Search This Blog

SEWATO (KOSA LA DAMU) - 4

 







    Simulizi : Sowato (Kosa La Damu)

    Sehemu Ya Nne (4)



    Mauaji ya kikatili yanaendelea kutokea ndani ya msitu mnene nchini Congo,baada ya kiumbe wa ajabu kufunguliwa bila ya kotokujua na mwanachuo mmoja(jofu)na kusababisha maafa hayo,

    Ndani ya msitu huo bado hali ni tete kwa wanachuo waliosalia research/utafiti wao unaingiwa dosari,angel akiwa ajitambui yupo chini kaanguka askari pori wanakuja kutoa msaada baada ya kusikia kelele/yowe zisizokuwa za kawaida wanapofika eneo la tukio wanakutana na jambo linalosababisha baadhi yao kupoteza uhai*********

    kisha kikapiga hatua za kikakamavu kumfuata inspecta mkuta akiwa ana angaza angaza huku na huko kumtafuta mbwa mwitu,bila ya kujua yule kiumbe anamfata kwa nyuma..songa nayo sasa,,,,,



    Kutokana na mafunzo haliyofundishwa jeshini,inspecta mkuta anahisi adui yupo nyuma yake,anageuka kikomando huku silaha yake ipo active kwa kutema risasi,anapogeuka anaona tu takataka za miti,kumbe yule kiumbe alipotea ghafla wakati alipogeuka,kiumbe huyo akatokezea kwa askari mwingine, kwa nyuma yake huku kikichilizika damu mdomoni kama maji,damu iyo ilimdondokea askari huyo na kumfanya ajiguse sehemu aliyodondokewa na kitu kama maji maji alipashika kwa mkono wake ,alipotazama mkononi pake alishituka baada ya kuona ni damu ndio iliyomdondokea,aligeuka kwa kasi ya ajabu ili apambane lakini alikuwa ameisha chelewa kile kiumbe kilimkaba kooni na kumyanyua juu kisha kikatoa moshi mweusi mdomoni na kumpulizia mdomoni mwa askari pori huyo,nayeye akawa kama yule askari wa kwanza,macho yakawa meupe kisha ngozi ikampauka kama kamwagiwa saruji/cement.

    Purukushani hizo ziliwashitua askari pori wengine na kuwafanya kwenda mbio upande alio kuwepo,walishuudia mwenzao akiwa teyali kapoteza uhai na yule kiumbe ametoweka,ikabidi wamchukue angel na kuondoka naye kurudi walipo acha gari yao aina ya land cruiser,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****😈😈😈😈🙈🙈😈😈😈😈😈😈😈😈****

    Upande wapili askari wa mfalme gumbo walisikia milio ya risasi zilizofanya wagundue kuna watu mle msituni,lakini prof moses pamoja na madam mary waligundua iyo milio ya risasi si ya silaha ndogo walijipa matumaini ya kuwa salama kwani milio ya silahaa hizo zilikuwa ni za ma askari tu ndio wenye kuzimiliki silaha hizo,walikubaliana wasitengane walishikana mikono wote na kutembea kuelekea kule ulipo mkufu,walitembea hadi ikatimia saa 5:30 za jioni,walihisi kuchoka na kumuomba kiongozi wao aliyeitwa siso,wapumzike lakini haliwaambia hawana mda wa kupumzika,wakiwa wanatembea kivivu vivu huku macho yakiwa hayatulii sehemu moja kwa kuangalia juu chini,kulia na kushoto mmoja wao hanakanyaga sehemu iliyokuwa imechimbwa shimo na kufunikwa na matawi ya miti kama mtego,

    mtego huo ulichimbwa na yule mwanakijiji aliyekutwa amepoteza maisha na maiti yake ikiwa haina kichwa,kwa kuwa walikuwa wameshikana mikono aliingia shimoni na kujikuta akimvuta mwenzake aliyekuwa ameshikwa naye mkono walidumbukia shimoni humo na kutobolewa na miti yenye ncha kali iliyowekwa kwa ajili ya kumnasa mnyama,wote walikufa hapo hapo huku mwingine naye akiserereka na kutumbukia shimoni humo sababu walikuwa wameshikana mikono,alichomwa na miti hiyo kwenye kanyagio za miguu yake,alipatwa na maumivu makali mno,walimtoa shimoni humo na kubebwa na mmoja wa askari hao,huku madam mary naye hakiponea chupuchupu kuingia shimoni humo waliendelea na safari yao huku yule aliyechomwa hakitoka damu nyingi sana ikabidi wapumzike ili wamtibu mwenzao,haliwekewa madawa ya kuzuia damu isitoke,halikata tamaa ya kuishi huku hakimuomba mungu achukue tu roho yake kuliko kumpa yale mateso alioongea kwa lugha yao,wenzake walimwonea huruma na kumpa moyo kuwa hatakuwa vizuri mda si mrefu,ghafla bila yakutokutegemea kile kiumbe kinatokezea katikati Yao ,wanatimua mbio baadhi ya askari akiwemo prof Moses pamoja na mary,kile kiumbe kinamtia kucha za kifuani yule askari wa mfalme aliyechomwa miguuni na kumtoa moyo kisha kikautafuna huku kikicheka kwa sauti ya kutetemesha hadi nyasi,

    siso anachukua hule mshale wa dawa na kuuweka ndani ya upinde analenga shaba ya mgongoni yule kiumbe,lakini yule kiumbe anahuhisi huo mshale na kupotea ghafla, hule mshale unapitiliza na kumchoma askari wa mfalme mwingine aliyekuwa na yeye akijaribu kumlenga yule kiumbe upande wa pili,kabla ajauachia hule mshale unamuingia kooni na kumtokezea kwa nyuma na yeye anauachia mshale wake sababu ya mshituko wa kasi ya hule mshale kumuingia kooni,mshale huo unaelekea moja kwa moja kwa siso.....



    Kwa ustadi wa hali ya juu siso hanaukwepa ule mshale unakwenda moja kwa moja kuchoma kwenye mti,siso anakwenda kumwaangalia mwenzake,cha kushangaza siso hakumuona mwenzake alishangaa sana huku hakijiuliza ametowekaje haraka hivyo bila ya hata kumuona akiondoka,anahamua kuondoka zake kuwasaka wenzake waliokimbia,alipopiga hatua moja mbele alihisi kudondokewa na matone kama ya maji kichwani,alijifuta kwa mkono wake alishituka baada ya kugundua ni matone ya damu ndio yaliyomdondokea alipoatizama juu alishuudia yule kiumbe hakiwa anamnyofoa mwenzake viungo vyake na kuvitafuna,wazo likamuijia akarudi nyuma kwa kunyata ,kisha akachukua mshale wenye dawa maalum waliopewa na mganga ambao hutamtia jeraha lisilopona kwa haraka na kumpa maumivu makali,

    Haliutia kwenye upinde kisha hakauvuta kwa nguvu na kuachia,mshale ulifyatuka kwa kasi na kutii amri ukazama moja kwa moja kwenye kifua cha yule kiumbe,kilipiga kelele kali huku kikiuachia mwili wa yule askari kisha kikajikunja kwa maumivu makali huku kikijaribu kuuchomoa,lakini siso alichukua tena mshale mwingine na kuuvuta, nao hukatii amri kwa kumuingia ubavuni mwa kiumbe huyo,kiumbe huyo wa ajabu alipoona hali imekuwa ngumu aliruka juu ya miti na kutokomea ndani zaidi ya msitu huo mnene,

    Siso aliusogelea mwili wa mwenzake na kuanza kulia huku akimuomba msamahaa kwa kumsababishia kifo,ghafla hule mwili ukabadilika na kuwa majivu sababu ya sumu kali ya kiumbe huyo,siso halinyanyuka na kuanza tena safari ya kuutafuta hule mkufu,kwenye podo lake la mishale halikuwa na mishale mitatu tu,.

    *******😈😈😈😈🙈🙈😈😈😈😈************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa pili yule kiumbe halionekana akiwa juu ya mti mkubwa akiwa anaichomoa ile mishale,kiliuchomoa mshale wa kwanza na kuutupa kilihisi maumivu makali kilishangaa jeraha aliponi, kiliingiwa na hasira kisha kikaushika mshale wa pili nakutaka kuuchomoa,ghafla kikawaona askari wa mfalme wakipita chini ya mti huo,kiliuchomoa ule mshale nakushuka kwa kasi chini na hule mshale,nakumchoma nao askari mmoja utosini askari wengine walitimua mbio bila hata ya kutoa msaada kwa mwenzao,kile kiumbe kilitia meno shingoni pa yule askari na kumnyonya damu yote,kisha yale majeraha yakapona ghafla,wakati yale majeraha yanapona yalimpa maumivu makali kilipiga kelele za ajabu zilifanya hali ya hewa kubadilika,mawingu mazito ya mvua yalitanda angani huku radi na ngurumo zikipiga kwa pamoja,kile kiumbe kiliangaza kushoto na kulia kisha kikatoweka ghafla.

    ******""**************~!!!!!""?*****((***

    Wakiwa wamembeba angel walifanikiwa kuiifikia gari yao(land cruiser)walipanda askari pori hao,inspecta mkuta alichukua kifaa maalum kitumikacho kuwasiliana na makao makuu yao,mkuta alijaribu kuwasiliana na makao makuu yao lakini hali ya hewa hilikuwa mbaya na kufanya mtandao kupotea,ikabidi dereva awashe gari wakaondoka....

    , Mara angel hakiwa yupo usingizini hanaoteshwa nakumuona yule kiumbe akijitokeza mbele ya gari lao kisha dereva anamkwepa na kutoka bararabarani gari inamshinda dereva na kuingia porini huku aking'ang'ana kufunga break lakini break zikilimsaliti dereva kwa kushindwa kupunguza mwendokasi wa gari,wakati hakiwa yupo ndotoni wale askari wanamuona angel hakiweweseka huku shingoni pake cheni yake inawaka na kuzima mwanga kama moto,askari mmoja anahamua kumwamusha lakini haamuki,ndipo alipoishika ile cheni huku akiishangaa ghafla ikazima ule mwanga ndipo angel anashituka toka ndotoni,unajisikiaje alioji mkuta,angel hakuwajibu kitu akabaki anawashangaa huku hakijiuliza hawa wakina nani nawananipeleka wapi,ndipo askari mmoja akamweeleza kwamba walimkuta kadondoka chini akiwa kapoteza fahamu baada ya kupatwa na matatizo,inspecta mkuta akamuuliza

    eeh tuambie sasa ilikuwaje,angel alipoangalia nje alishituka baada ya kugundua yupo ndani ya gari tena likiwa linaendeshwa kwa kasi,ghafla ile sauti ikasikika masikioni mwake ikimwambia"shuka haraka mpo kwenye hatari shukaaaa..."angel alihisi kuchanganyikiwa ndipo kumbukumbu zikaanza kumuijia akakumbuka na ndoto aliyoiota angaunganisha matukio kichwani mwake ,wazo likamwijia akakurupuka na kumwambia dereva hasimamishe gari,"dereva dereva simamisha gari,"aliongea kwa wasi wasi,maaskari pori walidhahania kwamba labda kaingiwa na kichaa,ikabidi wamtulize kwa kumuhakikishia usalama wake."binti usijari upo na askari usi hofu tunakupeleka pahali salama"inspecta alimshawishi lakini angel halikataa na kuwaanza kufanya fujo kwa dereva ili gari isimame,ndipo ikabidi wamkamate kwa nguvu na kumzuia hasifanye fujo,

    Jamani tutukufa huko mbele kuna...kabla hajamaliza kusema askari mmoja alimchoma sindano ya usingizi shingoni ili hatulie hasije kusababisha ajali,dereva alizidi kukanyaga mafuta na kuongeza gia,gari ikawa inaenda kwa kasi,inspecta mkuta alijaribu tena kupiga simu lakini yule kiumbe alikuwa kaisha fanya hali ya hewa kuwa mbaya na kufanya network kupotea,dereva aliendesha gari kwa kasi sana hadi wakafika eneo ambalo angel alioteshwa ndotoni......



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva alizidi kuonganyaga mafuta nakufanya gari iende kasi sana ghafla bila ya kutegemea dereva alishituka baada ya kuuona kitu cha ajabu kimesimama barabarani bila hata kuwapisha,alipiga honi mfulululizo lakini haikusaidia kitu kwani kile kiumbe hakikuwapisha,dereva alikanyaga breki kwa nguvu lakini hazikumtii,ikabidi hakwepeshe gari,gari iliiacha njia na kuiparamia miti huku wakizidi kuingia ndani zaidi ya pori kila mtu alisali kumuomba Mungu kwa nanma yake,huku angel hakiwa bado hajazinduka tangu achomwe sindano ya usingizi,kutokana na gari kuwa kasi iligonga gogo la mti na kupinduka mara nne,askari pori walirushwa nje sababu walijisahau kufunga mikanda wote walipoteza fahamu huku hikisikika sauti kwenye kile kifaa maalum cha inspecta mkuta(yani radio call)kutoka makao makuu"inspecta johny hapa umenisoma over,inspecta johny hapa umenisoma over..."

    **(******😈😈🙈😈😈😈*********

    Upande wa pili kulikuwa na mtafutano mkubwa,askari wa mfalme gumbo walipoteana ndani ya msitu huo mnene,prof Moses hakiwa na madam Mary pamoja na askari wa mfalme wawili,wanajikuta wakiwa pekee yao huku kila mmoja wao hakiwa na wasi wasi kwani hakuna aliyetegemea kazi kuwa ngumu kiasi hicho,wasi wasi uliongezeka hasa ile taswira ya mauaji yaliyofanywa mbele ya macho yao na yule kiumbe wa ajabu inapozunguka ndani ya vichwa vyao kama mkanda wa filamu ya kutisha. Ilikuwa yapata saa kumi na moja jioni jua likiwa lishapungua makali yake kuashilia kuukaribisha usiku,walitamani kurudi ila ni mwiko kurudi bila ya huo mkufu ni bora wauliwe kuliko kurudi kijijini bila ya mkufu huo,prof hakiwa na wenzake waliendelea na safari,ghafla walikutana na wenzao wengine wawili jumla wakawa sita, walikumbatiana kwa furaha huku machozi yakiwatoka,hakika ujasiri wote uliwaisha askari hao mbele ya kiumbe huyo wa ajabu,ikabidi wajipumzishe kidogo,wakakaa chini ya mti mkubwa,askari mmoja aliona mti uliokuwa na matunda yalioiva vizuri(mti huo ulikuwa na asili ya mapasheni/passion),hamu ikamwiingia akaamuka na kuufata mti huo akachuma la kwanza akala,lilikuwa na radha nzuri,kwa uroho akaamua kuvuta matawi ya mti huo yaliyokuwa yamelanda kwenye mti,alivuta tawi moja bila ya kujua kama kuna nyoka mkubwa,alilitikisa kwa nguvu ili matunda yadondoke wenzake walikuwa wanamwaangalia tu wakiwa hoi wamechoka,ghafla yule askari alishitukia anadondokewa na yule nyoka,nyoka huyo alimkaba kwa kujizungusha shingoni mwake,alishindwa kupiga kelele akabaki anakoroma,yule nyoka alianza kumuingilia mdomoni mwa askari huyo,alidondoka chini na kuanza kufurukuta kama kuku aliyechinjwa,wenzake walishituka na kumfuata kwa kasi, walipomfikia walipigwa na bumbuwazi baada ya kumshuudia yule nyoka ndo anaishilia mdomoni mwa mwenzao,walijitahidi kumsaidia kwa kujaribu kumtapisha lakini walikuwa wameishachelewa,macho yaligeuka na kuwa mekundu mapovu yalimtoka mdomonina kukata roho,walisikitika sana,askari mmoja akawa kama vile amini alichokiona alinyanyuka na kurudi nyuma bila kugeuka huku machozi yanamtoka,alipokuwa anarudi nyuma alijihisi kujigonga kifuani mwa mtu lakini mtu huyo alikuwa kama vile amelowana alafu ni wa baridi sana,aliingiwa na wasiwasi akageuza shingo yake kumuangalia ni nani huyo,alipogeuka alipatwa na mshangao baada ya kumuona yule kiumbe kasimama mbele yake,alipiga kelele zilizowashitua wenzake,kile kiumbe kikamshika shingo na kumtia meno yake makali na kumnyonya damu,askari mmoja aliingiwa na hasira akamfuata yule kiumbe akiwa kashika sime alinyanyua sime yake ili amshushie yule kiumbe,lakini yule kiumbe alimuwahi kwa kumpiga kofi moja lilimnyofoa kichwa kikabaki kiwiliwili kikirusha damu kama bomba la maji,kile kiumbe kikawageukia prof henry,mary pamoja na askari mmoja wa mfalme aliyesalia walitimua mbio,walikimbia hadi wakakutana na siso,siso aliwashangaa na kuwauliza kimetokea nini walimueleza kilechotokea siso hakaingiwa na hasira akachukua mshale wenye dawa maalum na kuuweka kwenye upinde wake kisha akarudi kule kilipokuwepo kile kiumbe,walimzuia lakini hakutaka kumsikiliza mtu,alikimbia bila kujua amebakiwa na mishale mitatu tu,walimfukuza ili kumzuia ghafla kile kiumbe kikawatokea mbele yao,siso aliuvuta mshale na kuuwachia lakini yule kiumbe hakaukwepa siso akachukua wa pili nao kikaukwepa akachukua watatu na kuvuta kwa hasira mshale huo,ulilkwenda na kumuingia kiumbe huyo mguuni,siso alipopapasa kwenye podo lake la mishale akajikuta ameishiwa mishale yote ikabidi amvae yule kiumbe hivyo hivyo,lakini alishitukia ananyofolewa utumbo huku ana ona,prof na wenzake walipoona hali imekuwa ngumu wakakimbia,wakiwa wanakimbia madam Mary anajikwaa na kudondoka chini ,alipodondoka pale chini alifanikiwa kuuona hule mkufu................

    *********************************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa mida ya saa moja jua ndo linaihaga siku hiyo na kuukaribisha usiku,angel anasikia sauti ikimwambia akiwa usingizini,"angel binti yangu amka haraka kabla ujachelewa kuna hatari ipo karibu yako"angel alishituka kutoka usingizini na kujikuta yupo sehemu ambayo hakuitambua,alipoangalia pembeni aliona ile gari ikiwa imebondeka bondeka vibaya,alipoangalia pembeni akawaona watu watano ambao hakuwajua wakiwa kila mtu upande wake wamelala chini hawajitambui,mara ile sauti ikajirudia tena kichwani mwa angel tena safari hii na ile cheni yake ikiwaka mwanga mkali na kutoa ishara kwa kumuangazia njia ya kupita ghafla ikazimika,angel kila kitu alioona kama ndoto,kumbukumbu zake zilikuwa zimepotea,ghafla akiwa anawaza alisikia sauti ya ajabu ikitokea ndani ya msitu huo kama kicheko cha kutisha,alipojaribu kusimama alihisi maumivu makali kwenye bega lake la kushoto kikifuatiwa na kichwa kilichomfanya hajihisi kizungu zungu kikali,ghafla alishituka baada ya kumuona mtu wa ajabu hakitokea ndani ya msitu na kuja pale walipo huku wale maaskari wakiwa bado fahamu hazijawarejea.......





    Mtu huyo alizidi kuwasogelea pale walipo kuwa,mara angel akasikia ile sauti ikimwambia kichwani mwake "jifanye umepoteza fahamu sababu umeishachelewa kuondoka huyo ni mzimu wa Sewato ni hatari sana ila ntakusaidia lala chini na usipumue,bana pumzi yako wala usitikisike anaweza kukisia umekwisha poteza uhai"ile sauti ikatoweka angel akaitii na kujilaza chini huku akiwa amebana pumzi,kile kiumbe kiliwafikia na kuanza kukagua mmoja mmoja hadi kikamfikia angel,kilimwaangalia kwa makini kikaiona ile cheni kifuani pake,kikapeleka mkono kuishika.Kutokana kulikuwa na giza sana ndani ya msitu huo angel alikuwa anakichungulia kile kiumbe kwa kuibia ibia kwa kuyafumbua kope za macho yake pole pole ,alifumbua macho yake kidogo sana ili akione kinafanya nini sababu ya giza alilazimika kufumbua macho kwa kuyakodoa ili aone vizuri bila ya kujua kile kiumbe kipo karibu yake sasa nakinamsogelea sasa kuigusa ile cheni,angel alipoangalia vizuri alikiona kiumbe hicho kipo mbele yake na kinaleta mkono maeneo ya shingoni kwake,uwoga ukamuingia nakujikuta mwili wote unamsisimka,alianza kutetemeka hakisali kwa mungu amuepushe na hilo janga,kile kiumbe kili hisi kama angel yupo hai sababu halikuwa akitetemeka hadi meno yanagongana kama mtu aliyemwagia barafu,kabla akijaishika ile cheni yenye mzimu wa mama yake angel(malkia),askari pori mmoja alipata fahamu aliamuka kwa kukurupuka sababu ya giza tororo, liliyazonga zonga macho yake,akujua yupo wapi,akawa anaita kama kuna mtu anamsikia bila ya kujua,yupo hatarini ....



    **********************************

    Uongozi wa chuo kikuu cha jijini Dar es salaam(UDSM)kinaingiwa na wasi wasi mkubwa baada ya kutopata taarifa yoyote kutoka kwa maprof walioenda na wanachuo kwa ajili ya utafiti nchini congo,hakukuwa na mawasiliano yoyote kwa siku sita mfululizo hali hiyo pia inawatia wasi wasi mkubwa wazazi wa wanachuo hao,,ambao pia wanakuja chuoni mara kwa mara kuuluzia hali za vijana wao ambao wamekuwa hawapati mawasiliano nao kwa siku sita mfululizo,chuo kinafanya mawasiliano na serikali ya congo ili kujua nini kinaendelea huko congo,serkali ya congo inawa ondoa hofu kwa kuwahaidi kulishughulikia suala hilo,kikosi maalum cha maaskari kumi na sita wa congo kinaandaliwa kwenda ndani ya msitu wa sego kwenda kubaini tatizo ni nin,helicopter ya kijeshi inaandaliwa na kikosi hicho chini ya uongozi wa inspecta martin,wanaingia ndani ya helicopter kisha rubani anairusha juu kuelekea ndani ya misitu ya sego,kutoka kambini kwao hadi msituni ni mwendo wa saa moja na nusu,helicopta inawasili msituni na kuanza kuzunguka zunguka huku na kule kuangalia kama watawaona lakini hawaoni mtu kwa mbali wanauona mwili wa mtu ukiwa umetundikwa juu ya mti na umechunwa ngozi,hofu inawaingia juu ya usalama wawanachuo na maprof waliomo ndani ya msitu huo,wakiwa wanaendelea na safari yao wanaona tukio la ajabu likifanyika ndani ya msitu huo mbele ya macho yao nakufanya wakae tayali kwa vita huku wakizikoki silaha zao nzito za kivita......

    😈😈😈😈🙈🙈😈😈😈***((*CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kile kiumbe kinaachana na angel na kunyanyuka pale chini kisha kinasimama na kutoa kicheko kikali na cha kutisha,moyo wa askari pori huyo unapata mshituko na kumfanya aingiwe na wasi wasi,"We nani"??,alioji askari pori huyo huku kumbukumbu zake zikiwa zinamrejea polepole,"Nakuuliza we nani na unataka nini"??!!.akuna aliyemjibu kumbukumbu za mauaji ya kutisha ya yule kiumbe zikamrudia na kumfanya hazidi kuingiwa na uwoga wa hali ya juu,halitetemeka huku aja ndogo ikimtoka,ghafla akahisi kushikwa bega kwa nyuma alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani kuliko kufa huku anashuudia kwa macho yake alipogeuka nyuma kumuona ni nani aliyemshika bega, akumuona vizuri usoni sababu ya giza,kumbe alikuwa ni inspecta mkuta ndo kamshika bega,inspecta akamuonyesha ishara fulani iliyomuashiria anyamaze kimya,alinyamaza baada ya kugundua ni mwenzake,yule kiumbe halikuwa hakiwatizama tu bila ya wao kumuona,yule kiumbe akaamua kuwaacha kwanza na kumfata angel.Angel alimuona anavyokuja hakataka kusimama lakini maumivu ya bega yalimtesa nakujikuta akitoa sauti ya maumivu makali,yule kiumbe hanamfikia na kumshika angel kwa nguvu,angel anapiga kelele za kuomba msaada yule kiumbe ananyanyua mkono wake wenye kucha kali juu ili kumnyofoa angel utumbo huku kimemnyanyua juu kwa mkono mwingine.....



    Angel alijaribu kujisaidia kwa kukipiga mateke kile kiumbe,lakini haikusaidia kile kiumbe kilizamilia kummaliza angel kabisa,kilinyanyua mkono wake juu lakini kabla akijakusudia kumuua angel kinahisi kuapigwa na kitu kizito kichwani kina muachia angel,kilikasirika sana na kumgeukia aliyemsababishia asifanikishe dhamira yake,alikuwa ni inspecta mkuta ndio aliyempiga na kipande cha chuma cha gari kichwani,kile kiumbe kilimfata inspecta kwa Kasi ili kummaliza lakini inspecta alitimua mbio na kuwa onyesha ishara angel pamoja na yule askari waondoke,kile kiumbe kilimfukuza inspecta,angel halikuwa hakikohoa sana sababu alikabwa koo kisawa sawa,yule askari aliyekuwa akiitwa benedict,alimnyanyua angel na kuondoka naye japokuwa kulikuwa na giza tororo,waliwaacha wale askari wengine wawili pamoja na dereva wakiwa bado hawajazinduka.

    *******************************



    Kulipambazuka jua lilikuwa lishaanza kuchomoza madam mary pamoja na Prof Moses wakiwa na askari wa mfalme mmoja tu aliyebaki kati ya 15,walikuwa wamejipumzisha juu ya mti mkubwa usiku mzima,Mary alikuwa kaukota hule mkufu,walishuka chini ya mti huo nakuanza safari ya kwenda kumuangamiza yule kiumbe kwa kutumia mkufu huo,matumbo yaliwauma kwa njaa na kiu kali iliyatesa ma koo yao waliishiwa nguvu kabisa,walitembea wakiwa makini huku wakishikana mikono,kwa bahati nzuri yule askari alikuwa ni mzoefu na msitu huo,aliwaongoza njia ya kuelekea kwenye mto iliwaweze kukata kiu,walifika nakunywa maji kwa pupa madam mary akampa yule askari wa mfalme ule mkufu aliuuweka kwenye kibegi alichokiokota msituni mkufu huo ulijinasa kwenye zipu ya kibegi hicho bila ya yeye kujua,walikunywa maji kwa pupa baada ya kutosheka walielekea sehemu yenye matunda wakachuma na kuyafakamia,wakiwa wanaburudika na matunda ghafla wanakutana uso kwa uso na inspecta mkuta akiwa hoi katapakaa damu mwili mzima,kumbe yule kiumbe alimjeruhi,alidondoka chini huku akihema kwa tabu,walimchukua nakuondoka naye lakini kabla hawajafika mbali wanasikia sauti ya helicopter,wanapata matumaini mapya,wakiwa bado wanatahamaki yule kiumbe anatokeza mbele yao akiwa kashika mguu wa binadamu,inspecta aliugundua ni wa benedict kutokana na kiatu alichokuwa kakivaa marehemu,ghafla anawafata pale walipo,mary anamwambia yule askari wa mfalme autoe ule mkufu wamalize mchezo,kabla ajautoa yule kiumbe alimvaa yule askari akiwa bado hanaangaika kuuchomoa ule mkufu kwenye mfuko wake ukiwa umekwama kwenye zipu,kile kiumbe kilimkwaruza na makucha yake usoni,inspecta akajitoa mwanga na kuokota kipande cha mti akiwa anachechemea nakumfata yule kiumbe,prof Moses naye alihisi kuchanganyikiwa ajui afanye nini,ghafla helicopter ya askari pori inafika nakushuudia lile tukio,wanaamulishwa na inspecta martin kumshambulia yule kiumbe,risasi nyingi zinalengwa kwa yule kiumbe nakumfanya azidi kukasirika,anaachana na yule askari wa mfalme na kuanza kukwepa risasi,Prof moses na wenzake wanakimbia kutoka sehemu hiyo,yule kiumbe anaharibiwa aribiwa sura na zile risasi kutoka kwenye helicopter,kinaruka juu ya miti hadi kinaifikia ile helicopter na kuipa pigo moja liloisababisha ikose mwelekeo nakuanza kuyumba yumba ikitoa moshi,maaskari hao wanajishikilia kwa nguvu huku helicopter hikizunguka zunguka angani,rubani anajitahidi kuishusha lakini inamshinda,kwa bahati nzuri,rubani aliuona mti mkubwa wenye matawi mengi aliilengesha hapo,ilishuka kwa Kasi walijirusha nje na kuiacha helicopter ikienda chini bila mtu,mlipuko mkubwa ulitokea ndani ya msitu huo,wale askari waliumia na kupata majeraha madogo madogo.

    ************************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Prof Moses na wenzake walijikokota nakufika kwenye kambi yao,kabla hawajaingia ndani ya hema,wanamuona angel akiwa pekee yake bila ya yule askari pori,walimuuita ili aje,angel alipowaona alijawa na furaha,akapata nguvu kidogo,japokuwa aliishiwa chakula na maji alijihisi mwenye nguvu mpya,aliwakimbilia huku akiwa haamini kama hatakuja kukutana na walimu wake,lakini kabla hajafika ile sauti inasikika kichwani mwake ikimwambia"Angel usiende utauliwa kabla hujafika rudi".angel alisimama ghafla nakuangaza huku na kule,"jamani muondokeni hapo mtakuf....kabla hajamaliza kuongea yule kiumbe anatokea nyuma ya prof Moses tena kinapumua nakutoa moshi mweusi puani........



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog