Search This Blog

KIJIJINI KWA BIBI - 5

 







    Simulizi : Kijijini Kwa Bibi

    Sehemu Ya Tano (5)



    Martha akakurupuka kutoka katika godoro la chini, taratibu akavua nguo zake zote, kisha akapanda kitandani kwa hadhari ya kutomshtua Kayoza, akaingia ndani ya blanketi, kisha akaanza kufungua zipu ya suruali ya Kayoza,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "mmmh, mbona yuko hivi?",Martha aliguna baada ya kumuona Kayoza kalegea kama mtu aliepoteza fahamu, ila hiyo haikumzuia kuendelea na anachokifanya, akafanikiwa kuishusha suruali ya Kayoza hadi miguuni, sasa akawa anajiweka sawa ili atimize lengo lake, Kayoza aliinuka kama mshale, kwa kasi ya mwanga na meno yake yakapenya sawia katika shingo ya Martha,



    "mamaaaaaaaa nakufaaaaaaaaa",sauti ya Martha ilisikika kwa nguvu na kuwaamsha watu wote waliolala mpaka majirani.............



    ****"*******ENDELEA************



    ...Ni kitendo cha dakika tano tu, familia nzima ilikuwa imeuzunguka mlango wa chumba cha Martha,



    "we Martha fungua mlango, kuna nini?",Mkuu wa polisi aliita kwa sauti kubwa, lakini hakujibiwa na mtu, na kipindi hicho wale majirani wa karibu na nyumba ya Mkuu wa polisi walikuwa wameshafika kutoa msaada kwa tukio lolote haya ambalo lingetokea.



    Aliendelea kuita kwa muda wa dakika tano, lakini hali ilikuwa ile ile.



    Ndipo wakashauriana na baadhi ya majirani ambao walikuwa tayari wamefika kutoa msaada, kwa sauti moja wakakubaliana kuvunja mlango.



    "Tunaweza kupata kisu au bisibisi?" Jirani mmoja aliuliza baada ya kugundua ule mlango wa kitasa ni mgumu sana, yule bwana aliuliza huku akimuangalia Mkuu wa polisi aliyekuwa ameganda tu,



    "We Dada ebu tuletee kisu" Sajenti Minja alimwambia Dada wa kazi ambayo alikuwa jirani nae, kisha yule Dada akakimbilia jikoni haraka na kurudi visu viwili na kumpatia yule bwana jirani aliyeagiza hicho kifaa.



    Kisha kwa kushirikiana watu wengine waliopo ple wakafanikisha zoezi lao la kutegua kitasa cha mlango na mlango ukafunguka.



    Sasa walichokiona mbele yao ndicho kilikuwa kitu cha ajabu sana kilichopelekea mke wa Mkuu wa Polisi kupoteza fahamu pale pale.



    Mkuu wa polisi yeye aliangalia mara moja tu, kisha akatoka nje huku macho yake yakiwa yametawaliwa na machozi, baadhi ya majirani wakaenda kumfariji na wengine wenye roho ngumu walichukua shuka lililokuwepo juu ya kitanda na kuusitiri mwili.



    Ulikuwa mwili wa Martha ukiwa na chupi tu mwilini, ulikuwa umelala juu ya kitanda, na damu zikiwa zimemuenea shingoni zikiwa zimechirizika kwenda sakafuni, alikuwa tayari ni mfu, tayari mwili umetengana na roho kutokana na tamaa zake za mwili.



    "Ni nini kimemkuta?" Jirani mmoja alimuuliza Sajenti Minja,



    "Sasa Mimi nitajuaje ndugu yangu wakati mlango tumevunja wote na kuukuta mwili umelala?" Sajenti Minja alijibu huku moyoni mwake akiwa na mawazo ya kuwa inawezekana Kayoza ndiyo aliyefanya hill tukio.



    Sajenti Minja aliamini hivyo baada ya kuona sehemu ya dirishani kulikuwepo na vioo vilivyopasuka, pamoja na nondo kadhaa kuondolewa, akakumbuka Kayoza alishawahi kuondoka kwa mtindo huo kipindi cha nyuma alipojaribu kumtegea askari ndani ya lodge kipindi anaanza kuipeleleza hii kesi ya Kayoza mjini Dodoma.



    "Sasa kama ametoka akiwa kama mzimu si ataenda kupoteza fahamu maeneo ya jirani tu? Nitoke nikamuangalie nini? Nikitoka pia watu wa hapa si watanishangaa?, bora nibaki tu hapa hapa huku nikiomba Mungu amfikishe salama nyumbani" Sajenti Minja aliongea peke yake huku akielekea sebuleni alipokaa Mkuu wa polisi na majirani wengine waliokuwa wanamfariji.



    Ila hakuridhika kukaa tu pale, kuna fikra zilimjia. Akanyanyuka taratibu na kuelekea nje ya nyumba lakini ndani ya geti. Akamtafuta mlinzi na kumkuta akiwa amekaa kimajonzi sana,



    "Ni kitu kimefanya tukio hili?" Sajenti Minja alimuuliza mlinzi kwa ajili ya kutaka kujua kama ni kweli Kayoza alikuja hapo,



    "Nashindwa hata kueleza, ila nimekiona kiumbe cha ajabu sana kikitokea chumbani kwa Martha, sijui ni nini lile" Mlinzi aliongea huku akiwa anasimumuka mwili,



    "Kuna nani aliingia leo kipindi tumetoka?" Sajenti Minja alimuuliza tena huku akitaka kujua kama mlinzi atamtaja Kayoza ingawa tayari Sajenti Minja alishagundua kuwa yale mauaji yamefanywa na Kayoza, sasa hapo alitaka kujua kama Mlinzi anaweza kumtaja Kayoza ndio pekee aliyeingia kipindi hawapo au kuna wengine,



    "Aliingia yule mjomba wako mpole mpole" Mlinzi alijibu na kumfanya Sajenti Minja aone hatari iliyopo mbele yao, maana kama Mkuu wa polisi akimbana mlinzi kuhusu watu waliokuja siku hiyo, basi lazima atajwe Kayoza,



    "Huyo tupo nae ndani mbona, hakuna mwingine aliyekuja zaidi ya huyo?" Sajenti Minja alizuga ili kumfanya mlinzi asimuhisi vibaya Kayoza,



    "Leo hakuna zaidi ya huyo" Mlinzi alijibu na kumfanya Sajenti Minja ahisi hatari kubwa iliyopo mbele yao,



    "Sasa ndugu yangu, kwa usalama wako, ni bora tu ukimbie, kwa maana hii kesi unaangushiwa wewe, nimemsikia boss wako ndani akisema hivyo" Sajenti Minja aliongea baada ya kufikiria kwa muda, alifanya hivyo ili kumtisha mlinzi akimbie ili ushahidi wa Kayoza kuingia ndani kwa Mkuu wa polisi ufutike,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Lakini Mimi sijaua, kwanini nikamatwe?" Mlinzi aliuliza huku akitetemeka,



    "Haukamatwi kwa kuua, utakamatwa kwa uzembe wa kumuachia huyo muuaji apite" Sajenti Minja alizidi kumtisha mlinzi,



    "Lakini utakuwa uonevu huo" Mlinzi alilalamika huku akitaka kulia,



    "Acha ujinga, ni bora tu ukimbie kabla hujatiwa mikononi mpwa polisi, mpaka wake kujua wewe hujaua, itakuwa umeshakuwa mlemavu tayari kwa ajili ya mateso utakayopata" Sajenti Minja alizidi kumtisha mlinzi,



    "Dah, sasa utanisaidiaje?" Mlinzi aliuliza baada ya kufikiria kwa muda,



    "We mpumbavu nini, nikupe msaada gani zaidi ya huu niliokupa sasa hivi?" Sajenti Minja aliuliza huku akijifanya ana hasira,



    "Takimbilia Wapi na sina hata pesa ya nauli?" Mlinzi aliuliza,



    "Wewe mwanaume mwenzangu, nakusaidia huku nikiamini hata Mimi naweza kupata tatizo na wewe ndio unaweza kuna kuwa msaada" Sajenti Minja aliongea huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa noti nyingi nyingi zilizokaa bila mpangilio na kumpatia mlinzi,



    "Dah, asante sana" Mlinzi alipokea na kuzitia mfukoni,



    "Sasa usikimbie hivyo kama Mbwa, hapa unatakiwa utoke kama unaenda kujisaidia nyuma ya nyumba, ukifika tu nje ya geti ndio uanze riadha" Sajenti Minja alimwambia mlinzi ambayo aliishia kujibu kwa kichwa tu, kisha akafanya kama alivyoelekezwa na Sajenti Minja na kutokomea nje ya geti na kumuacha Sajenti Minja akisikitika kwa mengi, kwanza kumpotezea hajira huyo mlinzi, pili kumpoteza Martha, msichana mdogo aliyekuwa mchangafu na waliyezoena kwa Siku chache tu, na tatu ni Kayoza.



    ***************



    Majirani wengine wa mkuu wa polisi wakatoa taharifa polisi na hospitali,



    gari ya wagonjwa ikaenda usiku ule ule kuuchukua mwili wa Martha.



    Ambulance haikuchukua muda sana barabarani ilifika haraka sana nyumbani kwa Mkuu wa polisi, nadhani na cheo alichonacho kilichangia gari hiyo kuwahi kufika na sababu ya pili ni kutokana na kutokuwepo na magari mengi barabarani usiku ule.



    Gari ya hospitali ilipofika, mwili wa Martha ulibebwa juu juu na kuingizwa ndani ya gari, kisha gari ikaondoshwa kwa kasi sana, utasema ndani amelazwa mgonjwa ambayo anahitaji matibabu ya haraka, kumbe amelazwa maiti ambayo hata useme ukimbize gari mpaka iruke hewani kama ndege lakini bado hutoweza kuurudisha uhai wake.



    Ambulance ilikuwa inasindikizwa na gari mbili za polisi, moja walikaa askari wa kawaida wapatao sita, na nyingine alikuwepo Sajenti Minja na askari wawili, ila Sajenti Minja hapa alisimama kama mwanafamilia na wala hakuwa polisi.



    Iliwachukua dakika ishirini gari ya wagonjwa kufika hospitali.



    Walipofika walipokelewa haraka haraka, mwili wa Martha ukachukuliwa na kupelekwa chumba cha uchunguzi, baada ya uchunguzi, mwili ukapelekwa monchwari.







    *******************





    Kayoza alipomaliza kumnyonya Martha damu, alivunja nondo za madirisha na kutokea dirishani, mlinzi alimuona, ila kwa kuwa Kayoza alikuwa anatisha sana, yule mlinzi alichofanya ni kujificha katika bustani ya maua kwa kulala chini mpaka kayoza aliporuka ukuta na kutokomea pasipokujulikana.





    Mzimu uliendelea kumshika Kayoza mpaka alipofika katika mlango wa kuingilia kwao, alipofika mlangoni, akadondoka chini, kisha akapoteza fahamu.



    Mama Kayoza na Omari walikuwa hawajalala kwa sababu ya wasiwasi, walivyosikia kishindo mlangoni, wote wakashtuka,



    "ebu chungulia kuna nini?",Mama kayoza alimwambia Omari,



    "mh, mama",Omari alitoa mguno wa uoga baada ya kuambiwa achungulie nje kupitia dirishani,



    "ebu acha uoga uko, chungulia hata kwa hapo dirishani",mama Kayoza alizidi kumuandama Omari,



    Omari akafungua dirisha kidogo, kisha akachungulia,



    "eh!",Omari akashtuka,



    "Mbona umeshtuka hivyo, umeona nini?",mama Kayoza akahoji baada ya Omary kushtuka,



    "Kayoza",Omari alijibu huku akiundea mlango, alipoufikia alifungua, wakatoka nje.



    Omari na Mama Kayoza wakawa wanamuangalia Kayoza aliyekuwa amelala chini.



    Mama Kayoza aliogopa sana, kwa sababu hakuwai kumuona Kayoza akiwa ametoka kunyonya damu, ila Omari alijua kila kitu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Mbebe basi umuingize ndani" Mama Kayoza alimwambia Omary,



    "Sasa mama Mimi peke yangu nitamuweza?" Omary aliuliza huku akiwa anajaribu kumuinua,



    "Tatizo lenu uwa mnajilegeza sana" Mama Kayoza aliongea huku akijaribu kuibeba miguu ya Kayoza na Omary akiwa upande wa kchwa cha Kayoza huku nae akiwa anajitahidi kukiinua.



    Wakawa wanaangaika kumbeba ili wamuingize ndani.



    Wakiwa bado wanaangaika kumuinua Kayoza, walishtushwa na gari iliyokuwa inakuja upande waliopo, ghafla hata kabla hawajaamua chochote, lile gari tayari lilikuwa mbele yao, likaenda kusimama pale pale walipokuwepo.



    wote walishtushwa baada ya kugundua kuwa lile gari ni la polisi...



    ...kuona hivyo, Mama Kayoza akatoka mbio kuelekea ndani, Omari nae kwa taharuki, ikambidi nae aingie ndani kwa spidi ya ajabu, wakamuacha Kayoza akiwa amelala pale pale chini huku hajitambui.



    Baada ya dakika kadhaa, wakasikia mtu anagonga mlangoni,



    Mama Kayoza na Omari wakaangaliana, huku wote wakiwa wamelowa jasho la hofu, na wakiulizana kwa macho ni nani amfungulie huyo mgongaji?,



    "jamani nifungulieni, nina haraka",ilisikika sauti ya Sajenti Minja mlangoni na kuwafanya wapigwe na butwaa.





    Mama Kayoza na Omari wakawa kama hawaamini vile,



    "nani, Minja?",Mama Kayoza akauliza kwa wasiwasi huku akiwa haamini,



    "ndio, fungua dada",Sajenti Minja alijibu kwa haraka,



    Omari akiwa na hofu, alienda hadi mlangoni kisha akafungua mlango huku akitetemeka,



    "ebu njoo tumuingize huyu ndani",Sajenti Minja alimwambia Omari wakati akiwa amemshika Kayoza,



    Omari akaenda haraka, kisha wakamnyanyua Kayoza na kumpeleka chumbani kwake, kisha wote wakarudi sebuleni.



    "shikamoo dada",Sajenti Minja alimsalimia Mama Kayoza,



    "marhaba, vipi?",Mama Kayoza aliuliza,



    "yaani kilichotokea nashindwa hata kuamini",Sajenti Minja aliongea huku akiwa ameinamia chini,



    "ongea basi tukuelewe",Mama Kayoza alisema kwa jazba,



    "yaani Kayoza hapa ametoka kumuua mtoto wa bosi",Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,



    "weeh, acha utani!",Mama Kayoza alishtuka,



    "Martha au?" Omary nae aliuliza huku akiwa ameshika kichwa,



    "yaani hapa nimechukua gari mara moja, nimewatoroka wenzangu wapo hospitali ili nije niwape taharifa, ila kwa bahati nzuri nimekuta Kayoza kashafika, maana nilikuwa na wasiwasi nae sana",Sajenti Minja aliongea kwa utulivu,



    "duh!, hii kweli hatari, sasa?",Mama Kayoza alihoji,



    "tutaongea zaidi kesho, wacha niwahi ili nijue ratiba za uko",Sajenti Minja aliongea huku akielekea katika mlango wa kutokea,



    "haya baba, kukicha nitakuja msibani",Mama Kayoza aliongea huku akimtazama Sajenti Minja akipanda gari.



    Sajenti Minja akawasha gari, alafu akaondoka.



    Mama Kayoza akarudi ndani, wakajadiliana na Omari,



    "Kwanza ilikuaje kuaje mpaka akamuua?" Mama Kayoza alimuuliza Omary,



    "Sasa mama Mimi nitajuaje wakati Mimi na wewe tumeshinda wote hapa?" Omary alijibu mama Kayoza huku akimshangaa,



    "Nyie vijana, labda kuna vitu mnaambianaga" Mama Kayoza aliongea,



    "Kwa kweli Mimi sijui lolote" Omary alijibu,



    "Sawa, nadhani ni muda wa kulala huu ingawa tumepitiliza sana leo, ila kesho kukicha ndio tutajua cha kufanya" Mama Kayoza aliongea huku akijiondoa eneo la sebuleni na kuelekea chumbani kwake,



    "Sawa" Omary nae alijibu huku akiiendea swichi ya taa ya pale sebuleni, akazima na kuelekea chumbani kwao.



    Hapo tayari walikubaliana wakalale mpaka asubuhi, ndio wajue cha kufanya.





    ***************





    Baada ya msiba kuisha, Sajenti Minja aliomuomba Mkuu wa polisi kurudi nyumbani kwake, Mkuu wa Polisi akakubali kwa roho safi, Minja akahamia kwake rasmi.





    Toka ahamie kwake, Sajenti Minja alikuwa amemaliza wiki sasa, siku moja akaamua aende kwa dada yake ili wakajadili mambo yanayomtokea Kayoza, akachukua gari yake mpaka kwa dada yake, akakaribishwa mpaka ndani.



    Wakasalimiana na kwa pamoja wakasali na kumshukuru Mungu kwa kumsaidia Sajenti Minja kupona,



    "Kazini umeshaanza kwenda?" Mama Kayoza alimuuluza Sajenti Minja,



    "Hapana, Nina wiki mbili za kupumzika nyumbani, bado nimepewa muda wa kuiangalia afya yangu" Sajenti Minja alijibu,



    "Afadhali upumzike, maana hakuna aliyedhani kama utakuwa hivi leo" Mama Kayoza aliongea huku akifurahi,



    "Sidhani kama nahitaji kupumzika, huu muda niliopewa nipumzike nadhani nirudi kushughulika na Kayoza" Sajenti Minja aliongea,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Utashughulika nae vipi?" Mama Kayoza aliuliza,



    "Nafikiri safari ya Bukoba ni lazima itekelezeke, ila kabla hatujaenda huko ni lazima tumpate mganga mmoja wa mwisho hapa Shinyanga, labda anaweza kutusaidia" Sajenti Minja alitoa ushauri wake,



    "Waganga wa hapa wameshashindwa, nadhani jibu lipo Bukoba" Kayoza aliongea,



    "Bukoba tutaenda tu, ila tujaribu kwa Mara ya mwisho hapa, tukishindwa ndio twende uko Bukoba" Sajenti Minja alimuelewesha Kayoza,



    "Mi nafikiri mjomba wako yupo sahihi, ebu jaribu kumuelewa" Mama Kayoza alimuambia mwanae....





    ***************





    Yule kijana anayeitwa Ismail au Suma ambaye alipewa kazi na Mkuu wa Polisi, alipiga hatua kubwa sana katika upelelezi wake, aligundua kuwa mtu alijitambulisha kama Remmy kwa Mkuu wa Polisi, jina lake halisi ni Omari Hussein Mkwiji, na hana undugu wowote na wakina Sajenti Minja, ila anaishi pale kama rafiki wa mjomba wake Sajenti Minja(kayoza).



    Ila yule kijana hakutaka kumwambia Mkuu wa Polisi mpaka ahakikishe kwa macho mauaji yakitokea mbele yake, ili awe na ushaidi, na alikuwa anatembea na kamera kila anapoenda, na popote alipo Omari na yeye alikuwepo ila wakina Omari hawakumgundua.



    "Hii kazi imekuwa rahisi sana kama meli kuelea juu ya maji ya bahari" Suma aliongea huku akimtazama Omary ambaye alikuwa bize na mchezo wa Drafti, kisha Suma akatazama pembeni na kutabasamu.





    ****************





    Baada ya kushauriana kifamilia, walikubaliana watafute Mganga wa mwisho pale Shinyanga, nae akishindwa basi wataenda Bukoba kijijini kwa bibi yake Kayoza.





    Haikuchukua muda kumpata Mganga, walimpata Babu mmoja ambae alisifika kwa uganga wa kupiga ramli, wakajipanga.



    wakatafuta siku wakaenda, kama kawaida walikuwa watatu, Sajenti Minja, Omari na Kayoza, ila pia kulikuwa na mtu wa nne ambaye wao hawakumtambua, na huyo sio mwingine ila ni kijana Suma.



    Suma alikuwa anawafatilia kama kawaida bila wao kujua. Wao wakiwa katika gari ambayo ilikuwa inaendeshwa Sajenti Minja, yeye Suma alikuwa katika boda boda ambayo aliikodi kwa ajili ya kuifuatilia gari waliyokuwamo wakina Sajenti Minja.





    Walifika salama kwa mganga, na wakapanga foleni kwa sababu walikuta kuna wateja nje wakisubiri zamu zao zifike.



    Zamu yao ilipofika, wakaruhusiwa kuingia,





    "karibuni vijana",Babu mmoja Mzee aliwakaribisha kwa sauti iliyokwaruza,



    "asante, asante sana Babu",wakaitikia kwa pamoja,



    "Habari za mtokato wajukuu zangu?" Babu aliwauliza,



    "Uko kuna wema kabisa, ila kuna tatizo dogo kidogo" Sajenti Minja alijibu,



    "Sasa mtapenda niwaambie shida yenu au mtanieleza wenyewe?",Babu aliwauliza huku akiwatazama na macho yake makavu yalikuwa na ranging nyekundu,



    "Ningependa utuambie tu mzee",Sajenti Minja alijibu ili kupima uwezo wa huyo mganga,



    Babu akatoka nje, baada ya dakika mbili akarudi ndani na sufuria yenye maji, akawaambia wote waingize mikono ya kushoto ndani ya sufuria,



    walipotoa, akaweka dawa zake, kisha akachukua kikombe cha maji, akachota maji ya kwenye sufuria kisha akanywa, alipoyameza tu, akamgeukia Kayoza,



    "ni tatizo kubwa sana",Mganga aliongea huku macho yake yakiwa kwa kayoza,



    "ndio maana tumekuja ili utusaidie",Sajenti Minja aliingea,



    "kuwasaidia naweza, ila huo msaada utagharimu na maisha ya huyu kijana",Mganga aliongea huku akimuoneshea kidole Kayoza,



    "msaada gani huo?",Sajenti Minja aliuliza,



    "Msaada uliopo ni kwamba mnachinja kondoo, alafu huyu kijana anawekwa kitanzi kama anataka kunyongwa, ile damu ya kondoo ikishamuingia haswa puani, lazima mzimu atampanda, hapo hapo mnamnyonga huyu kijana, mzimu atashindwa kutoka, kwa sababu huyu bwana mdogo atakosa pumzi na mzimu hutegemea hewa zaidi katika kutoka na kuingia",Mganga alimaliza kutoa maelekezo,



    "hiyo ngumu, hamna zaidi ya hiyo?",Sajenti Minja aliuliza ya kufikiria kwa muda kidogo na kipindi chote hicho wakina Kayoza walikuwa wamekaa kimya,



    "ipo",Mganga alijibu kwa kifupi,



    "ipi hiyo?",Sajenti Minja akauliza,



    "anatakiwa apelekwe kijijinii",Mganga aliongea,



    "kijijini!?",Sajenti Minja aliuliza huku akishtuka,



    "ndio, huyu apelekwe kijijini, tena KIJIJINI KWA BIBI yake mzaa baba, uko ndipo lilipo suluhisho la tatizo lake",Mganga aliongea alichomaanisha huku akiwa amefunga macho.......



    ..."duh!, sawa babu, malipo ni kiasi gani",Sajenti Minja akamuuliza Mganga,



    "weka kiasi chochote",Mganga aliongea huku akimuelekeza Sajenti Minja sehemu ya kuwekea hela,



    Sajenti Minja akaingiza mkono mfukoni na kutoa shilingi elfu kumi, na kuiweka juu ya ungo wa Mganga,



    "haya babu tunaenda",Sajenti Minja akaaga kwa niaba ya wenzake,



    "haya karibuni tena, ila mnatakiwa muwahi kumpeleka, kwa sababu mkichelewa kidogo inaweza kuwagharimu zaidi",Mganga alitoa msisitizo huku akiwa awaangalii na badala yake alikuwa akizipanga panga vizuri dawa zake,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "hamna shida Babu, tutaenda wiki ijayo",Sajenti Minja alisema kwa sauti ya unyonge,



    "Wiki ijayo?, Mimi ndio ningekuwa nyie, yaani ningeenda muda huu kupanda gari" Mganga aliendelea kuongea,



    "Kwani mzee ni hatari sana tukienda wiki ijayo?" Sajenti Minja aliuliza huku akisimama kabisa, kwa maana mwanzo alikuwa anaongeo huku anatembea,



    "Mwenyewe fikiria kwenye kchwa chako alafu utaamua uende wiki ijayo au uende haraka iwezekanavyo" Mganga alitoa jibu lililomfanya Sajenti Minja akae kimya na kutoka zake nje.



    Baada ya hapo, wakina Sajenti Minja wakaondoka zao kurudi nyumbani.



    Walipofika, wakamkuta Mama Kayoza yuko sebuleni anaangalia kwaya,



    "karibuni jamani, za uko?",Mama Kayoza aliwakaribisha,



    "uko ni yale yale tu",Sajenti Minja alijibu katika sauti iliyokata tamaa,



    "yale yale yapi, ina maana na huyo Mganga ameshindwa?",Mama Kayoza aliongea kwa upole,



    "ndio, ila nae amesema dawa ipo",Sajenti Minja akasema kiunyonge,



    "si angewapa kama ipo",Mama Kayoza aliongea kwa mshangao,



    "amesema ipo KIJIJINI KWA BIBI yake Kayoza",Sajenti Minja alijibu,



    "mh, kweli ni yale yale",Mama Kayoza nae akawa mnyonge ghafla.



    Ikawabidi wajipange, na mwisho wakakubaliana kuwa, Sajenti Minja achukue likizo fupi kwa ajili ya safari ya Bukoba.



    *************************



    Yule kijana aliyepewa kazi ya upelelezi alukuwa ni mpelelezi haswa, unaweza kujiuliza kwanini asingepewa kazi usalama wa utaifa?



    Maana sio kufuatilia tu nyendo za Omary, ila mpaka baadhi ya maneno waliyokuwa wanaongea wakina Omary alikuwa anayapata kwakutumia ujanja anaoujua yeye.



    na hapa alikuwa ameyasikia maneno yanayohusu safari ya Bukoba, sasa alipoyasikia haya, akaenda hadi kwa Mkuu wa Polisi,



    "vipi bwana mdogo, kuna mafanikio?",Mkuu wa Polisi alimuhoji yule Kijana,



    "yapo mengi sana mkuu. Kwanza pole kwa msiba kwa maana kipindi kile nilikuja ila nilishindwa kuonana na wewe",Suma alijibu kwa kujiamini, na pia akatoa maneno ya pole,



    "Siwezi kusema asante kwa maana uchungu bado ninao, tena mkubwa tu, na ukizingatie mtoto mwenyewe alikuwa mmoja tu" Mkuu wa polisi alijibu,



    "Tatizo lilikuwa nini, maana Mimi nilisikia juu juu tu kuwa mlivamiwa?" Suma aliuliza,



    "Ndiyo hayo hayo mambo ambayo nilikuagize uyafuatilie ndio yamenirudia nyumbani kwangu" Mkuu wa polisi aliongea kwa unyonge,



    "Aisee pole sana. Sasa nimekuja hapa kukueleza nilipofikia" Kijana Suma aliongea huku akiweka note book yake mezani,



    "ehe, niambie kijana wangu",Mkuu wa Polisi aliongea huku akibadilisha mkao katika kochi,



    "kwanza kabisa, yule kijana unayemtambua kama Remmy, jina lake halisi ni Omari Mkwiji, ni mwenyeji wa Tanga, pia mwanafunzi wa UDOM pale Dodoma, na pale hana undugu na yeyote kati ya wale, ila anaishi pale kama rafiki wa mjomba wake Sajenti Minja, ambae anaitwa Kayoza. Na mahali walipokutana nae ni Dodoma pale Chuo kikuu.



    Huyu Kayoza ndio mwenye matatizo sasa, yeye ndio mnyonyaji wa damu, na Siku binti yako anafariki ni yeye ndio aliyemuua na hiyo habari niliisikia kwa Dada yake Sajenti Minja wakati wakiwa wanajadili kuumaliza ugonjwa wa Kayoza unaosababisha yeye kuwa katika hali ile ya kunyonya damu watu, na hapa ninavyokuambia ni kuwa Sajenti Minja atakuja kukuomba likizo ya muda kwa sababu walienda kwa mganga, wakaambiwa waende kijijini kwa bibi yake Kayoza ambapo ni Bukoba, uko ndipo waliambiwa kuwa kuna dawa ya kumponya Kayoza, kwa hiyo Sajenti Minja ataongozana na Kayoza na Omari kwa ajili ya Safari",yule Kijana alimaliza hivyo,



    "kwa hiyo Minja anajua mchezo mzima, hata ile kesi kumbe ni ujanja ujanja tu!",Mkuu wa Polisi aliongea kwa sauti yenye mawazo yaliyoificha hasira yake,



    "mimi nafikiri kazi uliyonituma nimeshaimaliza",sauti ya yule Kijana ilimshtua Mkuu wa Polisi aliyekuwa kazama ndani ya kina kirefu cha mawazo,



    "sawa, asante, ngoja nikuletee mzigo wako",Mkuu wa Polisi aliongea huku akinyanyuka na kuelekea ndani.



    Baada ya dakika chache alitoka na bahasha kubwa ya kaki, akamkabidhi yule kijana, yule Kijana akazitoa pesa ndani ya bahasha, akazihesabu, kisha akaagana na Mkuu wa Polisi.



    "Kijana uliniambia huna kazi?" Mkuu wa polisi alimuuliza Suma ambaye alikuwa ameshaanza kuondoka,



    "Ndio Mkuu" Suma alijibu huku akisimama,



    "Jiandae basi, maana nakuandalia barua itayokufanya uende moshi ukachukue mafunzo ya uaskari" Mkuu wa polisi alitoa maneno yalimfanya Suma amshukuru sana,



    "Asante sana, nine lini?" Suma aliuliza,



    "Nitaakutaharifu kupitia simu, we kaa tayari tu kwa maana itakuwa muda wowote kutoka sasa" Mkuu wa polisi alimjibu,



    "nashukuru sana mzee wangu.

    Ubaki salama", Suma aliongea na kuondoka sake na kumuacha Mkuu wa polisi akiwa sebuleni,







    "Sajenti Minja, Joel Minja, Minja, Minja, lazima nikuue kwa mkono wangu, wewe ndio umesababisha mwanangu amekufa kifo cha aibu",Mkuu wa Polisi aliongea kwa sauti ndogo huku akiwa ameuma meno kwa hasira,



    "Kwa hiyo Omary sio muuaji, Kayoza ndiyo kamuua binti yangu?, Minja unajua kila kitu ila umeficha mpaka mwanangu ameuwawa kinyama? Hakuna atakayesalimika kati yenu" Mkuu wa polisi aliongea na kisha akagida kinywaji kikali chenye rangi ya maji kilichokuwa katika chupa kubwa kama ya waini (wine) ila chenyewe ubavuni kiliandikwa MAGIC MOMENT.



    ******************** CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Siku iliyofuata, Sajenti Minja alipanga akaombe likizo, akajitayarisha vizuri, na kuwa nadhifu kama kawaida yake. Akachukua gari yake na kwenda nayo moja kwa moja mpaka ofisini.



    Ofisini aliingia saa nne asubuhi, alipokelewa na pole nyingi sana kutoka kwa askari wenzake, kwa sababu toka apate ajali ndio kwa mara ya kwanza alikuwa anaingia ofisini, baada ya salamu za hapa na pale, akawa anaelekea katika ofisi ya Mkuu wa Polisi, alipofika akagonga mlango,



    Mkuu wa Polisi alikuwa ndani,

    "nani?",Mkuu wa Polisi akauliza,



    "Minja",Sajenti Minja akajibu kwa nje,



    "leo ndio mwisho wako mshenzi na msaliti mkubwa wewe",Mkuu wa Polisi aliongea huku akijaza risasi katika bastola yake ndogo, alipomaliza, akamwambia Sajenti Minja aingie.....







    ...Sajenti Minja akaingia ndani,



    "vipi tena mkuu, mbona kifaa umekiweka mezani?",Sajenti Minja aliuliza baada ya kuiona bastola iko juu ya meza ya Mkuu wa Polisi,



    "nilikuwa naisafisha, karibu Minja",Mkuu wa Polisi aliongea huku akibasamu kwa tabasamu batili,



    "Tunatishana bwana, hivyo vyombo vya moto vinafichwagwa bwana" Sajenti Minja aliongea huku nae akitabasamu,



    "Kweli kabisa.. Vipi mbona umekuja leo kabla likizo yako haijaisha? Au uliwamisi wenzako?" Mkuu wa polisi alimuuliza Sajenti Minja,



    "Hata hiyo ni sababu pia, ila sababu juu iliyonileta ni kuja kuomba kuongezewa likizo" Sajenti Minja aliongea kauli ambayo mkuu wa polisi aliitegemea,



    "Haina shida Minja, je ungetaka likizo ya muda gani?" Mkuu wa polisi aliuliza,



    "Ningepata kama wiki mbili nyingune, ingekuwa safi sana" Sajenti Minja aliongea,



    "Mi nitakupa likizo ya mwezi mzima, najua hali yako haijatengemaa vizuri" Mkuu wa polisi aliongea,



    "Nashukuru sana, sasa ngoja nikaandae barua ili niiwasilishe baadae" Sajenti Minja aliongea,



    "Hapana, hakuna haja ya barua, we nenda tu Minja" Mkuu wa polisi alimzuia Sajenti Minja kuandika barua,



    "Haiwezi kuleta matatizo baadae?" Sajenti Minja alimuuliza mkuu wake,



    "Hakuna Shida Minja, Mimi ndiyo nimekuruhusu, usiwe na wasiwasi" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja.



    Baada ya Sajenti Minja kuongea kilichompeleka, haikuwa ngumu kukubaliwa, alipewa likizo ya mwezi mzima,



    "utakuwa hapa hapa au utarudi Dodoma?",Mkuu wa Polisi alimuuliza Sajenti Minja,



    "hapa hapana, nitaenda Moshi kwa wazazi, alafu wiki mbili za mwisho nitazimalizia Dodoma",Sajenti Minja alijibu,



    "haya bwana Minja, mi nakutakia likizo njema, na safari njema pia",Mkuu wa Polisi alihongea kwa sura aliyoibandika huzuni wa bandia,



    "shukrani sana Mkuu, tukijaaliwa",Sajenti Minja alisema wakati ananyanyuka kutoka kwenye kiti,



    Kisha akauendea mlango na kwenda zake.



    Mkuu wa polisi alisitisha zoezi la kumuua Sajenti Minja ofisini kwa sababu angekamatwa na kufungwa kwa sababu ushaidi ungekuwepo wa kutosha, aliamua kwenda kumuua Sajenti Minja huko huko Bukoba, Mkuu wa Polisi na yeye akajipa likizo.



    Likizo iliyokuwa maalum kwa ajili ya kisasi, likizo ambayo aliibatiza jina na kuiita LIKIZO YA MALIPO YA KIFO.



    *****************



    Siku ya safari ilipofika, Mama Kayoza aliwasindikiza mpaka stendi kuu ya mkoa, walipofika, wakafanikiwa kupata usafiri wa haraka haraka,



    "Jamani safari njema" Mama aliwaambia,



    "Lakini Dada kumbuka sisi tunaenda sehemu ambayo hatuhijui, kama una namba za wenyeji wetu ni bora uwape taharifa juu ya safari yetu" Sajenti Minja alimuambia Dada yake,



    "Kayoza anapajua huyo, au na wewe umepasahau?" Mama Kayoza aliongea huku akimuangalia Kayoza,



    "Mama ni muda sana, hata kumbukumbu sina vizuri" Kayoza alijibu,



    "Mimi na wewe ni nani ambae ametoka muda mrefu kule? Mbona mimi bado napakumbuka?" Mama Kayoza alimuuliza mwanae,



    "Tatizo sio kila sehemu naikumbuka, kuna njia sizikumbuki kabisa" Kayoza alijibu Mama yake,



    "Bwana nyie wanaume, mtafika tu, maana Mimi sina mawasiliano na mtu yoyote wa uko" Mama Kayoza aliongea,



    "Tutafika tu" Omary aliongea na kufanya wenzake wamuangalie,



    "Unavyoongea utasema unapajua, au umeshawahi kufika?" Sajenti Minja alimuuliza Omary,



    "Tuwe na imani tutafika tu" Omary alijibu na kufanya wenzake wacheke,



    "Achana na huyu mwendawazimu, ebu nichoree ramani kwenye karatasi" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,



    "Nipe hiyo karatasi na kalamu" Mama Kayoza akaongea na kumfanya Sajenti Minja ajisachi na kutoa kalamu na kitabu chake kidogo cha diary na kumpatia Mama Kayoza kisha akaanza kuwachorea ramani huku pia akiwaelekeza, alipomaliza akawaachia ile karatasi yenye mchoro.



    Wakaendelea kuongea na maongezi mengine mpaka muda wa kuondoka basi ulipofika ndipo mama Kayoza akaagana na wenzake hao na kuachana hapo huku wakipungiana mikono kipindi basi inaacha eneo la kituo kikuu cha mabasi ya mikoani.



    Baada ya gari kupotea machoni pake, Mama Kayoza aliondoka zake eneo hill huku akiamini Wakina Sajenti Minja watakaa wiki tu kisha watarudi.



    *****************



    Mkuu wa Polisi nae alipanda basi hilo hilo walilopanda wakina Sajenti Minja, ila yeye alipata nafasi siti ya mbele kabisa kwa dereva, wakati wakina Sajenti Minja wao walipata siti jirani na za nyuma. Na kingine ni kwamba mkuu wa polisi ilikuwa ngumu sana kumtambua kwa maana alivaa kama mzee wa kijijini kabisa.



    Kwa hiyo ndani ya basi kukawa na makundi mawili, moja la Sajenti Minja na lingine ni la mkuu wa polisi ila tofauti ni kwamba kundi moja lilikuwa la mtu mmoja na tayari alishawajua adui zake, na kundi la pili ni la Sajenti Minja ambalo walikaa bila kujua kama wanafuatiliwa na mkuu wa polisi.



    Bukoba waliingia saa kumi na moja jioni, wakatafuta usafiri wa kuwapeleka Vanga, kijijini kwa bibi yake Kayoza.



    Vanga waliingia saa moja kasoro robo, hawakupata shida kufika katika nyumba ya Bibi yake Kayoza, kwani ni ukoo wa kichifu, kwa hiyo ukoo wao ulikuwa maarufu sana pale kijijini.



    Na hata usiku ulipokuwa mwingi walitaka kuondoka ili wakatafute lodge ila walikataliwa na kuambiwa ni lazima walale pale kwa maana kuna nafasi za kutosha na hakuna haja ya kwenda kutafuta Guest.



    Kumbuka chote hicho Mkuu wa Polisi nae alikuwa akiwafuatilia kwa kila hatua na alitumia akili nyingi kuwafuatilia bila ya wao kujua.



    Mkuu wa Polisi alipojiaminisha nyumba waliyofikia wakina Sajenti Minja, na yeye akaamua kutafuta Guest iliyopo jirani na nyumba hiyo, alifanikiwa kupata Guest jirani na nyumba waliyofikia wakina Sajenti Minja.



    Wakina sajenti Minja walipokewa kama watu wa kawaida sana, ila baada ya kujitambulisha, vigelegele vilipigwa na shangazi zake Kayoza, usiku huo huo ndugu wa mbali walipigiwa simu kufahamishwa ujio wa Kayoza, Kayoza akaomba aonane na bibi yake, ila Baba zake wadogo wakamzuia, wakidai bibi yake ni mgonjwa sana, kama kuonana labda kesho ila kwa usiku ule isingewezekana.



    Asubuhi kulipokucha, Sajenti Minja na Omari waliamshwa mapema sana, kisha wakatayarishiwa ndizi zilizokorogwa kama uji, hicho ni chakula cha heshima katika kabila lao.



    Walipomaliza kula, wenyeji wakawa wanawatembeza katika mali ziliachwa na Baba yake Kayoza, na moja ya hizo mali pale kijijini ni ile Guest aliyofikia mkuu wa Polisi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakaenda pale Guest, wakawa wanaoneshwa eneo la Guest yote, mara Sajenti Minja akaomba aelekezwe Choo kilipo, akaelekezwa na kisha akawa anaelekea katika mlango wa chooni sasa ambao ulitazamana na mlango wa chumba alichofikia Mkuu wa Polisi.



    Mkuu wa polisi alikuwa anatoka ili aelekee kutafuta kifungua kinywa, aliupa mlango wa chooni mgongo wakati anafunga na ufunguo mlango wa chumbani kwake, na wakati huo huo Sajenti Minja nae alikuwa anatoka chooni, anaelekea pale alipo mkuu wa Polisi maana pale ndipo kulipokuwa na njia ya moja kwa moja mpaka nje...



    "JESUS!",Sajenti Minja akashtuka alipomtazama mgongoni Mkuu wa polisi..





    ...ila sauti yake haikumfikia Mkuu wa Polisi, Sajenti Minja akarudi ndani ya choo, kisha akafunga mlango, akawa anachungulia kupitia tundu la ufunguo, akamshuhudia Mkuu wa Polisi akielekea nje.



    "Amekuja kufanya nini huku? Au amejipa likizo na yeye kutokana na kifo cha mwanae? Au anatufuatilia?" Sajenti Minja alikuwa anajiuliza mwenyewe huku akiwa bado yupo ndani ya choo.



    Baada ya dakika tano, Sajenti Minja alitoka chooni na kuelekea walipo wakina Kayoza,



    "vipi anko, mbona umekaa muda mrefu sana?",Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,



    "tumbo limenishika si mchezo, mimi naona nirudi nikapumzike, nyie endeleeni na ziara",Sajenti Minja hakutaka kusema ukweli, ingawa mshtuko wa kumuona Mkuu wa Polisi ulimfanye achoke ila hakuwa na sababu ya kuwaambia wenzake ukweli kutokana na yeye kutokuwa na jibu haswa juu ya uwepo wa Mkuu wa polisi katika eneo lile,



    "sisi tumeshamaliza, tulikuwa tunakusubiri wewe tu",Kayoza alimwambia Sajenti Minja,



    "haya bwana, mimi naelekea mjini, nyie nendeni tu nyumbani, njia si mnaikumbuka?",Mwenyeji wao aliwauliza,



    "tunaikumbuka bwana mkubwa",Sajenti Minja alijibu huku akijilazimisha kutabasamu,



    Kisha wakaagana na mwenyeji wao, na wao wakashika njia ya kurudi nyumbani.



    Sajenti Minja akaona huo ndio muda mzuri wa kuwaambia alichokiona, ingawa alitaka kuwaficha ila akaona haitakuwa vyema kuwaficha kwa kuwa wao ni wamoja na wamefika mkoa ule kwa lengo moja.



    "jamani nimemuoona Mkuu wa Polisi pale hotelini",Sajenti Minja aliongea kisha akawa anasubiri swali,



    "Mara hii umeshaonana na mkuu wa polisi wa mkoa huu, kweli nyie maaskari mnajuana sana" Omary aliongea huku akishangaa,



    "Sio wa mkoa huu, yule wa Shinyanga" Sajenti Minja alitoa Maelezo yaliyowafanya wenzake washtuke,



    "itakuwa umemfananisha",Omari aliongea huku akiwa bado anamshangaa Sajenti Minja,



    "nimemfananisha vipi?, wakati namfahamu fika",Sajenti Minja aliongea kwa kupaniki,



    "sasa huku kafuata nini?",Omari akamuuliza,



    "huwezi jua bwana, yule ni polisi, inawezekana anatufatilia sisi",Sajenti Minja aliongea kwa uhakika,



    "duniani wawili wawili mjomba",Kayoza aliongea baada ya kuwa kimya muda mrefu,



    "ok, mmeshinda, ila mtaniambia wenyewe",Sajenti Minja alimaliza, kisha wakaendelea na stori nyingine, huku Sajenti Minja akiwa hana amani kabisa katika moyo wake.



    Walipofika nyumbani, wakapelekwa moja kwa moja hadi kwenye chumba cha Bibi yake Kayoza, wakamsalimia, kisha wakatambulishwa, Bibi Kayoza alifurahi sana, alipomuona Kayoza, waliongea sana,



    "ila bibi pamoja na kukusalimia, kuna jingine lililonileta huku",Kayoza alimwambia Bibi yake,



    "hata usiniambie mume wangu, najua lililokuleta",Bibi yake Kayoza alimkatisha Kayoza,



    "nateseka sana bibi, naishi maisha ya kutafutwa na askari kama jambazi",Kayoza aliongea kwa majonzi,



    "ilikua lazima upitie hiyo hali mume wangu",Bibi yake Kayoza alisema na kumfanya Kayoza avute kamasi kwanza,



    "kivipi bibi?",Kayoza alihoji huku akifuta machozi,



    "bila ubishi wa baba yako na kiburi cha mama yako, yote yasingekukuta hayo",Bibi Kayoza alisema, kisha akawapa hadithi ile ile waliyopigiwa na Mama Kayoza.



    "yote hayo yamepita, kilichonileta huku ni dawa ya kuniachanisha na hili dudu",Kayoza aliongea kwa upole,



    "Futa kauli yako, usiseme hili dudu, kusema hivyo ni kosa kama mwananchi kumtukana rais wake" Bibi Kayoza alimwambia mjukuu wake tena hata sura yake ilionesha hakufurahishwa na kauli ya Kayoza,



    "Sasa ni jina lipi unaona linafaa kuitwa?" Kayoza aliuliza na yeye alipaniki baada ya kuna Bibi yake akikitetea kile kiumbe kinachomnyima yeye Furaha ya maisha,



    "Heshimu mazingira kama unataka kupona, kinyume na hapo hakuna kitakachowezekana" Bibi Kayoza aliongea maneno ambayo yalieleweka vizuri kwa Kayoza,



    "Sawa nimekuelewa bibi, sasa hapa nimekuja kufuata dawa" Kayoza alimwambia bibi yake,



    "dawa ipo, ila nitakupa usiku",Bibi yake kayoza alimwambia mjukuu wake,



    "kwani ni dawa gani bibi?",Kayoza aliuliza,



    "utaijua usiku huo huo",Bibi yake Kayoza alijibu,



    "Na kwanini iwe usiku bibi?" Kayoza aliendelea na udadisi wake,



    "Usiku kwa sababu ya kuwa watu wote wa hapa walioenda kazini watakuwa wamerudi nyumbani" Bibi Kayoza alijibu,



    "Kwani ni lazima wawepo?" Kayoza aliendelea kuuliza,



    "Ndio ni lazima wawepo, kwa sababu haya mambo yamekaa kimila, kwa hiyo basi ni lazima wanaukoo wote washiriki" Bibi Kayoza alijibu na kisha wakaendelea na hadithi zao binafsi kwa kushirikiana na Sajenti Minja na Omary ambao muda wote walikaa kimya ili kumuachia Kayoza uwanja mpana wa kuuliza maswali yake.



    **************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkuu wa Polisi alifanikiwa sio kupajua tu mahali walipofikia wakina Sajenti Minja, alipajua mpaka Mahalia wanapolala yaani chumba walichokuwa wanakitumia wakina Sajenti Minja.



    Mkuu wa polisi akapanga kuwa usiku huo ndio itakuwa mwisho wao kuvuta hewa safi ya duniani.



    ********************



    Usiku ulipoingia, wakakusanyika wanaukoo wote, kisha wakatangaza lengo la kuitwa pale, ambalo lilikuwa ni kumuamisha mzimu kutoka kwa Kayoza na kwenda kwa Baba yake mdogo. Watu wasiokuwa wa ukoo ule hawakuhusika kujumuika pale, kwa hiyo Sajenti Minja na Omari waliambiwa wakae vyumba vya uwani. Wakina Sajenti Minja wakaondoka na kuelekea uko uwani.



    Shughuli ikaanza ya kuuhamisha mzimu, yakaletwa maji masafi, mbuzi jike mwenye mimba na majani ya mitishamba ambayo waliyajua wao wenyewe.



    Kayoza akalazwa chini, na pembeni yake alikuwa baba yake mdogo, bibi akaanza vitu vyake.



    Muda wote huo, mkuu wa Polisi alikuwa anafuatilia kila kitu, mpaka kile kitendo cha wakina Sajenti Minja kuenda vyumba vya uwani alikiona, akawa anavuta muda ili akakamilishe azma yake, muda wake alioupanga ulipofika, akawa anaelekea kwenye chumba walichokuwepo Sajenti Minja na Omari, alipofika akagonga, bila ya kufikiria kuuliza mgongaji nani?, Omari akaundea mlango kisha akafungua, hakuamini macho yake alipomuona mkuu wa Polisi amesimama mlangoni huku kashika bastola, Omari kabla hajafanya chochote, alipigwa risasi kama nne hivi za kifuani, na kuanguka chini kwa kishindo mithili ya embe kubwa ambayo halijakomaa lililopopolewa mtini.



    Na kule nje kwenye tambiko, wakati bibi anaendelea na tambiko, ulisikika mlio wa risasi ulisababisha mstuko na kumpelekea bibi kuanguka na kufa kwa presha iliyotokana na mshtuko wa ulisababishwa na mlio wa risasi, Bibi akawa amekufa bila hata kufanikisha zoezi la kuuhamisha mzimu.



    Baada ya mlio wa risasi kusikika na bibi kuanguka chini kama mzigo, watu wote katika eneo lile walikurupuka, wingine wakiundea mwili wa bibi na wengine walikimbilia eneo ambalo mlio wa risasi ulitokea, wakakuta mtu akitokomea gizani kwa mbele yao mlangoni alikuwa Omary aliyekuwa amelala chini huku damu zikiwa zimemtapakaa,



    Sajenti Minja akamsogelea na kukaa chini huku machozi yakimtoka na kuchukua kchwa cha kayoza na kukiweza mapajani mwake, akawa anamuangalia Omary aliyekuwa anatabasamu huku kila akitoa funda la pumzi lilikuwa likitoka huku limeambatana na damu.



    Wenyeji wa pale walikuwa wanashangaa na wasijue la kufanya.



    Omary akafumbua macho na kumuangalia Sajenti Minja aliyekuwa analia, kisha Omary akaongea maneno machache tu,



    "Mk....juu ...wa...pol...isi" Omary aliongea kauli ambayo watu wengine hawakuielewa isipokuwa Sajenti Minja pekee.



    Omary baada ya kutamka maneno hayo, shingo yake ililegea na kuanguka, huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya Omary, roho yake ikatengana na mwili akiwa ugenini, kauli ya babu yake ikatimia.....



    ..maneno aliyoyatamka Omari, watu wote ambao walikuwa jirani nae akuna hata alielewa alichokimaanisha, Sajenti Minja peke yake ndiye aliyekuwa anaelewa kinachoendelea,



    Sajenti Minja alipogundua Omari amekufa, alilia sana. Na Kayoza ndio alichanganyikiwa zaidi, kwa maana alipata mapigo mawili kwa Mara moja, la kwanza ni kifo cha rafiki yake aliyetoka nae mbali toka mwanzo wa matatizo mpaka walipofikia, na pigo la pili ni kifo cha bibi yake ambaye ndio alikuwa msaada pekee wa kumsaidia mzimu umuachie.



    Sasa ikawa misiba miwili ndani ya nyumba moja.



    Misiba iliyoletwa na mkuu wa polisi, mmoja aliudhamilia ila mwingine hakuhudhamilia ila umetokea tu pasipo kutegemea na aliyesababisha hiyo misiba hana habari kama kitendo chake kimemuondoa mtu ambaye hausiki kabisa katika mipango yake.



    Na jambo vzuri ni kwamba hakuna aliyemuona mkuu wa polisi wakati akifanya tukio hilo isipokuwa Omary pekee ambaye nae ameshamtaja aliyemuua.



    Wanandugu walikaa na Sajenti Minja, na mwisho wakakubaliana kuwa Omari azikwe pale pale ili kuepusha gharama. Lakini Sajenti Minja alipinga na kusema yeye atagharamia kila kitu kuhusu mwili wa Omary, na alichofanya ni kuwasiliana na wazazi wa Omary na kisha ndugu wa Omary walifika Bukoba na wakauona mwili wa ndugu na wenye kulia wakalia.



    Baada ya hapo ndugu hao waliondoka na mwili wa ndugu yako na kwenda nao Tanga kwa ajili ya maziko.



    Huku kwa Bibi Kayozs Wakafanya maziko ya Bibi yake Kayoza.

    Walifanya maziko ya heshima kwa bibi Kayoza kwa maana yeye nae alikuwa make wa chief ambaye ndiye Babu yake Kayoza ambaye ndiye inaesemekana ndio huo mzimu aliokuwa nao Kayoza.



    Msiba ulipoisha, Sajenti Minja alimuita Kayoza na kumuweka kitako,



    "yaliyotokea nafikiri umeyaona, ni kama ajali kazini na hakuna jinsi zaidi ya kujipanga upya, maana bibi yako tuliekuwa tunamtegemea kuwa msaada kwako, amekufa, na Omari nae amekufa",Sajenti Minja alimwambia Kayoza ambae muda wote alikuwa amekaa kimya,



    "kwani huyo aliyempiga risasi Omari ulimuona?",Kayoza akamuuliza Sajenti Minja,



    "sikumuona na wala sikubahatika kuongea na Omari, ila neno la mwisho aliloniambia ni MKUU WA POLISI",Sajenti Minja alimfahamisha Kayoza,



    "ina maana Mkuu wa Polisi ndiye aliempiga risasi?",Kayoza akahoji,



    "mimi ndio nimeelewa hivyo, na niliwaambia kuwa nilimuona Mkuu wa Polisi, nyie mkabisha, haya ndio matokeo yake sasa",Sajenti Minja aliongea kwa uchungu,



    "nafikiri atakuwa bado hajaondoka pale Guest, na naimani ataondoka maiti",Kayoza aliongea huku akiwa anaondoka, hiyo kauli ikamshtua Sajenti Minja,



    "njoo, unakwenda wapi?",Sajenti Minja alimzuia Kayoza,



    "nipo hapa hapa",Kayoza alijibu huku akiwa amesimama mlangoni,



    "sasa mbona unaondoka huku tukiwa bado hatujafikia muafaka?",Sajenti Minja alimuuliza Kayoza,



    "muafaka gani tena?",Kayoza aliuliza kwa jazba,



    "ya yaliyotokea na hatua za kuchukua",Sajenti Minja aliongea kwa kubembeleza,



    "wewe uliniambia imetokea kama ajali na muafaka ulioniambia ni kujipanga upya, ila kwa kuwa huyu Mkuu wa Polisi amefanya ujinga kama kulipa kisasi kwa binti yake, ila akamuua Omari ambae hausiki na kifo cha binti yake, pia amesabisha zoezi la kutolewa mdudu mwilini kwangu lishindikane, basi adhabu anayostahili ni kifo, tena nitamuua nikiwa mzima kabisa, tena kwa mikono yangu miwili",Kayoza aliongea huku machozi yakimtoka, moja kwa moja akaamua kuenda nje kwa kuwa aliona kuendelea kuogelea hilo jambo ni kujiongezea hasira tu,



    "hapa nisipokuwa makini, naweza kumpoteza na huyu Kayoza",Sajenti Minja aliongea huku akijilaza katika kajitanda cha pale chumbani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mkuu wa polisi anachofanya ni kisasi, kama amemuua Omary, basi na Kayoza nae anahitajika kuuwawa, sio Kayoza peke yake, hata Mimi ni mmoja kati ya watu wanaowindwa na mkuu wa polisi, sasa sijui yupo peke yake au amekuja na watu wengine wa kumsaidia? Hii ni vita, tena vita ambayo tunapigana na adui aliye na silaha, cha muhimu ni kuwa makini, au tuondoke tu huku kwa maana hatuna cha kufanya tena, kilichotuleta kimeshindikana" Sajenti Minja alikuwa anawaza



    ******"***********



    Mkuu wa Polisi aliamini kwa asilimia zote kuwa, pale alipofikia, hakuna aliegundua kati ya wakina Sajenti Minja.



    "nimeanza na yule kibaraka, alafu anafata yule mshenzi Minja, Yuda Eskarioti, anaisaliti serikali?",Mkuu wa Polisi alijiuliza mwenyewe huku akijimiminia mzinga wa konyagi katika glass ndogo iliyokuwepo juu ya meza katika chumba chake.



    "Hivi kwanini nilivyogonga mlango asingekuja Minja kufungua? angeanza yeye kufa kazi ingekuwa rahisi sana. Ila hata hivyo sawa tu, kwa maana wanapambana na adui wasiyemtambua, hata atumie mbinu zake za kijeshi sijui, hawezi kunijua" Mkuu wa polisi aliongea kisha akatoa cheko kubwa sana alilolishushia na tusi la nguoni kumuelekea Sajenti Minja kisha akagida tena ile konyagi iliyokuwa katika glass yake ndogo iliyopo juu ya meza.



    "Alafu hii kazi imekuwa rahisi sana, kumbe naweza kuimaliza mapema kuliko hata nilivyodhani?, inawezekana, inawezekana kabisa, nataka Sikh ninayorudi shinyanga, nirudi nikiwa sina kisasi na mtu, nirudi nikaanze upya katika maisha yangu. Hivi utajisikiaje unapobahatika kupata mtoto mmoja, tena kwa tabu sana na miaka Mingi sana sana ya kusubiri huku ukivumilia maneno mengi sana kutoka katika jamii iliyokuzunguka?, alafu anatokea mpumbavu mmoja na kumuua huyo mtoto, ni lazima uchanganyikiwe, ni lazima uone dunia inakuelemea, dah jamani Martha wangu, my martha, baba yako nipo kwa ajili ya kukulipia kisasi, damu yako haijapotea bure mwanangu" Mkuu wa polisi aliongea huku akiwa anaiangalia picha ya Martha iliyokuwa katika simu yake ya mkononi.



    Siku hiyo aliifanya kama sherehe kwake, maana alikuwa anakunywa tu, huku alitaja sana jina la Sajenti Joel Minja.



    Saa moja baadae akawa hajitambui wala hajielewi, alizima huku akiwa amekaa katika kochi la chumba cha Guest.



    *********************



    "Hivi si naweza tu kummaliza huyu mtu, mbona hanishindi kabisa, au nitakuwa namuonea? Lakini mbona na yeye amemuonea Omary, Omary hana hatia, Omary alipaswa kufa kwa mipango ya Mungu na wala hakupaswa kufa kinyama namna hii tena ugenini. Ni vipi wazazi wake watajisikia? Haiwezekani kwa kweli, hii kitu kuivumilia ni sawa na kuacha matatizo yaendelee ingali una ufumbuzi wa kufumbua kinachokukabili" Sajenti Minja alikuwa akifikiri huku macho yake yakiangalia juu ambapo kulikuwa na paa ya nyumba ambayo ilijaa uchakavu kiasi.



    Sajenti Minja baada ya kufikiria sana, akaamua kwenda katika Guest aliyofikia Mkuu wa Polisi, akupata tabu kuingia ndani, akaenda mpaka ulipo mlango wa chumba alichofikia Mkuu wa Polisi, kwa taratibu na tahadhali kubwa, huku akiwa ameweka chupa ya soda katika mfuko wake wa suruali, kwa ajili ya kummaliza Mkuu wa Polisi.



    Tayari roho ya kinyama ilikuwa imefunika damu ya Sajenti Minja, roho iliyokuwa na imani ya kuwa njia nzuri ya kujilinda ni kumuua adui unayepambana nae.



    Sajenti Minja ameamua kuua na hakutaka kwenda na bastola bali ameona silaha inayomtosha ni chupa ya soda tu.



    Akashika kitasa cha mlango, kisha akaminya kwa chini...





    ..mlango haukufunguka,

    "amejifungia kwa ndani huyu",Sajenti Minja aliongea peke yake.

    Kisha akainamisha jicho lake mpaka kwenye tundu la ufunguo, pia hakuweza kumuona kwa ajili ya ufunguo uliokuwepo pale.

    Sajenti akaamua kuahirisha hazma yake, akatoka nje na kuelekea nyumbani.



    Kayoza muda wote alikuwa na mawazo tu, alikuwa hataki kuongea na yeyote zaidi ya Sajenti Minja. Nyele alikuwa hachani, mafuta hapaki, nguo moja aliweza kuvaa hata wiki, hakuwa mtanashati tena kama zamani, wageni wa eneo lile walikuwa wanamuona kama mvuta bangi.



    "vipi anko?",Kayoza alishtuliwa na sauti ya Sajenti Minja,

    "safi, ulikuwa wapi?, maana sijakuona muda mrefu kidogo",Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

    "nilienda pale hotelini kumchunguza huyo bwana mkubwa",Sajenti Minja aliongea huku akikaa chini,

    "umefanikiwa?",Kayoza akauliza kwa ufupi,

    "nilifika pale hotelini, ila yeye alikuwa ndani na mlango alikuwa ameufunga kwa ndani",Sajenti Minja alimjibu Kayoza,

    "kumbe ulitaka kuingia mpaka ndani!?",Kayoza akauliza kwa mshtuko,

    "ndio",Sajenti Minja akajibu kwa kifupi,

    "sasa ungefanikiwa kuingia ndani ungemfanya nini?",Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

    "unaona hii chupa, ndio ingekuja kutoa ushaidi wa chochote ambacho ningemfanyia",Sajenti Minja alijibu huku akimuonyesha Kayoza chupa ya soda,

    "na afadhali hukufanikiwa",Kayoza akaongea huku akikwepesha macho yake yasigongane na Sajenti Minja,

    "alah!, kwanini!?"Sajenti Minja akahoji,

    "nilishakuambia kuwa yule nitamuua kwa mikono yangu mwenyewe",Kayoza alijibu akiwa anaelekea ndani,

    "mh, hii kasheshe",Sajenti Minja alijisemea peke yake.



    Jioni ya siku hiyo, pale kwa bibi yake Kayoza kulikuwa na shughuli ya kutoa ng'ombe ambao ni wagonjwa, ili kesho alfajili wapelekwe mnadani, hiyo kazi ilifanywa na vijana wa pale, wakiwemo Kayoza na Sajenti Minja.



    Mkuu wa Polisi baada ya kuzinduka, akaenda kuoga kisha akaenda kuagiza chakula, baada ya kula akaingia chumbani kwake, kisha akaibeba bastola yake na kuelekea walipofikia wakina Sajenti Minja, giza lilikuwa limeshachukuwa nafasi yake,

    "afadhali wako nje",Mkuu wa Polisi alisema, baada ya kuona watu ndani ya zizi la ng'ombe.

    Akaenda sehemu ambayo imejificha na pia karibu na zizi waliokuwemo wakina Kayoza, akatoa bastola yake na kumuweka Sajenti Minja katika shabaha yake, aliweza kumtambua kutokana na taa ya chemri ambayo Sajenti Minja alikuwa kainyanyua juu usawa wa kichwa chake kwa ajili ya kuwamulikia wenzake.

    Mkuu wa Polisi akaikamata vizuri bastola yake,

    "ukalale mahali pabaya motoni Minja, usaliti ndio umekuponza, moja..mbili...tatu",Mkuu wa Polisi aliongea kwa sauti ndogo, kisha akahesabu na kufyatua risasi kumuelekea Sajenti Minja





    ...ukafuata mlio mkali ulioambatana na risasi, kisha kwa macho yake, Mkuu wa Polisi akashuhudia giza limetanda ndani ya zizi la ng'ombe alilokuwamo Sajenti Minja, huku kukifatiwa na kelele za watu, na wengi wao walikuwa wakionekana wanakimbia huku wakitoka ndani ya zizi la ng'ombe na tena wakiomba msaada.



    Kuona hivyo, Mkuu wa Polisi akaondoka katika lile eneo taratibu bila kuonekana na mtu, hata kama ungekutana nae njiani usingedhani kuwa ule mlio wa bastola uliosikika muda muchache uliopita ni yeye ndiye aliyefyatua, kwa maana nae alikuwa anakimbia hivyo kama watu wengine wa eneo lile walioshtuliwa na mlio wa risasi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijitahidi kukimbia kwa dakika mbili kisha akaanza kutembea mwendo wa kawaida, ni baada ya kuiacha kwa mbali nyumba aliyoifanyia tukio muda mchache uliopita.



    "asante Mungu, sasa nimebakiza kazi ndogo tu, kumuua yule anaejifanya shetani",Mkuu wa Polisi aliongea huku akiwasha sigara yake na kuvuta funda moja kisha apuliza taratibu na kuuangalia moshi uliokuwa unaelekea juu,



    "Kama sinema vile au hadithi ya kisasi kwa jinsi ninavyofanya matukio yangu, au kama Rambo anavyowamaliza wavietnam" Mkuu wa polisi aliongea peke yake na kisha akatoa tabasamu moja haya sana.



    Alikuwa kama hajitambui ni mtu wa aina gani? mtu anayeua na kufurahi hii inaonesha sio mzika, ila yeye hakujali wala hakufikiria hilo, baada ya kufanya tukio hilo la kinyama, alichokuwa akikiwaza muda huu ni pombe tu, tena alizidisha hatua zake za kutembea ili awahi kufika hotelini akanywe pombe, koo lilikuwa limemkauka.



    **************



    Baada ya Mkuu wa Polisi kufyatua risasi, ile risasi ilichomoka moja kwa moja na kulenga taa ambayo ilikuwa imeshikiliwa na Sajenti Minja usawa wa uso wake, risasi ikapasua kioo cha chemri na kusababisha baadhi ya vipande vya chupa kuingia kwenye macho ya Sajenti Minja hali ambayo ilisababisha maumivu makubwa sana machoni kwa Sajenti Minja, ila hakutaka kupiga kelele kwa kuhofia adui akimsikia amepiga kelele anaweza kusogea na kummalizia kabisa.



    Sajenti Minja aliamua kutulia chini kimya kama amekufa huku maumivu akiyavumilia.



    Baada ya muda mchache eneo lile lililokuwa na vurugu zilizotokana na mlio wa risasi lilitulia, ndipo wajomba zake Kayoza walipokuja sehemu aliyolala Sajenti Minja.



    "Mjomba upo salama?" Kayoza alimuuliza baada ya kumuona akijigeuza,



    "Nahisi nipo salama, ila macho yanauma sana, sijui kama yamesalimika" Sajenti Minja aliongea huku mikono yake ikiwa imeziba macho yake,



    "Ebu toa mikono nikuangalie" Kayoza alimwambia mjomba wake,



    "Hapana, bora nikishika hivi nasikia nafuu kidogo. Nipelekeni hospitali" Sajenti Minja aliongea,



    Wakina Kayoza wakambeba Sajenti Minja ambae alikuwa anaugulia maumivu na kumkimbiza ndani,



    "mjomba uko salama?",Kayoza alirudia tena kumuuliza Sajenti Minja,



    "macho, macho yangu jamani, naomba mniwaishe hospitali",Sajenti Minja alijibu katika sauti iliyoashiria anataka kulia,



    Bila kupoteza muda, wanaume wawili wakambeba juu juu na kumpeleka nje ambapo walienda barabarani na kukodi gari iliyompeleka hospitali.



    Walipofika hospitali, wakapokelewa na wauguzi na kupelekwa katika chumba cha Daktari, ambae alimuangalia kwa dakika kumi, na kuwaambia wauguzi wampeleke theatre.



    Baada ya Sajenti Minja kuingizwa katika chumba hicho, waliingia madaktari wapatao watano kwa ajili ya kumfanyia upasuaji mdogo wa macho Sajenti Minja,



    "Vipi mgonjwa, ilikuwaje kuwaje mpaka ikawa hivyo?" Daktari mmoja alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa amelazwa kitandani,



    "Hata sijui, sisi tulikuwa tunatoa mifugo zizini ndio tukasikia mlio wa risasi ghafla na inaelekea ilipiga taa niliyoibeba na vipande vyake vilinirukia machoni" Sajenti Minja alizungumza,



    "Mlipitia polisi kuchukua PF3?" Daktari aliuliza,



    "Uko ni kupoteza muda, kwa hiyo ningeendelea kupata maumivu kiss PF3?" Sajenti Minja aliuliza,



    "Lakini ndio utaratibu huo, bila PF3 hakuna matibabu" Daktari aliendelea kutoa maneno yaliyomchukiza Sajenti Minja,



    "Hata mimi ni polisi, kama hamtaki kunitibu niambieni" Sajenti aliongea kwa hasira huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kitambulisho chake,



    "Tufanye kazi jamani, tuache malumbano" Daktari mwingine wa kike alizungumza huku akivaa mipira (gloves) mikononi,



    "Mwenzako sio muelewa" Sajenti Minja aliongea,



    "Mgonjwa nawe mtata sana, haya jiandae nakuchoma nusu kaputi" Daktari wa kike aliongea kisha akamchoma sindano Sajenti Minja na kisha Sajenti Minja akapoteza fahamu, matibabu yakaanza sasa usiku huo huo.



    *****************



    Mkuu wa Polisi alirudi katika guest aliyofikia, kisha akaoga vizuri, akaagiza konyagi, alafu akajifungia ndani kujipongeza kwa kazi aliyofanya.



    Kama kawaida yake alikuwa anakunywa huku akitukana matusi kumuelekea Sajenti Minja, na safari hii kabla hajaweka jina Sajenti Minja, alikuwa anaanza na neno marehemu Sajenti Minja, kwa maana alikuwa anaamini amemuua kwa ile risasi moja aliyomlenga, hakujua kama imemkosa.



    Baada ya kunywa pombe nyingi, Mkuu wa polisi alilala pale pale kwenye kochi kama kawaida yake, hii ni siku ya tatu hakijui kitanda.



    Siku iliyofuatia, majira ya saa nne za asubuhi, Mkuu wa Polisi aliamua apitie katika maeneo ya karibu na nyumba waliyofikia wakina Kayoza kwa ajili ya kuangalia hali ilivyo, lakini alichotarajia kukiona hakukikuta, alitegemea kukuta msiba pale lakini akakuta hali ya kawaida ila kulikuwa na watu ambao walikuwa wamejitenga mafungu mafungu kuzungumzia tukio la siku iliyopita.



    "kuna nini kijana, mbona mko kimafungu mafungu hivyo?",Mkuu wa Polisi alimuuliza kinafiki kijana ambae alikuwa jirani na yeye,



    "ina maana hujui kilichotokea, au wewe mgeni hapa?",yule Kijana alihoji badala ya kujibu,



    "sasa ningejua ningeuliza?, vijana wa Sikh hizi sijui mkoje?",Mkuu wa Polisi akarudishia swali,



    "ni hivi mzee wangu, jana kuna mtu kapigwa risasi hapa ila kwa bahati nzuri hajafa, na wiki kadhaa zilizopita kuna mtu katika nyumba ile ile alipigwa risasi na kufa papo hapo",yule Kijana alimueleza Mkuu wa Polisi,



    "umesema aliyepigwa risasi hajafa!?",Mkuu wa Polisi aliuliza kwa mshangao,



    "ndio, kwani vipi mzee?",yule Kijana aliushangaa mshangao wa Mkuu wa Polisi,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hiyo risasi alipigwa wapi mpaka asife?, maana risasi sio kitu cha mchezo" Mkuu wa polisi alihoji huku akiwa ahamini kama ile risasi aliyopiga imemkosa Sajenti Minja,



    "Nasikia haijampata, ila ilipiga taa ambayo alikuwa ameibeba" Kijana alijibu na kumfanya Mkuu wa polisi akunje Sura kwa kusikia kuwa ile risasi ilimkosa Sajenti Minja,



    "Huu ujinga huu" Mkuu wa polisi aliongea kwa hasira na kujisahau kama na mtu mwingine,



    "Kwani vipi mzee?" Kijana aliuliza huku akishangaa hali aliyokuwa nayo Mkuu wa polisi,



    "hakuna kitu kijana, kwa hiyo kapelekwa hospitali?",Mkuu wa Polisi alihoji,



    "ndio, kapelekwa hospitali ya mkoa",yule Kijana alijibu.



    Mkuu wa Polisi akutaka hata kuaga, akageuka na kurudi guest,



    "mh!, yule mbwa ana bahati gani?, hapana, lazima nikammalizie pale pale hospitalini",Mkuu wa Polisi aliongea kimoyo moyo, kisha akachukua bastola yake na safari ya kuelekea hospitali ikaanza.



    Alipofika hospitalini, hakujua Sajenti Minja amelazwa wodi namba ngapi, ila baada ya kuuliza uliza kwa madaktari alifanikiwa kufika katika wodi aliyokuwepo Sajenti Minja, akaingia ndani ambapo alimkuta Sajenti Minja peke yake huku katika macho yake kukiwa na bandeji zilizomzuia kuona, alifungwa bandeji kubwa machoni make kutoka na upasuaji mdogo aliofanyiwa.



    Mkuu wa Polisi aliingia ndani ya wodi na kisha akaanza kumsogelea taratibu Sajenti Minja, alipomfikia, akaichomoa bastola yake, kisha akawa anajitayarisha kummaliza Sajenti Minja, tena alidhamiria kabisa, hata sura na macho yalionesha hivyo.....



    ..mara mlango wa wodi ukafunguliwa, alikuwa ni Daktari, Daktari alishtuka sana baada ya kumkuta Mkuu wa Polisi kashika bastola, Mkuu wa Polisi aliliona hilo, akawai kutoa kitambulisho,



    "alah, kumbe ni polisi, nimekuja kumpa huduma mara moja kwa hiyo nakuomba ukae nje kidogo",Daktari aliongea huku akitabasamu,



    Mkuu wa Polisi akatoka nje bila hata kuongea neno huku akishukuru kwa daktari kutokujua kitu chochote na pia alilaani kwa daktari kuingia ghafla kwa maana alimuaribia mpango wake.



    "polisi yuko wapi?",Sajenti Minja alihoji baada ya kusikia daktari akiongea na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi,



    "si mlikuwa nae hapa ndani",Daktari akajibu huku akimshangaa Sajenti Minja,



    "hapana, hakuna aliengia na kuniambia yeye ni polisi",Sajenti Minja aliongea kwa mkazo huku akimbishia Daktari,



    "Unachoongea ni kweli au unatania, kwa hiyo wewe unasema hujamuona!?",Daktari aliuliza kwa mshangao,



    "amini nilichokuambia, huyo polisi yukoje, na umejuaje kuwa ni polisi?",Sajenti Minja aliendelea kuhoji,



    "umri wake kati ya miaka 45 mpaka 50, alikuwa kashika bastola, aliponiona alinionesha kitambulisho ambacho kinaonesha ni polisi wa shinyanga",Daktari alieleza kwa urefu,



    "umesema wa shinyanga!?",Sajenti Minja alihoji kwa mshangao,



    "ndio, vipi unamjua?",Daktari aliuliza,



    "mhm, hapana",Sajenti Minja alijibu lakini mawazo yake yote akayahamishia kwa Mkuu wa Polisi,



    "ina maana amejua niko hospitali na amenifuata na bastola ili animalize?",Sajenti Minja aliongea kwa fikra.



    "Au ana mpango gani na mimi? Nani amemwambia nipo hapa? Huyu mzee ni hatari aisee" Sajenti Minja aliendelea kuwaza,



    "Mheshimiwa mimi natoka, nilikuja kukubadilishia drip tu" Daktari aliongea na kumfanya Sajenti Minja Stoke mawazoni,



    "Jamani kuweni makini na watu wanaoingia humu, sasa kama huyo uliyesema amekuja na bastola hata simjui, angalieni wasije wakanidhuru" Sajenti Minja aliongea kwa kulalamika kwa maana yoga ulimuingia tayari,



    "Sasa sisi hatuwezi kuzuia mtu, tunajua wote ni ndugu zako" Daktari alijibu Sajenti Minja,



    "Nyie ndugu zangu si mnawajua, kwanza msimruhusu mtu yoyote kuingia humu mpaka awepo yule kijana mwenye nywele nyingi zisizochanwa" Sajenti Minja aliongea huku akimaanisha ni Kayoza,



    "Lakini hata wewe si ni polisi?, hata huyu aliyeingia nae ni polisi mwenzako" Daktari alimwambia Sajenti Minja,



    "Atakuwa sio polisi, usikute amegushi tu kitambulisho, msimruhusu tena" Sajenti Minja aliongea,



    "Inaelekea una maadui wengi sana bosi" Daktari aliongea,



    "Fuata nilichokuambia, sitaki maneno mengi" Sajenti Minja aliongea huku zile bandeji zikiwa bado katika macho yake,



    "Sawa bosi, lakini kumbuka huwezi kuna alafu unaniletea ubabe" Daktari aliongea kwa utani huku akiondoka,



    "Kwa kuwa sioni ndio mumuingize kila mtu humu ndani?" Sajenti Minja aliuliza lakini hakuna aliyemjibu, Daktari alikuwa ameshatoka ndani kitambooo.



    Baadae wakina Kayoza walipofika, Sajenti Minja alimsimulia Kayoza kila kitu, Kayoza alishtuka, na kuahidi hatoondoka katika eneo la hospitalini mpaka Sajenti Minja apone.



    "Sasa wewe ukikaa hapa muda wote ni Mani ataniletea chakula?" Sajenti Minja alimuuliza Kayoza,



    "Sasa unadhani ni nini kifanyike kukulinda kipindi hiki ambacho una bandeji machoni?" Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,



    "Mi nadhani tumtafute mtu awe analeta chakula, alafu wewe ushinde hapa mpaka usiku alafu unaondoka" Sajenti Minja alimwambia Kayoza,



    "Sio kushinda tu, itanibidi nilale kabisa" Kayoza aliongea,.



    "Kulala na mgonjwa hawaruhusu" Sajenti Minja alimwambia Kayoza,



    "Itabidi waruhusu tu, kwa maana hawajaweka ulinzi wa kutosha" Kayoza aliongea huku hasira zikianza kumtawala,



    "Muda mwingine kuvunja sheria za mahali penye uongozi wake, unaweza kujitafutia matatizo, ni bora ufanye kama nilivyokuagiza" Sajenti Minja alimwambia Kayoza ambaye hakutaka kuendelea na mabishano badala yake alikitoa kwenye kikapu chakula walichomletea Sajenti Minja,



    "Hicho chakula mbona kinanukia vizuri, inaelekea kitakuwa kitamu sana" Sajenti Minja aliongea baada ya kusikia harufu ya chakula.



    "We ongea yote, ila usiku wa leo itanibidi niwe eneo hili" Kayoza aliongea kisha akatoka nje kwenda kununua maji na kumuacha Sajenti Minja akiongea mwenyewe



    ******************



    Mkuu wa Polisi baada ya kushindwa kufanikisha azma yake, alirejea katika Guest aliyofikia na kujipanga upya, baada ya kupita pita katika kichaka cha fikra zake, akaamua kuwa usiku lazima arudi kule hospitalini.



    Nae alishajua inawezekana asubuhi ile alishtukiwa baada ya kuondoka, na yeye sasa akaongeza akili za ziada ili usiku aweze kufanikisha lengo lake, na ilimbidi siku hiyo asiguse hata pombe kabisa. Chakula alichokula Sikh hiyo ni matunda tu, ndio alliamini kufanya hivyo kutaifanya akili yake ifanye kazi vizuri.



    Baada ya kula alipumzika nusu saa kisha akaenda kuoga, alipotoka kuoga alipanda kitandani na kulala ili kujiandaa na misheni aliliyopo mbele yake. Kumbuka hapo ilikuwa ni saa name mchana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamka saa mbili usiku na kwenda kuoga tena, kisha akavaa nguo zake za mazoezi na raba nyeusi, kisha akaichukua bastola yake na kuifanyia ukaguzi kidogo na kisha aliipachika kibindoni, alafu akachukua kisu kidogo kiasi na kukitia mfukoni kisha akanywa maji mengi sana na kushusha pumzi ndefu,



    "Mwenyezi Mungu naomba unilinde kwa kila hatua ninayopiga" Mkuu wa polisi aliongea na kutoka chumbani kwake na kuelekea nje.



    Safari ya hospitali ilikuwa inaanza sasa.



    Usiku wa saa tano na dakika zake, mkuu wa Polisi alikuwa katika maeneo ya hospitali, akajipenyeza mpaka mahali ilipo wodi aliyolazwa Sajenti Minja, kipindi hicho chote Kayoza alikuwa anamuona, Kayoza nae akawa anafuata kila hatua iliyokuwa inafanywa na Mkuu wa Polisi.



    Mkuu wa polisi alifanikiwa kupenya penya na mpaka kuingia katika wodi aliyolazwa Sajenti Minja.



    Mkuu wa Polisi baada ya kuingia katika wodi aliyolazwa Sajenti Minja, aliingia kisha akafunga mlango kwa ndani, akachomoa kisu kilichokuwa katika mfuko wake. Aliamua kutumia kisu kwa maana aliona akitumia bastola inaweza kutoa sauti kubwa na kusababisha watu kujaa eneo lile, kwa hiyo kufanya hivyo ni kujiweka hatarini.



    Kwa hiyo maamuzi aliyofikia ni kutumia kisu tu ili kutimiza dhamira yake.



    "Nani wewe?" Sajenti Minja aliuliza baada ya kusikia vishindo vya mtu vikimsogelea,



    "Mimi ni mtu mbaya" Mkuu wa polisi alijibu kwa sauti kavu iliyojaa utulivu,



    "Usiku huu unataka nini kwangu?"Sajenti Minja aliuliza huku akijitahidi kupapasa engo za kitanda,



    "Minja nimekuja kukuua, nimekuja kukuua Minja",Mkuu wa Polisi aliongea kwa hasira, wakati Sajenti Minja anataka kunyanyuka ili ajiokoe ilihali haoni, Mkuu wa Polisi alikishusha kishu katika jicho la kushoto la Sajenti Minja, na kujikuta Sajenti Minja akipiga kelele ambazo ziliwashtua wagonjwa wa wodi za jirani ambao wenye ahueni walienda katika mlango wa wodi ambako walimkuta Kayoza anaangaika kufungua, huku akilia kwa maana alihisi tayari mjomba wake yupo katika hatua za kupigania uhai wake kutokana na kelele alizozitoa.



    Wakashirikiana na kufanikisha kuuvunja mlangp, walipofika ndani kila mtu mwenye moyo mwepesi aliishia kulia au kuzimia, Sajenti Minja alikuwa amelala kitandani huku akiwa amejaa damu mwili wote, na kisu kikubwa kiasi kikiwa kimeshindiliwa katika jicho lake la kushoto, ila ndani hawakumkuta mtu mwingine zaidi ya Sajenti Minja peke yake na hakukuwa na dalili ya dirisha kuvunjwa wala njia nyingine iliyoonesha kuna mtu alitumia kutokea mule ndani.



    Watu wakawa wanashangaa lile tukio, wengine walidai ni mambo ya kishikirina, wengine wakasema alitaka kujiua, ila Kayoza yeye aliamini mule ndani kuna mtu, kwa hiyo akawa anaangaika kuangaza angaza kila mahali huku akiendelea na kilio kilichoambatana na chuki zilizojaa hasira.



    **********************



    Mkuu wa Polisi baada ya kumchoma visu visivyo na idadi Sajenti Minja, alisikia watu wakijaa mlangoni, alichoamua ni kupanda juu na kuingia kwenye singboard, lengo lake lilikuwa ni kutembea juu mpaka katika eneo ambalo atakuwa salama, ili atoke.



    Alitembea juu ya Dari mpaka alipofika usawa wa choo, akashuka na kuanza kuelekea nje, alitoka salama kabisa na alifanikiwa kwenda katika guest aliyofikia salama salmini, akiwa na imani kuwa kazi yake imekamilika, na sasa anadili na Kayoza pekee.



    Alipofika chumbani kwake aliingia bafuni na kunawa mikono, kisha akarudi ndani na kujitupa juu ya kochi, akajijiminia konyagi katika glass yake na kuigida yote kwa fujo...



    Mkuu wa polisi akainuka katika kiti na kuelekea tena bafuni, akaoga na kutoka kisha akavaa suruali ya kitambaa na shati, kichwani akavaa kofia ya uviringo maarufu kama parma au watu was miaka ya themanini na tisini uwa wanaziita Marlboro kutokana na nembo moja maarufu ya sigara ambayo ilikuwa na picha ya mtu akiwa juu ya farasi huku akiwa amevaa kofia ya namna hiyo, pia baadae hiyo picha iliweza kuweka kwenye picha za mifuko ya Tanzania na hiyo mifuko ikapewa jina hilo, yaani mifuko ya Marlboro.



    Mkuu wa polisi akatoka na kuelekea mitaa ya nyumba ya bibi yake Kayoza ili aone kama atakutana na habari za msiba wa Sajenti Minja.



    Aliweza kufika kwenye mtaa huo ila hakubahatika kusikia habari yoyote, ikaendelea kuzunguka zunguka pale bila mafanikio yoyote na mwisho akaamua arudi zake katika ile nyumba ya wageni huku akiamini kuwa tayari Sajenti Minja ameshakufa, aliamua kuamini hivyo tu ingawa hakusikia habari yoyote, aliamua tu kuamini kutokana na ule unyama alioutenda kule hospitali.



    Aliingia ndani ya chumba chake na kuvua shati lake na kofia, kisha akajitupa kitandani na kuwasha runinga na kuangalia vipindi vilivyokuwa vinaoneshwa kipindi hicho.



    *******************



    Ndani hospitali kulikuwa na patashika, madaktari walimuweka Sajenti Minja katika kitanda cha magurudumu na kuanza kusukuma kile kitanda kitanda mpaka chumba cha upasuaji, walipofika ndani ya chumba kile, walimuondoa nguo zote mwilini na kuanza kumfuta damu iloyokuwa imemtapakaa mwili mzima, walipomaliza kumfuta damu walikuta mwili wake una majeraha matatu tu, walikuta amechomwa kisu mbavuni, kifuani na katika jicho lake la kushoto.



    Walichofanya ni kuangalia kama hivo visu alivyochomwa kama vina madhara makubwa, mwisho waligundua kisu cha mbavuni na kifuani havina madhara sana, walichofanya ni kusafisha vidonda hivyo na kuvipaka dawa kisha wakavifunga na bandeji laini, ila tatizo kubwa lilikuwa katika kisu alichochokwa katika jicho lake la kushoto, ilionekana ndio kina madhara makubwa sana.



    "Ni nani mwenye ujasiri huu was kuingia hapa na kufanya unyama wa namna hii?" Daktari mmoja aliuliza,



    "Hapa kwetu usalama hakuna, huo ndio ukweli, na kama hii habari itafika ngazi za juu, basi tutakuwa mashakani" Daktari mwingine alijibu,



    "Ila mtu aliyefanya hivi inaelekea ana kiasi na huyu bwana, haiwezekani atoke uko na kuja moja kwa moja katika wodi aliyolazwa huyu bwana" Daktari mwingine alijibu,



    "Hilo sio jukumu letu, tunachotakiwa ni kumtibu tu mgonjwa, hayo mengine ni ya walinzi" Daktari wa tatu aliongea,



    "sasa itakuaje?", Daktari mmoja aliuliza huku akitegemea jibu kutoka kwa wenzake, lakini ilikua tofauti, kwa sababu hakuna hata mmoja alienyanyua mdomo wake kujibu,



    "ina maana hamjanisikia au?", yule Daktari aliuliza tena baada ya kuona kimya,



    "hapo mkuu hamna jinsi, itabidi aondolewe tu!",Daktari mmoja aliyevaa suruali ya jeans alijibu hivyo,



    "kwa hiyo inabidi afanyiwe uperation, si ndio?", yule Daktari ambae ndio alionekana mkuu aliuliza tena.



    "Hamna jinsi, itabidi iwe hivyo" Daktari mwingine aliongezea,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na makubaliano waliyofikia ilikua ni kumuondoa Sajenti Minja jicho lake.



    Na ndipo jicho lake la kushoto likaondolewa, na kupata kilema cha milele kilichotokana na shambulio lililofanywa na mkuu wa polisi.



    Kipindi chote, Kayoza alikuwa amekaa nje ya wodi huku machozi yakimtoka, mara ghafla Kayoza akashuhudia mlango wa wodi ukifunguliwa na wakatoka wauguzi wawili ambao walikuwa wanakisuma kitanda chenye magurudumu manne, huku wakifuatiwa na Madaktari wawili, Kayoza nae akaamka, kisha akaongozana nao mpaka katika mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi, Madaktari wakaingia ndani, Kayoza alibaki nje, muda wote Kayoza alikua hatulii, mara akanyanyuka kwenda katika mlango wodi aliyolazwa Sajenti Minja, akawa anatafuta upenyo ili aweze kuona kinachoendelea ndani, lakini bado hakufanikiwa, mwisho akaamua kusimama tu! kama mtu aliyekosa matumaini.



    Baada ya dakika kadhaa za kusubiri pale nje, Daktari mmoja akatoka ndani huku akiwa anaelekea maeneo zilipo ofisi za hospitali, ila alipofika usawa wa viti vya watu wanavyokaa watu wanaosubili wagonjwa wapo, Kayoza akasimama na kumkimbilia daktari,



    "Samahani Daktari, mgonjwa wangu ana hali gani?" Kayoza aliuliza huku akimuangalia Daktari aliyekuwa anatembea,



    "Mgonjwa wako yupi?" Daktari aliuliza huku akiendelea kutembea,



    "Yule aliyevamiwa na kuchomwa visu" Kayoza alijibu,



    "Ooooh. kijana, mgonjwa ni ndugu yako?",Daktari alimuuliza Kayoza,



    "ndio dokta",Kayoza alijibu,



    "mbona uko peke yako, hakuna watu wakubwa ulioongozana nao?",Daktari akauliza swali lingine,



    "hakuna, kwani vipi?",Kayoza akauliza huku akiwa na wasiwasi,



    "ok, nifuate ofisini",Daktari aliongea huku akiwa anaondoka.



    Kayoza akaongozana na Daktari mpaka katika ofisi ya huyo Daktari, akakaribishwa kiti, akakaa,



    "bila kupoteza muda kijana, hali ya ndugu yako umeiona na hakuna jinsi zaidi ya kuondolewa jicho, kwa hiyo tunasubiri azinduke, maana amepoteza fahamu, fahamu zikimrudia itambidi asaini kitabu cha upasuaji ili tumuondoe lile jicho",Daktari alikuwa anampa maelezo Kayoza,



    "hakuna shida Dokta",Kayoza alijibu,



    "sio unasema hakuna shida tu, je pesa ipo?",Daktari alimuuliza Kayoza,



    "kwani inahitajika shilingi ngapi?",Kayoza akauliza,



    "laki tatu",Daktari akajibu,





    "hakuna tatizo, pesa ipo",Kayoza alimwambia Daktari.



    "Wewe unafanya kazi?" Daktari akamtupia swali lingine Kayoza,



    "Hapana, mimi ni mwanafunzi" Kayoza alijibu,



    "Sasa pesa utazitoa wapi?" Daktari aliuliza,



    "pesa ipo kaka" Kayoza alijibu kwa kifupi,



    "Basi wewe nenda kalete hela" Daktari alimwambia Kayoza,



    "Je naweza kumuona mgonjwa wangu?" Kayoza aliuliza,



    "Hapana, utamuona akishafanyiwa upasuaji?" Daktari alijibu,



    "Sawa" Kayoza alijibu kwa unyonge.



    Kisha Kayoza akatoka katika ofisi ya Daktari, na kuelekea nyumbani, njia nzima alikuwa anawaza mtiririko wa matukio yanayomtokea, ila kwa sasa aliamini adui yake mkubwa ni Mkuu wa Polisi.



    Kayoza akaondoka na kwenda katika bar iliyo jirani na pale hospitali, akanywa soda, kisha akaondoka huku akiwa na mawazo mengi sana,





    "lazima nimuue yule mzee, ameniharibia tumaini langu la kupona na sijui hatma yangu ya maisha mpaka sasa, Mjomba minja anakuwa mlemavu kwa sababu yangu mimi, Omari rafiki yangu kipenzi nisamehe, umenisaidia sana ila mwisho umekuwa maiti kwa sababu yangu mimi, Denis nilikupenda sana jamaa yangu, ila...",Kayoza akashindwa kuendelea machozi yakawa yanamtoka, akasimama pembeni ya barabara huku machozi yakimtoka.



    Akashindwa hadi kutembea, akakodi taxi ya kumfikisha nyumbani.



    Kayoza alipofika nyumbani, aliwaambia waanze kutayarisha chakula cha mgonjwa, kisha Kayoza akaenda kuoga, alipotoka akaenda kuvaa, kisha akala chakula, alafu akachukua chakula cha mgonjwa na safari ya kuelekea hospitali ikaanza ingawa hakuwa na uhakika kama Sajenti Minja ataweza kula ila ilibidi abebe tu hivyo hivyo.



    alipokuwa anatoka nje, ndipo macho yake yalimshuhudia mtu ambae alikuwa anaelekea katika nyumba aliyokuwepo yeye.



    Kayoza machozi yakaanza kumtiririka katika mashavu yake, sababu ya uchungu wa yaliyomtokea, aliamua kulia kwa sauti kubwa huku akimuangalia yule mtu anaekuja, mwisho akaamua kuweka chakula chini na kukimbia kumuelekea yule mtu, yule mtu nae alikua anakimbia kumuelekea Kayoza....





    ...jinsi walivyozidi kusogeleana ndio machozi katika macho yao yalizidi kuongezeka, walikumbatiana kwa furaha iliyoambatana na uchungu wa kumbukumbu mbaya za nyuma, kwa dakika nzima hakuna aliyemsemesha mwenzake,



    "pole mwanangu, hiyo yote ni mitihani ya dunia", ndivyo mama Kayoza alianza kuongea maneno hayo ambayo aliamini yatamfariji mtoto wake,



    "kwanini mimi tu mama, kila uchungu unapita katika njia ya moyo wangu, kwanini mimi, nimemkosea nini Mungu?", Kayoza aliongea huku akilia,



    "yanapita hayo mwanangu, vumilia na uamini mungu yuko pamoja na wewe", Mama kayoza aliendelea kumfariji mwanae, kisha akaendelea,



    "hata mimi mjomba wako aliponipigia simu na kunieleza kifo cha Omary na bibi yako, nilisikitika sana na mbaya zaidi aliniambia kuwa bibi yako alikufa wakati anajiandaa kukutoa hilo dubwana linalokusumbua", Mama Kayoza alipofika hapo akanyamaza baada ya kuona Kayoza analia kwa uchungu sana.



    "mjomba wako yuko ndani?", Mama Kayoza aliuliza swali lililozidisha kilio kwa mwanae,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ina maana mama hujui?", Kayoza akajikuta anamtupia swali mama yake,



    "sijui nini?, mbona unanipa wasiwasi tena!", Mama Kayoza aliuliza kwa mshangao,



    "habari za mjomba Minja", Kayoza akaendelea kumfafanulia mama yake,



    "ehe, kaka yangu kafanyaje tena", Mama Kayoza akaendelea kuuliza huku tayari akiwa amejaa wasiwasi sana, kwa maana kauli za Kayoza zilianza kumtisha,



    "Mjomba minja alipigwa risasi, ila hakufa na jana kavamiwa na mtu asiejulikana na akamchoma kisu cha...", Kayoza alishindwa kumalizia baada ya mama yake kuanguka chini na kupoteza fahamu.



    Ikambidi Kayoza awaite ndugu zake wamsaidie, dakika tano zikapita bila Mama Kayoza kuzinduka.



    "Umemfanyaje mama yako?" Baba ake mdogo Kayoza alimuuliza Kayoza,



    "Sijamfanya kitu" Kayoza alijibu,



    "Amekuja saa ngapi?" Baba mdogo aliendelea na Maswali,



    "Ameingia muda si mrefu" Kayoza alijibu,



    "Mbona hajasema kama anakuja, au wewe alikupa taharifa?" Baba mdogo aliuliza,



    "Na wewe nawe punguza maswali yako bwana, si umsubiri azinduke ndio umuulize yeye mwenyewe hayo maswali" Kayoza aliongea kwa hasira baada ya kuona maswali yamekuwa mengi kuliko vitendo,



    "We unamjibu nani hivyo?" Baba mdogo aliuliza kwa hasira,



    "Kwani naongea na nani, au naongea na nyani?" Kayoza nae aliongea kwa hasira, na kufanya baba yake mdogo atake kumvaa ila ndugu wengine waliingilia kati na kumzuia baba yake mdogo apunguze hasira,



    "Kwanza tokea mmekuja hapa ndio matatizo nayo yamekuja, mna mikosi tele imewajaa" Baba mdogo aliongea kwa hasira,



    "Na bado mkosi mwingine unakuja" Kayoza alijibu huku akimpepea mama yake aliyekuwa bado amepoteza fahamu,



    "Tusijibishane Kayoza ujue nitakupiga" Baba mdogo aliongea huku akimnyooshea kidole,



    "Kunipiga huwezi, na sitaki tena malumbano na wewe, vinginevyo nitafanya kitu ambacho hutokaa unisahau" Kayoza aliongea huku akimuangalia baba yake mdogo kwa jicho Kali sana,



    "Utafanya nini sasa wewe?, we si Mbwa tu" Baba mdogo aliongea kwa hasira na kufanya watu wamtoe eneo lile kwa maana waliona hakukuwa na umuhimu tena watu hao kukaa pamoja muda huo.



    Baada ya baba mdogo kutolewa kidogo amani ilirejea katika eneo lile,



    "Mimi naona hawezi kuamka, ni bora tumpeleke hospitali" Ndugu mmoja aliongea huku akimuangalia Kayoza,



    "Hata mimi nilikuwa na wazo kama hilo" Ndugu mwingine aliongezea,



    "Twendeni tu, Hamna jinsi" Kayoza aliongea.



    Uhamuzi uliopitishwa ni kumpeleka hospitali, wakakodi gari la abiria, wakampakia mama Kayoza, huku Kayoza na Shangazi yake wakichukua jukumu la kumsindikiza.



    Walipokaribia eneo la hospitali, mama Kayoza alirejewa na fahamu zake,



    "unajisikiaje wifi?", Shangazi yake Kayoza alimuuliza Mama Kayoza,



    "safi, tunaelekea wapi?", mama Kayoza aliuliza,



    "hospitali", Kayoza alimjibu mama yake,



    Mama kayoza baada ya kusikia neno "hospitali", kumbukumbu zikamrudia, akaanza kuangua kilio ndani ya gari huku akitaja jina la Sajenti Minja.



    "Mama na wewe bwana, kwani amekufa?" Kayoza aliuliza kwa jazba,



    "Muache alie ili apunguze uchungu" Shangazi yake alijibu,



    "Sasa inakuwa ni Makelele tu kama tunamsiba bwana" Kayoza aliongea kwa kulalamika,



    "Siku hizi umekuwaje wewe, hivi hata hujioni kuwa upo tofauti?" Shangazi yake aliuliza huku akiwa amemkazia macho Kayoza na kufanya Kayoza akae kimya tu.



    Walipofika hospitali, Kayoza akaenda katika chumba cha Daktari. Maana alishakariri kila sehemu ya hospital na karibu madaktari wote wa ile hospitali walikuwa wanamjua Kayoza kutokana na kushinda sana eneo la Hospitali.



    "ooh, afadhali dogo umekuja, maana tulikuwa tunakusubiri wewe", Daktari alikua akimwambia Kayoza maneno hayo,



    "vipi hali ya mgonjwa wangu?",Kayoza alimtupia swali Daktari,



    "mgonjwa wako bwana,...tayari tumeshamfanyia upasuaji, na tumefanikiwa kulitoa jicho lake la kushoto, ila tumemuwekea jicho la kondoo", Daktari alijibu kwa ufasaha swali la Kayoza,



    "kwa hiyo gharama zote ni kiasi gani?", Kayoza aliuliza,



    "ni milioni mbili na laki tatu, kwa sababu hata hilo jicho la kondoo tumelinunua kwa pesa nyingi kidogo", Daktari alimuelewesha Kayoza,



    "Ila dokta si ulisema ni laki tatu tu?" Kayoza alimuuliza daktari huku akimshangaa,



    "Ila si nimekwambia hilo jicho la kondoo tumelinunua" Daktari aliongea huku akitabasamu,.



    "Sasa hicho la kondoo ndio milioni moja?, si ungeniambia mimi nilete, ningekuja nalo tu kwa maana nyumbani tuna kondoo wengi tu" Kayoza aliongea huku akimshangaa daktari,



    "Ninaposema jicho la kondoo simaanishi ni jicho la kondoo mnyama, ninachomaanisha ni jicho la bandia" Daktari aliongea huku akitabasamu,



    "Ila milioni mbili na laki tatu ni nyingi sana, siwezi kuzimudu" Kayoza aliongea kwa sauti ya unyonge.



    "Wewe una shilingi ngapi?" Daktari alimuuluiza,



    "Mimi nilijiandaa na hiyo laki tatu, ila itanibidi niongeze na laki mbili, kwani ndio niliyonayo" Kayoza alizungumza,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa nipe hiyo, ila mwenzangu yoyote akikuuliza useme umenipa laki tatu" Daktari aliongea huku akimtazama Kayoza,



    "Ila hapa sina" Kayoza alijibu,



    "Aaaagh dogo, zikwapi sasa?" Daktari aliuliza huku akionekana hajafurahishwa na kauli ya Kayoza,



    "Nitakuletea kesho asubuhi" Kayoza alimuelewesha Daktari,



    "Zamu yangu inaisha leo ila itanibidi nikusubiri mpaka kesho utakapoleta, na ulete kweli kesho" Daktari aliongea kwa mkazo,



    "sawa dokta, nitazileta kesho hasubui", Kayoza alijibu.



    Baada ya hapo, Daktari akatoka na Kayoza na kwenda katika wodi aliyolazwa Sajenti Minja, huku wakiambatana na Mama na Shangazi wa Kayoza.



    **********************



    BAADA YA MWEZI



    Jumamosi asubuhi ndiyo siku ambayo Sajenti Minja aliruhusiwa kurudi nyumbani huku akiwa na ulemavu wa maisha. Kayoza na Mama yake ndio walikwenda kumchukua hospitali.



    Walipofika nyumbani, walipokelewa kwa furaha sana,



    "itabidi leo tufanye sherehe ya kumshukuru Mungu kwa maajabu aliyoyaonesha kwa bwana Minja", Baba yake mdogo Kayoza alitoa wazo,



    "hapana baba, sherehe iwe kesho",Kayoza aliongea huku akiwa na sura ya furaha,



    "kwanini unataka iwe kesho mwanangu?", Baba yake mdogo alimuuliza Kayoza,



    "kwa sababu kesho nataka kufanya kitu ambacho kitakua kama historia ya kumbukumbu nzuri ya ushujaa kwangu", kama kawaida yake, Kayoza aliongea huku akiwa na tabasamu,



    "mh! kitu gani hicho?", Mama Kayoza alimuuliza mtoto wake,



    "hampaswi kuwa na haraka, nyie ngojeni nataka iwe kama tukio la kushtukiza kwenu", Kayoza alimjibu mama yake,



    "haya bwana, sisi tunasubiri kwa hamu.



    ******************



    Kesho yake ambayo ilikua jumapili, mida ya saa nne asubuhi, Kayoza akaondoka kwao bila ya kuaga na kuelekea katika ile guest aliyopanga Mkuu wa Polisi, alipofika mapokezi, alimuuliza yule muhudumu kama mtu aliyemfuata yupo, akajibiwa yupo tena amelewa sana, Kayoza akaenda mpaka katika mlango wa chumba cha Mkuu wa Polisi, aliingiza mkono katika mfuko wa suruali na kutoa kitambaa ambacho alifunga puani, kama mtu anayezuia harufu fulani.



    kisha akagonga mlango huku akiwa kashika chupa tupu ya soda mkononi, mkuu wa Polisi akauendea mlango, kisha akaufungua, alipofungua tu, alikutana na chupa ya kichwa iliyompeleka moja kwa moja sakafuni, Kayoza akatumia vizuri nafasi ya kumshambulia mfululizo mpaka Mkuu wa Polisi akawa hatamaniki kwa jinsi alivyokuwa anavuja damu kichwani, ghafla Mkuu wa Polisi akampiga teke Kayoza na kusababisha chupa imponyoke Kayoza, Mkuu wa Polisi kwa kasi ya mshale, akakimbilia katika kitanda chake, akaunyanyua mto, kisha akachukua bastola yake na kumuelekezea Kayoza,



    "mwanaharamu mkubwa wewe, kwa kitendo ulichonifanyia, sio rahisi nikikuacha hai", Mkuu wa Polisi aliongea huku akikoti risasi katika bastola yake, Kayoza alitawaliwa na hofu na kukata tamaa. Aliamini hapo ndipo mbio za kupambana na Mkuu wa polisi zake zilipoishia.



    Mkuu wa polisi akaweka target katika paji la uso wa Kayoza, Kayoza akafumba macho kuashiria kukata tamaa, Kisha Mkuu wa Polisi akafyatua risasi..



    ...lakini risasi haikutoka, Mkuu wa polisi akajaribu tena, lakini hali ikawa ile ile, bastola ilikua haina risasi, Mkuu wa Polisi akaruka mpaka kwenye kabati, akachukua mfuko wa risasi, Kayoza kuona hivyo, akaikimbilia chupa ya soda aliyokuja nayo, ambayo ilikuwa karibu na mlango, ile kuikota ili amuwai akakuta tayari Mkuu wa Polisi anaikoki bastola, Kayoza akamuwai, akarusha ile chupa ambayo iliupiga mkono wa Mkuu wa Polisi ambao ulikua umeshika ile bastola na kufanya ile bastola iende chini, Kayoza akaruka juu na kumpiga teke Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Polisi akadondoka chini, Kayoza akaiokota ile bastola na kumfyatulia Mkuu wa Polisi risasi zisizo na idadi mpaka akafa. Kisha hapo ndipo akakiri kuwa ana kosa sasa la mauaji, kwa maana ameua kwa kukusudia tofauti na anavyoua kipindi mzimu unapompanda.



    Kayoza akaenda katika kabati na kuvunja kioo, akachukua kipande cha kioo, kisha akachukua ndoo iliyo mule ndani na kwenda sehemu ulipo mwili wa Mkuu wa Polisi, akaanza kuuchinja huku akikinga damu kwa kutumia ile ndoo, mpaka aliporidhika. Na kumbuka kipindi chote hicho alikuwa na kitambaa puani ambacho alikipulizia pafyumu kwa ajili ya kuzuia harufu ya damu ya aina yoyote ile.



    Baada ya kufanya ukatili huo ambayo hakutaka kabisa kuujutia, Kayoza alicheka mwenyewe ndani ya chumba ambacho alifanyia mauaji na kisha Kazi kubwa ambayo ilimkabiri kwa wakati huo ikawa ni kutoka nje, maana watu walishajaa nje.



    Akachukua kichwa cha Mkuu wa Polisi akakiweka ndani ya ndoo, kisha akaifunika ndoo, safari ya kwenda nje ikaanza, alipofungua mlango watu wote wakatawanyika, kwa maana waliamini Kayoza sio mtu wa kawaida kabisa, na ili kuwatisha zaidi, Kayoza akapiga risasi hewani, watu wakakaa nae mbali kabisa, nguo zote alizozivaa zilikuwa zimetapakaa damu, ila yeye hakuweza kuisikia harufu ya damu kutokana na kitambaa alichojifunga puani kwa ajili ya kuhofia mzimu kumpanda endapo harufu ya damu itapenya puani mwake.



    Akatoka na ndoo yake mpaka kwao, huku akifuatwa na kundi la watu na waandishi wa habari walikuwepo, tena wengi walikuwa na furaha kwa sababu ya kupata habari itakayouza magazeti yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Njia nzima alikuwa akitembea huku kundi kubwa sana la watu likimfuata na kila mmoja akisema lake kutokana na ukatili ule waliokuwa wanaushuhudia mubashara, kwa maana vitu kama vile walishazoea kuviona katika filamu za watu wa mashariki mpwa dunia au kukutana navyo katika simulizi za wakina ALEX KILEO.



    Alipofika kwao, akatoa onyo kuwa, mtu yeyote asimsogelee, na mtu ataekaidi amri, atampiga risasi. na kweli walimuogopa kwa maana Kayoza wa siku hiyo hakuwa na chembe za ubinadamu kabisa, hata sura yake ilidhihirisha hiyo kwa maana zile damu zilizomtapakaa mwili mzima na macho yake yalivyokuwa mekundu yalionesha hakuna hatari anayoiona mbele yake. Tayari alishaamua kuwa mnyama na aliona hiyo ndiyo bora ya kufanya kwa wakati huo.



    Baada ya kufika kwao, Kayoza akaingia katika chumba chake akajifungia mlango kwa ndani, hapo ndipo alipodhamilia kufanya kama Maelezo ya mganga wa mwisho kumtembelea yalivyosema, akakumbuka kuwa mganga alisema kuwa njia ya kuundoa huo mzimu inaweza kugharimu na maisha yake, yaani maisha ya Kayoza, hata Sajenti Minja alipouliza ni njia gani hiyo? Mganga alijibu kuwa itabidi achinjwe kondoo alafu Kayoza awekwe katika kitanzi ili harufu ya damu itakapoingia puani kwa Kayoza ni lazima mzimu umpande, na hapo ndipo ile kamba ya kitanzi ivutwe na imnyonge kayoza, ni lazima kayoza ni lazima afe na mzimu ufe kwa maana mzimu hutegemea pumzi katika kutoka na kuingia katika mwili wa Kayoza.



    Baada ya Kayoza kuyakumbuka maneno hayo, alijikuta akitabasamu, tabasamu la umauti lililokuwa linatoka pasipokuwa na furaha ila hasira zilizotokana na kukata tamaa ya kupata suluhisho la matatizo yake.



    kisha akachukua kamba akaitundika juu na kuweka kitanzi, kisha akaweka stuli na kupanda juu, alafu akaifunua ile ndoo ambayo aliiwekea damu ya Mkuu wa Polisi, akakitoa kile kichwa na kukitupia chini ya kitanda, kisha akajifungua kile kitambaa puani, harufu ya damu ikampenya sawa sawa katika matundu ya pua yake, alivyoanza kuhisi dalili ya kupandwa na mzimu akaitupa ile ndoo, na kuitegua stuli, mzimu ukawa tayari umeshampanda, na kitanzi kikambana sawa sawa, Kayoza na mzimu wake, akaanza kupiga kelele kwa sauti ya ajabu, hali iliyofanya watu waliokuwa nje ya nyumba watawanyike.



    Nje, kwanza ilipiga radi kubwa sana, huku ikifuatiwa na upepo mkali sana, mpaka nyumba zenye udhaifu zilianguka, alafu ikanyesha mvua kubwa sana ikiambatana na jua kali sana.



    Kayoza ilimchukua kama dakika thelathini kuangaika juu ya kitanzi, mwishowe alitulia kimya kabisa, na ukawa ndio mwisho wa maisha yake na mzimu wake.



    Polisi ndio walikuja kuvunja mlango na kuukuta mwili wa Kayoza unatoa moshi na ulikuwa mweusi sana kuashiria alikuwa anaungua, macho na masikio yalikuwa yametoboka, hakika kilikuwa kifo kilichosikitisha sana, kifo ambacho kilihitimisha urithi wa kimizimu katika ukoo.



    Sajenti Minja alilia kama mtoto kutokana na yote aliyofanya katika kumlinda Kayoza na uhai wake, lakini ilikuwa kama bure, na mbaya zaidi aliyakumbuka maneno ya Kayoza ya jana yake, ambayo Kayoza alidai anataka sherehe ifanyike leo kwa sababu anataka kufanya jambo la kukumbukwa daima.



    "kumbe jambo lenyewe ndio hili, umelifanya mapema sana mjomba, ungesubiri mjomba, kama ungesubiri nina uhakika uhai wako usingetoweka", Sajenti Minja aliongea mbele ya jeneza la Kayoza ambalo liliwekwa mbele ya watu kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu Kayoza.



    Mama Kayoza alianguka na kuzimia mara nne, kitendo ambacho kilisababisha apelekwe hospitali na ikagundulika mshtuko wa moyo.



    Mambo ya maziko yalienda kama kawaida na kumalizika salama.



    Kwa upande wa Mkuu wa Polisi, mwili wake ulizikwa na manispaa ya mkoa wa Kigoma kutokana na kutopatikana kwa kichwa chake ambacho Sajenti Minja alikificha makusudi ili kupoteza ushahidi na baada ya Siku alienda kukizika.



    Uko kwao Shinyanga hawakupata taharifa yoyote, habari zilizotangazwa kwa wafanyakazi wenzake yaani polisi wenzie ni kuwa amepotea na hajulikani halipo.



    BAADA YA MIAKA 3



    Anaonekana Sajenti Joel Minja akiwa na familia yake, wakiweka shahada la maua katika kaburi la Mama Kayoza ambae alikufa mwaka mmoja uliopita kutokana na ugonjwa wa mshtuko wa moyo alioupata kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye kipenzi (Kayoza).

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sajenti Minja aliacha kazi kutokana na ulemavu alioupata, sasa hivi ni mjasiliamali ambae ana kampuni yake binafsi ya usafirishaji wa abiria, ambayo inamiliki mabasi, maroli, daladala na taxi. Mabasi yake ni maarufu sana katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Tanga, Yanaitwa GHOST MEMORY.



    Ana mke na watoto wawili, wa kwanza anaitwa Kayoza, na wapili anaitwa Omari, ikiwa kumbukumbu kwa watu wake wa karibu.



    ******* MWISHO *******



0 comments:

Post a Comment

Blog