Search This Blog

A BOOK OF SATAN ( KITABU CHA SHETANI ) - 3

 







    Simulizi : A Book Of Satan ( Kitabu Cha Shetani )

    Sehemu Ya Tatu (3)



    ILIPOISHIA:

    “Natamani kuwaona mkioana na kuishi kwa amani kama mume na mke lakini kuna vikwazo vingi sana katikati yenu ambavyo vinahitaji nguvu za ziada kuvivuka,” alisema mganga Shiwinga lakini kabla hajamalizia, wote walishtushwa na muungurumo wa pikipiki iliyokuwa inakuja kwa kasi nyumbani kwa mganga huyo.

    “Mungu wangu, siyo baba huyo?” alisema Samantha kwa mshtuko mkubwa.

    SASA ENDELEA...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni yeye! Mungu wangu, hata sijui itakuwaje! Njooni huku,” alisema mganga Shiwinga huku akikimbilia kwenye chumba chake kidogo alichokuwa anahifadhia dawa na tunguli zake.

    Harakaharaka akafunua ngozi aliyokuwa ameitandika chini kisha akainama, akawa anafukua kitu ambacho hakuna aliyejua ni nini. Edmund na Samantha wakapigwa na butwaa kuona mganga Shiwinga akifungua kitu kama mlango uliokuwa umechimbiwa ardhini.

    “Kunatisha lakini hakuna namna, inabidi muingie. Msifike chini, kaeni hapa jirani kwenye ngazi,” alisema mganga huyo, Edmund na Samantha wakatazamana wakiwa ni kama hawaamini.

    Tayari mlio wa pikipiki ulikuwa unasikika jirani kabisa na pale nyumbani kwa mganga, wakawa hawana namna zaidi ya kuingia kwenye shimo hilo lenye giza totoro lililokuwa limechimbwa chini ya ardhi, ndani ya chumba cha mganga Shiwinga.

    “Naogopa.”

    “Usiogope, jikaze,” Edmund alisema huku akimkumbatia Samantha ambaye alionesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake. Mganga Shiwinga akafunga mlango kisha wakamsikia akirudisha kila kitu katika mpangilio wake wa kawaida.

    “Mbona kama kule chini kuna watu?”

    “Shhh!” Edmund alimnyamazisha Samantha aliyekuwa anaendelea kutetemeka. Japokuwa Edmund naye alikuwa akiogopa mno kutokana na mazingira ya shimo hilo, alijikaza kisabuni kwani alijua endapo baba yake Samantha atagundua kwamba yupo pale, huenda huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yake.

    “Karibu! Karibu ndani,” Edmund na Samantha walimsikia mganga Shiwinga akimkaribisha mtu, wakawa na shauku kubwa ya kusikia ni nani. Japokuwa walikuwa ndani ya shimo hilo la kutisha, waliweza kusikia kila kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba ya mganga huyo.

    “Ahsante, nimerudi tena. Nina tatizo mzee wangu,” Edmund na Samantha almanusra wafe kwa kihoro baada ya kuisikia sauti hiyo. Hakuwa mwingine bali baba yake Samantha.

    “Tatizo gani tena?”

    “Kila nikijaribu kumtafuta yule mshenzi kwenye rada zangu simuoni.”

    “Nani tena?”

    “Yule kijana ambaye Samantha alileta uzembe kwenye kukamilisha kafara lake. Mambo hayaendi vizuri, biashara zimekuwa nzito. Nahitaji kufanya kafara ili mambo yanyooke na tayari Samantha alishamuandaa japo alifanya uzembe.”

    “Mh! Kwa hiyo ulikuwa unasemaje mwanangu?”

    “Nataka unisaidie kuniongezea nguvu kidogo ili rada zangu ziweze kumnasa vizuri mahali alipo, nahitaji kukamilisha kazi yangu leoleo,” alisema baba yake Samantha, kauli ambayo ilisikika vyema kwenye masikio ya Edmund na Samantha.

    “Hilo tu, mbona kazi ndogo sana hiyo,” alisema mganga Shiwinga na kumwambia amsubiri kidogo, akaingia ndani ya chumba chake cha kuhifadhia tunguli, akachukua baadhi ya vifaa na kusogea pale kwenye mlango wa kuingilia kwenye lile shimo alimokuwemo Samantha na Edmund.

    “Msiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema mganga Shiwinga kwa kunong’ona, Samantha na Edmund wakamsikia vizuri. Kauli hiyo kidogo ilipunguza wasiwasi kwenye moyo wa Edmund, akashusha pumzi ndefu na kumbusu Samantha kwenye paji la uso, wakaendelea kukumbatiana.

    Mganga Shiwinga akatoka na kurudi pale alipomuacha baba yake Samantha, akaanza kupiga manyanga huku akiimba nyimbo ambazo si Edmund wala Samantha aliyezielewa.

    “Huyu kijana inaonesha ni mzito.”

    “Mzito kivipi baba.”

    “Inaonesha ameaga kwao, rada zangu hazimuoni kabisa. Amefanyiwa zindiko kali. Hata nikikuongeza nguvu itakuwa ni sawa na kazi bure.”

    “Sasa itakuwaje?”

    “Mi nakushauri uachane naye, tafuta mtu mwingine, huyu anaweza kukuletea matatizo zaidi. Samantha si yupo? Mwambia afanye kazi yake.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Samantha yupo, nimemuacha nyumbani, hata hajui kama nimekuja huku. Nimeona nikimshirikisha katika hili atanikwamisha kwa makusudi maana hata simuelewi,” alisema baba yake Samantha.

    “Basi inabidi muandae tukio jingine ili kutimiza hicho unachokitaka. Huyu kijana sijui anatokea wapi maana yuko vizuri sana,” alisema mganga Shiwinga, baba yake Samantha akainamisha kichwa na kutafakari kwa muda kisha akamgeukia mganga Shiwinga.

    “Basi itabidi nifanye kama ulivyoniambia, Samantha amenigharimu sana kwa sababu ya ujinga wake. Akirudia tena itabidi nimtoe yeye mwenyewe kafara, nampenda mwanangu lakini naupenda zaidi utajiri, nitakuwa sina namna,” alisema baba yake Samantha, akaingiza mkono mfukoni na kumtolea fedha mzee huyo, akamkabidhi kisha akatoka mpaka nje ambako dereva wa bodaboda alikuwa anamsubiri.

    Akaaga na kupanda bodaboda, akaondoka kwa kasi. Ni mpaka mlio wa bodaboda ulipopotelea mbali kabisa ndipo Samantha na Edmund walipoamini kwamba hatimaye wapo salama.

    “Namchukia baba.”

    “Hapana Samantha, usiseme hivyo.”

    “Namchukia sana, si umesikia mwenyewe anachokisema, eti yupo tayari hata kuniua ilimradi apate utajiri, hivi ni haki kweli hii! Eti babu ni haki kweli?” alisema Samantha huku akianza kulia, muda mfupi baada ya mganga Shiwinga kuwafungulia kutoka pale mafichoni. Edmund akawa na kazi ya ziada ya kumbembeleza.

    “Baba yako amebadilika sana siku hizi, yaani tamaa ya utajiri imemfanya aone kupoteza uhai wa mtu kuwa kazi nyepesi sana, afadhali kama Mungu ameanza kukubadilisha. Mimi huwa namsaidia tu lakini kiukweli sifurahishwi na anachokifanya,” alisema mganga Shiwinga kwa msisitizo.

    “Ahsante kwa kunitetea babu, yaani hata sijui nitawalipa nini wewe na Samantha,” alisema Edmund huku akiwa bado amemkumbatia Samantha.

    “Usijali kijana, nilishakwambia nitakusaidia, furaha yangu ni kuona unamkomboa Samantha kutoka kwenye shimo la mauti alilozama,” alisema mganga Shiwinga.

    “Naomba basi utufundishe meditation maana naona mambo yanazidi kuwa magumu.”

    “Mpo tayari?”

    “Ndiyo babu.”

    “Mbona naona mwenzako bado analia? Mbembeleze kwanza halafu inabidi tufanye harakaharaka huyu arudi nyumbani. Najua baba yake akifika lazima ataenda kumtafuta.”

    “Sawa babu, halafu nilitaka kukuuliza jambo. Mbona kwenye lile shimo ulilotufungia kama kuna watu kule chini?” alihoji Edmund, kauli iliyomfanya mganga huyo ashtuke sana, akakosa cha kujibu.



    “Edmund, mbona una maswali mengi namna hiyo? Kamuulize Samantha ndiyo anayejua kila kitu,” alisema mganga huyo huku akiendelea kuandaa mahali pa kuwafundishia wawili hao namna ya kufanya tahajudi (meditation) kama walivyokuwa wamemuomba.

    Ilibidi Edmund amfuate Samantha na kuanza kumbembeleza, akatumia uwezo wake wote kumshawishi na hatimaye akafanikiwa kumfanya atulie. Akamshika mkono na kumuinua pale alipokuwa amekaa, akamkumbatia na kumbusu kwenye paji lake la uso.

    “Usijali, haya yote yatafikia mwisho,” alisema na kumuongoza Samatha kuelekea kule mganga Shiwinga alikowaandalia sehemu ya kujifunzia tahajudi.

    “Piteni mkae,” alisema mganga Shiwinga na kuanza kuwaelekeza namna ya kukaa. Wakakaa kwa kukunja miguu yao vizuri kama alivyokuwa akiwaelekeza.

    “Lazima miguu yako uikunje vizuri kama hivi,” alisema baada ya kuona mkao huo unawashinda wote wawili, baada ya kuelekezana sana, hatimaye wote waliweza kukaa mkao huo.

    “Hakikisha mgongo unanyooka kabisa ili kuwezesha nguvu kuingia na kutoka vizuri kwenye mwili wako wakati wa kufanya tahajudi,” alisema mganga Shiwinga kisha kabla ya kuanza kuwaelekeza hatua iliyokuwa inafuatia, akaanza kuwapa maelezo muhimu kuhusu tahajudi (meditation).

    “Kama nilivyowaambia, ni vigumu kujibu swali la wewe ni nani na kwa nini upo hapa duniani lakini kupitia tahajudi, ni rahisi kujijua wewe ni nani. Nimeshawaambia, sisi siyo hii miili yetu tunayoiona, wala siyo majina yetu, kazi zetu wala vitu vinavyofanana na hivyo.

    “Wengi hawajui thamani zao ndiyo maana wanaishi maisha ya ajabu. Baba yako ni miongoni mwa watu ambao hawajui thamani zao wala hawajui thamani ya maisha ndiyo maana amefikia hatua ya kuwa kama mnyama. Sitaki na nyie muwe miongoni mwa mamilioni ya watu wasiojitambua, wanaoishi duniani leo hii.

    “Tahajudi ni chombo ambacho kitakusaidia kusafiri vizuri safari yako ya kuelekea kujitambua. Zipo aina nyingi za tahajudi lakini ambayo tutaanza nayo ni tahajudi ya pumzi au kwa Kiingereza wanaita ‘breath meditation’. Mkiifanya hiyo vizuri kwa uaminifu, hatua ya pili inaitwa Mantra.

    “Bila shaka kila mmoja wenu anajua kwamba anapumua,” aliuliza mganga Shiwinga, wawili hao wakatazamana kwani waliliona swali hilo kuwa jepesi sana.

    “Babu kwani kuna mtu ambaye hajui kwamba anapumua?”

    “Nilijua mtasema hivyo lakini ukweli ambao hamuujui, watu wengi sana wanapumua lakini hawajui kama wanapumua mpaka uwakumbushe. Najua hata nyie mlikuwa mmesahau kama mnapumua mpaka nilipowauliza swali hili.

    “Msingi wa tahajudi ya pumzi, ni kuzifuatilia pumzi zako kwa utulivu zinavyoingia na kutoka. Ukikaa na kutulia kisha ukawa unapumua kwa uhuru, ukitoa pumzi ndefu na kuvuta pumzi ndefu japo kwa nusu saa tu, huku ukijitahidi kutowaza jambo jingine lolote zaidi ya kuzitazama pumzi zako tu, ukiwa umefumba macho, hiyo ndiyo inaitwa tahajudi ya pumzi.

    “Unapoanza huwa inakuwa ngumu kama mtakavyoona lakini ukizoea unaweza hata kukaa saa tatu au nne ukiwa kwenye hali hiyo. Unajua watu wengi wanakufa kwa magonjwa mbayo yanasababishwa na msongo wa mawazo, presha au vitu vinavyofanana na hivyo, wengine wanaugua magonjwa ambayo hata vipimo mahospitalini havioneshi ni ugonjwa gani kumbe tatizo linaanzia kwenye akili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tahajudi hii ina uwezo wa ajabu wa kutuliza kabisa akili yako, kama ulikuwa na msongo wa mawazo, ulikuwa na hasira, hofu, mashaka au huzuni kali na umekata tamaa ya kuishi, ukifanya zoezi hili japo mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, utaweza kuondokana kabisa na matatizo yote hayo na taratibu utaanza kuona maisha yako yanabadilika kuanzia ndani ya mwili wako mpaka nje.

    “Sitaki niwe mzungumzaji mkubwa, nataka kila mtu ajionee mwenyewe, wote fumbeni macho na anzeni kuzifuatilia pumzi zenu kwa utulivu kabisa, mawazo yakiwa yanakuja ndani ya vichwa vyenu msiyazuie ila elekezeni ufahamu kwenye pumzi, haya moja, mbili, tatu...” alisema mganga huyo kisha wote wakafumba macho na kutulia, wakifuatilia maelekezo waliyopewa na mganga huyo.

    Utulivu wa ajabu ukatawala ndani ya nyumba hiyo, hakuna sauti wala kelele yoyote iliyosikika, kila mtu alikuwa kimya kabisa. Dakika thelathini baadaye, mganga Shiwinga alitoa ishara akiwaamuru wote wafumbue macho yao, wakatii walichoaambiwa.

    “Haiwezekani! Haiwezekani babu.”

    “Hata siamini kilichotokea, siamini... babu unataka kutufundisha uchawi?” Samantha na Edmund walikuwa wakizungumza kwa pamoja, walichokishuhudia ndani ya muda huo mfupi kiliwashangaza mno na hakuna aliyewahi kufikiria kwamba anaweza kutokewa na hali kama hiyo.

    “Leo sitaruhusu mjadala wa aina yoyote, Samantha muda umeenda sana, jiandae urudi nyumbani, kama una maswali yahifadhi utakuja kuniuliza kesho au siku nyingine, na wewe Edmund huu ni muda wa kunywa dawa,” alisema mganga Shiwinga akionesha kutotaka majadiliano nao kwani alijua kwa wakati huo hakuna ambaye anaamini alichokiona.

    “Lakini babu...”

    “Lakini nini Samantha, muda umeenda sana, rudi nyumbani baba yako atakuwa anakutafuta.”

    “Kwa hiyo naruhusiwa kwenda kufanya kama hivi tena hata nikiwa nyumbani kwetu?”

    “Ndiyo, fuata masharti kama nilivyokwambia,” alisema mganga Shiwinga, Samantha akaachia tabasamu hafifu na kumgeukia Edmund ambaye naye bado alikuwa amepigwa na bumbuwazi.

    “Umejisikiaje?”

    “Nahisi kama nilikuwa napaa angani, nimeogopa sana, sijawahi kujisikia hali kama hii hata siku moja tangu nimezaliwa.”

    “Mimi nahisi kama nilikuwa kwenye ndoto, ngoja nikifika nyumbani nitaenda kurudia tena ili nihakikishe kama ni kweli au ni ndoto,” alisema Samantha huku akianza kujiandaa.

    Japokuwa walikuwa wakilalama, ukweli ni kwamba kilichowatokea kilikuwa kigeni kabisa na kila mmoja alitamani kuendelea kuwa kwenye hali hiyo, japokuwa nafsi zao pia zilikuwa na hofu kwani walihisi kama wanafundishwa ushirikina, jambo ambalo mganga Shiwinga hakutaka kabisa kulizungumzia.

    Baada ya kumaliza kujiandaa, Samantha alimpigia simu yule dereva wake wa bodaboda ambaye walikubaliana kwamba akamsubiri kwenye barabara ya lami ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kugundua kuwa Samantha alikuwa nyumbani kwa mganga huyo.

    Wakati akiendelea kumsubiri dereva huyo wa bodaboda, Samantha na Edmund walipata nafasi ya kuzungumza kwa kina kwani sasa Edmund alikuwa na nafuu kubwa tofauti na alivyokuwa mwanzo.

    “Unanihakikishia kweli upo tayari kuondokana na mambo yote ambayo baba yako alikuwa anakutumikisha?”

    “Jamani Edmund, mpaka nimekubali kuanza kujifunza tahajudi huamini tu kwamba nahitaji kuachana na kila kitu? Nakupenda sana mwenzio, hata sielewi umenipa nini lakini amini nakwambia nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yako. Nataka hili tatizo likiisha, wewe ndiyo mwanaume wa kwanza kuujua mwili wangu,” alisema Samantha kwa sauti ya kubembeleza.

    Akawa anayazungusha macho yake mazuri huku na kule kuonesha msisitizo wa kile alichokuwa anakisema, Edmund akashusha pumzi ndefu na kutabasamu, akamkumbatia, akambusu shavuni, msichana huyo naye akafanya hivyohivyo.

    “Naomba usije kunigeuka mbele ya safari, nayakabidhi maisha yangu mikononi mwako, ni wewe pekee ndiye unayeweza kuniokoa.”

    “Usijali Edmund, ilimradi upo kwenye mikono ya babu Shiwinga, amini upo kwenye mikono salama,” alisema Samantha na kuingiza mkono kwenye pochi yake ndogo, akatoa noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi na kumkabidhi Edmund.

    “Na hizi ni za nini?”

    “Zitakusaidia kwa matumizi madogomadogo, hata kama siyo leo,” alisema Samantha huku akimshikisha Edmund fedha hizo, akaachia tabasamu pana, wakawa wanatazamana.

    “Nataka unizalie watoto wazuri kama wewe jinsi ulivyo,” Edmund alisema huku akimkumbatia tena msichana huyo, kauli hiyo ikaonesha kumfurahisha mno Samantha, akaangua kicheko cha furaha.

    “Enhee! Kuna jambo nilitaka kusahau.”

    “Jambo gani tena mpenzi wangu?”

    “Muda ule wakati tumejificha kule kwenye lile shimo wakati baba yako amekuja, kule chini si uliona kama kuna watu wengi ndani ya lile shimo? Nimemuuliza mganga Shiwinga wale ni akina nani ameniambia wewe ndiyo una majibu. Hebu naomba unieleze ukweli,” alihoji Edmund huku akiwa anamtazama Samantha machoni.

    Katika hali ambayo hakuitegemea, alishangaa kuona swali hilo limemfanya Samantha abadilike kabisa usoni, uso wake ukajaa huzuni na muda mfupi baadaye akaanza kuangua kilio. Akabaki amepigwa na butwaa. Kwa mbali, muungurumo wa bodaboda ukaanza kusikika kuashiria kwamba yule dereva alikuwa jirani akija.

    “Mbona sikuelewi? Nisamehe kama nimekosea kukuuliza,” alisema Edmund, msichana huyo akamkumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia kwa huzuni, Edmund akazidi kuchanganyikiwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Najisikia vibaya sana Edmund, kama ningekuwa naweza kurudisha siku nyuma ili niweze kurekebisha makosa yangu ningefanya hivyo.”

    “Huna haja ya kujilaumu sana Samantha, kila jambo huja kwa sababu maalum. Isitoshe mi najua wewe hupendi kuwadhuru binadamu wenzako bali unalazimishwa na baba yako.”

    “Ahsante kwa kuwa mwelewa, nakupenda sana Edmund ila naomba uniahidi kwamba hata utakapoyajua mambo yangu yote niliyowahi kufanya hutanikimbia.”

    “Usiwe na wasiwasi Samantha, nilishakwambia kwamba hata iweje siwezi kukuacha.”

    “Kweli Edmund?”

    “Kweli kabisa.”

    “Basi wale watu kwenye lile shimo kule ndani kwa mganga ni miongoni mwa wanaume waliofiakwenye mikono yangu,” alisema Samantha, kauli iliyosababisha Edmund ashtuke mno.

    “Kama sijakuelewa hivi?”

    “Unajua mtu akitolewa kafara, anakuwa hajafa kabisa mpaka sikualizoandikiwa na Mungu zifike.”

    “Unataka kusema wanakuwa bado wanaishi?”

    “Ndiyo lakini hawawi kama binadamu wa kawaida, wanaitwa misukule.”

    “Mungu wangu! Halafu inakuwaje?”

    “Ndiyo wanatumika kufanya kazi mbalimbali, wengine baba anawatuma kwenda kuiba hela kichawi kwenye mabenki na maduka makubwa,” alisema Samantha na kumfanya Edmund ahisi kwamba yupo ndotoni.

    Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana na tayari yule dereva wa bodaboda alishafika, ilibidi Samantha aondoke. Akamuacha Edmund amesimama palepale, akiendelea kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.

    “Vipi ameshaondoka?” sauti ya mganga Shiwinga ndiyo iliyomzindua Edmund kutoka kwenye dimbwi la mawazo.

    “Ndiyo, ameshaondoka,” alijibu Edmund na kushusha pumzi ndefu.

    “Vipi mbona umeduwaa? Amekujibu?”

    “Ndiyo amenijibu,” alisema Edmund na kumsogelea mganga Shiwinga, akaendelea kumdadisi maswali mengi, akitaka kujua kama alichoambiwa na msichana huyo mrembo ni kweli.

    Mganga Shiwinga alimfafanulia kila kitu, akajikuta akipatwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.

    “Wala huna sababu ya kuogopa, hawawezi kukudhuru kwa chochote.”

    “Sasa huwa wanakula nini?”

    “Chakula chao kikuba ni pumba,” alijibu mzee huyo, Edmund akaendelea kumdadisi kwa muda mrefu.

    “Inatosha sasa, maswali mengine utauliza siku nyingine,” mganga Shiwinga alimkatisha Edmund ambaye alikuwa akiendelea kuuliza maswali mengi kuhusu jambo hilo.

    Siku hiyo ilipita, mganga Shiwinga akawa anaendelea kumpa dawa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuzindika mwili wake ili baba yake Samantha asiweze kumdhuru kwa chochote. Pia aliendelea kumkazania kufanya tahajudi (meditation) mara kwa mara.

    Siku mbili baadaye, Samantha alienda tena kumtembelea nyumbani kwa mganga huyoambapo mbali na mambo mengine, walipanga watakavyokuwa wakiendesha mapenzi yaoa kwani siku za Edmund kukaa kwa mganga zilikuwa zimeisha.

    “Babu Shiwinga anasema mpaka baada ya siku arobaini ndiyoi tunaweza kukutana kimwili na wewe, anasema uchawi uliowekwa mwilini mwako utakuwa umeisha kabisa.

    “Jamani siku arobaini zote hizo, nakuhitaji Edmund, nataka nikupe zawadi yako,” alisema Samantha na kumkumbatia Edmund kimahaba.

    “Halafu nataka uhame pale unapoishi, leo nikirudi Dar nitaenda kuongea na madalali watutafutie nyumba nzuri, inabidi upate nyumba nzima mpenzi wangu ili tuwe huru,” alisema msichana huyo na kumfanya Edmund aachie tabasamu hafifu.

    Kama alivyomuahidi, kweli Samantha alivyorejea Dar, alipitiliza moja kwa moja mpaka benki ambapo alitoa fedha za kutosha kupanga nyumba nzima pamoja na kununua samani za ndani kwa ajili ya Edmund.

    Akaenda kuonana na madalali wa nyumba ambapo alipelekwa mpaka kwenye nyumba nzuri iliyopo Masaki. Kwa kuwa fedha hazikuwa tatizo kwake, siku hiyohiyo alilipa na kukabidhiwa funguo.

    Hakutaka kulaza damu, akaelekea kwenye maduka ya fenicha za kisasa ambapo alinunua vitu vingi vya thamani na kukodi gari la kuvibeba na kuwachukua watu maalum wanaofanya kazi ya kubuni mpangilio mzuri wa fenicha ndani ya nyumba.

    Ilipofika jioni, kila kitu kilikuwa kimekamilika, akafunga nyumba hiyo na kurejea nyumbani kwake, akitumia gari la kifahari, Jeep Grand Cherokee.

    “Leo umetoa fedha nyingi sana benki, umezifaanyia nini?”

    “Eeh! Baba kwani fedha si zangu au mi siruhusiwi kuchukua pesa?”

    “Mi nimekuuliza tu kwa sababu siyo kawaida yako. Halafu leo kazini hukuwepo kabisa, ulikuwa wapi?”

    “Kuna vitu nilikuwa nimeenda kununua,” Samantha alimdanganya baba yake, muda mfupi tangu aliporejea kutoka kwenye mizunguko yake. Hakutaka kumwambia chochote kuhusu Edmund na alipanga kuendelea kufanya kila kitu kuwa siri yake. Harakaharaka akapitiliza mpaka chumbani kwake kwani hakutaka baba yake aendelee kumhojihoji akihofia kwamba anaweza kujichanganya kwenye maelezo yake.

    “Nataka uwe na furaha mpenzi wangu, nitafanya kila kitu ili nikuone unafurahi,” Samantha alijisemea mwenyewe akiwa amejilaza kitandani kwake. Penzi la Edmund lilikuwa likifukuta ndani ya moyo wake.



    Siku hiyo ilipita, kesho yake Samantha akawahi kuamka kama kawaida yake na kuanza kujiandaa kuelekea kazini. Ilikuwa ni lazima afike kwanza ofisini kwake kwani alijua baba yake ameshaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu nyendo zake hivyo anaweza kuwa anamfuatilia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama kawaida yake, alitumia muda mrefu nyuma ya kioo, akajipamba na kuufanya uzuri wake wa asili uzidi kuongezeka. Akachagua nguo nzuri za ofisini na kuvaa, akamalizia kwa kujipulizia manukato mazuri ya bei mbaya, akatoka akiwa ananukia mithili ya jini.

    Akaenda mpaka kwenye maegesho ya magari yao ambapo aliingia kwenye gari lake alilokuwa akilipenda zaidi, Jeep Grand Cherokee (New Model) na safari ya kuelekea Mikocheni iliko ofisi yake ikaanza.

    Njia nzima alikuwa akiendelea kumfikiria Edmund, kila alipokuwa anakumbuka hali inayomtokea anapokumbatiana au kubusiana na kijana huyo, alikuwa akiachia tabasamu pana na kugongagonga usukani.

    Akawa na kazi ya kubadilisha nyimbo nzuri za mapenzi kwenye gari lake, hasa zile alizokuwa akizipenda zaidi, mmoja wa V- Bozeman uitwao What is Love na mwingine wa Good Enough, zote zikipatikana pia kama ‘soundtracks’ ya filamu maarufu ya mwendelezo (series) iitwayo Empire ambayo nayo alikuwa akipenda sana kuitazama anapokuwa nyumbani kwao.

    Safari iliendelea, akafika mpaka eneo la Sinza Afrika Sana, eneo ambalo kwa mara ya kwanza alikutana na Edmund baada ya dereva wa bodaboda aliyekuwa amembeba kijana huyo kuligonga gari la Samantha kwa nyuma.

    “Ama kweli mapenzi yana namna nyingi za kukutana, ajali imesababisha nimempata mwanaume wa maisha yangu, nakupenda sana Edmund,” alisema Samantha huku safari hii akishindwa kujizuia kuangua kicheko.

    Kama gari lake lisingekuwa na vioo vyeusi (tinted) huenda watu ambao wangefanikiwa kumuona wangehisi msichana huyo mrembo amechanganyikiwa kwani alikuwa anacheka wakati hakukuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya gari.

    Akaendelea na safari, alipofika eneo la Bamaga, mahali Edmund alipokuwa akifanyia kazi, aliachia tena tabasamu na kuendelea na safari yake mpaka Mikocheni. Akaingiza gari lake mpaka sehemu ya maegesho ambapo mlinzi wa kike alifika haraka na kumpokea mkoba wake uliokuwa na ‘laptop’ na kumsaidia kuuingiza mpaka ofisini kwake.

    Kwa kuwa hakufika kazini hapo kwa siku kadhaa, alikuta kazi nyingi zikiwa zimerundikwa kwenye meza yake, jambo ambalo lilimkasirisha kwani alijua atachelewa kutoka kwa ajili ya safari ya kumfuata mpenzi wake Edmund.

    “Naomba akija mtu yeyote kuniulizia mwambie niko bize,” alisema Samantha kwa ukali akimpa maelekezo katibu muhtasi (secretary) wake, kisha akaanza kufanya kazi harakaharaka. Alikagua mafaili ya mizigo iliyoingia na kutoka kwa siku zote ambazo hakukaa ofisini, akakagua pia ripoti ya mhasibu kuhusu fedha zilizoingia pamoja na zile zilizotumika.

    Alihakiki oda za wateja na kuidhinisha wapelekewe bidhaa walizokuwa wanazihitaji kisha baada ya hapo, akiwa ameshapunguza karibu nusu ya mafaili aliyotakiwa kuyakagua, alimuita sekretari wake.

    “Nimepunguza kazi kidogo lakini nina dharura nataka kutoka mara moja, baba akiniulizia mwambie nimeenda kwenye kikao cha bodi ya wakurugenzi, hizo kazi nyingine nitakuja kumalizia nikirudi,” alisema Samantha huku akichezeshachezesha funguo ya gari mkononi.

    Baada ya kumpa maelekezo hayo sekretari wake, alitoka mpaka kwenye maegesho ya magari, akaingia kwenye gari lake na safari ya kuelekea Bagamoyo ikaanza mara moja. Kabla hajafika mbali aliingia kwenye ‘supermarket’ na kununua zawadi mbalimbalai kwa ajili ya Edmund kisha akaendelea na safari.

    Njia nzima aliendelea kumuwaza Edmund, baada ya safari iliyochukua takribani dakika arobaini, tayari Samantha alikuwa ameshawasili Bagamoyo. Akaenda kupaki gari lake kwenye hoteli moja maarufu kwa ajili ya usalama kisha akakodi bodaboda iliyompeleka mpaka kijijini kabisa alikokuwa anaishi mganga Shiwinga.

    Baada ya kuwasili, Samantha na Edmund kama kawaida yao, waligandana kama ruba kwa dakika zisizopungua tano, wakibusiana na kukumbatiana huku kila mmoja akiwa na furaha ya ajabu. Mganga Shiwinga aliwaachia nafasi, yeye akaendelea na shughuli zake za kuandaa dawa huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.

    Baada ya kila mmoja kutulia, mganga Shiwinga hakutaka kupoteza muda, aliwaingiza sehemu ya kufanyia tahajudi na kazi ikaanza. Tofauti na jana yake ambapo wawili hao walianza kufanya ‘meditation’ kwa mara ya kwanza, safari hii walionekana kuwa watulivu zaidi, wakionesha kuelewa walichokuwa wanakifanya.

    Mganga Shiwinga aliwaongezea muda, wakafanya kwa saa moja mfululizo, alipowaambia wafumbue macho, kila mmoja alionesha kuwa na mabadiliko makubwa mno.

    “Babu mbona najisikia hivi?”

    “Unajisikiaje kwani Edmund.”

    “Najiona kama nimekamilika mno, zile hofu, wasiwasi, mashaka na hisia za namna hiyo hazipo tena. Akili yangu imetulia sana na nahisi kujiamini mno kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu.”

    “Sasa wewe hupendi kuwa hivyo?”

    “Napenda sana babu, lakini mbona sijawahi kuwa hivi?”

    “Kwa sababu hukuwahi kufanya tahajudi. Wewe Samantha unajisikiaje?”

    “Na mimi najihisi hivyohivyo, halafu naona kama mwili wangu unakuwa mwepesi sana, utafikiri mwanzo nilikuwa nimebebeshwa gunia la mchanga, kwa kifupi najisikia raha sana, nataka tufanye tena,” alisema Samantha na kusababisha wote waangue vicheko.

    Mganga huyo akaendelea kuwaambia kuwa wakiendelea na utaratibu huo, kwa muda wa wiki moja tu, nguvu zote mbaya zilizokuwa kwenye mwili wa Samantha zitakuwa zimefifia kabisa kiasi kwamba hataweza kumsababishia tena madhara Edmund hata wakikutana kimwili, jambo ambalo wote walilichekelea.

    “Sijamaanisha mnaruhusiwa kukutana kimwili kabla hamjaoana, itabidi mjizuie mpaka mipango yote ya ndoa itakapokamilika maana vijana wa siku hizi hamuaminiki nyie,” alisema mganga Shiwinga, Edmund na Samantha wakatazama na kukonyezana.

    Mganga Shiwinga aliendelea kuwafundisha mambo mengi ambayo hakuna aliyewahi kuyasikia hata mara moja.

    “Binadamu tumeumbwa kwa namna ambayo nafsi zetu zinatafuta sana ukamilifu. Na inapotokea nafsi yako inaanza kutafuta ukamilifu, ndipo unapoanza kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Kwa mfano utajiuliza kwa nini ulizaliwa, lengo la kuishi kwako hapa duniani ni nini na vitu vya mfano huo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pia utajiuliza maswali mengi kuhusu mazingira yanayokuzunguka, kwa mfano milima ilitokeaje? Inakuwaje mpaka mbegu inaota na kuwa mmea mkubwa, utajiuliza kwa nini maua yanakuwa na rangi nyingi tofautitofauti na utajiuliza ni nani anayesimamia mambo yote haya yanayoendelea kwenye ulimwengu.

    “Ukifikia hatua hiyo, tunasema kwamba nafsi yako inakuwa imeanza kuamka au kwa Kiingereza inaitwa ‘spiritual awakening’. Huu ni mwanzo wa safari ya kiroho ambayo ni binadamu wachache sana wanaofikia. Wengine wanaifikia kwa kupitia dini, kwamba unakuta mtu anakuwa ni wa maombi sana au anaswali sana, basi huyo naye anakuwa amefikia hatua ya nafsi kuamka.

    “Nafsi ikiamka inakufanya utambue kwamba kumbe mambo yote yanayoendelea kwenye hii dunia, hayatokei kwa sababu yametokea tu, kwa lugha nyepesi tunasema hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya. Watu wanazaliwa, watu wanakufa, mimea inaota, inachanua na kutoa mbegu, upepo unavuma, mvua zinanyesha, jua linawaka na mambo mengine chungu nzima, hakuna linalotokea kwa bahati mbaya.

    “Lazima ipo nguvu ambayo ndiyo inayoratibu mambo yote haya, swali ambalo nafsi ya mtu iliyoanza kuamka inakuwa inajiuliza mara kwa mara ni je, ni nguvu gani au ni nani anayeratibu mambo yote haya? Kwa wanaoamini katika dini, wanaamini kwamba Mungu ndiye anayeratibu yote haya na ni katika kipindi hiki ambacho hujisogeza karibu zaidi na Mungu wao.

    “Kwa ambao hawaamini katika dini, pia huamini kwamba kuna nguvu kuu au kwa Kiingereza huitwa ‘universal power’; ambayo ndiyo inayoamua nini kitokee wapi na kwa sababu gani. Vyovyote ambavyo utaiita nguvu hii, iwe ni Mungu, nguvu kuu au vyovyote, hii ndiyo nguvu inayoamua aina ya maisha utakayoishi, uwe unajua au uwe hujui.

    “Kwa kawaida kila binadamu anazalisha nguvu kwa hiyo ukiona mtu anafanikiwa sana maishani mwake, maana yake ni kwamba anazalisha nguvu chanya na ukiona mtu anaishi maisha ya kimaskini au anaandamwa na mabalaa ya kila aina, ujue anazalisha nguvu, iwe anajua au hajui,” alisema mganga Shiwinga na kusababisha wote wawili washushe pumzi ndefu, Samantha na Edmund wakatazamana kwani walichokisikia kilikuwa kitu kipya kabisa kwao.



    Mganga Shiwinga aliwafundisha vitu vingi mno, akaendelea kuwafanyia dawa mpaka aliporidhika kwamba Samantha hawezi tena kumdhuru Edmund. Akawaruhusu kuondoka huku akiwasisitiza kufuata maelekezo aliyowapa.

    Wakaondoka na safari ya kurudi Dar es Salaam ikaanza. Kwa jinsi Samantha alivyokuwa na shauku, aliona kama wanachelewa kufika. Hatimaye waliwasili Dar na kwenda moja kwa moja mpaka Sinza Vatican.

    “Edmund.”

    “Nambie mpenzi wangu.”

    “Yaani nimefurahi sana mganga Shiwinga alivyotusaidia na kurahisisha kazi. Unajua nilipokuwa nafikiria kuendelea kukusubiri kwa siku arobaini nilikuwa najisikia vibaya sana.”

    “Siyo wewe tu mpenzi wangu, hata mimi pia nilikuwa najisikia vibaya lakini nashukuru ameturahisishia kazi, si unaona hata hazijafika na tayari tupo huru! Niambie unajisikiaje kuwa na mimi?”

    “Yaani maneno ya kutosha kuelezea jinsi ninavyojisikia hayapatikani. Nakupenda sana mwenzio,” alisema Samantha na kumkumbatia Edmund kwa nguvu, kila mmoja akajihisi mkondo wa ajabu ukitembea ndani ya mishipa yake ya damu.

    “Nakupenda pia mke wangu mtarajiwa.”

    “Edmund! Umeniitaje?”

    “Mke wangu mtarajiwa.”

    “Whaoo! Nimefurahi sana kusikia ukiniita hivyo, natamani ufike muda ambao utakuwa unaniita mkeo tena kihalali kabisa.”

    “Usijali, hilo litatimia. Ila kuna kitu kimoja naomba nikuulize.”

    “Uliza tu mpenzi wangu,” alisema Samantha huku akimtazama Edmund kwa macho kama ya mtu anayesikia usingizi.”

    “Siku ile uliniambia umepata nyumba Masaki lakini hapa ni Sinza Vatican. Imekuwaje? Halafu unanihakikishiaje usalama wangu? Baba yako akijua kwamba nipo hapa huoni kwamba huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yangu?”

    “Ni kweli kuna nyumba nyingine nimepanga Masaki na ina kila kitu ndani lakini nahisi kama baba alituma watu wanichunguze siku wakati nahamishia samani nilizonunua kwa ajili yako. Machale yakanicheza kwa sababu namfahamu baba yangu, akishatilia shaka jambo lazima ataufahamu ukweli ndiyo maana nimeamua kutafuta huku kwenye mchanganyiko wa watu.”

    “Maskini mpenzi wangu, si unatua fedha nyingi sana kwa ajili yangu?”

    “Usijali kuhusu fedha, kwanza nilipanga ukirudi wewe ndiyo utafute madalali wa kuipangisha ile nyumba ya kule kwa mteja mwingine mpaka kodi yangu itakapoisha, baada ya hapo tutatafuta nyumba kubwa zaidi ili tuchanganye vitu vya kule na huku, nataka kujenga familia na wewe mpenzi wangu.”

    “Kwa hiyo na kule kuna vitu kama hivi?”

    “Ndiyo, kama hivihivi, halafu unauliza kama hivi kwani umeviona vyote? Hebu njoo nikutembeze ujionee mwenyewe,” alisema Samantha na kumpiga Edmund kimahaba mgongoni kisha akamshika mkono Edmund, akaanza kumtembeza kuanzia jikoni, wakaenda sehemu ya kulia chakula, wakaenda bafuni na chooni, wakarudi tena sebuleni na mwisho wakaingia kwenye chumba cha kulala.

    “Hapa ndiyo tutakapokuwa tunalala.”

    “Whaoo!” Sijawahi kulalia kitanda kikubwa na kizuri kama hiki,” alisema Edmund na kujirusha juu ya kitanda kikubwa na cha kisasa, Samantha naye akamfuata kwa juu, wakawa wananesanesa juu ya godoro kubwa huku kila mmoja akionesha kuwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake.

    Samantha ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanza ‘uchokozi’, akamsogelea Edmund wakiwa wamejilaza palepale juu ya kitanda, taratibu akausogeza mdomo wake karibu na wa Edmund, wakagusanisha ndimi zao, kitendo kilichosababisha Samantha aanze kuhema kwa nguvu mithili ya mtu aliyetoka kukimbia mbio za mita mia moja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali haikuwa tofauti sana kwa Edmund, japokuwa nyumba hiyo ilikuwa na kiyoyozi, alijikuta kijasho chembamba kikimtoka. Hakutaka kuamini kwamba hatimaye ile siku aliyokuwa anaisubiri kwa hamu kubwa, hatimaye ilikuwa imewadia.

    Kwa jinsi alivyokuwa anampenda msichana huyo kwa dhati, kutoka ndani kabisa ya moyo wake, hakutaka kulaza damu. Akamsogeza karibu zaidi na kumkumbatia kwa nguvu huku wakiendelea kugandana kama ruba. Japokuwa Edmund hakuwa fundi kwenye uwanja huo wa kikubwa, alijikakamua kadiri ya uwezo wake.

    Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Samantha, japokuwa hiyo haikuwa mara yake ya kwanza kubaki wawili tu na mwanaume chumbani, lakini mara zote alikuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kazi maalum na hakuwahi kuwa na hisia kama alizokuwa nazo siku hiyo.

    Hata wanaume wote aliowahi kuwa nao mara kadhaa chumbani, waliishia tu kumbusu na kumkumbatia kisha akatimiza alichotumwa na baba yake lakini siku hiyo hali ilikuwa tofauti kabisa. Kutoka ndani ya moyo wake alikuwa tayari kumruhusu Edmund avuke mipaka ambayo hakuna mtu aliyewahi kuivuka tangu azaliwe, kila mmoja akawa anavuta pumzi ndefu huku mapigo ya moyo yakiongezeka.

    “Edmund,” aliita Samantha kwa sauti ya kunong’ona iliyotokea puani, akajibiwa kwa sauti ya kugugumia, Samantha akaendelea:

    “Unanipenda kweli?”

    “Nakupenda sana, tena zaidi ya sana.”

    “Nikikupa mwili wangu hutanichezea na kuniacha?”

    “Nakuapia Samantha, utakuwa peke yako ndani ya moyo wangu, niamini,” alisema Edmund kwa sauti ya kubembeleza huku mikono yake ikiendelea kuvinjari sehemu mbalimbali za mwili wenye mvuto wa kipekee wa msichana huyo mrembo, hali iliyomfanya awe anaweweseka kama yupo ndotoni.

    Kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo hali ilivyokuwa inazidi kubadilika kwa kila mmoja, Edmund akawa anameza mate kama fisi aliyeona mfupa, kwa ujanja wa hali ya juu akafanikiwa ‘kumsaula’ Samantha kisha na yeye akafanya hivyohivyo, muda mfupi baadaye, wote wakawa wamevaa ‘suti za kulalia’, wakagandana tena kama ruba, safari hii kila mmoja akilihisi vilivyo joto la ngozi ya mwenzake.

    Miguno ya kimahaba ikaendelea kusikika hapa na pale huku hisia tamu zikiendelea kupita kwenye kichwa cha kila mmoja, kufumba na kufumbua sijui Edmund alifanya nini, akampindua Samantha na sekunde chache baadaye, msichana huyo alionekana kuuma meno kama mtu anayeugulia maumivu makali kuliko kawaida lakini Edmund hakujali chochote.

    Alitumia nguvu kubwa na hatimaye akafanikiwa kuivunja ‘ngome’ imara ya mpinzani wake, Samantha akashindwa kujizuia na kupiga kelele kwa nguvu akiugulia maumivu makali aliyokuwa anayahisi lakini bado Edmund hakujali, akaendelea kufanya alichokuwa anakifanya. Ilibidi Samantha atumie nguvu, akamtoa na kumsukumia Edmund pembeni huku akiendelea kuugulia maumivu makali.

    “Mungu wangu, kumbe ulikuwa unasema kweli? Ahsante Samantha kwa zawadi hii,” alisema Edmund huku akionesha kushtushwa mno na alichokiona pale kitandani. Eneo lote lilikuwa limebadilika na kuwa kama machinjioni, rangi nyekundu ilisambaa kila sehemu.

    Samantha hakumjibu chochote zaidi ya kuendelea kuugulia maumivu makali, ikabidi Edmund aanze kazi nyingine ya kumbembeleza lakini haikuwa rahisi. Samantha alionesha kumchukia mno Edmund kwa wakati huo na hakutaka hata kumsikia, Edmund akawa anaendelea kumbembeleza kwa maneno ya upole yaliyoonesha kumuingia msichana huyo, taratibu hasira zake zikaanza kupungua lakini bado hakutaka Edmund amguse huku akimlaumu kwa kutomuonea huruma.

    “Sasa unafikiri nitarudije nyumbani?” alisema Samantha kwa sauti ya chini iliyoonesha bado yupo kwenye maumivu makali. Kabla hata Edmund hajajibu chochote, simu ya msichana huyo ilianza kuita mfululizo, awali hakutaka hata kuisikia lakini alipoona inaendelea kuita, ilibidi amuagize Edmund amchukulie kwani hakuwa hata na uwezo wa kuinuka pale alipokuwa.

    “Uko wapi wewe mtoto? Nataka urudi nyumbani haraka iwezekanavyo, nakupa dakika kumi,” aling’aka baba yake Samantha na kabla hajajibu chochote, tayari simu ilikuwa imeshakatwa.



    “Vipi!”

    “Baba! Anafoka hatari.”

    “Sasa itakuwaje?”

    “Hebu fanya haraka nenda hapo dukani kaninunulie dawa inaitwa Flamar-X, inasaidia kupunguza maumivu, ni lazima niende nyumbani sasa hivi, inaonesha kuna tatizo kubwa,” alisema Samantha kwa sauti iliyoonesha kwamba bado anaugulia maumivu, harakaharaka Edmund alikimbilia bafuni na muda mfupi baadaye, alitoka akiwa ameshaoga.

    Akajiandaa harakaharaka na kutoka kuelekea dukani. Kwa kuwa alikuwa mgeni mtaani hapo, ilimlazimu kuuliza kwa wenyeji, akaelekezwa ambapo muda mfupi baadaye tayari alikuwa ameshapata alichoagizwa. Akarudi ndani na kumkuta Samantha naye ameshaenda kuoga.

    Akawa anajiandaa na muda mfupi baadaye, tayari alishamaliza, akanywa dawa.

    “Inabidi ujifunze kuendesha gari bwana, huoni kama sasa hivi ungenisaidia kunipeleka mpaka nyumbani? Yaani naumwa hapa najikaza tu,” alisema Samantha, akamkumbatia Edmund na kumbusu mdomoni kimahaba kisha wakaagana.

    “Usiende popote, funguo zile pale mezani,” alisema Samantha na kutoka huku akijivuta mpaka kwenye gari lake lililokuwa limepaki nje ya nyumba hiyo. Akaingia na kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwao.

    Huku nyuma, Edmund alibaki akichekacheka mwenyewe kama mwendawazimu. Hakutaka kuamini kwamba kweli Samantha, licha ya uwezo mkubwa wa kifedha na urembo usio na kifani, hakuwa akimjua mwanaume mpaka umri huo. Kwake huo ulikuwa ni zaidi ya ushindi, akajiapiza kumpenda kwa moyo wake wote na kujiepusha na jambo lolote ambalo lingeweza kumuumiza moyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Harakaharaka alibadilisha mashuka chumbani na kwenda kuyaloweka bafuni kwa ajili ya kuyafua kisha kwa mara nyingine akaanza kukagua kitu kimoja baada ya kingine ndani ya nyumba hiyo.

    Maisha aliyokuwa akiishi awali yalikuwa tofauti kabisa na maisha mapya. Kila kitu kilikuwa kigeni kwake, akajikuta akipiga magoti na kuinua mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu kwani japokuwa alikuwa na ndoto za siku moja kuishi maisha ya kifahari kama hayo, alikuwa anajua isingekuwa rahisi kuyafikia kama ilivyotokea.

    Baada ya kuridhika, alienda kukaa kwenye masofa ya kifahari pale sebuleni na kuwasha runinga kubwa ya ukutani (flat screen). Akawa anaendelea kuchekacheka mwenyewe, wakati mwingine akijihisi yupo kwenye ndoto tamu ambayo itaisha muda wowote.

    ***

    “Umefanya nini Samantha!”

    “Kwani vipi baba?”

    “Unaweza kuniambia ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini? Usinifiche kwa sababu najua kila kitu.”

    “Nilikuwa kwa rafiki yangu Aneth, leo ni ‘bethidei’ yake.”

    “Usinidanganye Samantha, najua kila kitu,” alisema baba yake Samantha huku akionesha kuchanganyikiwa kuliko kawaida. Licha ya ukali wake wote, Samantha hakuwahi kumuona baba yake akiwa kwenye hali kama hiyo.

    Alionesha kuchanganyikiwa mno, akawa anaongea peke yake kama mwendawazimu huku akitembea kutoka kona moja ya sebule mpaka nyingine.

    “Mama kwani nini kimetokea?”

    “Maduka mawili ya baba yako yameungua katika mazingira ya kutatanisha, tena yote kwa wakati mmoja. Lile la Kariakoo na jingine la Posta,” alisema mama yake Samantha, kauli ambayo ilimshtua mno Samantha, akajua kazi imeanza.

    Harakaharaka alikimbilia chumbani kwake na kujifungia. Alijua lazima baba yake amejua kwamba ameingiliwa na mwanaume kwani siku zote alikuwa akimuonya kwamba kitendo cha kufanya mapenzi na mwanaume yeyote, kingemaanisha kuanza kupotea kwa utajiri mkubwa walioutafuta kwa kipindi kirefu.

    Samantha aliendelea kuwaza kwa muda mrefu lakini baadaye akaamua kupiga moyo konde kwani alichokuwa anakitaka kwa kipindi kirefu, ilikuwa ni kuondokana na maisha ya kitumwa, jambo ambalo hatimaye lilikuwa limetimia.

    Akili zake zilitua kwenye tukio walilolifanya muda mfupi uliopita na Edmund, japokuwa alikuwa kwenye maumivu makali, alishindwa kulizuia tabasamu pana lisiupambe uso wake.

    Kwa kitendo walichokifanya na Edmund, alijikuta akizidi kumpenda kijana huyo na kutamani muda wote awe pembeni yake. Aliendelea kuwaza huku tabasamu pana likiwa limemtawala, hakutaka kuumiza kichwa chake kwa kuendelea kuwaza matatizo ya baba yake kwani aliona kama amejitakia.

    Kutokana na jinsi alivyokuwa amechoka, alijikuta akipitiwa na usingizi mzito. Akalala fofofo mpaka alipokuja kuzinduliwa na kelele za mlango uliokuwa unagongwa na mama yake. Harakaharaka akafungua mlango, mama yake akaingia chumbani kwake.

    “Samantha.”

    “Abee mama.”

    “Mbona umelala muda huu wakati siyo kawaida yako?”

    “Najihisi kuchoka mama. Vipi baba amefikia wapi?”

    “Ameondoka, yaani amechanganyikiwa kuliko kawaida. Hakuna kitu kilichookolewa kwenye maduka yote mawili, vitu vyote vimeteketea kabisa. Lakini kwa sababu ya ubishi wa baba yako, kila siku mimi namwambia aachane na huu utajiri wa kishirikina hanisikii, ngoja yamkute,” alisema mama yake Samantha huku akikaa vizuri kwenye kitanda cha binti yake.

    Samantha hakuwahi kumsikia mama yake akizungumzia jambo hilo hata siku moja. Mara zote, alikuwa anajua kwamba mama yake anamuunga mkono baba yake, kauli hiyo ikamfanya ashushe pumzi ndefu huku akijishauri kama amueleze ukweli kuhusu Edmund au la!

    “Vipi, mbona unaonekana una mawazo?”

    “Nafikiria matatizo yaliyomtokea baba.”

    “Achana naye, anazeeka vibaya huyo. Halafu hivi wewe hujawahi kufikiria kutafuta mwanaume wa kukuoa hata mara moja? Natamani kuwa na wajukuu kama wanawake wenzangu, huu utajiri si lolote kwani tutakufa na kuuacha,” alisema mama yake Samantha, kauli iliyozidi kumuweka njia panda mwanaye. Kuna wakati alihisi huenda mama yake anamtega akitaka kuujua ukweli lakini upande mwingine ukamfanya kuamini kwamba alikuwa anamaanisha kile anachokisema.

    Mwisho aliamua kupiga moyo konde, akakaa pale kitandani vizuri na kumgeukia mama yake.

    “Mama.”

    “Abee mwanangu.”

    “Kuna jambo nimekuwa nataka kukwambia kwa kipindi kirefu lakini nimekuwa naogopa.”

    “Wewe na baba yako lenu si moja! Mnaona utajiri ndiyo jambo la maana. Angalia hata hutaki kuwa karibu na mimi mama yako, wewe na baba yako tu! Haya niambie nini kimekusibu,” alisema mama yake Samantha huku na yeye akijiweka sawa kutaka kusikia mwanaye anataka kumwambia nini.

    “Naomba unisamehe lakini kama nitakuwa nimekukosea mama.”

    “Usijali mwanangu, kuwa huru kuzungumza kitu chochote unachotaka. Mimi ndiyo mama yako.”

    “Mi nina mpenzi mama.”

    “Mpenzi? Nilivyokwambia kuhusu suala la mchumba nilitaka uniachie mimi ndiyo nikusimamie kukutoa hayo mashetani yanayoua wanaume kwanza ndiyo mengine yafuatie. Wewe si unajua matatizo yako? Sasa naye si atakufa kama hao wengine walivyokufa?”

    “Hapana, hawezi kufa mama. Kuna jambo nimefanya ila nakuomba sana usimwambie baba,” alisema Samantha kwa sauti ya chini, akaanza kumsimulia mama yake kila kitu, kuanzia jinsi alivyokutana na Edmund, alivyomkosakosa kumuua na yote yaliyofuatia baada ya hapo.

    “Mh! Makubwa, hebu kaniletee maji ya kunywa kwanza nishushie,” alisema mama yake Samantha huku akishusha pumzi ndefu. Samantha akajikaza kisabuni na kuinuka pale kitandani kwani bado alikuwa anahisi maumivu makali kutokana na tukio lililotokea kati yake na Edmund, saa chache zilizopita.

    Mabadiliko ya namna alivyokuwa anatembea, yalimshtua mno mama yake, kwa kuwa yeye ni mtu mzima, akawa ameshaelewa kilichotokea ingawa bado alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia kutoka kwa Samantha mwenyewe.

    Muda mfupi baadaye, Samantha alirejea akiwa na chupa ya maji baridi pamoja na glasi, akammiminia mama yake kisha akarudi kukaa kitandani. Mama yake akayanywa maji hayo huku akiendelea kumchunguza kwa macho ya udadisi. Alipomaliza akakaa vizuri tena pale kitandani na kumgeukia Samantha.

    “Kuna jambo moja bado hujaniambia ukweli.”

    “Jambo gani mama?”

    “Hujamaliza kuniambia kuhusu wewe na huyo Edmund wako. Mmeshawahi kukutana kimwili mara ngapi?” alihoji mama yake Samantha huku akiwa amemkazia macho mwanaye. Swali hilo lilimshtua mno Samantha kwani alijua mama yake ameshamshtukia na miongoni mwa mambo aliyokuwa akimuonya mara kwa mara, ilikuwa ni kutokutana kimwili na wanaume.

    “Mbona hujibu?” mama yake Samantha alizidi kumbana binti yake kwa maswali, Samantha akawa anang’atang’ata kucha huku akiogopa hata kumtazama mama yake usoni. Baada ya kumbana sana, ilibidi Samantha awe mkweli, akamwambia kuwa siku hiyo ndiyo ilikuwa mara yao ya kwanza.

    “Nilijua tu! Niliposikia maduka mawili ya baba yako yameungua nilijua ni kwa sababu gani, si ajabu hata yeye mwenyewe anajua na ndiyo maana amechanganyikiwa sana. Umekosea mwanangu! Umefanya kosa kubwa sana.”

    “Nisamehe mama!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi sina tatizo, ila baba yako anaweza hata kukuua, ilibidi uniambie kabla! Majanga makubwa sana yanakuja,” alisema mama yake Samantha huku naye akionesha kuchanganyikiwa mno. Ukimya mkubwa ukapita kati yao.

    Walikuja kuzinduliwa na kelele za mlango uliokuwa ukigongwa kwa nguvu, wakajua kazi imeanza kwani hakuwa mwingine zaidi ya baba yake Samantha.

    “Fungua kabla sijauvunja huu mlango,” alifoka baba yake Samantha, ikabidi mama yake Samantha ndiyo ainuke na kuufungua mlango huo ambao Samantha aliufunga kwa ndani alipompelekea mama yake maji.



    “Kumbe wewe na mwanao ndiyo mnafundishana ujinga si ndiyo?” alifoka baba yake Samantha baada ya kumkuta mkewe akiwa ndani ya chumba cha binti yao.

    “He! Mwenzetu vipi? Mbona umekuwa hivyo? Hebu tulia utueleze nini kimetokea.”

    “Wewe ni binti yako mnajua! Mnajua kabisa mlichokifanya, ‘sheli’ yangu ya Kibaha nayo imewaka moto,” alizidi kufoka baba yake Samantha. Kila mmoja akapatwa na mshtuko kufuatia habari hizo kwani ndani ya muda mfupi tu, vitega uchumi vitatu vilikuwa vimeteketea kwa moto.

    Duka la Kariakoo na jingine la Posta yote yalikuwa yameungua na sasa ilikuwa ni kituo cha mafuta cha Kibaha.

    “Umeanza umalaya si ndiyo? Sasa leo nitakukomesha,” alisema baba yake Samantha huku akikunja mikono ya shati alilokuwa amevaa na kuvua tai yake lakini kabla hajafanya chochote, mama yake Samantha aliingilia kati kwani alijua mumewe alivyokuwa na hasira chochote kinaweza kutokea.

    Kitendo cha yeye kuingilia kati na kuanza kumtetea Samantha ilikuwa sawa na kumwagia petrol kwenye moto, kwa jazba kama faru aliyejeruhiwa, baba yake Samantha alimkamata mkewe na kuanza kumshushia kipigo kwa hasira.

    Samantha alitumia upenyo huo kuchoropoka, alichokumbuka kubeba ilikuwa ni pochi yake ndogo tu, akatoka mbio mpaka nje akiwa pekupeku, akikimbia mpaka getini, jambo lililomshangaza sana mlinzi wao.

    “Kuna nini Samantha?”

    “Baba anamuua mama, nifungulie geti,” alisema Samantha, harakaharaka mlinzi huyo bila kufikiria mara mbili akamfungulia Samantha mlango. Japokuwa alikuwa anasikia maumivu makali, Samantha alijikaza na kukimbia mpaka barabarani. Kwa bahati nzuri, kuna pikipiki ilikuwa inakuja, akaipungia mkono kwa nguvu huku akiwa amechanganyikiwa, ikasimama.

    Kabla hata hajapanda, alisikia geti lao likifunguliwa, akamuona baba yake akitoka mbio kumfukuza, harakaharaka akapanda na kumhimiza dereva huyo kuondoka kwa kasi kubwa, jambo alilolitii. Akaondoa pikipiki kwa kasi kubwa na kumuacha baba yake Samantha mita chache nyuma, akiendelea kutoa vitisho vya hali ya juu.

    Alipoona Samantha amemkimbia, harakaharaka alirudi ndani na kuwasha gari, wakiwa umbali wa takribani mita mia tatu, Samantha aligeuka nyuma na kuona gari likitoka kwa kasi kwenye geti, akajua ni baba yake ameamua kumfuatilia.

    Kwa jinsi alivyokuwa anamfahamu baba yake, alijua akizembea anaweza kumdhuru vibaya, akamhimiza dereva kuongeza kasi na kumtaka wapite njia za vichochoroni, jambo ambalo alilitii.

    “Kwani tunaenda wapi sista?”

    “Sinza Vatican, pita vichochoroni baba anakuja, ukinifikisha nitakupa kiasi chochote cha fedha unachokitaka,” alisema Samantha huku akihema kwa nguvu, utulivu ukiwa umemuisha kabisa.

    Kwa bahati nzuri, dereva huyo wa bodaboda alikuwa na uzoefu wa kutumia pikipiki hiyo, akafanya kama mteja wake alivyomuelekeza, muda mfupi baadaye wakawa wameshampoteza kabisa baba yake Samantha. Bodaboda ikawa inakatiza vichochoro kwa kasi kubwa, hali iliyomshtua kila aliyeiona.

    ***

    “We kijana! Kijanaa!”

    “Naam bosi, unahitaji usafiri?”

    “Kuna bodaboda imepita sasa hivi kwa kasi kubwa imeelekea huku vichochoroni, umeiona?”

    “Ndiyo mzee.”

    “Nataka ufanye kila unachoweza kuhakikisha tunaikimbiza mpaka tunaipata. Nitakupa kiwango chochote cha fedha unachokitaka. Hili gari naweza kulipaki hapa?”

    “Hakuna tatizo, lipaki tu kuna ulinzi wa kutosha ingawa itabidi ulipie.”

    Sekunde chache baadaye, baba yake Samantha naye alikuwa juu ya bodaboda, akifuata njia ileile ambayo yule dereva aliyempakiza mwanaye amepitia, akawa anamhimiza dereva kuzidi kuongeza kasi.

    Sekunde chache baadaye, baba yake Samantha naye alikuwa juu ya bodaboda, akifuata njia ileile ambayo yule dereva aliyempakiza mwanaye amepitia, akawa anamhimiza dereva kuzidi kuongeza kasi.

    Dereva bodaboda aliyekuwa amempakiza Samantha alizidi kuchanja mbuga, akawa anakatiza mitaani kwa kasi kubwa huku akitumia uwezo wake wote kuhakikisha anatimiza alichoambiwa na mteja wake.

    Huku nyuma, dereva mwingine aliyekuwa amembeba baba yake Samantha naye alikuwa akikimbiza pikipiki kwa kasi kubwa akijaribu kuwafuata akina Samantha. Kila alipohisi amepotea, alikuwa akisimama na kuuliza kwa wenyeji kama wameiona bodaboda yoyote iliyopita kwa kasi eneo hilo, wakawa wanaelekezwa.

    Safari iliendelea kwa kasi kubwa utadhani madereva wapo kwenye mashindano ya mbio za pikipiki maarufu duniani, MotoGP lakini haikuwa hivyo. Baada ya kukimbizana kwa umbali mrefu, dereva aliyekuwa amembeba Samantha alifanikiwa kuwapoteza ‘maboya’ baada ya bodaboda nyingine kadhaa kuingia katikati yao.

    “Washenzi kabisa hawa lakini najua wameelekea wapi, hebu geuza tuelekee Masaki,” alisema baba yake Samantha kwa hasira baada ya kugundua kuwa tayari wamewaacha kwenye mataa. Dereva huyo wa bodaboda alifanya kama alivyoambiwa, safari ya kuelekea Masaki ikaanza.

    Upelelezi wa chini kwa chini alioufanya mzee huyo kwa kuwatumia vijana wake, ulimfanya afahamu kwamba siku mwanaye alipotoa fedha nyingi benki kwa mara ya kwanza, alionekana akizungumza na madalali wa nyumba wa Masaki.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kufuatilia sana, alifanikiwa kuifahamu mpaka nyumba aliyopangisha japokuwa hakutaka kuonesha dalili zozote kwamba anafahamu mwanaye anafanya nini. Alichokuwa anakisubiri ilikuwa ni kwenda katika muda ambao Samantha hajategemea ili abaini ukweli wa alichokuwa anakifanya.

    Baada ya bodaboda kukimbia kwa umbali mrefu, hatimaye waliwasili Masaki, akamuelekeza dereva huyo kwenda moja kwa moja mpaka kwenye nyumba ambayo alikuwa na taarifa kwamba Samantha ndiye aliyepangisha.

    “Huyu si anajifanya mjanja? Sasa leo nitamdhihirishia kwamba mimi nina akili zaidi yake,” alisema baba yake Samantha, akashuka kwenye bodaboda akiwa amevimba kwa hasira kama faru aliyejeruhiwa.

    Akatembea harakaharaka na kwenda mpaka kwenye mlango wa nyumba hiyo, akaanza kugonga kwa nguvu huku akilitaja jina la Samantha.

    ***

    Baada ya kufanikiwa kuwaacha dereva wa bodaboda na baba yake, Samantha alimuamuru dereva wake kupita njia ya kuzunguka na hatimaye wakawasili Sinza Vatican bila kushtukiwa.

    Kwa kuhofia kwamba dereva huyohuyo akibanwa anaweza kueleza ukweli mahali alikompeleka, Samantha alijifanya kuelekea upande mwingine kabisa. Alipohakikisha dereva huyo wa bodaboda ameshaondoka, harakaharaka alikimbia mpaka pale kwenye nyumba aliyopanga.

    Edmund aliyekuwa akitazama runinga kwa ‘kujiachia’, akiwa amejilaza kwenye masofa sebuleni, alishtuka baada ya kusikia mlango ukigongwa kwa nguvu, harakaharaka akainuka na kwenda kufunua pazia, akachungulia nje.

    “Samantha! Mungu wangu,” alisema Edmund baada ya kumuona mpenzi wake huyo akiwa katika hali isiyo ya kawaida. Harakaharaka akafungua mlango ambapo Samantha aliingia kwa kasi, miguuni akiwa pekupeku na akiwa hajajipamba kama ilivyo kawaida yake kila wanapokutana, Edmund akajua lazima kuna tatizo kubwa.

    “Vipi mpenzi wangu?”

    “Funga milango yote, funga kwa funguo na uzime kila kitu,” alisema Samantha na kupitiliza mpaka chumbani, Edmund akazidi kupigwa na butwaa. Hata hivyo, ilibidi afanye kama alivyoelekezwa, akafunga milango yote na kuzima runinga na redio, akamfuata Samantha chumbani.

    “Vipi nini kimetokea kwani?” alisema Edmund kwa sauti ya upole, Samantha akamkumbatia kwa nguvu huku akitetemeka. Ilimchukua dakika kadhaa kutulia na kurudi kwenye hali yake ya kawaida ambapo alianza kumueleza kila kitu kilichotokea.

    Taarifa hizo zilimshtua pia Edmund lakini akajikaza kisabuni na kuendelea kumbembeleza Samantha ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.

    “Nahatarisha maisha yangu kwa sababu yako Edmund, siku ukiniumiza moyo wangu basi huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yangu,” alisema Samantha huku akiendelea kulia lakini Edmund kwa kutumia ushawishi wa hali ya juu, aliendelea kumbembeleza mpaka akatulia.

    “Naona umechafuka sana na mwili wako wote umelowa jasho, twende nikakuogeshe mpenzi wangu,” alisema Edmund, kauli ambayo ilimfurahisha sana Samantha, akamkumbatia Edmund kwa mahaba mazito. Edmund alitimiza wajibu wake kwani alijua ni mambo gani yanayoweza kumfanya Samantha akarudi kwenye hali yake ya kawaida.

    Baada ya kumaliza kumuogesha Samantha kama mtoto mdogo, walirudi chumbani na kuendelea na mazungumzo yao ya hapa na pale, huku mara kwa mara msichana huyo mrembo akimsisitiza kwamba siku akigundua kwamba ana mwanamke mwingine, atayakatisha maisha yake kwa kujiua.

    Ndani ya muda mfupi tu aliokaa na Edmund, Samantha alisahau kabisa kila kitu kilichotokea, wakawa wanapiga stori na kucheka kwa furaha, muda ukawa unayoyoma na hatimaye giza likaingia.

    “Leo nataka kulala na wewe, siwezi kurudi nyumbani kwa sababu najua bado baba ana hasira kali juu yangu, anaweza hata kunimeza mzimamzima,” alisema Samantha, wazo ambalo Edmund aliliunga mkono kwani na yeye alikuwa akijisikia raha sana kukaa karibu na msichana mrembo kiasi hicho, aliyekamilika kwa kila kitu.

    ***

    Baada ya kugonga mlango kwa muda mrefu bila kupata majibu yoyote, baba yake Samantha aliamua kusogea pembeni na kuanza kuichunguza vizuri nyumba hiyo. Hata hivyo hakuona kama kulikuwa na dalili ya kuwepo kwa mtu yeyote ndani yake, akamfuata yule dereva wa bodaboda ambaye bado alikuwa akimsubiri.

    Akamuelekeza kumpeleka mpaka kwenye mgahawa mmoja uliokuwa jirani na eneo hilo ili wawe wanafuatilia kama kuna mtu yeyote ataingia kwenye nyumba hiyo. Hata hivyo, baada ya kukaa kwa zaidi ya dakika arobaini, hakukuwa na dalili za mtu yeyote kuingia wala kutoka kwenye nyumba hiyo.

    “Twende nirudishe pale uliponitoa, tutarudi tena baadaye,” alisema baba yake Samantha huku akionesha kuwa na hasira kali. Safari ya kurejea Upanga ikaanza huku njia nzima akiendelea kuangaza macho huku na kule kama atamuona Samantha.

    Dakika kadhaa baadaye, tayari walikuwa wameshawasili pale alipoacha gari lake, akamlipa dereva wa bodaboda fedha zake kisha akachukua gari lake na kurudi nyumbani kwake.

    Alipoingiza gari na kuingia ndani, alishtushwa na hali aliyomkuta nayo mkewe ambaye alikuwa amelala sebuleni akiugulia maumivu makali ya tumbo aliloumizwa na mumewe katika purukushani chumbani kwa Samantha.

    Kwa hali aliyomuona nayo, alijikuta hasira zote zikimuisha na kuanza kujilaumu kwa alichokifanya. Japokuwa alikuwa akisifika kwa ukali, hakuwahi kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mkewe hata mara moja tangu walipooana miaka mingi iliyopita, akajikuta akijilaumu sana kwa kilichotokea.

    Ilibidi awe mpole na kumuomba radhi mkewe ambaye bila hiyana alikubali kumsamehe, ikabidi ampigie simu daktari wa familia hiyo ambaye alifika haraka nyumbani hapo na kuanza kumpima mama Samantha kabla ya kumpa dawa za kutuliza maumivu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dawa alizopewa zilisaidia kumpunguzia maumivu, mumewe ambaye sasa hasira zote zilikuwa zimeisha na kumfanya abaki na majuto, alimsaidia kumuinua na wakaelekea chumbani kwao.

    “Mke wangu narudia tena kukuomba msamaha lakini naomba unisaidie kuniambia ukweli, najua lazima Samantha atakuwa amekwambia ni mwanaume gani anayemzuzua.

    “Nakuomba uniambie au unielekeze huyo mwanaume ni nani na anaishi wapi, nipo tayari hata kutuma watu wakampige risasi afe, siwezi kukubali utajiri wangu niliouhangaikia kwa kipindi kirefu leo hii upotee kirahisi namna hii,” alisema baba yake Samantha huku akionesha kumaanisha kile alichokisema.

    Mama yake Samantha akashusha pumzi ndefu na kumtazama mumewe.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog