niyanini” Alijibiwa na yule dada kuwa “Wifi hata hivyo hakukatwa shavu peke yake bali alikatwa na maziwa pia” mzungu akauliza kwamba



    “jamani ongeeni kingeleza na mimi nielewe”



    alielezewa pia  ila alimuonea huruma sana mama,



    Kipindi dada anaanza kukauka vidonda vyake na kuanza kuwa salama kiasi doctor alimuruhusu aende nyumbani akamalizie dawa ili awe salama zaid,



    Na siku hiyo hiyo yule mzungu alikuwa anarudi kwao Germany na alikuwa anaondoka na yule dada.



    Mama yangu wa kambo alipo sikia zile taarifa akaanza kulia huku akisema “jamani best yangu wewe ukienda kuolewa uko na mme wako huyo mzungu mimi nitaishi vipi jamani sina msaada wowote mimi”



    Yule dada akamwambia “kwa sasa siwezi kubaki maana kila mtu ameisha juwa, nimewaaga watu wangu wote kuwa naenda germany kwa mme wangu sasa kubaki siwezi”Kipindi wanazozana pale mama akasema ile kazi siifanyi tena manusra iniue, yule dada akasema hii kazi imenipatisha mume,tena mume wa kizungu ila siifanyi tena,



    Yule dada akamuuliza mama “sasa ukitoka hapa utafanya kazi gani ndugu yangu maana ata kazi sahivi ngumu kupata”Mama akamjibu kuwa “nitafanya kazi yoyote ile atakama ni kazi za ndani nipo tayali kufanya”Mama aliposema kuwa ata kazi za ndani anaweza kufanya, mama danieli alikuwepo pale akasema “we dada kama kazi za ndani unaweza kufanya basi usijali mimi nilikuwa natafuta mfanyakazi wa ndani! kama upo tayari tukitoka hapa hospitari twende moja kwa moja mpaka kwangu”.



    Yule dada alijiandaa jioni yake akaenda na mmewe uwanja wa ndege akasafili kuolewa kabisa na mmewe na akaishi maisha mazuri sana kule.Mama yangu wa kambo akachukuliwa na mama yangu mlezi (mama danieli) kisha akamleta  nyumbani ili awe mfanyakazi wetu wa ndani.



    Kipindi anafika nyumbani alipokelewa na mdogo wangu wa kike,



    Wakati mimi natoka chumbani kwangu nakuja sebreni ili nimuone mgeni.Dooh! Nilishangaa kumuona mke wa baba pale kama mfanyakazi niliogopa maana nilikuwa najua ni mchawi na……



    Nilishangaa sana kumuona mke wa baba kwamba ndiyo mfanyakazi wetu wa kazi za ndani, sikutegemea, niliogopa na kushituka kidogo maana nilikuwa namjua mama vizuri yani kwamba baba alikuwa akimpa pesa na alikuwa akipendeza sana na anachukua vijana wa aina yoyote atakayo kwa pesa zake, Na nilimjua kuwa ni mchawi na niliumia sana maana ndiye alie sababisha mama yangu afukuzwe nyumbani na akafa jamani.kibaya zaidi ndiye alie sababisha mpaka nikapelekwa na baba polisi kufungwa! huyuhuyu mama ndiye alifanya mpaka nisimzike mama kipindi amefariki, nilijikaza kwa yote ila nilipo jitazama katika mkono wangu nikakumbuka alama ya marehemu mke wa hans alie taka kumchoma mama kisu tumboni sababu alimfumania na mmewe ila mimi nikakinga mkono wangu ili mama asife, Nilikumbuka jinsi nilivyo kuwa nikinkuta mama yangu wa kambo na wanaume ndani baba akiwa hayupo! Yani sikutamani ata kumuona lakini nilishangaa kumtazama alivyo alibika sura yake maana alikuwa ana makovu  usoni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama alionyesha sura ya huruma sana ali kadharika alionyesha kunywea sana pale sebureni mpaka nikamuonea huruma ata sikutaka kusema chochote kibaya kuhusu yeye kwa mama danieli.



    Kipindi mama daniel ameenda chumbani kwake kulala ikabidi nimfate mama wa kambo chumbani, nikamuuliza.



    Mama baba yuko wapi? Alafu mbona upo hivyo umechoka sana na umekuwa mbaya sana sahivi? Na kwanini ufanye hizi kazi? Alafu kwanini nyumba yetu imeungua nilikuta imebomokabomoka? Na imekuwajekuwaje umefikia hatua yakufanya hii kazi?



    Mama wa kambo alinisimulia kila kitu maana nilimuonya asipo niambia ukweli namsemea kwa mama danieli ili afukuzwe kazi



    Alipo nielezea ndipo nikapata kujua historia yote kuhusu (damu ya baba)



    Sikuwa na kinyongo nae maana nilimuonea huruma hivyo nikamuacha aishi pale pale nyumbani.



    Siku za kwanza mama alikuwa akipika chakula kitamu! Alikuwa akifanya kazi zote vizuri mpaka mama dani akampenda sana akaanza kumtunza kama mdogo wake akimpa pesa ya nguo na matumizi yote,



    mama alivyo anza kupendeza upya ndipo akapata roho ya kutu tena, akataka kuniua mimi pamoja na mama dani! ili abaki yeye pale nyumbani maana mama dani hakuwa na mme wala ndugu, hivyo mama alitaka kumiliki zile mali mwenyewe jamani! Ndipo…



    Mama yangu wa kambo akukumbuka fadhila na mazuri yote aliyo tendewa na mama Danieli, Alitamani amuondoe mama dani duniani ili yeye abaki kuwa mumiliki wa mali zote zile nyumbani, Maana mama dani alikuwa na nyumba kubwa yenye ghorofa moja, mbele ya nyumba alikuwa na fulemu za maduka tisa na pili alikuwa na magari ya kifahali sana jamani.



    Siku moja usiku kipindi mama wa kambo anapika chakula mdogo wangu wa kike alimuona akiwa anatoa dawa kwenye fundo la kanga kisha akanyunyizia kwenye chakula.



    Mdogo wangu hakuniambia kama kaona sumu inawekwa bali alikimwaga kile chakula chote chini, Mama dani alimgombeza sana “kwanini unatulaza njaa sisi? yani unamwaga chakula makusidi kabisa, nahisi utakuwa na maleria kesho nakupeleka hospitari”



    Mdogo wangu alikuwa mkimya kama marehemu mama hivyo hakusema chochote.



    Baada ya mama wa kambo kufeli mpango wake wa kwanza, ndipo sasa akamfata yule ndugu yake ambaye baba alimuona usiku kule makabulini na wachawi wenzake wakimfufua Zabroni ili awe mwenzao,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Yule ndugu yake alimlaumu sana mama kwanini kakaa kimya siku zote zile.



    Ila alimkubalia ombi lake la kumpa dawa za kishirikina ili aweze kuteketeza familia yetu yani mimi, mdogo wangu wa kike na mama danieli.



    Mama yangu wa kambo alimfanya kitu kibaya sana mama danieli



    Ilikuwa ni jumamosi mama danieli akiwa amepata wateja kutoka Germany hivyo akataka kumuachia pesa za matumizi mama ili aweze kusimamia kila kitu pale nyumbani kipindi mama daniel anatoka chumbani kwake kumpelekea pesa mama!



    Kipindi anavuka mlango wake tu aliangua chini vibaya sana  mama danieli! mimi nilikuwa naoga lakini nilikisikia kile kishindo.



    Kumbe mama alikuwa ametega dawa pale mlangoni.



    Nilimpeleka mama hospitali huku mama wa kambo anajifanya analia kumbe yeye ndiye mchawi.



    Mama dani mguu wake ulianza kuvimba  ulitanuka sana ukajaa maji na kuweka mikato mikato mingi, Docta akasema ile ni kansa! hivyo mama akaambiwa akatwe mguu, doh alikataa akasema nikikatwa miguu biashala zangu zitakufa zote jamani,Ikabidi arudi nyumbani maana alikataa kukatwa kabisa, mguu uliendelea kuharibika sana alianza kuoza mguu wake! mimi nilisikitika sana pale nilipo waona wadudu aina ya funza kwenye mguu wa mama dani nililia sana …



    Hali ya mama danieli iliendelea kutisha ata kila aliye kuja kumtazama alijua lazima afe tu, mama yangu wa kambo alionyesha tabasamu la kinafiki ili tujue na yeye kaumia kumbe ndiye chonzo kikuu.  Mguu uliendelea kuonyesha kuwa hauwezi kupona tena na mama danieli alikataa, akasema, “hii sio kansa maana kwetu hamna huu ugonjwa, vilevile  nikitu cha ghafla sana kwahiyo siwezi katwa”, Mimi umri wangu ulikiwa umeenda pia maana nilikuwa na miaka 22 hivyo nikajiongeza palepale nikamfata mganga wa kienyeji aje kumsaidia, ila wote tulishangaa sana! mganga alizidiwa nguvu kabisa akasema awezi kutibu na akasema mama dani awezi kupona! Nilihisi anatania ndipo nikawaita mashee, mapadri na wachungaji wa kilokole! Ila wote walikata nao tamaa kabisa.



    Mama danieli aliendelea kuwaza sana chakushangaza, mama dani Akaanza kutoa harufu ya kuoza, mule ndani kukawa kunanuka sana hivyo ata wageni wakaacha kuja.



    Ilipo fika usiku mida ya saa tisa nikiwa nimelala tu nawaza nikilia maana nilikuwa nampenda sana mama dani jamani! Mzimu wa marehemu mama yangu ulinitokea ukiwa umevaa nguo nyeupe sana niliogopa maana sikuamini na nilishangaa sana.



    Ukaniambia, “mama danieli amelogwa na mama yako wa kambo, na mama yako alimtegea dawa mlangoni kwake ili akivuka tu aweze kuugua, hata na nyie mpo hatarini sana hivyo nakuomba mwanangu nenda juu ya kaburi langu chukua mchanga wa kaburi langu juu  kisha njoo umwagie mama danieli kila alipo patwa na tatizo mwilini mwake! ukifanya hivyo atapona mda huohuo! usichelewe unatakiwa kufanya hivyo kabla ya saa moja asubui kesho hivyo amka sahivi kisha nenda!”



    Nilimwambia kuwa



    “Mama kaburi lako silijui”, “nenda nitakuelekeza mwanangu”



    Niliamka haraka haraka kumbe mama wa kambo alisikia kila kitu!



    Ndipo akaanza kuniweka vipingamizi vingi ili nisifike makabulini.



    Kipindi nafungua mlango taratibu mida ya saa tisa kukiwa na giza sana,dooh nilishangaa sana kuona paka mweusi sana mlangoni akiwa analia kama mtoto mchanga! nilishika jiwe kisha nikamponda ili akimbie aache kutulilia!



    kumbe hakuwa paka ila ni mama wa kambo anafanya mambo yake



    Nilipo mponda tu paka sauti yangu ikapotea ghafla, miguu yangu na mikono ikaishiwa nguvu nikashindwa ata kwenda makabulini…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Niliishiwa nguvu sana na nilishindwa ata kupiga kelele ili mdogo wangu aje kunisaidia maana kipinda namponda yule paka nilisema “TOKA HAPA” ndipo sauti yangu pia iligoma kutoka hivyo nikalala pale pale nje nikiwa sina nguvu ata ya kuingia ndani wala kuwaita watu wanitoe nje, mzimu wa mama ulishindwa kunisaidia pia maana wale wachawi walikuwa na nguvu sana hivyo mama angeingilia tu na yeye ange hadhibiwa.



    mda ulikuwa inaenda sana kufika saa moja mda wa mama dani kufariki!



    Mama wa watu alilia sana akaomba mungu ampe nguvu tena japo amalizie kutusomesha tu ila ndiyo alikuwa anaendelea kuharibika mwili mzima, mama danieli alioza mpaka sura yake ikawa aitambuliki



    mule ndani kwetu n’zi walijaa sana hakukua ata na uafadhali.



    Ilipo fika saa moja kamili mama danieli alipoteza uhai wake jamani, macho yake yakawa ya bluu sana! mda huohuo na mimi nikapata nguvu zangu zote ghafla na sauti yangu ikarudi kama zamani.



    Dah nililia sana maana mama danieli alikuwa kanisomesha mpaka chuo hivyo nilikuwa nimebakiza mwaka mmoja tu kumaliza masikini.



    Tatizo likaja kwenye kumzika sasa! maana ata kumtoa ndani ilikuwa ni shida,  Alikuwa ananuka sana mama wawatu.



    Mama wa kambo akawa asaidii chochote ndipo mimi nikaenda kituo cha polisi kulipoti ili serikari iweze kutusaidia kumzika mama dani sababu mama dani pia alikuwa hana ndugu yoyote tofauti na mama yake kijijini, ila na mama yake alikuwa mzee sana, maana mama dani alikuwa mtoto wa mwisho kwao kuzaliwa.



    Serikari ilimzika mama danieli jaman ila tuliumia sana ata majirani waliumia sana pia.Baada ya miezi 4 mama akaanza kuingia kwenye chumba cha mama daniel kutazama mali zake.Kweli mama wa kambo alianza kumiliki kila kitu sijui alitufanyaje na sisi tukaanza kumsikiliza yeye kwa kila asemacho bila kumpinga.Siku moja mvua inanyesha mama akatoka na gari la marehemu mama danieli kisha akaenda kutembea wakati yupo njiani akamuona Baba.



    Mama alikimbiza sana gari kisha akakanyaga taili makusudi kwenye bonde yale matope yakamrukia baba! Kipindi baba analalamika mama akafungua dirisha kisha akamwambia “bado unatembelea gongo shauli zako”Baba alilia sana akajutia kwanini alimfahamu huyo mwanamke.



    siku moja usiku sana kipindi tumelala …



    Mama wa kambo alikuwa akifanya mambo yake ya kishirikina usiku pale nyumbani, wote tulikuwa tumelala ila mimi niliangaika kupata usingizi siku hiyo, kipindi bado natafuta usingizi nilisikia sauti ya mama yangu wa kambo akilia kama mtoto mida ya saa nane na robo! Niliamka nikaanza kunyata polepole ili niende kusikia na kutazama nini kinaendelea mule chumbani kwa mama yangu wa kambo.Sikuamini nilicho kisikia kwa masikio yangu jamani, kumbe mzimu wa mama daniel ulikuwa unamsumbua na kumtesa  mama kila saa nane kamili usiku!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com



    Ulikuwa ukimtokea na kumwambia kuwa. “nilikusaidia maisha yako lakini umeniua, nilijitahid kukupenda sana lakini umetoa uhai wangu”.



    Mama alikuwa hapati usingizi kila siku anapo lala maana mzimu ulikuwa unalia na ulikuwa unapiga kelele sana chumbani kwake.



    na mala nyingi mama alikuwa akilala sana mchana maana alikuwa akiteseka kila siku usiku anasumbuliwa na mzimu wa mama dani,



    Nilimsikia mama akilia chumbani akisema, “mama dani nisamee, niache niishi kwa amani jamani”



    Niliondoka polepole kisha nikaenda kulala chumbani kwangu.



    Mama wa kambo aliamua kuomba msaada kwa ndugu yake alie mpa uchawi ili wazuie kilio cha mama dani kinacho mtokea kila siku usiku mama wa kambo ili mama aishi kwa furaha.



    Mama alikubaliwa kusaidiwa ili asiweze kusumbuka tena, lakini mama alipewa sharti moja tu,



    Alitakiwa kuondoa na kuhakikisha ana muua mdogo wangu wa kike ili miungu iweze kumsaidia asiweze sumbuliwa na mzimu wa mama dani kila siku usiku.



    Mama aliingia chumbani kwa mdogo wangu kisha akaweka dawa zake za kichawi chini ya godoro ili mdogo wangu  akilala tu afe, na sisi tumkute asubui kaisha kufa tena bila mama  kugundulika kama ni yeye kafanya mauaji.



    Baada mama wa kambo kutega dawa zake, mdogo wangu na yeye alikuwa amerudi kutoka kwenye mizunguko yake hivyo kipindi mdogo wangu anafika nyumbani, dawa zilikuwa tayali zimetegwa hivyo mdogo wangu akilala tu anafariki hapohapo.



    Mdogo wangu alipo fika nyumbani alienda kuoga ili aweze kupumzika maana alikuwa amechoka sana siku hiyo, kipindi anataka kulala kitandani akakumbuka hatujaonana, maana mimi na mdogo wangu tulikuwa tunapendana sana hivyo akaja kwanza chumbani



    Kwangu kuniaga ili akalale.



    Kipindi mdogo wangu yuko chumbani ananiaga ili akalale alionyesha sura ya upole na aliniaga kama vile anaenda kufa masikini.Alisema “kaka yangu nimechoka sana leo, yani nahisi nikilala naweza kufa kabisa”Nilicheka nikamwambia hapana mdogo wangu hauwezi kufa.Aliniambia usiku mwema kaka tutaonana kesho,Wakati anatoka chumbani kwangu anaelekea kwake alipo toka tu kwangu, akashangaa sana kumuona mama sebreni akiwa anatamani mdogo wangu akalale ili afe.



    Mdogo wangu akamuuliza mama “mama mbona macho yako yamekuwa mekundu sana? alafu umenuna hivyo? na umefunga kwa kujikaza kitambaa chekundu kichwani kama waganga wa kyenyeji.



    Mama akasema  kwa sauti sana kwamba,



    ” WEWE KIMYA, NENDA UKALALE KITANDANI KWAKO UKO, NATAKA KUISHI KWA AMANI MIMI”



    mdogo wangu hakujua kuwa mama ni mchawi hivyo hakuelewa chochote mda ule,



    Akauliza tena “mama mbona leo unanilazimisha nikalale, siku zingine mbona nalala mda ninao utaka mimi”



    Mama aliamka kimya kimya bila kujibu chochote akiwa anamtazamia jicho kubwa sana huyu mdogo wangu.Mdogo wangu alishangaa sana yale matendo,Mdogo wangu akaanza kwenda chumbani kwake ili akalale, mama alifurahia sana kipindi mdogo wangu anaenda ndani kwake maana alijua akilala tu kitandani, mzimu wa mama dani utapumzika na utaacha kumsumbua.



    Mdogo wangu aliingia ndani kwake kisha akasukuma mlango ili aweze kujitupa kitandani kupumzika.



    Mama alifurahia sana alivyo ona mdogo wangu kafunga mlango wake ili alale akajua lazima mpango wake utakamilika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com



    Kipindi mdogo wangu yupo chumbani kwake kabla hajalala alikuwa anapenda sana kuandaa nguo zake za kuvaa kesho shuleni ili asiweze kuchelewa.



    Mdogo wangu viatu vyake vya shule alikuwa akipenda sana kuviweka uvunguni mwa kitanda.



    Hivyo akataka kuvitoa ili aviandae mapema ili kesho akiamka aweze kuwai kwenda shuleni bila kuchelewa vipindi vyake vya twisheni. Aliinama chini kuvichukua viatu vyake, ila vilikuwa kwa mbali, asingeweza kuvichukua kwa wepesi, Ndipo akapata wazo la kubinua godoro ili aweze kuvitoa viatu vyake. Kipindi anabinua godoro alishangaa kuona vitu vya kichawi ndani kwake!Maana ulikuwa ni mjusi umeoza na umefungwa wembe aina ya “gillete” pamoja shanga ya plasitic.Doh Alipiga kelele sana..



    Mdogo wangu alipo piga kelele, sikusikia mala ya kwanza maana tayari nilikuwa nimepitiwa na usingizi.Mdogo wangu Alilia tena akisema “kaka njoo unisaidie, kaka yangu”Mimi nilihisi kama kuna vitu naota ndotoni hivyo nikashtuka, ndipo nikamsikia mdogo wangu analia akiniita! Maana aliogopa sana kutazama ule mjusi ulio fungwa shanga ya palastiki pamoja na wembe ya gillete juu.Nilipo ingia chumbani kwake nikamuuliza “mdogo wangu tatizo nini” akanijibu “kaka fungua ilo godoro uone”Nilipo fungua nikalitupa hapohapo chini maana nilijua moja kwa moja kuna uchawi humu ndani na iliogopa pia.Nikamwambia subilia ngoja nikamuite mama aje atusaidie.



    Nilipo enda kwa mama kumuita nilishangaa sana kusikia analia mwenyewe chumbani kwake akisema. “Mama dani nisamee, nihurumie unanitesa sana mama dani”Dah nilishituka sana ingawa sikuelewa chochote ndipo nikagonga mlango wake ili atoke twende chumbani kwa mdogo wangu.Alipo fungua mlango, nikamwambia mama “mdogo wangu amepatwa na matatizo chumbani kwake twende kumuona”.Mama akajua tayari kafanikisha mpango wake wa kumuua mdogo wangu! Akaanza kulia akisema”jamani mtoto wangu umefariki nilikupenda sana mwanangu”



    Sikumuelewa kabisa pale nikamuuliza mama mbona unasema amefariki wakati bado ni mzima kabisa.Tulipo ingia ndani kwa mdogo wangu mimi pamoja na mama wa kambo.Mdogo wangu akamwambia mama kuwa.”Mama nilikuwa nabinua godoro ili nichukue kiatu chini ya uvungu, ila nimeshangaa sana kukutana na mjusi huyu chini ya godoro”Mama akamwambia “we mtoto kwahiyo siku hizi usiku unabinua magodoro sio, ebu rudisha huyo mjusi labda mama dani alimuweka mwenyewe kipindi yupo hai”



    Mimi Nikamwambia kuwa”mama dani alikuwa hana hayamambo ya kishirikina”



    Mama akasema we mtoto umejuaje kama huu ni ushirikina?



    Nikamwambia ”



    mama sisi ni watu wazima sahivi tunaelewa sana,mjusi auwezi kujifunga shanga na kujifunga wembe, ni binadamu pekee ndiye alie pewa akili ya kufanya mambo kama haya sio wadudu wala wanyama”



    Mama akasema ebu leteni nikamchome moto huyo mdudu labda ni uchawi kweli.



    Mama alichukua ule mjusi kisha akaubeba kwenye mfuko mweusi kwa usitaharabu sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kumbe mama akawa amepanga kesho amuue mdogo wangu tena macho kwa macho



    Ilipo fika asubui kipindi wote mimi na mdogo wangu tumeisha jiandaa ili twende shule,



    Mama aliamka mda huohuo akasema, “wanangu naomba mnisikilize, jana usiku sikulala vizuri, yani najisikia naumwa sana hivyo siwezi kubaki mwenyewe hapa nyumbani, sasa naomba huyu mdogo wako wa kike abaki nyumbani na mimi, ili aweze kuniangalia na kunisaidia baadhi ya kazi maana nina umwa sana jamani”Kumbe mama alikuwa anataka kumuua mdogo wangu pale nyumbani wakibaki wawili ndani.Dah mimi nilipatwa na moyo wa huruma sana kwa mama alipo sema anaumwa  hivyo nikasema “mama ngoja nibaki mimi nikuangalie, wacha mdogo wangu yeye aende shule ”



    Mama akasema “hivi tangu lini mwanaume akauguza mwanamke, mbona unaniletea ubishi wewe, Haya sasa twende ukaniogeshe maana sina nguvu kabisa mikononi!”Nikamwambia “sikujua kama unaumwa kiasi hicho”Mdogo wangu roho yake ilikuwa inamsuta sana kubaki akasema “leo tuna mtihani hivyo nikiukosa itakuwa ni shida”



    Mama akamwambia “kumbe unipendi ehh haya sawa nenda niache ndani tu nife peke yangu”



    Mdogo wangu akakubali kubaki akijua wazi kuwa mama anaumwa, kumbe ulikuwa ni mpango tu wa kuondoa maisha yake jamani.



    Niliamua kuondoka na kuwaacha wakiwa wawili ndani.



    Mama akamwambia naomba ukanichemshie maji jikoni alafu urudi sebreni hapa nikutume nje.



    Mdogo wangu alivyo toka tu, yule kaka mchawi ndugu yake mama akaja ili kumsaidia mama yale mauwaji. Kipindi mdogo wangu anatoka jikoni anarudi kumsikiliza mama sebreni, akakuta mgeni anaetisha, maana yule kaka alikuwa amevaa kanzu nyekundu akiwa amejipaka majivu usoni. mdogo wangu alipo taka kukimbia milango yote ilikuwa imefungwa na funguo.



    Yule kaka akamshika mdogo wangu kwa nguvu kisha akamwagia dawa mdomoni mwake.



    Na alipo mwagiwa dawa  kichwani mdogo wangu alikaa chini kimya bila kusumbua kisha mama akaambiwa “Sasa unaweza kumuua sasa ila usimpake maji kabla ajafa”



    ndipo yule kaka akaondoka.Mama akabaki yeye na mdogo wangu tu ndani,



    kipindi hicho mimi nipo darasani nasoma bila kujua kinacho endelea kwa mdogo wangu masikini



    Mama akamwambia “sikupenda kukuua mwanangu lakini nitakuua maana nisipo kuua wewe, nitaendelea kuteseka maana mzimu wa mama dani unanitesa sana silali kila siku mimi.



    Baada ya mama wa kambo kumwambia mdogo wangu kuwa anamuua ili asiteswe na mzimu wa mama dani. Mdogo wangu alilia sana masikini akasema “mama naomba usiniue, Nisamee kama nilikukosea, natamani kusoma mama, kuishi ili ukizeeka nikutunze mimi.”



    Mama alisema siwezi kukuacha maana usiku silali nateseka sana wala ata sifurahii maisha, Wakuu wamesema nikikuua tu sisumbuki tena,



    mdogo wangu akasema “mama kumbe we mchawi, kumbe wewe ndo umemuua mama dani kwanini unafanya hivi mama”



    Mama wa kambo alichukua kile kipembe cha mbuzi ili amgusishe kichwani mdogo wangu afe,



    Kipindi amekinyanyua kipembe cha mbuzi kilicho pakwa damu ili amuue mdogo wangu.



    Wakati anataka kumwekea kichwani mdogo wangu alilia sana masikini akisema “hee mungu wangu nisaidie”Wakati mama wa kambo amekaribia kumuua mdogo wangu! Palepale mzimu wa marehemu mama mzazi ukaja na kumshika kimiujiza mama wa kambo.Mama wa kambo akauwambia mzimu, “hivi wewe mama mbona unanifatilia ebu niache”mzimu ulimwambia “kama marehemu mama dani anakusumbua katubu dhambi zako usimuue mwanangu”



    Mama wa kambo akasema, “lazima afe tu leo”Mzimu wa mama ukamwambia mdogo wangu “amka kimbia huyu mwanamke ameshika pembe nashindwa kukisaidia vizuri”Mdogo wangu alikimbia mpaka jikoni, mama wa kambo akamfata hukohuko, na mzimu wa mama ukaangaika kumfata mdogo wangu kumsaidia jikoni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mdogo wangu akachukua sipea ya ufunguo ili akafungue mlango akimbie.



    Kipindi mdogo wangu anataka kukimbia! Pale jikoni kulikuwa na maji chini ya sakafu, hivyo akateleza akaanguka chini, wakati ana nyanyuka ili aweze kukimbia, Ndipo mama akachukua yale maji ya moto aliyo mwambia achemshe kisha akamwagia usoni mdogo wangu! Doh alilia! sura yake ikaaribika jamani



    ila akajikaza mpaka akatoka nje ya nyumba.



    Mdogo wangu alipo toka nje ya nyumba hakutaka tena kurudi pale nyumbani na hakutoka na chochote,vilevile hakuniambia ata mimi anakimbilia wapi?



    Kipindi mimi nipo shule nilihisi kichwa kinaniuma sana na sikuwa na raha kabisa hivyo nikaamua kurudi nyumbani.Nilipo fika nikamkuta mama mwenyewe! Nikamuuliza mdogo wangu yuko wapi? Akasema amefatwa na mwanaume wake wakaondoka wote, nilimsubilia sana lakini hakuja, kesho yake nikamuuliza tena mama……..



    Siku ya pili ilipo fika bila kumuona mdogo wangu,akili haikukaa sawa kabisa nikamuuliza mama, mdogo wangu yuko wapi.



    Mama alinijibu kuwa “labda ameisha olewa uko alipo, maana jana binti amefatwa na bwana yake, kama asipo rudi ujue kampenda bwana ake na ameisha olewa kabisa”



    Nilimwambia mama kuwa “mdogo wangu hana tabia kama hizo, unamsingizia, na tangia umekuja hapa familia inaangamia tu, najuta sana kwanini sikumwambia  mama dani kuwa wewe unatabia za kishirikina”Mama akasema hapana mwanangu mimi sio machawi nilisha acha zamani hayo mambo ya uchawi mimi.



    Nilitoka nje kisha nikaanza kumtafuta mdogo wangu alipo, kila nilie muonyesha picha yake alisema hamfahamu.



    Ila walisema kuna dada alilala nje ya lile duka jana usiku  lakini yeye alikuwa ameungua sura yake na urefu wanalingana lingana na hii picha.



    Mimi niliwambia sura yake aijaungua ipo sawa na ajawai kuungua,



    kumbe kweli alikuwa ni mdogo wangu kaunguzwa na maji ya moto masikini.



    Mdogo wangu aliamua kupanda kabisa usafiri na kuamia mkoa mwingine maana alichanganyikiwa kabisa kwa vitu alivyo viona na kuvisikia ndani ya ile nyumba na alitokea kumchukia sana mama maana alitaka kumuua.



    Wakati mdogo wangu anapanda lile (Bus) hakuwa na nauli yoyote mfukoni hivyo akapanda tu hivyo hivyo.Kipindi basi limeenda  mbali sana vijijini kabisa ndipo konda akaanza kuomba tiketi ili ajue walio lipa na ambao hawajalipa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mdogo wangu alikuwa na kidonda chake usoni masikini, alianza kuogopa atasema nini endapo konda akimuomba tiketi.Konda alipo mfikia mdogo wangu akamuomba tiketi.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog