Search This Blog

SEWATO (KOSA LA DAMU) - 5







    Simulizi : Sowato (Kosa La Damu)

    Sehemu Ya Tano (5)



    angel alipowaona alijawa na furaha,akapata nguvu kidogo,japokuwa aliishiwa chakula na maji alijihisi mwenye nguvu mpya,aliwakimbilia huku akiwa haamini kama hatakuja kukutana na walimu wake,lakini kabla hajafika ile sauti inasikika kichwani mwake ikimwambia"Angel usiende utauliwa kabla hujafika rudi".angel alisimama ghafla nakuangaza huku na kule,"jamani muondokeni hapo mtakuf....kabla hajamaliza kuongea yule kiumbe anatokea nyuma ya prof Moses tena kinapumua nakutoa moshi mweusi puani..Songa nayo sasa......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Angel alikiona kile kiumbe ila wao hawakukiona sababu walikipa mgongo,"prooofesa angaaliiaa nyuumaaa yakoo utakufa,ondoka haraaka"

    Prof aligeuka nyuma nakumuona yule kiumbe uso kwa uso,kilimkaba shingo nakumrusha mbali,kisha kikamfata yule askari wa mfalme aliyekuwa na ule mkufu wakumfungia kiumbe huyo,askari huyo alijerehuriwa na huyo kiumbe kipindi akijaribu kuitoa cheni kwenye begi lake hivyo alikimbia kwa shida,kiliruka na kwenda kumrukia askari huyo,kikaangka naye chini kisha,kikamkaba koo,askari huyo alifumbua mdomo nakukoroma huku akitapa tapa kujaribu kijiokoa,kilitoa moshi mweusi puani mwake huku kikihema kwa hsira,kilitapika wadudu wengi jamii ya funza kutoka kinywani mwake,wadudu hao walitambaa na kuanza kumuingilia mdomoni yule askari.

    Madam mary pamoja na angel wakiwa na inspecta mkuta walimkimbilia prof moses pahali alipodondokea,walimunyanyua kwa tabu nakukimbia huku nyuma walimuacha yule askari wa mfalme akisurubishwa na yule kiumbe.



    Yule askari wa mfalme alijaribu kuufumba mdomo wake lakini kile kiumbe kilimkaba koo nakumfanya aufumbue ili wale wadudu wamuingilie,ghafla akakumbuka hana ule mkufu ndani ya begi,alipitisha mkono hadi ndani ya begi nakuushika lakini kwa bahati mbaya ulikuwa umenasa kwenye zipu ya begi,ikabidi haunyanyue hivyo hivyo na begi nakujaribu kumvaalisha yule kiumbe,lakini aliishiwa nguvu,kwa bahati nzuri ule mkufu ulimgusa yule kiumbe ukawaka nakutoa ile miyonzi kile kiumbe kiliona hatari ipo mbele yake kikapotea nakumuacha pale yule askari,iyo ndio ikawa pona pona yake,akaanza kuwatapika wale wadudu.huku akiwa haamini kama kaponea chupu chupu,alihisi kichwani kitu kikimuendesha alianza kutoka damu puani huku macho yake yanabadilika nakuwa kama ya yule kiumbe alihisi kutetemeka na mwili kuhisi baridi kali ajabu,akajikokota huku akiyumba yumba kama mlevi wa pombe aliutoa ule mkufu kwenye begi nakuushikilia mkononi



    **********************************

    Upande wapili baada ya kufanikiwa kuruka kutoka kwenye helicopter,kikosi cha askari pori waliotumwa kuja kufatilia wanachuo wana hali gani,Nao wanajikuta katika hali ngumu kila kitu Chao kililipuka ndani ya helicopter ikiwemo risasi na simu za satellite kwa ajili ya mawasiliano na makao makuu yao,walijikokota wakiwa hawajui waeleke wapi japokuwa walikuwa ni askari pori,walipiga hatua wakiwa makini,kwani tayali walishajua ndani ya msitu huo mkubwa wa sego,kuna kiumbe hanafanya mauaji,walikuwa jumla kumi na tano,silaha walikuwa nazo ila risasi zilikuwa chache,walipokuwa wanatembea walisikia sauti za ajabu zikiwafata,zilikuwa zinawachanganya na kuwazidishia uhoga,sauti hizo hazikuwa na pahali sahihi zinakotokea,wao walishitukia tu wanasikia kama mtu anacheka nyuma yao walipogeuka nyuma zinazikika tena kwingine,ghafla askari mmoja alipotea kwa mazingira yakutatanisha wakiwa bado wanashangaa mwingine tena anapotea,kiongozi wao inspecta martin akatoa amri kila mtu ajiweke tayali kwa mashambulizi,kila mtu akachukua eneo lake nakujibanza,askari mmoja alijibanza kwenye mti mara akadondokewa na kitu kama maji maji kichwani alipotizama juu yule kiumbe kumbe alikuwa juu ya mti,alimnyofoa kichwa kikabaki kiwiliwili kikifyatua risasi ovyo,risasi hizo ziliwakosa kosa wenzake,walipoona hali imekuwa ngumu wakaamua kukimbia lakini kabla hawajakimbia maiti za wenzao wawili zinarushwa nakudondokea mbele yao zikiwa zimekauka kama zilianikwa juani miaka mitatu huku macho yamekuwa meupe pee,

    Ghafla tena kile kicheko kinajirudia na hapo hapo askari mwingine anashikwa miguu nakuvurutwa nyuma kwa kasi na yule kiumbe,askari pori hao wanamfukuzia huku wakimumiminia risasi mithili ya mvua ,kile kiumbe kiliwacha hatua chache nyuma wale askari pori,ghafla kikakutana uso kwa uso na yule askari wa mfalme tena kaushika hule mkufu mkononi,kile kiumbe kilimwachia mguu yule askari pori kisha kikamfata yule askari wa mfalme kwa kasi huku kikianda kucha zake kwenda kumfyekelea mbali.........

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Askari wa mfalme gumbo alijianda kupoteza maisha yake ila alihapa kufa na kiumbe huyo,yule kiumbe alizidi kumsogelea kwa Kasi ya hatari,ghafla kilisita nakusimama huku kikimwangalia yule askari kwa kumshangaa,yule askari wa mfalme alikuwa hoi kachoka baraa na yeye ghafla akasita kumsogelea yule kiumbe,kumbe wale wadudu waliomuingilia walianza kumbadilisha akili Yule askari wa mfalme,kile kiumbe kikaanza kucheka huku kikiangalia juu na kunyanyua mikono yake juu kuashiria ushindi,yule askari wa mfalme akaanza kubadilika usoni kwa kubadilika macho na kuwa kama ya yule kiumbe,huku akitapika damu nyingi,kichwa kilimuuma nakuanza kuangaika lakini aliona huo ndio muda mzuri wa kumuangamiza yule kiumbe alimsogelea nakuunyanyua ule mkufu ili amvalishe yule kiumbe,wakati huo huo wale askari pori nao ndio wanafika nakushuudia mambo ya ajabu,yule askari wa mfalme alipotaka kumvisha yule kiumbe,alijikuta akili yake inabadilika hapo hapo nakuhairisha,ghafla anahisi kiu ya damu mbichi pamoja na njaa akiwa bado ajielewi hule mkufu unawaka nakumchoma kwakuwa na yeye sasa alikuwa ameishabadilika akili,alihisi maumivu makali aliurusha hule mkufu juu,ukaenda moja kwa moja na kumuingia yule kiumbe kwenye moja ya pembe zake nakukwama.

    ghafla ukatoa miyonzi mikali nakumuingia yule kiumbe.mwili wake ukawaka moto kama wa petrol kiliangaika sana,kiliwaka moto huku kikimomonyoka kiuongo kimoja kimoja nakuwa majivu,kwa bahati mbaya wakati kinahaangaika hule mkufu ulichomoka kutoka kwenye pembe ghafla ule moto ukaanza kuzimika,bila kuchelewa wale askari pori walimwagia mvua ya risasi nyingi.kilipasuka pasuka nakuwa mchanga.Yule askari wa mfalme alitimua mbio nakutokomea ndani zaidi ya msitu huku akitetemeka kama aliyemwagiwa barafu.

    Wale askari pori waliusogelea ule mchanga nakuushanga askari mmoja akauona ule mkufu,akafanya tena kosa jingine akaunyanyua kutoka kwenye ule mchanga,akawa amemuamsha tena yule kiumbe,ghafla ule mchanga ukamrukia usoni,akaanza kuungua kama vile amemwagiwa asidi.aliungua nyama zote nakubaki mifupa.hule mchanga ukaanza kutambaa nakuwafata wale askari pori wengine kwa kasi.walitimua mbio kila mtu njia yake,ule mkufu ukabaki pale chini.



    **********************************

    Upande wa pili inspecta mkuta pamoja na angel na madam mary walimkokota Prof Moses hadi kwenye hule mto ambao walipelekwa na yule askari wa mfalme. Wakupumzika hapo giza lilikuwa lishaingia walikula matunda pori nakulala.asubuhi na mapema walidamka salama bila ya matatizo,Angel alikwenda kunawa uso mtoni kwa mbali akamuona mtu anakuja upande wao akiwa hoi kabisa,angel alihisi kusisimuka. Ghafla yule mtu akapotea machoni pake,mara akahisi tofauti tofauti ile hali ya kusisimuka ilikuwa tu ya kawaida tofauti alivyokuwa amevaa ile cheni mara ya kwanza,akajishika shingoni akuiona ile cheni wasi wasi ukamshika akakimbia nakuchukua kioo kidogo alichokuwa nacho kwenye kibegi chake nakujiangalia hakuuona,"mh! hii si kawaida mbona ile sauti siisiki tena alafu huu mkufu nao mbona si huoni?,au umedondoka?!!"angel alijiuliza maswali ambayo akuyapatia majibu,akaanza kuutafuta kama chizi,alifunua hadi mawe kama umedondoka kapo,lakini akufanikiwa kuupata.hadi wenzake wakaanza kumshangaa,madam mary akumuuliza anatafuta nini,angel akaanza kulia.ikabidi madam Mary amsogelee nakumbebeleza huku akimuuliza kipole amepoteza nini.angel akamwambia kwamba amepoteza cheni yake aliyopewa kama zawadi na wazazi wake kwamba haitunze kama moyo wake.madam mary akampa pole nakuanza kumsaidia kuutafuta.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mbali yule askari wa mfalme aliwaona angel na wenzake,aliamua kuwafata,lakini alihisi njaa kali akaona matunda kwenye mti akayapalamia kwa pupa nakuyachuma akachukua moja nakulila kwa pupa,ghafla alihisi lina radha mbaya kama ya mwarobaini,akallitema alihisi kukosa nguvu akajikokota nakufika hadi kwenye mto alihisi kiu kali,akachota maji kwa mkono nakuyanywa mara akayatema baada ya kuhisi ni machungu sana,akakosa kabisa hamu,akaamua kuwafata wenzake safari hii aliishiwa nguvu kabisa alipauka ngozi na mdomo wake kuchanika chanika nakutoa maji maji,aliwafikia akadondoka chini kama mzigo,walishituka sana kumuona walimgundua sababu ya mavazi yake japo yalikuwa yameraruka raruka,wakamfata nakumweka kimvulini angel akamchotea maji na kumpa,aliyanywa lakini akayatema walimsihii anywe ili apate nafuu lakini yalimshinda.aliyanyuka baada ya kuuona mti fulani ambao aliamini ni dawa aliufikia nakuuchuma,lakini haukung'ooka kwa bahati mbaya tawi la mti huo lilimkata kidoleni,akaamua kuinyonya damu yake ili isiendelee kotoka,alipopitisha kukiweka mdomoni kidole,pua zake zikahisi harufu nzuri ajabu,alipokiweka mdomoni kidole alianza kunyonya ile damu yake,alihisi radha nzuri ambayo akuwahi kuhisi maisha yake yote,alijingata aili damu iendelee kutoka,aliinyonya kwa kasi sana mara damu yake ikamkifu/ikamkinai.angel alibaki mdomo wazi hanamushangaa tu.ghafla yule askari akaliona jeraha la inspecta mkuta akahisi harufu ya damu akaanza kumfata kwa kasi wakati huo huo askari pori mmoja kati ya wale walioruka kutoka kwenye helicopter alikuwa anakuja upande wao kwa kasi huku akihema,nyuma yake hule mchanga ulikuwa unamfukuza kwa Kasi sana,alifika na kudondoka chini.inspecta mkuta alimjua nakumuuliza kuna nini bila ya kutojua anafatwa na yule askari wa mfalme,yule askari pori alijikuta anashindwa kuongea kutokana nakuhema sana alibaki anaonesha tu kwa kidole kule hule mchanga unapotokea.ghafla yule askari wa mfalme alimn'gata kwenye mguu wa inspecta mkuta nakumunyonya damu........



    inspecta alihisi maumivu makali sana,alimpiga teke moja lililomuondoa yule askari wa mfalme kwenye mguu wake,kila mtu akabaki mdomo wazi akiwa amini alichokiona,yule askari wa mfalme alipodondoka alinyanyuka huku akijiramba damu,akahisi nafuu kidogo baada ya kunywa damu,mara akamwangalia madam mary kwa uchu wa damu na kiu aliyokuwa nayo,wakati huo huo hule mchanga ukatia timu kwa kasi, ukaanza na yule askari pori,ulimrukia nakumuangamiza,alimomonyoka kama aliyemwagiwa asidi.Angel alimshika mkono prof Moses hakisaidiana na madam mary wakatimua mbio nakutokomea ndani ya msitu huo.akabaki inspecta mkuta na yule askari wa mfalme.mkuta alitambaa kujaribu kujiokoa,yule askari alikuwa bado ana njaa akamfata inspecta mkuta,lakini ghafla hule mchanga ukamrukia yule askari wa mfalme,yeye akuungua ila alianza kubadilika mwili wake,inspecta alishuhudia tukio zima,hule mchanga ambao ndio yule kiumbe wa ajabu ukauungana na askari wa mfalme,mkuta alikata tamaa ya kuishi akabaki tu anasubiria yule kiumbe amuangamize kwani akuweza tena kukimbia wala kutambaa sababu damu nyingi ili mvuja kwenye jeraha lake ambalo sasa limetoneshwa kwa kung'atwa na askari wa mfalme.

    baada ya ule mchanga kuungana na askari wa mfalme,alibadilika nakuota manyoya mwili mzima kichwani pembe zikachomoza nakurefuka kucha zikaongezeka nakuwa ndefu ajabu,meno yalitokeza nje kwa urefu,inspecta alipo ona hivyo aligahiri kufa sababu alikuwa anatisha sana yule kiumbe inspecta alipiga kelele za kuomba msaada,kwa bahati nzuri wenzake walikuwa karibu na eneo hilo wakasikia kelele za inspecta mkuta,walizifuatilia zinakotokea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kile kiumbe kiliuvaa mwili wa yule askari,kilijinyoosha kisha kilitoa kicheko cha ajabu na cha kutisha ghafla hali ya hewa ikabadilika,wingu zito likatanda angani,radi zilipiga zikifuatiwa na ngurumo kali,kilimgeukia inspecta mkuta pale chini akipiga kelele kuomba msaada kikapiga hatua za kibabe kumfata inspecta,kidogo wenzake wanafika nakumuona inspecta mkuta akiwa yupo chini na yule kiumbe anamsogelea,inspecta martin anawaamurisha kushambulia,walimumiminia risasi mfululizo,kile kiumbe kikahairisha kumfata mkuta kikawageukia walio kuwa wanamsambulia,akikudhuhurika na zile risasi kwani ziliingia nakutoka kisha jeraha linapona,ghafla mmoja mmoja risasi zikamuishia hadi wakajikuta wamemaliza risasi wote na adui bado mzima kabisa,wakiwa wanaangaliana yule kiumbe anaruka na kumkamata mmoja wao kinamnyanyua juu kisha kinamnyofoa kichwa huku wanashuhudia,ikabidi wamcheze mchezo yule kiumbe martin alimfata yule kiumbe akiwa kashikilia kipande cha mti mkononi,anaanza kupambana nae,huku inspecta mkuta akinyanyuliwa na askari wengine kisha wakatokomea naye nakuelekea waliko kubaliana kukutana,inspecta martini alipoona wenzake wameondoka na yeye akaacha kupambana na yule kiumbe,akamrushia kile kipande cha mti yule kiumbe kikaudaka,inspecta martini akageuka nakuanza kutimua mbio kama swala,yule kiumbe alimrushia kile kipande cha mti kikaenda na kumpiga kichwani akaanguka chini inspecta mart,kisha kikamfata kwa hasira na kumnyanyua juu kwa mkono wake mmoja,kisha kikamsogeza karibu na uso wake,wakawa wanatizamana uso kwa uso,martini aliogopa sana kwani kile kiumbe kilitisha sana,kikamnusa kwa pua zake,kisha kikafunua mdomo wake nakutoa meno yake nje ili kimn'gate shingoni nakumnyonya damu lakini kabla akijamtimia meno kikahisi hali ya hatari kikamuachia inspecta martini hakadondoka chini,kile kiumbe kikawa kinaangalia juu huku kikigeuka geuka rangi yake ya mwili wake nakuwa nyekundu ghafla kikapotea nakumuacha inspecta martini akiwa amini kama yupo hai,alisimama huku kashika kichwani nakukimbia kuelekea kule waliko wenzake..

    ****************************

    Angel akiwa na walimu wake wanakimbia nakujikuta wamerudi kule ambako yule kiumbe alibadilika nakuwa mchanga wakiwa wamechoka,wanajipumzisha kidogo chini ya mti mmoja,Kimya kikuu kinatawala kati yao zikisikika tu pua zao zinavyovuta hewa safi ya oksijeni,Angel anahisi kumulikwa na kitu chenye mn'gao fulani kilichoakisi mwanga wa jua nakutoa miale sababu yakumulikwa na jua,angel anaamua kukifuata,anapokifikia hanagundua ni mkufu akauokota nakuangalia,"mh! Huu utakuwa wa nani??,aliwaza,akaamua kuutupa sababu akuzoea kuokota vitu hasivyovijua nakuvichukua sababu ya familia hanayotoka kujiweza kiuchumi.alipoutupa hule mkufu ukadondokea pale ambapo yule kiumbe alibadilikia nakuwa mchanga,pakafuka moshi ulioongezeka kidogo kidogo,Angel alirudi nakupumzika na wenzake,Ghafla akauona hule moshi akashituka.

    Eeeh huo moshi umewashwa na nani??,akasimama haraka nakwenda kuuzima,alipofika alipigwa na butwaa baada ya kuuona hule mkufu ndio unatoa moshi,aliinama nakuokota ghafla ule moshi ukazima,akiwa anauangalia aliushangaa sana kwa hayo maajabu,ghafla yule kiumbe akatokea mbele yake akuwa amekasirika sana,Angel alipoinua kichwa kuangalia alipiga kelele nakutaka kukimbia lakini...............



    Lakini yule kiumbe alimuwahi nakumkwaruza mgongoni na kucha zake za kutisha alidondoka chini,Angel alikuwa ameuondoa hule mkufu pale ulipokuwa unatoa moshi akawa ameushika mkononi,kwa hali hiyo yule kiumbe alirudi kwenye hali yake kwa kubadilika ile rangi nyekundu,kwani kipindi hule mkufu unapachoma pale chini kile kiumbe kilikuwa kinaumia.

    Kilipojisikia vyema kikajinyoosha kisha kikaanza kumfata Angel pale chini,wakati huo madam Mary pamoja na Prof Moses aliyekuwa hajiwezi sababu ya kukoswa koswa na kiumbe wa ajabu,walikuwa wakimpigia kelele Angel amke pale chini kwani yule kiumbe alikuwa anamfata ili kummaliza,Angel aliugulia maumivu makali pale chini ghafla bin vuu yule kiumbe akamfikia kilitoa kicheko cha kutisha kilichowafanya wazibe maskio yao kwa mikono yao,Angel alijigeuzwa nakulalia mgongo yule kiumbe alimsogelea na kutaka kumnyonya damu,Angel alinyanyua mikono yako ili kujaribu kumzuia yule kiumbe hasimdhuru,Angel alilia sana huku akimsihi yule kiumbe asimdhuru/asimuue.hule mkufu aliushikilia mkononi akiwa hana wazo lolote kuhusu mkufu, huo ndio hulikuwa wakati mzuri wa kumvalisha mkufu kiumbe huyo,yule kiumbe alimkaba kwa nguvu kooni nakumvuta kwake,Angel alimgusa yule kiumbe akiwa ameushika hule mkufu,ghafla hule mkufu uliwaka na kutoa miyonzi iliyong'aa kama moto,ilimwingia yule kiumbe kifuani nakumsababisha amwachie Angel,kikaanza kung'oa miti ovyo huku kikipiga kelele za kutisha,msitu mzima hulitulia tuli kelele zake tu ndizo zilisikika msitu mzima,ghafla kikapotea kimiujiza.

    Angel alidondoka chini nakukohoa mfululizo madam mary alimkimbilia nakumnyanyua wakaondoka.



    ********_________-----------_______*** mvua ilianza kunyesha kwa Kasi ilikuwa ni mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali,ndani ya basi la abiria,wanaonekana abiria wakiwa wamepitiwa na usingizi sababu ya baridi,basi lilienda kwa mwendo wa kawaida,dereva alipata wakati mgumu sababu upepo ulipiga kwa nguvu sana,ikabidi hapaki pembeni kidogo karibu na msitu wa sego,upepo ulipuliza na kufanya hadi basi litikisike,miti mingi ilivunjika nakurushwa mbali.

    Baada ya takribani masaa matatu mvua ilipungua nakubaki manyunyu,dereva akawasha basi ili waondoke akapachika gia kisha akaachia krachi nakukanyaga mafuta basi lilitoa tu mungurumo ila halikusogea kumaanisha barabara ilijaa tope,basi likaanza kusogea kidogo kidogo hadi likarudi barabarani,lakini lilianza kuteleza nakuyumba yumba ghafla lilkateleza nakuacha barabara nakuingia ndani ya msitu,liligonga mti mmoja nakuzima,abiria walikuwa wanapiga makelele huku wakihangaika ndani ya basi.Basi lilisimama abiria wakashuka haraka haraka,dereva alilikagua basi nakugundua limeharibika upande wa mbele,aling'ang'ana kuliwasha ila injini ilikaidi kuwaka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo huo wale askari pori waliosalia walikuwa wanaendelea kutembea kutafuta njia yakuwatoa ndani ya msitu huo,walilowana kwa kunyeshewa na mvua,walikuwa na hali mbaya sana miili yao ilitetemeka sana lakini hawakukata tamaa,hawakuamini kama wanakimbia vita hakuna aliuyeju kama watakuta hali ni ngumu kiasi hicho.

    Walisogea sogea hadi wakafika sehemu fulani nakusikua watu wakiwa wanaongea kwa kulalamika na kulaani kitu fulani,waliingiwa na furaha sana,wakaongeza mwendo hadi wakafika kwenye ile ajali,abiria wote wakawa wanawashangaa wale askari namna walivyochoka nakutetemeka,wale askari nao walishangaa ile basi ilivyogonga mti hakutia neno juu ya huaribifu huo wa misitu walikonyezana kutulia kwanza wafanikiwe kutoka eneo hilo salama ,dereva alifanikiwa kuiwasha aliirudisha nyuma ghafla likazima kabisa,aliamua kupiga simu kwenye kampuni anayoifanyia kazi,mawasiliano yalikuwa ya tabu sana alipanda juu ya basi nakufanikiwa kuongea nakuomba basi lingine lije.

    Abiria walisubiria takribani saa zima,ghafla walianza kusikia sauti za vicheko vya ajabu,abiria wote walikimbilia kwenye basi,mara askari mmoja akashikwa miguu nakuvutiwa chini,abiria mwingine alishitukia amefungwa miguu nakamba kisha akavutwa nyuma,abiria wote pamoja na wale askari walijifungia ndani ya basi,wakatulia tuli,wakashitukia kishindo kizito juu ya basi ikachirizika damu kutoka juu nakupita kwenye vioo....





    Kelele zilisikika ndani ya basi hilo kila mtu alikuwa na hofu kuu,hatua chache kutoka sehemu lilipo basi linasikika basi jingine la kampuni hiyo likija upande huo huo likuwa lina dereva peke yake.wakati huo huo yule kiumbe hanatokea ndani ya basi hilo bila ya dereva kugundua,anaendesha basi hadi anafika kwenye lile basi lililogonga mti,abiria wanamshukuru Mungu nakushuka ndani ya basi hilo.ghafla yule kiumbe anamuingilia yule dereva,nakubadili akili ya dereva, baada ya abiria wote kuingia ndani ya basi hilo yule dereva analiondoa basi kwa kasi nakuwafanya wale abiria waingiwe na hofu,dereva alizamisha basi ndani ya msitu kwa kasi,askari pori mmoja akamfata dereva kwa jazba,kwa spidi ya ajabu yule dereva alimrukia yule askari nakuliacha basi likizidi kuingia bondeni, akamgongesha yule askari kwenye chuma,akapoteza maisha hapo hapo,yule kiumbe akamtoka yule dereva kisha akapotea huku akitoa kicheko cha kutisha,dereva alibaki akiwa haamini kama kamtoa mtu uhai,basi lilifika sehemu yenye mseleleko mkali(gentle slope).

    Likapinduka nakwenda kujigonga kwenye jiwe,mlipuko mkubwa ukatokea abiria wote pamoja na askari pori wote wakapoteza maisha hapo hapo hakuna aliyepona.

    **********************************

    Upande wa pili hofu ilizidi kutanda juu ya wanachuo pamoja na maprof walioenda nchini congo kwa ajili ya utafiti,hakuna yoyote aliyejua wana hali gani,hakuna taarifa yoyote juu yao iliyopatikana,uongozi wa chuo ukaamua kutuma timu ya watu kumi kwenda nchini congo kwa ajili ya kwenda kufuatiria nakuleta taarifa,walijianda na kukata tiketi za kusafiria pamoja na pass ya kusafiria,safari ikaanza walitua congo mida ya asubuhi nakwenda moja kwa moja hotelini wakapumzika kesho yake wakaenda kwenye idara inayohusiana na wageni wanaoingia nchini congo,walipewa taarifa ambazo hazikuwalizisha ikabidi waombe msaada utakaowapeleka ndani ya msitu huo,wakapewa askari nakuanza safari ya kuelekea kwenye msitu wa sego.wakiwa ndani ya range rover wanatia timu ndani ya msitu huo.wanashuka sababu gari lao lisingeweza kuingia msituni,wanaingia ndani ya msitu huo,wakiwa wanatembea bila ya kujua kwamba kuna matatizo ndani ya msitu huo,yule kiumbe anatokea juu ya mti mmoja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    -----------------/-------//////------------------\

    Angel akiwa na madam Mary pamoja na Prof Moses wanaendelea kutembea bila ya tumaini la kupona,wakati huo Angel anazidi kuzidiwa sababu halikuwa anatokwa na damu nyingi sana mgongoni,wanatembea hatimaye wanafanikiwa kufika kwenye kijiji cha sego,wanapelekwa moja kwa moja hadi kwa mfalme,wanapokelewa kisha angel anapelekwa kwa mtaalamu wao,anawekewa dawa iliyokuwa imepondwa pondwa,kisha wanaletewa chakula wanakula wakati huo Angel alikuwa kapoteza fahamu,yule mganga anaampaka mafuta fulani mwilini mwake anapomshika mkono wake anashituka baada yakuona ule mkufu mkononi mwake angel,anauchukua kisha anamtizama angel nakumfananisha na malkia ambaye alikwisha fariki,anaamua kutizama nyota yake,baada ya muda kidogo anagundua kwamba angel ndiye binti mfalme aliyesadikika amekufa,habari zinamfikia mfalme kuhusu hule mkufu pamoja na bintiye,akaamua kuja kujionea mwenyewe,alipomtizama angel kweli alifanana na marehemu mke wake anapomgusa, angel anaapata fahamu nakufumbua macho,anapoangalia huku na huko anashituka kujikuta yupo na watu asio wajua,anakurupuka nakupiga kelele za uoga na kutimua mbio,anazuiriwa na walinzi nakurudishwa ndani,mfalme anamuongelesha angel lakini hawakuelewana,ikabidi aitwe madam Mary aje kumtuliza,angel alipomuona madam Mary akapata matumaini,akaletewa chakula.akala kisha akaelezwa kisa cha kiumbe huyo na chimbuko lake akiwa anatafsiriwa na madam Mary,Angel alikataa kwamba yeye anaundugu nao,ikabidi aonyeshwe na yule mganga,akawasha moto kisha akanuizia maneno haliyoyajua yeye ghafla hule moto ukalipuka nakuwa wa rangi ya blue,badala yakumuonesha angel kilichotokea akiwa mdogo,hule moto ukatoa ile sauti ambayo angel huwa anaisikia, ikasema waondoke eneo hilo hatari kubwa inakuja kisha ukazimika,kila mtu akabaki ameduwaa hadi mganga naye akawa haelewi,wakiwa bado wanajiuliza angel alijua kitakachotokea akawaambia waondoke lakini walikaidi wakijiamini wakijua yule kiumbe hawezi kufika hapo walipo,angel alimnyakua yule mganga hule mkufu kisha akawaambia madam Mary na Prof Moses wakakikimbia,walinzi wakaanza kuwafukuza mfalme aliwaonya wasimzuru binti yake ila akamatwe nakuletwa kwake akiwa hai,lakini kabla hawajaondoka kijijini hapo wingu zito linatanda angani na upepo mkali kama kimbunga unavamia kijiji hicho nakuharibu vitu,wanakijiji wanatahamaki nakukimbia ovyo ndani ya kile kimbuga anatokea yule kiumbe wa ajabu akiwa kashikilia vichwa vya askari wawili ambao walikuja na kile kikosi kilichotoka tz kwa ajili ya kuja kuangalia kuna nini kimewatokea wanachuo waliokuja kufanya utafiti,kile kiumbe kinavirusha vile vichwa kisha kinamrukia mganga nakumuangusha chini,upepo uliendelea kupiga kwa kwa kasi nakufanya wanakijiji washindwe kukimbia nakubaki wakishikilia miti ili upepo usiwafute,angel na wenzake nao hawakufika mbali wakajishikiliza kwenye mti,yule kiumbe alimtia meno shingoni yule mganga nakumnyonya damu,kisha kikageuka nyuma nakumuona angel,kilitabasamu nakupiga hatua kumfata angel pale alipo.............



    Wanatembea huku wanapiga picha kwa simu zao pamoja na camera madhari ya msitu huo wa sego,juu yao anaonekana yule kiumbe akiwa tizama kwa chini bila ya wao kumuona.

    Mmoja wao anachukua kipande cha karatasi kilicho chorwa ramani ya msitu huo nakuwaelekeza wenzake sehemu ilipo kambi ya wanaowatafuta.walipokuwa wakiitizama ile ramani,udenda mzito wa damu unadondoka kutoka juu nakuidondokea ile karatasi wanaangaliana Kisha wanainua vichwa vyao juu lakini hawaoni kitu,wanarudi kuiangalia ile ramani wanaikuta imejaa damu,wanabaki wameduwaa.hali hiyo inahashiria hatari kubwa ipo mbele yao,askari mmoja anaona kitu kinapita kwa Kasi ya ajabu nakupotea,anafuatilia kule halikoona,tena anahisi kitu kinapita nyuma yake kwa Kasi,anapogeuka nyuma anakutana uso kwa uso na yule kiumbe wa ajabu,anapiga yowe huku akimfyatulia risasi yule kiumbe,wenzake wanashituka na kuanza kukimbia kuelekea kule alipoelekea mwenzao,wanapofika wanakuta kiatu tu pamoja na silaha yake mwenyewe hayupo, wote wanajua sasa hali si shwari msituni humo,wanaweka silaha zao tayali kwa kujihami,ghafla kati kati yao yule kiumbe anafumuka kutoka ardhini,wote wanamuona yule kiumbe mubashara kabisa,wanaanza kumfyatulia risasi mfululizo,Yule kiumbe anazikwepa kwa Kasi ya ajabu,wanajikuta wao kwa wao wanauwana,askari watano wanaanguka chini pamoja na mtu mmoja kutoka tanzania naye anapoteza maisha hapo hapo baada ya kupigwa risasi,wanabaki askari wawili pamoja na watu tisa kwenye kikosi kilichotoka Tz,yule kiumbe anaruka juu na kutua nyuma yao,nakumkaba mtu mwingine kooni,wale askari pori wakamfyatulia risasi tena,kikaingiwa na jazba kilimtoboa tumbo nakumtoa utumbo yule mtu kisha kikafyatuka kama mshale nakuwafikia wale askari,kiliwafyekelea mbali vichwa vyao vikadondoka chini,kile kikosi kikatawanyikia ndani zaidi ya msitu huo wasijue wapi wanaelekea,kile kiumbe kilihisi hali ya hatari kikaangalia angani kisha kikainama chini nakuvichukua vile vichwa vya wale askari pori,kisha kikabadilika nakuwa upepo mkali,anga lote likatandwa na mawingu mazito pamoja na radi zilizoambatana na ngurumo,upepo huo ukaelekea kule kijijini hukivuta vitu nakuvirusha mbali.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********************************************************************

    Upepo ulivuma kwa kasi sana nakuzidi kuongezeka kila dakika,Angel alishikilia mti kwa nguvu ili upepo huo husimvute,yule kiumbe wa ajabu akawa anamfata pale halipo,kilipomfikia kilinyanyua mkono juu ikatokea shoka mkononi mwake,angel mda huo alikuwa kafumba macho sababu ya hule upepo,yule kiumbe alijiandaa kumfyeka Angel,kiliinyanyua ile shoka juu kwa mikono miwili,lakini upepo ulimzidi angel nguvu hatimaye akajikuta anavutwa na hule upepo,yule kiumbe anashusha shoka ili amuangamize anamkosa kosa Angel kinagadhibika nakumfata kwa kasi,Angel anakwama kwenye mizizi ya mti mkubwa kwa bahati mbaya hule mkufu unadondoka chini angel anajivuta ili hauokote punde si punde yule kiumbe anamfikia nakumshushia shoka Angel anamuona kwa tabu sababu ya vumbi jingi lililosababishwa na hule upepo akajibiringisha pembeni,ile anatoka tu shoka inamkosa kosa na kunasa nguo yake,yule kiumbe anaichomoa chini ile shoka na kutaka kumuua Angel lakini upepo tena unamvuta sababu akujizuia,kile kiumbe kinaamua kuuzuia hule upepo utulie ili afanye kazi yake bila tabu kwani kilijua Adui yake mkubwa ni angel,mara upepo ukamtii na kutulia tuli,Angel anapoangalia mbele yake anafanikiwa kuuona hule mkufu,lakini yule kiumbe halikuwa karibu yake.akaamua kujitoa sadaka,akasimama nakuufata hule mkufu yule kiumbe naye alimfata Angel kwa kasi,alifanikiwa kuuokota hule mkufu,anapoinuka yule kiumbe anamuwahi nakumpiga na shoka begani inamuingia kisha kile kiumbe kinamvuta kwa nguvu na hile shoka kisha kiinainua mkono wake juu wenye makucha ya kutisha nakumchoma nayo kifuani kwake,Angel anahisi kuishiwa nguvu,lakini akajikaza nakumvalisha yule kiumbe hule mkufu kwenye pembe zake.kilimnyofoa Angel moyo nakumrusha mbali.ghafla kilihisi kusisimuka hule mkufu huliwaka nakutoa miyonzi mikali iliyokwenda angani kisha zikarudi kwa Kasi nakumuingia yule kiumbe kifuani.kilipiga kelele kali zilifanya msitu mzima utikisike.ardhi ilipasuka na yule kiumbe akatumbukia ndani kisha ikajifunga huo ndio hukawa mwisho wa yule kiumbe.Angel alitoa tabasamu kuashiria amefanikisha kulitatua tatizo na kulipiza kisasi juu ya vifo vya wenzake alizikumbuka taswira za wazazi wake waliomlea pamoja na marafiki zake chozi likamtoka kisha akakata pumzi.

    Wanakijiji walioshuhudia walimkimbilia Angel lakini alikuwa ameishafariki,mfalme alilia sana kwa kuipoteza familia yake aliyoangaika kuilinda nakusababisha matatizo hayo kutokea hatimaye yote imeondoka yote alijifungia ndani mwake kisha akajichoma kisu nakufa msiba mkubwa hulikitawala kijiji cha sego.Prof Moses pamoja na madam Mary bao walipatwa na majonzi makubwa kwa kupiteza wanafunzi wao wote walibaki hawajui wafanye nini kile kikosi kilifanikiwa kufika kwenye kijiji hicho nakuwaona Prof Moses na mary waliwachukua nakuondoka kurudi tz angel alizikwa na kijiji hicho kama shujaa wao pamoja na mfalme......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******MWISHO******

 

0 comments:

Post a Comment

Blog