Search This Blog

SEWATO (KOSA LA DAMU) - 3

 







    Simulizi : Sowato (Kosa La Damu)

    Sehemu Ya Tatu (3)



    july aliishiwa nguvu kabisa,na kudondokea kwenye kile kichaka puu,prof aliamrisha bastola yake iteme risasi kwa kuvuta trigger,paa paa paa,risasi tatu zilisikika huku zikifuatiwa na kilio cha maumivu makali,mamaaaaaa...Songa nayo sasa..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wote walishituka baada ya kusika kilio cha mtu,mwanachuo mmoja akaropoka"prof umeua mtu jamani",no hayakuwa makusudi yangu mi nilihisi ni hatari ipo mbele yetu,hatakuwa nani lakini guyz,ebu tuone.

    Walipokagua kwenye kichaka hicho hawakuamini macho yao,ooh my God huyu si july huyu,ndio yeye.

    Wote walichoka akili baada ya kumuona mwenzao teyali kaisha haga dunia,walilia kwa uchungu huku wakimtupia lawama prof henry kwa kuamua kufanya kitendo cha ghafla namna hile,prof akuamini macho yake kama ni kweli ni yeye aliyemuua july.

    Lakini yule guider alishituka baada ya kumkagua vizuri angel maeneo ya mgongoni alikuwa ana damu iliyokuwa imeishaganda,alipomkagua vizuri aligundua kwamba july alikuwa na jeraha kubwa sana mgongoni.

    Jamani ebu naomba muangalie vizuri hapa iko inaonekana kama alipataga na mashida(aliiongea kwa lafudhi ya kikongo),ndipo wakajua kwamba wenzao walikuwa wamepata matatizo.

    Kweli prof,alidakia madam shani,mh! hili sasa lishakuwa jambo kubwa,kwa hali hii itabidi tuchukue hii maiti na kurudi kwanza hotelini si mnaona muda unazidi kupotea,aliongea prof henry kwa majonzi.akachagua wavulana wanne waichukue maiti ya july na kuipeleka pahali pa usalama,kisha prof akamuambia yule guider awasiliane na askari pori waje kuwasaidia kumtafuta jofu,yule guider alijaribu kupiga simu lakini hakukuwa na mtandao,alipojisachi kutafuta redio call yake aligundua hatakuwa kaidondosha kwani pahali halipokuwa kaiweka haikuwepo,ikabidi hatumie simu yake ya mkononi lakini hakishika mtandao ikabidi kutafuta mtandao alisogea kwa pembeni huku hakiwa kainyanyua simu yake juu alifanikiwa kunasa mtandao,aliongea na askari wa pori na kuwapa taarifa ya kupotea mmoja wa wanachuo na mwengine kukutwa amefariki.ok nyie mpo upande upi wa msitu kwa sasa,sisi iko tunakwendaga kwa hoteli saa hii hi na tupo,mara mtandao ukapotea,hawakuelewana,akaamua kurudi kwa wenzake,alipogeuka nyuma alijikuta hakipiga yowe lililowashitua wenzake,alikutana na yule kiumbe uso kwa uso.alijaribu kukimbia lakini alikuwa kachelewa kwani teyali yule kiumbe alikuwa kaishamuwahi na kumvunja shingo kwa kumgongesha kwenye mti.

    ****************

    Wakiwa wanajiandaa sasa kuibeba maiti na kurudi hotelini,walishitushwa na kelele za yule guider.walitimua mbio kuwahi waone kuna nini,wakati wengine wameelekea walibaki marafiki zake july wawili anety na neema,wakiendelea kulia kwa uchungu kwa kuondokewa na rafiki yao kipenzi,ambaye walikuwa naye masaa machache tu nyuma.neema aliichukua ule mkufu shingoni mwa july,ili iwe kumbukumbu yake bila kujua ule mkufu ndio ile kufuli la kumfungia kiumbe huyo ambaye bado hawajamjua kama hanawamaliza,kundi la watu 25 wamekwisha uwawa watu wanne.



    Wale waliokimbia kumsaaidia yule guider walifika na kukuta maiti yake ikiwa imevunjwa shingo,wote sasa waliingia na wasiwasi mkubwa.mh!? kutakuwa na mnyama au mtu humu msituni hanauwa watu si buree aliongea prof henry,itabidi tuwatafute wenzetu haraka na kurudi hotelini hii ishakuwa too much,wakati prof anaongea mara wanasikia kelele zikitokea kule walipokuwa mwanzo,ikabidi warudi safari hii walikimbia sana huku Henry akikoki bastola yake.kile kiumbe kiliwavamia neema na anety pale walipokuwa wanamlilia mwenzao kilimpiga kwa makucha yake neema kofi liliomrusha mbali kidogo kisha likamfata anety,anety alikiomba kiumbe kile kimwache lakini kilikuwa na roho ya ukatili ajabu,kikamtoboa tumbo na kumtoa maini huku neema anashuhudia hakiwa yupo chini analia kwa maumivu,kilimtoa maini anety na kumuwacha akigombania roho,kisha kikayatafuna yale maini na kumfuata neema pale chini



    ***************

    Upande wa pili katika lile kundi la tatu wao hawakujua nini kinaendelea,walitembea huku wakiendelea kuwaita july na jofu,walipoona hawaonekani wakaamua kurudi hotelini kama walivyokuwa wamekubaliana,ilikuwaishatimia mishale ya saa kumi na mbili jioni,wakiwa porini humo kurejea hotelini baada ya kuwakosa wenzao,wanatumia muda huo kutalii kidogo msituni humo,kundi hili liliongozwa na raisi wa wanachuo ambaye pia alikuwa miongoni mwa listi ya waliokuja kufanya research/utafiti msituni humo,aliitwa hassan,mmoja wao alibaki nyuma kidogo aking'ang'ana kutafuta mtandao ili aperuzi mtandaoni lakini hakuunasa,alijikuta amebaki mwenyewe..........

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hawa nao wanajifanya wanawahi sijui hata wamepita njia gani,alijiongelesha mwenyewe huku akiwa hajui apite wapi sababu ya msitu huo kushonana sana na vichaka pamoja na miti mikubwa,ikabidi aanze kuwaita wenzake,aliwaita sana lakini hakuna aliyeitika.



    Wenzake walikuwa tayali wanakaribia kufika kambini,kenedy ambaye ni kaka yake na latifa(aliyeachwa nyuma)aliangaza angaza kwa kumuangalia kila mtu lakini hakumuona latifa,hichi kitoto kitakuwa wapi,(alijiuuliza) ikabidi hawaulize wenzake,jamani hivi latifa yupo wapi ,we si halikuwa nyuma yangu hanachezea simu labda tumemuwa.........,kabla hajamaliza kuongea mara hakatokea mwenzao ambaye alikuwa kwenye kundi la pili(la wakina fide)alikuwa anakuja anakimbia yupo hoi,jamani hapa si salama,kuna nini wewe,hapana tuondoke hanakuja,nani anayekuja yu yu yule,NANI BWANA,muuaji,muuuwaji walishituka wote kwa pamoja.hacha masihara yako na prof moses yupo wapi si mlikuwa naye kundi moja alihoji Hassan,sijui hata cha msingi tuondokeni humu msituni si salama



    ********************

    Upande wa pili yule kiumbe wa ajabu alimfata neema pale chini na kumkaba koo,na kumyanyua juu kwa mkono mmoja,neema alikuwa kaishika ile cheni,alipokuwa aking'ang'ana kujisaidia ile cheni(mkufu) ilimgusa yule kiumbe na kutoa ile mionzi mikali, kilimwachia neema na kuanza kupiga kelele za kutisha na kufanya ndege wakimbie mitini,wakati huo huo prof henry na kundi lake nao wanafika walimshuudia yule kiumbe live kabisa,henry alichukua bastora yake na kuhikoki,kisha akafyatua risasi kama mvua,zile risasi hazikufanya kitu kwani kila zinapoingia mwilini mwake zinatoka nje na jeraha linapona kwa sekunde,bastora yake ikaishiwa risasi,kwa bahati mbaya ule mkufu ulimtoka neema mkononi na kudondoka chini baada ya kuwa ameachiwa na yule kiumbe,ile miyonzi ikazimika kikapata nafuu,kilimshika neema na kupotea naye huku wanashudia,kwa kitendo kile kila mtu alikimbia kivyake,angel alikimbia huku kashikwa mkono na baraka,prof halishindwa kuwazuia wasikimbie kwani teyali walikuwa wameishaiingia na hofu kubwa,kila mtu alitimua mbio huku wakipiga kelele,alibaki prof mwenyewe,hakaamua na yeye sasa kukimbia kuokoa nafsi yake,lakini kabla hajaondoka aliuona hule mkufu,nafsi ikawa inamwambia auchukue,lakini wazo jingine linamwambia auwache isije ikawa ni mkufu wa kimajini kama inavyosemwaga mitaani,lakini hakuipa imani wazo ile kwakuwa yeye ni msomi akauchukua na kuweka kwenye mfuko wake wa shati aliyovaa nakuondoka huku akioongeza risasi kwenye bastora yake.

    ************************

    Wakati bado hawajahamini kwamba ndani ya msitu huo kuna muuaji ghafla wakasikia ile milio ya risasi kwa mbali kidogo hikisikika na zile kelele,ndipo wakaingiwa na wasiwasi,kenedy alipatwa na hofu juu ya usalama wa ndugu yake.ikabidi amurudie dada yake,

    we kenedy unaenda wapi pekee yako ni hatari huko,lakini hakutaka kusikia jambo lolote ikabidi wale warudi kambini haraka,

    Kenedy alimwita latifa kwa sauti,lakini hakujibiwa akazidi kuingia ndani zaidi ya msitu,mara hakakutana tena na wenzake wawili wanakimbia,no kenedy huko si salama usiende,hapana lazima ni mpate mdogo wangu siwezi kurudi mwenyewe bila yeye,akaongozana nao kumtafuta kwa bahati nzuri latifa aliwasikia wanamuita,akaitika kwa kuwaita,wakafanikiwa kumuona lakini wakati wanakimbiliana yule kiumbe alitokea katikati yao huku ametapakaa damu mwili mzima,kilimkamata rameck na kumyofoa moyo na kuutafuna,kikawageukia na wale wengine walitimua mbio huku wakimvuta latifa ambaye alikuwa kagoma kuondoka hakimlilia kaka yake huyo ambaye hawakuzaliwa naye tumbo moja,yeye alilelewa na baba yake na latifa tangu mdogo alipookotwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************

    walifanikiwa kufika kambini lakini hawakumkuta mtu,walishangaa wakabaki wanajiuliza wapi prof henry na wenzao wengine walipo hawakupata majibu.

    Mita chache kutoka hapo kambini angel pamoja na baraka walikuwa wanakimbia kuelekea kule kambini,mara kile kiumbe kikatokea mbele yao na kumkabaa kooni angel,baraka alipoona angel amekabwa aliangaza angaza pembeni na kuona kipande cha mti halikiokota na kumchoma nacho yule kiumbe kifuani kwa nguvu,kilimuingia na kumtoboa yule kiumbe, kikatokeza upande wa pili,kilimpiga kofi baraka na kumrusha mbali halidondokea kichwa na kuvunja shingo akapoteza maisha hapo hapo kile kiumbe kikamwachia angel,na kuanza kuangahika kukichomoa kile kipande cha mti huku angel hakiwa hanakohoa pale chini,kwa bahati nzuri prof henry alifika alikiongezea risasi lakini hazikumzuru,kilifanikiwa kukichomoa kile kipande cha mti lakini kilipata maumivu makali na jeraha lilikuwa kubwa halikupona haraka kama mwanzo,kilimrukia prof na kumkaba shingo mara hule mkufu uliwaka mle mfukoni mwa Prof Henry baada ya kuguswa na kiumbe huyo wa ajabu hukatoa ile mionzi na kumuingia yule kiumbe pale kwenye jeraha,kilimwachia Henry na kuanza kupiga kelele zilizozua upepo mkali mithili ya kimbunga,prof alimfata angel ambaye alikuwa anamlilia baraka ambaye tayali alikuwa kaishapoteza uhai na kumnyanyua pale chini kwa kutumia nguvu maana alikuwa ataki kumuacha baraka,lakini prof alimbebeleza wakaondoka huku yule kiumbe hakiwa hanageuka na kuwa moshi mzito mweusi........



    Prof henry alifanya makosa kuondoka eneo lile kwani alivyoondoka tu ile miyonzi ikazima kwa kitendo hicho yule kiumbe aligeuka na kuwa moshi mzito mweusi ulisambaa angani kisha moshi huo ukasogelea maiti ya baraka pale chini,ukamwingilia ndani kwa kupitia pua zake,uliingia wote mara baraka akazinduka kwa kufumbua macho yake, akaanza kubadilika macho yake na kuwa mekundu na yenye mboni kama ya paka,ngozi yake ikawa kama vile imechunwa kwani nyama pekee ndio zilikuwa zinaonekana na baadhi ya mifupa yake kuonekana hasa ya mdomoni alikuwa hakipumua kwa kasi huku moshi mweusi hukiwa hunatoka kwenye pua zake,hakika halibadilika na kuwa kiumbe wa kutisha,alitoa kicheko kikali kisha hakapotea.



    ****************************

    Prof Henry pamoja na angel walifika kambini na kukutana na wenzao,ilikuwa ishakuwa giza ikabidi wapumzike walipo weka kambi ili kuwasubiri wenzao ambao bado hawajafika ili warudi hotelini,angel muda wote alikuwa analia akimwaza baraka, alihisi kuhumia moyoni kwani akuwahi kumwambia kama anampenda ilizidi kumuumiza,akachukua kibegi chake na kuchukua leso ili ajifute machozi,wakati anachukua kitambaa hule mkufu wenye mauzauza aliopewa kama zawadi na wazazi wake hukadondoka aliuokota na kuwakumbuka wazazi wake bila ya kujua kwamba wale si wazazi wake,akaamua kuuvaa ule mkufu ghafla hakahisi kusisimuka mwili mzima,alijishangaa nakuhisi labda hule mkufu ndo unamsababishia hali hiyo ya kusisimuka,ikabidi auvue lakini cha kushangaza haukuwepo shingoni akaziidi kushangaa alipojipapasa hakuweza kuushika shingoni pake,akaamua kupuuzia,labda umepotea,aliwaza

    Wakati huo prof henry naye alikuwa ndani ya ndimbwi zito la mawazo hakujua hatafanya nini,hakujua maprofesa wenzake wawili walipo,prof moses na madam mary,mara hakakumbuka ile mionzi iliyowaka kutoka mfukoni mwake,ikabidi aungalie ule mkufu, wazo likamuijia kwamba hii ndio kinga pekee waliyo nayo kwani alishuudia ile miyonzi ikimwadhibu yule kiumbe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kulipambazuka wakiwa salama kipindi wanalala wote pale kambini waliofika walikuwa jumla kumi na tatu,prof akawahesabu asubui hiyo kuona kama wapo sawa cha kushangaza walikuwa kumi na moja tu,wakaingiwa na wasi wasi juu ya usalama wa wenzao wawili,mara angel hakawa anahisi kusisimuka mwili wake huku hakisikia sauti inamwambia akilini mwake kwamba geuka uangalie nyuma yako,alipogeuka tu alishangaa kuona michirizi ya damu chini,prof ona ona jamani ona hii si damu hii,aliongea kwa wasi wasi huku akiwaonyesha wenzake,waliifuatilia michirizi hiyo hadi nyuma ya hema moja waliifuatilia hadi wakaa wanaiacha kambi mita chache nyuma walishituka baada ya kukuta mauaji ya kutisha,wanachuo wawili walikuwa wamenyofolewa baadhi ya viungo vyao,ghafla ile sauti ikasikika tena kichwani mwa angel ikimwambia waondoke hapo haraka,hakiwa haelewi elewi kama ni sauti ya kweli au ni mawazo yake na ni kwa nini anahisikia yeye mwenyewe,ghafla mmoja wao hanashitukia kafungwa mguu na kamba kama mizizi ya miti na kuvutwa nyuma,walitawanyika tena ovyo na kupoteana msituni baada ya mwenzao kuvutwa



    ********************

    Prof moses alikutana na madam mary hakiwa hoi na kukumbatiana,wako wapi wengine,alihoji mary,sifahamu cha msingi hapa ni kutafuta njia ya kutoka hapa,kwa mbali wanasikia watu wanaongea,kumbe walikuwa karibu na kijiji cha sego,ikabidi waende kuomba msaada,walifanikiwa kufika walipokelewa na wanakijiji hao,wakapelekwa moja kwa moja kwa mfalme ambaye sasa alikuwa kaisha zeeka sana,waliongea lugha tofauti na kiswahili, kwa bahati nzuri madam mary alikuwa ni mtaalamu wa lugha kidogo alielewa baadhi ya maneno, kwa lugha mbovu mbovu aliwaeleza kilichowatokea kule msituni,mfalme alishituka sana kwani alijua lile tatizo halitokuja tokea tena,ikabidi aitishe kikao cha ghafla,wakajadili juu ya suala hilo.

    Mfalme aliwahoji moses na mary huko wapi hule mkufu uliochukuliwa pangoni,mary alikuwa haujui na hata hajawai kuuona,alimwambia mfalme kwamba hawakuchukua mkufu,mfalme alikataa akamwambia kwamba kama hawajauchukua yule kiumbe asinge hamuka,ikabidi sasa mtaalamu wao haitwe aangalie wapi ule mkufu ulipo na ni kweli yule kiumbe amefufuka.



    **********************

    Wakati huo prof alikuwa na angel pamoja na hassan wakikimbia kuelekea hotelini,mara ile sauti ikamwijia angel kichwani tena na kumwambia kwamba huko wanakoenda si salama asiende,akuitilia uzito sauti hiyo na kuipuuza akaendelea kwenda ghafla prof alichomwa na mkuki kwenye paja lake na kudondoka chini,ule mkufu ukadondoka kutoka mfokoni mwake,

    yule kiumbe alikuja huku hakiwa kashika kichwa cha mwanakijiji mmoja anakinyonya macho,prof aliuchomoa ule mkuki na kwa kusaidiwa na angel pamoja na hassan haliuvuruta mguu wake na kuendelea kukimbia bila ya kujua ule mkufu kauacha pale chini.kile kiumbe kiliwafata kwa kasi na kumshika hassan na kumtia kucha za tumbo na kuuvuta utumbo nje,angel alipiga kelele hakiwa hajui hafanye nini,prof henry alijipapasa mfukoni kuutafuta ule mkufu lakini hakuupata,hakajua huo ndio mwisho wake,akamwambia angel aendelee kukimbia amuwache yeye kwani wakiingozana wote watapata matatizo, angel akakimbia na kumwacha prof mwenyew,prof henry alioona bora tu afe kuliko kuendelea kushuudia mauaji ya wanafunzi wake,ntapambana na wewe hadi nikuue,alijihami huku akichukua bastola yake na kuikoki alianza kumshambulia kwa kufyatua risasi mfululizo,lakini ziliingia nakutoka kisha jeraha linapona kwa sekunde.....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kile kiumbe kilizidi kumsogelea prof Henry,risasi ziliisha kwenye bastora yake alijipapasa kwenye mifuko yake kama bado hana risasi,halifanikiwa kuzipata aliziweka kwenye kitako cha bunduki yake na kuikoki lakini alikuwa ameisha chelewa kwani kile kiumbe tayali kilikuwa kisha mfikia karibu yake,kilimrukia pale chini na kumnyonya damu,prof henry alipiga kelele huku hakifyatua risasi ovyo ovyo mfululizo,milio ya risasi hilisikika hadi kwa askari pori waliokuwa wamepigiwa simu na yule guider kabla hajauliwa na kiumbe huyo wa ajabu,waliulizana askari hao tisa,kengele ya hatari ililia vichwani mwao,inspecta mkuta pamoja na kikosi chake waliingiwa na wasi wasi wa wageni walioingia msituni humo baada ya kusikia milio ya risasi ikitokea msituni humo,walifanikiwa kufika kwenye kambi yao waliofika wageni hao (wanachuo)lakini hawakukuta mtu,askari mmoja aliona michirizi ya damu nyuma ya hema moja,alilikwenda kuripoti kwa mkuu wao inspecta mkuta,afande kuna michirizi ya damu upande huu,walikwenda kushuudia, walifata michirizi hiyo ya damu na kuziona zile maiti mbili za wanachuo walio uwawa usiku,walikoki bunduki zao na kugawanyika pande mbili na kuingia ndani zaidi ya msitu kumtafuta muuaji na kujua wapi walipo wengine.

    ***************"**

    Angel alishitushwa na milio hile ya risasi pamoja na makelele ya prof alitamani kurudi lakini ile sauti ilimuambia asiendee, tena safari hii hakihisii kuungua shingoni alikimbia sana hatimaye hakakutana na wenzake watano waliosalia kati ya 25,wakiwa wapohoi wanakimbia huku hawajui wapi pa kuelekea,walipumzika chini kidogo ya mti,kutokana na uchovu walipitiwa na usingizi,lakini angel hakupata usingizi kwani ile sauti ilimwamuru aondoke haraka kile kiumbe kinakuja,halipowambia wenzake waling'ang'ana wapumzike kidogo kwanza,lakini angel halisisitizwa huku ile cheni hikiwa ina mchoma shingoni,ikabidi hawalazimishe,wakiwa bado wanabishana yule kiumbe alitokea nyuma ya angel huku hakiunguruma kama simba aliyejerehuliwa..

    ******😈😈😈🙈🙈🙈😈😈*****

    upande wa pili kule kijijini haliitwa yule mtaalamu(mganga),alifika na kuanza mambo yake halichukua kitamba cheupe na kukitandika chini kisha akachukua vipande vya mti fulani na kuviweka juu yake na kuwasha moto ulitoa rangi ya bluu alinyunyizia dawa zake huku akiongea maneno yasiyo eleweka mara ule moto ukalipuka na kuwa mwingi, ajabu ni kuwa lilionekana lile tukio ndani ya pango jinsi jofu alivyoitoa ile cheni pahali pake,wote walishituka hasa madam mary na prof Moses hawakuamini macho yao,kisha likaonekana na lile tukio la Prof Henry kuuchukua ule mkufu alafu ukadondoka toka mfukoni mwake,matukio yote hayo yalionekana ndani ya moto huo,ghafla ule moto ukazimika,mfalme alikasilishwa na kitendo kilichofanywa na wageni hao,ikabidi kiandaliwe kikosi cha mfalme ili waende kuutafuta ule mkufu,na wafanye juu chini wahakikishe wanamvalisha kiumbe huyo shingoni na huo ndo utakuwa mwisho wa kiumbe huyo,yule mganga haliwapaka madawa iwe kama ndio sumaku ya kuwaonyesha wapi huo mkufu ulipo,"yeyote kati yenu hatakaye usogelea huo mkufu hutatoa miyonzi na kuhumilika mwili wake sababu ya hiyo dawa niliyo wapaka,mtauchukua na kumwiinda adui yetu mkimpata hakikisheni mnavalisha shingoni mwake na sio sehemu nyingine,na ntawapa dawa ambayo mtaipaka kwenye silaha zenu,dawa hii mkimchoma na kumuingia kiumbe huyo haitomuangamiza ila itamsababishia jeraha lisilopona sawa"sawa waliitikia askari hao kumi na moja shupavu baada ya kupewa maelekezo na mganga huyo,kisha safari ilianza kwenda msituni kumuwahi kiumbe huyo kabla hajaja ndani ya kijijii chao na kuzua maafa makubwa.

    Kutokana na makosa walioyafanya wenzao mfalme alitoa amri Prof Moses pamoja Mary nao wapakwe ile dawa waende kusaaidia na askari hao wa mfalme kumi na moja kwenda kumuangamiza kiumbe huyo.

    Wakaanza safari mida ya jua kali ilikuwa kama mishale ya saa sita mchana,waliingia porini humo huku wakiangaza angaza huku na kule kuangalia hali ya usalama,walikwenda kwa kufuata maelekezo, jinsi walivyoelekezwa na yule mganga sehemu ulipodondokea mkufu kutoka mfukoni mwa prof Henry,walifika katikati ya msitu huo na kuamua wapumzike kwanza kidogo huku wakiweka silaha zao sawa,mmoja wao aliamka na kwenda kujisaidia haja kubwa pembeni kwenye kichaka,akiwa huko linajitokeza joka kubwa ajabu na kumkamata yule askari wa mfalme kwa meno yake yenye ncha kali.......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    joka hilo la humo msituni lilikuwa na hasira na watu kwani ndio waliofanya mwenzake afe,(lile joka lililokufa baada ya kuchomwa na miyonzi ya ule mkufu wakati likitaka kumdhuru malkia akiwa bado mdogo angel)lilimtafuna mzima mzma,kelele zake ziliwashitua askari wengine,wakaja kupambana nalo,liliwakamata askari wengine wawili na kuwatupa mbali kwa mdomo wake kisha likawa linawachapa na mkia wake wale askari wengine wa mfalme ,askari mmoja kwa ujasiri aliruka kwa kudunda juu ya gongo la mti na kwa jambia lake halilikata kichwa lile joka likadondoka chini na huo ukawa ndo mwisho wa joka hilo la humo msituni,wale waliokuwa wametupwa mbali na joka hilo mmoja alikufa baada ya kupiga mgongo kwenye mti,waliendelea na safari yao kuingia ndani zaidi ya msitu huo,wakiwa wanatembea tembea walikutana na maiti ya mtu haina kichwa walipoichunguza vizuri waligundua ni ya wanakijiji mwenzao,maiti hiyo ilinyofolewa kichwa na yule kiumbe,waliifunika maiti hiyo kwa matawi ya miti,nakuendelea na safari yao,huku kila mmoja wao hakiingia na wasiwasi juu ya usalama wao kutokana na mauaji ya kikatili yanayofanyika ndani ya msitu huo,prof moses alijilaamu kwanini alikuwa prof,ghafla wanasikia milio ya risasi mfululizo nakuwafanya wazidi kuingiwa na wasi wasi.

    ********😈😈😈🙈😈😈😈😈😈********

    Upande wa pili kile kiumbe kilikuwa kimetokea nyuma ya angel,wakati wakiwa wanabishana kuondoka,kilitoa mlio kama simba,akili ziliwaruka wote walitimua mbio na kumuwacha angel akiwa anatetemeka akiwa ajui afanye nini,alibaki ameganda kama sanamu huku jasho likimchirizika kama kamwagiwa maji,aligeuka nyuma taratibu huku anatetemeka,alipogeuka alimwona yule kiumbe uso kwa uso,uzalendo ukamshinda alijikuta anapiga yowe,nakumfanya yule kiumbe amfate kwa kasi,kilipomfikia kilijaribu kumkaba angel lakini kilishangaa hakiwezi kumgusa kila kikijaribu hakimgusi,angel mda huo alikuwa kadondoka chini na kupoteza fahamu,kilipoona hakimwezi kilikasirika na kuanza kung'oa miti ovyo na kuirusha mbali,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo huo wale askari pori walizisikia zile yowe alizokuwa akizipiga angel,wakajua kwamba muuaji hayupo mbali na wao,wakakimbia kufatilia zile yowe wakiwa wanakimbia askari mmoja alijikwaa na kudondoka alipokuwa akisimama kipande cha mti mkubwa ulio rushwa na yule kiumbe kilimwingia mgongoni na kutokezea kifuani,alikufa papo hapo huku damu nyingi zikimrukia askari mwingine,walishangaa kwa kitendo cha miti kurushwa rushwa ovyo bila shaka huyu si binadamu wa kawaida.mwenye uwezo wa kung'oa miti namna hii,aliongea askari mmoja huku wakiendelea kusonga mbele,walifanikiwa kufika eneo la tukio na kumshuudia yule kiumbe akiwa anafanya yake huku chini yupo angel akiwa ajitambui,inspecta mkuta alitoa amri,"open your fire""shoot"open youre fire"...walimimina risasi nyingi sana kwa kiumbe huyo,kutokana nakuwa na silaha nzito za kivita zilimtoboa toboa kiumbe huyo mwili wake na kumfanya hasiifurukute,risasi zilimzidi ujanja ikabidi kiumbe hicho kijibadilishe na kuwa mbwa mwitu mkubwa mweusi,wale askari walishituka kidogo lakini hawakuacha kumshambulia kiumbe huyo aliyebadilika sasa na kuwa mbwa mwitu,kwa ustadi mkubwa mbwamwitu huyo alikwepa risasi hizo huku hakiwafata kwa kasi,askari walishambulia huku wakirudi nyuma,kile kiumbe kilitimua mbio nakuwapotea,walihisi kakimbia nakuondoka zake ghafla bila ya kutegemea askari mmoja aliuwawa kikatili kwa kupitiwa utumbo na mbwa mwitu huyo aliyekuja kwa kasi na kumtia meno ya tumbo na kutoka na utumbo,ndipo sasa askari pori hao chini ya uongozi wa inspecta mkuta,walimfyatulia risasi kwa kumfukuza,yule mbwa mwitu aliwaacha mbali,akabadilika tena na kurudi katika umbile lake la kutisha,safari hii alitisha zaidi kwani pembe zake kichwani ziliongezeka urefu,meno na kucha zilikuwa ndefu zaidi,huku akiwa katika umbile la kibinadamu asiye na ngozi(yani nyama hazikufunikwa na ngozi)kilipotea na kutokezea nyuma ya askari pori mwingine na kumziba mdomo kisha kikampulizia moshi mweusi puani,aliaanza kuishiwa damu macho yakawa meupe pee ngozi ikapauka ghafla kikamwachia akadondoka chini huku akitoka vumbi kama aliyeoshwa kwenye saruji,kisha kikapiga hatua za kikakamavu kumfuata inspecta mkuta akiwa ana angaza angaza huku na huko kumtafuta mbwa mwitu,bila ya kujua yule kiumbe anamfata kwa nyuma......





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog