Search This Blog

DAMU YA BABA - 2

 







    Simulizi : Damu Ya Baba

    Sehemu Ya Pili (2)



    Mdogo wangu alipo fikishwa hospitali hali yake ilikuwa mbaya sana tena ya kuogopesha! kitendo kilicho mfanya mama Daniel kuogopa na kujua kuwa lazima mtoto atafariki! Doctor akamuuliza “mama Daniel huyu mtoto mbona kabakwa na bado mdogo sana! tena inaonyesha alizibwa pumzi asipige kelele hivyo imempelekea kupoteza fahamu kabisa, mama nani kafanya mchezo huu, maana anatakiwa kufungwa kifungo cha maisha kabisa!” Mama daniel akajibu “mimi nimemkuta huyu mtoto njiani ikabidi nimsaidie kumleta kwako dokta wangu”

    Mimi nilikuwepo nikaguna! Nikataka kusema ukweli kuwa mwanae anae itwa daniel ndiyo kam’baka mdogo wangu! Ila mama daniel akanikonyeza! Nilijiongeza nikanyamaza pia. Doctor alimpima tena mgonjwa kisha akasema mama daniel mgonjwa wako ana mawili kupona au kufa maana yuko na hali mbaya sana! Kabanwa pumzi yake kwa mda mrefu!. Mama daniel alipo sikia kuwa mgonjwa anaweza kufa akaogopa! akajua kuwa mtoto akifa mwanae atakamatwa hivyo akampigia simu Daniel wake akamwambia “mtoto wangu kwanini unabaka kwanini umefanya kitendo hichi” kisha akamuelekeza Daniel achukue pesa chumbani kwake ili aweze kutoroka aende kijijini kwa bibi yake” Danieli alifanya hivyo lakini Dani alikuwa amepagawa maana alijua ameua na aliogopa haibu mtaani kwao na kwa ndugu zake! Hivyo dani alichukua zile pesa.

    Kipindi anatoroka na basi limefika mkoa wa KIMBIGO basi lilipinduka! wakapata ajali mbaya mungu saidia deleva na watu wote hawakufariki ila Daniel tu ndiyo akawa amepoteza maisha yake !

    Kipindi mama daniel anapigiwa simu kuwa mtoto wake amepata ajali maana na ndiye mtoto wake wa pekee na alikuwa amempata kwa tabu sana maana alikuwa hana uwezo tena wa kuzaa na umli wake ulikuwa umeenda! Mama daniel alilia pale hospital akijutia kwa mambo mwanae aliyo yafanya;

    mda huo huo mdogo wangu akapata nafuu na kuzinduka palepale akishangaa amefikaje hospital huku akisema “kaka nasikia maumivu sehemu zangu za kujisaidia”nilimwambia utapona mdogo wangu! Mazishi ya daniel yaliisha salama! Mama dani sikumoja akatuita na kutwambia kuwa “wanangu mimi sijawazaa wala mimi sio ndugu yenu lakini naomba mnieshimu naomba mniite mama, nipo tayali kuwasaidia mtasoma na mtaishi maisha mazuri….



    Tulimsikiliza na tukamueshimu sana mama Danieli; ila bado hakuridhika kabisa akahisi labda tunaweza siku moja kumgeuka na kumkana maana hakuwa na mtoto tena na umli wake ulikuwa umeenda! Alikuwa anaishi mwenyewe bila mume! Mama Daniel ikabidi aseme kuwa kwanzia leo mimi nitaitwa Daniel kama marehemu kijana wake na huyu binti ambae ni mdogo wako sasa ataitwa Neema;

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    hatukubisha maana yeye ndiye alie kuwa msaada wetu mkubwa hivyo tukakubali kwa majina tuliyo pewa.



    Tuliendelea kujitahidi sana katika masomo yetu maana tulipelekwa shule nzuri tu na tuliendelea kumuheshimu kila mtu alie kuwa ametuzunguka!

    Lakini jamani Baba angu kule nyumbani sababu damu yake ilikuwa imechezewa aliendelea kufanyiwa vitu vibaya sana bila yeye kutambua,



    maana mama wa kambo alivyo kuwa amemficha yule awala yake chini ya uvungu baba akujua, Baba akauliza hiyo mipila ya kufanyia mapenzi juu ya droo ya kitanda changu niya nani?



    Mama akajibu hapana mme wangu usijali huu ni uchafu tu mme wangu; baba akamuuliza acha kunifanya mimi kama mtoto hiyo mipila imetoka wapi? Mama akasema mme wangu kwahiyo uniamini siku hizi sio? Basi mimi naondoka! kwa sababu baba tayali damu yake ilisha chezewa alisema hapana mke wangu usiondoke nakupenda sana!



    Yule awala ya mama alikuwa uvunguni mwa kitanda alafu alikaa mda sana mule akawa amechokaa sana na nguo zake alikuwa hajavaa zilikuwa chini ya godoro pia. Baba alikuwa na wasiwasi ila alijikaza tu maana alikuwa anampenda mke wake. Mke wa baba akaanza kuogopa maana alijua mme wake atamuona yule mkaka alie kuwa chini ya uvungu wa kitanda! Mama akamfata baba chumbani akasema mme wangu nimekuandalia chakula twende ukale. Baba akasema ohh mke wangu nimetoka nimekula! nimeshiba maana ulisha sema nikiwa nakuja nije nimekula nisikusumbue wewe kupika.



    Mama akasema mme wangu twende chumba cha wageni nimekisafisha vizuri nataka nikupe mahaba sana leo ufurahi mme wangu.

    Baba akajibu hapana mke wangu chumba cha wageni ni wageni sio mahaba mke wangu yule mwanaume aliekuwa chini ya uvungu uvumilivu ulimshinda ikabidi atoke kisha akava nguo zake haraka haraka; Baba akasema mke wangu huyu mwanaume ndiye mnafanya nae upuuzi ndani kwangu baba akaenda kufunga mlango.



    Mama akamwambia awala yake “kimbia kabla hajaamka mme wangu ana nguvu!” Kipindi yule kaka anataka kufungua mlango aweze kukimbia baba alijikaza akaamka kwa nguvu kisha akampiga teke yule kaka! Ndipo yule kaka akaangukia kwenye kabati mpaka kabati likaangukia chini!



    Dooh! Kumbe nyuma ya kabati kulikuwa na tunguli ambalo damu ya baba ilikuwa imewekwa baba akauliza hicho nini mbona kama mizimu? mke wake akasema hapana mme wangu! Baba akauliza tena kumbe mwanangu alisema ukweli wewe ni mchawi sio?



    Mama akasema hapana nisamee mme wangu! Baba akakipasua kile kitunguli! palepale damu zikamwagika chini ndipo baba akili zake zikamuijia akawa sawa palepale!



    Akashangaa sana akauliza we dada malaya! mke wangu na mtoto wako wapi? Na umefata nini humu chumbani?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Baba alipo funga mlango, akamkamata mkono yule kaka kisha akampiga kofi shavuni! mama akasema mme wangu muache unamuumiza! Baba akamuuliza “kwahiyo mimi na yeye nani bora” mama akasema “msamee jamani” yule kaka alikuwa kashikiliwa mkono wake na baba yani kwamba ata kuchomoka asinge weza ilikuwa ngumu! Mama alikuwa anampenda yule kaka! maana alikuwa mda mwingi analidhika kwa mapenzi moto moto anayo mpa kipindi baba akiwa kazini, Hivyo alisikitika baba alivyo mpiga teke la kumkata miguu aanguke!



    Mama akasema mme wangu jamani muache! mama akaanza kulia kwa hisia, Yule kaka akachukia sana akasema “jamani nihurumieni sitarudia tena kuja kwako, mke wako ndiye alinilazimisha! mimi nilikataa akanilazimisha akisema kwamba hauwezi kutufumania” baba hakumuachia akasema “lazima ufe hivi unajua nikiasi gani cha pesa namuhudumia huyu mke wangu we unakula tu kiwepesi wepesi” mama alipo sikia kuwa baba anasema kwamba lazima afe alichomeka pasi kwenye umeme! kipindi bado baba ameangalia kwa mbele akiwa amemkaba shingo yule mkaka pasi ilivyo pata moto mama akaongeza moto mkali tena! Kisha akachukua ile pasi ikiwa na moto mkali sana jamani!



    pasi uliyochomekwa kwenye soketi ya umeme mama akamtundikia baba sikioni ile pasi! Dooh baba alipiga kelele akamuachia yule kaka alisikia maumivu makali sana akaanguka chini kabisa akisema “mke wangu kwanini unanichoma jamani” machozi yakiwa yanamtoka sana baba....





    Baba alisikitika pale alipo kuta mke wake hayupo na mimi mtoto wake sipo kwake maana alikuwa anatupenda sana; Baba akamuuliza mama kwamba, we mwanamke kwanini upo ndani kwangu? Mama hakujibu! Baba akasema Nakuuliza ebu nijibu? Baba akasema tena ujue nahisi kama naota vile maana sielewi kabisa! Hivi jamani We mwanamke ulieshindikana mtaa mzima kila mtu anakujua ulivyo na tabia za kubadilisha wanaume inakuwaje leo upo chumbani kwangu! Baba akaanza kulia maana hakuelewa kinacho endelea! Akasema tena naomba unipe mtoto wangu maana ndiye mmoja tu niliepewa na mungu sikuwa na uwezo tena wa kuzaa zaidi ya kijana wangu mmoja tu Nirudishie kijana wang; mama akajibu nisamee mme wangu!



    Weee!! Baba akampiga kofi zito sana; kisha akamwambia naomba usirudie kuniita mmeo ushindwe; Naitaka familia yangu naamini nitaipata tu!



    Mke wa baba akasema “kama hunitaki naondoka” baba akasema sawa ondoka sikutaki kisha akamtolea vitu vyake vyote nje.



    Baba akajiuliza inawezekanaje nimeishi na huyu changudoa! hapana siamini lazima umeniloga lazima umenichezea akili wewe! Baba akapiga nduru akasema alafu sura yangu nitaificha wapi mimi! maana mtaa mzima unakujua tabia yako ilivyo.



    inakuwaje mimi nimefukuza familia yangu nzima kwajili yako.

    Mke wa baba alikuwa hana cha kusema hivyo akafukuzwa kutoka pale kisha akaanza kuzunguka mtaani maana hakuwa na pakukaa.

    Ndipo baba akatoka haraka haraka ndani kisha akaenda kwa ndugu zake, ili kuangalia kama walimtunzia mke wake na mtoto wake ambae ndiye mimi.



    Baba alipo fika alimkuta kaka yake akamuuliza “samahani kaka jamani mimi nahisi kama naota, nahisi sielewi, yani sikumbuki chochote kuhusu familia yangu, na nimekuja kumuulizia mke wangu labda unaweza ukawa unaishi nae hapa” baba amkubwa kabla ya kumjibu machozi yalimtoka akatoa kitambaa na kijifuta usoni kisha akamwambia kuwa “mdogo wangu ulinifukuza kwako ukasema nisikanyage tena! ukamfukuza mke wako na akabakwa na vijana usiku, akaishi maisha magumu sana mpaka akaugua akafaliki,ulimfukuza mama yetu alie kuzaa! kisa mkeo

    hata hivyo tulikusamee maana tulijua ni mapito lakini tulishangaa sana ulivyo mpeleka mtoto wako kwa mikono yako,kituo cha police ukitaka afungwe na achapwe kila mda.



    Baba alilia akasema “hapana kaka mimi sijafanya hivyo kaka, akasema ohh! jamani nitakuwa mgeni wa nani mimi” baba mkubwa akasema, “maneno niliyo kwambia yanatosha mdogo wangu maana nikizidisha unaweza kulia mpaka ukatoa kamasi! Kwa sababu, yani wewe sio wa kukataa kumzika mke wako wakati unajua alikuwa yatima! Hana baba, hana mama, wala hana ndugu yoyote yule! Wewe ndo ulikuwa tegemezi lake”…



    Baba akasema kaka unanisingizia mimi siwezi kumkana mke wangu kabisa siwez kukataa kumzika kaka! Baba mkubwa akamwambia “kama unabisha muulize mtu yoyote mtaani au muulize ata mtoto mdogo toyote anajua kuwa ulimkataa mke wako na mtoto!



    ” Baba alishika kichwa kisha akasema lazima nimuue yule malaya awezi kunialibia maisha yangu bila sababu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Baba mkubwa akasema “mdogo wangu nenda ukamuombe mapema msamaha mama, kabla ajafa maana ulipo mfukuza kwako alikulahani sana na anakuchukia sana hivyo kamuombe msamaha nyumbani maana nimgonjwa sana. akifaliki atakuachia lahana kubwa sana! Baba alikimbia kupanda gari mpaka kwa bibi ili aweze kusamehewa na mama yake! Ila alipo fika nyumbani masikini ya mungu alikuta watu wengi sana! Alipatwa na wasiwasi akauliza, doh alisikitika kusikia mama yake kafariki£ sababu ya pesa kukosekana kwajili ya matibabu na wakati baba alikuwa na pesa ila alimpatia mke wake kila alipo pata pesa lakini mke wake alikuwa akizitumia vibaya kwa kuonga wanaume na kwenda starehe za kila aina.



    Baada ya mazishi kuisha baba akaamua kwenda kumtafuta mama angu wa kambo ili amuulize vizuri ilikuwaje mpaka akamfanya vile,

    Maana baba aliumia sana moyoni, lakini tayali mke wake alikuwa ameanza kujiusisha na biashala ya kujiuza ili aweze kukidhi maitaji yake! maana alikuwa hana sehemu yoyote ya kupata msaada.



    Baba alipo fatilia kiundani aliambiwa kuwa “siku moja alikuwa amelewa sana kwenye Bar, kipindi hicho amekunywa sana Bia, yule mke wake alikuwa anajiuza na alikuwa anajiusisha na mambo ya kishilikina pia, hivyo kipindi baba anaenda nyumbani! aliyumba na kujikwaa akaumia damu nyingi zilimtoka kwenye kiganja chake akiwa chini maana pande la chupa lilimkata



    Akaambiwa ndipo Mkeo akachukua damu yako bila wewe kujua, kisha akakufanyia mazingala ukampenda na kumkana mkeo”



    Baada ya baba kugundua na kuambiwa yale maneno aliishiwa nguvu kabisa! Akasema kuwa “Hee marehemu mke wangu nisamee popote ulipo jamani, ehhh mama yangu mzazi pia nisamee mwanao nilikukosea, huku chozi likimtoka sana baba akasema sio mimi jamani ni pombe tu na uchawi wawatu wasiopenda maendeleo ya watu ndo ulinifanya niwe mbaya kwenu, ehh mama yangu nisamehe. Baba akasema mtoto wangu popote ulipo kama ujafa au kama mzima nisamehe baba yako nakutafuta jamani.



    Baba aliamua kuwa mpole ingawa jamii ilikuwa inamtenga na aliogopwa ata na watoto wadogo ” maana walishangaa alivyo nifukuza mimi rafiki yao ambae ni mtoto wake”

    Baba aliamua kuweka kikao cha kuomba msamaha kwa ndugu zake ili waweze kumjali na kumtembelea maana mkewe alikuwa tayali kawafukuza ndugu zake wote! Ndugu na jamaa walimsamee! Shangazi alikuwa na mtoto akamuomba baba akae nae maana baba alikuwa hana ndugu yoyote na alikuwa anakaa mwenyewe kwake baada ya mke wake kuondoka.

    Baba aliendelea kupambana na kazi zake maana alikuwa mpambanaji sana, lakini masikini offisi ilimtumia barua ya kumsimamisha kazi! Baba alilia kama mtoto maana alikuwa hana akiba ata ya shilingi mia moja ndani! maana mke wake pesa zote alizitumia kwa starehe.



    Baba akaenda kuomba msamaha na kuuliza kwanini wanamuachisha kazi jamani! walimzuia asiingie ndani! Baba alirudi nyumbani akamwambia mtoto wa shangazi kuwa! mtu asiingie ndani awe mwangalifu kisha baba akapanda pikipiki haraka kwenda kumwambia kaka ake mambo yaliyo mkuta ya kuachishwa kazi kipindi yupo barabarani dereva alikimbiza sana na alikosea kunyoosha pikipiki bahati mbaya wakayumba na kudondoka mtaloni! Baba alikuwa amevaa elementi! dereva alikuwa hajavaa chochote kichwani dereva alifaliki palepale ulimi ukamtoka nje kabisa, Baba alivunjika mguu na kuzilai! Alipo pelekwa hospital madaktali hawakuwa na jinsi zaidi ya kumkata mguu wake.



    kipindi baba anaanza kupata nafuu ya ulema! akapigiwa simu kuwa mtoto wa shangazi alikuwa anachezea moto ndani hivyo godoro likashika moto na kuunguza nyumba nzima na kila kitu chake ndani; Baba alilia maana alipoteza kazi na mguu wake pia na nyumba doh!

    Baba akawa kilema masikini ndipo akaanza sasa kuombaomba msaada mtaani.



    Maisha ya baba yalikuwa magumu sana na hakuwa na msaada wa kifedha ata kidogo maana ata ndugu zake hawakuwa na pesa kivile za kuweza kumtunza na kumpa baba kila alicho itaji, hivyo baba hakuwa na njia nyingine ya kujitafutia riziki maana kila alipo enda kuomba kazi hakupata kazi, walimwambia “usilie kaka kazi tungekupa lakini tatizo ni ulemavu wako tu” baba alijiona takataka,  akajiona hana bahati kabisa duniani, akaona bora aendelee kuombaomba ata miamia barabarani apate japo hela ya kula.



    Siku moja tukiwa tunatoka “super market” mimi na mdogo wangu wa kike tunaelekea nyumbani, mdogo wangu akasema “kaka twende kuwapa wale walemavu hela kidogo tulizo baki nazo waweze kutumia na wao labda hawajala masikini” mimi sikuwa na hela yoyote mfukoni, nikamwambia “wewe nenda ukawape mimi nakusubilia hapa ” mdogo wangu akasema kaka mimi sina hela nyingi naenda kumpa mmoja tu pale; nilimsubilia, kumbe mdogo wangu alienda moja kwa moja mpaka kwa baba yangu anapo ombea msaada sehemu ambayo baba yangu anakaa akamkuta baba analia mdogo wangu akamuonea huruma akampatia baba hela, Cha kushangaza mdogo wangu aliwaacha watu wote akampatia baba bila kujua kama yule ni baba yangu masikini; mimi sikujua kama baba yangu yuko pale nilijua bado yupo na mama wanakula maisha maana walinifukuza kwao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama yangu wa kambo aliendelea na biashala zake za kujiuza lakini alichoka maana serikali ilikuwa hairuhusu hivyo, wadada wote wanao jiuza walikuwa wanakamatwa na polisi na kupelekwa kituoni kila siku wanatoa faini! hivyo akaona bora aache hiyo kazi, ata hivyo mama yangu wa kambo alikuwa amepata pesa kidogo akaona ni bora aanzishe genge lake ili aanze kujishugulisha na uuzaji wa nyanya na mbogamboga mtaani;



    Biashara za mama ziligoma pia akakosa ata mia moja ndani, siku moja mama alikosa pesa kabisa hivyo akaenda sehemu za kuombea msaada akijifanya mgonjwa,

    kipindi amekaa amejifunika kanga, usoni ameweka Tsh50 chini ya kibakuli chake watu walikuwa wanampita tu mama bila kumpa msaada, mama alivyo geuza kichwa upande mwingine alishangaa sana kumuona mme wake akiwa hana mguu anaomba msaada! Mama alishtuka sana ila baba  alikuwa bado hajamuona.

    Mama akaona bora atoroke haraka haraka;



    Mama hakuweza kuamini kabisa kama mme wake anaweza kuwa kilema, hakuweza kuamini kama mme wake anaweza kuwa ombaomba, maana alimuacha akiwa kwenye nyumba safi na kazi yake nzuri! Mama Aliona aibu hivyo alikimbia sana akasahau ata bakuli lake na tsh 50 iliyo kuwemo. Kweli “Malipo ni hapa hapa duniani” kipindi mama anaondoka alitembea barabarani bila kijielewa.



    Ndipo akaenda kukaa sitendi ya mabasi yaendayo mikoani! Alimuomba kaka mmoja hela ya kula akisema “kaka yangu nisaidie pesa kidogo nikale” akajibiwa “we dada acha hizo bhana mjini pesa hazitoki kiulaini hivyo, twende kwangu ukale uoge tulale nikulipe hela” kwa sababu mama alikuwa mzoefu katika biashala za kujiuza hivyo hakuwa muoga akakubali,

    kweli walipo fika nyumbani alinunuliwa chakula aina ya (chips yai) mama alikula akaoga akaomba apumzike yule kaka akasema “sikusema uje upumzike hapa nilisema tulale yani tufanye kabisa tendo!” Mama akamwambia “basi nenda ukanunue kinga tulinde afya zetu” kaka akasema sawa ndipo akatoka kwenda duka la madawa kuulizia.



    Alipo rudi akakuta mama hayupo tena kaiba hela kwenye droo ya kitanda na simu yake pia!

    Yule kaka alichanganyikiwa akazitupa chini zile kinga akakaa kitandani akajutia kuleta watu asio wafahamu kwake,Kipindi yule kaka amekaa na vijana wenzake mtaani akamuona mama anapita akawambia “oya yule dada siku moja nimemleta kwangu akaiba hela akaiba simu yangu alafu akatoroka ndani” wakasema “lazima ajute leo” vijana walikuwa 9 kwa idadi.



    Mama wakati anapita ameshikilia chakula wawili walienda na kumkamata. mdomo wake wakaujaza karata walizo kuwa wakicheza akawa awezi kupiga kelele walimbaka mama bila ata kutumia kinga vijana tisa! mama alijaribu kuvumilia maana alikuwa amezoea kujiuza lakini alishindwa maana kipindi anajiuza alitumia madawa ya kulevya ili asisikie uchovu ila hapa walimbaka hivyohivyo tena vijana walikuwa wachafu sana hivyo mama akapata magonjwa ya zinaa! mama alibaki pale mtaani mwenyewe nguo zake zikiwa zimechanwa.

    kipindi watu asubui wanaenda kazini walimkuta mama akiwa analia akiwa uchi wakamuuliza tatizo nini akajibu “nilibakwa usiku ” wakamuuliza kwako wapi? Akasema jamani sina sehemu ya kuishi!

    Dada mmoja akasema mimi.



    Mama alisaidiwa na yule dada kwa kila jambo! akaishi vizuri tu.

    Siku moja mimi niliamua kwenda nyumbani kwetu maana nilitamani sana kumuona baba ingawa alinitupa lakini “damu nzito kuliko maji”,Nilisikitika sana nilivyo kuta nyumba yetu imeungua yote nilikuwa nimeenda na gari maana tayari nilikuwa nimekuwa kijana mkubwa hivyo gari za nyumbani nilikuwa naendesha mda wowote ule sikushuka nje ya gari maana nilijua tayari siwezi kumpata baba yangu. Ila baba yangu alikuwa na nyota pia maana alikuwa akipata msaada kushinda wale omba omba wengine.



    Siku moja baba amekusanya karibia kama elfu 50, mda huo omba omba wenzake hawajakusanya kitu chochote.

    Walimpiga baba na kumnyang’anya pesa zote wakisema kuwa “we baba tangu uje hapa wenzako hatupati hela unatubania riziki bwana” baba alilia akiwa na mguu mmoja “jamani msininyan’ganye hela zangu” watu walijaa sana pale. wakawazunguka wagonvi mimi pia nilikuwa  napita maeneo yale sikujua kama baba ndiye anapigana na watu masikini na ata sikutaka kuchungulia kuna nini kinaendelea nilipita tu!



    kumbe ningejua ningemsaidia baba labda asingeumia na kupata alama kubwa usoni mwake.Nilivyo fika nyumbani nikamkuta mama Daniel katoka mkoani maana alikuwa na biashala zake akizifanya hivyo alikuwa anaweza kukaa ata mwaka mzima bila kurudi nyumbani,Nilimsalimia mama daniel na nikamuuliza hali ya atokako ila nilishangaa sana kuona hanijibu

    Bali ananitazama macho yangu kihisia vile, sikutaka kujua anacho kiitaji ila nilihisi labda alikuwa amelewa siku hiyo mpaka macho yake yakalegea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama yangu wa kambo aliendelea kukaa kwa yule dada mpaka akawa rafiki yake mkubwa wakaaminiana sana.

    mama aliendelea kupendeza kwa nguo alizo kuwa akinunuliwa na yule dada mpaka vijana wakaanza kumtamani bila kujua kuwa mama ni mwasilika,Mme wake yule dada alie msaidia mama akaanza kumtamani mama sababu alipendeza kuzidi ata mkewe.

    Siku moja Mume wa rafiki wa mama akawai kutoka kazini akarudi nyumbani akijua kuwa mke wake awezi kurudi nyumbani mda huo, Alimuita mama chumbani kwake akamshikisha laki tatu mkononi akimwambia, “naomba tufanye mapenzi ila mke wangu asijue na mimi nitakuwa nakupa pesa  na nitakutunza kama mke wangu humu ndani! Mama akasema….



    Mama alipo shikishwa laki 3 mkononi, huruma ya kukumbuka fadhila za mke wa huyo mwanaume zikapotea,

    mama akawa mwepesi! Akamwambia “mimi naogopa shemeji” uku akionyesha macho ya kukubali! Shemeji yake alipo mshika mwili wake na kuupapasa! Mama akasema tutumie kinga shemeji maana tayali umeisha nipandisha!

    Shemeji akasema “mbona sina kinga hapa kwani kinga za nini” palepale wakaanza kuburudika bila kinga tena mbaya zaidi chumbani mwa rafiki yake, na wakati huo mama alikuwa ni mwasilika wa virusi vya ukimwi! Na mama alijigundua alipo pimwa baada ya kubakwa na wale vijana 9.



    mke wa yule mwanaume kipindi yupo ofisini alijihisi kama kichwa kinamuuma, na alipo kula alishangaa sana maana alijin’gata ulimi wake!

    Kumbe kweli mme wake alikuwa anasaliti ndoa,yule mwanaume alifurahia sana ile dhambi walio kuwa wamefanya na akaona utofauti pia kwa kumsifia mama kuwa “unaweza zaidi ya mke wangu” kumbe mwanaume nae akawa amepata maambukizi ya virusi vya ukimwi siku hiyohiyo masikini.



    Mwanamke wake alipo kuja jioni hakugundua kitu chochote! Alicheka vizuri na mama, maana walikuwa marafiki sana! Ila mama alionyesha wasiwasi kidogo siku hiyo na kujutia alicho mfanyia mwenzake

    Ilipo fika usiku kipindi yule dada amelala na mmewe alitamani sana kufanya tendo la ndoa siku hiyo, mme wake pia akashiriki nae, ndipo masikini wa mungu yule dada nae akaamishiwa maambukizi ya virusi vilivyo toka kwa rafiki yake ambae ni mama!

    Maisha yaliendelea kwenda  hakuna alie gundua kuwa kaathirika zaidi ya mama kuitunza siri yake.



    Siku moja yule mwanaume aliwai tena kutoka kazini akiaga anafata pesa benki kwajili ya matumizi ya ofisi, kumbe alikuwa anarudi nyumbani ili wafanye tena mapenzi na mama yangu wa kambo

    Alipo rudi mama akamwambia,



    Mama..shemeji mbona umewai kurudi leo?



    Shemeji..nimerudi kwajili yako mpenzi wangu, maana nafurahia sana kila ninapo kutana na wewe



    Mama..mke wako akitukuta je?



    Shemeji..hapana usiwe na wasiwasi nimeisha mpanga na awezi kuwai nyumbani bila kunitaarifu.



    Mama..sawa shemeji nimekuelewa!



    Shemeji..hapana usiniite shemeji, niite jina zuri la mapenzi!



    Ndipo wakaingia ndani wakifurahia,  wakaenda kuoga chumbani mwa rafiki yake mama

    walipo maliza kuoga..



    Waliingia bafuni wakiwa wamevaa taulo na wote wakiwa wamevaa  nguo za ndani nyeupe tu,Walipo Maliza kuoga wakaongea

    Shemeji..mpenzi unanipa raha sana kuzidi mke wangu natamani kumfukuza kabisa.

    Mama..hapana usimfukuze na wala asijue, maana bila yeye  usinge nijua.



    Shemeji..sawa mpenzi wangu nakuhaidi siwezi kukuacha maisha yangu yote, wewe ndiye mwanamke niliye kuwa nikimtaka maisha yangu yote lakini sikumpata, ila namshukuru sana mungu kupitia mke wangu wa ndoa nimempata!

    Mama..ata mimi pia nafurahi na ninamshukuru mungu kukufahamu maana unanijari na unanipa mapenzi mpaka naridhika.



    Shemeji.. asante sana mpenzi wangu nitaendelea kukupa vitu vizuri uendelee kufurahia kuwa na mimi na husijutie ata kidogo kunifahamu. Mama.. sawa mpenzi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Siku hiyo mke wa yule mwanaume alikuwa amesahau vitu vya ofisini nyumbani hivyo akaamua kurudi haraka nyumbani kuvifata maana vilikuwa na umuhimu sana pale kazini.

    Alipo mpigia mme wake simu ili amuelezee hiyo taarifa, mwanaume akawa hapokei simu maana aliisahau sebureni,

    akawa anachepuka na mama yangu wa kambo chumbani.

    Mke wa yule mwanaume alivyo ona mme wake hapokei simu ikabidi aende hivyo hivyo, kumbe nyumbani anapo enda mme wake anachepuka na rafiki yake.



    Alivyo fika nyumbani akafungua mlango wa nje.

    Alipo ingia ndani akakuta kimya sana, alivyo angalia mezani akakuta simu ya mmewe pale.

    Ikabidi ampigie rafiki yake, simu ikaitia palepale sebreni.

    Ndipo akaanza kukagua vyumba vya ndani.

    Akaanza na chumba cha rafiki yake hakumkuta, alivyo enda chumbani kwake akasikia sauti za mapenzi mlangoni hakuamini kwanza kama ni rafiki yake maana hakuzania kama angeweza kumsaliti na hakufikilia kama mme wake anaweza kumsaliti.

    Alichungulia vizuri kwenye tundu la kupitisha funguo maana lilikuwa linaonyesha kitanda kizima.



    Alisikitika sana maana alimuona rafiki yake kwa macho yake akiwaa uchi wa mnyama akifanya mapenzi na mmewe. Yule dada  Aligonga mlango kwa nguvu sana akisema “fungua haraka  fungua mlango” mme wake akaanza kutetemeka

    Mama akasema “nilikwambia shemeji kuhusu mke wako! unaona sasa! nitaificha wapi sura yangu jamani.



    Shemeji..ehh mungu wangu namwambia nini mke wangu jamani namwambia nini mimi!



    Shemeji yake alimwambia mama akafungue mlango maana yeye tayali alikuwa kaisha ogopa,

    yule dada aliingia ndani akiwa analia sana masikini, mpaka kamasi linamtoka puani kabisa kwa maumivu na uchungu “hama kweli mume wa mtu mchungu” yule dada akasema “rafiki yangu fadhila zote zile, leo unanilipa hivi”.



    Akamwambia na mme wake “mme wangu hii ndiyo ahadi yetu tulio peana kanisani sio?ya kulala na mwanamke tena mbaya zaidi kwenye kitanda changu” Huku akiwa analia sana dada wawatu mpaka macho yakabadilika rangi na kuwa mekundu.

    Mama yangu alianza kulia akisema “nisamee rafiki yangu sirudii tena kuja chumbani kwako rafiki yangu nisamee shetani na ibilisi kanipitia” Mme wake akasema “mke wangu hatujafanya chochote kibaya nilikuwa namwambia aniandalie chakula maana leo nimewai kutoka kazini nilijihisi mchovu! nisamee sikukupa taarifa mke wangu.



    Yule dada alimpiga kofi chungu sana mme wake! akamwambia ebu angalia hiyo nguo ya ndani uliyo vaa kama ni yako.

    Mme wake alivyo jitazama alikuwa hajafunga taulo vizuri na alikuwa amevaa nguo ya ndani ya mama!

    kilicho mchanganya ni langi maana zote zilikuwa nyeupe

    Na walivaa nguo haraka haraka kwa huoga kuwa wamekamatwa,

    mama na yeye alivyo jitazama akakuta amevaa nguo ya ndani ya shemeji yake.



    Yule dada machozi yanamtoka akamwambia mme wake “utamuitaje huyu mwanamke ndani akiwa amevaa utupu hivi. Nyie hamjaanza leo mmeanza zamani leo nashukuru mola kanionyesha waziwazi”.

    Yule dada alikuwa na roho ya huruma sana alimwambia yule mwanamke “Sina cha kukufanya maana tayali umeisha tembea na mume wangu nacho omba chukua nguo zako na kila kitu chako uondoke”

    Mama alipiga magoti akasema “nisamee rafiki yangu mme wako alinilazimisha sana mpaka nikajikuta nashawishika sirudii tena rafiki yangu!



    Dada akasema..Mme wangu huyu mwanamke nilimkuta sehemu amebakwa! tena mbaya zaidi alibakwa na vijana tisa wa mtaani, nilipo muona hana sehemu ya kuishi nikaona ni bora tukae nae wote hapa! Sasa wewe umetembea nae! una uwakika gani kama ni mzima ki afya na nimekutazama ata kinga hujatumia wewe unasaliti ndoa tu,  Mme wake akasema…nisamee mke wangu nakuhaidi siwezi kurudia hivi tena.

    Mama akasema nisamee pia rafiki yangu..



    Yule dada aliwasamee wote mama na mmewe ila akamuonya mme wake sana asirudie kile kitendo! Ikafika hatua yule mwanamke akawa anatoroka kazini kwake kuja kuangalia kama mme wake anaweza kurudia kile kitendo, lakini mme wake alishangaa kwanza mke wake alivyo msamee! na maneno ya mke wake kuwa yule mwanamke alibakwa na vijana tisa yalimfanya mme wake amuogope mama kabisa.Baada ya week kadhaa mama yangu wa kambo alianza kuonyesha dalili tofauti sana kwenye mwili wake, kumbe alikuwa kapata ujauzito wa mme wa yule dada! Kutokana na yule dada kutoroka kazini mala kwa mala kuja nyumbani akihisi mmewe bado anachepuka offisi iliamua kumuachisha kazi!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Dada alilia sana maana hakuwa na sehemu yoyote ya kupata kazi tena kwa mda ule.

    Kipindi yupo nyumbani anawaza sana ni jinsi gani atapata kazi, alikuwa hajagundua kabisa kama mama anaujauzito wa mme wake!

    na tumbo la mama likikuwa dogo sana hivyo ilikuwa ngumu kumgundua na ile mimba ilimtuma sana mama kufanya kazi hivyo asingeweza kugundulika mapema maana hakuwa mchovu mchovu ila siku moja mama amebeba ndoo,  dada akashangaa kuona tumbo la mama kama kunakitoto kinajigeuza geuza tumboni akamuuliza.. Dada akasema.. best una mimba.



    Mama…sina mimba best kweli tena.



    Dada..usiogope niambie kama unayo nitakusaidia maana utaangaika



    Mama.. nisamee mimi kweli mimba ninayo!



    Dada..mimba ya nani?



    Mama..best kipindi kile ulipo nifumania mme wako alinipa! Lakini sijamwambia mpaka sasa.



    Yule dada alianguka chini akawa amepoteza fahamu! maana yeye kizazi chake kilikuwa mbali! na alikaa mda sana na mmewe bila kushika mimba ila rafiki yake mda mchache tu akapata ujauzito.



    Mama akaanza kumpepea yule dada, alipo pata fahamu tu aliishiwa nguvu dada wawatu maana kazi alisha fukuzwa! nyumbani pia ndoa yake inavurugika

    Mme wake alipo fika kutoka kazini tu

    Akamkalisha chini akamwambia “kwanini umeharibu mipango yetu ya maisha?

    Nimefukuzwa kazi sababu yako! Kibaya zaidi umempa mimba huyu rafiki yangu”.

    Mwanaume alishtuka kusikia kampa mimba mama

    hicho kitendo kilimuuma sana akaikataa mimba akisema sio yake!Yule dada akaokoa ndoa yake, akamfukuza mama kwake! Kipindi yule dada anarudi ndani alishangaa sana kukuta mme wake amejiua na kisu



     Yule dada alilia sana alipo kuta mume wake kajichoma kisu tumboni na kujiua kabisa jamani! Alishtuka maana hakutegeme kitu kama hicho, Alilia sana akisema kwanini nilimsaidia yule dada mimi! amenialibia maisha jamani mda huo akiwa ameshika kichwa cha marehemu mme wake pale sebreni.



    Kipindi anageuka kidogo akaona ujumbe  mme wake kauandika kwenye karatasi kabla hajafa.

    Kwamba

    ” Mke wangu naomba unisamee kwa kujiondoa uhai mwenyewe, nimeshindwa kuishi maana ningekosa amani na furaha niliyo kuwepo nayo hapo awali sababu ya haibu ya kuvunja ndoa yangu na kutembea na rafiki yako, Nimeona haibu pia kumpa mimba huyo dada wakati bado sijakupa wewe mke wangu wa ndoa.

    Nisamee mke wangu Maana nasikitika sana nilipo enda kupima nikakuta tayali rafiki yako ameniambukiza maambukizi ya virusi vya ukimwi! Nisamee sana ni mimi mmeo Samweli maisha mema”

    Yule dada alivyo juwa mmewe kaambukizwa na yeye moja kwa moja akajua kaathirika! Alichanachana ile barua kwa hasira akiwa analia kama mtoto majirani walikuja ndani walishangaa kumkuta yule dada kashika kile kisu tumboni kwa mme wake! Ndipo wakakimbia polisi kumshtaki kuwa ameua!



    Kweli polisi walipo kuja walimkamata yule dada kwa nguvu na kumvika pingu mikononi.

    Alilia akisema” jamani sijaua mimi sijaua jamani” hawakumuelewa kabisa ata kidogo.



    dada alikosa ushahidi maana ile barua mmewe aliyo andika yeye aliichanachana kwa hasila  alipo maliza kuisoma hivyo hakuwa na ushahidi wowote

    Ndugu zake yule mwanaume walilalamika sana na kumshtaki yule mwanamke eti,

    “wewe umemuua kaka yetu ili ubaki na mali, sasa mali hupati na unaozea jela”

    Yule Dada akawajibu “sijaua jamani”

    mahakama ikafatilia kazini kwa yule

    dada.

    bosi wa ofisi akawambia “tulimfukuza kazi huyu dada maana alikuwa anatoroka mala kwa mala kwenda nyumbani! nazani ndiyo alikuwa anafanya mipango na mikakati ya kumuua mmewe”



    Ndipo yule dada akakamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha mkoa wa “Tantala”

    Mama aliangaika sana na ile mimba mtahani! Na maisha yalikuwa magumu sana kwake hivyo akaamua ameze dawa ya kutoa  mimba asiweze kuendelea kuteseka!

    Mama alimeza dawa mimba ikafa lakini bahati mbaya katoto kakawa kagumu kutoka tumboni! Mpaka harufu ikaanza kumtoka mwilini

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama yangu wa kambo alianza kutoa harufu kali sana! baada ya kile kitoto kugoma kutoka tumboni aliona haibu kuwambia watu maana alihisi watamcheka,

    Yani mama kutokana na ugumu wa maisha alikosa msaada kabisa eti ata alipo kuwa akikaa n’zi nyingi zilikuwa zikimfata,

    kibaya zaid mama alipo kuwa akiongea na watu harufu yake ya mdomoni ilikuwa chafu sana yenye harufu mbaya! Ata pale alipo kuwa akitoka jasho pia alitokwa na harufu mbaya mwilini mwake  jamani harufu kama ya kitu kimeoza sana.



    Siku moja mama yangu wa kambo alizidiwa  sana nusra ya kufa maana mwili wake uli badilika ghafla yani mama alivimba mwili na kunuka kama mtu aliyekufa;

    vijana walalahoi wa ule mtaa walimuonea sana huruma mama, maana mama alikuwa analia kama mtoto akiomba msaada akisema “nisaidieni nakufa jamani, naumwa sana tumbo ndugu zangu” ,Kibaya zaidi  mama alienda kuwatilia harufu yake kwenye mtaa wa wale vijana hivyo basi, Ikabidi wamfunike shuka na kumpakia kwenye usafili kama marehemu huku wamejivika vitambaa puani mwao kupunguza harufu! wakimpeleka hospitali ili akatibiwe tena  kwenye  hospitali za serikali.



    Mama alivyo fikishwa hosipital dah! Masikini wale manesi walikuwa hawataki ata kumtibu maana alikuwa ananuka tena kibaya zaidi mama yangu wa kambo alikuwa ameachama mdomo wake kama vile amekufa yani! ata ukimtazama unamuogopa jinsi mwili wake ulivyo kuwa maana macho yake pia yalibadilika rangi yalikuwa makubwa na ya njano sana.

    Dakitali mkubwa wa hospital aliwambia manesi wamtibu.

    ndipo mama aliwekewa diripu ya maji ili aweze kupata nafuu.

    Hali ya mama alikuwa mbaya sana mda ule! ikabidi daktali mkuu aje kumcheki ili amfanyie matibabu ya uangalifu zaidi.

    Ndipo alipo gundulika kuwa katoto kalifia tumboni kwa mama na kukawa na ugumu wa katoto kutoka,mama yangu wa kambo alifanyiwa oparesheni ndipo kikatolewa kile kitoto kikiwa kimeoza vibaya mno “kweli udaktali sio kusomea tu unaitaji moyo”

    Yule daktali alimuhudumia mama vizuri  akamsafisha vizuri kabisa mpaka mama akapona na kupata nafuu akawa salama.



    Kipindi mama ametoka hospital na hana sehemu ya kuishi masikini! alirudi kuangalia kama rafiki yake yupo ili amwambie kuwa ametoa ile mimba ya mme wake ili waishi tena wote ila.



    Mama yangu wa kambo alishangaa sana na kushtuka alipo fika kwa yule dada rafiki yake maana hakumkuta na ndiyo ilikuwa mida yake ya kutoka kazini. Aliwaza sana ataishi wapi na atalala wapi siku hiyo maana alitaka kumuakikishia rafiki yake kuwa hana mimba tena na hawezi kurudia kulala tena na mme wake.



    Mama aliwaza jamani isitoshe mama alikuwa amepewa dawa alizo toka nazo hosiptali na alitakiwa kuzimeza ili apone vizuri.

    Kipindi anataka kuondoka wifi yake rafiki yake alikuwa anafika pia! maana ndiye aliekua amerithi nyumba ya marehemu kaka yake kwa sababu yule dada alifungwa.



    Wifi akamuuliza mama kuwa.. Wifi..dada karibu naona unataka kuondoka!



    Mama..ahsante namuulizia rafiki yangu niliishi nae hapa nimekuta hayupo na mme wake pia hayupo



    Wifi.”machozi yalimtoka kwanza” akasema mme wake alisha fariki! na huyu muuaji rafiki yako kafungwa na tena ni kifungo cha maisha.



    Mama alishtuka sana akaogopa na akaondoka.

    Alipo fika nje ya nyumba akamkuta jirani yake alikuwa amezoeana nae akamuuliza kama kweli mwanaume alikufa! na je mke wake kakamatwa?



    Yule dada alimwambia kuwa! “mwanaume wake alijiua baada ya mke wake kugundua ukweli kuwa unatembea nae na pia umepata mimba ya mmewe na pia anamaambukizi, hivyo wewe ndo unatakiwa kuwa shahidi wake au mtetezi wake ili kifungo chake kisitishwe”

    Mama aliwambia majirani na marafiki zake rafiki yake kuhusu ukweli wa kwamba mwanamke hajamuua na alipo fika mahakamani akasema kwamba. “Mimi nilisaidiwa na huyo dada kuishi kwake, ila mme wake alinilazimisha kimapenzi! Bahati mbaya nikapata mimba yake, baada ya mkewe kujua ndipo akajiondoa uhai wake”

    Serikari ilifanya uchunguzi na kugundua kweli yule dada hakuua ndipo wakaamua kumuachia huru,Maisha ya yule dada yalikuwa niyakukosa raha sana alijaribu kutafuta kazi hakupata, alijaribu kurudi kwake ndugu wa mme hawakumuitaji ndipo akaanza kujishugulisha na biashala ndogondogo tu na mama yangu wa kambo.

    Baba yangu aliendelea kuteseka pia na maisha yake maana tayali alikuwa kapoteza mguu ndipo familia ikamshauli aende kupiga magoti kwenye kabuli la mke wake na mama yake ili aweze kuomba msamaha maana alifanya kosa bila kujua.

    Kipindi baba yupo makabulini dooh!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Baba alipo fika makabulini, alienda moja kwa moja kwanza kwenye kabuli la marehemu mke wake. Baba alianza kulia akisema “Nisamee mke wangu nakuomba msamaa maana najutia mabaya yote niliyo kutendea, sio mimi  jamani ni shetani tu, sikujua kama nilikataa kukuzika na sikujua kama nilikufanya uteseke! leo nipo juu ya kabuli lako nakuomba msamaa maana mimi ndiyo chanzo cha kifo chako natamani ufufuke tuishi tena kama zamani mke wangu! Ona jinsi ninavyo teseka angalia jinsi nilivyo kilema kwa sababu ya rahana nilizo zibeba kutoka kwenu Tazama machozi yanavyo nitililika machoni mwangu, naomba unisamee niweze kuishi kwa amani maana ata mda mwingine natamani kufa tu maana sioni raha ya kuishi duniani, mke wangu kila siku usiku silali naota tu ndoto za ajabu sana mala nafukuzwa mala nachinjwa mda mwingine naota mizimu imenizunguka mimi! ehh mke wangu nihurumie nisamee mzazi mwenzangu”



    Baba aliongea maneno hayo akiwa amesimama mbele ya kabuli la mama akitokwa na machozi sana kipindi baba anataka kuendelea kuongea alishangaa kuona upepo mkali sana unavuma, baba alihisi labda ni hari ya kawaida tu! Mala ila alishangaa upepo hauishi tu na uliendelea kuwa mkali  kabulini yani mpaka ukamuangusha baba chini maana alikosa balansi sababu ya mguu wake mmoja.



    Kipindi baba anataka kukimbia upepo ukapotea mala kukawa kimya! baba alibaki haelewi tu.

    Mala ghafla akaona mguu ulio katwa juu ya kabuli la mkewe, Na mguu ulikuwa una kipande cha suruali ambayo hiyo suruali ilikuwa ya baba kipindi alipo katika mguu wake kwenye ile ajali!

    Baba akuamini kutazama mambo ya ajabu kama yale kipindi baba yupo tu bila kuelewa!

    alishangaa kuona kile kibuyu kilicho kuwa nyuma ya kabati chenye damu yake pale pia.

    Doh Baba aliogopa sasa!

    Pale pale mzimu wa mama yangu ukatokea ukiwa umevaa nguo zenye damu iliyo ganda kama nyeusi,ukaanza kuongea.



    “Mme wangu sikusamei ata kidogo ulinitesa sana ulininyanyasa sana nimepoteza uhai wangu sababu yako! Kwanini ulinitesa? Kwanini uliniumiza vile ulisababisha nikabakwa, ulisababisha nikaugua magonjwa ya ajabu mimi! Kibaya zaidi mme wangu nipale ulipo kataa kunizika na kumzuia mtoto wangu kunizika mimi yani wakati ulijua mimi ni yatima sina ata ndugu jamani”



    Yale maneno ya marehemu mama yangu mzazi yalimuumiza sana baba.

    Baba akasema, “marehemu mke wangu sio mimi nilifanya vile na wala nilikuwa sijitambui hata kidogo mke wangu mpaka kukufukuza wewe! nafikiri nilichanganywa akili yangu mke wangu! ebu fikilia jinsi tulivyo kuwa tunapendana jamani”

    Alijibiwa na mzimu wa mama kuwa, “mme wangu nilikuzuia sana kunywa pombe! Na pombe ndiyo chanzo cha wewe kukutana na matatizo yote haya, Ebu jitazame sasa hauna mguu angalia kazi yako tayali umeisha ipoteza tazama hauna nyumba tena! na wala haufahamu mwanao alipo mpaka sasa sababu tu ya huyo mkeo”.



    Mzimu wa mama ukamwambia baba; “mme wangu  nakupenda sana na nashindwa kukusamee maana najua ata nikikusamee bado tu utaendelea kuteseka! maana mzimu wa mama yako mzazi na rahana alizo kuachia zinaendelea kukuzunguka, yani kila uendapo hauwezi kufanikiwa mpaka ukaombe msamaa kwanza, Maana mama yako mzazi amekufa akiwa na kinyongo sana na wewe

    Baada ya siku tatu, baba aliamua kwenda mpaka kabulini kwa mama yake mzazi kwenda kuomba msamaa ila.



    Kutokana na maisha ya baba kuwa magumu, Baba aliamua kwanza aende  sehemu ya kuombaomba msaada ili apate pesa kidogo, ila siku hiyo hali ilikuwa ngumu hivyo baba akaona akaekae mpaka jioni ili aweze kupata japo pesa kiasi kwa wapita njia.

    Jioni ilipo fika  ndipo akaamua kwenda kuomba msamaa kwenye kabuli la mama yake muda ule wa jioni, kabuli lilikuwa makabulini baba alikuwa ajui chochote yeye alienda moja kwa moja kwenye kabuli akapiga magoti chini akitoa machozi huku akisema “mama yangu mzazi tazama jinsi mwanao ninavyo teseka, najua nilifanya kosa kubwa sana la kusahau kuwa wewe ni mama yangu, ila naomba unisamee mama nisamee mama yangu, naomba unijibu mama yangu”

    Baba aliyasema maneno hayo akiwa mwenyewe kabulini!

    Ila baba alishangaa sana kwanini mama yake hamjibu kama mkewe.

    Baba akaamua asubilie mpaka mama yake amtokee kama marehemu mkewe, ila hakumtokea!

    ilipofika saa nane kamili usiku kipindi baba akiwa amelala juu ya  kabuli la mama yake, alianza kusikia sauti ya ndege ikipiga kelele juu yake! baba alishtuka alipo amka akakuta Bundi ameng’aa macho akiwa kasimaa juu ya msalaba wa kabuli la mama yake usiku.



    Kipindi baba anataka kumfukuza yule bundi, kumbe sio bundi jamani ulikuwa ni mzimu wa marehemu mke wake unamuonyesha kuwa sehemu aliyoko sio salama kuna wachawi pale.

    Baba alivyo geuka pembeni tu! Palepale akainama chini haraka maana aliona watu wamevaa nguo nyeupe na wakiwa wamejifunika vitambaa vyekundu kichwani huku mikono yao imeshikilia mishumaa katikati ya makabulini. Baba hakuamini kutazama watu kama wale maeneo kama yale usiku!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kipindi baba amelala chini kwa kujificha, alishangaa pia kusikia wachawi wakisema kimzimu kuwa “Ohh wewe Zabroni mwaka, tajili wa wilaya nzima, tumekuja kukuchukua sasa kukutoa humu kwenye kabuli! Maana tayali jamii ilikuzika ikitambua umekufa! Lakini Kumbe wewe bado ni mzima na sisi tumependa nyota yako! unanyota nzuri sana zabroni  Mwaka,

    Na  kwanzia leo utaishi na sisi na hii nyota yako tutawauzia waganga kwa kienyeji ili na wenyewe wakaiuze kwa wale wanaotaka nyota za watu ili wapate utajili”

    Baba alisikitika sana maana huyo zabron alikuwa rafiki yake sana na alifariki kila mtu akajua amekufa kumbe hapana yupo hai ila gogo tu ndiyo limezikwa.



    Kipindi baba akiwa anawatazama



    Mwanaume Mmoja kati ya wale wachawi alisimama akashika jogoo mweusi sana kisha akamnyongwa  na kumrusha kabulini mwa zabroni, mda huohuo zabron alitoka kabulini akiwa amevaa sanda, ndipo akavuliwa na kuvalishwa kichawi kama wenzake, alinyweshwa damu ya binadamu na kuvalishwa bangili la kishirikina mkononi mulemule katikati ya makabuli.

    Baba alimshangaa sana yule kaka alie mnyonga jogoo maana yule kaka alikuwa ni ndugu yake na mama yangu wa kambo na baba alikuwa akila nae na kucheka nae pale huyo kaka alipo watembelea nyumbani.



    Mizimu alianza kuimba na kupanda kwenye usafili wao ambao ni ungo kisha wakapaa na kuondoka.

    Baba hakuamini kwa alicho kiona usiku ule ilimbidi akae palepale mpaka asubui.



    Nyumbani pia mama Danieli alitukumbusha kuwa tunatakiwa kwenda kwenye kabuli la mwanae siku hiyo maana ndiyo ilikuwa siku yake ya kufariki, hivyo tulijiandaa kwenda kulifanyia usafi kabuli lake.



    Na baba yangu mzazi pia siku hiyo alikuwa bado palepale kabulini na mimi nilikuwa sijaonana na baba siku nyingi na baba pia alitamani sana kuniona mwanawe



    Tulipo fika makabulini kumbe na baba yangu mzazi alikuwepo pia lakini bahati mbaya sikuweza kuonana nae maana sikuweza kufikilia kuonana nae sehemu kama zile na sikuwa na fikila ata za kuchunguza watu pale.

    Hivyo tulifanya kusafisha kabuli la Daniel! maana mama yake alikuwa anampenda sana mwanae, na alilia sana pale kabulini akisema, “mwanangu Danieli nimetumia pesa nyingi sana kukusomesha, Kukutunza nimekuzaa kwa shida mwanangu leo hii haupo nasi mtoto wangu ehh jamani mungu” mama Danieli alilia sana ila tulipo maliza kupamba yale maua tuliondoka na kurudi nyumbani.

    Baba mipango yake ya kuomba misamaa ikawa haijakamilika kabisa maana roho ya mama yake mzazi iligoma kuweka wepesi wa msamaa kwa mtoto wake,



    Baba aliendelea kutahabika sana! Siku moja baba akiwa ametoka katika miangaiko yake ya kuombaomba misaada alikutana na vijana wawili wameshika Bibria walimsimamisha baba na kumwambia kuwa.

    Vijana,, mzee mimi ni muumini wa kikristu na huyu pembeni yangu ni mchungaji wa kanisa letu.

    Baba akajibu,, ahsante nafurahi kuwafahamu, mlikuwa na shida gani waumini.

    Vijana,, “mungu ni mwema” tumemuona mungu ndani yako na tunataka kukuondolea misukosuko ya maisha yako yote.

    Baba akajibu,, nitafurahi sana wachungaji maana mimi nina matatizo, marehemu mke wangu na mama yangu niliwafanyia vibaya sana leo nawaomba msamaa  hawataki kunisamee! ili mimi niweze  kuishi huru bila mawazo na matatizo.



    Vijana,, baba tayali dhambi zako zimeisha samehewa mizimu imekusamee pia. Ila unacho takiwa kufanya ni kitu kimoja tu uweke pesa zako zote ulizo kusanya leo hapa juu ya biblia kisha geuka nyuma dakika kadhaa tukiwa tunaziombea taratibu ili uweze kuondoka gundu na mikosi.

    Baba siku hiyo alikuwa kakusanya pesa nyingi alizibeba zote na kuziweka juu ya biblia kisha akageuka kama alivyo ambiwa!



    Kipindi baba amegeuka nyumba akawauliza kinyumenyume bila kuwaona maana walikuwa nyuma yake kwamba “jamani vipi tayali mmeondoa mikosi” akaona kimya alivyo geuka hakukuta mchungaji wala mtumishi

    baba alilia kama mtoto alijigalagaza chini mpaka baadhi ya watu wakahisi labda atakuwa hayupo sawa kiakili kumbe alikuwa kachanganyikiwa tu kidogo. Huku mama yangu wa kambo na yule dada  wenyewe wa…



    Maisha ya mama yangu wa kambo na yule dada aliyetoka jela yalikuwa magumu sana.

    waliamua kuishi pamoja kuangalia kama wanaweza kufanikiwa kimaisha lakini hali ilikuwa ngumu zaidi! Maana kila kazi waliyo jaribu kuifanya ilikuwa ngumu kwa upande wao,

    Lakini yule dada alikuwa amesoma zaidi ya mama yangu wa kambo ila kutokana na ile kesi ya mauwaji ilimfanya asiaminike katika ofisi yoyote hivyo ata alipo tumia vyeti vyake kutafuta kazi ilikuwa ni ngumu sana  kupata maana alionekana ni muuwaji alie muua mmewe ili abaki na mali! Kumbe ni uongo tu masikini.Siku moja usiku wakiwa wamelala njaa bila kula!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mama wa kambo akamuuliza yule dada.Mama wa kambo,,rafiki yangu tazama leo tumelala njaa bila kuweka chochote kinywani! Hivi tutaishi maisha haya mpaka lini?

    DADA,,ata mimi sielewi kabisa maana ndugu zangu wote wamenikataa wakiamini kuwa nilimuua mme wangu, elimu yangu sasa sioni thamani yake kabisa, natamani kufa mimi niondoke kwenye hizi shida za dunia.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog