Search This Blog

NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE - 3

 







    Simulizi : Nilifanya Mapenzi Na Maiti 20 Nitajirike

    Sehemu Ya Tatu (3)



    YULE mzee sikuweza kumfahamu kwa kipindi kile lakini sauti yake, hapo baadaye nilimfahamu kwani nilikutana naye mara kwa mara. Baada ya kuzungumza hivyo, akatoa kidumu na kumpa mlinzi yule ambaye akakichukua na kuondoka nacho.



    Sikutaka kubaki hapo nje, nikamfuata mlinzi mule mochwari alipokwenda. Nilipoingia, nikakuta akimwambia mwenzake kwamba kulikuwa na dili jingine, kuna mtu alifuata maji ya maiti.



    “Hakuna tatizo! Twende kule kwenye maiti za wiki iliyopita!” alisema mlinzi aliyeletewa taarifa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWAGIKA NAYO HAPA…



    Wakatoka na kuelekea kwenye moja ya masanduku yaliyokuwa mwisho kabisa ambayo yalikuwa na maiti zilizokuwa na muda mrefu humo mochwari. Wakafungua sanduku moja, wakatoa maiti ya msichana na kuiweka juu ya meza moja kisha kuanza kuiosha huku wakikinga maji na kuyaweka katika sufuria kubwa kabla ya kuyaweka katika kidumu kile.



    “Mungu! Kumbe haya ndiyo yanayotokea!” nilijikuta nikisema.



    Waliendelea na zoezi lao mpaka walipomaliza na kujaza kile kidumu, yule mlinzi akaelekea nje na kumpa yule mzee, gari likawashwa na kuondoka mahali hapo.



    Wakati ikiwa imefika saa nane usiku, hapo ndipo mganga yule akatokea hapo ndani na kunifuata. Kabla ya kuzungumza lolote, akaniangalia machoni, aliiona hofu niliyokuwa nayo.



    “Upo sawa?” aliniuliza.



    “Ndiyo! Nipo sawa na nipo tayari kwa kazi,” nilimwambia.



    Alichokifanya mganga yule ni kuuchukua usinga wake, akaanza kuimba wimbo ambao sikuwa nikiuelewa. Aliimba kwa sauti kubwa iliyonifanya nione kama wale walinzi wangesikia lakini haikuwa hivyo.



    Waliendelea kupiga stori huku mganga yule akiendelea na wimbo wake. Alipomaliza, akalifuata sanduku moja, akalitoa pale lilipokuwa. Nilibaki nikiwa nimeduwaa tu, sikuamini kilichokuwa kikiendelea, sanduku lilikuwa zito lakini yeye alivyolishika ilikuwa ni kama mtu aliyeshika kikaratasi.



    Akaliweka chini, akalifungua na kisha kuiangalia maiti ile. Niliogopa, hata kusogea kule sikuweza. Wakati nimesimama huku nikiwa nimeduwaa, yule mganga akachukua unga fulani na kuipaka maiti ile kisha kuanza kuzungumza maneno ambayo sikuyaelewa, ghafla, katika hali iliyonishtua, nikaiona maiti ile ikiinua mkono wake.



    “Mungu wangu!” nilisema kwa mshtuko, sikuamini kile nilichokiona. Mganga yule hakunyamaza, aliendelea kuzungumza maneno yale, mbali na mkono, ile maiti ikainuka na kisha kukaa kitako mulemule kwenye sanduku. Mpaka kufikia hatua hiyo, nilitamani kukimbia. Jasho lilinitoka.



    Kuna kipindi nilihisi kile kilichokuwa kikitokea kilikuwa ni ndoto, nilitamani kukimbia lakini miguu ilikuwa mizito.



    Kadiri muda ulivyozidi kusonga mbele ndivyo nilivyozidi kushikwa na hofu. Kumbuka kwamba hiyo ilikuwa usiku wa manane, tena tukiwa mochwari, najua umeshapata picha ni jinsi gani nilikuwa na hofu moyoni mwangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule mganga hakunyamaza, akawa anazungumza maneno ambayo sikuyaelewa kabisa. Aliponitupia macho niliyahamisha yangu na kuiangalia ile maiti iliyokuwa imeketi kitako kama mtu aliyekuwa akitaka kuzungumza na yule mganga.



    “Usiogope Zakia,” aliniambia huku akiniangalia lakini nilikuwa na hofu.



    Nikaanza kuyakumbuka maneno ya yule mganga aliyoniambia kipindi cha nyuma kwamba kama kweli nilitaka kuwa tajiri basi ilinibidi nikubali sharti la kufanya mapenzi na maiti ishirini, kwa hiyo ile maiti iliyokuwa mbele yangu ilikuwa ya kwanza.



    Nilikubali lakini ndani ya mochwari ile lilionekana kuwa jambo gumu mno, kufanya mapenzi na maiti. Tena kama ile iliyokuwa ikitisha iliyoonekana kabla ya kuwa maiti, mtu huyo alipata ajali mbaya, kama si gari, basi ilikuwa treni kwani mwili wake ulikuwa na majeraha mengi.



    “Njoo huku,” aliniambia yule mganga, nikaanza kusogea kule alipokuwa.



    Akaniambia nikae kwanza, nilitakiwa kuvuta pumzi na sikutakiwa kuogopa. Nilikuwa kimya, nilikuwa na hofu sana nikiogopa.



    Maiti ile ikafumbua macho yake na kuanza kuniangalia, kuna kipindi nilikuwa nikijiuliza kama kweli ile ilikuwa maiti au nilikuwa nikichezewa mchezo. Majibu ya Swali langu hilo lilipatikana kila nilipokuwa nikiuangalia mwili wake, ilionesha dhahiri kwamba ilikuwa maiti.



    “Upo tayari?” aliniuliza mganga.



    “Ndiyo! Ila….”



    “Ila nini tena?”



    “Nitaweza kweli?”



    “Usijali! Utaweza. Kwani hujawahi kufanya mapenzi na mwanaume?” aliuliza mganga huku akiniangalia usoni.



    “Nimewahi!”



    “Basi jua hakuna tatizo,” aliniambia.



    Nilibaki nikimwangalia tu, kuna kipindi nilijuta kwa nini nilitaka kuwa tajiri na wakati masharti ya utajiri wenyewe yalikuwa magumu kiasi hiki. Nilibaki nikisononeka lakini kumbuka kwamba nilitamani kuwa tajiri hivyo chochote kilichokuwa kinatokea mbele yangu, nilikubaliana nacho.



    “Vua nguo zako,” aliniambia.



    Wakati hayo yakiendelea ndani ya mochwari, wale walinzi hawakuwa wakijua kitu chochote kile, hawakutuona hivyo kufanya kila kitu kwa kujiachia. Baada ya kumaliza kuvua nguo zangu na kubaki kama nilivyozaliwa, akaniambia nipande juu ya meza, nikafanya hivyo, nikalala chali.



    Ndugu yangu, ninachokwambia hapa ni kweli kabisa, kilinitokea katika maisha yangu, kipindi kile nilipokuwa nikisaka utajiri kwa udi na uvumba. Ghafla nikaiona maiti ile ikisimama kutoka ndani ya sanduku na kuanza kuvua nguo zake zilizokuwa zimechanikachanika kutokana na ajali, baada ya hapo, akapanda pale juu.



    “Mkimaliza, utatoka nje, hili sanduku usiwe na hofu nalo, litarudi tu lilipokuwa,” aliniambia yule mganga na kisha yeye kutoka ndani ya mochwari ile na kwenda kunisubiri nje.



    ****



    Kilichoendelea ndani, ni kufanya mapenzi na maiti ile. Huwa ninasikia maumivu mno moyoni mwangu kila ninapokumbuka mambo haya ambayo yalinitokea. Ninaamini kwamba mtu anapokufa, kuna roho huwa inabaki na ndiyo maana unapofika makaburini usiku, kuna sauti huwa zinasikika, mbali na roho iliyokufa, kunakuwa na roho nyingine ambayo bado ina uhai.



    Hiyo ndiyo roho aliyokuwa nayo ile maiti, roho yake ya kwanza ilikuwa imekwishatoka na kwenda kwenye hukumu, iliyokuwa ikifanya yote hayo ni roho ya pili ambayo ilimpa pumzi.



    Pale juu, niliendelea kufanya mapenzi na maiti ile, ilikuwa ni kama nafanya mapenzi na binadamu aliyekuwa hai. Nilisikia maumivu makali chini ya kitovu, nilipiga kelele lakini haikujali, iliendelea kama kawaida yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitendo kile kilichukua dakika arobaini, ilipomaliza, ikasimama, ikavaa na kisha kuingia ndani ya sanduku lile. Sikuvaa, nilibaki kuangalia nione kitu gani kingetokea. Wakati imeingia kwenye sanduku lake, likajifunga na kuanza kuinuka, likajiingiza katika sehemu yake na kutulia.



    Sikutaka kubaki humo, nilichokifanya ni kuinuka, kuvaa nguo zangu na kutoka ndani ya mochwari ile. Walinzi walikuwa wakipiga stori, sikujali, nikatoka mpaka nje, nilipofika huko, nikamkuta mganga akiwa na tabasamu pana kabisa huku akitingisha kichwa chake juu chini, chini juu kuonyesha kukubaliana na kile kilichofanyika.



    ****



    Mganga alinipa uhakika kwamba kila kitu kingekuwa kama kilivyotakiwa kuwa. Kwa kweli nilimwamini sana na kuona kuwa hivi karibuni ningekuwa tajiri mkubwa mno nchini Tanzania na hivyo kurudi kijijini nikiwa shujaa.



    Siku iliyofuata, mganga akaniambia nirudi nilipokuwa nikiishi ambapo sikutakiwa kumwambia mtu yeyote juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Sasa ratiba ikawa ni kwenda kwa mganga kila siku, ananichukua kimazingara na kunipeleka mochwari ambapo kama kawaida nilikuwa nikiendelea kufanya mapenzi na maiti.



    Siku ya kwanza niliogopa sana lakini siku zilivyoendelea kwenda, hofu ikaniondoka na hivyo kuwa na ushujaa mkubwa moyoni mwangu. Nilipitia mengi kipindi hicho, wakati mwingine nililetewa maiti zilizoungua moto, zilitisha sana lakini ilikuwa ni lazima nifanye nazo mapenzi, wakati mwingine nililetewa maiti zilizopata majanga mengine, zote hizo, nilivumilia.

    Siku zilikatika mpaka nilipobakiza maiti moja. Mganga akaniambia kwamba hiyo sikutakiwa kufanya nayo kule mochwari bali nilitakiwa kufanya nayo sehemu nyingine kabisa, tena makaburini.



    Kwa kweli niliogopa sana, sikujua kitu kilichonitisha kwani kiukweli kati ya makaburini na mochwari, mochwari kulitisha zaidi. Usiku, mganga akanichukua na kuniepeleka katika makaburi fulani yaliyokuwa jijini Dar. Nilipofika karibu na makaburi hayo, akaniambia niingie ndani ya eneo la makaburi na kisha kuelekea katika kaburi moja la jamaa mmoja aliyekufa miaka kumi iliyopita, huyo jamaa aliitwa Samweli Ramadhani.



    “Nitalijuaje?”



    “Utalijua tu, una uwezo mkubwa wa kulijua kaburi hilo, wewe nenda,” aliniambia mganga.



    Wakati nimeingia ndani ya eneo la kaburi hilo, kwa macho yangu niliweza kuwaona wachawi, walikuwa zaidi ya ishirini, walisimama pembeni ya kaburi moja la mtoto ambapo maiti yake ilikuwa ikihitajika sana.



    Sikujua kwa nini, sikufika pale kuwafuatilia achawi wale niliowaona ila wao hawakuniona, nilifika pale nikiwa na mambo yangu, hivyo sikujali. Nilitembea kwa tahadhari, makaburini kulitisha sana, kulisisimua kupita maelezo.



    Nilipofika katika kaburi moja, nikasimama, sikujua kama lilikuwa lenyewe au jingine, nikasogelea kuangalia jina, nikakuta limeandikwa Samweli Ramadhani, nikashangaa, nimejuaje kama hilo kaburi ndilo lenyewe.



    “Ila kwa nini maiti hii?” nilijiuliza, ghafla nikasikia mganga akinijibu.



    “Kwa imani zetu wanadamu, tunasema jina la Samweli ni la Kikristo na Ramadhani ni la Kiislamu, hivyo ukifanya mapenzi na maiti hii, Wakristo na Waislamu wote watakuheshimu, na utajiri wako utamsisimua kila mtu,” nilimsikia vema mganga huyo.



    Nilisimama huku nikiwa sijui nini cha kufanya, nilisubiri maelekezo, nikaisikia sauti ya mganga ikiniambia nisubiri, nikafanya hivyo, ghafla, katika hali ambayo sikuitarajia, nikaona hirizi kubwa ikiwa imefungwa kiunoni mwangu, ilikuwa nzito, kilichonishangaza, hirizi ile kama ilikuwa na moyo, kwani niliweza kuyasikia mapigo kama ya moyo yakidunda kutoka katika hirizi hiyo.



    Mara ghafla, upepo mkali ukaanza kuvuma mahali hapo, matawi ya miti iliyokuwa makaburini hapo yakaanza kuyumbishwa huku na kule. Nikasikia kelele za watu wengi, sikujua zilitoka wapi lakini nilizisikia masikioni mwangu.



    Nikaanza kutetemeka, mara nikahisi kama kuna mtu alikuwa nyuma yangu, sikugeuka kuona alikuwa nani, mtu huyo akanisogelea, na kunishika bega kwa nyuma, pumzi zake nilisikia vema karibu kabisa na masikio yangu . Nikashindwa kuvumilia, nikageuka nyuma, cha kushangaza sikuona mtu.



    Wakati nikiendelea kutetemeka kaburini pale, ghafla nikaliona lile kaburi likianza kujifukua lenyewe na ndani yake kuona jeneza likiwa limefunguliwa na ndani yake hakukuwa na maiti yoyote ile, nikashangaa sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ghafla mwili wangu ukaanza kusisimka sana, nikahisi tena kwamba nyuma yangu kulikuwa na mtu, nilitaka kugeuka, nikashindwa kufanya hivyo, nikahisi nikishikwa bega kwa nyuma, nilitetemeka zaidi, kijasho chembamba kikanitoka mno.



    “Unanukia vizuri mpenzi wangu!” nilisikia sauti hiyo nyuma yangu, nikazidi kutetemeka.



    “Wewe nani?” nilijikuta nikiuliza huku mihemo ya mtu huyo ikisikika vema nyuma yangu.



    Niliuliza swali hilo huku nikitetemeka sana, nilitamani nipotee na kutokea sehemu tofauti na hiyo. Mwili haukuacha kusisimka, kuna kipindi niliyasikia kabisa mapigo yangu ya moyo yalivyokuwa yakidunda kwa nguvu.



    “Mimi ni mpenzi wako uliyemfuata hapa makaburini, una ngozi laini sana, hakika wewe ni mwanamke wa ndoto yangu,” niliendelea kuisikia sauti hiyo.



    Mara mguso wa mtu huyo ukahama kutoka begani mwangu na kuanza kuelekea chini, nilizidi kutetemeka mno, mikono yake ikahamia katika mgongo wangu na kuanza kuushikashika, baadaye akahamia katika kiuno changu, nikabaki nikianza kulegea mwili wangu.



    “Ni kipindi kirefu kimepita, miaka kumi pasipo kumgusa mwanamke yeyote yule, upo tayari mpenzi wangu?” aliniuliza.



    Sikumjibu, nilibaki kimya, wakati nikiwa nimesimama vilevile, ghafla nikaanza kuona mazingira ya mahali pale yakianza kuondoka na mazingira mengine kuingia.



    Mbele yangu kukaonekana kuwa na kitanda kikubwa, ndani ya chumba kikubwa, alichonifanya ni kunisukumia kitandani, niliona kweli nimeangukia kitandani, ila ukweli ni kwamba niliangukia ndani ya kaburi lake, kitanda, lilikuwa jeneza lake, alichokifanya, naye akaja kwa juu yangu mgongoni, nikajigeuza ili nimuone, sikumuona, ila miguso yake, ilionyesha kabisa kwamba alikuwa hapo pamoja nami kwani yeye ndiye alianza kunivua nguo, yaani nalivuliwa nguo na mtu nisiyemuona.



    Nilitakiwa kutulia vilevile, kumbuka kwamba nilifanya mapenzi na maiti kumi na tisa na hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho, hivyo niliona kuwa na sababu zote za kutulia kwani baada ya hapo, nilikuwa na uhakika wa kupata utajiri kama alivyoniambia mganga yule.



    Ndani ya kaburi lile ndipo tulipoanza kufanya mapenzi, maiti ile ilikuwa ikinuka sana, sikuwa nikiiona ila niliihisi miguso yake kila kona katika mwili wangu.



    Nilifanya naye mapenzi kwa saa moja ndipo akamaliza, nikahisi akiondoka mahali hapo na kuisikia sauti ya mganga ikinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya, sasa ningekuwa tajiri mkubwa.



    “Umefanikiwa, sasa utakuwa tajiri mkubwa tu,” nilisikia sauti ya mganga.



    Nilichokifanya ni kutoka nje ya kaburi na kuvaa nguo zangu. Kilichonishangaza, ghafla nikaanza kuona moshi mzito ukifuka kutoka ndani ya kaburi lile, sikujua nini kiliendelea, moshi ule mzito ukalifunika kaburi lote hata lisionekane, wakati nashangaashangaa tu, ghafla moshi ule ukakatika na kaburi lile kujifukia kama lilivyokuwa mwanzo.



    Sikutaka kubaki mahali hapo, nikatoka na kuelekea nje ya eneo la kaburi lile huku tayari ikiwa ni saa nane usiku. Nilimkuta mganga akiwa amekaa pembeni akinisubiri, aliponiona, kwanza akatoa tabasamu pana, nikamsogelea.



    “Hongera sana, hakika umenifanya nijisikie fahari sana,” aliniambia mganga yule.



    “Kwa hiyo lini nitapata utajiri?”



    “Utaanza kesho, ila nataka ufanye kitu.”

    “Kitu gani?”



    “Biashara yoyote ile…”



    “Mmh!”



    “Ndiyo hivyo! Utakapoanza, amini kwamba ndipo utajiri utakapoanzia..” aliniambia huku akinikazia macho.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilichokiamini ni kwamba mara baada ya kufanikiwa kufanya mapenzi na maiti zile basi ningepata utajiri kwa kukuta begi la fedha liwakiwa sehemu kumbe sivyo.

    Akaniambia kwamba natakiwa kufanya biashara ambayo ndiyo ingekuwa chanzo cha utajiri wangu, sikuwa na jinsi, japo kwa kishingo upande, nikakubaliana naye. Na hivyo kuondoka mahali hapo.



    Siku iliyofuata, nikamwambia Dickson pale Ubungo kwamba nilitaka kufanya biashara na biashara yenyewe ambayo niliichagua ilikuwa ni kuuza magazeti, akanikubalia hivyo kutafuta meza na kuanza kufanya harakati zote za kuhakikisha magazeti yanauzwa mara moja.



    Siku mbili zilizofuata, tayari nilikuwa na meza yangu, niliweka juu magazeti mengi, nikatafuta vitabu vya hadithi na kutulia. Kitu cha ajabu ambacho sikuwahi kukiona ni pale watu walipoanza kumiminika katika meza yangu na kuanza kununua magazeti.



    Nilishangaa, huwa ni vigumu kwa magazeti kumalizika kwa saa moja, lakini huwezi kuamini, magazeti mia moja niliyopewa, yote yaliishia ndani ya saa moja tu. Si mimi nileyeshangaa, hata watu wengine wa pale walishangaa pia.



    Haikuwa kawaida kabisa na sidhani kama iliwahi kutokea. Magazeti yakaisha lakini nikashangaa watu wengine wakija mezani kwangu, waliiona meza ikiwa tupu ila wakawa wananiuliza kuhusu magazeti, yapo au yamekwisha, nilishangaa, meza ilikuwa tupu, sehemu zingine zilikuwa na magazeti, kwa nini hawakwenda huko?



    Huo ulikuwa mwanzo, niliendelea kufanya biashara ya kuuza magazeti, ikaanza kuyabadilisha maisha yangu, nikawa naongezewa magazeti mengi, nikaanza kuyaona maisha yakianza kubadilika, fedha ziliingia, baadaye nikaanzisha biashara nyingine ya kuuza juisi na maji, hiyo ndiyo iliyoniingizia fedha zaidi na hivyo kupanga chumba Manzese Midizini.



    Naweza kusema huo ulikuwa mwanzo tu, ndani ya miezi mitatu tangu nianze kufanya biashara hizo, nikashangaa nikiwa na akiba ya milioni tatu chumbani kwangu. Sikujua nilizipataje, ila nilichokijua ni kwamba kulikuwa na nguvu fulani nyuma yangu, nikafanikiwa zaidi.



    Ulipoingia mwezi wa tano tangu nifanye biashara hizo, nikajikuta nikiwa na milioni tano. Nikashtuka, utajiri ukaanza kuninyemelea pasipo kukumbuka kwamba unapokuwa na utajiri wa kishetani huwa huna furaha, huna amani, ni utajiri unaotesa na kuumiza mno. Huo ndiyo ukaanza kuninyemelea. Mara ya kwanza, sikujali, ila baadaye, nilikuja kujuta kwa nini nilitaka utajiri.



    Kusema ukweli hakukuwa na kipindi nilichokuwa na furaha kama kipindi hicho, sikuamini kilichokuwa kikiendelea, masikini mimi, ambaye niliishi katika maisha ya umasikini mkubwa mkoani Morogoro, eti leo hii na mimi nilikuwa na mamilioni ndani ya chumba changu.



    Maisha yalibadilika kabisa, nilifanya biashara kwa kujituma kiasi kwamba hakukuwa na mtu aliyehisi kwamba fedha zangu zilikuwa za kishirikina, nilitaka niwe tajiri mkubwa, mwenye biashara nyingi, niingize hata milioni mia moja kwa mwezi.



    Nilijitahidi kufungua biashara mbalimbali tena zilizoniingizia fedha. Fedha zilimiminika, hakukuwa na aliyejua kilichokuwa kikiendelea zaidi ya Dickson tu ambaye alikuwa rafiki yangu wa karibu na ndiye aliyenipokea mara baada ya kufika Dar es Salaam.



    Nilifanikiwa sana, nikaanza mipango ya kujenga nyumba yangu kubwa maeneo ya Goba huku nikinunua gari yangu nzuri kwa ajili ya kutembelea. Ndiyo hivyo, maisha yalibadilika na nilikuwa na kila sababu ya kutumbua pesa nilivyotaka.



    Nakwambia kuhusu maisha yangu, nakwambia kwamba inawezekana kupata utajiri wa kishirikina lakini kamwe utajiri huo mwisho wake huwa mbaya mno. Niliwahi kuzungumza na watu wengi, najua nchi yetu imejaa masikini lakini kamwe usithubutu kupata utajiri kwa njia za kishirikina kwani huwa na gharama yake, shetani hatoi kitu pasipo kukuumiza, hatoi kitu pasipo kukupa masharti ambayo anajua kwamba utashindwa tu.



    Wengi waliniona kama mwanamke anayejua kufanya biashara sana pasipo kujua kwamba nyuma ya maisha yale kulikuwa na nguvu kubwa ya kishetani. Kumbuka kwamba familia yangu ilikuwa masikini sana, wazazi wangu walihangaika kwenda shambani kila siku asubuhi, hivyo nilikuwa na kila sababu ya kuwasaidia.



    Nilichokifanya baada ya siku kadhaa ni kurudi kijijini kwetu, sikupanda basi, nilitumia gari yangu binafsi, Harrier nyeusi, mpya kabisa. Sikutaka kwenda kijijini moja kwa moja, nilitaka kupitia Ifakara kuonana na Mudi, yule mwanaume, utingo aliyenisaidia kiasi cha fedha kilichonifikisha Dar es Salaam, unamkumbuka?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipofika Ifakara, nikaelekea mpaka katika kituo cha daladala. Wanaume wote wakabaki wakiniangalia kwa matamanio, nilikuwa mrembo mno, niliyenukia fedha kila nilipopita, walinitamani lakini kwa kuniangalia tu, hawakuona kama nilistahili kuwa nao.



    “Unamuulizia Mudi anayeishi Mazobezobe?” aliniuliza mwanaume mmoja.



     “Ndiyo! Yupo wapi?”



    “Ametoka, ila msubiri, atarudi muda si mrefu, amekwenda Zilimpompa,” aliniambia kijana huyo, Zilimpompa ulikuwa mmoja wa mitaa hapo Ifakara.



    Sikuwa na jinsi, sikutaka kuondoka mahali hapo, nakumbuka niliwahi kumwambia Mudi kwamba nilikuwa nikielekea Dar kutafuta utajiri na kuna siku ningekuwa tajiri, hakuwa akiamini, alinisaidia lakini najua aliona kwamba nakwenda Dar kupoteza muda, kujiuza na kufanya mambo mengine.



    Leo hii nilirudi tena kwake, sikuwa Zakia yule masikini, nilikuwa Zakia mwenye pesa, niliyeendesha gari, niliyejipulizia manukato ya The Princess ambayo yalikuwa ni zaidi ya shilingi laki tano, nilikuwa na gari la kifahari, yaani kila nilichokuwa nacho, kilionyesha kwamba nilikuwa na pesa.



    Baada ya saa moja, huku nikiwa garini nimesinzia, mara nikasikia kioo cha gari langu kikigongwa, nilipoyafumbua macho yangu na kumwangalia mgongaji, alikuwa Mudi. Uso wake ulikuwa kwenye mshangao mkubwa, kwanza hakunijua mimi nilikuwa nani, nikakishusha kioo.



    “Mudi, mambo vipi?” nilimsalimia huku nikimuonyeshea tabasamu pana.



    “Poa,” alinijibu huku uso wake ukiwa kwenye maswali mengi.



    “Unanikumbuka?”



    “Hapana! Wewe unanijua?” alinijibu na kunitupia swali.



    “Jamani mpenzi! Kweli hunikumbuki?” nilimuuliza huku nikimfungulia mlango na kumtaka aingie.



    Akaingia, alionekana kujishtukia sana, alikuwa mchafu, mavazi yake yalichakaa sana. Humo, bado alikuwa na maswali mengi, mimi nilikuwa nani na kwa nini nilimuita ndani ya gari? Hapo ndipo nikamuweka wazi kwamba mimi nilikuwa Zakia, mwanamke yule wa miezi kadhaa iliyopita ambaye nilikuwa na safari ya kwenda Dar.



    “Zakia! Ni wewe?” aliniuliza huku akinishangaa.



    “Ndiyo! Nimeona nije kukusalimia,” nilimwambia.



    “Imekuwaje tena?”



    “Nini jamani?”

    “Kuwa hivyo!”



    “Hahaha! Nilikwambia nakwenda Dar kutafuta utajiri, si unaona nimeupata,” nilimwambia huku nikitoa tabasamu.



    Alibaki akinishangaa, sikutaka kujali sana, nilimwambia kwamba siku hiyo nilikuwa mgeni wake, nilitaka kulala naye, kumbuka alinisaidia nauli, elfu hamsini, nilitaka nimlipe, siyo fedha bali kumpa mapenzi motomoto ambayo asingeweza kuyasahau maisha yake yote.



    Tukaondoka na kuelekea katika hoteli moja iliyokuwepo hapo Ifakara, nikachukua chumba na kuingia chumbani, tulipofika, akakaa kitandani, akavua nguo, akaenda bafuni, ila aliporudi, nikashangaa sana, hakuwa yule Mudi ninayemfahamu, alibadilika na kuwa moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi, maiti iliyojaa damu ambayo nguo zake tu zilionyesha kwamba alipata ajali. Nikashtuka sana!



    “Kuna nini mpenzi?” aliniuliza swali hilo, hapohapo nikamuona akibadilika na kuwa Mudi.



    Kiukweli nilichanganyikiwa sana, nilitetemeka mwili mzima na kuuhisi mwili wangu kama umepigwa shoto fulani ya umeme. Mudi akanisogelea, akanitupa kitandani na kutulia juu yangu. Nilibaki nikimwangalia kwa macho yenye kurembua, tayari nilianza kuingia katika ulimwengu mwingine wa mahaba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unanukia vizuri mpenzi wangu…” aliniambia, ghafla nikashtuka.



    Maneno kama hayo niliambiwa na maiti ile ya kule makaburini kipindi alichotaka kufanya mapenzi na mimi. Maneno yaleyale ndiyo aliyoyazungumza Mudi, karibu kabisa na masikio yangu.



    “Nashukuru!” nilijibu huku nikiachia tabasamu pana lenye hofu.



    “Umetafuta sana utajiri, hakika utakuwa zaidi ya hapa, ninachokitaka ni wewe kuwa mpenzi wangu milele,” alisema Mudi.



    Kiukweli alinichanganya sana, hapohapo nikamuona akitoka katika sura ya Mudi na kurudi katika sura ya moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi mochwari, hakika ilinitisha sana. Nikataka nijitoe pale kitandani, akanikandamiza zaidi. Nikahisi kifua kikianza kubana na pumzi kuanza kukata.



    Bado macho yangu yalikuwa yakiiona maiti juu yangu, ilikuwa imenikandamiza vilivyo pale nilipolala, sikumuona Mudi kabisa, nilijitahidi kujitoa kutoka hapo kitandani lakini nilishindwa kabisa.



    Nilianza kuhema juujuu, kuna wakati nilihisi kama ningekufa kwani nilibanwa sana kiasi kwamba nguvu zikaanza kuniisha mwilini mwangu. Wakati sura ile ikiendelea kuwa ya hiyo maiti, ghafla ikabadilika na kuwa sura ya Mudi, nilishangaa, hata kule kubanwa kote kukatoka.



    “Kuna nini?” aliniuliza Mudi huku akiniangalia usoni.



    “Hakuna kitu,” nilijibu huku nikionekana kuwa na hofu kubwa usoni mwangu.



    “Hapana! Kutakuwa na tatizo, kuna nini?” aliniuliza Mudi huku akiwa amenikazia macho.



    Ni kweli kulikuwa na tatizo lakini sikutaka kumwambia, najua hakuwa akifahamu lolote lile, niliiona maiti lakini kama ningemwambia kuwa nimeiona maiti badala ya kumuona yeye, angeniikiriaje?

    Nilijaribu kumwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile hivyo angeendelea kama kawaida yake. Tulifanya mapenzi siku hiyo, sikutaka kuondoka, nililala na Mudi hotelini hapo huku usiku mzima nikiota ndoto za ajabu sana, mara nakimbizwa makaburini na watu waliovalia mashuka meupe, mara nakuchukuliwa na kupelekwa mochwari kisha kuingizwa katika masanduku ya kuhifadhia maiti.



    Mpaka tunaamka asubuhi, niliota ndoto mbili, zote zilikuwa za kutisha mo, sikujua kwa nini ilikuwa hivyo, nilitamani nipate majibu juu ya ndoto zile kwamba kwa nini kipindi cha nyuma sikuwa naota ndoto mbaya ila kipindi hicho zilikuwa zikija kwa sana?



    Sikutaka kujali japokuwa moyo wangu ulikuwa na hofu kubwa. Asubuhi hiyo tukanywa chai na kumwambia Mudi kwamba ningeondoka kuelekea katika kijiji chetu cha Mbingu.



    “Ni lazima niondoke mpenzi,” nilimwambia kwa sauti ndogo, ilikuwa kama saa nne asubuhi.



    “Sawa! Ila ningependa niendelee kuwa nawe, ila haina jinsi, kwenda kuwaona wazazi ni jambo la msingi sana,” aliniambia kwa unyonge ambao ulinionyesha kwamba hata yeye hakupenda kabisa kuniona nikiondoka.



    Hakukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima niondoke kuendelea na safari yangu. Tulipoagana na kwenda ndani ya gari langu, nikatulia, nikauegemea usukani na kuanza kufikiria kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.



    “Tatizo nini tena?’ nilijiuliza lakini sikupata jibu.



    Sikutaka kubaki mahali hapo, nikaondoka zangu na kuendelea na safari yangu. Njiani, sikuwa na furaha hata kidogo, wakati nikiwa nimebakiza kilometa kumi kabla ya kufika kijijini, nikashangaa kuona gari likipunguza mwendo na kisha kusimama pembezoni mwa barabara.



    Nilishangaa, gari hilo halikuwa bovu, kulikuwa na mafuta ya kutosha, sasa kwa nini lilipunguza mwendo na kisha kujizima, nilibaki nikijiuliza sana lakini hata kabla sijapata jibu, niliisikia sauti ya mtu ikiniambia niangalie nyuma kwani kulikuwa na kitu.



    Harakahara nikayapeleka macho yangu katika siti za nyuma, nilichokiona ni boksi kidogo likiwa limefungwa vizuri kabisa. Kwanza nikashtuka, sikujua ni nani aliliweka boksi hilo na ndani kulikuwa na nini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliamini hakukuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kufungua mlango wa gari langu na kisha kuingia ndani kwani ufunguo nilikuwa nao, sasa nani alidiriki kuufungua mlango na kuliweka boksi hilo? Nikakosa jibu.



    Nikatoka hapo mbele na kuelekea nyuma, boksi lile liliandikwa jina langu kwa juu, nilikuwa na hofu kubwa lakini nilitakiwa kufungua, ilikuwa ni lazima nijue ndani kulikuwa na nini kwa nini lilikuwa ndani ya gari langu.



    Wakati nimelichukua boksi hilo, cha kushangaza kabisa mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu mno, kijasho chembamba kikaanza kunitiririka, sikujua sababu ya kuwa kwenye hali hiyo, kumbuka hapo ilikuwa porini, nilizungukwa na miti kila kona, sikuogopa kuwa hapo, ila hilo boksi ndilo lililonitia hofu.



    Nikafungua na kuangalia ndani. Kitu nilichokutana nacho, kilinishtua sana, kulikuwa na kisu kilichofungwa kitambaa chekundu katika mpini wake, nikajiuliza sababu ya kisu hicho kuwa humu garini ilikuwa nini?



    “Umekiona hicho kisu?” niliisikia sauti ya mganga, niliangalia huku na kule, sikuona mtu, nikashangaa.



    “Ndiyo mkuu!”



    “Unatakiwa kutoa sadaka moja kila baada ya miezi miwili,” nilimsikia akiniambia.



    “Sadaka?”



    “Ndiyo! Bado tuna kazi kubwa na wewe, ni lazima ufanye tunachokuagiza ili utajirike zaidi,” aliniambia.



    “Tuna?”



    “Ndiyo! Sipo peke yangu, mimi na watu wa giza,” aliniambia.



    “Watu wa giza?”

    “Ndiyo!”

    “Wakina nani?”

    “Waliokupa utajiri,” alinijibu.



    Hakika nilishangaa sana, maneno aliyoniambia kama sikuwa nikiyaelewa, ilikuwaje aseme kwamba yeye alishirikiana na watu wengine katika kunipa utajiri na wakati nilichokijua ni kwamba yeye peke yake ndiye aliyenipa utajiri huo?



    Nilishangaa sana lakini bado sikuridhika, nilitaka kujua zaidi kuhusu hizo sadaka alizosema kwamba nilitakiwa kuzitoa, zilikuwa sadaka za nini? Fedha au?



    “Ni lazima uue?” nilisikia sauti hiyo ikinipa majibu.



    “Niue?”



    “Ndiyo! Utajiri uliokuwa nao ni utajiri wa damu, huwezi kuwa nao milele mpaka utakapotoa damu, ni lazima uue kila baada ya miezi miwili, hakika utajiri utaongezeka na kuwa mwanamke tajiri kuliko wote nchini Tanzania,” aliniambia.



    “Mimi niue?”

    “Ndiyo! Hakika hautomfuata mtu na kumuua, angalia tena kwenye boksi,” iliniambia sauti hiyo, harakaharaka nikaangalia kwenye boksi, macho yangu yakakutana na kioo.



    “Unakiona hicho kioo? Kichukue, kiangalie, unaona nini?” iliniuliza, nikakichukua na kuanza kukiangalia, sikuiona taswira yangu, taswira ambayo niliiona ilikuwa ni ya baba yangu.



    “Ichome taswira hiyo kwa hicho kisu,” iliniambia.



    “Unasemaje?” niliuliza huku jasho likinitiririka, hakika niliogopa kwani nilijua kwamba endapo ningeichoma taswira ile, basi baba yangu angekufa.



    “Ichome…” sauti ya mganga iliniambia, nikabaki nikitetemeka.



    Nilibaki nikitetemeka, sikujua ni kitu gani nilitakiwa nikifanye mahali hapo. Jinsi mganga yule alivyoniambia kwamba niichome taswira ya picha ya baba yangu katika kioo kile.



    Kumuua baba yangu! Kilikuwa kitu kisichowezekana kabisa, nilikumbuka namna alivyokuwa akiyasumbukia maisha yangu kipindi cha nyuma, nilikumbuka jinsi alivyokuwa akijinyima kwa ajili yangu, yaani nipate maisha mazuri, hakujali kama alikuwa akila au la, alichokijali ni mimi kula na kulala sehemu nzuri.



    Nilifanikiwa, nilitaka nimuonyeshee baba kwamba hatimaye ule umasikini uliokuwa umetutafuna kwa kipindi kirefu usingekuwepo tena, nilitaka niwaonyeshee wanakijiji kwamba kitendo changu cha kuondoka nyumbani kwetu na kwenda kijijini kilikuwa sahihi kwani kile nilichokitaka, tayari nilikipata.



    Nilibaki nikiiangalia taswira ile, mawazo yote hayo yalinijia kichwani mwangu wakati ambao nilishika kisu kile. Mapigo ya moyo yalikuwa juu mpaka kuhisi kwamba kama angepita mtu yeyote mahali hapo basi angeyasikia kwa jinsi yalivyokuwa yakidunda.



    “Zakia, ichome taswira hiyo,” niliisikia sauti ya mganga huyo.



    “Siwezi…ninashinwa,” nilisema pasipo kuogopa kitu chochote kile.



    “Kwa nini unashindwa?” aliniuliza.



    “Nilitafuta utajiri kwa ajili ya wazazi wangu, sasa kwa nini nimuue na wakati kila kitu nilichokuwa nacho naye alitakiwa kukiona?” niliuliza swali nililoliona kuwa na hoja, ila kwa mganga huyo, halikuwa na hoja yoyote ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi acha tuuchukue utajiri wetu, utarudi na kuwa masikini, tena masikini mkubwa zaidi ya ulivyokuwa,” aliniambia mganga yule.



    Nilichanganyikiwa, sikutaka kuuachia utajiri ule kwani tayari nilishaonja utamu wake, nilitaka kuwa nao milele, yaani hata maisha baada ya kifo kama kungekuwa na matumizi ya fedha basi nitakapokufa niende nao kwani ulikuwa mtamu mno.



    Kitendo cha kuniambia mamneno hayo, nikashindwa kuvumilia, sikuwa tayari kuona utajiri huo ukiondoka mikononi mwangu, ilikuwa ni lazima nimuue baba yangu.



    Kwanza nikafikiria kwamba alikuwa mzee, hakuwa na nguvu za kutosha, kama ningemuacha basi mwaka huohuo hapo baadaye ilikuwa ni lazima afariki kwani umri ulikuwa umekwenda sana.



    Kitendo cha kufikiria hayo, nikashangaa kupata majibu kwamba ilikuwa ni lazima nimuue, kama nisingemuua mimi basi angekufa miezi michache ijayo. Sikutaka kujiuliza tena, mawazo hayo yakanipa nguvu na hivyo kuchoma taswira ile. Nilipomaliza, mganga akaniambia niwashe gari, nikawasha na kuanza kuondoka mahali hapo.



    Nilichukua saa mbili, nikafika katika Kijiji cha Mbingu. Kwanza wanakijiji walipoliona gari hilo, wakashangaa sana, hakukuwa na gari lolote la kifahari lililowahi kufika kijijini hapo, magari yote ambayo yaliwahi kufika yalikuwa yale ya mizigo ambayo yalifuata nafaka hapo kijijini, sasa watu wakawa wanajiuliza, je, huyo aliyeingia na gari la kifahari alikuwa nani?



    Sikutaka kuteremka, unapofika kijijini kwetu, kwa jinsi ilivyokuwa ilikuwa vigumu sana kufika na gari mpaka karibu na nyumba yetu, ilikuwa ni lazima ufikie mbali, uteremke na kuanza kutembea kuelekea huko.



    Watoto na watu wengine walishasogea mahali gari lilipokuwa na kuanza kuliangalia. Hawakujua ndani ya gari hilo kulikuwa na nani kwani vioo vya gari hilo vilikuwa ‘tinted’.



    Najua walikuwa na maswali, nilichokifanya baada ya kukaa ndani ya gari kwa dakika kama tano, nikateremka, wengi waliponiona, hawakunifahamu, kwa jinsi nilivyovaa, miwani yangu na nguo za thamani, hakukuwa hata na mtu mmoja aliyehisi kwamba mwanamke huyo aliyekuwa akitembea nilikuwa mimi.



    “Huyu ni Mzungu?” nilimsikia mtoto mmoja akiuliza, watoto wengine walikuwa wakinifuata kwa nyuma.



    Nilitembea mpaka nilipofika karibu na nyumba yetu, kilichonishtua ambacho sikuwa nikikumbuka ni msiba uliokuwapo. Watu zaidi ya hamsini walikuwa mahali hapo, nilisikia vilio kutoka kwa watu kadhaa waliokusanyika nyumbani kwetu, nilishangaa lakini baada ya kukumbuka kwamba niliichoma taswira ya baba katika kioo kile nilichopewa ndani ya gari, moyo wangu ukaumia sana kwani niligundua kwamba mimi ndiye niliyemuua baba yangu.



    “Baba amekufa! Nimemuua baba!” nilijisemea moyoni na kuanza kuelekea kule walipokusanyika watu wengi.



    Wanaume wengi ndiyo waliokuwa wamekusanyika mbele ya nyumba yetu, kama walivyokuwa watu wengine kule nilipoaki gari, hata hapo hakukuwa na yeyote aliyegundua kwamba msichana aliyefika, ambaye alivalia kisasa alikuwa yule Zakia aliyeondoka mwaka mmoja uliopita.



    Nilisalimia, wakabaki wakinishangaa, nikaingia ndani, nikaelekea mpaka chumbani ambapo nilikuta ndugu zangu kadhaa wakiwa na mama yangu. Hakukuwa na mtu aliyenigundua zaidi ya mama ambaye baada ya kuniona tu, kilio kikaongezeka, kila mtu akabaki akijiuliza mimi ni nani.



    Moyo wangu uliumia mno, sikuamini nilichokuwa nikikona, sikuwahi kumuona mama yangu akilia kama siku hiyo, nilijuta, mimi ndiye niliyemuua baba kwa sababu ya tamaa za kubaki na utajiri niliokuwa nao.



    Nikaungana nami, nikajitambulisha kwamba nilikuwa nani, watu wote wakashangaa. Kitu cha ajabu kabisa kutokea, moyo wangu haukuwa na maumivu makubwa sana, nilisikitika kwa kuwa baba alifariki lakini kusema kwamba nilie sana kama watu wengine, kwangu haikutokea kabisa.



    Watu walinishangaa, walijiuliza sana kuhusu mimi, nilionekana kabisa kwamba nilikuwa na fedha, nilikuwa na utajiri mkubwa, sikutoka ndani, nilibaki nikiwafariji wengine, harakati zote zikaendelea siku hiyo, saa kumi jioni, tukaenda kuzika katika makaburi ya kijiji na kisha kurudi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila niliyemwangalia, alionekana kuwa na hamu ya kufahamu, utajiri mkubwa namna hiyo niliutoa wapi? Kwani hata gari nililokuwa nalo, lilikuwa gumzo sana kijiji kizima na hata vijiji vya jirani . Eti yule Zakia aliyekataliwa kuolewa na wanaume kibao, leo alikuwa tajiri! Haikuwaingia akilini.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog